Ikaja siku ambayo sitaweza kuisahau, siku
iliyoharibu uataratibu mzima wa maisha yangu, kwakweli siku hiyo sitaweza
kui...Ilikuwa ni jioni jioni baada ya kazi, bosi aliniambia nimchukue Mdada
nimfikishe kwake, kwasababu huyo mdada kamwambia bosi hajisikii vizuri, na
aliomba lifti kwa bosi, lakini bosi alikuwa na safari sehemu nyingine.
‘Sinauweza kumchukua kwa gari langu, nina
safari seehmu nyingine, unaweza kumchukua na pikipiki yako, maana nina kikao muhimu
sana, mchukue umfikishe kwake..’akaniambia bosi.
‘Oh, nilitaka kupitia kwenye mazoezi kwanza, lakini
sio shida nitampeleka nyumbani kwake,hakuna shida,....’nikasema na bosi
akaondoka.
Nilimchukua vyema Mdada, na safari ya kwenda
kwake, inapitia kwenye ile hoteli au kama wanavyoiita nyumba ya wageni, yeye
huwa anaipenda sana sehemu hiyo, akaniomba tuingie tupate angalau soda, mimi
niamkatalia kwa sababu nahitajika kwenye mazoezi,..
‘Basi itabidi unisubiri hapa kidogo, nikanunue
kinywaji, maana bila ya kuchukua kinywaji sitaweza kulala...huwa hii ndio dawa
yangu ya kichwa, kikianza kuniuma, hata ninywe dawa gani, hakitulii, ni mpaka
nipate kinywaji...’akaniambia.
‘Na wewe bwana kwanini unajidekeza kiasi
hicho, kwani ni lazima unywe..hilo ni tatizo la kwenda hospitalini, ukinywa
pombe, ni kujiumiza kidogo kidogo, wewe hujui tu, na kuna sababu ya hayo maumivu
ya kichwa, waone wataalamu’ nikamwambia.
‘Tatizo lako wewe hujajua starehe za dunia
hii, maisha ni mafupi usipoyatumia vyema, ukiwa hai, utakufa na wenzako watakuja
kuyatumia yao na vile ulivyoviacha,...ni bora utumia sasa, na uyatumie maisha
yako mafupi, pale unapoweza usije ukajutia ukiwa hujiwezi tena, na wenzako
wakitami ufe haraka, ili waweze kurithi mali yako...’akasema
‘Ina maana hakuna starehe nyingine mpaka unywe
pombe,...huko ni kutaka kujiua kidogo kidogo..’nikasema.
‘Ni nani kasema najiua, ..mimi nakunywa kistaarabu,
nikijisikia, kwasasa nakunywa zaidi kwasababu ya mawazo..’akasema.
‘Unawaza nini, huna familia huna majukumu?’
nikamuuliza.
‘Nakuwaza wewe, wewe hutaamini hilo kwasaabbu
umeniona kuw labda mimi ni muhuni...nikuambie ukweli, mimi kila nikilala,
nikiamuka, nakuwaza wewe, najiuliza wewe upoje, mbona haupo sawa na wanaume
wengine, ...’akaniambia.
‘Kwani mimi nipoje?’ nikamuuliza kwa mshangao.
‘Sijawahi kusumbuka akili yangu na mwanaume
kama nilivyosumbuka dhidi yako, lakini kwa vile mnaona wanawake hawana haki ya
kusema ukweli kuwa na wao wanatokea kupenda, mnaona mwanamke akiongea labda ni mimi
ni malaya, ...lakini sivyo hivyo, nikuambie ukweli tangu nifike hapa ni
mwanaume mmoja tu aliyeweza kuingia kwenye anga zangu, wengine wote ni washika
pembe..’akasema huku akinishika mkono kunivutia tuingie ndani ya hiyo hoteli,
nikaona nisje kuonekana na watu nikivutana na huyo binti nikakubali, tukaingia
kwenye hiyo hotel, huku akinisimulia mambo yake.
‘Umesema ni mwanaume mmoja tu, uliywahi
kutemba naye tangu ufike hapa, ina maana ni huyo mchumba wako...?’ nikamuuliza
‘Ni kweli ni huyo tu basi, lakini sio kwamba
nilimpenda, hapana, ilitokea tu, kwa vile ni yeye aliyenipokea, akawa ananijali,
nikatumia sana pesa zake, na akawa ni mtu wa karibu sana kwangu kipindi hicho
nilikuwa na matatizo mengi ya familia
nilipotoka, akawa akiniliwaza, na kuanza kunifundisha maisha, yeye ndiye
alinifundisha haya kunywa pombe, nikahisi huyu ndiye mwanaume wa kuishi naye,
lakini siku zilivyozidi kwenda nikagundua kuwa nimepotea maboya, ..’akasema
‘Kwanini?’ nikamuuliza.
‘Huoni, yeye ndiye kaniharibia mpangilio
mnzuri wa maisha,usifikiri haya ninayoyafanya nayapenda, sivyo nilivyokuwa
hivi...nikawa natafuta njia ya kuachana naye, lakini ikawa ngumu, maana wanaume
wengi wanamuogopa..’akasema.
‘Na wale waliopigana kwa ajili yako sio wapenzi
wako?’ nikamuuliza.
‘Wale..hahahaha, kwa ni wale tu, wapo wengi,
wameshawahi kupigana kwa ajili yangu, wote hawo, ni washika pembe tu,
wanajigonga kwangu lakini hakuna hata lepe la upendo kwao, na sijawahi hata
kufikiria kuwa nao kama wapenzi, niliwachukulia kama kaka zangu wa ofisini tu,
lakini kumbe moyoni wameshakwenda mbio, hata walipopigana, nilijiuliza
wanapigania nini,...ujinga wao...’akasema.
‘Na sasa wamerudi kazini, utakuwa ukitembea na
nani kati ya hwo wawili?’ nikamuuliza.
‘Kutembea nani kwenda wapi, chakula cha mchana,..mmh, yoyote
aliyekuwa tayari ilimradi asinibore..lakini
mimi nakutaka wewe tu.’akasema,
‘Lakini mdada mimi nakuomba sana, usinifanyie
hivyo vituko vyako, mimi nakuheshimu sana, na nitafurahi kama tutaishi kama mtu
na kaka yake, sio zaidi ya hapo, tafadhali sana...’nikasema na yeye
akaniangalia halafu akacheka sana na kusema;
‘Wewe ni kaka yangu, mimi sina maingiliano ya
damu na wewe...sikiliza nikuambie kitu, mimi nitakukubalia jambo moja, kuw nitakuwa
mpenzi wako a siri...hakuna atakayejua hilo, ...maana siwezi kukudanganya kuwa
nitakuangalia hivi hivi tu wakati moyo wangu unauma,..usiona nauambia hivi
ukafikiria labda mimi ni mwanamke rahisi,...’akasema huku akijiangalia.
‘Kama unabisha uliza watu, wengi wanafikiria
hivyo, lakini wakinijia wanajikuta sivyo wananavyofikiria, mimi nina msimamo
wangu, na kiukweli ni kwamba nikitaka jambo ni lazima nilipate, kama silitaki
hata ufanye nini hupati kitu kwangu..na kwangu mimi kuongea ni sehemu ya starehe,
ninaweza kuongea, lakini sivyo nilivyo...’akasema.
‘Unataka kusema nini?’ nikamuuliza.
‘Kwamba mimi nakutaka wewe uwe mpenzi wangu
basi...sitaki mwingine,...hilo halina mjadala, na nitajitahidi mchumba wako
asifahamu ilimradi tu utimize yale ninayo yataka,..siwezi kuhangaika moyo wangu
wakati wewe upona nikikamlisha matakwa yangu , ninaweza kusema basi sikutaki
tena,lakini sijui kama nitaweza kuishi bila wewe ...’akasema.
‘Kwahiyo unataka nifanye nini kwako, maana
mimi nimeshakuambia msimamo wangu,...ni ni matwakwa gani hayo unayotaka
kutimiza kwangu...?’nikamwambia wakati huo nilikuwa nakunywa soda.. nakumbuka
kabisa ilifunguliwa mbele yangu, nikanywa fundo la kwanza, la pili nikaanza
kuona macho yakiishiwa nguvu,..
‘Usijali ...wewe kunywa halafu utajua ...ni
lazima uwe mjanja,wenzako walikuwa hivyo hivyo, sasa hivi wapo hapa..’akasema
akiniangalia mchoni n kuonyesha mkono wake huku kipiga piga kiganja chake kwa
mkono wa pili.
‘Mbona....’nikaiangalia ile soda , na Mdada
akacheka, na kusema.
‘Kwisha kazi, leo umepatikana, unajifanya
mjanja eeh,...sasa mchezo unaanza inuka twende huku....washikaji mpo tayari....’akasema
na sikukumbuka, nilichokuwa nikikifanya, nilikuwa kama zezeta fulani, na akili
ilikuwa sio yangu,...nilizindukana kikaili nikiwa juu ya kitanda, nikajaribu
kuinua kichwa, lakini kichwa kilikuwa kizito,..nikatulia na baadaye
nikajitahidi nikainuka, nilikuwa kama nilivyozaliwa..
‘Oh, kumetokea nini?’ nikajiuliza, lakini
hakuna wa kunipa jibu,...nikainuka na kwenda bafuni, niliporudi nilimkuta mdada
akiwa kakaa pembeni ya kitanda, akitabasamu na kusema;
‘Kumbe na wewe wamo eeh,...’akasema huku
akiniangalia kwa macho yaliyojaa dharau
‘Unasema nini?’ nikauliza
‘Sasa umeshaingia kwenye anga zangu, wewe na
mimi ni wapenzi, kuanzia leo hii, sitaki kusikia habari za mchumba wangu au
nani, na utafanya kila ninachkuambia ufanye...’akasema.
‘Una maana gani...?’ nikamuuliza na mara
akawasha simu yake, simu yake ina sehemu inayochukua kitu kama video na unaweza
kumulika ukutani ikaonyesha kama vile unavyoangalia kwenye cinema, na
ikaonyesha picha kubwa tu ....oh, sikuamini.
Kwa haraka nikataka kumnyang’anya ile simu, na
yeye akainuka na kukimbilia nje, n ikabakai nimeduwaa...sikuamini kuwa ni mimi
niliyekuwa nikifanya yale niliyoyaona kwenye simu ya mdada, nilikuwa nafanya
kwa hiari yangu mwenyewe kama ilivyokuwa ikionyesha..aibu tupu..
Nikataka kumnyang’anya ile simu, akakimbia na
kutoka nje, kwa vile bado nilikuwa uchi sikuweza kufukazana naye akasema;
‘Usisumbuke, kila kitu kipo salama, ni wewe
tu...’akasema huku akifunga mlango.
Nikainuka na kuichukua nguo zangu na kutoka
kwenye kile chumba, nilikuwa kama kuku aliyelowana maji, nikatoka hadi nje ya
hiyo hoteli, nikamkuta mdada yupo kwenye pikipiki akiwa ananisubiri, ilikuwa ni
kama saa tatu za usiku.
Sikuongea naye, na yeye alikaa kimiya, hadi
nikamfikisha kwake, na hakutaka hata kuongea nami akaondoka kuingia kwake, na alipofika
mlangoni akawa kama kasahau kitu akarudi na kunishika begani akasema;
‘Usiwe na wasiwasi, mimi nitakulinda kwasababu
na kupenda, imefanyika hivyo kwa vile natakiwa nifanye hivyo, lakini hata
hivyo, haitakuwa mbaya kama utakuwa namimi sambamba,...unasikia...’aaksema na
kunisbusu kwenye shabu, niligeuza kichwa nikamwangalai kwa macho yaliyojaa
chuki, hasira...sijui.
Nikamchukia sana huyo dada, nikamuona kaam sio
yule niliyekwua namfahamu, na kaam ningelikuwa na kitu cha kumfanya kwa wakitu
ule ningemdhuru, nikamwangalia akitembea kuelekea mlangoo wa nyumba yake, na
alipofika mlangoni, akafungua na kugeuka, akaniangalai na kutoa tabasamu lake,
lakini mimi nilikuwa nimekunaj uso wa hasira, hakujali, akaingia ndani.
Nilibalia pale nikiwa nimetulia, nikiwaza sana
halafu nikaondoka kurudi kwangu, nilipofika kwangi , nikaingia chumbani kwangu
na kitandani nikaona bahasha, nilipoifungua nikaona picha za utupu, nikiwa na
huyo mdada, lakini mdada alikuwa kafichwa sura yake ..
‘Ukitaka usalama wako wa ajira yako, na
mchumba wako, fuata na tii kila utakaloambiwa vinginevyo, hizi picha zitafika
kwa baba mkwe wako...’karatasi ikandikwa hivyo,
‘Ina maana mdada ana kundi la watu, au ni nani
kaleta hiyo bahasha humu ndani na picha za tukio ambalo halijamaliza hata siku
moja,na je aliingiaje humu ndani kwangu, wakati ufunguo ninao peke yangu, ....’,
nikajiuliza huku kichwa kikiniuma sana.
Nilijaribu kukiweka maji lakini haikusaidia,
nikawa nahangaika na maumivu ya kichwa nikatafuta dawa za kutuliza maumivu
lakini ikawa kama nimekichokoza, na wakati nahangaika hivi nikakumbuka siku
moja mdada aliniambia;
‘Kichwa huwa kinanuuma sana, lakini nimegundua
dawa yake ni pombe, nikinywa kinatulia....’siku hiyo aliniambia hivyo na mimi nilimkatalia
kabisa kuwa pombe sio dawa ya kichwa, lakini kwa muda huo kwa jinsi kichwa
kilivyokuwa kikiuma nikaona nijaribu hiyo dawa ya mdada, nikatoka kwa haraka
hadi duka la jirani nikanunua pombe, nikarudi nayo ndani nikanywa kidogo,
nikaongeza, ooh, mpaka ikaisha, nikashikwa na usingizi.
Kesho
yake nikaamuka mapema, nikafanya mazoezi kidogo, nikajiandaa na kwenda kazini,
nilipofika nilikwenda moja kwa moja ofisini kwangu na kujaribu kusahau ya jana,
lakini haikuwa kazi rahisi, hadi bosi anafika, nilikuwa nipo kwenye dimbwi la
mawazo na wakati huo kichwa kilishaanza kuniuma
‘Vipi Mosi, upo safi nakuona kama unaumwa?’
akaniuliza
‘Kichwa kinaniuma sana, sijui kuna tatizo
gani?’nikauliza
‘Umekunywa dawa za kutuliza maumivu?’
akaniuliza
‘Ndio lakini haisaidii kitu..’nikasema na yeye
akaniangalia kwa mashaka na kusema;
‘Usije ukawa umekunywa mipombe yao au
wamekuwekea madawa, kuna haya madawa ya
kulevya, wakikuwekea utasumbuka sana, ...inabidi uwe makini sana, hasa
unapokwenda kwenye starehe na watu usio waamini..’akasema na kunifanya niingiwe
na wasiwasi, na kujiuliza kwanini kila linalofanyika anakuwa kama anaelewa,
nikasema;
‘Sizani kama ni pombe...’nikasema na yeye
akasema;
‘Kwa tahadhari, angalia sana, sio kila
atakayekuchekea ni rafiki yako, wengine wana malengo hasi dhidi yako, ....uwe
makini sana, hasa mnapokuwa kwenye makundi, hata kama sio makundi, hao hao
mabinti, marafiki zenu, wanaweza kuwageuka, wakiwa na malengo yao, dunia sasa
hivi imebadilika, mtu yupo tayari kuhatarisha amisha ya mwenzake, ili tu
afanikiwe jambo fulani,....’akasema na mimi nikakumbuka pale nilipokunywa ile
soda, lakini nakumbuka kabisa aliifungau mbele yangu.
‘Haya mimi sina zaidi ,kama kuna tatizo kubwa
linakukwaza niambie, nitakushauri na kuona jinsi gani ya kulitatua, lakini
usije ukadanganyika, ukatishwa kuwa ni lazima ufanya hivi, ndio utafanikiwa, ..usikubali
kama unaona sio sahihi, ...uwe na msimamo thabiti katika maisha yako, usije
ukatumbukizwa kwenye maisha ya utumwa, hasa utumwa wa pombe, utapotea, utaumia...’akaniambia
na mimi nikawa kimiya
‘Basi ngoja nienelee kukuhadithia kisa changu kidogo
, halafu kama bado kichwa kinauma inabidi uende hospitalini..’akaniambia na akaanza
kunihadithia sehemu ya kisa cha maisha yake
*********
Unafahamu mwili wa binadamu una thamani sana,
ukiwa hai, ukishakufa basi tena wewe ni mzoga, watu watauchezea mwili wako
wapendavyo, lakini kama upo hai, mwili wa binadamu,unastahili kulindwa, na
mlindaji ni mlindaji wa huo mwili ni wewe mwenyewe, watu wanatakiwa wajue hivyo...
Sio vyema kabisa, kuuchezea mwili wa mwenzako
ukauzalilisha, labda iwe ni kwasababu ya kitibabu..., hutaamini kuwa mimi nilitakiwa
kuchunguzwa mwili wangu na uchunguzi huo ni wa sehemu za siri.
Ndio nakubali aliyefanya hivyo ni mama yangu mzazi
akishirikiana na mama wa kambo lakini umri ukishapevuka, hata mama yako mzazi
anakuwa na mipaka yake, ndio maana mwanzoni mama yangu alisita kuifanya hiyo
kazi, akifahamu haki za kila mtu hasa katika mwili wa binadamu mwenzako, na
sehemu zenyewe ziwe za siri, ndio maana zinafunikwa...
Ninaona ajabu wale wanaochukua picha za uchi
za wenzao na kuziweka hadharani, kwenye mitandao na vyombo vya jamii, hilo ni
kosa kubwa, huku ni kuzalilishana, na niukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,
lakini hili watu hawalikemei, wanaliona ni la kawaida tu, ...wanakemea na kusuta
wale wanaojifunika mwili mzima eti hao ndio wanaozalilishwa, hao ndio haki zao
za binadamu zinavunja, sio hawo wanaokaa uchi, sio hao wanaweka uchi kwenye
mitandao, hao wanatimiza matamanio ya nafsi zao sio mbaya..ajabu kabisa.
Mama yangu na mama wa kambo wakaanza kazi ya
kunichunguza, nilijiskia vibaya sana, japokuwa mmoja wa waliokuwa walifanya
hivyo ni mama yangu mzazi, lakini moyoni sikupendezewa kabisa, ..hata hivyo
ningefanya nini,..nikaona i bora wafanye wapendavyo,sikuwa na njia nyingina ya
kulipinga hilo, wakafanya kama alivyotaka baba na mama wa kambo. Nia kubwa ni
kutaka kunizalilisha zaidi.
Moyoni nikawa najiuliza ni nani huyo
aliyediriki kuwapigia simu na kuwaambia yote hayo, kuwa mimi nilikuwa nafanya
umalaya hadi kufikia kubeba mimba na kuitoa, ni nani huyu aliyekuwa
akinifuatlia, kwa kwanini alitunga huo wongo, ...sikuwa na uhakika na hilo,
yote hayo nikamuachia mungu,
Walipoanza kazi yao, mimi kimoyo moyo
nikamuomba mungu anisaidie kwani mimi ni kiumbe tu, sikuwa na kosa lolote, na
sikuwa na mwingine angeliweza kuniamini, kwani kwa wakati huo hata mama yangu
mzazi anayenifahamu vyema, asingeliweza kuniamini, kwa jinsi baba na mama wa
kambo walivyolielezea hilo swala, sikuwalaumu.
‘Weka miguu hivi, unajibaragua nini, ukienda
leba kuzaa unafikiri utajiweka hivyo, na mbona ulipokuwa unafanya uhuni wako hukuon
aibu ...’akasema mama mdogo na mama yangu akamwangalia mama huyo kwa macho ya mshangao, akasema;
‘Sio kauli nzuri kwa mtoto, je kama tukukuta
hajafanya hivyo mnavyodai, utakuja kusema nini, ujue wewe ni mzazi kama mimi,
unafikiri kwa akuli hiyo mimi ninajisikia vipi,au ni kwa vile hujamzaa huyu
mtoto ...kumbe ndivyo ulivyokuwa ukiishi watoto wangu huko, ndio maana wakawa
wanajifanyia watakavyo,..’akalalamika mama.
‘Wewe hujui tu nilivyokuwa nikihangaika na hawa
watoto hasa huyu mtoto,ni mjeuri, hanisikii, ...na tabia yake ya uhuni ndio
iliyonifanya nishindwe kukaa naye, muulize hata baba yake kama mimi
ninamsingizia...’akasema mama wa kambo.
Mama akaniangalia machoni, huku machoni
nikihisi anataka kulia, akaniambia;
‘Usijali kama ni kweli tutaona, ....’akasema
na wakaanza kazi yao
Waliponikagua wakagundua kuwa kweli mimi
sijawahi kufanya hayo machafu waliyonisingizia, sijawahi kukutana na mwanaume,
mama wa kambo akabakia kimiya na alishindwa hata na la kuongea, akatoka mle
ndani kwa haraka, utafikiri kamwagiwa maji na mimi nikainuka na kumwangalia
mama , mama akaniangalia machoni, huku akitamani kulia, akanishikilia na
kunikumbatia akasema;
‘Usijali mwanangu nashukuru sana kwa
kunilinda, sijui nikupe nini....mungu mwenyewe ndiye anayefahamu jinsi gani ninavyojisikia
moyoni kwa sasa,..mungu atazidi kukulinda, endelea na msimamo wako huo huo,
usikubali hata siku moja wakudanganye wahuni, umenilinda na kuilinda heshima
yako,...’akasema na mimi sikuwa nimelewa, nikauliza
‘Mama mumegundua nini?’ nikamuuliza
‘Hujaguswa na mwanaume yoyote kama ulivosema,
...’akasema mama
‘Ni kweli mama, mimi nimewaambia alkini hawataki
kuniamini.
‘Usijali ndivyo wanadamu tulivyo, haya jiandao uje tusikie waatsema nini tena...’akasema
mama, akitoka na kuniacha ndani.
Mimi nilimshuku mungu, nikatoka kuwafuata huko
kwenye kikao, na nilipofika nikakuta baba na mama wa kambo wanaongea na
nilimwangalia baba nisikie atasema nini,au ataambiwa nini na mama zangu, lakini
mama wa kambo alichosema ni kuwa anataka waondoke siku hiyo hiyo kurudi mjini;
‘Tuondoke zetu, kuna kazi nimekumbuka ni ya
muhimu sana, nisipoifanya leo nitakosa pesa zangu, mimi silali hapa ..’akamwambia
baba na baba akawa kaduwaa, mama ndiye akasema;
‘Mume wetu anasubiri taarifa ya uchunguzi wetu
dhidi ya mtoto, mwambie ukweli umegundua nini...’mama yangu akasema.
‘Kwani wewe huna mdomo wa kumwambia,....’akasema
mama wa kambo akibenua mdomo kwa dharau.
‘Ndugu zanguni, shutuma zenu dhidi ya mtoto
sio kweli, binti yetu hajawahi kuguswa na mwanaume, bado ana usichaan wake...’akasema
mama
‘Una uhakika na unalolisema?’ akauliza baba
akiwa kaduwaa kwa mshangao, akageuka kumwangalia mke wake, yaani mama wa kambo,
na mama wa kambo akawa anajifanya kutafuta kitu kwenye mkoba wake, na mama
akasema;
.
‘Ndio hivyo muulize mke mwenzangu, naona
mlidanganywa na watu wasiompenda mtoto wetu,na ni makosa makubwa mliyoyafanya
kwani mlisikia taarifa na hamkuhangaika kuhakikisha ukweli wa hizo taarifa, na
baya zaidi mkakimbilia kumfukuza mtoto shule..’akasema mama.
‘Nimekuamba tuondoke bwana, kama haupo tayari
mimi naondoka..’akasema mama wa kambo, akianza kutoka nje, na baba akawa kimiya
akiogopa hata kuniangalai machoni. Mama akasema;
‘Lakini hatujamalizana na kikao, nyie ndio
mlikiitisha, na uchunguzi tumeshaufanya ni bora tulete taarifa na ukweli uwe
wazi, kwani ni kosa limefanyika, la kumshutumu mtu ambaye hajafanya hilo kosa,
kama wazazi inabidi tuseme ukweli kuwa tumekosea, ili binti naye moyo wake
ufurahi...’akasema mama yangu.
‘Unasema nini, unataka mimi nimuombe mtoto
msamaha, ...hapana, na sina uhakika na huo uchunguzi wenu, bado nitalifanyia
kazi ..’akasema baba akijiandaa kuondoka. Na mama akasema;
‘Mnajisumbua bure, na ipo siku mungu
atawaumbua, huo sio ulezi bora kwa watoto, leeni watoto wote sawa, mkijua kuwa
wote ni wazazi, na mtoto huyu ni damu yenu, kwanini mnagawa matumbo yenu ,kwa
ubaguzi...haya sasa ukweli mumeuona mnataka nini zaidi...’akasema mama.
Mimi
nilijua sasa wazazi wangu wataniamini na yale maneno ya kashifa yataisha,
lakini sijui mimi nilizaliwa na mkosa gani, na tukio hilo lilikuwa kama
limewazazlilisha wao, wakawa sasa kama wanataka kulipiza kisasi, kwani hali
haikuwa na mabadiliko kwani baba walipoondoka kesho yake nikaagizwa nirudi huko
mjini, nikasaidie kazi za nyumbani.
‘Mama unakubali niende tena huko?’ nikamuuliza
mama.
‘Baba yako kasema hivyo, kasema wewe ni mtoto
wake, inabidi umtii, nafikiri sasa hivi watakutahamini kwani wamegundua kuwa
wewe huna tabia kama waliyoisema wao..’akasema mama.
Basi mimi nikakubali kwa shingo upande
nikaenda huko mjini, na nilipofika nilikuta mateso yakiwa pale pale kila siku kunazuka
jipya, na mimi ndiye mkosaji,mimi ndiyeo muongo ,mie ndio malaya,nilishangaa
hiyo kauli ya kuitwa malaya bado walikuwa nayo mdomoni, hadi pale nyumbani
wakahisi kuwa huenda kweli mimi ni tabia yangu, kuwa mimi ni malaya, kwani baba
kila akiniita alikuwa haniiti kwa jina langu akawa ananiita kwa kusema;
`Wewe
malaya njoo hapa‘
Jina hilo lilinikera sana, ...umalaya huo
nimeufanya lini, hadi kupewa jina baya kama hilo ila baba yangu hakuweza kuwa
na aibu na kuendelea kuniita hivyo, `we malaya fanya hivi , wewe malaya ulienda
kwa mabwana zako,... ‘
Jinsi,maisha yalivyoenda na mateso ndio
yalivyo zidi .kuzalilika, kupuuzwa na
hata kumsema mama yangu kuwa ndiye aliyenilea hivyo vibaya ndio maana mimi ni
mvivu, malaya, sina adabu, kitu ambacho sio kweli, niliumia sana, lakini sikuwa
na la kufanya.
Siku moja ilikuwa ni jumapili, kukatokea
kupotea kwa vifaa, kama ilivyo kawaida shutuma hizo zikapelekwa kwangu, baba
alikuwa amekasirika kweli, aliposikia kuwa etu ni mimi nimefanya hivyo, ikawa
ni sababu ya kumalizia hasira zake, alizokuwa kaziweka moyoni, akachukuwa waya
wa pazia na kuanza kunitandika nao, ...
Kwakweli siku hiyo niliumia sana, sio kimwili
zaidi, lakini moyoni, nikawa na uhakika kuwa sio mimi niliyefanay hilo kosa,
ila ni uzembe wa wenzangu, na wao kwa umoja wao wakanisingizia mimi,
nikajiuliza hivi mimi nina tahamni gani kwa ahwa watu
Hapo nikawa sina jinsi, akili ikawa imechoka,
nikaona sina amani, sina thamani, naona sihitajiki tena hapa duniani, nikaingia
ndani, kulikuwa na vidonge vya pritoni vilikuwepo kwangu vilinunuliwa kwa ajili
ya mafua, nikaingia kwa mama, nikaona vipo vingine, nikaona havitoshi nikaenda
dukani nikaongezea, hadi vikafika vidonge 30, nikaona sasa hivyo vibatosha.
Nilirudi chumbani kwangu, nikaona niandike
ujumbe, nikaona haina haja, mwili wangu utakuwa ujumbe, nilishachoka
nilishafikia maamuzi ya kujiua, sikuwa an njia nyingine, nikamuomba mungu
anisamehe kwa kosa hilo, kwani nimevumilia nimechoka, nikavichukau vile vidonge
na maji nikavimeza, na kulala kutandani, .
NB: Mpendwa kachoka na maisha kaamua kujiua, je itakuwaje..
WAZO LA LEO: Sote ni wanadamu na sisi sote ni watoto wa Adamu na Hawa,
kwahiyo sote ni ndugu wa baba na mama mmoja, ni kwanini tuchukiane, ni kwanini
kuwe na sababu za kubaguana, na kuona huyu sio mtoto wangu, huyu sio ndugu
yangu, huyu sio mwenzetu, ...hayo yametoka wapi, ina maana unaposema hivyo wewe
sio mtoto wa Adamu, ...tupendane, ili dunia iwe kisiwa cha amani.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment