‘Mhh,unajua docta
nimekumbuka jambo, uliposema kama kuna
tukio mama alijifungua akafariki…kuna tukio liliwahi kutokea hapa hospitalini
ni muda sasa umepita…, lakini halihusiani na huyu mama…nina uhakika kabisa sio
huyu mama,….maana huyo mama tulikuja kusikia kaokotwa akiwa amefariki,
akazikwa, na mmoja wa nesi wa hapa alihudhuria mazishi yake…’akasema nesi ,
Je
huyu mama ni nani na kwanini mama huyu aje kudai kuwa kuna mtoto wake
alijifungulia hapo, na wakati muhuska mwenyewe, yaani mama aliyemzaa mtoto hapo akapotea kimujiza, anatambulikana kuwa ni marehemu?, …..
‘Kulikuwa na tukio la mama na mtoto si
ndio, .., mama akajifungua kukatokea kitu huyo mama akapotea,….halafu unasema
akaokotwa, akiwa amekufa…..sasa sisi tunahitajia kulifahamu hilo tukio, hata
kama sio lenyewe, lakini huenda likaleta picha…
‘Docta…’nesi akajitetea
‘Tunataka kusikia kuhusu hilo tukio, chukua muda fikiria kumbuka halafu utuambia kuhuus hilo tukio...unasikia nesi’akasisitiza docta
bingwa wa mambo hayo
Tuendelee na kisa chetu
**********
Nesi akabakia kaduwaa akikumbuka kuwa tukio hilo lilikuwa ni siri,
ni siri kati yake na wakubwa wake waliokuwepo siku hiyo maana linahusiana na
kesi ya mauji ya uzembe,..kesi ambayo ilitakiw akufikishwa mbele ya sheria,
lakini ikazimwa kinamna na yeye akiwa mshukiwa mkubwa,..lakini aliyejitahidi
kumtetea kwa juhudi zote ni docta aliyekuwa kijana kuliko wote siku
hiyo…nakumbuka docta huyo alimtetea na kupendekeza kumchukua mtoto amlee yeye.
Siku ile baada ya kutoka kuchukua maji ya kumuongezea mgonjwa na
dawa nyingine, alirudi chumba alicholazwa huyo mgonjwa,…na kukuta huyo mgonjwa
hayupo kitandani, na mipira imebakia ikiwa imening’inia kuonyesha kuwa mgonjwa
huyo ama kazichomoa mwenyewe au kuna mtu kaja kumuondoa ..
Alipoona hivyo akashikwa na butwaa hadi kudondodsha sinia
lililokuwa na maji na daa nyingine…akawa anajiuliza;
Huyu mama kaenda wapi?
Wazo kubwa kwake kwanza ilikuwa huenda madakitari walikuja kwa haraka wakamkuta huyo
mama kwenye hali mbaya wakaamua kumchukua kwenda chumba cha wagonjwa mahututi….akawazia
hivyo, lakini kwa jinis ilie mipira ya kuongezea maji ilivyo, haiwezekani
madocta wakafanya hivo, ipo shangala baghala bila mpangilio..sio kawaida ya
kiutendaji.
Au labda huyo mama alishakata roho wakamchukua kwenda chumba cha
maiti? Lakini tendo hilo limefanyika hivyo saa ngapi,..kwani aonavyo yeye hakukawia
huko alipokuwa amekwenda,… na kwanini lifanyike haraka kiasi hicho hata bila ya
huyo nesi kujua.
Haya yalikuwa maswali ya nesi siku ile.
Alipozinduka kwenye huo mshituka, akahisi huenda mgonjwa
kazindukana akatoka kwenda kjisaidia,..basi wazo hilo lilipomjia akilini, haraka haraka akakimbilia kukagua maeneo mbali
mbali, chooni na oisi ndogo iliyokuwepo hapo,..
‘Huenda kadondoka bafuni au chooni, akitaka kwenda kujisaidia au
kachanganyikiwa akawa anajiendea ovyo…’akawa anajiongelesha mwenyewe. Na alipohakikisha
kuwa sehemu zote hayupo, ndio kwa haraka akatoka mbio kuelekea kule walipo
madakitari wakiwa kwenye chumba cha mapumziko….
*********
Madocta wao walipona huyo
nesi haeleweki wakakimbilio hapo wodini…
Madaktari walipofika pale wodini na kukuta kuwa huyo mgonjwa
hayupo, walishikwa na mshituko, iweje mtu alikuwa katika ile hali, kazimia..hajiwezi, aweze kuinuka mwenyewe, na
kujichomoa ile mipira na kutoweka, kwa haraka kiasi hicho…au imetokea kitu
gani…
Wote sasa wakageuka kwa hasira, na muda hu nesi aliachwa nyuma, na
docta mkuu alieuwepo siku hiyo kwenye tukio hilo, akawa wa kwanza kugeuka
kutaka kurejea kuel alipomuacha nesi kupata ajibu ya maswali aliyokuwa nayo
kichwani lakini kabla hawajarudi huko, nesi akawa keshafika, na kila mmoja akamdaka
kwa maswali yasiyokuwa na mpangilio…
‘Huyu mgonjwa yupo wapi, nes umefanya nini..nesi
imekuwaje,..nesi.nesi….’
Nesi alibakia kachanganyikiwa hakujua amjibu yupi na majibu gani
atakayatoa ambayo yatawaridhisha hawa watu waliotahayari, kwani mgonjwa
keshatoweka , na haikujulikana moja kwa moja kuwa mgonjwa ameenda wapi,na ni
kitu gani kimemsibu.
‘Mimi sijui nilitka kwenda kuchukua maji ya kumuongezea,
niliporudi nimekuta hivyo..kama mnavyoona..’akasema nesi, na hapo kukawa hakuna
maswali zaidi ikabakia vitendo tu.
Ikabidi msako wa harakaharaka ufanyike kila kona, na kila eneo
hapo hospitalini, lakini hakupatikana cha mgonjwa au dalili zake, na haikujulikana
wapi alipoelekea kama alitoka nje au la, …hata walinzi wakadai kuwa wao
hakuwakuuona mgonjwa wa namna hiyo akitoka.
Wakati msako unaendelea, kikao cha dharura kikaitishwa na maswali
mengi yakaulizwa na yote aliulizwa nesi, kama ilikuwaje, kwanini uliondoka kwa
hali kama ile, je ulichukua muda gani, na uliporudi ulikuta nini…, naye
alielezea ilivyokuwa, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza wale madakitari.
Wote waliishia kumlaumu kuwa alifanya uzembe.
Yeye aliendelea kujitetea kuwa alitoka kidogo kwenda kuchukua dawa
na dripi za maji kwasababu iliyokuwepo ilikuwa inaanza kuisha, na wapo mashahidi
waliomuona..na aliporudi akakuta mlango upo wazi, na alipoingia ndani akakuta
mgonjwa hayupo kitandani, na ilionyesha wazi kuwa aliinuka na kuchomoa ile
mipira yote mwilini mwake na kuondoka humo ndani.
‘Una uhakika kuwa alichomoa yeye mwenyewe, au alichomolewa…?
akaulizwa
`Je ulijaribu kutafuta vyumba vingine kwa muda huo kama hakukuwa
na mtu mwingine wa kumsaidia…?' walimuuliza maswali mengi kwa mafululizo
`Nani angekuja amchomoe hiyo mipira na …sidhani kama kuna mtu
alifanya hivyo zaidi yake mwenyewe…’akasema docta mwingine.
‘Kwa hali kama ile inawezekana kweli..anaweza kuwa alizinduka,a
akiwa kachanganyikiwa..lakini yule mama alikuwa mzaifu sana…’akasema docta
mwingine.
‘Nesi akasema alipofika nakuona hivyo, alikagua sehemu zote lakini
hakuona hata dalili ya huyo mama..na ndio nikakimbiak kuja kuwafahamisha..,
kwani nilifikiria labda mumekuja kumchukua …' alisema huku akitetemeka.
Msako ukwa unaendelea hadi kufika meneo jirani..eneo lote la
hospitalini, chumba hadi chumba, vyooni, na kila mahala na mkuu wa ulinzi
alikuwa keshapitia kila mahala meneo yote kuzunguka hospitalini..vijna
wakasambazwa kila kona, lakini hawakukuta au kupata dalili ya mgonjwa kama
huyo, ikawa kama kayeyuka hewani!. Mwishowe ikabakia madocta kujiuliza watasema
nini kwa jamaa za mgonjwa pindi wakija kumuulizia mgonjwa wao…
Basi baadaye, baada ya kuhakikisha kuwa huyo mgonjwa hayupo eneo
la hospitalini, kikao cha nidhamu kiliitishwa, na hili lilifanyika baada ya
kuwahusisha mlinzi mkuu;
‘Sasa huyu mgonjwa inavyoonekana kapotea..na ni mara ya kwanza kwa
kitu kama hiki kutokea,..tunaogopa kukimbilia haraka kutoa taarifa kituo cha
polisi,…unasemaje mkuu wa ulinzi?’ akauliza mkuu.
‘Ni muhimu kama kuwafahamisha polisi maana hatujui ni kitu gani
kimetokea, lakini ni badaya kujirizisha wenyewe kuwa kweli tumeshindwa kumpata
maana hata tukitoa taarifa mara nyingi unaambiwa kusubiri masaa 24..sasa sisi
hayo tuyafanie kazi kwanza..’akasema mkuu
‘Haya endelee ni kazi yenu ila sisi ndio tutakaowaarifu ni nini
cha kufanya, ili tuone tatizo lipo wapi..’wakaambiwa walinzi na masako
uliendelea kwa siku hiyo na hata kesho yake.
Baadaye utawala ukaonana
polisi waarifiwe, na kituo cha karibu kikapewa taarifa, na wao wakasema
watafuatilia… na anayehusika na uzembe akaamiwa afike kituoni, na katika hali
ya utendaji wakaoiomba polisi kuwa mtu wao asishikiliwe kwanza, kwani bado wao
kama utawala wanafanya uchunguzi, kukawa na maelewano ya chini kwa chini….basi
polisi wakasema uchunguzi utafanyika..hakuna kilichoendelea kwa siku hiyo, na
hakuna kilichopatikana.
Kikao cha nidhamu kikautana, na kama ilivyotarajiwa na wengi kuwa
kikao hicho kikuatana kinakuwa hakina huruma..moja kwa moja ,ikaamuliwa kuwa
huyo nesi asimamishwe kazi kwa muda wakati uchunguzi unaendelea kufanyika, na
kama ikigundulika kuwa ni sababu ya uzembe wake itabidi afukuzwe kazi!
Nesi akaitwa kujiteta zaidi,…siku hiyo nesi hakuweza
kuvumilia,aliishia kulia na hakuwa na la kujitetea, angelijiteteaje, …alibaki
kuwaza mengi, kuwa sasa kazi ndio kaikosa, na ataishije,na hiyo ndio ilikuwa ni
ndoto yake…aliomba asamehewe….na wakati anaomba msamaha, akasikia sauti ambayo
aliiona kama `muokozi’ wake wa siku ile’
‘Jamani mimi naona tutakuwa hatujamtendea haki huyu nesi,…’
akainuka dakitari kijana kumtetea yule nesi, lakini kabla hajaelezea lolote.
Yule dakitari bingwa akamkatiza
‘Sikiliza kijana, huyu nesi alijua kabisa kuwa huyo mgonjwa yupo
katika hali mahututi, ndio maana tukamuacha na huyo mgonjwa, na anajua kabisa
alitoka kwenda, huko kuchukua dawa, lakini akajisahau na kuanza kupiga soga, ..tumeulizia
wenzake, na hata mkuu wa manesi kasema alimkuta akiwa anachngulia mdirishani.
‘Huu ni uzembe..alifika pale tunapofanyia kazi akawa anachungulia
kuona kama tumemaliza kazi, ili atoroke, au alikuwa na sababu gani nyingine ya
kuja kutuchungulia tukiwa tunaanya kazi..hili halivumiliki….halisameheki…nawajua
sana hawa manesi wa hapa, wanapenda sana kuongea kuliko kuchapa kazi, nami,
napendekeza kuwa itolewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine…’. akasema
dakitari bingwa wa kitengo hicho !
‘Hili hata mimi nakuunga mkono, nimeona tabia isiyorizisha kwa
watendaji wetu hasa manesi, wagonjwa wamekuwa wakilalamika…wana lugh
chafu…wanawabeza wagonjwa…huduma mbovu,..sasa hili litatuweka uchi kama likiika
kwa watu…kabla hatujaharibu kazi zetu mimi naona adhabu kali itolewe….’ akasema
kwa hasira yule dakitari mwingine!
‘Kwani wewe kijana ulikuwa unataka kusema nini , naona ulikuwa na
hoja, hebu tumsikilze kwanza huyu kijana..’ akasema mkuu wa hiyo hosptali.
‘Kutokana na maelezo ya huyo nesi inaonyesha kuwa , hata angekuwa
nani kosa hilo lingetokea…! Ndio alitakiwa kutumia simu kumfahamisha mwenzake
alete hizo dawa, lakini kama ujuavyo, unaweza ukapiga simu mpaka ukachoka,
mwenzako asikujibu, yeye aliona mgonjwa bado yupo kwenye ‘koma’, akaona akimbie mara moja kuichukua hiyo dawa na atamkuta
hajaamuka, inavyoonyesha huyo mgonjwa alizinduka ghafla na kuondoka.
‘Yah, lakini je alijaribu kupiga simu..maana usilaumu tu kuwa
ukipiga simu hakifanyiki kitu..yeye hakujaribu kufanya hivyo, kweli si kweli..?’
akauliza docta bingwa.
‘Ndio kosa limefanyika, lakini kwa kumhurumia, mimi napendekeza
kuwa yeye abebe jukumu la kumlea huyo mtoto, tukumbuke kuwa kuna mtoto mchanga
kaachwa, je mtoto huyo atalelewa na nani, ..sijui kuna taratibu gani, mimi
najiuliza kichanga hicho hakina mama wala baba au ndugu yoyote, nani atachukua
jukumu hilo…’ akasema dakitari kijana.
Kauli ya dakitari huyo kijana ikafanya jopoo zima la nidhamu kukaa
kimia kwa muda, kwani maneno yake yana hekima, ikabidi madakitari
waangaliane, walipogundua kuwa kweli mtoto anahitaji mtu wa karibu wa
kumuhudumia, wakawa kimya kidogo kuwaza kila mmoja akijua kuwa kumbe kuna
jukumu jingine, kama hakuna mu mmojawapo atabeba hilo jukumu…!.
‘Sawa kabisa,…mimi naona
Kijana kanena vyema,..jamani, hilo
hatukulifikiria, na mwisho wa siku tungelihangaika wapi pa kumpeleka huyo
mtoto. Na nafikiri hili halina mjadala, litakuwa jukumu lako wewe nesi kutafuta
jinsi gani ya kumhudumia huyo mtoto, na kama kuna mambo ya kisheria
yatahitajika baadaye, kama huyo mama au jamaa zake hawataonekana basi,
hospitali itatoa msaada huo.
‘Na sio kwamba sheri itakaa kimia bado tunaliuatilia hili jambo
kwa ukaribu wake,…kwa hivi sasa tunalifanya hili kwa kumsaidia nesi..kwahiyo
iwe siri….hili tunakubaliana hapa hapa..huku tukisema uchunguzi bado
unafanyika….’akasema mkuu huyo
Eti mnaonaje…nesi atamchukua huyo mtoto na yeye atajua la kufanya,
kama atahitajia msaada wa kisheria…hilo tutaliangalia…u kuna lolote zaidi uhusu
hilo jukumu..?’ akasema mkuu wa hospitalini na alipoona hakuna hoja ya zaidi,
akamgeukia yule nesi na kumuuliza kama analakusema, au bado anaona kaonewa kwa
adhabu hiyo, kwani vinginevyo angeishia kufukuzwa kazi….
Yule nesi akasema hana la kusema zaidi na atajaribu kutafuta njia
za kumlea huyo mtoto mpaka mama yake atakapoonekana…
Nesi japokuwa alikubaliana na hilo lakini kichwani akawa
anajiuliza kweli ataweza jukumu hilo, jisni gani ataweza kujigawa, kazi na
kulea huyo mtoto, ni kitu ambacho hakukitarajia na hakikuwa katika mpangilio wa
maisha yake ya karibuni, lakini akawa hana jinsi, vinginevyo kazi ataikosa, na
hata kufungwa…!
Baada ya hicho kikao, yule nesi alimtafuta dakitari kijana ili
apate angalau kumshukuru kwa kumukoa kwenye janga la kufukuzwa kazi, lakini
ikawa vigumu, kwani kazi zilikuwa nyingi wagonjwa mahututi walikuwa ni wengi,…na
wakitoka hapo wamechoka..lakini baadaye akapata nafasi ya kukutana naye;
Ilikuwa wakati yeya anatoka
kuelekea huko alipo mtoto kuangalia taratibu za kumchukua huyo mtoto na
dakitari kijana alikuwa katokea huko wanapohifadhiwa watoto, akiwa na simu
ambayo ina vii vingi ikiwemo kamera ya hali ya juu, video..na inaonekana
alikuwa akiitumia.
Kila mmoja alikuwa na haraka, wakajikuta wanagongana..na
walioanaliana kila mmoja akamtaja mwenzake kwa cheo chake;
‘Docta…
‘Nesi..
Nesi akiwa anaokota barua aliyopewa na utawala, akasimama haraka
kutaka kuongea na huyo dakitari kabla hajaondoka kwenye upeo wake, akasema;
‘Samahani docta naona siku ya leo itapita bila kupata muda wa
kuushukuru…japo kuwa kwa kaui tu..kauli tu ya kushukuru..’akasema nesi,a na
docta ambaye alishaanza kuondoka…akasema;
‘Oh..nesi.., usijali..ni kawaida tu…na usiwe na wasiwasi kwa
hilo.., hiyo ndio mitihani ya kikazi,a na tunapokutana sehemu za kazi kama hivi
na kuna namna ya kusaidiana ni wajibu wa kila mmoja wetu kufana hivyo, sisi
kutokana na kazi ni ndugu, hakuna cha ubosi au nani..anayejiona ni toauti,
kwasababu ya cheo huo ni ubainfasi wake tu..…’akasema docta.
‘Ni kweli lakini ueona ilivyokuwa,…madiktari wote walishakubaliana
kuwa nifukuzwe kazi kasoro wewe tu…yaani wamesahu mazuri yangu yote…na hili
sikukusuadia kabisa…na sikujua kabisa litatokea,…lakini nakushuru sana wewe
maana ..hata sijui niseme nini, umenitetea..sikutarajia kabisa…’akaziaid
kusema.
‘Hawakufanya hivyo kwa nia mbaya kuwa wanakuchukia hapana…ila
sheria inawabana..na mhh, usijali…mimi nilifanya nikijua ni sahihi kuanya
hivyo, hata wewe, ungelifanya hivyo…ni swala la kusema unavyoona ..au sio…’akasema
docta na nesi akawa anajaribu kusikiliza kwa makini anachoongea docta huyo,
lakini kwa jinsi kulivyokuwa na kelele , uoande ule wa ili wanapokuwa wagonjwa
wa nje, hakuweza kusikia vyema…akawa kama anabahatisha tu kuwa mwenzake kasema
nini.
‘Je wewe una mipango gani, kwani inatakiwa uhakikishe kuwa mtoto
anapata huduma zote, je utakuwa na nafasi hiyo?’ dakitari kijana akasema sasa
akijaribu kutaka kusema jambo muhimu kwa huyo nesi, na alitaka asikia
anachosema kwani aliona kuna umuhimu wa kuongea naye. Sasa akaonekana kutulia,
japokuwa mwanzoni alionekana kuwa na haraka.
‘Mipango ya nini…?’ akauliza nesi, hakusikia maneno ya mwanzoni,
vyema
‘Ya kulea huyo mtoto..?’ akasema docta.
‘Mhh, mimi kwakweli nimekubali tu maana hebu nambia pale
ningelisema nini tena…kwa hivi sasa hata sijui nitafanyaje..maana hata jinsi ya
kuishi na mtoto..mmh, sijajipanga kwa kweli najiuliza na kukosa jibu, ..’akasema
nesi huku akionekana kuwa mbali
kimawazo, na dakitari akalijua hilo kuwa huyo nesi anahitajia ushauri.
‘Kama unahitajia ushauri mawazo…useme mimi nipo, wapo madakitari
wengine ni muhimu upate ushauri wa kuja kukusaidia,..japokuw amamuzi
yameshatolewa..’akasema dakitari kijana.
‘Yaani kwa hivi sasa hata sijui niombe ushauri gani…mwenyewe
kichwani hata siamini..maana matukioo ametokea kwa haraka hili linakuja ..mara
jingine…unaonaeeh…nimejiuliza sana nifanye nini , nimeshindwa, na ….’
Akakatisha maneno alipoona dakitari kijana anamsogelea karibu yake kusikia
alichokisema maana hapo walipokuwa akiongelea kulikuwa na kelele nyingi za
wagonjwa.
Nesi akainua uso kumuangalia huyo dakitari, kwani alikuwa karibu yake sana na hakutarajia
itakuwa hivyo, kuwa naye wakiwa wawili, na sehemu ya upweke japokuwa sio sana,
maana watu wanaopita mwisho wajengo kwenye milango mikuwa ya kutokea wanawaona.
Nesi alipoona dakitari huyo kijana kamsogelea, na sasa wanaangaliana…akabakia kaduwaa,
dakitari alifanya hivyo akitarajia na nesi naye atasogea mbele zaidi ili kuzikwea
zile kelele, lakini nesi akawa kasimama pale pale, sasa wakawa wanaangaliana uso kwa uso, ilikuwa ni kwenye korido na
sehemu hiyo ni nyembamba kidogo, mtu akiwaona atajua hao ni wapenzi.…
Nesi hakutarajia hilo…na hakusogea, akawa kasimama pale pale tu…na
ile kuwa karibu na huyo dakitari, ambaye
muda mwingi alikuwa akimuwaza, ilimfanya yeye
ajisahau..na akili akiyasahau yaliyopo mbele yake… .
Nesi ghafla , bila kutajia akajihisi mwili mzima ukisisimuka. Nesi
kwa akili yake ya haraka alijua kuwa mwenzake kamsogelea hivyo kwa nia ya
kumliwaza kwa kumkumbatia, kwahiyo aakwa anasubiria kushikwa kinamna..., kumbe Dakitari
kijana, alimsogelea ili asikie nini anachoongea, kwani sauti ilikuwa haisikiki
vizuri, kutokana na upepo.
Akili ilivyo, tamaa na hamasa hutekwa mara moja na majambo kama
hayo,..hasa kwa matendo yale ya kufurahisha nafsi,..nesi akakumbuka jinsi gani
alivyokuwa akiisubiria hiyo nafasi na kuiombea itokee japokuwa, angalau kama
hivyo…japokuwa imekuja muda ambao sio muafaka..lakini akaona sasa muda ndio huo
akiukosa tena …basi, atajijutia..sasa akataka japokuwa sio sahihi, kumuonyesha
huyo dakitari kuwa kweli anamapenda...
Akainua uso wake kumtizama dakitari kijana usoni,….., akajikuta
dakitari kijana akiwa kamgeuzia sikio..akaona ajabu….,’Au kageuka tu kutizama
kwingine baada ya kuniona niminama, siuangalii…’…akawa anajiulia nesi
‘Umesema nini maana nilikuwa sikusikii vyema,..unajua kuna
kelele..unaweza kusogea huko, huko…ki-do-go…’dakitari kijana akaongea na
kuonyeshea kwa kiganja cha mkono ili nesi asogee, lakini nesi hakusikia hilo,
..alishazama kwenye dunia nyingine, akawa kasimama pale pale macho yake
hayabanduki kumungalia huyo dakitari usoni, akajikuta akisema;….
‘Ohhh, …hata sijui niseme nini…nikushukuruje dakitari wangu, bosi
wangu mhhh… mimi nakusikiliza wewe tu, maana
hapa akili sio yangu..leo kurwa natauta muda tuongee, nikushukuru…yaani we acha
tu….nilikuwa siku nyingi natafuta….’akasema nesi, lakini docta akamkatiza.
‘Sister, sikiliza nilikuwa nakuuliza hivi kwani wewe huna ndugu,
ambao wana nyumba,…yeney nafasi…si unajua…au
ndugu wanahitaji mtoto..si unaelewa,…., kwani dunia hii ilivyo…., wakati
wengine wanatupa watoto, kuna watu wengine wanawatafuta watoto hao hao..’akasema
docta na nesi akawa kimia.
‘Siumesikia hilo mara nyingi, hata kwa redio au kwenye runinga au
sio…hata wewe mwenyewe kulithibitisha hilo, au sio, kuna watu hawalali,
wanatamani kupata mtoto hata wa kule, …kwa udi na uvumba..au nimekosea sister
hawo…?’ Docta kijana alimwambia, na aliposema hayo maneno nesi akakumbuka kitu…..
Nesi uso ukapanuka kwa furaha..ni kama vile mtu kapewa kitu cha thamani
au zawadi ulani asiyoitarajia, jinsi gani uso unevyomemeteka kwa kuonyesha ile
furaha, ndivyo ilivyokuwa kwa huyu nesi, …akatoa tabasamu la nguvu, huku akimuangalia
dakitari kwa uso uliojaa bashasha…kwanza akatulia…, halafu akasema;
‘Umesema nyumba yenye nafasi…kwangu twaweza kuongea..kwangu
unapafahamu eeh…hata leo…kwani wewe ulisema unaishi bado na wazazi wako kwasasa…?’
akauliza huku akionekana kuwa na furaha hata dakitari akashangaa.
‘Kiukweli docta leo…ooh, pamoja na balaa hilo..lakini sijui
nisemeje..yaani niseme tu furaha isiyomithilika.
..kwanza umenisaidia,..maana nilishakata tamaa, unajua niliwapigia ndugu zangu simu,
nikashindwa hata la kuwaambia nikawa nalia tu,..nilijua nakwenda kufungwa…na
ukatokea wewe muokozi wangu…yaani..hata nisemeje,,,maana umenisaidia sana na bado..umeniambia
jambo..oh, docta niruhusu..oh’akatulia akionekana kujawa na furaha.
‘Kwani vipi sister mbona umebadilika ghafla….?’ Akauliza dakitari
kijana.
‘Unajau docta umeifungua akili yangu….maana sijui nisemeje…unajua
mungu ni mkubwa, bado tu… unaendelea kunipa ushauri ambao sikuwa nimeukumbuka…,
kwakweli niameamini kuwa wewe ni sehemu yangu kwenye nafsi yangu, moyoni
mwangu, nisamehe tu kama nitaongea vibaya, lakini kwanza hebu nifafanulie,
kwanza umeniulizia kuwa kuna sehemu yenye nafasi…ukasema nyumba yenye nafasi, ni
ili tuongee au….?’ akauliza nesi
‘Hapana..sikumaanisha hivyo… unajua nesi, nikaumbie ukweli, mimi hapa hospitalini, nipo kwa muda tu, na
nina lengo moja kufanikisha ndoto zangu za kuwa dakitarii bingwa..ni kiukweli
mimi…bado naishi na wazazi..sijajipanga kuwa na kwangu,…na- na bado naendelea
kusoma, sijajua mipangilio itakuwaje huko baadaye…’akasema dakitari.
‘Lakini unaweza kuanza mipango yako sasa haiwezi kuzuia kusoma au
? na vitu kama seehmu ya kukaa, hata chumba, au vyumba ni muhimu uwe navyo au? Na
wewe unahitajika hata kupewa nyumba, si ndio…halau mengina kama mke,..ynakuja
au..na mke inaanzia kwenye urafiki, au unaye tayari..?’ akauliza nesi.
‘Unajua sisiter..nimekuelewa, lakini kiukweli,… kila kitu na muda
wake..mimi hayo muda wake bado, siwezi kujidanganya…lakini ndio kam binadamu ni
lazima uwe na matarajio ya baadaye, yaweza ikawa ndoto, kama hutayafanyia kazi,…mimi
ni mwanasayansi, sitakiw sana kuishi kwenye ndoto…si unajua, naangalia
uhalisia,..’akasema
‘Najua…’akasema nesi.
‘Ndio…, nikianza kazi, na kutulia hayo ya sehemu ya kukaa, mke..yatakuja
yenyewe,....kwa hivi sasa hilo halijaniumiza kichwa ila mimi..sister, nilikuwa nakuulizia wewe...maana sasa una
mtoto, hana baba, lakini mama yake ni
wewe, na kwa ajili hiyo unahitajia sehemu yenye nafasi…au sio’akasema
‘Yah…nimekulewa, lakini kwa hali hii, najuauananihurumia sana, na
naogopa hata kukuombamsaada zaidi, …nikisema hata wewe unaweza kuwa baba yake,
sijui kama nitakwua nimekosea..au sio?’akasema nesi na dakitari akatabasamu na
kusema
‘Ni kweli …kiujumla huyo mtoto kila mwenye moyo wa huruma atakuwa
ni baba yake…wapo watoto kama hao, wengi, ..unawakuta mitaani, jamii haiwajali,
mimi ni baba wa hao watoto na kila
mwenye hekima, mwenye moyow a huruma ataliona hilo,..hebu jiulize wao walipenda
iwe hivyo, au tujiulize ina maana mungu hana huruma kwao, awaache hivyo…hapana
hilo ni mtihani kwetu, …ndio maana mimi kama baba nimeanza kwa kujitolea
kimawazo, au sio..’akasema dakitari.
‘Ndio ..dakitari, mawazo yangu ..natamani iwe hivyo, mimi na wewe tunaweza
tukamtunza huyu mtoto kwa pamoja, yaani akajiona kama ana wazazi aisgundue
kabisa....mimi na wewe kwani haiwezekani…?’akasema nesi, na dakitari
akatabasamu zaidi na kusema.
‘Acha,utani sister, mimi bado ..sinimekuambia bado nasoma…sasa
sister, naona tusipoteze muda,…hili ninalotaka kukuambia ni muhimu
sana…nilitaka kuulizia, kama unao ndugu ambao wanaweza kukusaidia, au ndugu ambao
wanahitajia mtoto, itakuwa bora zaidi kwako,..unaonaje hilo wazo..?’ akasema
dakitari ambaye alionekana kutokutulia kwa kuwa karibu karibu hivyo na huyo
nesi, wakiangalaina uso kwa uso.
‘Oh…ndio maana nikakuambia nina furaha sana moyoni, furaha
isiyoelezeka,..wewe umenikumbusha jambo, jambo muhimu sana, sijui kwanini
sikulikumbuka kabla…, …kweli wewe ni wa pekee …ahsante sana dakitari, unajua wazo
kama hilo lilikuwa limenitoka kabisa..naona wewe mmmh, hata sijui niseme nini
..tungeishi pamoja ingelikuwa ni bora zaidi, maana mawazo yako yanakwenda
sambamba na ya kwangu unaonaje…usinifikirie vibaya, ila naona hivyo tu samahani
kama nimekosea..’akasema nesi
‘Kwanini…ni kweli nimejiuliza sana furaha hiyo kubwa imetoka wapi
ghafla, maana tokea kwenye kikao nilikiona umenyong’onyea..?’ Akauliza dakitari
kijana, sasa akiwa anajaribu kusogea nyuma.
‘Mhh..unajua nahisi tukio hili limetokea kwangu ili …dada yangu
apate mtoto..’ akatabasamu na kuinua uso
kumuangalia dakitari kijana,..na dakitari kijana akakwepesha macho na kuangalai
kwingine.
‘Dada yako…apate mtoto..anahitajia mtoto au?’ akauliza dakitari
kijana kwa mshangao
Nesi alijikuta tu, keshainua mikono, huku akiwa kamsogelea
dakiatri kijana, na sijui ilikuwaje akajikuta kamkumbatia..na kwa haraka
akambusu shavuni…. Na tendo hili lilimuacha dikitari kijana akiwa kashikwa na
butwaa.
‘Ahsante sana..yaani ungelijua… sijui hata nikushukuruje……’akasema
nesi, na akataka kuachia mikono yake, kwani alijiona huenda kafanya jambo
lisilofaa, lakini alitamani liwe hivyo, na mikono ikawa mizito kuondoka mwilini
kwa dakitari huyo.
Dakitari kijana kwa muda ule hakulitarajia hilo tendo kabisa, na
kiukweli, japokuwa kama kijana alikuwa na damu inachemka…lakini hakupendelea
kabisa hali hiyo imtawale kipindi cha kazi, na mazingira yenyewe ambayo aliona
yamejaaa mitego mitego…alishajijengea msimamo wake, na hakutaka kuuvunja,
akajaribu kujizuia, na kuzuia hisia zozote kwa hasa kwa hao manesi hapo
hospitalini.
Ndio kama kijana kuna siku na siku analiwazia sana hilo, na hata
akikutana na wenzake kuna muda wanaliongelea, hasa ikizingatiwa kuwa hospitali
hiyo imejaliwa kuwa na manesi wazuri na warembo…basi wakikutana na wenzake kuna
muda wanabadilishana mawazo, na maswala kama hayo hayakosekani ..
Ni katika kuongea pia na wengine, kunahali ya kutaniana…na kwa
vile alikuwa kijana ukilinganisha na wenzake..na pia alijaliwa sura ya kuvutia,
wenzake wakawa wanamuulizia kuwa je yeye kamchagua nani kati ya warembo waliokuwepo
hapo..yeye kiukweli kama ingelikuwa ni lazima kufanya hivyo, kuchagua rafiki, huyo nesi angelikuwa ni chaguo lake..,. Yalikuwa
ni mawazo tu kichwani.
Hata siku moja wakati anaongea na wenzake, alisema;
‘Najua kabisa, ukijiingiza kwenye maswala ya mahusiano, ..hasa
kwenye sehemu za kazi utajikuta ukikwazika hapa na pale, na matokea yake
hutaweza kutimiza malengo yako..na utendaji wako unaweza kuwa na mapungufu …. Mimi
sitaki mahusiano na nesi yoyote hapa au sehemu yoyote nitakayokuja kufanyia
kazi…’akasema na wenzake wakawa wanamtania kuwa anawaficha ukweli, ni lazima
anaye rafiki hapo hospitalini.
‘Hii ni kawaida kwenye kazi zetu, maana sisi hapa tunajuana,…ilivyo
kwa vile muda wote tupo pamoja..hatuwezi kudanganyana.. kazi hizi zinachosha bwana…,
na sia mbaay ukipata muda kuwa na mwenzako mkabadilishan mawazo au sio..kazi na
dawa..au sio….’akaamba na jamaa ake waliyekuwa karibu naye sana, yeye akacheka
tu
‘Ndo hivyo…najua unaye ndio maana unacheka…, wakati mwingine
unaweza kukutana na staff mwenzako
maana mumezoeana naye, mkaliwazana..sio lazima muwe wapenzi wa kabisa
kabisa..ni kupotezeana mawazo tu..’akawa anashawishiwa na wenzake.
‘Mmm..mimi naona muda huo sina kwa hivi sasa..,hasa kwa wafanyazi
wenzangu wa kike, …..nawaheshimu kama dada zangu tu…si zaidi, ‘akasema
‘Mhh..wewe wasema tu…najua wewe una aibu sana,..lakini ipo siku
nitakufuma na yule nesi, nitakupiga picha niibandike ukutani…’akasema mwenzake.
‘Hahaha…haitatokea..wewe hunijui eeh,… ujue mimi nina
msimamo..usinione hivi…yaani unikute kipindi cha kazi nipo na msichana,
tunakumbatiana,..aah, hapana, mimi kwangu naona ni makosa ya kazi…na sitaki
kabisa nifanya hayo makosa, nina mengi ya kufanya nikiwa kazini sio hilo….’akasema
‘Nakuambia utakuja kuon siku yake unajifanya msiri sana..yule yule
mnayekuwa naye kazini wakati wote, huyo huyo anaweza kukubadili mawazo …ipo
siku nitakunasa naye..’akaambiwa.
‘Niamini, hilo halitaweza kutokea..’akasema
‘Unajua …kuna yule sister, nesi
mkuu, aliniambia kuwa wewe unajifanya huna habari na akina dada, lakini una
madhaifu yako,..kwa vile tu hujapata wa kukuchangamsha..na kaahidi kuwa ipo siku
atakunasa, aufichue unafiki wako..kwani kashakuona kuwa wewe na yule nesi mpo
marafiki, mnaangaliana kwa kujificha… na kasema siku akigundua tu…si unamfahamu
huyo dada alivyo.’akasema
‘Yule dada ..hata simuelewi…kuna siku kaniganda..unajua nilitamani
nimtie kibao…yaani dada mtu mzima,...yule si kaolewa na watoto hata wajukuu
anao ….hutaamini,..nilimchenjia… mdada mzima ovyo…, ana..weeeh, nilikasirika
mpaka akajua kweli nimekasirika…, halafu eti… badala ya kuona kuwa katenda
kosa,anacheka, …kwa dharau kweli…’akasema huyo dakitari kijana.
‘Yule ndivyo alivyo bhana…, ukimjulia wala huwi na shida naye, ni
mtu mnzuri sana, wewe akianza matani yake wewe jifanye kama unampenda vile…basi
anaona rahaaa…. Wewe waakti mwingine fanya atakavyo…ilimradi usiende mbali…maana
anakutega ukijifanya umenasa, atakuumbua, sio kweli anavyofanya ukahisi
kadhamiria,..’akasema
‘Sasa kwanini anafanya vile?’ akauliza
‘Ni mtu wa kihivyo, utani, mwingi…nakuonya usije ukahadaika
ukafikiri ni muhuni… uwe makini sana naye, kuna watu wameumbuliwa…basi
ukimjulia …aaha, utafurahia kuwa naye kazini lakini ukijifanya unamdharau
atakuchezea..atakufanyia vituko na ole wako uje kufanya kosa…hatakusamehe…’akasema
‘Mimi nilitata kumshitaki..’akasema dakitari kijana, na mwenzake
akacheka hadi kutoa machozi
‘Hahaha..kumshika, kwa kosa gani…hahaha, hivi wewe upoje..wewe mwanaume
kweli..hahahaha..nikuambie kitu ungefanya hivyo ungeumbuka…., hivi unamfahamu
yule dada alivyo, madakitari wenyewe wanamuheshimu…watu wasiomjua wanaweza
kumuhisi vibaya, lakini ..fika nyumbani kwake, huwezi amini..yeye anafana hivyo
kama kuwafanya watu wajione wapo pamoja..ni ..sijui niseme nini..katabia kake
tu…’akasema
‘Kwangu mimi nimemzarau…kiukweli sikutarajia kuwa atanifanyia
hivyo…lakini nimemsamehe..kama ni utani tu, basi,….’akasema
‘Unajua nikuambie kitu, yule dada anajua kuongea anajua kugeuzia
mambo..ungejidanganya ukaenda kushitaki,a ngetoaboa siri zako zote..auanjua
mengi kuhusu wafanyakazi,…nakuambia siku hiyo ungeaibika..’akasema mwenzake.
‘Mimi niliona ajabu anavyowashika -shika hata wasichana ‘akasema
‘Ndivyo alivyo..ni utani tu, na wasiomfahamu wanamfikiria vibaya,
hana lolote yule..ni seehmu ya kuwafanya wasichana wafurahi tu na wachape kazi,
…pamoja na utani hataki uzembe……’akasema mwenzake.
‘Mhh, hata mimi huko alipokwenda nilishambadilikia …mimi nikiwa
kazini ni kazini tu…’akasema
‘Mhh…ngoja ipo siku atakunasa na huyo nesi, ..humjui yule dada,
atakutundika uchi….unajua kutundikwa uchi, anakutangaza kusipofaa…nikuambie
kitu mchukulie kama mtani wako tu…utafurahia maisha yake..’akasema.
‘Unajau mmi sijui nipoje…naona kuwa nikiwa na urafiki wa namna hiyo kazini nitashindwa
kuwajibika..na kama nikitaka kutafuta rafiki nitafanya hivyo kwa wakati
muafaka, na sio hapa kazini, au sehemu nitakayofanyia kazi…….sitaki nije
kushindwa kazi kwa sababu ya mapenzi…’ alisema hivyo akiaongea na rafiki yake,
ambaye alitaka kujua kwanini yeye hana rafiki wa kike.
Leo anajikuta yupo na nesi..na walivyokuwa wamesimama mtu yoyote
atasema ni wapenzi…hakutaka kabisa aonekane na wakati anaangalia huku na kule
mara akamuona
Alikuwa yule mkuu wa nesi, alikuwa kwenye chumba cha juu
akiwaangalia na mwani yake akijifanya anasoma makabrasha yake…, na kashika kitu
kama simu…, ndio maana alijisogeza karibu na huyo nesi ilikuwa mbali na upeo wa
kuonekana,…na ilikuwa ni pamoja na kutaka kusikia anchoongea huyo nesi,na kwa
muda ule nesi yeye hakujua lengo la mwenzake
Nesi hakulifahamu hilo….
WAZO LA LEO: Kiongozi bora ni yule aliye mfano bora kwa watendaji wake, kitabia kikazi na hekima, na asiwe mkali wa kutisha na kuwafanya watendaji wake kama watumwa na kumuogopa yeye kama mnyapara...yeye kama kiongozi bora anatakiwa awe karibu na watendaji wake..na watendaji wake wajihisi ni sehemu ya familia hapo kazini....
Na kwenye masilahi, kiongozi bora, ni yule anayejali watu wake `kwanza', kabla hajajali 'tumbo' lake, na ajue kwa anabeba dhima, sio kwa hao watendaji wake tu na hata afikirie na familia za hao watendaji wake, kwani utendaji huanzia toka nyumbani, kwani akili ikitulia toka nyumbani, ndivyo utendaji utakavyokuwa mzuri ofisini na sehemu za kazi.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment