Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, May 1, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-19


‘Docta akaiweka simu hewani, na mara sauti ikasikika ikisema;

Sasa umefanya nini..mbona hajaonekana huku, na…umefanya nini mbona umeharibu, hatukuoni huku,…upo gizani,…na ile kazi imeishia wapi,…unakumbuka…ni lazima ikamilike kabla ya siku tano , zimebakia siku mbili, vinginevyo, utageukiwa wewe mwenyewe..unasikia, mbona hujibu kitu…wewe…sema …’mara akakata simu.

Huyu mkuu ni nani, inabidi tumchunguze kwanza huyu mtu, ili kupata jina lake, kwa vile kuna namba yake hapa, jifanye kama unamtumia pesa jina lake litatokea...'akasema docta

Na jina likatokea

Tuendelee na kisa chetu..

              *************

‘Unamfahamu huyu mtu…?’ docta akamuuliza binti.

‘Mhh, hapana simfahamu, hilo jina ni geni kwangu..., sio huyo mtu ninayewaambia, sijawahi kulisikia hilo jina,... eti baba, unaweza kumjua mtu kama huyu..?’ akaulizwa binti, na binti akamuuliza baba yake..na baba yake akawa kama anajaribu kutafakati, halafu akasema;

‘Hapana hilo jina hata mimi ni geni kwangu, nawafahamu watu wengi, lakini hilo,...mmh, simjui ni nani, ..hata ubini wake ni ....mgeni kabisa hapa kwetu,labda awe katumia simu ya mtu mwingine au, jina la mtu mwingine…’akasema baba.

‘Kwani huyo anayemiliki hiyo super market hana ndugu wengine…?' nikauliza

'Nani, huyu anayemiliki supermaketi kubwa, una maana huyo, ambaye ana udugu fulani na mhuyu mangaji wangu,...jamaa zao nawafahamu wote, hakuna jina kama hilo, na jamaa zao wengi  waliuhama mji, baada ya kuuza maeneo yao yote...waliobakia ni huyu jamaa na huyo mwenye super market, ..’akasema mzee.

‘Huyo wa super market, hatuwezi kufika kwake kwa hivi sasa….ujue huyo mtu anajijua, ana kila namna ya kujilinda, kwasababu ana pesa, hata kama yeye ndio kiongozi wa haya mauchafu, hawezi kukubali, na hata jinsi ya kumuingia inakuwa ngumu,…

'Unajua niwaambie kitu, watu kama hawa wenye uwezo, matajiri,..kwa nje, kwenye uso wa jamii wanaoneka wema sana si wanasaidia watu kwa unafiki fulani ili kujikosha,.., na ukimgusa tu, akianza kutembeza propoganda, utaonekana wewe ni mbaya sana , japokuwa ulitaka kusaidia na kufichua uchafu wake, ...mwenyepesa hata akiwa mhalfu, mdhulumaji,.. watu watamnyenyekea tu….sasa tunawezaje kufika kwake, bila ya yeye kutushuku..?’ akauliza docta, halafu akaendelea kusema

‘Mhh…mimi naona huyu mtu hapa anaweza kutusaidia ..’akasema akimuangalia jamaa aliyekuwa kalala sakafuni, jamaa alikuwa anatikisika kama anataka kuamuka,alikuwa ameshazindukana, na alipoona watu wanamuangalia yeye akasimama;

‘Nipo wapi..?’ akauliza

‘Wewe ulikwenda kwa nani…?’ akauliza docta.

‘Oh..kumetokea nini..mbona sielewi…akajinyosha halafu akakumbuka, akamuangalia docta

‘Samahani sana, nawaombeni nipo chini ya miguu yenu naombeni hicho kitu mlichochukua pale ndani, tafadhali…’akasema akionyesha mikono ya kuomba.

‘Hatujachukua kitu chochote pale kwako, una uhakika tumechukua nini,…’akasema docta na akawa kama anamuuliza

‘Hapana mumechukua mali yangu…nina uhakika kabisa na ….,niambieni mnataka nini, mimi nitawsaidia lakini mnirudishie hicho kitu, ni kitu changu muhimu sana, mtaniua mkinifanyia hivyo..’akasema

‘Kwahiyo kwako kinakulinda kwa wengine unakitumia kuwamaliza…’akasema docta

‘Hapana….sio kweli, hicho ni kinga yangu, niliyoachiwa na mababu zangu, hakina maana kwa watu wengine,…si umeona mwenye nyumba watu pale wamekimbia, lakini kwa vile mimi nina hiyo kinga, hakuna kinachweza kunisumbua, kinanisaidia mimi, sio kwa watu wengine..’akasema

‘Sasa sikiliza, tumegundua kuwa hicho kinatumika kuangamiza watu wengine na sisi ni lazima tukiangamize, hatuwezi kufuga mashetani yenye madhara kwa watu, unasikia, hicho tutakiangamiza, ila kabla tunataka utusaidie, na sisi tuona jinsi gani ya kukusaidia..’akasema docta,akikitoa kwenye mfuko, na jamaa alikiangalia kwa macho ya uchu,…akijua sasa anapewa kifaa chake

‘Nitashukuru sana ukinirejeshea na mimi nitawapa mnachokitaka, mnataka nini…kwanza muulizeni mwenye nyumba, huyu ni mtu wangu wa karibu sana, tumeishi na yeye miaka mingi, hebu waambie, tumetoka wapi…’akasema akimuangalia mzee

‘Nipe mafuta ya taa…’akasema docta

‘Unataka kufanya nini wewe,..mafuta ya taa ya nini…usifanye mzaha na hicho kitu, hilo ni bomu, litalipuka na kuangamiza hii nyumba yote, ohooo, mzee, hebu ongea na huyu mtu wako, utakuja kuharibiwa mali yako…’akasema akimuangalia mzee, na mzee alitaka kusema kitu lakini docta akaingilia kati...

‘Nataka kukiunguza na hivyo vilivyomo ndani yake vipotee, si ndio umemuweka taire wako humu ndani, huyu hatatoka salama, kama ni bomu, tutaona,..unasikia, sisi tunachotaka ni ukweli, tunajua wewe unatumika tu, tuambie ni nani anayekutuma kufanya hayo uliyoyafanya..?’ akauliza docta.

‘Sijafanya kitu, kwanini niwafanyie watu wangu ubaya, ninaishi kwenye nyumba yao, tumeishi na wao kwa amani, kwanini niwafanyie wao ubaya,..usitake kunigombanisha na ndugu yangu huyu..’akasema.

‘Narudia tena, ni nani waliokutuma,au kumbe ni wewe mwenyewe, mchana unajifanya wewe ni mtu mwema, ukifika usiku unawageuka, unakuwa adui, tuna ushahidi kwa hilo,…unakumbuka ulichokifanya..sema ukweli, au sasa hivi naanza kazi yangu..’akasema docta, sasa akifungua chupa ya mafuta ya taa.

‘Samahani sana nipo chini ya miguu yako usikiunguze, tafadhali, utaharibu kila kitu, utaniangamiza, wewe hujui tu…jinsi kilivyo muhimu kwangu, hata wao hawakijui…hahaha, wao wana mambo yao,…’akasema na kupiga magoti, lakini docta akakichukua, na kukiweka kwenye jiko la mkaa na kwanza akakimwagia mafuta yake, halafu akaanza kumwagia mafuta ya taa.

‘Mungu wako..unataka kufanya nini wewe, ina maana hunielewi, nitakuambia kila kitu, lakini sio mimi,..ni wao, kawaulize wao, hicho hakihusiani na wao…’akasema.

‘Hao akina nani, tutajie,…ni akina nani hao…’akauliza docta.

‘Siwezi kuwatajia, hamjui mnachopambana nacho...nitauwawa…watajua tu nikisema, na hata hivyo sasa hivi nipo matatani, sijui kama nitamaliza siku, tafadhali niamini,..nitawaambia nini jamani, hamuwajui hao watu jamani…usikiunguze hicho kitu hakiwahusu wao,...ukikiinguza utaniangamiza mimi sio wao…’akasema

‘Tunawataka kuwatambua hao..hao ndio tutapambana na wao, wewe si unatumwa tu, sasa tutajia, ni nai huyo mkuu wako..?’ akauliza.

‘Mkuu..oh,…nani kuambia habari za mkuu…mkuu, jamani ni nani huyo, sio mimi...?’ akaonekana kushtuka.

‘Katupigia simu, anakuhitaji,kasema yeye ni mkuu wako,..ulihitajika kwenye kikao, kuna kazi ulipewa hujamaliza... sasa tuambie ni nani huyo..?’ akaulizwa.

Sasa akaonekana kuwa na wasiwasi  kuliko hata awali, akashika kichwa, akawa ana hahaha, anatetemeka..na kuangalia huku na kule kama anawaona watu!

‘Oh, nimekwisha..nisaidieni jamani…nani, ..mkuu, mungu nimekwisha..wahenga mpo wapi, mbona mnaniacha...’akasema sasa akigeuka kuangalia mlangoni.

‘Pale ulipokuwa umekining’iniza juu ya moto, kilikuwa kifanya mambo yako, na wahenga wako...au sio..unatembea huku unajifanya huonekani, unakwenda makaburini, unafanya mambo yako, au sio…sasa hapa tunakiunguza kabisa..ili uweze kufanya zaidi..’akasema docta sasa akizan kukimwagia mafuta.

Jamaa jicho likaanza kumtoka, haamini, docta akawa anakimwagia mafuta huko anasoma mambo yake, mdomoni…

Jamaa akaanza kujishika shika kama anawashwa, akawa anahangaika kweli, huku anapiga ukelele kuwa anaungua..

‘Unaniua, unaniangamiza..subiri nitakuambia, subiri, subiri subiri...oohh..aaakkh…’akatikisa kichwa lakini mambo yakawa hayapandi kichwani tena, kabakia mkavu.

‘Sikiliza ili tukupe hiki kitu chako, kabla hakijateketea, tunataka utuambie ukweli, wewe ni nani…’akasema docta.

‘Mimi ananifahamu huyu mwenye nyumba, sina ubaya na mtu kabisa, na haya mengine ni katika kutafuta riziki, tu, na huyo mkuu, kiukweli hata mimi simjui…’aliposema hivyo docta akaongeza mafuta kwenye kila kibuyu..

‘Ooh, unaniunguza, acha nisema…unataka nisema nini..’akasema docta akaongeza mafuta huku akiendelea kusema maneno..mara jmaa akabadilika akaanza kuongea sauti nyingine ya besi.

‘Mimi ni kikaragosi cha mkuu…natumika tu kutekeleza mambo yake..nimekuwa mtumishi wake kwa muda sasa…nilitumwa kuingilia familia ya Mashauri, nimeshatoa kafara, kwa maagizo ya mkuu,….bado …bado…anahitaji mtu mwingine, mpenzi wa kafara,..kafara haiende bila mwenzake…wanamtaka mwenzake,…lakini nimeshindwa, wao wanamtaka kwa udi na uvumba.. naumia naumia…msinifanye hivyo jamani,…’akawa anatapa tapa, halafu akadondoka chini..

Docta akakiangalia kile kibuyu, kilikuwa kimeanza kuwa cheusi,..akachukua kibiriti,, akawasha na kurudi nyuma…kukatokea mlipuko,  jamaa aliyekuwa kalala, akasimama, akaangalia huku na kule, mara huyo akatoka mbio, ..utafikiri mwizi,..hakusimama, alikimbia na kuwaacha wenyeji wakiwa wameduwaa. Kile kibuyu kikateketea kabisa kwenye moto na kubakia majivu.

‘Mwacheni akimbie hana kitu sasa, ,…sizani kama kuna haja ya kumuita polisi kwa sasa, maana hatuna ushahidi kamili, zaidi ya sauti yake, kama alivyosema yeye anatumiwa, kuna mtu anamtumia, na huyo mtu, ni mkuu wake, sasa je huyo mkuu ndio huyo mwenye jina kwenye simu..’akasema docta.

‘Lakini kwa vile kakiri kuwa ndio yeye, kafanya hayo yaliyofanyika, wao wakiita ni kafara, kwanini tusiwaite polisi,  tuwaambie wao watajua ni nini cha kufanya…’akasema mama.

‘Amekiri kuwa kafanya kafara, la nini…kafara linaweza kuwa la mnyama, lakini sisi tunajua alichokifanya, je tunaweza kukiwakilishaje polisi kikaswihi, ujue polisi wanahitajia ushahidi wenye mshiko, kwa hivi sasa hili haliwezi kutusaidia, mnaona hapo ilivyo…’akasema docta.

‘Sasa tufanyeje…?’ akauliza mzee.

‘Huyo huyo mtu, anaweza kutusaidia..kama kweli watamuacha hai…nijuavyo, hawa watu wakijua mtu wao kawasaliti, hawataweza kumuacha hai…’akasema docta.

‘Ngoja nimpigia simu…’akasema mzee mashauri…na kuanza kupiga simu, simu iliita wee haikujibiwa, ..

‘Hawezi kupokea hapo alipo anatafuta njia ya kuukimbia mji, …’akasema docta

‘Sasa tufanyeje, tumuahini basi…’mimi nikasema

‘Ni kweli, sisi twende kwenye nyumba yako, tukamalize kazi,..hata tusipompata yeye, pale kuna kazi ya kumalizia, tukiwa na wewe mwenye nyumba, …na inabidi kiukweli tushirikiane na polisi, huyu mkuu ni nani, na anaonekana ni mtu mkubwa, pia yanaweza kutokea mauaji mengine, ikawa ni kesi kwetu…’akasema docta.

‘Jamani mnajua hao ni watu wa hatari sana,..mimi naona tuachane nao…’akasema bint akionyesha wasiwasi mkubwa.

‘Kwa hatua tuliyofikia hatuweza kuachana nao, tutapambana nao, msiogope, kitu, ondoeni hofu, hofu ndio silaha ya hawa watu,..hebu tuambie bint, kuhusu huyo mumiliki wa super market, hujawahi kufika ofisini kwake…mkaongea naye..?’ akauliza docta.

‘Afike kufanya nini..?’ akauliza mama

‘Subiri mimi, nataka binti atujibu, hili ni kwa manufaa yenu, unajua...anaweza akafahamu mambo yanayoweza kutusaidia,..binti hebu tuambie maana ukinyamaza, familia yako na wewe mwenyewe mtakuwa kwenye hatari……….’akasema docta.

‘Hatari ipi tena zaidi..hayo mnayoyafanya ni hatari zaidi,..mimi nimeshampoteza dada yangu, sasa unataka kuingiza familia yangu kwenye matatizo zaidi, mimi sijui,..sipendii baba, achana na mambo haya..’akasema binti akimuangalia baba yake.

‘Docta nilikuambia sitaki uje kumfanya binti yangu apate shida tena, ..unaona sasa…’akasema mzee.

‘Mzee…kumbuka jamb moja,…hawa watu wana mbinu nyingi sana, na moja wapo ni vitisho, wanaweza kufikia hata hataua ya kuua, kwa ajili ya kutishia watu, watafanya mambo ya ajabu, …’akasema docta.

‘Haya nimekuelewa, kwanini tusienda kwa huyu jamaa..tusipoteze muda, maana nilikuwa na mpango wa kutembea nyumba yangu,…’akasema mzee.

‘Usiende huko mume wangu,…’akasema mkewe

‘Kweli baba usiende huko kwenye hiyo nyumba, unakumbuka kulitokea nini huko,tukirudi huko yanaweza kutukuta yaliyomkuta dada, baba achana na mambo hayo, kwani sis tunataka nini tena, ..’akasema binti.

‘Nia na lengo letu ni kumpata huyu aliyemuua dada yako, unasikia, sasa tukikaa kimia itsaidia, nini je wataishie kwa dada yako tu...kabla hawajafanya lolote ni lazima tuwawahi sisi, usiwe na wasiwasi binti..au unajua lolote la kutusaidia..?’ akaulizwa.

‘Mhh..hata sijui, ila naogopa, itakuja kutokea hivyo…’akawa kama anataka kulia, na docta akasema;

‘Sikiliza binti, sasa hivi tupo kwenye mapambano, na mapambano haya nguvu yake kubwa ni umoja na kuondoa uwoga, ..kujiamini na kuamini kuwa mungu ndiye mlinzi wako..usitishike na viumbe ambavyo umeshapewa mamlaka navyo..unanielewa,… ‘akasema docta na bint kawa kainamisha kichwa chini tu.

‘Sasa hivi nyumba ipo salama, yale mauchafu yaliyokuwa yamejazwa kwenye hiyo nyumba hayapo tena, ila yanaweza kurejeshwa kama hao watu hatutaweza kuwadhibiti, kuwaangamiza kabisa…kama hatuweza kuharibu hizo itikadi zao mbaya za kishetani, tutakuwa bado kwenye mitihani ..unanielewa hapo…’akasema docta.

‘Tutawadhibitije, maana kwanza hatujawafahamu, ila wao wanatufahamu, na ukumbuke tumeshawachokoza…?’ nikauliza mimi.

‘Kwanza twende kwa huyu jamaa,..na sisi hatujawachokoza, wao ndio wachokozi wanaingilia majumba ya watu, wanawaumiza watu, wanaua…ukumbuke hilo, sasa hao sio binadamu, ni mashetani…mtu wetu wa kutusaidia hadi sasa ni huyo mlinzi, tukimbana vyema tunaweza kuyatambua mengi,..wasiwasi wangu, watu wake, wanaweza kumuwahi…polisi gani unamfaham mzee Mashauri..?’ docta akauliza.

‘Nawafahamu polisi wengi tu kwa hilo msiwe na shaka nalo,… ila ngoja nimuarifu huyu aliyeshughulikia hii kesi anaweza kutusaidia kwa karibu zaidi maana anajua kila kitu kinachoendelea…’akasema mzee na kumpigia simu huyo polisi, akamuelezea kwa kirefu na huyo polisi akasema tutakutana naye huko kwenye hiyo nyumba iliyohamwa, ili tuweze kumpata huyo mpangaji na mlinzi wake, kazi ikaanza hivyo…

‘Baba msiende jamani, mnajitakia mabaya zaidi...'akasema na alipoona baba yake hamsikiliza akamgeukia mama yake na kusema;

'Mama kwanini unakaa kimia unamuachia baba anakwenda kwenye matatizo,...mama, mzuie baba asiende huko, kuna mabalaa huko kwenye hiyo nyumba, unakumbuka kilichotufanye tuhame ni nini....’binti akawa analia huku kashika kichwa, …akipiga piga miguu chini, na mama kuona vile kwa binti yake akasogea mbele ya mume wake

‘Haendi mtu huko…msituletee matatizo kwenye nyumba hii..waacheni wafanye watakavyo,..lakini sitaki matatizo tena,..sitaki jamani..’akasema mama , docta akawa kasimama pembeni akimuangalia mzee atasemaje..

NB: Ni hatari...


WAZO LA LEO: Vita vya kiimani vina mitihani yake, kuliko vita vya macho kwa macho, kwani adui yako mkubwa anaweza kuwa ni wewe mwenyewe, ni NAFSI yako..ukitaka kuvishinda hivi vita pambana kwanza na nafsi yako, jitambue, kumbuka wewe ni nani katika hii dunia, na ni nani kakuleta hapa duniani, kwa madhumuni gani,..ukilitambua hilo, itakuwa rahisi kwako, kuishinda nafsi yako na nafsi yako itakuwa safi. Tumuombe mungu tuweze kushinda mitihani hii ya dunia maana mingine ni minzito kwetu, bila wewe mola wetu hatuwezi kuishinda.
Ni mimi: emu-three

No comments :