Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, February 11, 2017

FUPA LILOMSHINDA FISI….ni NANI ataliweza 2


 Mkuu maalumu wa mambo ya usalama, alikuwa kashikilia simu, tangia asubuhi amekuwa akiongea na mtu mmoja kwenye simu, na huyo anaongea kwa simu yake maalumu tu, na kila akisikia simu nyingine anaikata ile simu na kwenda kwenye simu ya mezani, au simu nyingine au vijana wake, halafu anarudi tena kuongea na huyo mtu wake aliyekuwa akiongea naye awali…

‘Sasa sikiliza,….hayo niachie mimi....subiri kidogo…’alisema hivyo aliposikia  simu yake nyingine ikiita, alipo angalia namba ya mpigaji, alishtuka, ....na kuhisi mwili wake ukimsisimuka,…kwa haraka akaikata hiyo simu aliyokuwa akiongea nayo awali na kuipokea hiyo simu ya sasa hivi.

‘Ndio muheshimiwa,…nilikuwa nawajibika na simu za vijana wangu…’akasema na kusikiliza halafu akakunja uso , kuashiria kuwa alichoambiwa ni kichungu kuliko shubiri, lakini hakuweza kukitema.

‘Ndio muheshimiwa, akitokea mtu nitakuambia, na…nitamuweka hewani umsikia anavyoongea, na nitahakikisha kuwa uchunguzi wote unafanyika, na ushahidi unakusanywa, …’akasema.

‘Lakini mkuu, hilo la kuwa kila mwananchi akija hapa kutoa taarifa unataka umsikie  anachokiongea, huoni ni usumbufu kwako maana ninajua una majukumu mengine makubwa, wanachi wengine ni hisia zao tu….wahana uhakika,…nilionelea kuwa…..’akakatizwa.

‘Sawa mkuu nitafanya hivyo…’akasema kwa shingo upande.

‘Ndio muheshimiwa, nitakupatia hayo majina yote leo, na nifanya kama alivyosema mtaalamu,…ndio nakusanya habari zote mkuu, na sasa napitia jina moja baada ya jingine, siunajua tena muheshimiwa…, siwezi kukuletea kazi isiyokuwa na maelezo ya kutosha na ushahidi…’akasema na kusikiliza.

‘Ndio…nilikuambia, na ndivyo itakuwa,…nimemwambia mpiga mbiu asema hivyo, ndio, nia ni kutokuwachanganya zaidi wananchi wetu…ila nilichotaka ni ili na wao wawe na uhakika kuwa kazi tunayoifanya ni ya uhakika kwa ajili yao, najua bado lakini hii ni mbinu na hatua muhimu kwetu..…’ akatulia.

‘Ndio ...muheshimiwa hizi ni mbinu za kijeshi mkuu, ukisema hivyo, hata hao maadui wataogopa…sio kuwadanganya wanachi….niamini mkuu’akasema.

‘Ndio muheshimiwa,...nimemwambia mpiga mbiu awaambia wnanchi kuhusu huyo mtaalamu,..unafahamu kijiji changu wanaamini sana wataalamu...hata hivyo kauli ya mtaalamu haisaidii kitu, ni lazima kwanza tukusanye ushahidi,...yeye ana kipaji cha kuona mbali,...'akatulia.

'Hizo pia ni mbinu zetu mkuu,... ujue hao watu tunaopambana nao ni wasomi, wana viona mbali wana mawakili,..wana kila kitu…sasa, na sisi nia yetu ni kuwaonyesha kuwa tuna mbinu za kila namna,...hata hivyo  hatuwezi kutegemea kauli ya mtaalamu pekee…’akatulia.

‘Hapana mkuu sikukudanganya, huyu ni mtaalamu kweli…namfahamu, nimeshamlipa, nia ni kuwaweka wananchi sawa, ...kwa imani zao watarizika kabisa,..…na sisi bado tunafanya akzi zetu...unajua hata hao maadui zetu, wanatumia mbinu hizo,...wanakwenda kwa hao watu,...ndio mkuu yeye anaendelea kufanya kazi yake, anaaminika sana..…’akasema.

‘Kama alivyosema mtaalamu, huyo mtu sifa zake ndio hizo, sisi katurahisishia kazi,...kazi ni kumkamata tu, hata hivyo hatuwezi kwenda kwa hao,...moja kwa moja, tunachukua hatua stahiki,na tutahakikisha kila kitu kinakwenda sawa, siku akifika mahakamani,..…’akasema na kukatizwa.

‘Kama ndio huyo tuliyekuwa tunamshuku, basi…hapana shaka muheshimiwa, wapo wengi, lakini huyo mkuu wao,...ndio muheshimiwa,.. mtaalamu kafanya kazi yake vyema, iliyobakia ni yetu,....’akatulia

‘Bado mkuu,… hatujawahi kumuona…. Tunamsikia tu…. na sifa alizotaja mtaalamu ni hizo hizo, ….ngoja tulifanyie kazi kwanza…ninajua mkuu, tukifanikiwa hili wananchi watakuwa na imani kwetu sana…..,…ninajua ni kazi nzito,..na ya hatari, waliojaribu awali, yaliwapata makubwa, lakini sisi tuna jua ni nini tunachokifanya mkuu…ngoja nilifanyie kazi, niamini mimi  muheshimiwa....ndio muheshimiwa, ahsante...’akasema na kukata simu.

  Mkuu huyu aliweka simu huku jasho likimtoka, aliangalia kipoozeo cha joto kama kinafanya kazi, akakuta kipo mpaka namba ya mwisho, akasogea hadi kwenye jokofu akachukua maji baridi, akachanganya na barafu akanywa, ….

‘Ohuuu….sasa huu mtihani,…lakini hakishindiki kitu….hii kazi nitaimaliza mimi mwenyewe…..hawataamini….’akasema huku akiangalia saa, kwa muda huo walitakiwa vijana wake wawe wameshafika kutoa taarifa alizowaagiza...na ghafla simu yake kutoka kwa katibu muhutasi wake ikaita.

‘Haloo, nilikuambia nipo bize..sitaki mgeni….’akasema akitaka kukata simu.

‘Ni wale watu uliosema kuwa kama wana taarifa waje wakuone wewe mwenyewe…’akasema katibu wake.

‘Ehee..ndio ndio..wapo wangapi?….’ akauliza.

‘Basi mpeleke chumba maalumu…..’akasema huku akikumbuka maneno ya mkuu wake
Ngoja, niishie hapa kidogo, maana kutumia simu huwezi kuandika maneno mengi, jembe langu limeharibika,..na kazi nyingi zilikuwa humo,….lakini sijakata tamaa, tupo pamoja.


WAZO LA LEO: Sio kila anayekuchekea ana mema na wewe,..sio kila linaloongelewa lina mantiki. Muhimu ni kufanya uchunguzi, kuweka subira na kuhakikisha unatenda kweli, haki na sahihi….
Ni mimi: emu-three

No comments :