Nesi akiwa ameinama akiwa kazama kwenye
mawazo, lakini pia akiongea, kumuongelesha docta, cha ajabu akawa hapati jibu
kutoka kwa docta, akainua kichwa,
na kuangalia pale alipokuwa kasimama
dakitari kijana….
Moyo ukamlipuka phaaa, kwanza hakumuona
huyo dakitari,…dakitari alikuwa keshaondoka zamani, lakini pale pale alipokuwa
kasimama dakitari kijana, akawa yupo mtu mwingine kasimama hapo…
Mtu aliyesimama hapo hakutaka kabisa
kukutana naye, ..kwanza keshaambiwa mtu huyo kapewa jukumu la kumchunguza,
kuona kwamba je kupotea kwa huyo mama ni uzembe wa utendaji au ni bahati, je
nesi huyo anamambo gani anayofanya kipindi cha kazi,…
Na hapo hapo…muda mchache uliopita dakitai
kijana alishamuambia kuwa nesi mkuu huyo yupo karibu anafuatilia nyendo
zake,..je alishasikia hayo waliyokuwa wakiongea, je aliona kile kitendo
alichokifana cha kumkumbatia dakitari kijana.
Akajikuta wanaangalia na huyo mdada, bosi
wake mkuu wa manesi, na hasimu wake mkuu…mwili ukaishiria kuishiwa nguvu, na
yule nesi kama kawaida yake akatoa tabasamu la kejeli huku akitkisa kichwa
kuthibitisha kitu…..
Tuendelee na kisa chetu.
***********
‘Mhh….sasa umemua …yale uliyokuwa ukifanya kwa siri sasa mumeamua
kuyaonyesha hadharani, au sio..hebu angalia muda mliosimama hapa na huyo bosi
wako, ..watu wanamtafuta huyo anayeitwa dakitari kijana, haonekani wapi alipo, kumbe mpo huku
mumekumbatiana kwa mahaba…’akasema nesi mkuu.
‘Hapana bosi…’akajitetea nesi
‘Hapana bosi..ina maana mimi ni muongo….Na kwanza wewe si
ulitakiwa uje kwangu…unieleze taratibu zako za kuondoka, nimekusubiria ofisni
kwangu masaa, huonekani…unataka kuonyesha nini, kuwa wewe hujali au sio…hili
lililotokea kwako ni sawa tu , hujali..maana sasa umepata mume; `handsome boy’…dakitari kijana au
sio..’akasema huyo nesi mkuu.
‘Sio hivyo sister,..sio hivyo bosi…’akasema akionyesha wasiwasi.
‘Nimewaona..muda mreu tu…, na nimekusikia kwa masikio yangu
mwenyewe…na sasa hivi nimekusikia, ukiendelea kuota ndoto za mchana…’akasema
‘Bosi nilikuwa naongea tu…’akasema
‘Binti nakuambia hivi, kazi sivyo inavyotakiwa hivyo..unasikia,
kazi siku hizi ni ngumu sana kuzipata ukishaikosa ujue utalia na kusaga mawe,
ukisingizia una bahati mbaya, kumbe bahati mbaya umejitakia mwenyewe…’akawa
sasa anamsogelea, na huyu binti akawa anarudi nyuma.
‘Hahaha sasa unajifanya muoga sio.., wakati muda mchache uliopita
ulijipeleka mwenyewe kwenye kifua cha yule mnafiki….unajua nimekumind sana wewe binti...sasa sikiliza, mimi nimeshapata
ushahidi wa kutosha kukufukuzisha kazi, …’akasema huku akiwa anaangalia simu
yake kama vile anataka kumuonyesha kitu huyo binti
‘Kwani mimi nimefanya nini..bosi?’ akauliza nesi akimuangalai huyo
nesi mkuu kwa macho yenye kutahayari.
‘Utaona hilo siku hiyo ikifika…na jiandae...sijui utakwepaje
kwenda jela, maana kuna taarifa zimesikika, ni za utata lakini inawezekaan
ikawa ni kweli….sitaki kukuambia ni tetesi gani kwa hivi sasa, ..lakini ni
mbaya…’akasema
‘Taarifa gani bosi….nimefanya nini tena..?’akauliza.
‘Wewe siunajifanya hutaki kuwa karibu na mimi, hebu waulize
wenzako tunaoshirikiana nao, wote hapa wananiona mimi ni dada yao mpenzi..wewe
tu na roho zako mbaya,….wote hapa kazini, ni kama wadogo zangu tu…nawasaidia,
na nikihisi kuna baya najaribu kutafuta mbinu za kuwasaidia..lakini wewe na
huyo mnafiki wako….mumenotoka…kabisa kabisaaah…’akasema nesi mkuu akiwa kashika
kiuno.
‘Lakini bosi mbona sijakufanyia lolote baya..’akasema kwa
kujitetea.
‘Unasikia, huyo mnafiki wako, ..anafikia kunisema kwa wakubwa kuwa
mimi nafanya mambo ya ajabu ajabu, na wasichana..eti sijui mimi …eti…sijui miiko
ya kazi, mimi sijui miiko ya kazi, miiko gani nisyoijua mimi…’akashika kiuono
huku akijitingisha kwa nyodo.
‘Lakini huo ni umbea tu..dakitari kijana hana tabia hiyo, yeye
muda wote yupo na kazi..’akamtetea dakitari kijana.
‘Hahaha wewe unamtetea, hujui mimi nina masikio marefu, yanasikia
kila kitu kinachoongelewa humu hospitalini…naona kila kona ya sehemu hii ya
kazi..leo hii eti anakuja kunifundisha kazi mimi…anajua nimeanzia wapi kazi,…’akasema
akionyesha kukasirika.
‘Mimi nimeanza kazi huko hospitali ya rufaa, hadi wakanipandisha
cheo, nimenzia kwenye kufagia…kutumwa tumwa..kwa utundu wangu nikajiunza
mengi…nikapelekwa shule….hivi mnafikiri hiki cheo nimepewa bure bure tu….wakubwa
wote wananiheshimu mimi..’akasema
‘Hata mimi nakuheshimu….sana bosi..’akasema nesi kwa sauti ya
unyonge.
‘Huyo hawara wako…huyo..huyooo , yeye kaja hapa anajifanya anajua
saana, msomi, na udakitari wenyewe baado, basi hicho kidogo alichokipta
anajiona kaiva…a wapi, mabingwa wenyewe hawajioni hivyo…anajiona mrembo, mwanaume utakuwa hivyo
usharobaro…wapi na wapi,…na hata sijui kama ni mwanaume kweli…nikuambie ukweli
kama mdogo huyo atakupotezea muda wako bure, tafuta mume wa kweli, sio huyo…’akasema akiwa kama ananong’ona.
‘Lakini sister, mimi naona….’akawa anataka kuongea, lakini huyo
bosi wake akamkatiza na kusema;
‘Tafuta mume..huyo sio mwanaume…na nakuambia ukweli, huyo kwangu
amefika, ataniona mimi ni nani, mwenyewe
ataikimia ii hospitali..na hatarudi tena hapa…na wewe kinyamkera wake…utarudi
kijijini….’akasema.
‘Kwani mimi nimefanya nini?’ akauliza nesi, sasa akionyesha
wasiwasi mkubwa zaidi.
‘Hahahaha, kwani wewe umefanya nini eehee, unajifanya hujui eeh,
huyo mama aliyetooroka yupo wapi, hebu niambie kama angekuwa mtu mwingine sasa hivi
si yupo jela, keshafikuzwa kazi, lakini nyie myai..watoto wa mabosi,
mnalelewatu, hilo sikubali…’akasema
‘Lakini mimi sina ndugu yoyote hapa hospitalini ambaye ni bosi…’akajitetea
nesi.
‘Mimi nimekuuliza huyo mama wa watu yupo wapi, huoni kuw aumefanya
kosa kubwa sana…hebu niambie isku ile wakati huyo mama anatoroka ulikuwa wapi,…?’
akawa anauliza
‘Ni kosa kubwa sana ulilolifanya..halafu watu wengine wanakutetea,..hapana
hili halikubaliki…’akasema
‘Lakini ni bahati mbaya, sikujua…’akasema
‘Ni bahati mbaya…mimi mwenyewe nilikuona, …nilikufuatilia wakati
unatoka pale kwenye chumba hadi unakwenda huko kwa yule rafiki yako mkaanza
kupiga soga za umbea…za kutaka wanaume…yote hayo nayafahamu…halafu ukatoka pale
ukaenda wapi? Sema mwenyewe, moyo unapwita, unataka umuone sharobaro wako….’akasema
‘Hapana bosi nilipotoka pale nilikwenda, nilipitia tu,
kuona…’akasita
‘Unanifanya mimi ni mtoto… wewe si ulikuwa unamchungulia huyo
hawara wako dirishani, kwanza nikashutua, na hata ukikataa kuwa sikukuona, mimi
nina shahidi wote, sifanyi vitu kwa fitina…ushaidi ninao…hapa….’akasema huku
akiinua simu yake juu
‘Bosi hayo yamekujaje….mbona sikuelewi…nakuomba tafadhali nipo chini
ya miguu yako…usiwaonyeshe wakubwa, nitafukuzwa kazi…na nimeshakubali kumchukua
mtoto, sasa ukianzisha mengine,….nitafukuzwa kazi…’akasema nesi akitaka kupiga
magoti.
‘Hahaha…umeonaeeh, sasa unajifanya unaogopa, siku zote unajifanya
kichwa maji,..sasa utaingia kwenye anga zangu, ….na bado…utajua kuwa mimi ni
nani, mimi nawaenga, taratibu, ukiengeka, aah, tupo pamoja lakini wewe na huyo
mnafiki, sitawavumilia tena, lazima mnielewa tu…hilo nimeahidi…’akasema
‘Lakini bosi kwani tumefanya nini…mimi hapa tulikuwa tunongea
jinsi gani nitaweza kumlea huyo mtoto na wakati natakiwa kazini, kwahiyo akawa
anajaribu kunielekeza na kunipa ushauri, kutokana na ushauri wake nikafurahi,
ndio nika..nika…….’akasema
‘Hahahaha…mbona humalizii, ukamkumbatai na kuanza kulana mate..si
ndivyo mnavyosema nyie wasomi…hebu angalia hapa…’akawa anaonyesha picha kwenye
simu yake.
‘Umeiona hii picha, hivi kweli,..ni nani hataamini kuwa nyie ni
wapenzi mnafanya mapenzi sehemu ya kazi..hivi utamdanganya nani..hivi ehe eti
waonyesha ishara ya kumshukuru, wakati macho yamelendemka, mweeeh, kama umekula
kungu. …hahaha, hivi waniona mimi wa juzi ehe…chunga hiki kitu kingine..’akasema
huku akimkazia macho huku akidi kuonyesha lile tukio kwenye simu yake na nesi
akabakia kaduwaa , katoa macho ya uwoga.
‘Bosi basi naomba samahani…nitafanya chochote
unachokitaka..unataka nifanye nini..naomba ufute kabisa hilo….naomba
tafadhali…unataka nikufanyia nini nesi..?’ akauliza nesi.
‘Unajau mimi sina ubaya na yoyote yule..muhimu mniheshimu…muhimu
mnione mimi ni mkubwa wenu, sipendi kabisa madharau…na kuniona mimi eti
sijasoma, eti nimepewa kazi tu kwa vile ni uzoeu t, najuana na wakubwa tu…mimi
sijuani na yoyote yule wanachofanya ni kujali utendaji wangu…’akasema
‘Sasa sikiliza hizo dharau zenu..sizitaki,..sitaki..sitaki mtu
kunidharau kunyodo…, ‘akasema na nesi akawa anafuta machozi,…kuonesha kuwa
analia.
‘Sasa unaoneeh..hujalai
bado, utalia…nakuambia ukweli..’akasema
‘Bosi naomba unisamehe…’akasema
‘Mhh..nikusamehe,..mimi sina uwezo huo…nyie wasomi ndio mnajua
kujitetea,..muda ukiika utajitetea,…maana mimi sijasoma, sijui sheria eeh,
miaka mingapi nimefanya mimi, nisijue…., sasa kama mimi sijasoma nimepewa kazi
kwa sababu ya hivyo mnavyosema, sasa nataka kuwaonyesha kuwa mimi nimesoma…hii
imetoka wapi..hebu angalia….’akasema huku akiendelea kuonyesha hilo tukio kweny
esimu yake.
‘Nyie mnaojiita wasomo…mnakuja na yenu, …angalia jinsi gani mnavyoharibu maadili ya kazi, halafu eti huyo
hawara wako anasema mimi ndio sijui maadili, sasa aseme mimi na yeye ni nani
anaharibu maadili..’akasema
‘Lakini mimi sijasema hujasoma…’akasema
‘Nyie…hasa mlitoka vyuoni huko, …ambao mnajifanya wasomi..si ndio…mnajifanya
nyie ni tofauti..hahaha, sasa mumepatikana mtajua mini ni nani…ni lazima mje
kwangu mnipigie magoti na muonyeshe hizo ngebe zenu..nataka niwaone kweli kama
nyie ni vibikira..hahaha…wakati mumekubuhu…na hata kufundwa
hamjafundwa…mna…nyie nyie…’akasema na kupita pale aliposimama nesi, na jinsi
alivyopita, kwa tambo, akampiga kikumbo huyo nesi na nesi akaishia kutaka
kudondoka chini.
‘Kuna taarifa za kutataisha
kuhusu huyo mama..ni taarifa gani….’ nesi akawa anatembea kuelekea sehemu
wanapohifadhiwa watoto tayari kumchukua huyo mtoto na kuelekea kijijini,
hakutaka kusubiri zaidi,hakutaka kuja kukutana na huyo bosi wake tena..lakini
hata hivyo alitaka kuonana na dakitari kijana amuelezee hayo aliyoyasikia, ili
awe na tahadhari
Haikuwa rahisi kumpata dakitari kijana, kwani kulikuwa na wagonjwa
wa dharura wengi, dakitari kijana akawa muda mwingi yupo chumba cha upasuaji
akitoka hapo anaingia chumba walipolazwa wagonjwa mahututi….hana muda kabisa,
akaona hilo halitawezekana, na simu yake muda wote imezimwa…
**********
Nesi akakutana na mtu anayesimamia watoto, na mtoto akafanyiwa
utaratibu wote ikiwemo na vipimo kuhakikisha kuwa yupo salama, kabla
hajakabidhiwa, na zoezi hilo lilipokamilika, kwa haraka akakabidhiwa mtoto ..na
mama mkunga na msaidizi wake,
Kwa muda ule, bosi wake
hakuwepo yaani nesi mkuu…na kwahiyo jukumu hilo akalichukua mama mkunga na
msaidizi wake wakawa wamempataka yule mtoto wakimuangalia na kuongea mawili ,
matatu, kabla hawajamkabidhi nesi , na mama mkunga akasema;
‘Unamuona mtoto alivyo na afya, mnzuri..hana tatizo lolote, sasa
sisi tunakukabidi, tunakutakia ulezi mwema..unasikia..’akaambiwa
‘Ndio mama mkunga…’akasema
‘Kama ilivyokubalika na wewe kukubali kubeba hili jukumu, sasa
mchukue mtoto awe kwenye mamlaka yako, na uhakikishe anapata huduma zote…na
mengine utakuja kuambiwa ..kama una lolote unaweza kusema …’ akaambiwa na
kukabidhiwa mtoto.
‘Mhh kwa hivi sasa sina..’akasema
‘Haya mchukue mwanao, kila laheri…’akaambiwa na kukabidiwa huyo
mtoto
Basi yeye akamchukua yule mtoto na usafiri alishapewa, akatoka nye
nje kuondoka, ikiwa na isafari ya kwenda kijijini, kumpeleka huyo mtoto kwa
dada yake, akijua kabisa ndugu yake atamkubalia.
Akawa sasa anaingia kwenye gari, mara kwa mbali akamuona dakitari
kijana,…akamuomba dereva kwanza akaagane na dakitari huyo, akatoka na kumuendea.
Dakitari kijana alikuwa hajamuona, hadi alipofika kariu yake,
akageuka na kumuangalia nesi huyo akiwa na mtoto, akamsogelea na kumuangalia
mtoto, akasema;
‘Mhh, ..ndio umemchukua kwahiyo sasa hivi unakwenda wapi?’
‘Docta mimi ndio naondoka kwenda kijijini..’akasema
‘Ok, ..basi ki-laheri, najua utafanikiwa huko uendapo..’akasema
dakitari huyo
‘Yah..i hope so…sina shaka na ndugu zangu…’akasema nesi
‘Ok, basi tutawasiliana, au ukirudi tutaongea, usijali, tupo
pamoja…’akasema na hawakuweza kuongea zaidi, maana dakitari huyo alikuwa na
haraka, na nesi akiwa karizika na ile kauli ya dakitari akajua sasa kweli wapo
pamoja, na akirudi tu kutoka huko kijijini, anakuja kuongea naye, na
atajitahidi amuonyeshe kuwa kweli ana nina njema kwake.
***********
Siku aliporejea
hospitalini, alikuwa na raha, na aliona kuwa tukio hilo la huyo mtoto na mama
yake ndio njia muhimu, itakayomfanya waweze kuwa karibu zaidi na huyo dakitari na
akaona aitumie njia hiyo hiyo, ….
‘Ni lazima kila siku nimfahamishe ni nini kinaendelea huko
kijijini, ajue kuwa mtoto yupo mikono salama..na najua kwa njia hiyo nitaweza
kuwa naye karibu zaidi..’akasema
Basi…siku hiyo alipotoka kijijini, alikuwa hana jingine kichwani zaidi ya kumuwaza dakitari kijana… Aliwaza
jinsi gani akikutana naye atakavyomchangamkia na kumshukuru sana kwa kumsadia
na kuwasaidia ndugu zake…akawa kamnunulia zawadi za kijijini....na kila hatua tabasamu
lilikuwa likimtooka mdomoni..
Alifika hospitalini akasalimiana na wenzake, na kila mmoja
akijaribu kumuuliza jinsi gani atakavyoweza kumlea yule mtoto, au imekuwaje…na
maswali mengi ambayo kwake aliona ni ya kumpotezea muda. Aliwajibu kwa mkato
tu..
Basi alipomalizana kusalimiana na wenzake, kwa haraka akaondoka
kuelekea chumba cha madakitari bingwa, ili akamuone dakitari kijana. Hakujali cha nesi mkuu…na alipopita ofisi ya
nei mkuu, akamkuta msaidizi wake, akamuuliza nesi mkuu yupo wapi, akaambiwa
yupo mapumzikoni, kapatwa na dharura…
‘Yesss..’akajikuta akisema
‘Vipi huko ulipotoka…?’ akaulizwa
‘Salama kabisa, nimeshamikisha mtoto na ndugu yangu yupo tayari
kuwa naye, ..na mengine ..ni ya kawaida tu..’akasema
‘Sawa…muhimu ni kujua yupo salama, na mengine…mmm, sio muongeaji
sana…wewe nenda kajiweke sawa, karibu kazini..’akaambiwa na yule nesi msaidizi
wa nei mkuu akawa anatoka nje.
‘Samahani nimeitwa huko kwa mkuu,…kwa dakitari mkuu, naona maemo
yameiva..’akasema
‘Mambo gani tena..’akauliza
‘Mhh, si ya kzi tena…yaani kaondoka mwenzangu kaniachia misala…baadaye
nina haraka..’akasema na kuondoka, na nesi akashukuru maana akutaka kukaa hapo
muda mrafu kwani alikuwa na yake.
Akiwa sasa anajiamini maana muhasimu wake hayupo akatembea
kuelekea ofisi ya anayokaa dakitari kijana…akagonga na kuingia…, kwenye meza ya
uyo dakitari kijana akamkuta dakitari mwingine mgeni, akashangaa.
‘Habari docta..’akasalimia
‘Njema nesi, nikusaidie nini..?’ akauliza huyo dakitari akiinua
uso kwani alikuwa akiandika kitu kwenye karatsi na huyo dakitari alipotua macho
yake kwa huyo nesi, akapitisha mkono usoni, na kuonyesha tabasamu.
‘Aaah, samahani nilikuwa nauliza…maana wakati naondoka ofisi hii
alikuwa anatumia dakitari mwingine…na…nakuona wewe..’akasema
‘Oooh, unasema dakitari kijana..hayupo,…kaondoka..’akasema
‘Kaondoka, kaenda nyumbani, ..kwani leo yupo mapumziko?’ akauliza
‘Mhh, hapana, mimi mwenyewe niliika tu, ..na hatukuweza kuongea
naye sana, ila ni kuwa… imekuja barua ya dharura kaondoka asubuhi…, na huenda
kesho anapanda ndege kwenda Ulaya…’akaambiwa.
Nesi aliposikia hivyo, alibakia kasimama, akili ikiwa sio yake
tena,..., akabaki kaduwaa,..akawa anajiuliza ina maana uyo dakitaria alijua
kwua anaondoka, na hakutaka kumuambia ukweli, kwanini…..akawa anajiuliza.
‘Lakini alisema bado muda wake wa kuondoka…?’ nesi akasema
akionyesha kusikitika kabisa, na dakitari huyo mgeni akamuangalia kwa uso wa
kushangaa, akasema;
‘Mimi sijui…maana nilifika hapa na yeye akawa anaunga funga, na
kuniamia hivyo kuwa kapata barua ya dharura,a aliyokuwa akiisubiria, ila
imekuja bila ya yeye kutarajia, lakini alishajiandaa…., kama vipi wasilina naye
kwa simu..’akaambiwa
‘Simu yake haipatikani…’akasema nesi akiangalia simu yake na kujaribu
kupiga hiyo namba ya dakitari kijana, na
hakupatikana.
‘Basi huenda ndio yupo kwenye maandalizi…ni kuwa inavyoonyesha, alishajiandaa
na alijua muda wowote inaweza kutokea hivyo, kwahiyo…keshaondoka..anaondoka
kesho kuelekea Dar, na akitokahapo, ndio saari….’akasema huyo dakitari mgeni.
‘Mhh, jamani mbona nina bahati mbaya..’akasema nesi akigeuka
kuondoka, na yule dakitai mgeni akasema;
‘Bahati mbaya kwa vipi… mimi nimekuja kushika nafasi yake kama
kuna lolote niambie mimi nitakusaidia,…kwanza, wewe ni nani, ooh, nimekumbuka
ndio wewe, nimeambiwa umechukua likizoa ya dharura, tutakuwa wote,
usijali..hivi unaitwa nani vile..?’ akauliza na nesi hakutaka hata kuongea
zaidi, akatoka.
Alipofika nje, akamfuata rafiki yake, rafiki yake ambaye
walishakosana kutokana an dakitari kijana, rafiki yake akisema kuwa yeye kamgeuka,
badala ya kumsaidia alichokitaka , yeye kachukua nafasi hiyo na kumuibia mpenzi
wake. Siku hiyo walizozana sana, hadi urafiki ukaisha.
‘Lakini sio mpenzi wako…’akasema siku hiyo akikumbuka ilivyokuwa.
‘Ina maana imefikia hivyo, unajuaje kuwa huyo sio mpenzi wangu…unajuaje kuwa hatukutani huko
nje…sikiliza mimi na wewe urafiki basi…’akaambiwa, na kweli kutoka siku hiyo
wakawa hawaongei tena na huyo rafiki yake.
Leo hii akaona amuendee tu hana jinsi…., huenda kama ni kweli walikuwa
marafiki wa siri..wanakutana baada ya saa za kazi kama alivyodai rafiki yake
huyo kitu ambacho haamini, basi atakuwa
anafahamu lolote kuhusu dakitari kijana.
‘Shoga… sahamani najua umeshanisamehe au..?’akasema kwa kumuuliza
rafiki yake , na rafiki yake akamuangalia kwa kumnyali, halau akatabasamu na
kusema
‘Yah..najua..maana mtu mwenyewe keshaondoka, kwanini tugombane, ...kaniaga
kwa busu kuwa anaondoka,..basi iliyobaki tutawasiliana kwa simu…’akasema
‘Kaondokaje?’ akauliza nesi huku akiwa kama haamini
‘Hahaha…kaondokaje, ni kama alivyokuja,..tuliobahatika basi….mimi nilikuambia
wewe wakati unabonyeza ndizi kuwa imeva, wenzako tunaimenya na kuila…hahaha,
wacheza na mie..hahaha…wewe kalagabahwe….na ujue nesi mkuu alikuwa anakulizia
jana..’akasema
‘Kwanini ananiulizia, wakati anajua mimi nimeondoka kwa
dharura..’akasema
‘Hivi umesikia kilichotokea..?’ akaulizwa shoga yake na nesi
akamuangalai shoga wake wa zamani kutaka kusikia zaidi, akauliza;
‘Kuhusu nini?’ akauliza
‘Ina maana hujui,…?!’ akaulizwa shoga wake kwa mshangao
‘Kuhusu nini,..kuwa dakiari kijna kaondoka, ..hilo ndio
nimesikia hapo ofisini kwao…kwani kuna
jingine..?’akauliza akionyesha wasiwasi.
‘Achana na yule mshamba, dakitari kijana, dakitari kijana…kuna
jingine nzito, na…sijui utaokokaje safari hii,..’akasema shoga yake
‘Kwanini, jingine nzito lipi hilo?…kwani kumetokea nini?’ akauliza
akionyesha wasiwasi, akihisi huenda bosi wake, nesi mkuu atakuwa kaeshapeleka
umbea wake kwa wakubwa na huenda kuna taarifa za kufukuzwa kazi.
‘Mhh kama hujasikia basi….ngoja ninyamaze, mimi nisiwe
mmbeya..maana hapa kazini siku hizi ni kila mtu kuchunga mzigo wake
mwenyewe..’akasema shoga wake huyo akiendelea na shughuli zake
‘Shoga-yangu bwana niambiee kuna nini tena…mwenzako unaniweka roho
juu..’akasema kwa sauti ya unyonge.
‘Mimi sikuambii…’akaonyesha kufunga mdomo kwa mkono, halafu
akaondoa mkono mdomoni na kusema;
‘Na sikia..ule ushoga wetu ule wa enzi zileee…eeh,… wa kuambizana
kila kitu sasa umekwisha, utabakia huo tu
wa kikazi, maana wewe sasa ni nuksi…unajau nuksi..wewe ni nuksi…tuachane
kabisa’akasema
‘Ndio imekuwa hayo…’akasema nesi
‘Ndio hivyo…kaa mbali na mimi kabisa, usije kunitia hatiani
buree…sitaki mambo ya kuitwa ushahidi, sitaki kabisa…’akasema
‘Ushahidi wa nini tena..?’ akauliza akiwa hataki kuondoka.
‘Utakuja kuambiwa bwana ondoka,…., mimi sitaki kuwa mpiga majungu
, wewe nenda sehemu yak o ya kazi, najua kwa vyovyote utaitwa…..na ..sijui kwanini
hujaitwa mpaka sasa...kwaheri..’akaambiwa na nesi akawa kashikwa na butwaa.
Kwanza akatulia na kujaribukumuangalia rafiki yake huyo wa zamani
kama atamuonea huruma na kuambia lolote, lakini akaona hakuna dalili…baadaye
akaona asipoteze muda akaondoka kuelekea sehemu yake ya kazi, na alipofika tu,
akakuta ujumbe;
‘Ulikuwa unahitajiwa kwa mkuu wa hospitali…’akaambiwa
‘Una maana kwa Dakitari mkuu wa hopsitali, kuna nini tena huko..?’
akauliza
‘Hatujui tumeambiwa ukifika tu uende kwake kwa haraka..’akaambiwa
na kabla hajakaa sawa, mara akaja mfanyakazi ambaye kazi yake ni kutumwa huku
na kule akasema;
‘Nesi unaitwa ofisini kwa dakitari mkuu, haraka…’akaambiwa.
WAZO LA LEO: Kuna watu wanaona kuwa kuongea ni ufahari…kuzuliana,
na kujiona wanajua zaidi, hata kama wanaloliongea hwana yakini nalo, lakini kwa
vile ni wataalmu wa kuongea, kugushi, kuzua, umbea..fitina, basi wao wanajiona
wameshinda. Na wengine ndio utaratibu wao wa maisha hata kipato wanachopata
kinatokana na tabia hiyo chafu. ..huo ni wizi, na ni dhuluma. Tabia kama hizo
ni ufinyu wa taaluma, huwezi kujinadi kuwa unajua au unatenda kazi hiyo kwa
ufanisi wakati sio kweli..kwa hali hiyo utakuwa unajidangana mwenyewe. Maana njia
za mnafiki huwa ni fupi sana, ipo siku utanasa na utaumbuka, kwanini
usijiendeleze, ukasoma, ukajua zaidi, kuliko kujifanya unajua kumbe hujui…
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment