Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 23, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-43


Mpelelezi alikuja pale nilipokuwa kama alivyoniagiza, alinitumia ujumbe kwa anataka kuonana na mimi kwa siri, lakini tuonane naye nje ya hiyo hoteli, ...

‘Tuonane kwa siri nje ya hiyo hotel, peke yako,ni muhimu sana ....’ujumbe ukasema, na nilikumbuka namba yake hii malumu aliyonipa, kuwa akitaka kuwasiliana na mimi, atatumia hii namba

‘Tukutane wapi?’ nikauliza kwa njia ya ujumbe

‘Nje ya hiyo hoteli, kuna mgahawa wa akina mama wa Kipemba,fanya kwa siri .....’akaandika, na eneo hilo nalifahamu sana, kwahiyo sikumjibu . Nikawa najiuliza kwanini nifanye kwa siri, ina maana huyu mtu hataki mdada au mtu mwingine afahamu kuwa tunakutakana...

Basi siku hiyo sikuwa na miadi mingi ya kukutana na watu, na wakili na mdada walisema wanafuatilia vielelezo kwa ajili ya kesi yetu, kwahiyo muda mwingi nilikuwa peke yangu,nilishaambiwa niwe nafika kwenye hiyo ofisi, ambayo waliniambia inatumika kwa ajili ya vikao maalumu, na aliyekuwa akiitumia ni marahemu.

Nilifika hapo hapo ofisini, nikawa natumia komputa iliyokuwepo, haikuwa na mambo emngi zaidi ya maelezo ya viao, ajenda na mambo mengine ambayo hayakuwa na maana kwangu, nilipochoka kukaa hapo ofisini, nikatoka, na kurudi chumbani kwangu. Nilijaribu kumpigia simu mchumba wangu lakini hakutaka kabisa kupokea simu yangu, nikamtumia ujumbe, lakini hakutaka hata kuujibu.

Niliiona siku hiyo ni ndefu sana, lakini baadaye ukafika muda ambao nilifahamu sitahitajika, nikabadili nguo na kuvaa nguo ambazo sio rahisi mtu kunifahamu kwa haraka, nikatoka hapo hotelini, kwa kupitia njia za nje ambazo nilikuwa nazifahamu mwenyewe nikatoka nje kabisa ya hiyo hoteli bila kujulikana.

Nilitembea kuelekea upande wa pili wa barabara, hadi nikafika sehemu barabara zinapokutana, hapo nikasimama kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayenifuata, na nilipoona hakuna dalili kama hiyo, nikaanza kutembea kutumia barabara kuu, nikirudi kuelekea kwenye hiyo hoteli, lakini kwa bara bara nyingine,hadi nikafika njia ya mkato, na hapo nikaelekea kwenye huo mgahawa ambao haukuwa mbali na hiyo hoteli.

Nilipofika hapo sikumuona huyo mpelelezi, nikaagiza maziwa, na keki nikawa nakunywa taratibu na nilipomaliza, nikahisi  mtu kasimama nyuma yangu, na huyo mtu akanigusa mgongoni, nilipogeuka nikakutana na uso jamaa akiwa kavaa mawani mapana na kofia pana, sio rahisi kugundua ni nani, lakini kwa haraka nikatambua kuwa ni huyo mpelelezi.

‘Nimekuja muda mrefu tu, nimekuona ukiingia hapa mgahawani, lakini nilikuwa nahakikisha kama kweli hakuna mtu yupo nyuma yako...’akasema

‘Ina maana umenioan nikiingia, ukatoka kuchunguza kuwa hakuna aliyenifuatilia, ina maana huniamini...?’nikasema

‘Sio swala la kuaminiana hapa, ukiwa kwenye kazi yetu kila jambo lina tahadhari yake, usikisie tu, unatakiwa uwe makini, na kufuatilia kwa karibu zaidi, ...Yupo mtu aliyekuwa akikufuatilia ulipotoka tu kwenye hoteli, inavyoonekana, alikutilia mashaka, akaona ahakikishe kama kweli ni wewe,, ...’akasema

‘Haiwezekani, maana njia niliyotumia hakuna mtu angeweza kunishuku, ...ni nani huyo?’ nikauliza.

‘Sikuweza kumtambua vyema, lakini jamaa huyo alikufuatilia hadi barabara kuu, na mimi nikaona nimuingilie kati, nilichofanya nikumkatishia mbele yake na kuanza kumuuliza njia ya kwenda sehemu nyingine , ....’akasema

‘Mhh, ukaongea naye?’ nikamuuliza

‘Hakutaka hata kuongea name, lakini kwa vile nilikuwa mbele yake, ikabidi aongee tu, na kuniambia hakufahamu na ana haraka....lakini kwa nafasi hiyo , nikajua umeshakata kona na kuingie sehemu nyingine...ile nimemuona yupo hapo nje bado anahangaika kukutafuta...’akasema

‘Unamfahamu?’ nikamuuliza tena

‘Nahisi ni hao  vijana wa mdada, ...’akasema

‘Kwahiyo basi ina maana mdada atakuwa amefahamu kuwa nimetoka hotelini?’ nikauliza

‘Atakuwa ameshafahamu kama ataambiwa na huyu mtu, halafu akaamua kuja hotelini kwako moja kwa moja, ...hata hivyo hilo sio muhimu sana,cha muhimu ni kuwa hafahamu unakwenda kuonana na nani?’ akazema

‘Haya niambie umeniitia nini maana naona ni vyema nikarudi hotelini haraka?’ nikamuuliza

‘Siku ile ya tukio, wewe ulijibadili,....katika uchunguzi wangu nimekuja kuchanganua na kugundua kuwa wewe ulivaa ndevu za bandia, je ni kwanini ulifanya hivyo?’ akaniuliza na kunifanya nishituke

‘Sio kweli, kwanini umefikia kuamini hivyo, wakati hata polisi hawajalizungumzia hilo, au ni nani kakuambia hivyo, sijafanya hivyo kabisa...’nikasema nikionyesha wasiwasi

‘Maumbile yako yanakushitaki, nimeongea na mlinzi mara nyingi, na jinsi anavyomuelezea huyo mtu, hakuan shaka ni wewe,niambie ukweli, kwanini ulifanya hivyo, nakuuliza hivyo nikiwa na maana kubwa sana....nimejaribu kuhakiki, kama kuna mtu mwingine aliingia nimeona uwezekano huo haupo, na hili linanifanya niwe na uhakika kuwa wewe ulijibadili sura...niambie ukweli ni kwasababu gani ulifanya hivyo?’ akaniuliza akiniangalia moja kwa moja usoni

‘Hizo ni hisia zako mimi sikujibadili sura....na ingelikuwa hivyo polisi wangeshagundua hilo..na kwanini nifanye hivyo....’nikasema nikiangalia pembeni.

‘Polisi hawawezi kuligundua hilo kwa sasa....kwani na wao hufanya kazi yao kutokana na amri, maelekezo,....na nionavyo mimi tukio hili kutokana na maelekezo toka kwa wakubwa zao,limetakiwa kufukiwa kinamna...kiukweli hawajalitilia maanani kwasababu zao muhimu, na kwa malengo yao, na kwao kwa sasa wanaona ni bora iwe hivyo, ....’akasema na kutulia kidogo.

‘Lakini hatua kwa hatua, wanaanza kugeukana, Kwani humo kuna watendaji wazuri, hawakubaliani na jinsi inavyokwenda, japokuwa kiukweli, hali zetu, maisha yetu, yanatulzimisha kuja kutii, hata kama unaona sio halali,....hakuna kitu kibaya kama umasikini, umasikini ni mtihani mkubwa sana....lakini nina imani kwa hao wachache, waliobakiwa na imani ya uadilifu, tutashinda tu....’akasema.

‘Ni vigumu sana....hasa unapokuwa wewe ni wa kutii amri tu,....ni mbaya sana,lakini kutokana na makosa yao wao wenyewe, ukweli utadhihiri,...na kwa hiyo mambo yanaanza kuwaendea vibaya...’akasema

‘Makosa gani yanayoanza kutokea na ni akina nani hao,...?’ nikauliza nikionyesha wasiwasi

‘Kwanza hiyo hatua ya kukimbilia kukufutia wewe kesi, ....kwanini wafanye haraka hivyo, huoni ni kuficha jambo fulani, pili, kwanini watu wa ushuru wakakimbilia kukuteua ushike nafasi ya huyo marehemu, ni kuhakikisha hawekwi mtu atakayekuja kugundua madhambi yaliyojificha hapo,...’akatulia akiangalia hewani.

‘Kwa mtu yoyote ni lazima atakuwa na maswali ya kujiuliza, hata mimi nilipona hivyo, nikajua kuna jambo, lakini nimuulize nani,mimi ni mtu mdogo tu, sina uhalali wa kuuliza wakubwa fulani falani mpaka nipate kibali kutoka juu..na siogopi kufanya kazi yangu hiyo, lakini ni nani wa kumwamini,..., inakuwa ngumu kwa kweli,...kwani hali ni mbaya...kila mmoja yupo kwa ajili ya nafsi yake,...ila kiukweli kuna jambo nyuma ya haya yote...’akasema

‘Mimi hapo sijakuelewa,...’nikasema nikiangalia saa, niliona nazidi kuchelewa,

‘Inahitajia kwanza, uniambie ukweli.....uniamini, na uniambie kile kitu,...ili niweze kufanikiwa kwa hili nililokusudia kulifanya....’akasema

‘Mhh, kwanza hebu niambie umesema kuna jambo nyuma ya haya yote, ni jambo gani mbona mimi hapo sielewi?’ nikauliza nikionyesha wasiwasi hata kugeuka huku na kule kuhakikisha hakuna mtu anayefuatilia maongezi yetu. Pale tulipokuwa tumekaa ni mbali kidogo na wateja wengine, na sauti ya mziki wa taarabu ilikuwa kubwa kuficha sauti ya maongezi yetu.

‘Ni kweli, unaweza kusema hivyo, kwa hali uliyona nayo kwa sasa...kwani nafsi yako inakushauri mengi, likiwemo la kuwa kama mtu fulani, kupata, ...au sio, ni nani hataki kupata, ni nani hataki cheo, ni nani hataki maisha mazuri...hakuna, kila mmoja anatakamani hivyo....sasa ni kazi kwako kupambana na nafsi yako....’akasema

‘Una maana gani kusema hivyo?’ nikamuuliza

‘Nikuambie ukweli, wewe hapo ulipo huoni, husiki, hulewi, kwani pamoja na yote, mdada keshaiteka nafsi yako.....lakini nikuambie ukweli, wewe wanakutumia na wataendelea kukutumia ili kuendelea kuficha mambo yao....’akaniangalia moja kwa moja usoni.

‘Mhh, una maana gani?’ nikauliza

‘Wanachotaka wao ni kuendelea kukuweka wewe kama chambo, pia wanahitajika mtu maalumu wa kuziba pengo la marehemu, mtu huyo anahitajika kwa haraka, ili aweze kufukia mashimo yaliyoachwa na marehemu,...mwisho wa siku inaonekana ni wewe ndiye uliyekuwa nyuma ya hayo yote ndio maana ukamuua mtoza ushuru, ndio maana ukaomba hiyo nafasi, ndio maana na ulipoipata ukaharibu ushahidi...’akasema

‘Mhh, kwanini mimi...?’ nikauliza huku nikionyesha kuwaza

‘Dunia hii ione hivi hivi tu, kila jambo linalotendeka ujue lina mipangilio yake, na mwisho wa siku ni kuwafaidisha watu fulanifulani, waliojiapanga kihivyo...kwahiyo masilahi ya hao watu yatalindwa kwa jinsi yoyote ile, mengine ni kama mchezo wa kuigiza tu ....ndio maana wakakimbilia kukuchukua wewe, walishakupima, na kufahamu udhaifu wako...’akasema

‘Mhh, haya bwana, nakuona unazidi kunichanganya tu, mimi naona niondoke, maana hata sijui kwanini umeniita hapa, naona nirudi hotelini, nisije kuambiwa nimekiuka mashati ya mdhamini wangu....’nikasema

‘Cha muhimu, nataka wewe uelewe hali halisi....’akasema na kuniangalia moja kwa moja usoni

‘Ok, ...tusema nimeanza kuelewa, nikuulize swali, katika uchunguzi wako hadi hapo ina maana una uhakika kuwa mimi sio niliyemuua mtoza ushuru?’ nikauliza nikionyesha kuchoka, na nikaangalai saa, nilikuwa na wasiwasi kuwa mdada atakuwa ananitafuta.

‘Kwangu mimi siamini kuwa ni wewe ndiye uliyemuua huyo mtoza ushuru,....yawezekana ukafanya hivyo, lakini ukiangalia kwa makini, unabakia kujiuliza kwanini, ...alabda tusema ulimuua kwa bahati mbaya,ukijihami, au ukitumiwa, bado siwezi kuoanisha yote hayo kutokana na uchunguzi wangu, ndio maana nataka ukweli kutoka kwako, ili nisitumie muda mwingi kulichunguza hilo, hata kama hutaniambia ukweli mimi nitaugundua tu,...’akasema

‘Kwahiyo kumbe hata wewe unaweza ukaamini kuwa mimi nimemuua huyo mtoza ushuru?’ nikamuuliza

‘Swali la kujiuliza ni kwanini ufanye hivyo, sioni sababu ya wewe kufanya hivyo,...lakini polisi wao walishafikia hatua ya kuamini hivyo, ....wana ushahidi wa kutosha tu, na hadi sasa wanaamini hivyo, ila kwa namna zao wamelifunika hilo swala kwa shinikizo fulani, ....’akasema akiniangalia kwa pembeni.

‘Shinikizo kutoka kwa nani?’ nikauliza na yeye akaendelea na maelezo yake bila kujali swali langu.

‘Mimi bado nina wasiwasi na jambo fulani, kwani kama ni kweli, ya kuwa ulijibadili sura na kujiweka ndevu za bandia..., hapo hata mimi nitakuwa na mashaka na wewe, labda unipe sababu za kufanya hivyo, ndio maana nikakuita hapa uniambie ukweli, ni kwanini ulifanya hivyo...’akasema

‘Mhh, sio mimi, sijabadili sura kwanini nifanye hivyo....’nikasema nikijilazimisha kutabasamu, moyo haukutaka kusema lolote kuhusu hilo.

‘Unafahamu kuna mashinikizo ya wakubwa,....kama hutafanya wanavyotaka wao, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kushikiliwa tena, na ikiwezekana upotee kiana,unaweza ukashikiliwa ukafia huko huko mahabusu, na safari hii unapelekwa gerezani moja kwa moja...na nina uhakika ukitoka huko hutachukua muda, utakufa kifo cha kawaida tu, wanafahamu wenyewe jinsi ya kufanya, hasa wakikuona wewe ni tatizo, badala ya faida waliyoitarajia ...ndio hapo nikaona ni bora mimi na wewe tuwe na mkakati wa pamoja...’akasema

‘Mbona unanitisha, mimi kiukweli haya yote siyataki na mpaka sasa najiuliza kwanini naingizwa kwenye haya majanga,sipati jibu...’nikasema

‘Sio kukutisha, ndivyo hali ilivyo,na huenda umeingia ili ujitoe kwa taifa lako, kwa watu , kwa jamii,....’akasema na mimi nikamtupia jicho la haraka na akatabasamu na kusema

‘Cha muhumi, kama nilivyokuambia ni ukweli wako kwangu, ili tusaidiane kwa hili, sitaki haraka, sitaki kukushinikiza, wewe kaa fikiri, tafakari,...nilijaribu kuonana na mzee, lakini nikasikia kapatwa na mshituko, nataka kujua ni kwanini hali hiyo ikamtokea, kuna sintofahamu inaendelea kati yao..yule mzee, ni imara sana, huenda ikawa ni mbinu, huenda, kweli, kuna jambo, nataka kulifuatilai nione ni kwanini ikatokea hivyo.....’akasema

‘Ina maana wewe hukuwahi kuongea naye?’ nikamuuliza

‘Niliwahi, mzee, alishaniona sipo naye, aliniita kama kunionya, na mimi sikutaka kuongea naye zaidi, nilimwambia kuwa mimi natimiza wajibu wangu, akaniambia anataka kuongea na mimi tena,...nikaondoka zangu, huku nyuma nasikia kapatwa na mshituko....sijui, na sina uhakika kwanini...nataka kulijua hilo....’akasema

‘Wakati unaondoka hukuona mtu akifika,...?’ nikamuuliza

‘Sikuona,..siku hizi sio lazima watu wakutane...na mzee yule ni mjuzi, mtaalamu, ni kichwa...sio utani, hadi sasa siwezi kumzania ubaya,...lakini kama nilivyokuambia, hali halisi, maisha na hata shinikizo, linaweza kumfanya mtu akafanya hata lile asilolipenda...’akasema

‘Unataka kuniambia huyo mzee ni nani, ana nini mpaka aweze kuingilia mambo ya ndani ya polisi,...kwanza ni mstaafu au?’ nikiamuuliza

‘Kwa kazi zetu hizi, hakuna cha kustaafu, ilimradi unapumua, siku yoyote na wakati wowote upo kazini..ndio kuna kupunguziwa majukumu, lakini kwa cheo alichokuwa nacho mzee, bado anahitajika sana...na sina uhakika..ndio maana nahitaji watu wakweli, tutakaosaidiana nao, ila wawe wavumilivu, kwani baada ya yote haya, nina imani,faraja itakuja tu....’akasema

‘Faraja...mmmh, kwa hali kama hii, mimi naona ni kujiweka katika maisha ya wasiwasi katika maisha yako yote...’nikasema

‘Ni heri ujitolee, kwa wema, ukweli na haki, ili hata ukifa, una akiba mbeleni, kuliko kufa kwa shinikizo la madhambi na dhuluma, ukifa hata maiti yako haina thamani tena zaidi ya watu kujaa na kukusifia tu, ...lakini huko mbeleni huna chako, utakuwa ni mtu wa kuadhibiwa milele na milele...mimi nina imani ya dini kwahiyo nayasema haya nikiwa na yakini hiyo....’akasema

 ‘Una maana gani kusema hivyo na huyo mzee, ni yupi, ?’ nikauliza

‘Nakutaka tushirikiane kwa hili,....japokuwa kiukweli ni hatari, lakini ni bora kuliko hivyo ulivyo sasa, hapo ulipo hajui kabisa ni nani adui yako, ....huwezi ukawaamini moja kwa moja akina mdada na washirika wake, wao wana malengo yao,  na zaidi wanasimamia kwenye masilahi yao,nakuonya kwa hilo ujaribu sana kuwa makini, hasa na akina mdada,...’akasema.

‘Mhh, hapo napo kunanitisha, hata sijui nifanya nini,..lakini mmhhh,, mimi nataka kufahamu ni nani yupo nyuma ya haya yote na kwanini wamuue mtoza ushuru, na kwanini wanitumie mimi....mimi kama unavyoniona ni mtoto wa mkulima sina mbele wala nyuma, kwanini mimi?’ nikauliza.

‘Masilahi yana ajizi fulani, mtu yupo tayari hata kumuua mtoto mchanga ili tu awe tajiri, watu wanaweza hata kutumia maandiko matakataifu kwa ajili tu ya kuficha uchafu wa mahambi yao kwa nia ya kupata masilahi, utatungwa uwongo mwingo, propaganda potofu, na kila hila ili mrai tu wafanikiwe...ndivyo, hao watu walivyo...wanaweza kujifanya ni watakatifu, wema, watu wa mungu, lakini mioyoni mwao wanalenga masilahi, hakuna kingine.....’akasema

‘Kwanini unasema hivyo...?’ nikamuuliza

‘Kwanini nasema  hivyo, ni kutokana na uchunguzi wangu, sisemi tu kwa nia mbaya, au kwa nia ya kuwazuia watu wasifanikiwe mambo yao, hapana...ila kwanini watu hawasemi ukweli, kwanini watu hawatendi haki, na kwanini tudhulumu haki za raia, ambao wanatesekeka, wanakuwa masikini kwasababu ya tamaa zetu....inaniuma sana...’akainama kidogo.

‘Mimi babu yangu alikufa masikini, baba akatumikia nchi, na hali ikawa hivyo hivyo, wakisimamia kwenye ukweli na haki, na mimi naona itakuwa hivyo hivyo...ina maana ukisimamia kwenye haki na ukweli ndio matokeo yake niyo hayo...hapana, ni lazima kuwa na njia ya kuyasimamisha haya, nina imani jamii ikilielewa hili tutafanikiwa...’akasema

‘Kutokana na hili tukio, kuna jambo limejificha hapa, na kuuwawa kwa huyu mtu, japokuwa huenda haikupangwa iwe hivyo,lakini ni katika kutapatapa kwa mfa maji, kuwa huenda jamaa huyu atatuuza, kuna lengo fulani limepangwa....’akasema

‘Mimi hapo sielewi,nakuona unaongea tu, lakini sijakuelewa, hebu nieleze kwanini huyu mtu aliuwawa, na huyo muuaji aliwezaje kuingia, na kufanya hayo bila ya hata mimi kufahamu?’ nikauliza

‘Mlinzi....’akasema.

‘Mlinzi ana nini?’ nikauliza

NB: Mpelelezi huyoooo, hebu tuone mwisho wa haya ni nini...tusichoke!

WAZO LA LEO:Ilivyo, nafsi ya mwanadamu inapotaka kitu, humtuma kufanya lolote lile, na kutafuata njia ya kujihalalishia hayo matendo, hata kama kiuhalisia tunafahamu fika, kuwa hayo tunayoyatenda sio sahihi. Usipoweza kuimudu nafsi yako,na kuitawala, na badili yake ukatawaliwa na hiyo nafsi, kamwe hutaweza kujizuia kutenda mambo mabaya, ikiwemo, ufisadi.



Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Impact crusher is the new type of mine crushing equipment that Hongxing absorbs the foreign advanced similar mining crushing equipment performance improvement on the old-fashioned impact crusher. As the secondary device configuration of jaw crusher and cone crusher, it plays an important role in many crushing production equipment, it together with impact crusher, hammer crusher and other secondary crushing equipment and form a reasonable crushing equipment system. Impact crusher is cost-effective, reliable work, high production efficiency, and its unique working principle achieves energy efficient production, the choice in many areas of production is the best. [b][url=http://fomachine.en.alibaba.com/product/1901089802-222364518/factory_price_multifunction_stainless_stell_chili_crusher.html] rice grinder [/url] [/b]Luckily, to clean your spice grinder, all you need is a bit of rice. This goes for coffee grinders, too, and is especially useful if you value your craft coffee and don't want any stale grinds in tomorrow's cup.Here's how to clean an electric grider swiftly, so you can switch from cardamom to cumin with no risk of cross-contamination. After all, variety is the spice of life. [b][/b]
It's hard to deny the convenience of wheat flour. One bag and you've got a million recipes at your fingertips. Venture even slightly into gluten-free recipes, and your grocery shopping list could double in length with various flours and starches. It gets especially frustrating when a recipe calls for just 1/4 cup of two or three different flours. Suddenly you're investing in a $5 to $10 bag of millet flour or gluten-free oat flour that will sit, virtually untouched, for months and months . To avoid this issue, and to simplify my pantry, I learned how to make gluten-free flours at home in a pinch. [b][url=http://fomachine.en.alibaba.com/product/1901202370-222364518/superior_quality_herb_to_powder_grinder.html]soya bean grinder [/url] [/b]Mechanism sand with the self-compacting concrete design resources distribution is limited by geographical constraints. traditional natural sand resources used to prepare self-compacting concrete are scarce in China's Yunnan, Guizhou, Sichuan and other regions, and pit sand and artificial sand resources is rich, but this material is not the best choice for self-compacting concrete on technical characteristics, which leads to the birth of the complete set of equipment of artificial sand maker production line. [b][/b]
These efforts will result in a new investment system under which investment is guided by the market, enterprises make their own investment decisions, banks examine creditworthiness independently, various forms of financing coexist, intermediary services are standardized and macro-control is efficient. [b][url=http://fomachine.en.alibaba.com/product/1901119683-222364518/superior_quality_rice_grinder.html] rice grinder [/url] [/b]Impact crusher is the new type of mine crushing equipment that Hongxing absorbs the foreign advanced similar mining crushing equipment performance improvement on the old-fashioned impact crusher. As the secondary device configuration of jaw crusher and cone crusher, it plays an important role in many crushing production equipment, it together with impact crusher, hammer crusher and other secondary crushing equipment and form a reasonable crushing equipment system. Impact crusher is cost-effective, reliable work, high production efficiency, and its unique working principle achieves energy efficient production, the choice in many areas of production is the best. [b][/b]