Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, July 4, 2014

DUNIA YANGU -1


Yaliyokuja kutokea baadaye....

Chumba kilikuwa kimya, zaidi ya mngurumo mdogo wa kipoozeo cha hali ya hewa, kulikuwa kama vile hakuna mtu ndani ya hicho chumba. Katikati ya makitaba hii ambayo pia ni chumba maalumu cha maongezi,kulikuwa na kiyoo kikubwa ambacho kilikuwa kikionyesha kila kitu kinachofanyika ndani na nje ya jengo hili.

Na kwa mbali kulionakana sura ya mama mtu mnzima kidogo, ikitokea kwenye chmba kingine, mama huyo mkononi alikuwa ameshika joho jekundu, hilo kwa imani zao ni joho la ufalme, ambalo mama huyu alilitengeneza mwenyewe, na kwa mantiki yake, joho hilo litakuwa likivaliwa na mfamle wa enzi zake, sasa alitaka kuanzia kwa mwanae.

‘Utawala sasa umebadilika, utakatifu sasa umekwisha, na sasa ni zama mpya, zama za ujanja, ujanja kupata, ujanja sio kuwahi, au haki tu, bali ni kuwahi na kupata...’akasema mama mtu kimiya kimiya.

Mama huyu akiwa na tabasamu mdomono akijua kile alichotaka kimeshafanyika, akafika eneo la chumba cha makitaba, kabla ya kufungua mlango akawa anaendelea kuwaza, akisema kimoyo moyo;

 `Hii ndio siku pekee niliyokuwa nikiisubiria kwa hamu, na yale niliyoyapanga sasa yametimia...’akasema na kushika kitasa cha malngo, hakutaka kubisha hodi, kwani utaratibu haupo tena, utumwa, kama alivyouita yeye haupo tena, kila mtu afanye apendavyo...

‘Hahahahaha, hii ni siku pekee kwangu, siku ambayo moyo wangu umeswajika na kurizika pia, kwani kile kisasi nilichokuwa nacho siku nyingi cha kuuwawa kwa wazazi wangu kimetimilizwa, japokuwa sio kwa yule mhusika mwenyewe,....’akasema kimoyo moyo

‘Familia hii iliwaua wazazi wangu kinyama, kisa hadi leo sikujui, halafu wanajifanya watakatifu, ....sasa tuone huo utakatifu wao umewapeleka wapi. Wazazi wangu walifanya nini hadi kufikia kupata adhabu yote hiyo, hapana, hata hili lilifanyika haliwezi kufikia hicho walichowafanyia wazazi wangu, ....’alipowaza hivyo, macho yake yakagubikwa na machozi na ile taswira ya kuuwawa kwa wazazi wake ikamjia akilini......

*******
Kipindi hicho akiwa binti mdogo, akiwa kwenye chumba alichofungiwa na hao watu, na wazazi wake walikuwa wamekamatwa, kuna watu waliingia kwenye nyumba yao, na kuwashika wazazi wake, yeye akaambiwa akajifunguie chumbani kwake, na kwa uwoga akafanya hivyo, huko barazani akasikia sauti ya kufoka, japokuwa hakuweza kusikia kilichokuwa kikifanyika

Akatafuta sehemu yenye upenyo, uwaza wa kuweza kuangalia huko barazani, na alikipata, akawa sasa anawaangalia wazazi kupitia kwenye kipenyo hicho, kulikuwa na askari, wamesimama mbele ya wazazi wake, wakawa wanaongea na wazazi, na wazazi wake, walikuwa wamepigishwa magoti..

Hawa walikuwa maaskari wa kata, ambao wakimshika mtu wanamsulubu kweli, na mara nyingi kukitokea wizi hasa wa ng’ombe, wahusika hukamatwa na kuteswa saana, mapaka wanataja wapi ng’ombe walioibiwa walipo, lakini yeye hakujua lolote, kama kweli wazazi wake waliiba ng’ombe...akaendelea kuchungulia kuona ni nini kitafanyika.

Wale watu ambao ni maaskari wa kata, walikuwa wakisema kwa hasira, kuwauliza wazazi wake, na hicho walichoulizwa wazazi wake, ilionekana hakikuwa kinakubalika kwa wazazi wake, kwani wazazi kwa pamoja walikuwa wakitikisa kichwa kukataa, japokuwa alimuona mama yake akionyesha kusita, mama huyo alifanya tendo kila anapomuona mume wake akifanya

Hli ili iliendelea kwa muda, wazazi wanaulizwa jambo, na wazazi wanakataa, sasa hali ikabadilika, alipofika mtu...kiongozi wa kata, huyu anaogopewa kali, kwani hataki mchezo, na alipoingia pale wazazi walionyesha wasiwasi mkubwa

Huyu mtu alipoingia akaonekana kufoka, na kuwasogelea wazazi wake, na akawa akiwashika shika kwa ukali, ilionekana kuwa kuna kitu wazazi wanakificha, na hapo kipigo kikaanza wazazi wake wakawa wanapigwa, na vipigo viliendelea na mwisho ikawa kukatwa viungo....wazazi wakawa wanapiga ukelele wa uchungu

Mama huyu akiwa binti mdogo hauweza kuvumilia, akajikuta akidondoka chini na kupoteza fahamu, na alipoamuka akajiukuta yupo kwenye nyumba ya mkuu wa kata yule yule aliyemuona akiwatesa wazazi wake, na alipouliza wazazi wake wapo wapi, akaambiwa wanatumikia kifungo cha wizi wa mali ya huyo mkuu..

‘Wewe sasa utelelewa hapa, usiwe na wasiwasi utapewa kila kitu, na kweli alilelewa hapo, na hakuwahi kuwaona wazazi wake, tena, na kila alipoulizwa jibu ni kuwa wazazi wake wanatumikia kifungo

Akiwa kwenye miliki hiyo ndio akaja kukutana na mtoto wa huyo kiongozi wa eneo hilo la kata, mtoto huyo akaonyesha kumpenda, lakini yeye alishaanza kujenga upendo na mtu mwingine, binamu wa familia yao, binamu huyo walielewana sana, wakiwa toka watoto, kwani kuna muda alikuwa akienda kushinda kwao, na kucheza michezo ya kitoto.

Hata alipokuwa akiwa kwenye hiyo miliki akawa anapata mwanya wa kukutana na binamu yake huyo, na wakajikuta wamefikia hatua ya kupendana, binamu kwako kimila iliruhisiwa kuoana, na binamu huyo siku moja akamwambia;

‘Kwa vile wazazi wako hawapo, na hujui wapi walipo, mimi naona nikuoe, tuishi pamoja, kuliko kukaa kwenye miliki ya hao watu waliowatesa wazazi wako...mimi mwenyewe nina kisasi nao,..walishamtesa baba yangu hadi wakamvunja mguu, kisa eti alipoteza ngombe wa huyo bwana mkubwa....’akasema

‘Hata mimi sitaki kukaa hapo, na wananichunga kweli, siwapendi mimi kama nini, naona nitoroke, lakini nitakwenda wapi, najua watanitafuta hadi wanione...na wakiniona wanaweza kuniua.....’akasema huyo binti.

‘Usijali, huwezi kulazimishwa kuolewa kwa mtu usiyemtaka, mimi ndiye nastahili kukuoa maana tunapendana...’akasema huyo binamu mtu, na kweli mahusiani ya siri kwa siri yakaendelea.

‘Kwenye hiyo himaya ya kiutawala, kulikuwa na kijana, kijana huyo ndiye aliyekuja kumuoa mama huyu, kijana huyu akatokea kumpenda huyu binti, na akajaribu kila iwezavyo kumweka karibu huyu binti, lakini huyu binti kwa chuki za hiyo familia hakutaka kabisa urafiki na huyo kijana

‘Siwezi kuishi na watu waliwatesa wazazi wangu, na sijui wazazi wangu wapo wapi mpaka sasa...’akawa akijisemea.

Hata hivyo siku zilivyozidi kwenda, akajikuta yupo karibu na huyo kijana, kwani alionekana mkarimu kwake, mpole, na aliweza kumpa kila alichokitaka, na wakati huo huo akawa anakutana na binamu mtu wakipanga njia za kutoroka...lakini haikuwezekana kwani baadaye, baba wa hiyo familia alifariki, na yeye akawa mfariji wa huyo kijana ambaye alisikia kuwa ndiye atakayerithi utawala wa eneo hili.

‘Huyu ni mtu mnzuri sana akishika uongozi eneo hili litabadilika, kutakuwa hakuna serikali ya mabavu tena, huyu ni mtu wa watu,...’akasikia watu wakisema

‘Mhh, na mimi nikiolewa naye, nitafurahia, japokuwa sikutka kuolewa nah ii familia iliyowatesa wazazi wangu...’akajikuta akijisema, na hata alipokutana na binamu wake, wakawa wakiliongelea hilo

‘Kwahiyo unataka kuolewa na huyo kijana wa hiyo familia?’ akamuuliza

‘Wamenilazimisha hivyo, na mimi nimeshindwa kuwakatalia, lakini moyo wangu upo kwako, hata hivyo tuendelee kuwa hivi kwa siri ipo siku itafika tutalipiza kisasi na mimi nitaondoka na wewe...’akasema

‘Oh, siku itafika, ukionogewa na utajiri wa hiyo familia hutanikumbuka tena, ni bora nijue moja kuwa wewe sio wangu tena, ....nitahama hiki kijiji maana sitaweza kuishi nikikuona ukiwa na mwanaume mwingine...’akasema huyo kijana

Ni kweli baadaye yule kijana akaondoka, na huku nyuma huyu binti akaolewa na mtoto wa hiyo familia ya uongozi, japokuwa alisikia kuwa familia haikulipokea hilo, haikutaka huyo kijana amuoe yeye, kwavile anatokea kwenye familia iliyogubikwa na tabia mbaya..

‘Familia hiyo sio nzuri, ni wezi, wanahulka za kichawi, wana tabia mbaya, huyo hafai kuwa mke wa kiongozi wa familia na kiongozi wa eneo letu...’akasikia wanafamilia wakipinga, lakini kijana huyo alishampenda, na hakuweza kusikia la mtu.

‘Mimi ni lazima nimuoe huyu binti, nimempenda, na amelelewa hapa kwenye hii familia kwa muda mrefu, kwahiyo anajua tabia za hapa, hawezi kuwa kama ilivyokuwa familia yao...ni lazima tuchanganye damu tulete mageuzi...’akasema huyo kijana,,

Babu wa huyo kijana alikuwa akikaa mbali, baadaye wakati wa kumuapisha huyo kijana babu huyo akaja, na alisikia kuwa babu huyo alikuja kumkabidhisha huyo kijana ufalme wa kimila na kutawaza rasmi kama mtawala wa eneo, na familia zao.na baadaye akafuata ndoa..

‘Kijana huyu binti namuona ni mnzuri, wa sura lakini nahisi hana hulka njema, nahisi kwenye njozi zangu, una uhakika kuwa utaweza kumdhibiti..?’ akaulizwa na babu yake

‘Babu hata baba alinikanya sana, lakini kumbukeni huyu binti kalelewa hapa hapa, anafahamika, hajawahi kufanya lolote baya, mimi sioni ubaya wake, nitamuoa tu babu, na nitahakikisha anakuwa sawa na familia yetu, na isitoshe mimi ndiye nitakayeishi naye....’akasema huyo kijana.

Ni kweli baadaye ndoa ikafungwa na huyo binti na huyo kijana wakaanza maisha ya kiutawala, na kila siku wakawa wakipelekwa huku na kule kuonyeshwa utawala, kufundishwa mambo mengi, ya ajabu...siku zikaenda, lakini kwa siri mama huyu akawa anatafuta mbinu za kuonana na binamu yake mchumba wa moyo wake.....

                                                       *********
Mama yule akiwa na lile joho jekundu mkononi, aliingia ndani ya makitaba na kumkuta mwanae amelowana damu, kapiga magoti, analia, huku ameshikwa na butwaa, hajui ni nini kilichotokea, anatetemeka analia kwa uchungu, hakuwa na uhakika kamili, na kile kisu kilikuwa pale kifuani kwa baba yake, kimeshatolewa mwilini, kimejaa damu...

Mama alipoingia tu mtoto yule akasimama na kuanza kuogopa, akijua sasa mama yake hatakuwa radhi naye, japokuwa mama yake alikuwa akionyesha chuki za wazi dhidi ya hiyo familia, na alishawahi kumuambia yeye aliolewa tu hapo kwa shinikizo..lakini kilichotokea hapo japokuwa hakifahamu vyema, hakisameheki, lakini mama mtu akamsogelea na cha ajabu mama huyo alimpiga piga mwanae mgongoni na kumwambia;

‘Usihofu mtoto wangu, haya yalipangwa yawe hivyo, hivi ndivyo ilitakiwe iwe, na sasa imekuwa hivyo, na sasa naweza kusema kisasi kimekamilika...’akasema mama huku akimfuta futa mtoto wake zile damu mkononi na mtoto akaanza kutulia, hakuwa mtoto, japokuwa mtoto kwa mzazi hakui, alikuwa ni kijana tu...

Yule mama akakichukua kile kisu na kukisafisha zile damu, lakini cha ajabu zile damu, au hazikuweza kusafishika kabisa, kile kisu kikabakia na rangi nyekund, hata hivyo yule mama hakujali, yeye akachukua kisu kingine akamshikisha yule baba mkononi na kukizamisha pale pale kwenye jereha hadi kisu kikazama, huku mkono wa yule mzee ukiwa umeshikishwa kwa nguvu....

‘Sasa toka hapa nenda kaoge, sahau kila kitu kilichotokea hapa, kwani wewe hujui na huhusiki, yaliyotokea hapa huyajui, kuna watu wamefannya hivyo na wewe ukajajikuta umemuona baba yako hivi...inawezekana ni mashetani yamefanya hivyo kulipiza kisasi, huwezi jua...’akasema huyo mama

‘Lakini huoni mama mimi ndiye nilikuwa na baba humu ndani hakukuwa na mtu mwingine, nakumbuka baba ndiye aliyenipa hicho kisu mkononi, sikumbuki kilichofuata baadaye...inawezekana ni mimi...mama...’akasema akilia kwa uchungu

‘Hapo usipopakumbuka, ndipo muhimu, ina maana kuna mashetani yalifika yakakupagawisha yao yakafanya haya mauaji, na wewe ukawa hujijui, ulipizindukana ndio ukayakuta haya, wewe hujui kitu , na ni vyema ukawa kimiya usije kumuambia yoyote haya yaliyotokea hapa, ole wako ukija kusema yaliyotokea hapa, ukisema unafungwa, na utanyongwa....’akasema yule mama.

Mtoto wake akaondoka akiwa na masikitiko moyoni...mama mtu akafanya mambo yake humo ndani kuhakikisha kila kitu kipo sawa, na baadaye akaanza kupiga ukelele kuomba msaada, na aliyefika kwa haraka alikuwa ni dakitari, na watu wengine walifika baadaye, mambo yakawekwa sawa, polisi wakaitwa, wakaongea na huyo dakitari, polisi wakakubali maelezo yaliyotolewa yakisaidiwa na huyo dakitari...  

Na kilichotokea baadaye ni habari za kujiua kwa bwana mapesa kwa kile kilichoitwa kutokuelewana na matajiri wenzake katika biashara na katika utawala. Na kwa vile pesa inaongea kesi haikuchukua muda , mambo yakarejea mikononi mwa mwana wa kufikia, mtoto wa nje,  akijulikana kwa jina la Diamu. Diamu, akachukua hatamu za utawala japokuwa haikupolewa vyema, hata hivyo ni nani angelipinga, wakati wote wanafahamu kuwa mtoto huyo ni wa huyo marehemu...

Ndivyo ilivyotokea miaka hiyo ya nyuma, kipindi Diamu akiwa kijana, kipindi alivyoweza kutwaa miliki ya familia hiyo ambayo ilikuwa ni tajiri sana eneo hilo, na baadaye mama akamjenga huyo mtoto kinamna anavyotaka yeye, mtoto akawa nyoka, mwenye sumu kali, na kutokana na utajiri asiojua umepatikana vipi, akaanza kuja na wazo kubwa, wazo lililokuja kuitetemesha dunia....

NB: Ni wazo gani hilo

WAZO LA LEO: Kiburi , tamaa ikishaingia moyoni, ubinadamu hutoweka, na kiburi huteka nafasi zetu, maana tunayo pesa na mali, tunao utajiri,tunacho cheo, wewe una nini.... Binadamu anakuja kutakabari, akawa anajiamini kupita kiasi, akaiona dunia yote ipo mikononi mwake, na mungu akasahaulika kabisa.


Tukumbuke,kamwe kiburi si uungwana, na kiburi ni hulka ya shetani, ambaye alikana amri ya mungu. Tusiwe hivyo, tukajisahau maana yote ni mapito, mali, watoto, ufalme, cheo, vyote ni mapito tu, mwisho wa yote tutarejea kwa muumba.

Rudia kusoma: utanguliziNi mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

What a shame it is for humanity to have declined to such levels where good
hearted individuals are forced to secretly observe and infiltrate
government sponsored organizations just to acquire a truth that we should have had from the
very beginning. " Licata says, making like a swatter with the automatic through the gauze of barely-see-ums. You can check out a set of screens featuring the first-person shooter in the slideshow to the left of this article and the details below:.

Look at my page; final kick hack