Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, June 23, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-81Shahidi , mpelelezi akawa anaendelea na kutoa maelezo yake...

‘Sasa hebu tuambie kuhusu huyu mtu wa kwanza, huyo mtu uliyemuona akiongea na mlinzi hapo getini kwake, na baadaye huyo mlinzi akaacha ulinzi wake ikionekana kuwa kamuachia ulinzi huyo mtu mwingine, kutokana na maelezo yako....’akasema wakili muendesha mashitaka na shahidi akataka kusema neno lakini wakili huyo akaendelea kusema;

‘Huyo mtu anaonekana anafahamiana na huyo mlinzi, maana hukusema kuwa waliongea kwa muda ili kutambushina, sasa ni vyema tukamfahamu huyo mtu kwa sifa zake, angalau, kabla hujatuambia jinsi gani kifo cha mtoza ushuru kinavyohusiana na hili kundi....’akasema wakili muendesha mashitaka, na kabla shahidi hajaendelea hapo, wakili huyo bado akaendelea kutoa maelezo kwa kusema;

‘Kwanza ulishamuelezea, jinsi huyu mtu alivyofika hapo,sasa hebu elezea huyo mtu alivyokuwa akiongea na huyo mlinzi, halafu uje kutuambia huyo mtu ni nani na,alionekana vipi, na je una picha yake, uliwahi kumpiga picha, kwani umesema ulikuwa na simu yako yenye kuchukua matukio?’ akaulizwa

‘Hapana kwa muda huo sikuweza kuchukua hayo matukio, kwahiyo sina picha yake, kwa muda ule nisingeliweza kufanya hivyo,ukizingatia kuwa nilikuwa kwa nje, na kuna watu walikuwa wanapita, na huwezi kujua, labda kulikuwa na watu wao,...wangeliweza kuniona, ...’akasema

‘Kwahiyo huna picha ya sura yake, inayoonyesha jinsi alivyokuwa akionekana,na pia hukuweza kumtambua kwa sura?’ akaulizwa.

‘Sina picha yake, na kweli sikuweza kumtambua kwa sura, kwa jinsi alivyokuwa amevalia,na hata nilipojaribu kumkisia kuwa ni nani, sikuweza kumuhisi kwa jinsi alivyokuwa,inaonekana ni mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kujificha, kimwili na kimatendo...’akasema

‘Oooh, je alionekana vipi?’ akaulizwa

‘Alikuwa kavalia koti refu, yale ya mvua, au baridi, toka juu mpaka chini, na kofia pana la kuificha kichwa, na mawani mapana...na japokuwa alikuwa akiongea na mlinzi lakini aliongea naye huku kainama, kiasi kwamba huwezi kabisa kupata sehemu ya uso wake...’akasema

‘Na mwendo wake ni wa haraka, hakuonyeshi kuchoka, ni mwili uliozoea taabu, au ukakamavu, alionekana kweli yupo kazini, na alipokuwa akiongea na mlinzi alionekana kutulia bila wasiwasi, kama vile anajua anachokifanya, na ilionyesha wazi mlinzi anamfahamu huyo mtu,....’akasema

‘Je mlinzi alionekana vipi mbele ya huyo mtu, utii, wasiwasi au....?’ akauliza

‘Ni kama askari mdogo akiwa kwa mkuu wake katika jeshi, naweza kuelezea hivyo...’akasema.

‘Hebu kwanza kabla hujatuelezea kuhusu huyo mtu, mlinzi ni nani, maana mahakama inaweza kumchukulia juu juu huyu mlinzi,na kuonekana ni mlinzi wa kawaida tu wa mitaani...’akasema na hapo kukatokea pingamizi, lakini hakimu akalikataa na kusema shahidi aendelee.

‘Huyu mlinzi alikuwa mmoja wa maaskari polisi, aliacha kazi hiyo kutokana na kuumwa ,a akiwa kazini, alipatwa na maradhi ya ajabu, akatibiwa lakini haikuwezakana ikabidi apelekwe kwao,..na huko alikaa muda mrefu akitibiwa kiasili zaidi, na baadaye mwenyewe akaandika barua ya kuacha kazi....’akasema

‘Katika kazi yake kabla hajashikwa na hayo maradhi alikuwaje?’ akaulizwa

‘Alikuwa askari mnzuri sana , jasiri, mchapakazi,asiyekata tamaa,  na mtiifu, na alipokuwa mafunzoni, alikuwa ni wa kwanza kumaliza kazi waliyopewa, na hakuwa mtu wa kulalamika...’akasema

‘Na sifa nyingine kama walivyoandika ni kuwa alipenda sana kula,...japokuwa alikuwa na mwili mdogo, lakini kula yake ilikuwa sio ya kawaida...’akasema na watu wakacheka.

‘Hatumsemi marehemu vibaya, ila tunataka tumfahamu huyu mtu vyema, ili haki yake itendeke, hata kama hayupo hapa kujitetea, lakini kile ambacho ni kweli alikuwa nacho, kinachoweza kumlindia haki yake ni lazima kisemwe, tusimsingizie vibaya...’akasema wakili na kumuashiria shahidi aendelee

‘Alikuwa mwepesi sana, na kama ni kazi ya kupanda mti, au mnazi, yeye alipewa hiyo kazi, alikuwa mwepezi kupanda sehemu zisizopandika kirahisi,kama asingelipatwa na hayo maradhi, angelikuwa mbali sana,...ni wale askari wanajua kutii amri, akiambiwa jambo  mara moja analitekeleza....na pia alikuwa na kipaji cha ufundi...’akasema

‘Ufundi wa vipi?’ akaulizwa

‘Ufundi wa magari, useremala, uwashi, yaani yeye, walivyomuelezea ni kuwa alikuwa fundi anayeweza kutengeneza kitu chochote, hata silaha ikileta matatizo yeye aliweza kugundua tatizo lipo wapi...’akasema

‘Ndio maana aliweza kuingia ndani na kubomoa kabati....’akasema wakili

‘Kwake hiyo ilikuwa kazi ndogo tu...’akasema shahidi

‘Unasema kuwa alikuwa jasiri na mvumilivu, kwahiyo ni askari asiyekata tamaa, kwa maelezo yake kama yalivyoandikwa...na wakati anaumwa hayo magonjwa mabaya, walisema ni magonjwa ya namna gani, na kwanini aliamua kutokurejea kazini mwenyewe, haikutolewa sababu?’ akaulizwa

‘Walitaja kuwa ni maradhi ya maumivu ya kichwa, kichwa kilikuwa kikimuuma sana, na ilifikia hatua anapiga ukelele wa maumivu, yalikuwa maumivu makali sana,...kuna muda watani zake walimshauri ajiue ili asiteseke, lakini yeye aliwaambia hawezi kijiua,...waliandika kuwa alisema;

‘‘Haya ni majaribu tu, nitapona, kama ni kufa wataniua wengine, lakini mimi siwezi kujiua mwenyewe hata siku moja...’

‘Na hayo maelezo uliyapatia wapi?’ akauliza

‘Niliyapata kwenye kumbukumbu zake za kiofisini, .....’akasema

‘Kwa bahati mbaya huyu mtu wamemuua, walijua kuwa ni shahdii muhimu katika hii kesi,hata hivyo, kuuwawa kwake pia kuliweza kufichua mengi, hadi kuweza kuwakamata wahusika wa kundi hilo kwa wingi, nab ado tutazidi kuwakamata wengine, ili wafikishwe mbele ya sheria,...’akasema muendesha mashitaka.

‘Shahidi,hebu tuambie kuhusu mauji yake, je ni kweli alijiua mwenyewe...najua watetezi watataka kuweka pingamizi, hapa, lakini mjue japokuwa maerehemu hayupo,lakini ukweli, na haki yake ni lazima ilindwe, hatutakaa kimiya, kumtetea, shahidi jibu swali je ni kweli kwa upelelezi wako, alijiua mwenyewe?’ akaulizwa

‘Kwanza kutokana na ushahidi wa kauli yake hilo halingeliwezekana, nahisi waliomu-ua, hawakufuatailia vyema kumbukumbu za maisha yake...wangelijua hilo wasingelimsingizia kuwa kajiua mwenyewe....’akasema shahidi
‘Sasa ilikuwaje, kwani hata taarifa ya kimatibabu docta kaandika hivyo...’akasema

‘Ni kweli docta aliandika hivyo kutokana na maelezo ya polisi, lakini sizani kwamba ni vyema yeye kulithibitisha hilo kuwa kajiua, yeye kama docta alitakiwa kusema huyo mgonjwa kafa kwa sumu,hiyo tu ingelitosha, tunaona ajabu docta mtaalamu mwenye uzoefu kuandika kauli ya kuthibistisha kuwa kweli mgonja alijiua mwenyewe ...’akasema shahidi kwa kusikitika.

‘Kwanini unasema hivyo shahidi, ....?’ akaulizwa

‘Yeye kama dakitari, hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa mgonjwa kajiua,yeye angaliandika kuwa mgonjwa kafa kwa sumu, kazi ya kujua kuwa kafa kwa kujiua au kwa kuuliwa hiyo ni kauli ya polisi, je huyo docta ana ushahidi gani kuwa sumu hiyo kainywa huyo mgonjwa kwa nia ya kujiua...na uchunguzi gani ulishafanyika kulithibitisha hilo..kweli za mwizi ni arubaini..’akasema shahidi

‘Kwa maelezi yako hapo inaonyesha kuwa kuna jambo limejificha, na je hukuweza kulifichua maana wewe ni mtaalamu na mpelelezi....?’ akaulizwa

‘Mimi kama mpelelezi, niligundua kuwa ....’akageuka kuangalia upande ule wa washitakiwa, na wakili mtetezi akawa anaweka pingamizi lakini hakimu alikuwa kama hamuoni, akawa anamsikiliza tu huyo shahidi na hakimu akakubali hilo pingamizi, hata hivyo wakili muendesha mashitaka akasema;

‘Najua huwezi kulisemea hilo, kwani huyo sio mtu tunayemzungumiza hapa lakini ni vyema ukaliweka wazi mbele ya mahakama, ili haki ya marehemu ijulikane, huyu mtu alikamatwa kama mshukiwa muhimu katika hii kesi,lakinia na alikuwa na haki yake, ikiwemo usalama wa maisha yake, na sehemu kubwa ya usalama wa ndani ilikuwa ni kazi ya watu wa usalama, hata hivyo, inavyoonekana ni kuwa mbinu zilifanyika hadi mtuhumiwa huyo akauwawa,...’akasema wakili

‘Wakili wake yupo wapi?’ akauliza hakimu akionyesha hasira na kukerwa.

‘Wakili wake ni mmoja wa washitakiwa muheshimiwa hakimu, tutakuja kutoa maelezo yake, ...’akasema wakili, na hakimi akageuka upande wa washitakiwa na kumuona yule wakili akiwa kainamisha kichwa chini.

Wakili muendesha mashitaka, alipoona hakimu katulia akimsubiria yeye kuendelea akasema;

‘Sasa hebu turudi kwa yule mtu aliyekuja kule getini, kule kwa mdada, akafika na kuongea kidogo na mlinzi, na mlinzi akaondoka pale getini na kuelekea ndani,...huyu mtu ni nani , maana mahakama inataka kumfahamu katika uchunguzi wako hukuweza kumgundua huyo mtu, kuwa ni nani?’ akaulizwa na pingamizi likatoka upande wa watetezi, na hakimu akawa kimiya kwa muda,

Kabla hakimu hajatoa kauli yake mara kukasikia vurumai upande ule wa mlangoni,na hakimu akageuka kutizama upande ule, na karibu watu wote waligeukia huko kuangalia ni nini kinachotokea, kwangu mimi niliyekuwa nimekaa kwenye benchi za hapo mahakamani, sikuweza kuona ni kitu gani kinachoendelea,kwani kwa nyuma yangu kulikuwa na watu, ambao kwa hamasa kwa muda huo walifikia kusimama kutizima upande huo

Kilichoonekana ni kuwa kuna mtu alikuwa kaingia, na amekuwa akisukuma watu ili apite mbele zaidi, lakini watu wakawa hawakubali, kwani kila mtu alitaka kuona kile kinachoendelea pale mbele wakati shahidi anatoa maelezo yake, hata hivyo, huyo mtu hakukubali, na ilionekana hayupo peke yake, kwani kulikuwa na msemaji wake...
Hakimu alipoona hivyo akasema;

‘Utulivu, kuna nini hapo maeneo ya mlangoni, ...walinzi hebu hakikisheni utulivu upo...’akasema hakimu hata hivyo, hali haikutulia, ilionekana bado kuna mtu anataka kupita mbele, na walinzi sasa wakawa wanawaondoa watu ili huyo mtu apate njia ya kupita.

‘Ni nani huyo anayevuruga utaratibu wa kimahakama kwani kuna umuhimu gani way eye kupita huku mbele, na kwanini, walinzi mnamruhusu huyo...’hakimu akakatiza maneno yake pale alipoona huyo mtu akiletwa sehemu ya mbele...

NB: Kwa leo naona niishie hapa, haya maeelzo kwenye kisa hiki ni muendelezo wa sehemu iliyopita, ila kwa jinsi ilivyo, kisa kimefikia ukingoni, na mwisho wa kisa hiki ndio mwanzo wa kisa kingine, kuna visa vingi vipo mbele yetu,lakini wadau na wapenzi wengi wa diary yangu, wameomba tuendelee na simulizi la bosi, ...sijui mnasemaje...Nikipata like nyingi, tutafanya hivyo,..

WAZO LA LEO: Tusipende kuzarau wenzetu, hata kama tunaona watu hao hawana umuhimu kwetu, hata kama sisi ni watu wa namna fulani na huyo mtu tunamuona ni mtu asiyefaa kufanya,au kuongea jambo lolote.


Katika vikao, katika kutenda jambo,kila mtu apewe haki yake, kwani huwezi kujua huyo mtu tunayemzarau anaweza kusema nini, na huenda anachotaka kukisema kikawa na manufaa kwetu, huenda mwenyezimungu akataka kauli yake ipitie kwa huyo mtu, na kauli yake ikaja kuwa suluhisho la matatizo yetu... 

Ni mimi: emu-three

No comments :