Mapenzi ni kitu cha
ajabu sana, unaweza ukapenda kitu kwasababu ndogo tu., au ukachukia kitu
kwasababu ndogo tu, na chuki inaweza pia kubadilika na kuwa upendo, upendo huo ukawa wa dhati kupindukia.
Siku ya kwanza ikapita
taratibu, ikaja siku ya pili, ya tatu,…sasa nikawa siwezi kuvumilia tena, nikachukua
simu na kuanza kupiga, simu yam dada ikawa haipatikani,…kwanini simu yake
haipatikani na mimi ninajua haina matatizo yoyote,nikawa kila mara najaribu
lakini ilikuwa kimia…, nikawa najiuliza bila kupata jibu.
Kwanza
nikawasiliana na docta, maana yeye ndio anawafahamu vyema huko kijini, mkewe
anatokea huko..nilitaka wajaribu kufuatilia, ni nini kinachoendelea, na jirani
yangu huyu…, docta akaniambia nitulie tu, nivute subira..
‘Wewe una wasiwasi
gani, subiria kwanza…kuna mambo yatakuwa yanaendelea huko kijijini, shemeji
yako anafuatilia kwa karibu, nitakujulisha mambo yakiwa tayari ’akasema docta,
kumbe alishajua ni nini kinachoendelea.
Mimi nikamuuliza
docta;
‘Je wakimlazimisha huyo
binti kuolewa na hao watu wa huko kijini itakuwaje, wakumbuek kuwa wao ndio
walimsikia mke wngu akitaka mimi nimuoe huyo binti, na wao wameshindwa
kuwashawishi hao wazazi…na ilitakiwa wao waende huko wakamsaidie huyo binti
maana nijuavyo mimi, huyo binti hawezi kuwakaidi wazazi wake...?’ Nikamuuliza
docta na docta kwanza akacheka kwa mdhaha na kusema;
‘Sikiliza ndigu
yangu kwanza hiyo sio kazi yetu, kazi yetu ilikuwa kusema ukweli, na ilitakiwa
wewe ndio ufanya juhudi hizo toka awali..lakini hata hivyo, unawasi wasi gani,
tusubirie matokea, huwezi kulazimisha hali halisi..mungu anajua zaidi…’akasema
docta.
‘Kwani shemeji si
yuko huko kijini anasemaje…?’ nikamuuliza
‘Anasema ….kuna
vikao vya kila siku vya wazazi....na ni kawaida lakini, hasa kwa binti kama
huyo ambaye wengi wamekuwa wakimtaka,…wazazi wanatamani vijana wao wamuoe binti
kama huyo, kutokana na tabia yake…’ akasema docta.
‘Sasa kweli mimi
watanikubalia…maana wananifahamu, ..lakini hawanifahami nilivyobadilika,..docta
mimi nimebadilika kabisa, na siwezi kurejea tabia yangu ya zamani kamwe..hilo
naapa…’nikasema
‘Mimi ninajua,
lakini je wale wazee wanakufahamu hivyo…?’ akaniuliza
‘Sasa wewe nisaidie kwa hilo …’nikasema
‘Mimi wakinihitajia …nitajaribu kukutetea..., lakini siwezi kukuahidi moja kwa moja, unajua tena hicho ni
kikao cha wazazi, wao kama wazazi wanajaribu kuona ni nani muhimu kwa binti yao...ila mimi nitajitahidi, hata semeji yako yuko huko anajaribu kadri ya uwezo wake, lakini mara nyingi, ....mtu baki hasikilizwi sana...muhimu kwasasa ni wewe umtegemee
mungu wako tu, wewe ushaiva kiimani kwanini unalegeza imani yako…’akasema
docta.
‘Oh…lakini ni
lazima hapo nifanye juhudi ya kuwaaminisha kuwa kweli nina nia hiyo ya kumuoa binti yao, na mimi nimeshabadilika sio mimi yule wa zamani....ujue mimi sijapeleka mshenga wala kitu chohote zaidi ya kauli ya binti...'nikasema
'Ndio najua...'akasema docta
'Sasa wewe huoni hapo kuwa mimi na nyie kama ...wewe uwe mshenga wangu mnisaidie twende huko kijijini, nikajitambulishe kwanza, unaona eeeh….’nikasema
'Mhh...mimi naona bado...ngoja kwanza....'akasema docta
'Ningoje, wakati wenzangu wameshajitambulisha, naisikia na wengine walishaanza kutoa vitangulizi, unajua wazee wa kule..ukitoa zawadi zawadi wanakuthamini...sasa mimi sijafanya hivyo...'nikasema
'Wewe usijali bwana,...hata wakitoa, kama binti hataki je....mimi nina imani huyo binti sasa hivi anakutaka wewe....'akasema docta..hapo mimi niliona docta halichukulii kwa uzito wake, kama walivyokuwa
wakinishawishi awali, nikahisi kuna jambo jingine limajificha, hawataki tu
kuaniambia, na akili yangu ya haraka haraka ikahidi huenda ni hali yangu ya
afya, huenda vipimo
‘Muda utasema
jirani yangu, wewe vuta subira,….wala usijali…kama huyo binti kapangiwa kuwa ni
wako ni wako tu…’akasema hivyo docta, niliona kama yeye hajali,hajui ni kiasi
gani napata shida!
**********
‘Rafiki yangu, duwa
ya…kumuomba mungu,ni silaha kubwa kwetu,wengi wetu hatulijui hilo, utasema
mbona kila siku naomba, namuomba mungu…lakini je unamuombaje mola wako, maana
kila mtu anaomba hata jambazi anaomba akienda kuiba au sio,…. Hebu kihalisia,
tujaribu kujiuliza utakwendaje kuomba kazi kwa bosi fulani ukiwa mchafu, unaweza kufanya hivyo kweli…huo
ndio mfano wetu kwa mambo dhahiri ya hapa duniani,..
Ninajua kwa mwenyezi mungu yeye haangalii miili yetu,usafi
wa miili yetu na mavazi yetu…zaidi ni usafi wa mioyo yetu, uchamungu wetu…, ile
ile nafsi inayotuamrisha tufanye hiki na kile ndiyo mola wetu anaiangalia zaidi,
je imetii maagizo yake, tumeweza kuidhiti hiyo nafsi….,umeonaeeh…’akasema rafiki
yangu akiendelea kunihadithia kisa chake…
‘ Na mimi mungu
akanijalia nikawa nacheza na hiyo nafsi,…na kama ulivyoona nilianza kwa kutubia,
kufunga kukesha na ilikuwa ni toba ya ukweli ya kutoka moyoni, na hiyo haikuwa
kazi rahisi kama ninavyoongea hapa…unaweza ukasema hapa mdomoni tu, nimetubu,
nimemuomba mungu wangu, nimeokoka, mimi ni msafi….lakini vitendoni ipo kazi,…ni
kazi kubwa sana, na nafsi zetu ni kichaka na uhalisia, na hatuwezi kumdanganya
mola wetu…’akatulia akitabasamu kidogo
‘Mhhh..sasa ilikuwaje
huyo binti alikupigia kuwa imekuwaje, au ilikuwaje, .?’ Nikamuuliza, nilipoona
haendi moja kwa moja kwenye tukio lenyewe.
*************
‘Hahaha.., anipiigie
simu mimi…wakati alipofika simu ikachukuliwa, wazazi wengine wakorofi…kiukweli…haikuwa
kazi rahisi kwa huyo binti, na ilifikia muda, akasalimu amri, na ikabidi
ayafuate matakwa ya wazazi wake…’akasema
‘Kwahiyo ina maana
hukuwahi kumuoa huyo binti…?’ nikamuuliza na hapo akakunja uso, kuashiria
huzuni na huku akitabasamu pia, akasema;
‘Ilikuwa tukio la
namna yake, na hapo ndio utafahamu toba ya kweli ilivyo..huyo binti alikubali
kweli amri ya wazazi wake,…na ikapangwa ndoa, kabisa, akawa hana jinsi,
akaridhia kuwa sasa anaolewa na chaguo la wazazi wake, na taarifa hiyo
nikaipata,…na hata docta akaipata ndio akaja kwangu kunipa moyo, maana alijua
nitakasirika sana, ninaweza kufanya mambo ya ajabu.
Ni kweli, taarifa
hiyo ilinivunja nguvu kabisa, kwanza nilijilaumu kwanini nilimruhusu huyo binti
aondoke, ni kwanini….ikawa nanilaumu kwa kila kitu…na hata kuwalaumu docta kwa vile hawakutaka tulichukulie kwa uzito wake, lakini docta akaniambia
‘Kiukweli hali
ilipofika, hatuna jinsi….inabidi tu tukubaliane na hali halisi, …’akasema docta
‘Hapana mimi
siwezi..ni lazima nifanya jambo, …yawezekana ni kwa vile mimi sijaenda huko…ni
kwa vile sijatoa chochote….’nikasema
‘Wewe usijali, kama
sio halali yako huwezi kuilazimisha, na wazazi wana mashaka na hali yako ya
kiafya ,..hatuwezi kuwaumu kwa hilo,..ila bado hawajafikia uamuzi, ngoja
tusubirie kwanza,..’akasema
‘Kwa vipi, …?’
nikamuuliza
‘Ninajua wao
wanaweza kunipigia simu,…wanaiulize kuhusu wewe mimi siwezi kuwaaambia lolote zaidi,
si unajua tena… naweza kukubali kuwa wewe umepona laini je nina uhakika gani kuwa umepona kweli,…maana vipimo vyako bado havijakubaliana na kauli hiyo, ndio maana hata mimi navuta subira, tuone mbeleni itakuwaje...bado kuna walakini..mimi naona
tusubirie tu…’alasema docta.
‘Kwahiyo unataka
kusema nini, kuwa wao wamepitisha hayo kuwa mimi ni mgonjwa, siwezi kuzaa au
sio…je wao, wana uhakika gani, wanajua matakwa ya mungu, mimi siwezi kukubaliani
na hilo ndio maana mimi ninataka kwenda kuonana na wao , ili niwathibitishie
kuwa mimi nimepona…’nikasema
‘Una uhakika gani
kuwa umepona, maana vipimo bado havionyeshe hivyo, ila kuna dalili kuwa
umepona, unanielewa hapo…?’ akaniuliza docta
‘Kwani vipimo
vyangu vinasemaje, kuna dalili kuna dalili, mbona unaitia mashaka, mbona mwanzoni ulinipa matumaini kuwa nimepona…?’ nikamuuliza docta na docta hakuweza kunipatia jibu la moja
kwa moja, lakini mimi nilishajiona nimepona, sikuwa na shaka na hilo, na sikuweza
kusibiria kama alivyosema docta , mimi kesho yake, nikafunga safari kwenda huko
kijijini kabla ili niweze kumshawishi huyo binti,, lakini sikuweza kuipata
nafasi hiyo.
Ndugu yangu kuna
mlolongo ulitokea, kuna mengi yalitokea, na naona kuna umuhimu wa kuyasimulia hayo kwa manufaa yetu, na vizazi vyetu. Tutasimulia kidogo tu ilivyotokea na na ndio itakuwa hitimisho la kisa chetu,....mungu akipenda.…’akasema msimuliaji
NB: Haya,..ndio hivyo,...tukae mkao wa
kula ili tupate hitimisho la kisa hiki, sikuweza kukimalizia kisa hiki kwa leo,maana jino linanisumbua,…tukutane kwenye hitimisho mungu akipenda
WAZO LA LEO: Wakati mwingine inabidi tukubaliane na hali halisi, ..wakati
mwingine hali halisi inatokea nia ni kutupima jinsi gani tulivyo, na huenda
ikawa ni kwa manufaa yetu , au ni mtihani tu, tukitulia na kufanya subira
tunaweza kupata kile tunachotaka kwa muda muafaka
Kwahiyo likitokea
jambo, likawa linakwenda kinyume na matakwa yetu, tusikimbilie kulaani,
kulalamika, kulia, na hata kukufuru, na wengine hujenga chuki kabisa, na
kumchukia kila mtu..muhimu …tuache hali halisi ifanye kazi yake na
mwenyezimungu anajua zaidi.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment