Malikia wa Mererani, alikuwa kasimama mbele ya askari, na
hakuonyesha dalili yoyote ya kuogopa, huku akiwa ameshika kiuni, akauliza kwa
ukali;
‘Haya niambieni mumeniitia nini hapa?’ akauliza.
‘Tumekuita hapa kwa kukuhoji ,kuna tatizo lilitokea kwa yuke
mzee wenu mgonjwa…inasadikiwa kuwa kuna mtu kamuwekea sumu kwenye maji, sasa
tunajaribu kuwahoji wanafamilia, na wewe ukiwa mmojawapo,’akasema yule askari.
‘Hivi nyie mnajua kazi yenu kweli, mimi ni mtu wa kuhojiwa
na vitu vidogo vidogo kama hivyo, nani amuwekee yule mzee sumu, mtu mwenyewe
anaelekea kuzimu, ina haja gani ya kumuwekea sumu…halafu mnasema `inasadakiwa’,
kwahiyo hamjafanya uchunguzi wa kina, basi, fanyeni uchunguzi, mkikamilika ndio
mniite kunihoji, na naomba msinipotezee muda wangu kwa vitu vya kijinga kama
hivyo,….’akasema huku akiondoka.
‘Ina maana unakaidi amri ya usalama, sisi hatujakuruhusu,
tumekuita kwa sababu tunahitaji maelezo yako, na sio wewe tu tuliyekuita, kuna
wengi akiwemo yule dada pale…..’akasema huyo askari akielekeza kidole kwa dada
mmoja aliyekuwa kaka kwenye benchi,…
Kwanza Malikia hakujali kuangalia ni dada gani, lakini
alipoona yule askari anatupa jicho mara kwa mara kwa huyo dada, akageuka
kuangalia kuwa ni nani huyo mwanadada. Alipotupa jicho la haraka, akajikuta
aksihituka, akageuka mzima mzima kuangalia pale alipokaa huyo mwanadada.
‘Na huyu naye ni mwanafamilia,….?’ Akauliza kwa mashaka.
‘Alikuwepo kwenye tukio….’akasema huyo askari.
‘Ahaa…safi kabisa,….manona wenyewe, kumbe mna mhalfu mkononi
mwenu,..halafu mnapoteza muda kwa mtu ambaye hahusiki..mnanipotezea mjuda
wangu.
‘Ni wajibu wetu kumhoji kila mtu…kwahiyo tunaomba utulie,
ili tuweze kuchukua maelezo yako,hatutachukua muda wako mwingi…’akasema huyo
askari huku akiendelea kutupa macho kwa yule mwanadada aliyekaa kwenye benchi.
‘Kwanza mimi nina wakili wangu, siwezi kuhojiwa mpaka
akiwepo….’kabla hajamaliza, akafika askari mwingine, na kusema;
‘Achaneni na dada…mzee kasema hana hatia, watayamaliza wenyewe
huko nyumbani, anasema hiyo kesi ifutwe kabisa, na walioshikiliwa wote waachiwe…’akasema
huyo askari, na Malikia akasonya na kugeuka kuondoka.
Alipotoka pale akapitia pale alipokaa yule mwanadada,
akampita bila kumwangalia, lakini akilini mwake, alikuwa na donge, akitaka
kumsemesha , lakini aliona kuwa akiongea naye, anaweza akapandisha hasira, na
huenda huyo mwanadada akapandisha….akaona atoke akamsubiri huko nje.
‘Mimi siku ya kumweka huyu binti humu ndani, nitahakikisha
hatanisahau, maana amejaa zarau, utafikiri ni mke wa waziri, au mtu mkubwa
serekilaini, lakini kumbe ni kimwanamke cha hapa hapa….hivi kwanini anajiamini kiasi
hicho?’ akauliza askari mmojawapo.
‘Achana naye huyo, dawa yake inachemka, ipo siku yake,
tunamfuatilia kwa karibu…mambo yake na kundi lake yapo karibu
kukamilika…’akasema huyo askari aliyeleta taarifa kuwa malikia aruhusiwe
kuondoka hana hatia.
*************
Maua ambaye kwa muda ule alikuwa hapo polisi, kama
walivyoamriwa na watu wa usalama, na baadaye na yeye akaambiwa yupo huru
anaweza kuondoka,…akatoka nje, na alipofika nje, akakutana na gari la malikia
likitaka kuondoka, na Malikia alikuwa akiangalia mlangoni jinsi anavyotoka huku
akiwa anasikiliza simu, na gari likiwa linaguruma kuonyesha kuwa anataka
kuondoka , na alipomaliza kuongea na simu, akashusha kiyoo cha gari lake na
kumwangalia Maua kwa dharau;
‘Wewe mwanamke…hivi niliwaambia nini…sasa sikiliza, unaona
umefika hapa kituoni, kwa kosa ambalo hujalifanya, sasa utafika kwa kosa ambalo…,
hutaweza kuondoka hapo, ulishawahi kufungwa jela wewe..sasa utafungwa jela kwa
wizi au kwa kuua…’akasema malikia.
‘Mimi sijakuelewa, kwani unataka nini kwangu?’ akauliza
Malikia akimwangalia yule mwanadada.
‘Nataka uondoke hapa Arusha,….hutakiwi hapa, unanuksi wewe….’akasema
Malikia.
‘Kwasababu gani unasema hivyo…., kwani tumekuzuia nini na
mambo yako?’ akauliza Maua.
‘Sikiliza….hilo ninalokuambia ni kwa manufaa yako…ondokeni
hapa mjini, na rudini huko mlipotoka,….sitawasemesha tena, …kwani mtakuja
kuumbuka vibaya sana, na nilishakuambia nenda katoe hiyo mimba, kama kweli una mimba…..itoeni
haraka kabla haijakuwa kubwa…’akasema huku akiangalia eneo la tumbo la Maua
‘Kwani hii mimba inakuhusu nini?’ akauliza Maua.
‘Hainihusu ndio….lakini inavuruga mambo yangu, na pili,
nawasikitikia kwa vile nyie ni watu wa kijijini kwangu, nisingelipenda mje
kuadhirika, unakumbuka nilishakuonyesha pete ya uchumba, sasa itakuwa ni aibu,
unaumbuliwa kwa kuiba mume wa mtu ….itakuwa ni aibu kwako na familia yenu,..nawajali
sana, ondokeni na wahini kuitoa hiyo mimba
mapema iwezekanavyo….kama hutanisikiliza mimi, basi ipo siku
utanikumbuka..’akasema.
‘Mimba haitatolewa na sitaondoka hapa mjini,…nitaondoka kwa
muda wangu…’akasema Maua na kuanza kutembea kuondoka.
‘Wewe utaondoka tu, hilo nakuhakikishia…’akasema Malikia na
kuondoa gari lake haraka.
***********
‘Rafiki yangu, nashukuru sana, umefanya kazi moja kubwa sana……’akasema
mzee huku akionyesha kupona kabisa.
‘Kazi gani hiyo..?’ akauliza huyo rafiki yake, akishangaa,
kwani kwa taarifa alizozipata awali ni kuwa huyo rafiki yake ni mgonjwa sana,
na anakumbuka alifika mara moja, na kumkuta akipumulia mashine, sasa anamuona
akiwa na afya yake, utafikiri sio yeye aliyekuwa akiumwa.
‘Ohh, yaani ile ndio dawa…hutaamini, kwani nilipomuona tu,
mwili wote ukarejeshewa nguvu zake, na hata yale matatizo ya moyo kwenda mbio,
kama mtu anataka kukata roho, yamepotea kiajabu…siamini, huu ni muujiza wa aina
yake….ulimpataia wapi yule mwanadada….?’ Akauliza huyo mzee.
‘Huu mji bwana, kuna warembo wengi..hujawahi kukutana nao,
ni yupi huyo, mbona sikumbuki kumtuma mtu hapa karibuni…ndio nakumbuka nilishawahi kuongea na wanawake kadhaa nilioona wanakufaa, nikjaribu kukupigia debe, na wengi walikubali haraka tu, sasa sijui, ni yupi kati ya
hawo aliyegusa moyo wako…’akasema huyo rafiki yake kwa hamasa.
‘Huyo aliyekuja ni chagua halisi….ooh,....lakini lifika kipindi kigumu kidogo,.... alifika akakutana na mambo ya
huyu muhuni wangu.....ila hayo kama ulivyosema, tuyaacha kama yalivyo, yanaweza kuzusha mabalaa mengine, na sina muda wa kulumbana ...ila kwanza kwa hasira niliwaita watu wa usalama, na ilivyo kawaida,
kila mmoja aliyekuwepo hapa ikabidi akahojiwe…wakamchukua na huyo binti...nauliza naambiwa kaondoka na polisi....’akasema huyo mzee.
‘Lakini nilishakuonya...kuwa ukiwa hapa ndani, uwe na mfanyakai wako unayemuamini, ....na akae hpo nje, kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeingia baada ya wewe kupata dawa yako....maana sasa umeanzwa kuandamwa na
matatizo…mimi pia narudia ushauri wangu, kuwa inabidi ukamrejee mkeo, nilishakuambia , wake wana laana zao, ukimuacha
kwa mabaya, ujue, hutaishi kwa wema’akasema huyo rafiki yake.
‘Kwa mtaji huo…siwezi kwenda kwake,…kama huyo mwanadada
atakubalina na mimi, …naona bora..tena boraa nitafute mke mwingine…na huyo mwanadada ananifaa, kwa jinsi
nilivyomuona, …unajua mimi nina machale, nikimuona mwanamke kwa mara ya kwanza tu,
ninaweza kumjua kuwa ni mwema au ni mbaya…huyo ni mwema.. na anaonekana kabisa ana maadili mema, na nina
uhakika anaweza kuishi na mimi….’akasema huyo mzee.
‘Ina maana mliongea naye akakubaliana na wewe kuwa awe mke wako na uzee wako huo, mbona mwanzoni ulisema hakuna
mwanamke anayeweza kukubali, kwa vile wewe ni mzee, watakukubali tu kwa ajili
ya mali yako, unauhakika gani kuwa huyo ni sawa na hawo wengine?’ akauliza huyo
jamaa.
‘Huyo nina uhakika, kwani hamkuwahi kuongea naye?' akauliza na kabla rafiki yake hajajibu akasema;
'Kwanza lipofika hapa alijali afya
yangu..hicho ni kipimo muhimu sana kwa mtu ninayemuhitaji kwa sasa, pili,
uvaaji wake..tatu, aibu , adabu….haya,....huo uzuri wake ndio usiseme….yaani nilijona
mwenyewe nimepona,…kwa uzuri, naweza kumlinganisha na ile nyumba ndogo iliyoota
mabawa, ila huyu kazidi kwa adabu, heshima….na kila kitu…’akawa anaongea
akionyesha furaha ya ajabu.
‘Naona kweli umependa…maana hata uso wako unang'aa na kuonyesha uhai....ninahamu sana ya kumuona huyo
mwanadada….unasema anafananaje maana sina uhakika sana ni yupi huyo, au jina lake ni nani...?’akauliza.
‘Mhh, ngoja, akija utamuona…niliwaambia watu wangu wachukue
namba yake…hebu nipe hiyo simu hapo mezani…’akasema huku akiinuka, na
kujinyosha, alionekana kuwa na afya na nguvu hata rafiki yaka akijikuta akitabasamu
na kutoamini mabadiliko hayo ya muda mfupi.
‘Hii hapa mkuu…’akampa huyo mzee simu, na yule mzee akatafuta
jina…..akaliona, na kabla hajaipiga mara mlango uakgongwa, akaingia wakili wake…
‘Oooh, afadhali umekuja, naona kila kitu sasa utakifanya
wewe,….’akasema na kumgeukia rafiki yake;
‘Usiondoke maana na haya yanakuhusu..’akasema akimshika
begani rafiki yake.
‘Nimekuja nimesikia kuna tatizo….la kutegewa sumu….?’ Akauliza
wakili akiwa kasimama
‘Achana na hilo…hawaniwezi, hawo, wataumbuka wenyewe…hilo
halina maana kwa sasa nisikilize kwa makini, haya malekezo yangu, na huyu hapa rafiki
yangu,atakuwa ndiye best man wangu..’
akasema na wakili akabakia kushangaa.
‘Sitaki kupoteza ,muda….naona ushauri wake, umenizindua,
ninaweza nikafa peke yangu humu ndani, na kanitafutia mtu ambaye ni chaguo
langu…..wakili kaa hapo nikuelekeze nini la kufanya…’ akasema mzee akiwa na
furaha ya ajabu.
Wakili
akakaa kwenye kiti,akatoa makabrsha yake na kuanza kumsikiliza mzee..
*******
Maua alipofika hapo hotelini alishangaa kuona mlango
umefungwa, na alipowauliza wahudumu akaambiwa kutokana na amrii ya askari,
hawatakiwi kukaa humo tena,…
‘Kama mlivyoambiwa siku ile…hamuhitajiki kukaa humu, na
mwenzako kasema utamkuta kituo cha mabasi ya kwenda Singida..’akaambiwa.
‘Kwenda Singida,..wapi huko?’ akauliza huku akiwa ameduwaa,
na kabla hajasema lolote simu yake ikaita..na alipoitizama akaona ni namba ya
mama yake mdogo.
‘Nipo hapa kituoni, navunga vunga, …maana huyo mwanamke
kanitishia amani ni vijihela vyake alivyonipa,..unakumbuka, alinipa mwenyewe
kwa mkono wake, sasa imekuwa ni nongwa…Unajua alichofanya, sasa anawatumia maaskari eti tumemtapeli pesa
zake…’akacheke kwa kebehi.
‘Lakini mama nilikuambia….’akawa anaongea Maua, na mama yake
mdogo akamkatisha na kusema.
‘Mimi ni mtoto wa mjini, ninaishi bongo bwana, mjini hapa…,
sasa wewe fika hapa kituoni, kuna hoteli nimepanga, ….ukifika nibeep, nitakuja
kukuchukua,…itabidi tujifiche fiche hadi hapo tutakapo-onana na Tajiri, nimempgia
simu anasema atafika hapo na atatuelekeza wapi pa kwenda, kwani anashindwa kuondoka kwasababu mjomba wake ni mgonjwa..’akasema
mama mdogo.
‘Kwahiyo……….?’ Akauliza Maua
‘Kwahiyo nini…wewe njoo hapa haraka,…kwanza umekuja na zile
pesa toka kwa huyo mzee?’ akauliza mama mdogo kwa hamasa.
‘Pesa gani wakati nimekutana na mikasa huko, nikaishia kupelekwa
polisi, hivi sasa natokea polisi, …’akasema Maua.
‘Polisi…usinitaje kabisa…mimi simo, nazijua jela za huku, …oooh,
sasa balaa, mimi usinitaje na wala sikujui…..’akasema mama mdogo na simu
ikakatika. Maua akacheka, …alishamjua mama yake mdogo alivyo, na kabla hajatulia
vyema simu yake ikaita;
‘Nani mwenzangu?’ akauliza Maua alipoona ni namba ngeni
kwenye simu yake.
‘Mimi ni wakili wa Mzee , Mjomba wake Tajiri…unaombwa ufike
nyumbani kwake haraka…’simu ikasema.
‘Kuna tatizo gani?’ akauliza kwa mashaka.
‘Hakuna tatizo lolote, mzee anataka muonane, …’akasema huyo
wakili
‘Lakin….’akaanza kulalamika Maua.
‘Unahitaji mtu aje akuchukue, tutatuma gari, wewe tuambie
upo sehemu gani’ akasema huyo wakili.
‘Hapana nitakuja mwenyewe, hakuna shida….’akasema Maua, huku
akiwa ameduwaa, akishindwa la kufanya, aende kwanza kwa mama yake au aende huko
alipitiwa….
NB: Kuanza na kumaliza kisa ni kazi kubwa sana….lakini ndio tupo kwenye hitimisho. Kwa wale wanaofuatilia kisa hiki nawashukuru sana,
…mungu awajaze baraka.
WAZO LA LEO: ‘Kwanini mimi siolewi?’ nimeulizwa hili swali
na binti mmoja mrembo, nikamwambia kuwa `vuta subira’ lakini uzuri wa sura sio
tija ya kuolewa, cha muhimu ni tabia yako, matendo yako..dini yako, na historia
ya familia yako,….ukumbuke kuwa chema huwa kinajiuza, kibaya kinajitembeza.
Nawatakia Ijumaa nje,
na wikiendi njema, nikisema Ishi na
majirani zako vyema, kwani wao ndio ndugu waliopo karibu.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
[url=http://vermoxonline.webcam/]where can i buy vermox medication online[/url] [url=http://albuterolinhaler.cricket/]albuterol inhaler[/url] [url=http://buyprovera.trade/]provera[/url] [url=http://viagra-100-mg.in.net/]viagra for sale online[/url] [url=http://indocin.site/]indocin[/url] [url=http://advaircost.science/]is there a generic advair[/url]
Post a Comment