Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, March 24, 2010

Kinga ni bora kuliko tiba.

`Hizi mvua sasa zimezidi...aaaha jamani..' Alikuwa akilalamika baba mmoja ambaye alisimama karibu yangu, tulikuwa tunanyeshewa na mvua hapo kituoni. Niligeuka kumwangalia, nikikumbuka wiki moja iliyopita yeye au mwingine alikuwa akilalamika kuhusu joto. Kwa mwanadamu kila kitu nikulalamika, lakini muumba ndiye mwenye hekima ya kujua kipi kije kwa wakati gani.
 'Lakini mbona hatuna wema, wewe siulakuwa ukilalamika kuwa joto linakuathiri, unapata vipele' mama mmoja aliyekaa naye karibu akasema, nafikiri ni mkewe.
'Aaah, lakini huoni kuwa tunalowana hapa. Magari hayaonekani, matope, maji yamejaa kila mahali muajiri utamwambia kuwa umechelewa sababu ya mvua' akajitetea yule baba.
'Hiyo ndiyo shukurani ya punda, nakuuliza, unataka joto au baridi?' akauliza yule mama'
'Vyote navitaka ilimradi visiniumize, sasa huoni mvua inanikwaza...' akasema yule baba.
 Huo mjadala uliniweka katika mawazo, nikiangalia maji yanayolundikana barabarani, mifereji imeziba, na barabara foleni haikatiki. Hivi ina maana hawa wanahudumia hizi barabara hawaangalii nyakati, kuwa sasa ni kipindi cha mvua, mifereji iwe misafi, kuhakikisha kuwa mvua ikija maji hayajai ovyo? Ni akina nani ho, labda ni halimashauri ya jiji!
 Lakini hata sisi kama raia, wapita njia na wafanyabiashara tuna wajibu wetu. Ina maana tukila matunda, tukinywa maji au vitu vyovyote hakuna sehemu za kutupia taka zake? Nafikiri zipo, kuna sehemu kuna mabokisi ya taka, ni nani anayatumia?
 Haya kuna balaa la mbu, mvua kama hizi zitazalisha mbu wengi, je tumejiandaaje na kupambana na mazalia ya mbu, au ule wimbo wa malaria haikubaliki tunaupokeaje? Tusiupokee kibiashara, tuupokee kivitendo kuwa malaria ni bora kuikinga kuliko kuitibu!
 Tuombe mvua ziwe za heri, na wale waliopo mabondeni wajihami mapema, na waliopo kwenye maeneo ya shamba wawahi kupanda kile kinachofaa. Na tukumbuke kuchemsha maji kwani kipindupindu na magonjwa ya kuhara hayapo mbali. Usemi bora kwa leo ni kinga ni bora kuliko tiba.
From miram3

3 comments :

Anonymous said...

Mimi nataka baridi kidogo, joto kidogo...mmmh, kati na kati

Anonymous said...

Mimi nataka baridi kidogo, joto kidogo...mmmh, kati na kati

Man of Hope... said...

Fun