Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, February 15, 2013

Uchungu wa Mwana aujuaye ni mzazi-62
Malikia wa Mererani, alikuwa kasimama mbele ya askari, na hakuonyesha dalili yoyote ya kuogopa, huku akiwa ameshika kiuni, akauliza kwa ukali;

‘Haya niambieni mumeniitia nini hapa?’ akauliza.

‘Tumekuita hapa kwa kukuhoji ,kuna tatizo lilitokea kwa yuke mzee wenu mgonjwa…inasadikiwa kuwa kuna mtu kamuwekea sumu kwenye maji, sasa tunajaribu kuwahoji wanafamilia, na wewe ukiwa mmojawapo,’akasema yule askari.

‘Hivi nyie mnajua kazi yenu kweli, mimi ni mtu wa kuhojiwa na vitu vidogo vidogo kama hivyo, nani amuwekee yule mzee sumu, mtu mwenyewe anaelekea kuzimu, ina haja gani ya kumuwekea sumu…halafu mnasema `inasadakiwa’, kwahiyo hamjafanya uchunguzi wa kina, basi, fanyeni uchunguzi, mkikamilika ndio mniite kunihoji, na naomba msinipotezee muda wangu kwa vitu vya kijinga kama hivyo,….’akasema huku akiondoka.

‘Ina maana unakaidi amri ya usalama, sisi hatujakuruhusu, tumekuita kwa sababu tunahitaji maelezo yako, na sio wewe tu tuliyekuita, kuna wengi akiwemo yule dada pale…..’akasema huyo askari akielekeza kidole kwa dada mmoja aliyekuwa kaka kwenye benchi,…

Kwanza Malikia hakujali kuangalia ni dada gani, lakini alipoona yule askari anatupa jicho mara kwa mara kwa huyo dada, akageuka kuangalia kuwa ni nani huyo mwanadada. Alipotupa jicho la haraka, akajikuta aksihituka, akageuka mzima mzima kuangalia pale alipokaa huyo mwanadada.

‘Na huyu naye ni mwanafamilia,….?’ Akauliza kwa mashaka.

‘Alikuwepo kwenye tukio….’akasema huyo askari.

‘Ahaa…safi kabisa,….manona wenyewe, kumbe mna mhalfu mkononi mwenu,..halafu mnapoteza muda kwa mtu ambaye hahusiki..mnanipotezea mjuda wangu.

‘Ni wajibu wetu kumhoji kila mtu…kwahiyo tunaomba utulie, ili tuweze kuchukua maelezo yako,hatutachukua muda wako mwingi…’akasema huyo askari huku akiendelea kutupa macho kwa yule mwanadada aliyekaa kwenye benchi.

‘Kwanza mimi nina wakili wangu, siwezi kuhojiwa mpaka akiwepo….’kabla hajamaliza, akafika askari mwingine, na kusema;

‘Achaneni na dada…mzee kasema hana hatia, watayamaliza wenyewe huko nyumbani, anasema hiyo kesi ifutwe kabisa, na walioshikiliwa wote waachiwe…’akasema huyo askari, na Malikia akasonya na kugeuka kuondoka.

Alipotoka pale akapitia pale alipokaa yule mwanadada, akampita bila kumwangalia, lakini akilini mwake, alikuwa na donge, akitaka kumsemesha , lakini aliona kuwa akiongea naye, anaweza akapandisha hasira, na huenda huyo mwanadada akapandisha….akaona atoke akamsubiri huko nje.

‘Mimi siku ya kumweka huyu binti humu ndani, nitahakikisha hatanisahau, maana amejaa zarau, utafikiri ni mke wa waziri, au mtu mkubwa serekilaini, lakini kumbe ni kimwanamke cha hapa hapa….hivi kwanini anajiamini kiasi hicho?’ akauliza askari mmojawapo.

‘Achana naye huyo,  dawa yake inachemka, ipo siku yake, tunamfuatilia kwa karibu…mambo yake na kundi lake yapo karibu kukamilika…’akasema huyo askari aliyeleta taarifa kuwa malikia aruhusiwe kuondoka hana hatia.

*************
Maua ambaye kwa muda ule alikuwa hapo polisi, kama walivyoamriwa na watu wa usalama, na baadaye na yeye akaambiwa yupo huru anaweza kuondoka,…akatoka nje, na alipofika nje, akakutana na gari la malikia likitaka kuondoka, na Malikia alikuwa akiangalia mlangoni jinsi anavyotoka huku akiwa anasikiliza simu, na gari likiwa linaguruma kuonyesha kuwa anataka kuondoka , na alipomaliza kuongea na simu, akashusha kiyoo cha gari lake na kumwangalia Maua kwa dharau;

‘Wewe mwanamke…hivi niliwaambia nini…sasa sikiliza, unaona umefika hapa kituoni, kwa kosa ambalo hujalifanya, sasa utafika kwa kosa ambalo…, hutaweza kuondoka hapo, ulishawahi kufungwa jela wewe..sasa utafungwa jela kwa wizi au kwa kuua…’akasema malikia.

‘Mimi sijakuelewa, kwani unataka nini kwangu?’ akauliza Malikia akimwangalia yule mwanadada.

‘Nataka uondoke hapa Arusha,….hutakiwi hapa, unanuksi wewe….’akasema Malikia.

‘Kwasababu gani unasema hivyo…., kwani tumekuzuia nini na mambo yako?’ akauliza Maua.

‘Sikiliza….hilo ninalokuambia ni kwa manufaa yako…ondokeni hapa mjini, na rudini huko mlipotoka,….sitawasemesha tena, …kwani mtakuja kuumbuka vibaya sana, na nilishakuambia nenda katoe hiyo mimba, kama kweli una mimba…..itoeni haraka kabla haijakuwa kubwa…’akasema huku akiangalia eneo la tumbo la Maua

‘Kwani hii mimba inakuhusu nini?’ akauliza Maua.

‘Hainihusu ndio….lakini inavuruga mambo yangu, na pili, nawasikitikia kwa vile nyie ni watu wa kijijini kwangu, nisingelipenda mje kuadhirika, unakumbuka nilishakuonyesha pete ya uchumba, sasa itakuwa ni aibu, unaumbuliwa kwa kuiba mume wa mtu ….itakuwa ni aibu kwako na familia yenu,..nawajali sana, ondokeni na wahini kuitoa hiyo mimba  mapema iwezekanavyo….kama hutanisikiliza mimi, basi ipo siku utanikumbuka..’akasema.

‘Mimba haitatolewa na sitaondoka hapa mjini,…nitaondoka kwa muda wangu…’akasema Maua na kuanza kutembea kuondoka.

‘Wewe utaondoka tu, hilo nakuhakikishia…’akasema Malikia na kuondoa gari lake haraka.

***********
‘Rafiki yangu, nashukuru sana, umefanya kazi moja kubwa sana……’akasema mzee huku akionyesha kupona kabisa.

‘Kazi gani hiyo..?’ akauliza huyo rafiki yake, akishangaa, kwani kwa taarifa alizozipata awali ni kuwa huyo rafiki yake ni mgonjwa sana, na anakumbuka alifika mara moja, na kumkuta akipumulia mashine, sasa anamuona akiwa na afya yake, utafikiri sio yeye aliyekuwa akiumwa.

‘Ohh, yaani ile ndio dawa…hutaamini, kwani nilipomuona tu, mwili wote ukarejeshewa nguvu zake, na hata yale matatizo ya moyo kwenda mbio, kama mtu anataka kukata roho, yamepotea kiajabu…siamini, huu ni muujiza wa aina yake….ulimpataia wapi yule mwanadada….?’ Akauliza huyo mzee.

‘Huu mji bwana, kuna warembo wengi..hujawahi kukutana nao, ni yupi huyo, mbona sikumbuki kumtuma mtu hapa karibuni…ndio nakumbuka nilishawahi kuongea na wanawake kadhaa nilioona wanakufaa, nikjaribu kukupigia debe, na wengi walikubali haraka tu, sasa sijui, ni yupi kati ya hawo aliyegusa moyo wako…’akasema huyo rafiki yake kwa hamasa.

‘Huyo aliyekuja ni chagua halisi….ooh,....lakini lifika kipindi kigumu kidogo,.... alifika akakutana na mambo ya huyu muhuni wangu.....ila hayo kama ulivyosema, tuyaacha kama yalivyo, yanaweza kuzusha mabalaa mengine, na sina muda wa kulumbana ...ila kwanza kwa hasira niliwaita watu wa usalama, na ilivyo kawaida, kila mmoja aliyekuwepo hapa ikabidi akahojiwe…wakamchukua na huyo binti...nauliza naambiwa kaondoka na polisi....’akasema huyo mzee.

‘Lakini nilishakuonya...kuwa ukiwa hapa ndani, uwe na mfanyakai wako unayemuamini, ....na akae hpo nje, kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeingia baada ya wewe kupata dawa yako....maana sasa umeanzwa kuandamwa na matatizo…mimi pia narudia ushauri wangu, kuwa inabidi ukamrejee mkeo, nilishakuambia , wake wana laana zao, ukimuacha kwa mabaya, ujue, hutaishi kwa wema’akasema huyo rafiki yake.

‘Kwa mtaji huo…siwezi kwenda kwake,…kama huyo mwanadada atakubalina na mimi, …naona bora..tena boraa nitafute mke mwingine…na huyo mwanadada ananifaa, kwa jinsi nilivyomuona, …unajua mimi nina machale, nikimuona mwanamke kwa mara ya kwanza tu, ninaweza kumjua kuwa ni mwema au ni mbaya…huyo ni mwema.. na anaonekana kabisa ana maadili mema, na nina uhakika anaweza kuishi na mimi….’akasema huyo mzee.

‘Ina maana mliongea naye akakubaliana na wewe kuwa awe mke wako na uzee wako huo, mbona mwanzoni ulisema hakuna mwanamke anayeweza kukubali, kwa vile wewe ni mzee, watakukubali tu kwa ajili ya mali yako, unauhakika gani kuwa huyo ni sawa na hawo wengine?’ akauliza huyo jamaa.

‘Huyo nina uhakika, kwani hamkuwahi kuongea naye?' akauliza na kabla rafiki yake hajajibu akasema;

'Kwanza lipofika hapa alijali afya yangu..hicho ni kipimo muhimu sana kwa mtu ninayemuhitaji kwa sasa, pili, uvaaji wake..tatu, aibu , adabu….haya,....huo uzuri  wake ndio usiseme….yaani nilijona mwenyewe nimepona,…kwa uzuri, naweza kumlinganisha na ile nyumba ndogo iliyoota mabawa, ila huyu kazidi kwa adabu, heshima….na kila kitu…’akawa anaongea akionyesha furaha ya ajabu.

‘Naona kweli umependa…maana hata uso wako unang'aa na kuonyesha uhai....ninahamu sana ya kumuona huyo mwanadada….unasema anafananaje maana sina uhakika sana ni yupi huyo, au jina lake ni nani...?’akauliza.

‘Mhh, ngoja, akija utamuona…niliwaambia watu wangu wachukue namba yake…hebu nipe hiyo simu hapo mezani…’akasema huku akiinuka, na kujinyosha, alionekana kuwa na afya na nguvu hata rafiki yaka akijikuta akitabasamu na kutoamini mabadiliko hayo ya muda mfupi.

‘Hii hapa mkuu…’akampa huyo mzee simu, na yule mzee akatafuta jina…..akaliona, na kabla hajaipiga mara mlango uakgongwa, akaingia wakili wake…

‘Oooh, afadhali umekuja, naona kila kitu sasa utakifanya wewe,….’akasema na kumgeukia rafiki yake;

‘Usiondoke maana na haya yanakuhusu..’akasema akimshika begani rafiki yake.

‘Nimekuja nimesikia kuna tatizo….la kutegewa sumu….?’ Akauliza wakili akiwa kasimama

‘Achana na hilo…hawaniwezi, hawo, wataumbuka wenyewe…hilo halina maana kwa sasa nisikilize kwa makini, haya malekezo yangu, na huyu hapa rafiki yangu,atakuwa ndiye best man wangu..’ akasema na wakili akabakia kushangaa.

‘Sitaki kupoteza ,muda….naona ushauri wake, umenizindua, ninaweza nikafa peke yangu humu ndani, na kanitafutia mtu ambaye ni chaguo langu…..wakili kaa hapo nikuelekeze nini la kufanya…’ akasema mzee akiwa na furaha ya ajabu.
Wakili akakaa kwenye kiti,akatoa makabrsha yake na kuanza kumsikiliza mzee..

                                               *******

 Maua alipofika hapo hotelini alishangaa kuona mlango umefungwa, na alipowauliza wahudumu akaambiwa kutokana na amrii ya askari, hawatakiwi kukaa humo tena,…


‘Kama mlivyoambiwa siku ile…hamuhitajiki kukaa humu, na mwenzako kasema utamkuta kituo cha mabasi ya kwenda Singida..’akaambiwa.

‘Kwenda Singida,..wapi huko?’ akauliza huku akiwa ameduwaa, na kabla hajasema lolote simu yake ikaita..na alipoitizama akaona ni namba ya mama yake mdogo.

‘Nipo hapa kituoni, navunga vunga, …maana huyo mwanamke kanitishia amani ni vijihela vyake alivyonipa,..unakumbuka, alinipa mwenyewe kwa mkono wake, sasa imekuwa ni nongwa…Unajua alichofanya,  sasa anawatumia maaskari eti tumemtapeli pesa zake…’akacheke kwa kebehi.

‘Lakini mama nilikuambia….’akawa anaongea Maua, na mama yake mdogo akamkatisha na kusema.

‘Mimi ni mtoto wa mjini, ninaishi bongo bwana, mjini hapa…, sasa wewe fika hapa kituoni, kuna hoteli nimepanga, ….ukifika nibeep, nitakuja kukuchukua,…itabidi tujifiche fiche hadi hapo tutakapo-onana na Tajiri, nimempgia simu anasema atafika hapo na atatuelekeza wapi pa kwenda, kwani anashindwa  kuondoka kwasababu mjomba wake ni mgonjwa..’akasema mama mdogo.

‘Kwahiyo……….?’ Akauliza Maua

‘Kwahiyo nini…wewe njoo hapa haraka,…kwanza umekuja na zile pesa toka kwa huyo mzee?’ akauliza mama mdogo kwa hamasa.

‘Pesa gani wakati nimekutana na mikasa huko, nikaishia kupelekwa polisi, hivi sasa natokea polisi, …’akasema Maua.

‘Polisi…usinitaje kabisa…mimi simo, nazijua jela za huku, …oooh, sasa balaa, mimi usinitaje na wala sikujui…..’akasema mama mdogo na simu ikakatika. Maua akacheka, …alishamjua mama yake mdogo alivyo, na kabla hajatulia vyema simu yake ikaita;

‘Nani mwenzangu?’ akauliza Maua alipoona ni namba ngeni kwenye simu yake.

‘Mimi ni wakili wa Mzee , Mjomba wake Tajiri…unaombwa ufike nyumbani kwake haraka…’simu ikasema.

‘Kuna tatizo gani?’ akauliza kwa mashaka.

‘Hakuna tatizo lolote, mzee anataka muonane, …’akasema huyo wakili

‘Lakin….’akaanza kulalamika Maua.

‘Unahitaji mtu aje akuchukue, tutatuma gari, wewe tuambie upo sehemu gani’ akasema huyo wakili.

‘Hapana nitakuja mwenyewe, hakuna shida….’akasema Maua, huku akiwa ameduwaa, akishindwa la kufanya, aende kwanza kwa mama yake au aende huko alipitiwa….

NB: Kuanza na kumaliza kisa ni kazi kubwa sana….lakini ndio tupo kwenye hitimisho. Kwa wale wanaofuatilia kisa hiki nawashukuru sana, …mungu awajaze baraka.

WAZO LA LEO: ‘Kwanini mimi siolewi?’ nimeulizwa hili swali na binti mmoja mrembo, nikamwambia kuwa `vuta subira’ lakini uzuri wa sura sio tija ya kuolewa, cha muhimu ni tabia yako, matendo yako..dini yako, na historia ya familia yako,….ukumbuke kuwa chema huwa kinajiuza, kibaya kinajitembeza.

Nawatakia Ijumaa nje, na wikiendi njema, nikisema Ishi na majirani zako vyema, kwani wao ndio ndugu waliopo karibu.


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

[url=http://vermoxonline.webcam/]where can i buy vermox medication online[/url] [url=http://albuterolinhaler.cricket/]albuterol inhaler[/url] [url=http://buyprovera.trade/]provera[/url] [url=http://viagra-100-mg.in.net/]viagra for sale online[/url] [url=http://indocin.site/]indocin[/url] [url=http://advaircost.science/]is there a generic advair[/url]