Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, July 1, 2013

WEMA HAUZO-27


Kumbe aliyeniokoa alikuwa mtoto wangu…..’akaendelea kuongea mama kuhusiana na kisa chake.
‘Mtoto wako, ina maana ni mimi mama, mbona nimesahau?’ nikamuuliza mama na yeye akachekea huku akiendelea kunisimulia kisa cha maisha yake….

*******

Kipindi mazungumzo yanaendelea kumbe mtoto hakuwa na amani, akaingiwa na wasiwasi kuwa huenda hawo watu waliopo ndani wanaweza wakamdhuru mama yake,…, akawa anacheza karibu karibu na mlango,hakuenda mbali, kama nilivyotarajiwa, alikuwa akichezea kigari chake alichopew na baba yake mkubwa pembeni ya mlango, huku akiangalia kwa ndani kwenye upenyo wa mlango, kuhakikisha kuwa mama yake hadhuriki...

Na aliposikia sauti za ukali kutoka kwa baba yake mkubwa, akahisi hatari akafungua mlango kidogo,na kuchungulia ndani, na hapo ndipo akaona baba yake mkubwa akiwa anamkaba mama yake. Japokuwa alikuwa mtoto, hakuweza kuvumilia, akaona ni lazima afanye lolote, kumuokoa mama yake, akageuka nyuma,… na bahati nzuri akamuona huyo mtu akipita barabarani, wazo la haraka, likamjia alichofanya ni kumkimbilia na kumweleza ni ni kinachotokea huyo mpita njia.

Kiukweli huyo mtu alikuwa na safari zake lakini mara kwa mara alipendelea kupita kwa huyo mama na kumsalimia kumjulia hali,….lakini leo alikuwa kikazi zaidi, alikuwa katumwa na ofisi, hakutaka kupoteza muda, sasa kasikia kuna tatizo kwenye hiyo nyumba, ikabidi kwa haraka , kutokana na kauli ya mtoto aingie ndani ya hiyo nyumba, kuona kuna nini, …..

Akafika kwenye mlango wa hiyo nyumba, na akagonga mlango mara moja , na mara pili akawa keshaingia ndani, hakusubiri kukaribishwa.Aliogopa asichelewe na kukuta mtu keshaumizwa au kuuwawa…

‘Kuna tatizo gani humu ndani ….’Akatoa sauti kali ya kiaskari, na suati ile iliwashitua wote waliokuwmo humo ndani,…sauti hiyo  ikamzindua shemeji ambaye kwa hasira zake hakujua kile kitendo alichokuwa kikifanya kuwa kingeliweza kumtoa mtu roho, alikuwa kanishikilia shingoni kwa nguvu, na hata sauti ilikuwa haiwezi kunitoka, ulimi ulishaanza kunitoka, na macho yakwa ynanitoka kwa woga, hata pale nilipojaribu kuutoa mkono wake sikuweza kufanya hivyo, nahisi ndipo wakati kisu kiliponyoka.

Shemeji mdogo, ambaye alikuwa kashikwa na butwaa, pale kaka yake alipoanza kuonyesha dalili za hasira, hakuweza hata kuinua mkono kumshika kaka yake, lakini hatua aliyoiona kwa muda ule , akamsogelea kaka yake na kumshika mgongoni, na kaka yake alipoguswa tu, na huo mkono bila kugeuka, akageuza mkono wake, huo ulikuwa huru,na kwa nguvu moja akamsukuma mdogo wake, na  kwa vile mdogo wake hakujiandaa na huo msukumo, akajikuta akiserereka hadi sakafauni na ni muda huo huo, ndipo mlango ukafunguliwa na aliyeingia kumbe alikuwa ni askari akiwa kavalia kiraia.

‘Hakuna tatizo afande….’alisema shemaji mdogo,akijizoa zoa skafuni, na kaka yake, aligeuza kichwa kwa haraka kutizama ni nani aliyeingia, na alipooona ni nani, akamwachia shemeji yake na kujifanya kama vile alikuwa akimshika shika shameji yake shingoni.

‘Oh, afande hakuna tatizo, nilikuwa nafanya mzaha na shemeji yangu hapa….’akasema na mimi ndio nikapata muda wa kupumua, na kikohozi kikanishika, nikakohoa mfulululizo….mwili mzima ulikuwa hauna nguvu,nikajikuta nikikaa chini bila kupenda.

‘Unafanya mzaha na shemji yako, huo mzaha gani wa kumkaba mtu hadi anakosa hewa,…kumbe ni kweli eeh,…sasa upo chini ya ulinzi, kwanza kwa kuhusika na mauaji yanayoendelea hapa kijijini,…nilikuwa njiani kuelekea kwako, sikujua kuwa nitakukuta hapa, na pili, kwa kutaka kudhuru….’akasema huyo askari, akitoa pingu tayari kwa kumfunga shemeji mkubwa, hapo moyo wa huruma ukanijia.

‘Afa—fa-nde, hakuna shida…’nikasema na nikamgndua yule askari, ambaye alinitupia jicho mara moja,akasema.

‘Hakuna shida eeh, unafikiri kama nisingelifika mapema hapa ungelikuwa wapi wewe…, kweli najua hakuna shida,….mimi sio mjinga kihivyo, natimiza wajibu wangu kisheria…hata kama hamtatoa ushirikiano…’akasema  huku akimshika huyo jamaa mikono kwa nyuma.

‘Nyie wanawake mtauliwa majumbani kwenu kwasababu ya ujinga wenu, hili nimelishuhudia mwenyewe, kwa macho yangu, kama sitafanya jambo, hali hii inaweza ikaleta madhara kwenye hiki kijiji, ni lazima tatizo hili likome kabisa hapa kijijini…’akasema huku akimfunga pingu shemeji mkubwa ambaye alionekana kutahayari, hakuleta ubishi, akatulia hadi pingu zikafungwa mikononi.

‘Afande, umeingia nyumbani kwa mtu, bila hodi, na kumshika mtu bila kosa, huoni kuwa unakiuka sheria?’ akasema shemeji mdogo.

‘Na wewe mwanasheria unatetea uhalifu, hivi kweli hapa nimekiuak sheria, unadiriki kutoa kauli hii wakti umeona fika, kuna mtu alitaka kudhuriwa…?’ akauliza.

‘Afande hizi hasira tu za kujibishana maneno, hakukuwa na lengo baya….’akasema huyo mwanasheria.

‘Hivi wewe kweli unfahamu sheria vyema, wewe ndiye kijana wetu tulitegemea tushirikiane kuondoa huu uchafu unaoendelea hapa kijijini, wewe unaufumbia macho, ulikuwa kimiya wakati kaka yako…..’akasema .

‘Hapana afande, wakati unaingia ndio nilikuwa najaribu kusuluhisha,…’akasema.

‘Ahaa..kumbe unafahamu hilo, kuwa kaka yako alikuwa  anataka kumdhuru mtu, hebu niambie….na pili heni niambie kwanini ulikuwa umedondoka sakafuni, kama sio ulikuwa ukijaribu kumtetea huyo shemeji yako mhalifu…na ilionekana kushindwa kufanya lolote, je kama nisingelifiak mapema, ingelitokea nini, au kwa vile huna uchungu na huyo mwanamke…’akasema.

‘Wewe kijana wakati umefika wa kulikomesha hili tatizo hapa kijijini. Mimi ni askari, na bahati nzuri nimezaliwa hapa kijijini, huwezi kunidanganya kitu…kama wewe umedanganyika na familia yako, iendelee kuharibu amani ya hiki kijiji, mimi sijadanganyika….’akasema huku akimwelekeza shemeji mkubwa kutoka.

‘Twende kituoni, bwana mzee, mimi natimiza wajibu wangu, sitaweza kuvumilia hii hali…’akasema na wakaanza kutoka nje.

‘Na wewe mdogo mtu, kama unataka kuja kumtetea kaka yako fika kituoni, na nakutahadharisha ufuate sheria, maana kaka yako huyu kakalia kuti kavu…ana kesi nyingi za ubabe wake, sijui kama sfari hii ataokoka….’akasema wakiwa wameshatoka nje, hapo shemeji mdogo,  akaniangalia kwa macho yaliyojaa huruma na kusema;

‘Shemeji pole sana, ngoja niwafuate hawa watu, maana hili sasa limekuwa ni tatizo, sijui kwanini kaka yangu anashindwa kuhimili hasira zake…’akasema.

‘Sasa hivi ndio unaongea, wakati kaka yako alikuwa karibu kunitoa roho,anataka kuniua huku wewe umetulia,hukuweza kabisa kufanya lolote, na…’nikasema.

‘Shemeji, shemeji…nilijitahidi kukusaidia, lakini namfahamu sana kaka yangu, akikasirika, hashikiki….nakuomba shemeji ukiulizwa useme hakukuwa na tatizo lolote…ili umuokoe kaka, huyo ni shemeji yako, baba mkubwa wa mtoto wako…..nakuhakikihishia tutayamaliza haya yote kwa amani kifamilia...’akasema.

‘Unasema nidanganye kuwa kulikuwa hakuna tatizo...kweli kulikuwa hakuna tatizo, tusidanganyane, najua damu ni nzito kuliko maji,....wewe mwenyewe ulijionea ni nini kama yako alitaka kukifanya, je angeniua ungelikuja kusema nini….na wewe mwanzoni ulijadi kuwa umeachiwa hii familia kuilinda, ndio kuilinda hi familai kwa namna hiyo…..sikuelewi kabisa, ngoja  huyo kaka yako akafundishwe adabu….’nikasema.

Na yeye akaniangalia kwa macho ya kushangaa, na haraka akageuka na kutoka nje, na alipotoka tu, mtoto wangu akanikimbilia na kunikumbatia akisema;

‘Pole mama, ….nilimuona huyu mtu, kumbe ni askari nikamwambia kuwa baba mkubwa  anataka kumuua mama, …’akasema huku akihema kama vile alikuwa anakimbia.

‘Ahsante sana mwanangu, umefanya jambo la maana….’nikasema.

‘Mama  kwanini baba mkubwa alitaka kukuua…..?’ akauliza huku akiwa kalishikilia gari lake mkononi.

‘Hakuwa anataka kuniua, …..aliku-wa-ameka-ka-sirika tu,…..’nikasema huku nikishika shika shingo yangu kuhakikisha mfupa wa shingo haujavunjika maana ilikuwa kama komeo la chuma lilikuwa limeshika shingoni mwangu, hata kisu kilivyonidondoka mkononi, sikuweza kutambua.

‘Mama kwanini baba mkubwa ni mkali sana….?’ Maswali ya mtoto yakaendelea.

‘Kwasababu ni baba mkubwa, …hataki kuchezewa…’nikamjibu huku nikiwaza tukio zima,niliwaza mengi, hasa ya huyu shemeji mkubwa ambaye alishakamatwa na polisi, nikajiuliza je kama nitaitwa huko mahakamani kwa ajili yake nitasema nini,……je nikubali kuwa huyo jamaa alitaka kunidhuru, ili akapambane na mkono wa sheria, au nikatae na kusema ….

Kama nitasema ukweli, jamii na familia nzima itanisakama na kuniona sina ubinadamu, hakuna atakayekumbuka kuwa huyo jamaa angeniua kama isingelikuwa huyo askari kuja kwa wakati, muafaka. Najua hata semeji mdogo alishaanza kunishawisi nikatae kuwa huyo jamaa hakuwa na lengo baya kwangu. Nikamwangalia mwanangu akiwa anachezea kigari chake alichopewa na baba yake huyo mkubwa na hapo nikasikia maneno yake akiongea na mtoto wangu;

‘Haya chukua zawadi yako hii, kachezee, hizi ndio zawadi za kuchezea, usichezee uchafu, unanisikia eeh, mtoto mnzuri, mimi ni nani….’

Lakini wakati namuhurumia huyo shemeji yangu, nikakumbuka maneno ya huyo polisi , siku moja tulipokuwa tukiongea nay eye. Huyo askari polisi ni mmoja wa wazaliwa wa hapo kijijini siku moja nilikutana naye akaniambia anasikitishwa na uvunjifu wa amani hapo kijijini, na yeye akaapa kuwa atafanya kila awezavyo kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinakuwepo hapo kijijini.

‘Tatizo kubwa ni wanakijiji wenyewe…..’akasema.

‘Kwanini unasema hivyo…?’ nikamuuliza.

‘Unauliza kwanini, wakati nyie wenyewe mnafahamu fika kuwa mnayo nyoka ndani, lakini hamshirikiani kumuua,….na nyoka huyo ana sumu kali. ….’akasema kwa mafumbo.

‘Ndio hali ilivyo, unajua  wengi wanaogopa kuwa wakubwa wanalindwa, ukiongea tu, unaweza ukajikuta wewe mwenyewe uliyejitolea kuongea ukweli  unaingia matatani…’nikasema.

‘Hakuna cha kulindwa wala nini, ni uwoga wenu na uzumbuekuku wa wanakijiji wenyewe, amukeni mtetee haki zenu, amkeni, muwafichue watu wahalifu ili hata kama utaonekana mbaya, lakini familia zenu zije kuishi kwa amani…..’akasema.

‘Tatizo na nyie maaskari, mnatusaliti, tunaweza tukajitolea na kuja kuwaelezea kuwa mtu fulani ni mvunja amani, lakini nyie badala ya kumshughulikia  yeye, mnakwenda kuongea naye, mnaelewana, na huyo aliyejitolea anageuziwa kibao…’nikasema.

‘Sio kweli….kama mna umoja wa dhati, na mpo pamoja kuwafichua wahalifu,hilo halitawezekana, maana sisi ni watendaji tu, ….nyie ndio washika dau, mkitaka kuwe hivi au vile mnaweza, lakini muwe kitu kimoja, na muhakikishe mnasimamia kwenye haki na kweli, tatizo ni kuwa nyie wenyewe mumejigawa mapande mapande….’akasema.

‘Hilo ni kweli, kuna ukoo mashuhuri, kuna watu mashuhuri, …..na wengi wanaangaliwa kutokana na hali za kipato chao, cheo chao….na..na, . Mwenyewe unajua toka lini maskini akawa na haki ..’nikasema.

‘Huo pia ni unyonge wa kujitakia, haki haina cha umasikini au utajiri…kukitokea kuonewa kwa masikini kutetewe sawa kama kwa tajiri , halikadhalika, tatizo likitokea kwa watu mashuhuri, litetewe sawa sawa na wale wasio masuhuri, mkikubali kujigawa kwa makundi ya namna hiyo, mkawa mapande mapande kwa hali za kimaisha, itikadi za imani, itikadi za kikabia, ukoo….katika kutetea haki basi dhuluma inapenyeza makucha yake, na hali kama hiyo inajenga uhasama na chuki, na baadhi ya watu kuona kuwa wao wanaonewa….’akasema.

‘Ni kweli afande, sasa wewe utatusaidiaje?’ nikamuuliza.

‘Kwanza mjisaidie wenyewe…mimi sitaweza kuwasaidia kama nyie wenyewe hamtaweza kujisaidia, mimi kama mlinda amani, nikiona kuna tatizo ,nitatimiza wajibu wangu na kuwafikisa wausika kwenye vyombo stahiki, lakini mwisho wa siku, lazima sheria za kimahakama zihakiki kosa hilo, na ili ijulikane kuwa ni lazima waite mashahidi walioshuhidia, au wanaofahamu uhalifu wa huyo mtu kama mashahidi….je kwa mfano kama wewe limetokea tatizo eneo lenu, upo tayari kusimama kizambani na kutoa ushahidi wa uhalifu, hata kama uhalafu huo kautenda ndugu yako…ukoo wako, mtu wa imani yako?’ akaniulizwa.

‘Kama ni muhalfu kweli nitasimama na kusema ilivyokuwa…maana nikificha uhalafu mwisho wa siku ninaweza na mimi nikakutana na janga kama hilo….’nikasema.

‘Wewe unasema tu kwasababu tunaongea, lakini mimi naifahamu vyema jamii yetu hii ninayoishi nayo, wakinamama kila siku wanapigwa, wanaumizwa, lakini kesi ikipelekwa mahakamani, utasikia watu wamekwenda kwa hakimu na kumuomba kuwa kesi hiyo ikaongelewe nyumbani, na ikifikia hapo, ujue, wameshaitana pembeni, na mwanamke aliyeumiza kahadaiwa, au katishiwa, ….basi tena, yule askari aliyewajibika kusaidia kumkata huyo mhalifu anaonekana mnoko, mtu  mbaya. Hapo unafikiria nini….?’ Akauliza.

‘Ni huruma, na ujinga…’nikasema.

‘Sio huruma, …ni hivyo unavyoita kuwa ni ujinga, maana huyo aliyevunja amani, akamuiza, atakuwa haogopi kutenda hilo kosa tena, na wengine hawatajifunza,…. ndio maana unaona uvunjifu wa amani, unaongezeka kila siku, …..sababu kubwa ni kutokutimiza wajibu wenu kama raia,…..raia mwema anatakiwa kusirikiana na vyombo vya usalama, …kama nyie hamtoi msaada wa kufichua uhalifu, sisi kama watendaji tutafanyaje…..nakubali kuwa na sisi pia kuna wenye udhaifu, wakiona hivyo wanatumia usemi usemao mwenye kisu kikali ndiye mla nyama…..eeh, ..ndio maisha tumeyachagua wenyewe, …tusilaumiane kwa hilo….’akasema.

‘Nimekuelewa afande, mimi ninakuahidi kuwa likitokea tatizo kwangu, nitakuwa nawe bega kwa bega, kuhakikisha sheri inafuata mkondo wake, maana nisipoziba ufa nitakuja kujenga ukuta kwangu kwa gharama kubwa sana….nipo na wewe afande…’nikasema.

‘Sisi tupo, ahadi kama hizo tumezisikia sana…na watu kama sisi ambao tumeamua kujiunga na kazi hii kwa moyo mmoja, hatutavunjika moyo, hata kama nyie raia mtashindwa kushirikiana na sisi….mimi nikiona uhalafu nitaufanyia kazi, wewe raia ukisindwa kutimiza wajibu, ni shauri lako, ….maana kuna leo na kesho, usije ukalalamika siku maji yakikufika shingoni…..’akasema .

‘Nashukuru sana afande, tunahitajia watu kama nyie….’nikasema na kuagana na huyo afande.

Haya, leo hii huyo afande kajitolea kumnasa huyu jamaa, shemeji mkubwa, kiongozi wa familia ya marehemu mume wangu, ambaye alitaka kunitoa roho….je nikae kimiya, nimsaliti huyu askari polisi, au niwe pamoja na wanajamii…?’ nikajiuliza huku nimeshika kwa mawazo.

Mara mlango ukagongwa, na sauti ya shemeji mdogo, ikasikika, nikajua sasa mambo yameiva ninaitwa kutoa ushahidi, au hunda kaja kunibembeleza ili nisikubali hayo yaliyotokea, ….nikafungua mlango, na nikajikuta nikiwa nimesimama mbele ya kundi la wazee, wakiwa wameongozana na huyo shemeji mdogo, akiwemo na mjumbe

‘Mbona ugeni wa ghafla….?’ Nikauliza.

‘Wazee hawa wamekuja kwa ombi moja, …kaka yangu yupo matatani, na wewe peke yako ndiye utakayeweza kumsaidia, tafadhali shemeji, tupo chini ya miguu yako….’wakasema na kwa mbali nikamuona baba wa kufikia akija kuelekea hapo nyumbani huku akichechemea na bakora, kuashiria madhara aliyoyapata kutokana na hawa hawa watu. 

Je nitafanyaje…

NB: Kwa leo naishia hapa ngoja nikajiandae kumpokea Raisi wa Marekani, Baraka Obama japo kwa kuteseka kwenye foleni za daladala, maana ….kufa kufaana, na mgeni aje mwenye afanye nini vile..?.


WAZO LA LEO: Uvunjifu wa amani, ukiukaji wa sheria, yote haya yanafanyika katika maeneo yetu, iwe majumbani, mitaani hata maofisini, na wanaotenda hivyo tupo nao, na tunawafahamu, na tunawalinda, tunasahau kuwa watu kama hao ni kama kufuga nyoka mwenye sumu, ipo siku anaweza kuja kukuzauru wewe mwenyewe. Teteeni haki kwa kufichua maovu, bila ubaguzi, kwani kila mtu anawajibika kuwa mlinzi wa taifa letu ili liwe la amani, upendo , mshikamano na utulivu.

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Unknown said...

Muache akaonje joto ya jiwe wala usimuonee huruma nyoka huyu, kuwa na msimamo ktk maisha yako.

Unknown said...

Hata wahi kaka sisi engine tutasikia tu, huyo dada aseme ukweli asiogope kutetea haki yake.

Unknown said...

Hata wahi kaka sisi engine tutasikia tu, huyo dada aseme ukweli asiogope kutetea haki yake.

Unknown said...

Mpe hii Obama, mgeni krbu mwenyeji apone lkn tutapona kweli!!!

Anonymous said...

Mhhh, ndugu yangu Nancy, jana na juzi, dada, leo kaka M3...mmh, kweli mwandihsi hana jinsia, M3, unakubali kuwa kaka au dada? tehetehe...

Ama kwa uhakika, tuwe wakweli, maana nijuavyo mimi, wanawake, ni wepesi sana kusamehe, huenda akasamahe, ngoja tuone kwenye sehemu ijayo.
`kaka au dada m3, tupo uhondo'

emuthree said...

NAWASHUKURUNI SANA WAPENDWA, KUNIUNGA MKONO, INANIPA FARAJA NIKIJUA NIPO NA WATU, HATA JAPO KIMIYAKIMIYA, MIMI NASEMA TUPO PAMOJA, TUKIMSUBIRI OBAMA.

Best @mwajuma, ndugu yangu @ Nancy,na nani vile @ Anony. Tupo pamoja wapendwa.

Unknown said...

Jamani @ anonymous, unajua me ckujua huyu mtu anayetupa raha na mafundisho ni jinsia gani mn niliona km Miriam kuja kufwatilia kumbe nakosea ni mira3 nsameheeni jamani km bdo nakosea na pia mnijulishe ni kaka au dada,mana ni ndugu yangu huyu.

Unknown said...

Jamani @ anonymous, unajua me ckujua huyu mtu anayetupa raha na mafundisho ni jinsia gani mn niliona km Miriam kuja kufwatilia kumbe nakosea ni mira3 nsameheeni jamani km bdo nakosea na pia mnijulishe ni kaka au dada,mana ni ndugu yangu huyu.

Unknown said...

Mnijulishe nsizidi kukosea jamani