Shahidi
, mpelelezi akawa anaendelea na kutoa maelezo yake...
‘Sasa
hebu tuambie kuhusu huyu mtu wa kwanza, huyo mtu uliyemuona akiongea na mlinzi hapo
getini kwake, na baadaye huyo mlinzi akaacha ulinzi wake ikionekana kuwa
kamuachia ulinzi huyo mtu mwingine, kutokana na maelezo yako....’akasema wakili
muendesha mashitaka na shahidi akataka kusema neno lakini wakili huyo
akaendelea kusema;
‘Huyo
mtu anaonekana anafahamiana na huyo mlinzi, maana hukusema kuwa waliongea kwa
muda ili kutambushina, sasa ni vyema tukamfahamu huyo mtu kwa sifa zake,
angalau, kabla hujatuambia jinsi gani kifo cha mtoza ushuru kinavyohusiana na
hili kundi....’akasema wakili muendesha mashitaka, na kabla shahidi hajaendelea
hapo, wakili huyo bado akaendelea kutoa maelezo kwa kusema;
‘Kwanza
ulishamuelezea, jinsi huyu mtu alivyofika hapo,sasa hebu elezea huyo mtu alivyokuwa
akiongea na huyo mlinzi, halafu uje kutuambia huyo mtu ni nani na,alionekana
vipi, na je una picha yake, uliwahi kumpiga picha, kwani umesema ulikuwa na
simu yako yenye kuchukua matukio?’ akaulizwa
‘Hapana
kwa muda huo sikuweza kuchukua hayo matukio, kwahiyo sina picha yake, kwa muda
ule nisingeliweza kufanya hivyo,ukizingatia kuwa nilikuwa kwa nje, na kuna watu
walikuwa wanapita, na huwezi kujua, labda kulikuwa na watu wao,...wangeliweza
kuniona, ...’akasema
‘Kwahiyo
huna picha ya sura yake, inayoonyesha jinsi alivyokuwa akionekana,na pia
hukuweza kumtambua kwa sura?’ akaulizwa.
‘Sina
picha yake, na kweli sikuweza kumtambua kwa sura, kwa jinsi alivyokuwa
amevalia,na hata nilipojaribu kumkisia kuwa ni nani, sikuweza kumuhisi kwa
jinsi alivyokuwa,inaonekana ni mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kujificha,
kimwili na kimatendo...’akasema
‘Oooh,
je alionekana vipi?’ akaulizwa
‘Alikuwa
kavalia koti refu, yale ya mvua, au baridi, toka juu mpaka chini, na kofia pana
la kuificha kichwa, na mawani mapana...na japokuwa alikuwa akiongea na mlinzi
lakini aliongea naye huku kainama, kiasi kwamba huwezi kabisa kupata sehemu ya
uso wake...’akasema
‘Na
mwendo wake ni wa haraka, hakuonyeshi kuchoka, ni mwili uliozoea taabu, au
ukakamavu, alionekana kweli yupo kazini, na alipokuwa akiongea na mlinzi
alionekana kutulia bila wasiwasi, kama vile anajua anachokifanya, na ilionyesha
wazi mlinzi anamfahamu huyo mtu,....’akasema
‘Je
mlinzi alionekana vipi mbele ya huyo mtu, utii, wasiwasi au....?’ akauliza
‘Ni
kama askari mdogo akiwa kwa mkuu wake katika jeshi, naweza kuelezea hivyo...’akasema.
‘Hebu
kwanza kabla hujatuelezea kuhusu huyo mtu, mlinzi ni nani, maana mahakama
inaweza kumchukulia juu juu huyu mlinzi,na kuonekana ni mlinzi wa kawaida tu wa
mitaani...’akasema na hapo kukatokea pingamizi, lakini hakimu akalikataa na
kusema shahidi aendelee.
‘Huyu
mlinzi alikuwa mmoja wa maaskari polisi, aliacha kazi hiyo kutokana na kuumwa
,a akiwa kazini, alipatwa na maradhi ya ajabu, akatibiwa lakini haikuwezakana
ikabidi apelekwe kwao,..na huko alikaa muda mrefu akitibiwa kiasili zaidi, na baadaye
mwenyewe akaandika barua ya kuacha kazi....’akasema
‘Katika
kazi yake kabla hajashikwa na hayo maradhi alikuwaje?’ akaulizwa
‘Alikuwa
askari mnzuri sana , jasiri, mchapakazi,asiyekata tamaa, na mtiifu, na alipokuwa mafunzoni, alikuwa ni
wa kwanza kumaliza kazi waliyopewa, na hakuwa mtu wa kulalamika...’akasema
‘Na
sifa nyingine kama walivyoandika ni kuwa alipenda sana kula,...japokuwa alikuwa
na mwili mdogo, lakini kula yake ilikuwa sio ya kawaida...’akasema na watu
wakacheka.
‘Hatumsemi
marehemu vibaya, ila tunataka tumfahamu huyu mtu vyema, ili haki yake itendeke,
hata kama hayupo hapa kujitetea, lakini kile ambacho ni kweli alikuwa nacho, kinachoweza
kumlindia haki yake ni lazima kisemwe, tusimsingizie vibaya...’akasema wakili
na kumuashiria shahidi aendelee
‘Alikuwa
mwepesi sana, na kama ni kazi ya kupanda mti, au mnazi, yeye alipewa hiyo kazi,
alikuwa mwepezi kupanda sehemu zisizopandika kirahisi,kama asingelipatwa na
hayo maradhi, angelikuwa mbali sana,...ni wale askari wanajua kutii amri,
akiambiwa jambo mara moja
analitekeleza....na pia alikuwa na kipaji cha ufundi...’akasema
‘Ufundi
wa vipi?’ akaulizwa
‘Ufundi
wa magari, useremala, uwashi, yaani yeye, walivyomuelezea ni kuwa alikuwa fundi
anayeweza kutengeneza kitu chochote, hata silaha ikileta matatizo yeye aliweza
kugundua tatizo lipo wapi...’akasema
‘Ndio
maana aliweza kuingia ndani na kubomoa kabati....’akasema wakili
‘Kwake
hiyo ilikuwa kazi ndogo tu...’akasema shahidi
‘Unasema
kuwa alikuwa jasiri na mvumilivu, kwahiyo ni askari asiyekata tamaa, kwa
maelezo yake kama yalivyoandikwa...na wakati anaumwa hayo magonjwa mabaya,
walisema ni magonjwa ya namna gani, na kwanini aliamua kutokurejea kazini mwenyewe,
haikutolewa sababu?’ akaulizwa
‘Walitaja
kuwa ni maradhi ya maumivu ya kichwa, kichwa kilikuwa kikimuuma sana, na ilifikia
hatua anapiga ukelele wa maumivu, yalikuwa maumivu makali sana,...kuna muda
watani zake walimshauri ajiue ili asiteseke, lakini yeye aliwaambia hawezi
kijiua,...waliandika kuwa alisema;
‘‘Haya ni majaribu tu, nitapona, kama ni kufa
wataniua wengine, lakini mimi siwezi kujiua mwenyewe hata siku moja...’
‘Na
hayo maelezo uliyapatia wapi?’ akauliza
‘Niliyapata
kwenye kumbukumbu zake za kiofisini, .....’akasema
‘Kwa
bahati mbaya huyu mtu wamemuua, walijua kuwa ni shahdii muhimu katika hii kesi,hata
hivyo, kuuwawa kwake pia kuliweza kufichua mengi, hadi kuweza kuwakamata
wahusika wa kundi hilo kwa wingi, nab ado tutazidi kuwakamata wengine, ili
wafikishwe mbele ya sheria,...’akasema muendesha mashitaka.
‘Shahidi,hebu
tuambie kuhusu mauji yake, je ni kweli alijiua mwenyewe...najua watetezi
watataka kuweka pingamizi, hapa, lakini mjue japokuwa maerehemu hayupo,lakini
ukweli, na haki yake ni lazima ilindwe, hatutakaa kimiya, kumtetea, shahidi
jibu swali je ni kweli kwa upelelezi wako, alijiua mwenyewe?’ akaulizwa
‘Kwanza
kutokana na ushahidi wa kauli yake hilo halingeliwezekana, nahisi waliomu-ua,
hawakufuatailia vyema kumbukumbu za maisha yake...wangelijua hilo wasingelimsingizia
kuwa kajiua mwenyewe....’akasema shahidi
‘Sasa
ilikuwaje, kwani hata taarifa ya kimatibabu docta kaandika hivyo...’akasema
‘Ni
kweli docta aliandika hivyo kutokana na maelezo ya polisi, lakini sizani kwamba
ni vyema yeye kulithibitisha hilo kuwa kajiua, yeye kama docta alitakiwa kusema
huyo mgonjwa kafa kwa sumu,hiyo tu ingelitosha, tunaona ajabu docta mtaalamu
mwenye uzoefu kuandika kauli ya kuthibistisha kuwa kweli mgonja alijiua
mwenyewe ...’akasema shahidi kwa kusikitika.
‘Kwanini
unasema hivyo shahidi, ....?’ akaulizwa
‘Yeye
kama dakitari, hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa mgonjwa kajiua,yeye
angaliandika kuwa mgonjwa kafa kwa sumu, kazi ya kujua kuwa kafa kwa kujiua au
kwa kuuliwa hiyo ni kauli ya polisi, je huyo docta ana ushahidi gani kuwa sumu
hiyo kainywa huyo mgonjwa kwa nia ya kujiua...na uchunguzi gani ulishafanyika
kulithibitisha hilo..kweli za mwizi ni arubaini..’akasema shahidi
‘Kwa
maelezi yako hapo inaonyesha kuwa kuna jambo limejificha, na je hukuweza
kulifichua maana wewe ni mtaalamu na mpelelezi....?’ akaulizwa
‘Mimi
kama mpelelezi, niligundua kuwa ....’akageuka kuangalia upande ule wa
washitakiwa, na wakili mtetezi akawa anaweka pingamizi lakini hakimu alikuwa
kama hamuoni, akawa anamsikiliza tu huyo shahidi na hakimu akakubali hilo
pingamizi, hata hivyo wakili muendesha mashitaka akasema;
‘Najua
huwezi kulisemea hilo, kwani huyo sio mtu tunayemzungumiza hapa lakini ni vyema
ukaliweka wazi mbele ya mahakama, ili haki ya marehemu ijulikane, huyu mtu
alikamatwa kama mshukiwa muhimu katika hii kesi,lakinia na alikuwa na haki
yake, ikiwemo usalama wa maisha yake, na sehemu kubwa ya usalama wa ndani
ilikuwa ni kazi ya watu wa usalama, hata hivyo, inavyoonekana ni kuwa mbinu
zilifanyika hadi mtuhumiwa huyo akauwawa,...’akasema wakili
‘Wakili
wake yupo wapi?’ akauliza hakimu akionyesha hasira na kukerwa.
‘Wakili
wake ni mmoja wa washitakiwa muheshimiwa hakimu, tutakuja kutoa maelezo yake,
...’akasema wakili, na hakimi akageuka upande wa washitakiwa na kumuona yule
wakili akiwa kainamisha kichwa chini.
Wakili
muendesha mashitaka, alipoona hakimu katulia akimsubiria yeye kuendelea
akasema;
‘Sasa
hebu turudi kwa yule mtu aliyekuja kule getini, kule kwa mdada, akafika na
kuongea kidogo na mlinzi, na mlinzi akaondoka pale getini na kuelekea
ndani,...huyu mtu ni nani , maana mahakama inataka kumfahamu katika uchunguzi
wako hukuweza kumgundua huyo mtu, kuwa ni nani?’ akaulizwa na pingamizi
likatoka upande wa watetezi, na hakimu akawa kimiya kwa muda,
Kabla
hakimu hajatoa kauli yake mara kukasikia vurumai upande ule wa mlangoni,na
hakimu akageuka kutizama upande ule, na karibu watu wote waligeukia huko kuangalia
ni nini kinachotokea, kwangu mimi niliyekuwa nimekaa kwenye benchi za hapo
mahakamani, sikuweza kuona ni kitu gani kinachoendelea,kwani kwa nyuma yangu
kulikuwa na watu, ambao kwa hamasa kwa muda huo walifikia kusimama kutizima
upande huo
Kilichoonekana
ni kuwa kuna mtu alikuwa kaingia, na amekuwa akisukuma watu ili apite mbele
zaidi, lakini watu wakawa hawakubali, kwani kila mtu alitaka kuona kile kinachoendelea
pale mbele wakati shahidi anatoa maelezo yake, hata hivyo, huyo mtu hakukubali,
na ilionekana hayupo peke yake, kwani kulikuwa na msemaji wake...
Hakimu
alipoona hivyo akasema;
‘Utulivu,
kuna nini hapo maeneo ya mlangoni, ...walinzi hebu hakikisheni utulivu
upo...’akasema hakimu hata hivyo, hali haikutulia, ilionekana bado kuna mtu
anataka kupita mbele, na walinzi sasa wakawa wanawaondoa watu ili huyo mtu
apate njia ya kupita.
‘Ni
nani huyo anayevuruga utaratibu wa kimahakama kwani kuna umuhimu gani way eye kupita
huku mbele, na kwanini, walinzi mnamruhusu huyo...’hakimu akakatiza maneno yake
pale alipoona huyo mtu akiletwa sehemu ya mbele...
NB:
Kwa leo naona niishie hapa, haya maeelzo kwenye kisa hiki ni muendelezo wa
sehemu iliyopita, ila kwa jinsi ilivyo, kisa kimefikia ukingoni, na mwisho wa
kisa hiki ndio mwanzo wa kisa kingine, kuna visa vingi vipo mbele yetu,lakini
wadau na wapenzi wengi wa diary yangu, wameomba tuendelee na simulizi la bosi,
...sijui mnasemaje...Nikipata like nyingi, tutafanya hivyo,..
WAZO
LA LEO: Tusipende kuzarau
wenzetu, hata kama tunaona watu hao hawana umuhimu kwetu, hata kama sisi ni
watu wa namna fulani na huyo mtu tunamuona ni mtu asiyefaa kufanya,au kuongea
jambo lolote.
Katika
vikao, katika kutenda jambo,kila mtu apewe haki yake, kwani huwezi kujua huyo
mtu tunayemzarau anaweza kusema nini, na huenda anachotaka kukisema kikawa na
manufaa kwetu, huenda mwenyezimungu akataka kauli yake ipitie kwa huyo mtu, na
kauli yake ikaja kuwa suluhisho la matatizo yetu...
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment