Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 20, 2015

NANI KAMA MAMA-47Nesi akiwa ameinama akiwa kazama kwenye mawazo, lakini pia akiongea, kumuongelesha docta, cha ajabu akawa hapati jibu kutoka kwa docta,  akainua kichwa, na  kuangalia pale alipokuwa kasimama dakitari kijana….

Moyo ukamlipuka phaaa, kwanza hakumuona huyo dakitari,…dakitari alikuwa keshaondoka zamani, lakini pale pale alipokuwa kasimama dakitari kijana, akawa yupo mtu mwingine kasimama hapo…

Mtu aliyesimama hapo hakutaka kabisa kukutana naye, ..kwanza keshaambiwa mtu huyo kapewa jukumu la kumchunguza, kuona kwamba je kupotea kwa huyo mama ni uzembe wa utendaji au ni bahati, je nesi huyo anamambo gani anayofanya kipindi cha kazi,…

Na hapo hapo…muda mchache uliopita dakitai kijana alishamuambia kuwa nesi mkuu huyo yupo karibu anafuatilia nyendo zake,..je alishasikia hayo waliyokuwa wakiongea, je aliona kile kitendo alichokifana cha kumkumbatia dakitari kijana.

Akajikuta wanaangalia na huyo mdada, bosi wake mkuu wa manesi, na hasimu wake mkuu…mwili ukaishiria kuishiwa nguvu, na yule nesi kama kawaida yake akatoa tabasamu la kejeli huku akitkisa kichwa kuthibitisha kitu…..

Tuendelee na kisa chetu.

***********‘Mhh….sasa umemua …yale uliyokuwa ukifanya kwa siri sasa mumeamua kuyaonyesha hadharani, au sio..hebu angalia muda mliosimama hapa na huyo bosi wako, ..watu wanamtafuta huyo anayeitwa dakitari kijana,  haonekani wapi alipo, kumbe mpo huku mumekumbatiana kwa mahaba…’akasema nesi mkuu.

‘Hapana bosi…’akajitetea nesi

‘Hapana bosi..ina maana mimi ni muongo….Na kwanza wewe si ulitakiwa uje kwangu…unieleze taratibu zako za kuondoka, nimekusubiria ofisni kwangu masaa, huonekani…unataka kuonyesha nini, kuwa wewe hujali au sio…hili lililotokea kwako ni sawa tu , hujali..maana sasa umepata mume; `handsome boy’…dakitari kijana au sio..’akasema huyo nesi mkuu.

‘Sio hivyo sister,..sio hivyo bosi…’akasema akionyesha wasiwasi.

‘Nimewaona..muda mreu tu…, na nimekusikia kwa masikio yangu mwenyewe…na sasa hivi nimekusikia, ukiendelea kuota ndoto za mchana…’akasema


‘Bosi nilikuwa naongea tu…’akasema

‘Binti nakuambia hivi, kazi sivyo inavyotakiwa hivyo..unasikia, kazi siku hizi ni ngumu sana kuzipata ukishaikosa ujue utalia na kusaga mawe, ukisingizia una bahati mbaya, kumbe bahati mbaya umejitakia mwenyewe…’akawa sasa anamsogelea, na huyu binti akawa anarudi nyuma.

‘Hahaha sasa unajifanya muoga sio.., wakati muda mchache uliopita ulijipeleka mwenyewe kwenye kifua cha yule mnafiki….unajua nimekumind sana wewe binti...sasa sikiliza, mimi nimeshapata ushahidi wa kutosha kukufukuzisha kazi, …’akasema huku akiwa anaangalia simu yake kama vile anataka kumuonyesha kitu huyo binti

‘Kwani mimi nimefanya nini..bosi?’ akauliza nesi akimuangalai huyo nesi mkuu kwa macho yenye kutahayari.

‘Utaona hilo siku hiyo ikifika…na jiandae...sijui utakwepaje kwenda jela, maana kuna taarifa zimesikika, ni za utata lakini inawezekaan ikawa ni kweli….sitaki kukuambia ni tetesi gani kwa hivi sasa, ..lakini ni mbaya…’akasema

‘Taarifa gani bosi….nimefanya nini tena..?’akauliza.

‘Wewe siunajifanya hutaki kuwa karibu na mimi, hebu waulize wenzako tunaoshirikiana nao, wote hapa wananiona mimi ni dada yao mpenzi..wewe tu na roho zako mbaya,….wote hapa kazini, ni kama wadogo zangu tu…nawasaidia, na nikihisi kuna baya najaribu kutafuta mbinu za kuwasaidia..lakini wewe na huyo mnafiki wako….mumenotoka…kabisa kabisaaah…’akasema nesi mkuu akiwa kashika kiuno.

‘Lakini bosi mbona sijakufanyia lolote baya..’akasema kwa kujitetea.

‘Unasikia, huyo mnafiki wako, ..anafikia kunisema kwa wakubwa kuwa mimi nafanya mambo ya ajabu ajabu, na wasichana..eti sijui mimi …eti…sijui miiko ya kazi, mimi sijui miiko ya kazi, miiko gani nisyoijua mimi…’akashika kiuono huku akijitingisha kwa nyodo.

‘Lakini huo ni umbea tu..dakitari kijana hana tabia hiyo, yeye muda wote yupo na kazi..’akamtetea dakitari kijana.

‘Hahaha wewe unamtetea, hujui mimi nina masikio marefu, yanasikia kila kitu kinachoongelewa humu hospitalini…naona kila kona ya sehemu hii ya kazi..leo hii eti anakuja kunifundisha kazi mimi…anajua nimeanzia wapi kazi,…’akasema akionyesha kukasirika.

‘Mimi nimeanza kazi huko hospitali ya rufaa, hadi wakanipandisha cheo, nimenzia kwenye kufagia…kutumwa tumwa..kwa utundu wangu nikajiunza mengi…nikapelekwa shule….hivi mnafikiri hiki cheo nimepewa bure bure tu….wakubwa wote wananiheshimu mimi..’akasema

‘Hata mimi nakuheshimu….sana bosi..’akasema nesi kwa sauti ya unyonge.

‘Huyo hawara wako…huyo..huyooo , yeye kaja hapa anajifanya anajua saana, msomi, na udakitari wenyewe baado, basi hicho kidogo alichokipta anajiona kaiva…a wapi, mabingwa wenyewe hawajioni  hivyo…anajiona mrembo, mwanaume utakuwa hivyo usharobaro…wapi na wapi,…na hata sijui kama ni mwanaume kweli…nikuambie ukweli kama mdogo huyo atakupotezea muda wako bure, tafuta mume wa kweli, sio huyo…’akasema  akiwa kama ananong’ona.

‘Lakini sister, mimi naona….’akawa anataka kuongea, lakini huyo bosi wake akamkatiza na kusema;

‘Tafuta mume..huyo sio mwanaume…na nakuambia ukweli, huyo kwangu amefika,  ataniona mimi ni nani, mwenyewe ataikimia ii hospitali..na hatarudi tena hapa…na wewe kinyamkera wake…utarudi kijijini….’akasema.

‘Kwani mimi nimefanya nini?’ akauliza nesi, sasa akionyesha wasiwasi mkubwa zaidi.

‘Hahahaha, kwani wewe umefanya nini eehee, unajifanya hujui eeh, huyo mama aliyetooroka yupo wapi, hebu niambie kama angekuwa mtu mwingine sasa hivi si yupo jela, keshafikuzwa kazi, lakini nyie myai..watoto wa mabosi, mnalelewatu, hilo sikubali…’akasema

‘Lakini mimi sina ndugu yoyote hapa hospitalini ambaye ni bosi…’akajitetea nesi.

‘Mimi nimekuuliza huyo mama wa watu yupo wapi, huoni kuw aumefanya kosa kubwa sana…hebu niambie isku ile wakati huyo mama anatoroka ulikuwa wapi,…?’ akawa anauliza

‘Ni kosa kubwa sana ulilolifanya..halafu watu wengine wanakutetea,..hapana hili halikubaliki…’akasema

‘Lakini ni bahati mbaya, sikujua…’akasema

‘Ni bahati mbaya…mimi mwenyewe nilikuona, …nilikufuatilia wakati unatoka pale kwenye chumba hadi unakwenda huko kwa yule rafiki yako mkaanza kupiga soga za umbea…za kutaka wanaume…yote hayo nayafahamu…halafu ukatoka pale ukaenda wapi? Sema mwenyewe, moyo unapwita, unataka umuone sharobaro wako….’akasema

‘Hapana bosi nilipotoka pale nilikwenda, nilipitia tu, kuona…’akasita

‘Unanifanya mimi ni mtoto… wewe si ulikuwa unamchungulia huyo hawara wako dirishani, kwanza nikashutua, na hata ukikataa kuwa sikukuona, mimi nina shahidi wote, sifanyi vitu kwa fitina…ushaidi ninao…hapa….’akasema huku akiinua simu yake juu

‘Bosi hayo yamekujaje….mbona sikuelewi…nakuomba tafadhali nipo chini ya miguu yako…usiwaonyeshe wakubwa, nitafukuzwa kazi…na nimeshakubali kumchukua mtoto, sasa ukianzisha mengine,….nitafukuzwa kazi…’akasema nesi akitaka kupiga magoti.

‘Hahaha…umeonaeeh, sasa unajifanya unaogopa, siku zote unajifanya kichwa maji,..sasa utaingia kwenye anga zangu, ….na bado…utajua kuwa mimi ni nani, mimi nawaenga, taratibu, ukiengeka, aah, tupo pamoja lakini wewe na huyo mnafiki, sitawavumilia tena, lazima mnielewa tu…hilo nimeahidi…’akasema

‘Lakini bosi kwani tumefanya nini…mimi hapa tulikuwa tunongea jinsi gani nitaweza kumlea huyo mtoto na wakati natakiwa kazini, kwahiyo akawa anajaribu kunielekeza na kunipa ushauri, kutokana na ushauri wake nikafurahi, ndio nika..nika…….’akasema

‘Hahahaha…mbona humalizii, ukamkumbatai na kuanza kulana mate..si ndivyo mnavyosema nyie wasomi…hebu angalia hapa…’akawa anaonyesha picha kwenye simu yake.

‘Umeiona hii picha, hivi kweli,..ni nani hataamini kuwa nyie ni wapenzi mnafanya mapenzi sehemu ya kazi..hivi utamdanganya nani..hivi ehe eti waonyesha ishara ya kumshukuru, wakati macho yamelendemka, mweeeh, kama umekula kungu. …hahaha, hivi waniona mimi wa juzi ehe…chunga hiki kitu kingine..’akasema huku akimkazia macho huku akidi kuonyesha lile tukio kwenye simu yake na nesi akabakia kaduwaa , katoa macho ya uwoga.

‘Bosi basi naomba samahani…nitafanya chochote unachokitaka..unataka nifanye nini..naomba ufute kabisa hilo….naomba tafadhali…unataka nikufanyia nini nesi..?’ akauliza nesi.

‘Unajau mimi sina ubaya na yoyote yule..muhimu mniheshimu…muhimu mnione mimi ni mkubwa wenu, sipendi kabisa madharau…na kuniona mimi eti sijasoma, eti nimepewa kazi tu kwa vile ni uzoeu t, najuana na wakubwa tu…mimi sijuani na yoyote yule wanachofanya ni kujali utendaji wangu…’akasema

‘Sasa sikiliza hizo dharau zenu..sizitaki,..sitaki..sitaki mtu kunidharau kunyodo…, ‘akasema na nesi akawa anafuta machozi,…kuonesha kuwa analia.

‘Sasa  unaoneeh..hujalai bado, utalia…nakuambia ukweli..’akasema

‘Bosi naomba unisamehe…’akasema

‘Mhh..nikusamehe,..mimi sina uwezo huo…nyie wasomi ndio mnajua kujitetea,..muda ukiika utajitetea,…maana mimi sijasoma, sijui sheria eeh, miaka mingapi nimefanya mimi, nisijue…., sasa kama mimi sijasoma nimepewa kazi kwa sababu ya hivyo mnavyosema, sasa nataka kuwaonyesha kuwa mimi nimesoma…hii imetoka wapi..hebu angalia….’akasema huku akiendelea kuonyesha hilo tukio kweny esimu yake.

‘Nyie mnaojiita wasomo…mnakuja na yenu, …angalia jinsi gani  mnavyoharibu maadili ya kazi, halafu eti huyo hawara wako anasema mimi ndio sijui maadili, sasa aseme mimi na yeye ni nani anaharibu maadili..’akasema

‘Lakini mimi sijasema hujasoma…’akasema

‘Nyie…hasa mlitoka vyuoni huko, …ambao mnajifanya wasomi..si ndio…mnajifanya nyie ni tofauti..hahaha, sasa mumepatikana mtajua mini ni nani…ni lazima mje kwangu mnipigie magoti na muonyeshe hizo ngebe zenu..nataka niwaone kweli kama nyie ni vibikira..hahaha…wakati mumekubuhu…na hata kufundwa hamjafundwa…mna…nyie nyie…’akasema na kupita pale aliposimama nesi, na jinsi alivyopita, kwa tambo, akampiga kikumbo huyo nesi na nesi akaishia kutaka kudondoka chini.

Kuna taarifa za kutataisha kuhusu huyo mama..ni taarifa gani….’ nesi akawa anatembea kuelekea sehemu wanapohifadhiwa watoto tayari kumchukua huyo mtoto na kuelekea kijijini, hakutaka kusubiri zaidi,hakutaka kuja kukutana na huyo bosi wake tena..lakini hata hivyo alitaka kuonana na dakitari kijana amuelezee hayo aliyoyasikia, ili awe na tahadhari

Haikuwa rahisi kumpata dakitari kijana, kwani kulikuwa na wagonjwa wa dharura wengi, dakitari kijana akawa muda mwingi yupo chumba cha upasuaji akitoka hapo anaingia chumba walipolazwa wagonjwa mahututi….hana muda kabisa, akaona hilo halitawezekana, na simu yake muda wote imezimwa…

**********

Nesi akakutana na mtu anayesimamia watoto, na mtoto akafanyiwa utaratibu wote ikiwemo na vipimo kuhakikisha kuwa yupo salama, kabla hajakabidhiwa, na zoezi hilo lilipokamilika, kwa haraka akakabidhiwa mtoto ..na mama mkunga na msaidizi wake,

Kwa muda ule,  bosi wake hakuwepo yaani nesi mkuu…na kwahiyo jukumu hilo akalichukua mama mkunga na msaidizi wake wakawa wamempataka yule mtoto wakimuangalia na kuongea mawili , matatu, kabla hawajamkabidhi nesi , na mama mkunga akasema;

‘Unamuona mtoto alivyo na afya, mnzuri..hana tatizo lolote, sasa sisi tunakukabidi, tunakutakia ulezi mwema..unasikia..’akaambiwa

‘Ndio mama mkunga…’akasema

‘Kama ilivyokubalika na wewe kukubali kubeba hili jukumu, sasa mchukue mtoto awe kwenye mamlaka yako, na uhakikishe anapata huduma zote…na mengine utakuja kuambiwa ..kama una lolote unaweza kusema …’ akaambiwa na kukabidhiwa mtoto.

‘Mhh kwa hivi sasa sina..’akasema

‘Haya mchukue mwanao, kila laheri…’akaambiwa na kukabidiwa huyo mtoto

Basi yeye akamchukua yule mtoto na usafiri alishapewa, akatoka nye nje kuondoka, ikiwa na isafari ya kwenda kijijini, kumpeleka huyo mtoto kwa dada yake, akijua kabisa ndugu yake atamkubalia.

Akawa sasa anaingia kwenye gari, mara kwa mbali akamuona dakitari kijana,…akamuomba dereva kwanza akaagane na dakitari huyo, akatoka na kumuendea.

Dakitari kijana alikuwa hajamuona, hadi alipofika kariu yake, akageuka na kumuangalia nesi huyo akiwa na mtoto, akamsogelea na kumuangalia mtoto, akasema;

‘Mhh, ..ndio umemchukua kwahiyo sasa hivi unakwenda wapi?’

‘Docta mimi ndio naondoka kwenda kijijini..’akasema

‘Ok, ..basi ki-laheri, najua utafanikiwa huko uendapo..’akasema dakitari huyo

‘Yah..i hope so…sina shaka na ndugu zangu…’akasema nesi

‘Ok, basi tutawasiliana, au ukirudi tutaongea, usijali, tupo pamoja…’akasema na hawakuweza kuongea zaidi, maana dakitari huyo alikuwa na haraka, na nesi akiwa karizika na ile kauli ya dakitari akajua sasa kweli wapo pamoja, na akirudi tu kutoka huko kijijini, anakuja kuongea naye, na atajitahidi amuonyeshe kuwa kweli ana nina njema kwake.

***********
 Siku aliporejea hospitalini, alikuwa na raha, na aliona kuwa tukio hilo la huyo mtoto na mama yake ndio njia muhimu, itakayomfanya waweze kuwa karibu zaidi na huyo dakitari na akaona aitumie njia hiyo hiyo, ….

‘Ni lazima kila siku nimfahamishe ni nini kinaendelea huko kijijini, ajue kuwa mtoto yupo mikono salama..na najua kwa njia hiyo nitaweza kuwa naye karibu zaidi..’akasema

Basi…siku hiyo alipotoka kijijini, alikuwa hana jingine kichwani  zaidi ya kumuwaza dakitari kijana… Aliwaza jinsi gani akikutana naye atakavyomchangamkia na kumshukuru sana kwa kumsadia na kuwasaidia ndugu zake…akawa kamnunulia zawadi za kijijini....na kila hatua tabasamu lilikuwa likimtooka mdomoni..

Alifika hospitalini akasalimiana na wenzake, na kila mmoja akijaribu kumuuliza jinsi gani atakavyoweza kumlea yule mtoto, au imekuwaje…na maswali mengi ambayo kwake aliona ni ya kumpotezea muda. Aliwajibu kwa mkato tu..

Basi alipomalizana kusalimiana na wenzake, kwa haraka akaondoka kuelekea chumba cha madakitari bingwa, ili akamuone dakitari kijana.  Hakujali cha nesi mkuu…na alipopita ofisi ya nei mkuu, akamkuta msaidizi wake, akamuuliza nesi mkuu yupo wapi, akaambiwa yupo mapumzikoni, kapatwa na dharura…

‘Yesss..’akajikuta akisema

‘Vipi huko ulipotoka…?’ akaulizwa

‘Salama kabisa, nimeshamikisha mtoto na ndugu yangu yupo tayari kuwa naye, ..na mengine ..ni ya kawaida tu..’akasema

‘Sawa…muhimu ni kujua yupo salama, na mengine…mmm, sio muongeaji sana…wewe nenda kajiweke sawa, karibu kazini..’akaambiwa na yule nesi msaidizi wa nei mkuu akawa anatoka nje.

‘Samahani nimeitwa huko kwa mkuu,…kwa dakitari mkuu, naona maemo yameiva..’akasema

‘Mambo gani tena..’akauliza

‘Mhh, si ya kzi tena…yaani kaondoka mwenzangu kaniachia misala…baadaye nina haraka..’akasema na kuondoka, na nesi akashukuru maana akutaka kukaa hapo muda mrafu kwani alikuwa na yake.

Akiwa sasa anajiamini maana muhasimu wake hayupo akatembea kuelekea ofisi ya anayokaa dakitari kijana…akagonga na kuingia…, kwenye meza ya uyo dakitari kijana akamkuta dakitari mwingine mgeni, akashangaa.

‘Habari docta..’akasalimia

‘Njema nesi, nikusaidie nini..?’ akauliza huyo dakitari akiinua uso kwani alikuwa akiandika kitu kwenye karatsi na huyo dakitari alipotua macho yake kwa huyo nesi, akapitisha mkono usoni, na kuonyesha tabasamu.

‘Aaah, samahani nilikuwa nauliza…maana wakati naondoka ofisi hii alikuwa anatumia dakitari mwingine…na…nakuona wewe..’akasema
‘Oooh, unasema dakitari kijana..hayupo,…kaondoka..’akasema

‘Kaondoka, kaenda nyumbani, ..kwani leo yupo mapumziko?’ akauliza

‘Mhh, hapana, mimi mwenyewe niliika tu, ..na hatukuweza kuongea naye sana, ila ni kuwa… imekuja barua ya dharura kaondoka asubuhi…, na huenda kesho anapanda ndege kwenda Ulaya…’akaambiwa.

Nesi aliposikia hivyo, alibakia kasimama, akili ikiwa sio yake tena,..., akabaki kaduwaa,..akawa anajiuliza ina maana uyo dakitaria alijua kwua anaondoka, na hakutaka kumuambia ukweli, kwanini…..akawa anajiuliza.

‘Lakini alisema bado muda wake wa kuondoka…?’ nesi akasema akionyesha kusikitika kabisa, na dakitari huyo mgeni akamuangalia kwa uso wa kushangaa, akasema;

‘Mimi sijui…maana nilifika hapa na yeye akawa anaunga funga, na kuniamia hivyo kuwa kapata barua ya dharura,a aliyokuwa akiisubiria, ila imekuja bila ya yeye kutarajia, lakini alishajiandaa…., kama vipi wasilina naye kwa simu..’akaambiwa

‘Simu yake haipatikani…’akasema nesi akiangalia simu yake na kujaribu kupiga hiyo namba ya dakitari kijana, na  hakupatikana.

‘Basi huenda ndio yupo kwenye maandalizi…ni kuwa inavyoonyesha, alishajiandaa na alijua muda wowote inaweza kutokea hivyo, kwahiyo…keshaondoka..anaondoka kesho kuelekea Dar, na akitokahapo, ndio saari….’akasema huyo dakitari mgeni.

‘Mhh, jamani mbona nina bahati mbaya..’akasema nesi akigeuka kuondoka, na yule dakitai mgeni akasema;

‘Bahati mbaya kwa vipi… mimi nimekuja kushika nafasi yake kama kuna lolote niambie mimi nitakusaidia,…kwanza, wewe ni nani, ooh, nimekumbuka ndio wewe, nimeambiwa umechukua likizoa ya dharura, tutakuwa wote, usijali..hivi unaitwa nani vile..?’ akauliza na nesi hakutaka hata kuongea zaidi, akatoka.

Alipofika nje, akamfuata rafiki yake, rafiki yake ambaye walishakosana kutokana an dakitari kijana, rafiki yake akisema kuwa yeye kamgeuka, badala ya kumsaidia alichokitaka , yeye kachukua nafasi hiyo na kumuibia mpenzi wake. Siku hiyo walizozana sana, hadi urafiki ukaisha.

‘Lakini sio mpenzi wako…’akasema siku hiyo akikumbuka ilivyokuwa.

‘Ina maana imefikia hivyo, unajuaje kuwa huyo  sio mpenzi wangu…unajuaje kuwa hatukutani huko nje…sikiliza mimi na wewe urafiki basi…’akaambiwa, na kweli kutoka siku hiyo wakawa hawaongei tena na huyo rafiki yake.

Leo hii akaona amuendee tu hana jinsi…., huenda kama ni kweli walikuwa marafiki wa siri..wanakutana baada ya saa za kazi kama alivyodai rafiki yake huyo kitu ambacho haamini,  basi atakuwa anafahamu lolote kuhusu dakitari kijana.

‘Shoga… sahamani najua umeshanisamehe au..?’akasema kwa kumuuliza rafiki yake , na rafiki yake akamuangalia kwa kumnyali, halau akatabasamu na kusema

‘Yah..najua..maana mtu mwenyewe keshaondoka, kwanini tugombane, ...kaniaga kwa busu kuwa anaondoka,..basi iliyobaki tutawasiliana kwa simu…’akasema

‘Kaondokaje?’ akauliza nesi huku akiwa kama haamini

‘Hahaha…kaondokaje, ni kama alivyokuja,..tuliobahatika basi….mimi nilikuambia wewe wakati unabonyeza ndizi kuwa imeva, wenzako tunaimenya na kuila…hahaha, wacheza na mie..hahaha…wewe kalagabahwe….na ujue nesi mkuu alikuwa anakulizia jana..’akasema

‘Kwanini ananiulizia, wakati anajua mimi nimeondoka kwa dharura..’akasema

‘Hivi umesikia kilichotokea..?’ akaulizwa shoga yake na nesi akamuangalai shoga wake wa zamani kutaka kusikia zaidi, akauliza;

‘Kuhusu nini?’ akauliza

‘Ina maana hujui,…?!’ akaulizwa shoga wake kwa mshangao

‘Kuhusu nini,..kuwa dakiari kijna kaondoka, ..hilo ndio nimesikia  hapo ofisini kwao…kwani kuna jingine..?’akauliza akionyesha wasiwasi.

‘Achana na yule mshamba, dakitari kijana, dakitari kijana…kuna jingine nzito, na…sijui utaokokaje safari hii,..’akasema shoga yake

‘Kwanini, jingine nzito lipi hilo?…kwani kumetokea nini?’ akauliza akionyesha wasiwasi, akihisi huenda bosi wake, nesi mkuu atakuwa kaeshapeleka umbea wake kwa wakubwa na huenda kuna taarifa za kufukuzwa kazi.

‘Mhh kama hujasikia basi….ngoja ninyamaze, mimi nisiwe mmbeya..maana hapa kazini siku hizi ni kila mtu kuchunga mzigo wake mwenyewe..’akasema shoga wake huyo akiendelea na shughuli zake

‘Shoga-yangu bwana niambiee kuna nini tena…mwenzako unaniweka roho juu..’akasema kwa sauti ya unyonge.

‘Mimi sikuambii…’akaonyesha kufunga mdomo kwa mkono, halafu akaondoa mkono mdomoni na kusema;

‘Na sikia..ule ushoga wetu ule wa enzi zileee…eeh,… wa kuambizana kila kitu sasa umekwisha, utabakia huo tu  wa kikazi, maana wewe sasa ni nuksi…unajau nuksi..wewe ni nuksi…tuachane kabisa’akasema

‘Ndio imekuwa hayo…’akasema nesi

‘Ndio hivyo…kaa mbali na mimi kabisa, usije kunitia hatiani buree…sitaki mambo ya kuitwa ushahidi, sitaki kabisa…’akasema

‘Ushahidi wa nini tena..?’ akauliza akiwa hataki kuondoka.

‘Utakuja kuambiwa bwana ondoka,…., mimi sitaki kuwa mpiga majungu , wewe nenda sehemu yak o ya kazi, najua kwa vyovyote utaitwa…..na ..sijui kwanini hujaitwa mpaka sasa...kwaheri..’akaambiwa na nesi akawa kashikwa na butwaa.

Kwanza akatulia na kujaribukumuangalia rafiki yake huyo wa zamani kama atamuonea huruma na kuambia lolote, lakini akaona hakuna dalili…baadaye akaona asipoteze muda akaondoka kuelekea sehemu yake ya kazi, na alipofika tu, akakuta ujumbe;

‘Ulikuwa unahitajiwa kwa mkuu wa hospitali…’akaambiwa

‘Una maana kwa Dakitari mkuu wa hopsitali, kuna nini tena huko..?’ akauliza

‘Hatujui tumeambiwa ukifika tu uende kwake kwa haraka..’akaambiwa na kabla hajakaa sawa, mara akaja mfanyakazi ambaye kazi yake ni kutumwa huku na kule akasema;

‘Nesi unaitwa ofisini kwa dakitari mkuu, haraka…’akaambiwa.


WAZO LA LEO: Kuna watu wanaona kuwa kuongea ni ufahari…kuzuliana, na kujiona wanajua zaidi, hata kama wanaloliongea hwana yakini nalo, lakini kwa vile ni wataalmu wa kuongea, kugushi, kuzua, umbea..fitina, basi wao wanajiona wameshinda. Na wengine ndio utaratibu wao wa maisha hata kipato wanachopata kinatokana na tabia hiyo chafu. ..huo ni wizi, na ni dhuluma. Tabia kama hizo ni ufinyu wa taaluma, huwezi kujinadi kuwa unajua au unatenda kazi hiyo kwa ufanisi wakati sio kweli..kwa hali hiyo utakuwa unajidangana mwenyewe. Maana njia za mnafiki huwa ni fupi sana, ipo siku utanasa na utaumbuka, kwanini usijiendeleze, ukasoma, ukajua zaidi, kuliko kujifanya unajua kumbe hujui…
Ni mimi: emu-three

No comments :