Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, February 4, 2014

BAADA YA DHIKI FARAJA-8
Ikaja siku ambayo sitaweza kuisahau, siku iliyoharibu uataratibu mzima wa maisha yangu, kwakweli siku hiyo sitaweza kui...Ilikuwa ni jioni jioni baada ya kazi, bosi aliniambia nimchukue Mdada nimfikishe kwake, kwasababu huyo mdada kamwambia bosi hajisikii vizuri, na aliomba lifti kwa bosi, lakini bosi alikuwa na safari sehemu nyingine.

‘Sinauweza kumchukua kwa gari langu, nina safari seehmu nyingine, unaweza kumchukua na pikipiki yako, maana nina kikao muhimu sana, mchukue umfikishe kwake..’akaniambia bosi.

‘Oh, nilitaka kupitia kwenye mazoezi kwanza, lakini sio shida nitampeleka nyumbani kwake,hakuna shida,....’nikasema na bosi akaondoka.

Nilimchukua vyema Mdada, na safari ya kwenda kwake, inapitia kwenye ile hoteli au kama wanavyoiita nyumba ya wageni, yeye huwa anaipenda sana sehemu hiyo, akaniomba tuingie tupate angalau soda, mimi niamkatalia kwa sababu nahitajika kwenye mazoezi,..

‘Basi itabidi unisubiri hapa kidogo, nikanunue kinywaji, maana bila ya kuchukua kinywaji sitaweza kulala...huwa hii ndio dawa yangu ya kichwa, kikianza kuniuma, hata ninywe dawa gani, hakitulii, ni mpaka nipate kinywaji...’akaniambia.

‘Na wewe bwana kwanini unajidekeza kiasi hicho, kwani ni lazima unywe..hilo ni tatizo la kwenda hospitalini, ukinywa pombe, ni kujiumiza kidogo kidogo, wewe hujui tu, na kuna sababu ya hayo maumivu ya kichwa, waone wataalamu’ nikamwambia.

‘Tatizo lako wewe hujajua starehe za dunia hii, maisha ni mafupi usipoyatumia vyema, ukiwa hai, utakufa na wenzako watakuja kuyatumia yao na vile ulivyoviacha,...ni bora utumia sasa, na uyatumie maisha yako mafupi, pale unapoweza usije ukajutia ukiwa hujiwezi tena, na wenzako wakitami ufe haraka, ili waweze kurithi mali yako...’akasema

‘Ina maana hakuna starehe nyingine mpaka unywe pombe,...huko ni kutaka kujiua kidogo kidogo..’nikasema.

‘Ni nani kasema najiua, ..mimi nakunywa kistaarabu, nikijisikia, kwasasa nakunywa zaidi kwasababu ya mawazo..’akasema.

‘Unawaza nini, huna familia huna majukumu?’ nikamuuliza.

‘Nakuwaza wewe, wewe hutaamini hilo kwasaabbu umeniona kuw labda mimi ni muhuni...nikuambie ukweli, mimi kila nikilala, nikiamuka, nakuwaza wewe, najiuliza wewe upoje, mbona haupo sawa na wanaume wengine, ...’akaniambia.

‘Kwani mimi nipoje?’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Sijawahi kusumbuka akili yangu na mwanaume kama nilivyosumbuka dhidi yako, lakini kwa vile mnaona wanawake hawana haki ya kusema ukweli kuwa na wao wanatokea kupenda, mnaona mwanamke akiongea labda ni mimi ni malaya, ...lakini sivyo hivyo, nikuambie ukweli tangu nifike hapa ni mwanaume mmoja tu aliyeweza kuingia kwenye anga zangu, wengine wote ni washika pembe..’akasema huku akinishika mkono kunivutia tuingie ndani ya hiyo hoteli, nikaona nisje kuonekana na watu nikivutana na huyo binti nikakubali, tukaingia kwenye hiyo hotel, huku akinisimulia mambo yake.

‘Umesema ni mwanaume mmoja tu, uliywahi kutemba naye tangu ufike hapa, ina maana ni huyo mchumba wako...?’ nikamuuliza

‘Ni kweli ni huyo tu basi, lakini sio kwamba nilimpenda, hapana, ilitokea tu, kwa vile ni yeye aliyenipokea, akawa ananijali, nikatumia sana pesa zake, na akawa ni mtu wa karibu sana kwangu kipindi hicho nilikuwa  na matatizo mengi ya familia nilipotoka, akawa akiniliwaza, na kuanza kunifundisha maisha, yeye ndiye alinifundisha haya kunywa pombe, nikahisi huyu ndiye mwanaume wa kuishi naye, lakini siku zilivyozidi kwenda nikagundua kuwa nimepotea maboya, ..’akasema
‘Kwanini?’ nikamuuliza.

‘Huoni, yeye ndiye kaniharibia mpangilio mnzuri wa maisha,usifikiri haya ninayoyafanya nayapenda, sivyo nilivyokuwa hivi...nikawa natafuta njia ya kuachana naye, lakini ikawa ngumu, maana wanaume wengi wanamuogopa..’akasema.

‘Na wale waliopigana kwa ajili yako sio wapenzi wako?’ nikamuuliza.

‘Wale..hahahaha, kwa ni wale tu, wapo wengi, wameshawahi kupigana kwa ajili yangu, wote hawo, ni washika pembe tu, wanajigonga kwangu lakini hakuna hata lepe la upendo kwao, na sijawahi hata kufikiria kuwa nao kama wapenzi, niliwachukulia kama kaka zangu wa ofisini tu, lakini kumbe moyoni wameshakwenda mbio, hata walipopigana, nilijiuliza wanapigania nini,...ujinga wao...’akasema.

‘Na sasa wamerudi kazini, utakuwa ukitembea na nani kati ya hwo wawili?’ nikamuuliza.

‘Kutembea nani  kwenda wapi, chakula cha mchana,..mmh, yoyote aliyekuwa tayari ilimradi asinibore..lakini mimi nakutaka wewe tu.’akasema,

‘Lakini mdada mimi nakuomba sana, usinifanyie hivyo vituko vyako, mimi nakuheshimu sana, na nitafurahi kama tutaishi kama mtu na kaka yake, sio zaidi ya hapo, tafadhali sana...’nikasema na yeye akaniangalia halafu akacheka sana na kusema;

‘Wewe ni kaka yangu, mimi sina maingiliano ya damu na wewe...sikiliza nikuambie kitu, mimi nitakukubalia jambo moja, kuw nitakuwa mpenzi wako a siri...hakuna atakayejua hilo, ...maana siwezi kukudanganya kuwa nitakuangalia hivi hivi tu wakati moyo wangu unauma,..usiona nauambia hivi ukafikiria labda mimi ni mwanamke rahisi,...’akasema huku akijiangalia.

‘Kama unabisha uliza watu, wengi wanafikiria hivyo, lakini wakinijia wanajikuta sivyo wananavyofikiria, mimi nina msimamo wangu, na kiukweli ni kwamba nikitaka jambo ni lazima nilipate, kama silitaki hata ufanye nini hupati kitu kwangu..na kwangu mimi kuongea ni sehemu ya starehe, ninaweza kuongea, lakini sivyo nilivyo...’akasema.

‘Unataka kusema nini?’ nikamuuliza.

‘Kwamba mimi nakutaka wewe uwe mpenzi wangu basi...sitaki mwingine,...hilo halina mjadala, na nitajitahidi mchumba wako asifahamu ilimradi tu utimize yale ninayo yataka,..siwezi kuhangaika moyo wangu wakati wewe upona nikikamlisha matakwa yangu , ninaweza kusema basi sikutaki tena,lakini sijui kama nitaweza kuishi bila wewe ...’akasema.

‘Kwahiyo unataka nifanye nini kwako, maana mimi nimeshakuambia msimamo wangu,...ni ni matwakwa gani hayo unayotaka kutimiza kwangu...?’nikamwambia wakati huo nilikuwa nakunywa soda.. nakumbuka kabisa ilifunguliwa mbele yangu, nikanywa fundo la kwanza, la pili nikaanza kuona macho yakiishiwa nguvu,..

‘Usijali ...wewe kunywa halafu utajua ...ni lazima uwe mjanja,wenzako walikuwa hivyo hivyo, sasa hivi wapo hapa..’akasema akiniangalia mchoni n kuonyesha mkono wake huku kipiga piga kiganja chake kwa mkono wa pili.

‘Mbona....’nikaiangalia ile soda , na Mdada akacheka, na kusema.

‘Kwisha kazi, leo umepatikana, unajifanya mjanja eeh,...sasa mchezo unaanza inuka twende huku....washikaji mpo tayari....’akasema na sikukumbuka, nilichokuwa nikikifanya, nilikuwa kama zezeta fulani, na akili ilikuwa sio yangu,...nilizindukana kikaili nikiwa juu ya kitanda, nikajaribu kuinua kichwa, lakini kichwa kilikuwa kizito,..nikatulia na baadaye nikajitahidi nikainuka, nilikuwa kama nilivyozaliwa..


‘Oh, kumetokea nini?’ nikajiuliza, lakini hakuna wa kunipa jibu,...nikainuka na kwenda bafuni, niliporudi nilimkuta mdada akiwa kakaa pembeni ya kitanda, akitabasamu na kusema;

‘Kumbe na wewe wamo eeh,...’akasema huku akiniangalia kwa macho yaliyojaa dharau

‘Unasema nini?’ nikauliza

‘Sasa umeshaingia kwenye anga zangu, wewe na mimi ni wapenzi, kuanzia leo hii, sitaki kusikia habari za mchumba wangu au nani, na utafanya kila ninachkuambia ufanye...’akasema.

‘Una maana gani...?’ nikamuuliza na mara akawasha simu yake, simu yake ina sehemu inayochukua kitu kama video na unaweza kumulika ukutani ikaonyesha kama vile unavyoangalia kwenye cinema, na ikaonyesha picha kubwa tu ....oh, sikuamini.

Kwa haraka nikataka kumnyang’anya ile simu, na yeye akainuka na kukimbilia nje, n ikabakai nimeduwaa...sikuamini kuwa ni mimi niliyekuwa nikifanya yale niliyoyaona kwenye simu ya mdada, nilikuwa nafanya kwa hiari yangu mwenyewe kama ilivyokuwa ikionyesha..aibu tupu..

Nikataka kumnyang’anya ile simu, akakimbia na kutoka nje, kwa vile bado nilikuwa uchi sikuweza kufukazana naye akasema;

‘Usisumbuke, kila kitu kipo salama, ni wewe tu...’akasema huku akifunga mlango.

Nikainuka na kuichukua nguo zangu na kutoka kwenye kile chumba, nilikuwa kama kuku aliyelowana maji, nikatoka hadi nje ya hiyo hoteli, nikamkuta mdada yupo kwenye pikipiki akiwa ananisubiri, ilikuwa ni kama saa tatu za usiku.

Sikuongea naye, na yeye alikaa kimiya, hadi nikamfikisha kwake, na hakutaka hata kuongea nami akaondoka kuingia kwake, na alipofika mlangoni akawa kama kasahau kitu akarudi na kunishika begani akasema;

‘Usiwe na wasiwasi, mimi nitakulinda kwasababu na kupenda, imefanyika hivyo kwa vile natakiwa nifanye hivyo, lakini hata hivyo, haitakuwa mbaya kama utakuwa namimi sambamba,...unasikia...’aaksema na kunisbusu kwenye shabu, niligeuza kichwa nikamwangalai kwa macho yaliyojaa chuki, hasira...sijui.

Nikamchukia sana huyo dada, nikamuona kaam sio yule niliyekwua namfahamu, na kaam ningelikuwa na kitu cha kumfanya kwa wakitu ule ningemdhuru, nikamwangalia akitembea kuelekea mlangoo wa nyumba yake, na alipofika mlangoni, akafungua na kugeuka, akaniangalai na kutoa tabasamu lake, lakini mimi nilikuwa nimekunaj uso wa hasira, hakujali, akaingia ndani.

Nilibalia pale nikiwa nimetulia, nikiwaza sana halafu nikaondoka kurudi kwangu, nilipofika kwangi , nikaingia chumbani kwangu na kitandani nikaona bahasha, nilipoifungua nikaona picha za utupu, nikiwa na huyo mdada, lakini mdada alikuwa kafichwa sura yake ..

‘Ukitaka usalama wako wa ajira yako, na mchumba wako, fuata na tii kila utakaloambiwa vinginevyo, hizi picha zitafika kwa baba mkwe wako...’karatasi ikandikwa hivyo,

‘Ina maana mdada ana kundi la watu, au ni nani kaleta hiyo bahasha humu ndani na picha za tukio ambalo halijamaliza hata siku moja,na je aliingiaje humu ndani kwangu, wakati ufunguo ninao peke yangu, ....’, nikajiuliza huku kichwa kikiniuma sana.

 Nilijaribu kukiweka maji lakini haikusaidia, nikawa nahangaika na maumivu ya kichwa nikatafuta dawa za kutuliza maumivu lakini ikawa kama nimekichokoza, na wakati nahangaika hivi nikakumbuka siku moja mdada aliniambia;

‘Kichwa huwa kinanuuma sana, lakini nimegundua dawa yake ni pombe, nikinywa kinatulia....’siku hiyo aliniambia hivyo na mimi nilimkatalia kabisa kuwa pombe sio dawa ya kichwa, lakini kwa muda huo kwa jinsi kichwa kilivyokuwa kikiuma nikaona nijaribu hiyo dawa ya mdada, nikatoka kwa haraka hadi duka la jirani nikanunua pombe, nikarudi nayo ndani nikanywa kidogo, nikaongeza, ooh, mpaka ikaisha, nikashikwa na usingizi.

 Kesho yake nikaamuka mapema, nikafanya mazoezi kidogo, nikajiandaa na kwenda kazini, nilipofika nilikwenda moja kwa moja ofisini kwangu na kujaribu kusahau ya jana, lakini haikuwa kazi rahisi, hadi bosi anafika, nilikuwa nipo kwenye dimbwi la mawazo na wakati huo kichwa kilishaanza kuniuma

‘Vipi Mosi, upo safi nakuona kama unaumwa?’ akaniuliza

‘Kichwa kinaniuma sana, sijui kuna tatizo gani?’nikauliza

‘Umekunywa dawa za kutuliza maumivu?’ akaniuliza

‘Ndio lakini haisaidii kitu..’nikasema na yeye akaniangalia kwa mashaka na kusema;

‘Usije ukawa umekunywa mipombe yao au wamekuwekea madawa, kuna haya  madawa ya kulevya, wakikuwekea utasumbuka sana, ...inabidi uwe makini sana, hasa unapokwenda kwenye starehe na watu usio waamini..’akasema na kunifanya niingiwe na wasiwasi, na kujiuliza kwanini kila linalofanyika anakuwa kama anaelewa, nikasema;

‘Sizani kama ni pombe...’nikasema na yeye akasema;

‘Kwa tahadhari, angalia sana, sio kila atakayekuchekea ni rafiki yako, wengine wana malengo hasi dhidi yako, ....uwe makini sana, hasa mnapokuwa kwenye makundi, hata kama sio makundi, hao hao mabinti, marafiki zenu, wanaweza kuwageuka, wakiwa na malengo yao, dunia sasa hivi imebadilika, mtu yupo tayari kuhatarisha amisha ya mwenzake, ili tu afanikiwe jambo fulani,....’akasema na mimi nikakumbuka pale nilipokunywa ile soda, lakini nakumbuka kabisa aliifungau mbele yangu.

‘Haya mimi sina zaidi ,kama kuna tatizo kubwa linakukwaza niambie, nitakushauri na kuona jinsi gani ya kulitatua, lakini usije ukadanganyika, ukatishwa kuwa ni lazima ufanya hivi, ndio utafanikiwa, ..usikubali kama unaona sio sahihi, ...uwe na msimamo thabiti katika maisha yako, usije ukatumbukizwa kwenye maisha ya utumwa, hasa utumwa wa pombe, utapotea, utaumia...’akaniambia na mimi nikawa kimiya

‘Basi ngoja nienelee kukuhadithia kisa changu kidogo , halafu kama bado kichwa kinauma inabidi uende hospitalini..’akaniambia na akaanza kunihadithia sehemu ya kisa cha maisha yake

*********

Unafahamu mwili wa binadamu una thamani sana, ukiwa hai, ukishakufa basi tena wewe ni mzoga, watu watauchezea mwili wako wapendavyo, lakini kama upo hai, mwili wa binadamu,unastahili kulindwa, na mlindaji ni mlindaji wa huo mwili ni wewe mwenyewe, watu wanatakiwa wajue hivyo...

Sio vyema kabisa, kuuchezea mwili wa mwenzako ukauzalilisha, labda iwe ni kwasababu ya kitibabu..., hutaamini kuwa mimi nilitakiwa kuchunguzwa mwili wangu na uchunguzi huo ni wa sehemu za siri.

Ndio nakubali aliyefanya hivyo ni mama yangu mzazi akishirikiana na mama wa kambo lakini umri ukishapevuka, hata mama yako mzazi anakuwa na mipaka yake, ndio maana mwanzoni mama yangu alisita kuifanya hiyo kazi, akifahamu haki za kila mtu hasa katika mwili wa binadamu mwenzako, na sehemu zenyewe ziwe za siri, ndio maana zinafunikwa...

Ninaona ajabu wale wanaochukua picha za uchi za wenzao na kuziweka hadharani, kwenye mitandao na vyombo vya jamii, hilo ni kosa kubwa, huku ni kuzalilishana, na niukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, lakini hili watu hawalikemei, wanaliona ni la kawaida tu, ...wanakemea na kusuta wale wanaojifunika mwili mzima eti hao ndio wanaozalilishwa, hao ndio haki zao za binadamu zinavunja, sio hawo wanaokaa uchi, sio hao wanaweka uchi kwenye mitandao, hao wanatimiza matamanio ya nafsi zao sio mbaya..ajabu kabisa.

Mama yangu na mama wa kambo wakaanza kazi ya kunichunguza, nilijiskia vibaya sana, japokuwa mmoja wa waliokuwa walifanya hivyo ni mama yangu mzazi, lakini moyoni sikupendezewa kabisa, ..hata hivyo ningefanya nini,..nikaona i bora wafanye wapendavyo,sikuwa na njia nyingina ya kulipinga hilo, wakafanya kama alivyotaka baba na mama wa kambo. Nia kubwa ni kutaka kunizalilisha zaidi.

Moyoni nikawa najiuliza ni nani huyo aliyediriki kuwapigia simu na kuwaambia yote hayo, kuwa mimi nilikuwa nafanya umalaya hadi kufikia kubeba mimba na kuitoa, ni nani huyu aliyekuwa akinifuatlia, kwa kwanini alitunga huo wongo, ...sikuwa na uhakika na hilo, yote hayo nikamuachia mungu,

Walipoanza kazi yao, mimi kimoyo moyo nikamuomba mungu anisaidie kwani mimi ni kiumbe tu, sikuwa na kosa lolote, na sikuwa na mwingine angeliweza kuniamini, kwani kwa wakati huo hata mama yangu mzazi anayenifahamu vyema, asingeliweza kuniamini, kwa jinsi baba na mama wa kambo walivyolielezea hilo swala, sikuwalaumu.

‘Weka miguu hivi, unajibaragua nini, ukienda leba kuzaa unafikiri utajiweka hivyo, na mbona ulipokuwa unafanya uhuni wako hukuon aibu ...’akasema mama mdogo na mama yangu akamwangalia mama huyo  kwa macho ya mshangao, akasema;

‘Sio kauli nzuri kwa mtoto, je kama tukukuta hajafanya hivyo mnavyodai, utakuja kusema nini, ujue wewe ni mzazi kama mimi, unafikiri kwa akuli hiyo mimi ninajisikia vipi,au ni kwa vile hujamzaa huyu mtoto ...kumbe ndivyo ulivyokuwa ukiishi watoto wangu huko, ndio maana wakawa wanajifanyia watakavyo,..’akalalamika mama.

‘Wewe hujui tu nilivyokuwa nikihangaika na hawa watoto hasa huyu mtoto,ni mjeuri, hanisikii, ...na tabia yake ya uhuni ndio iliyonifanya nishindwe kukaa naye, muulize hata baba yake kama mimi ninamsingizia...’akasema mama wa kambo.

Mama akaniangalia machoni, huku machoni nikihisi anataka kulia, akaniambia;

‘Usijali kama ni kweli tutaona, ....’akasema na wakaanza kazi yao

Waliponikagua wakagundua kuwa kweli mimi sijawahi kufanya hayo machafu waliyonisingizia, sijawahi kukutana na mwanaume, mama wa kambo akabakia kimiya na alishindwa hata na la kuongea, akatoka mle ndani kwa haraka, utafikiri kamwagiwa maji na mimi nikainuka na kumwangalia mama , mama akaniangalia machoni, huku akitamani kulia, akanishikilia na kunikumbatia akasema;

‘Usijali mwanangu nashukuru sana kwa kunilinda, sijui nikupe nini....mungu mwenyewe ndiye anayefahamu jinsi gani ninavyojisikia moyoni kwa sasa,..mungu atazidi kukulinda, endelea na msimamo wako huo huo, usikubali hata siku moja wakudanganye wahuni, umenilinda na kuilinda heshima yako,...’akasema na mimi sikuwa nimelewa, nikauliza

‘Mama mumegundua nini?’ nikamuuliza

‘Hujaguswa na mwanaume yoyote kama ulivosema, ...’akasema mama

‘Ni kweli mama, mimi nimewaambia alkini hawataki kuniamini.

‘Usijali ndivyo wanadamu tulivyo,  haya jiandao uje tusikie waatsema nini tena...’akasema mama, akitoka na kuniacha ndani.

Mimi nilimshuku mungu, nikatoka kuwafuata huko kwenye kikao, na nilipofika nikakuta baba na mama wa kambo wanaongea na nilimwangalia baba nisikie atasema nini,au ataambiwa nini na mama zangu, lakini mama wa kambo alichosema ni kuwa anataka waondoke siku hiyo hiyo kurudi mjini;

‘Tuondoke zetu, kuna kazi nimekumbuka ni ya muhimu sana, nisipoifanya leo nitakosa pesa zangu, mimi silali hapa ..’akamwambia baba na baba akawa kaduwaa, mama ndiye akasema;

‘Mume wetu anasubiri taarifa ya uchunguzi wetu dhidi ya mtoto, mwambie ukweli umegundua nini...’mama yangu akasema.

‘Kwani wewe huna mdomo wa kumwambia,....’akasema mama wa kambo akibenua mdomo kwa dharau.

‘Ndugu zanguni, shutuma zenu dhidi ya mtoto sio kweli, binti yetu hajawahi kuguswa na mwanaume, bado ana usichaan wake...’akasema mama

‘Una uhakika na unalolisema?’ akauliza baba akiwa kaduwaa kwa mshangao, akageuka kumwangalia mke wake, yaani mama wa kambo, na mama wa kambo akawa anajifanya kutafuta kitu kwenye mkoba wake, na mama akasema;
.
‘Ndio hivyo muulize mke mwenzangu, naona mlidanganywa na watu wasiompenda mtoto wetu,na ni makosa makubwa mliyoyafanya kwani mlisikia taarifa na hamkuhangaika kuhakikisha ukweli wa hizo taarifa, na baya zaidi mkakimbilia kumfukuza mtoto shule..’akasema mama.

‘Nimekuamba tuondoke bwana, kama haupo tayari mimi naondoka..’akasema mama wa kambo, akianza kutoka nje, na baba akawa kimiya akiogopa hata kuniangalai machoni. Mama akasema;

‘Lakini hatujamalizana na kikao, nyie ndio mlikiitisha, na uchunguzi tumeshaufanya ni bora tulete taarifa na ukweli uwe wazi, kwani ni kosa limefanyika, la kumshutumu mtu ambaye hajafanya hilo kosa, kama wazazi inabidi tuseme ukweli kuwa tumekosea, ili binti naye moyo wake ufurahi...’akasema mama yangu.

‘Unasema nini, unataka mimi nimuombe mtoto msamaha, ...hapana, na sina uhakika na huo uchunguzi wenu, bado nitalifanyia kazi ..’akasema baba akijiandaa kuondoka. Na mama akasema;

‘Mnajisumbua bure, na ipo siku mungu atawaumbua, huo sio ulezi bora kwa watoto, leeni watoto wote sawa, mkijua kuwa wote ni wazazi, na mtoto huyu ni damu yenu, kwanini mnagawa matumbo yenu ,kwa ubaguzi...haya sasa ukweli mumeuona mnataka nini zaidi...’akasema mama.

 Mimi nilijua sasa wazazi wangu wataniamini na yale maneno ya kashifa yataisha, lakini sijui mimi nilizaliwa na mkosa gani, na tukio hilo lilikuwa kama limewazazlilisha wao, wakawa sasa kama wanataka kulipiza kisasi, kwani hali haikuwa na mabadiliko kwani baba walipoondoka kesho yake nikaagizwa nirudi huko mjini, nikasaidie kazi za nyumbani.

‘Mama unakubali niende tena huko?’ nikamuuliza mama.

‘Baba yako kasema hivyo, kasema wewe ni mtoto wake, inabidi umtii, nafikiri sasa hivi watakutahamini kwani wamegundua kuwa wewe huna tabia kama waliyoisema wao..’akasema mama.

Basi mimi nikakubali kwa shingo upande nikaenda huko mjini, na nilipofika nilikuta mateso yakiwa pale pale kila siku kunazuka jipya, na mimi ndiye mkosaji,mimi ndiyeo muongo ,mie ndio malaya,nilishangaa hiyo kauli ya kuitwa malaya bado walikuwa nayo mdomoni, hadi pale nyumbani wakahisi kuwa huenda kweli mimi ni tabia yangu, kuwa mimi ni malaya, kwani baba kila akiniita alikuwa haniiti kwa jina langu akawa ananiita kwa kusema;

 `Wewe malaya njoo hapa‘

Jina hilo lilinikera sana, ...umalaya huo nimeufanya lini, hadi kupewa jina baya kama hilo ila baba yangu hakuweza kuwa na aibu na kuendelea kuniita hivyo, `we malaya fanya hivi , wewe malaya ulienda kwa mabwana zako,... ‘

Jinsi,maisha yalivyoenda na mateso ndio yalivyo zidi .kuzalilika, kupuuzwa  na hata kumsema mama yangu kuwa ndiye aliyenilea hivyo vibaya ndio maana mimi ni mvivu, malaya, sina adabu, kitu ambacho sio kweli, niliumia sana, lakini sikuwa na la kufanya.

Siku moja ilikuwa ni jumapili, kukatokea kupotea kwa vifaa, kama ilivyo kawaida shutuma hizo zikapelekwa kwangu, baba alikuwa amekasirika kweli, aliposikia kuwa etu ni mimi nimefanya hivyo, ikawa ni sababu ya kumalizia hasira zake, alizokuwa kaziweka moyoni, akachukuwa waya wa pazia na kuanza kunitandika nao, ...

Kwakweli siku hiyo niliumia sana, sio kimwili zaidi, lakini moyoni, nikawa na uhakika kuwa sio mimi niliyefanay hilo kosa, ila ni uzembe wa wenzangu, na wao kwa umoja wao wakanisingizia mimi, nikajiuliza hivi mimi nina tahamni gani kwa ahwa watu

Hapo nikawa sina jinsi, akili ikawa imechoka, nikaona sina amani, sina thamani, naona sihitajiki tena hapa duniani, nikaingia ndani, kulikuwa na vidonge vya pritoni vilikuwepo kwangu vilinunuliwa kwa ajili ya mafua, nikaingia kwa mama, nikaona vipo vingine, nikaona havitoshi nikaenda dukani nikaongezea, hadi vikafika vidonge 30, nikaona sasa hivyo vibatosha.

Nilirudi chumbani kwangu, nikaona niandike ujumbe, nikaona haina haja, mwili wangu utakuwa ujumbe, nilishachoka nilishafikia maamuzi ya kujiua, sikuwa an njia nyingine, nikamuomba mungu anisamehe kwa kosa hilo, kwani nimevumilia nimechoka, nikavichukau vile vidonge na maji nikavimeza, na kulala kutandani, .

NB: Mpendwa kachoka na maisha kaamua kujiua, je itakuwaje..


WAZO LA LEO: Sote ni wanadamu na sisi sote ni watoto wa Adamu na Hawa, kwahiyo sote ni ndugu wa baba na mama mmoja, ni kwanini tuchukiane, ni kwanini kuwe na sababu za kubaguana, na kuona huyu sio mtoto wangu, huyu sio ndugu yangu, huyu sio mwenzetu, ...hayo yametoka wapi, ina maana unaposema hivyo wewe sio mtoto wa Adamu, ...tupendane, ili dunia iwe kisiwa cha amani.

Ni mimi: emu-three

No comments :