Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 13, 2015

NANI KAMA MAMA-44


‘Karibu nesi…utuambie uliyoyapata huko kijijini, …tunasubiria kwa hamu , maana hali ya mgonjwa kwasasa inahitajia zaidi kujua historia yake, ili tujue chimbuko la tatizo lake limetokana na nini, …unajua kuna kitu kinatushangaza, ..iweje huyo mama akunyoshee kidole wewe…’akasema docta

‘Ananinyoshea kidole mimi, kwa vipi?’ akauliza nesi akiwaangalia mabosi wake kwa sura ya kushangaa, na kukunja uso kidogo.

‘Hebu kwanza kaa kwenye kiti  tusikie uliyoyapata huko….maana huyo mama anaongea mengi…ni kuonyesha kuwa huyo mama alipatwa na jambo, hilo tatizo likaziba ufahamu wake wa nyuma…kwa hivi anaonyesha dalili za kuanza kukumbuka..kwahiyo atasema mengi, na kawaida hayo anayoyaema ni yale yaliyotokea kabla hajapatwa na hilo tatizo, kwahiyo ni ya ukweli…’akasema docta bingwa.

‘Ina maana….’akataka kusema nesi lakini akashindwa aongee nini, na docta msaidizi akasema;

‘Anadai wewe umechukua mtoto wake..’akasema docta msaidizi..na wakati huo nesi alikuwa hajakaa kwenye kiti na aliposikia hivyo, sasa akakaa kwenye kiti huku akili ikianza kuchemka.

Tuendelee na kisa chetu.

**********
‘Hebu tuambie ulichokipata huko kijijini..’akasema docta mkuu, na mwenzake naye akawa kashika kidevu huku wote wakimkazia macho nesi, nesi akainua uso na kuwatizama, akasema;

‘Unafikiri, hakuna la muhimu nimelipata,….hakuna cha zaidi kinachoweza kusaidia,..ni yale yale tu…imani zao…na….kumshutumu huyo mama, kwa mambo yasiyoelezeka…’akaanza kusema

‘Hayo hayo uliyoyasikia , ..tunataka na sisi tuyasikie..’akasema docta msaidizi.

Nesi aliwaelezea wale mdocta yote aliyoyakuta huko kijijini na jinsi gani anavyofahamu , na mwisho akasema

‘Na hiyo kauli ya huyu mama kuwa eti mimi nina mtoto wake, sio kwangu tu, hiyo ni kauli yake hata kabla mimi sijamfahamu…sijaonana naye.., yeye nasikia lipoika hapo kijijini kutoka huko alipotoka, kila aliyekutana naye anamwambia hivyo, na … kwa kila mtu..na hasa akikuona una mtoto basi atakuganda…’akasema nesi.

‘Unajua tangia nianze hii kazi, watu kama hawa wakianza kuongea , huwa wanaongea yale ya kweli, yale yaliyowahi kutokea kwenye maisha yao huko nyuma kabla hawajapoteza kumbukumbu zao…, lakini wanayazungumza pasipo na mpangilio..ni vitu kama njozi vinakuja akilini mwao…na hatimaye atakuja kukumbuka yote….’akasema docta.

‘Kwahiyo labda  mnahisi kuwa ni kweli kuwa mimi nimemchukua mtoto wake..kwanini nifanya hivyo…?’ akauliza nesi

‘Hapana sio hivyo hatumaanishi hivyo…kama ulivyosema kuwa huyu mama anashutumu yoyote yule…sisi tunajaribu kuona kama kuna ukweli kidogo..’akasema docta ka kabla nesi hajasema kitu yeye docta akaongezea swali;

‘Hebu tukuulize, wewe ..maana unasema na hasa akikuona una mtoto, hebu kumbuka vyema siku hiyo ulipokutana naye ulikuwa na mtoto au kabla..katika kufika kwako huko, huenda uliwahi kuwa …au kupakata mtoto wa mtu mwingine akakuona..’akasema docta

‘Mtoto..!?’nesi akauliza kwa mshangao, akawa anawaza, akijaribu kukumbuka.

‘Unajua huyu mama alifikia kuniambia, kama shitaka kuwa wewe ndiye umemchukua mtoto wake, nikamuuliza kwa vipi, akasema alikuona ukimchukua,..na akakuona ukiwa naye huko…anasema tu hukooo, ukimuuliza wapi, anaendelea kusema tu hukoo, na hapo anakuwa kama anajaribu kukummbuka ..’akasema docta.

‘Mimi sioni ajabu kwa kauli yake hiyo, kwani kama angeninyoshea kidole mimi tu, labda ningelisema kuna hoja…lakini sio mimi tu, hata ndugu zangu, majirani na yoyote pale kijijini anamwambia hivyo hivyo, na hata akawa anaimba wimbo wake akisema ‘anataka mtoto wake’..’akasema nesi.

‘Hebu turudi nyuma kidogo..siku ulipokutana naye, ulikwenda kijijini kufanya nini, ..najua ilikuwa ni mapumziko au kulikuwa na ni kitu maalumu… , labda tukumbushane hivyo..?’ akauliza docta msaidizi.

‘Mhh, ni siku nyingi..na mara kwa mara huwa na kwenda huko kijijini kusalimia tu..maana nimelelewa huko..lakini kwa vile nimeshakuwa na mahali pangu pa kuishi,..huku mjini, siwezi kwenda huko kukaa saana.., ila ninachokumbuka ni kuwa …mimi nilikutana na huyo mama wakati naelekea kituoni, kutafuta usafiri wa kurudi huku kazini.’akasema

‘Ulikuwa na mtoto?’ akauliza docta.

‘Hapana, mtoto wa nini …maana narudi kazini , na sikuwa na mtu yoyote ambaye labda nilimsaidia mtoto…nikamuona nikajaribu kumuongelesha, na kama anavyowafanyia watu wengine..basi na mimi akanifanyia hivyo hivyo, akawaanadai kuwa eti mimi nina mtoto wake..shutuma zake dhidi yangu zikaanzia hapo…’akasema nesi.

‘Hebu kumbuka,….kipindi hicho, maana wewe ndiye nesi peke yake uliyebakia hapa wa muda mrefu, na hata madocta wote sisi hapa ni wageni..kipindi hicho ulichoenda huko kijijini,….ukakutana na huyo mama, ulikwenda vipi, kulikuwa na tukio, au ilikuwa likizo yako tu…. hakuna tukio ….lolote hivi….linaloweza kuwiana-wiana, yaani hakuna jambo lililokufanya kwenda huko kijijini, au hapa hospitalini hakukutokea jamb lolote la mama kama huyu….?’ akauliza docta.

‘Tukio kama lipi….mmh, sikumbuki, mimi nahisi ilikuwa ni siku ya mapumziko nikaamua kwenda kusalimia tu..unajua ni muda sikumbuki vyema …aaah ndio ilikuwa ni ..mapumziko kama haya….ama kwa hapa hospitalini mmmh, tukio ..kama lipi..?’ akawa anaonga na kujaribu kutafakari

‘Unajua najaribu kuoanisha, hili analodai huyu mama kuhusu huyo mtoto wake,…na tatizo lake..la udhaifu katika kumbukumbu, na kuchanganyikiwa...huyu mama , nimemchunguza kwenye tumbo lake kuna dalili za kuwa alifanyiwa upasuaji..’akasema docta.

‘Mhh..upasuaji…?’ akauliza nesi kwa mshangao.

‘Lakini haina, nahisi hivyo huenda haina, mahusiano,… hilo kwangu sio tija, nataka tu kujua, wewe kipindi hicho ulipowkenda huko kijijini hukuwahi kumbeba mtoto…huenda alikuona ukiwa na mtoto kitu kama hicho na je hao ndugu zako hawana mtoto, hawakuwa na mtoto mchanga?’ akaulizwa

‘Kubeba mtoto wa mtu mwingine..mmmhe..hapana docta…..mhhh, ..sijui maana mimi kwa mara ya kwanza kukutana naye ni hapo,..na ilikuwa ni barabarani, sio nyumbani hapo kwa ndugu zangu…na ilikuwa ni  wakati naondoka..mmh, ok, labda…lakini haiwezekani, maana mimi sikuwahi kutoka nje na huyo mtoto wadada yangu..?’ akasema nesi.

‘Kwahiyo kumbe uliwahi kubeba mtoto, yaani..sio wa huyo mama, ila uliwahi kubeba, huenda akakuona lakini wewe hukuweza kumuona kwa wakati yeye anakuona,..je uliwahi kumbeba mtoto hata kama ni wa jirani, …?’ akaulizwa

‘Lakini kama ni huyo, mimi sikuwahi kutoka naye nje..?’ akasema.

‘Huyo mtoto ni wa nani hebu tuanzie hapo?’ akauliza docta.

‘Doctor, lakini huyo mtoto hana mahusiano na huyo mama..nina uhakika kabisa..’akasema

‘Mhhh..hatujasema hivyo…kuwa ni mtoto wa huyu mama, wewe is umesema kuwa huyu mama kila mwenye mtoto anamshuku au sio..lakini imetokea kushuku kwake kwako kuwe na uzito zaidi…’akasema docta

‘Kwa vipi iwe hivyo?’ akauliza nesi.

‘Mimi nakuambia hili kwasababu wamekuja watu wakiwa na watoto wao, na mimi mwenyewe nikajribu kmpima huyo mama kuona kama hiyo hali ya kudai kila mtu mwenye mtoto ni wake…nikajaribisha kwa hao waliokuja na watoto wao…’akasema docta.

‘Hakudai kuwa hao watoto au huyo ni mtoto ni wa kwake?’ akauliza nesi.

‘Kwa muda ambao kaanza kupata kumbukumbu, hakudai hivyo…nilipomuuliza hakusema ni mtoto wake, …ila anapenda watoto..’akasema docta

‘Ina maana hakudai kabisa kwua ni mtoto wake..?’ akauiliza tena nesi.

‘Nilimjaribisha hivyo, nikamuliza ni mtoto wake, akasema hapana mtoto wake kachukuliwa na nesi, nikamuuliza nesi yupi,… akasema ..huyo mnayemuita nesi mkuu..’docta akasema

‘Alisema hivyo..?’ akauliza nesi kwa mshangao na kutahayari.

‘Ndio..ndio maana najaribu kutafuta ukweli…kama unavyoona, ilivvyo. Ina maana sasa huyu mama kumbukumbu zimeshaanza kujijenga mpaka anakumbuka nesi yupi , kasema huyo mnayemuita nesi mkuu,…na nikajaribu kumleta nesi mwingine akasema sio huyo…labda kama unabisha tutakwenda sote nikamuulize mbele yake..uone..lakini hilo sio muhimu kwa sasa..muhimu ni kutaka kujua..huedna kuna kitu kilitokea….’akasema docta mkuu.

‘Mimi sielewi kabisa…mimi nitamchukuaje mtoto wake kwa lipi…sijui mnanielewa…mtu mwenyewe mnaomuona alivyo, hivi kweli aliwahi kuwa na mtoto..?’ akauliza nesi kwa mshangao.

‘Aliwahi…aliwahi kuwa na mtoto…’akasema docta na nesi akamtupia jicho la mshangao.

‘Ulimchunguza?’ akauliza nesi..

‘Hiyo operesheni aliyowahi kufanyiwa inaonyesha kuwa aliwahi kuzaa kwa upasuaji…aliwahi kupata mtoto, sasa sijui kama mtoto alikuwaje, hai..au vipi, lakini huo upasuaji ni wa uzazi…’akasema docta na wote wakawa kimia kwa muda.

‘Nesi hebu kumbuka kipindi hicho hakuwahi kufika mama kama huyu, mwenye matatizo, mtindio wa ubongo… , kuchanganyikiwa..akajifungua mkafanya taratibu za kumchukua mtoto wake?’ akauliza docta msaidizi.

‘Kama huyu..mmmh, hapana…maana kuna taratibu kama akitokea mama kama huyo , nikimaanisha mwenye matatizo ya akili,si zipo taratibu jamani… ikitokea hivyo mtoto anakabidhia kwa ndugu zake,..hizo taratibu zilikuwepo hata kabla hamjafika nyie…ni kweli imetokea hivyo mara kwa mara na taratibu zikafuatwa, kweli si kweli…sasa mimi sikumbuki vyema…na mama kama huyu mwenye kuchanganyikiwa kihivyo sikumbuki kumuona kabla…sikumbuki, ..’akasema nesi.

‘Katika kipindi hicho cha nyuma,..hakukuwahi kuzaliwa mtoto, …akawa hana mzazi…labda mama yake akapatwa na jambo, akafariki..kitu kama hicho…?’ akauliza docta.

‘Sasa kama mama yake alifariki huyu atakujaje kudai mtoto ni wake , au na nyie mnaamini mambo hayo ya kijijini wanaodai kuwa mama huyo alikufa na sasa kafufuka kuja kulipiza kisasi..’akasema nesi.

‘Hapana…unajua tunajaribu kuangalia kumbukumbu za nyuma….maana kama mama huyu ni wa maeneo ya vijiji vinavyozunguka maeneo haya ya hii hospitali na nijuavyo mimi hakuna hospitalini nyingine kubwa kwa maeneo haya ya wilaya inayotambulikana kwa upasuaji kama huo ni hapa tu…hivi kuna hospitali nyingine..eeh, hakuna..eeh, sasa kwa vyovyote basi huyu mama alifanyiwa upasuaji hapa…’akasema docta.

‘Hata mimi naona hivyo…labda nesi ukumbuke vyema..’akasema docta msaidizi

‘Kwahiyo ina maana huyu mama kama aliwahi kujifungua kwa upasuaji atakuwa alijifungulia hapa..au sio…sasa mtoto wake yupo wali..labda ni kachukuliwa na ndug zake..labda…lakini je alijifungulia hapa?’ akauliza docta akimgeukia docta mwenzake.

‘Au aliwahi kujifungulia sehemu nyingine na kuhamia vijiji vya eneo hili..’akaongezea docta msaidizi….

‘Mhh,unajua docta nimekumbuka jambo,  uliposema kama kuna tukio mama alijifungua akafariki…au..mmh, nimekumbuka…lakini sio huyu mama,…kuna tukio liliwahi kutokea hapa hospitalini, lakini halihusiani na huyu mama…nina uhakika kabisa sio huyu mama,….maana huyo mama tulikuja kusikia kaokotwa akiwa amefariki, akazikwa, na mmoja wa nesi wa hapa alihudhuria mazishi yake…’akasema nesi

‘Huyo yeye ilikuwaje?’ akaulizwa.

Nesi akashika kichwa akijaribu kukumuka tukio hilo analoikiria yeye, maana yapo matukio mengi, ila hilo moja analikumbuka kwani lina mambo mengi kichwani mwake..lakini kama ni hilo tukio hakupenda kuliongelea.

Sasa akawa anajuta kwanini kalikumbuka hilo tukio, maana lile tukio halikutakiwa kuhadithiwa kabisa, kwani ilikuwa ni siri yao, yeye na madkitari na ndugu zake..na aliwahi kukanywa kuwa ikitokea akavujisha siri anaweza kupoteza ajira au hata kufungwa kwani walichokuwa wamekifanya wao ni kumsaidia yeye kwa uzembe wake,..uzembe uliosababisha kifo…maana taarifa zilikuja baadaye kuwa huyo mama kaokotwa, na amekiwsha kufa.

Na siki taaarifa ilipofika, wakati wameshachukua maamuzi, kuwa nesi huyo abebe jukumu la kumlea mtoto…., ilibidi wakae tena kikao cha siri…, na kuambizana kuwa tukio hilo sasa liwe siri kubwa sana.

‘Mhh, lakini docta, hilo tukio halihusiani kabisa na huyu mama…’akajitetea nesi

‘Sawa liwe halihusiani, au linahusiana , mimi nikilisikia ninaweza kupata japo fununu..mimi ninahisi huyu mama aliwahi kufika hapa…’akasema

‘Umejuaje hilo…?’ akauliza docta mwenzake.

‘Kuna muda nilimuuliza huyo mtoto wake anayedai kachukuliwa alichukuliwa wapi…basi akasema atanionyesha, nikamwambia anionyeshe,…akasimama na kutembea hadi chumba cha upasuaji cha wazazi akasimama hapo mlangoni akasema alichukuliwa humo..’ akasema docta na baadaye akaongezea kusema;

‘Mimi nikamuuliza ni nani alimchukua, akasema alichukuliwa na docta na nesi…unaona, sasa hapo akasema na docta na nesi….docta yupi, nikamuuliza kama aliwahi kumuona..akasema huyo docta hajawahi kumuona hapo tena…’akatulia docta akimuangalia nesi

‘Kama kasema hivyo, kuwa alichukuliwa na docta…maelezo yake yanaonyesha uhalisia fulani…., maana madocta ndio wenye kezi hiyo, na nesi, ndiye eliyemchukua mtoto kwenda kumuhifadhi…hebu angalia ilivyo, …haionyeshi ni kauli ya mtu mwenye kuchanganyikiwa, ..huyu mama kaanza kukumbuka yaliyotokea, ndio maana nahisi..anayozungumza yana ukweli…’akasema docta.

‘Lakini kama ni hilo tukio,…docta huyo mama likufa, sio huyo…hata maumbile yake huyu hayafanani kabisa na yule…mimi siwaelewi, mnataka kusema huyo mma kafufuka, na ndiye huyu anakuja kudai mtoto wake..’akasema nesi.

‘Eheee..sasa unaona kulikuwa na tukio…si ndio, ..na tukio hilo linamuhusu mama na mtoto….sasa sisi tunahitajia kulifahamu hilo tukio, hata kama sio lenyewe, lakini huenda likaleta picha..’akasema docta.

‘Mabosi zangu tutakuwa tunapoteza muda tu…maana nina uhakika huyu mama sio yeye, kwa vile yule tulipata habari kuwa keshafariki..alipotoka hapa, alizidiwa njiani akadondoka,…akaja kuokotwa na watu akiwa ameshafariki,…maiti yake ilikuwa katika hali mbaya, wakamzika haraka…’akasema nesi.

‘Unajua nesi nikuambie kitu….hapa hatupotezi muda, maana hiyo nimoja ya kazi yangu…na tukio hili linanifanya niendelee uchunguzi wangu, kuhusu hizi imani..mtu kufa na baadaye kuonekana…au mtu kuonekana kafa, na baadaye anazindukana..kuna maeelzo ya kiimani, na kisayansi, nataka kuyaonaisha kiuchunguzi zaidi…’akasemda docta.

‘Kwahiyo unaamini kuwa mfu anaweza kufufuka kwa lengo la kulipiza kisasi…au una maana gani kwenye uchunguzi wako…..?’ akaulizwa na docta mwenzake.

‘Mfu hawezi kufufuka…mtu akishakufa amekufa,  mfu ni mfu tu…sasa iweje watu waamini kuwa kuna wafu wanaweza kufufuka…hiyo ndio hoja…kisayansi, tunaona hilo halipo, ..sasa hawa watu wanaoamini hivyo wanakigezo gani…nalichukulia hili tukio, maana naona kama linaweza kuleta hoja fulani, nataka kuliangalia kihivyo kwanza..japokuwa mimi naamini mu hawezi kufufuka, na ndivyo sayansi inavyosema…’akasema docta.

‘Sasa docta huoni kuwa tunafanya kitu ambacho kitatuchanganya tu…hebu niambie huyu mama ana nini zaidi mwilini mwake..?’ akauliza nesi, na docta kwanza akacheka , halafu, akatulia akiliwazia hilo, akasema;

‘Aaah, sio kwamba ana kitu cha ajabu mwilini…, zaidi ni hiyo alama ya upasuaji mengine ni kawaida tu,..majeraha usoni ya kukatwa, katwa na mapanga…vinginevyo  ni mwanadamu kamili aliyekamilika, kama ulikuwa na wasiwasi kuwa huenda huyo sio mwanadamu, labda ni mzuka,…. hapana huyo ni mwanadamu kamili…..’aksema docta.

‘Lakini docta ..kama ni mwanadamu kamili, basi….sio yeye,…maana  nilikuwepo, na  narudia tena..yule mama alikufa…mimi nilikuwepo nilimfahamu vyema huyo mama, maana mimi nilimuhudumia,..akazaa kwa upasuaji, na ilikuwa yeye au mtoto kupona, na bahati wakapona wote…kwahiyo nilimuona alivyokuwa…na huyu mama wa sasa ni mwingine na tofauti kabisa..’akasema nesi

‘Yawezeka hivyo…lakini, hebu tuone tukio hilo lilikuwaje kwanza…’akasema docta.

‘Docta nawaambia ukweli, huyu mama… hajawahi kufika hapa, labda kama alifika mimi nikiwa sipo…nina kumbukumbu zangu kabisa..huyu mama ni mgeni kabisa katika hospitali hii..labda kama alifika kwa matatizo ya kawaida, lakini kama yalikuwa mazito kiasi kikubwa na jinsi anavyoonyesha kuwa kachanganyikiwa….hajawahi kufika hapa…’akasema nesi

‘Usijali..hebu tuambie hilo tukio lilikuwaje….wewe lisimulie hatua kwa hatua, kama alikufa basi huenda ni mzimu wa huyo mama umekuja kwa namna nyingine..’akasema docta msaidizi akitabasamu huku akimuangalai docta mwenzake.

‘Yah…mimi nina hamu sana ya kusikia hilo tukio…tafadhali lielezee, na usiogope, sisi hapa ni watendaji wenzako…hatuwezi kufanya lolote , tupo kitu kimoja…na zaidi ya hayo tunachotaka ni nini, ni kumsaidia huyu mama, na wewe utakuwa karibu na huyo mama kuanzia sasa, …maana kama kapona hataweza kukataa kujifunua…pili hawezi kuleta matatizo, ningelitaka wewe tu ndiwe uwe karibu yake..’akasema docta.

‘Mimi nimeshaanza kumuogopa..’akasema nesi

‘Kwanini..?’ akauliza docta msaidizi.

‘Maana nyie ambao nawategemea kiutalaamu, mumeshaanza kujenga hoja kuwa huenda tukio hilo linahusiana na huyu mama,…ambaye nijuavyo mimi, huyo mama alishafariki, sasa iweje awe ni huyu mama…hamuoni ni kama kuamini mambo yasiyoelezeka, na mambo kama hayo mara ningi yanajenga hofu kichwani…’akasema nesi.

‘Ili ysijenge hofu, hebu jaribu kukumbuka hilo tukio, utusimulie, ili tuweze kusaidiana na kuliweka sawa, huenda huyu mama akaja kupata msaada tu, kutokana na hilo tukio hata kama sio yeye…unasikia,…muhimu ni kupata chochote kile kitakachoweza kusiadia….ila, narudi atena kwa uzoefu wangu… mimi naamini hayo anayoyasema huyo mama yana ukweli..’akasema docta.

‘Hapa ndio sikuelewi docta…ni nini unataka kuthibitsha…’akaulza docta mwenzake.

‘Ubongo wa mwanadamu uchukulie ni kama kumputa..unavyoweza kupokea taarifa na zile taarifa zikahifadhiwa mahali, na ukizitaka zile taarifa unazipata kwa kuitisha jina la ile taarifa ulivyoiweka,…sasa inakuja kuwa taarifa fulani ni kuba kuliko ile asili yake..komputa inashindwa kubeba…maana uzito wa kitu nao ni muhimu sana…sijui mnanielewa.

‘Watu hawa wanaochanganyikiwa, wanaweza kubeba kitu ambacho wakiwa na akili zao hawawezi kukibeba..umeshaona hiyo kitu..sasa ni uwiano gani wa akili, ..ambao uliwezesha mwili kuwa na nguvu zaidi…hapo ndipo imani za ghaibu zinakuja..uwezo kuzidi uwezo halisia…ni kitu gani kinafanya iwe hivyo…tuliache hilo..’akatulia

‘Mtu anaonekana kafa kabisa….kabisa..hata vyombo vya kitaalamu vinathibitisha hilo,..baadaye anazindukana,..hebu rejea mtoririko wa damu,..na msihipa ya fahamu, damu ikisimama ukaona hakuna mapigo, mwili unakuwa hauna uhai..ina maana basi pale mnapoona mtu kafa, kuna mshipa fulani kwenye ubongo utakuwa bado unafanya kazi, damunakila kitu ..lakini unakuwa hauna mawasiliano kabisa na mwili…..’akatuliza

‘Docta hapo unatuchanganya…hatukuelewi..’akasema nesi

‘Najua hamtanielewa,..na mimi ndio nafanyia uchunguzi..ndio maana nina hamu kabisa ya kusikia hilo tukio….na ili tusipoteze muda, …mimi nakupa nafasi ya kulifikiri ..ukiwa tayari tuambie..au tutaongea wawili..mwenzangu anaweza kwenda kuendelea na kazi zake, au mnaonaje..?’ akauliza docta.

‘Hata mimi nina hamu saan ya kulisikai hilo tukio..lina nipa hamasa, ilikuwaje…?’ akasema docta msaidizi.

Na hapo nesi akatuliza kichwa, akatafakari,…akaona kabla hajalisimulia, ni bora mwenyewe apate muda wa kuliwaizia, kwa makini, kabla hajasema lolote, na ikibidi kuwasiliana na wale madocta walikuwepo, akiwemo yule docta kijana ambaye ndiye alichukua jukumu la kumtetea…ndipo akili yake ikaanza kulikumbuka tukio hilo hatua kwa hatua…akaanza kukumbuka ilivyokuwa….

NB: Sehemu ijayo itafunua kile kilichotokea nyuma siku ile nesi alipokutwa na tatizo , tatizo lililochukuliwa kama uzembe, na likafikai yey kumpata mtoto, mtoto ambaye yupo mikononi mwa ndugu zake,…..je siku ile kulitokea nini…tuzidi kuwepo


WAZO LA LEO: Unapopata taarifa zisizo na uhakika, ambazo huenda ni mzigo kwako, au zinakutia mashaka, jaribu kwanza kuwa na subira,..chunguza ukweli wake… usikimbilie kuzikuza, ukaanza kupatwa na wasiwasi, uwoga…huzuni, ,,au kukimbilia kushutumu kwanza... 

Ukifanya hivyo utapunguza nguvu za mwili za kuhimili, utajipandikizia magonjwa ya moyo..shinikizo la damu,…kabla ya ukweli wa hiyo taarifa,  hata taarifa hiyo ikija huenda ikawa ni kweli au sio kweli..na kwa hali hiyo, utakuwa huna gunvu sahihi tena ya kuzipokea hizo taarifa…ndipo unakut mtu anaptwa na kiharusi, au kupoteza fahamu, au kushikwa na ugonjwa wa moyo. Ndio maana tunasema,  Tusijitwike mzigo kabla haujatua kichwani

Ni mimi: emu-three

No comments :