Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, December 31, 2012

Yote ni majaliwa ya muumba-Heri ya mwaka mpya 2013                                             Picha hii imechukuliwa: http://www.shout-africa.com
 

Kwa mara nyingine tena nilijikuta nipo mitaa ya hospitali kubwa hapa nchini, hospitali ambayo wanasema ukiambiwa nenda nyumbani huku bado unaumwa, basi ujue wewe ni wa kuhesabu masaa, au masiku kama siku zako hazijafika. Hapo ndipo kitivo cha wataalamu wetu, japokuwa kuna hospitali nyingine kama KCMC, Bugando, na nyinginezo, lakini kwa hapa Dar, tunaamini kuwa Muhimbili ndio penye wataalamu wote.

Nikiwa kwenye mitaa ya hiyo hospitali huku nikiangalia kwa juu kwenye maneno na viashiria vinavyoonyesha wapi wodi ilipo, nilitembea huku nikisoma majina ya hizo wodi, huku kuna wodi ya Siwahaji, huku Kibasila,….na kule ni Mwaisela, na nikajiuliza majina haya yalikuwa ya watu, waasisi au ni majina  ya akina nani…

Tukiwa na haraka ya kuwahi kumuona mgonjwa wetu, maana muda wa kuona wagonjwa ulkuwa unakaribia kufika, tukakutana na jamaa yetu akiwa na uso wa furaha, akatuambia kuwa hatimaye mgonjwa wao kapatiwa damu, kwani walikuwa na mgonjwa  wao aliyekuwa na uhaba wa damu, na alipofikishwa hapo, wakaambiwa kwanza wachangie damu, na wakafanya hivyo,..na baadaye kweli mgonjwa wao akapatiwa huduma hiyo, sasa anaendelea vyema.

Hatujasogea kidogo mbele kidogo tukakutana na kilio, wakina mama wakiwa wameshikilia mwenzao, huku wakiwa na kikapu walichokuwa wamebebea chai, ..chai ambayo waliibeba kwa ajili ya mgonjwa wao, na wanadai mgonjwa wao jana tu, alikuwa na afya njema, baada ya mitababu, na walijua kuwa keshapona, na walijua kuwa baada ya siku mbili hivi watakuwa na nyumbani na mgonjwa wao huyo, lakini leo wamefika, wamemkuta hayupo, walipouliza wakaambiwa, tunasikitika mgonjwa wenu keshaiaga dunia.

Hatujatulia kidogo, mara gari la ambulasi, likapita, na wenye mioyo ya kutaka kujua kuna nini, wakakimbilia kuangalia, na kilichnekana hapo, na damu, mejeruhi,…jamaa ambao walikuwa kwenye sherehe zao, za kuuga mwaka, walipinduka na gari, na hali yako ni taabani. Wengi wao walikuwa ni vijana, ambao walijimwaga kwenye maukumbi ya starehe, wakanywa na kufanya kial aina ya starehe, na wakati wanarejea majumbani wakakutana na ajali hiyo.

Mimi pale nilipo nikabakia mdomo wazi, nikageuka kushoto na kukimbilia wodini angalau nikamuone mgonjwa wangu, moyoni nikiomba nimkute akiwa katika afya njema, nikiogopa kusema nimkute akiwa hai, lakini kwa hapo lolote lawezekana, kwani hawo waliofika asubuhi, wakiwa wamebeba chai ya mgonjwa wao, walikuwa na mawazo kama hayo, lakini hawakumkuta mgonjwa  wao, waliambiwa mgonjwa wao keshaiaga dunia,….

Niliwaza na kuwazua, nikiifikiria hii dunia, dunia ambayo ipo pale pale,.lakini mabadiliko yake ni mengi, ya jana sio ya leo, ….je ni nani anaweza kusema kuwa mimi nina uhakika wa kuifikia kesho, au anajua kuwa kesho atakuwa nani, na kaa ni tajiri, atendelea kuwa tajiri hivyo, na kama ni mzima hataweza kupatwa na kilema.

Kiuhakika hakuna mwenye uhakika wa hilo. Wapo waliokuwa matajiri, yalikuwepo makampuni makubwa ya kutisha, lakini yote hayapo tena, imebakia historia, na mengine mapya yamejitokeza, hatujui hatima ya kesho, ndio maana kila tunalodhamiria kufanya, tusijiwekee uhakika, tunachotakiwa ni kusema `mungu akipenda’, kwani hatuna mamlaka ya uhai wetu wa baadaye.

Ingawaje hatuna uhakika wetu wa baadaye, lakini tunatakiwa tujitume, tuwajibike, kama vile tutaishi milele,hilo tusilisahau, maana bila kazi mkono hautaweza kwenda kinywani ….Hata hivyo, kama wanadamu ambao hatuna uhakika wa kesho au keshokutwa tunatakiwa tumuombe yule aliye na mamlaka ya uhai wetu, tuombe kwa imani zetu kama vile ndio tunamalizia uhai wetu…

Tujue yote haya yanayotokea ni ishara kubwa za kumjua mwenyezimungu, kuwa yupo na atendela kuwepo, yeye ndiye mwenye mamlaka ya uhai wetu, …..  Na tukumbuke kuwa kila mmoja ana mwake wake,…mwaka huu wa ujumla ni mwaka wa kinadharia tu. Na siku ikiisha, au mwezi ukiisha au mwaka ukiisha tunahitajika kumshukuru yeye, ambaye ametuwezesha kuumaliza huo mwaka. 

Je sherehe mbwembwe, makelele, na vifijo vinaashiria nini, kuwa ndio tumashukuru muumba, je kulewa  kufanya fujo kunaashiria nini, kuwa tumemshinda nani? Sijui labda kila mmoja nafsini mwake aliweka nadhiri hiyo na huenda hiyo ndio imani yake…..

Au labda aliiweka ahadi kuwa akimaliza mwaka, atalewa, au atafanya fujo. Lakini tukumbuke hawo ambayo wameshatangulia walikuwa na ahadi kama hiyo, hawo ambao wapo mahospitalini, walikuwa na ahadi hiyo, lakini mwenye mamlaka ya uhai wetu, katimiza yale aliyokuandikia.

Jamani tunapomaliza mwaka, tukae chini na kuomba, tumshukuru muumba, maana hujui nini kitatokea kesho. Na kama una uwezo wako, hebu jaribu kuwakumbuka wale ambao hawajiwezi. Kuwajali wao ni akiba yako ya maisha yako ya baadaye. Ukumbuke wapo ambao wakiamuka  asubuhi hawajui watakula nini, hawajiwezi, wapo wagonjwa mahututi, wanaumwa, hawana pesa, huenda wangelikuwa nazo wangelipata matibabu mazuri, lakini wapo kitaandani wakiomba majaliwa ya mungu.

Heri na baraka katika dunia hii zitapatikana pale tutakapowaona wenzetu kuwa ni kama wewe, hata kama yupo katika hali, gani, na kile ulichojaliwa japo ni kidogo, ukawa radhi kumgawia mwenzako, ili na yeye ajione binadamu kama wewe. ….

 Nyie  mnaofanya sherehe ya mamilioni ya pesa, ambayo inatumika kwa siku moja tu, tena kwa kufuru ya hali ya juu, kwanini kila kwenye sherehe kama hizo muwe na taratibu za kutoa msaada wa kuwasaidia wale wasio na uwezo. kwasababu na wao wanaohitaji kuwasomesha watoto wao kwenye shule nzuri kama wewe, wanahitaji kutibia wagonjwa wao, wanahitaji angalau mlo mmoja kwa siku, wanakosa,….

Tusijione tunacho tukajenga kiburi, tusijiona tuna elimu, tusijione tuna madaraka, tusijione tuna uwezo tukajenga kiburi,…hicho kiburi hakitakufikisha mbali, wapo waliokuwa na kiburi zaidi yako lakini leo hawapo duniani tena. Huko walipo wanajuta , wanajuta na kusema ningelijua mali yangu yote ningeliwasaidia wasiokuwa na uwezo…maana huo msaada utakaotoa ndio akiba yako ya kuondoka nayo, vingine vyote utaviacha hapa duniani

Ni hayo kwa leo, nikiwaombea wagonjwa wetu waliopo kitandani, mahospitalini, na popote walipo wapone, ili na wao waweze kujumuika na wengine katka harakati za kutafuta tonge la mdomoni, na tunawaombea wale waliotangulia mbele za haki makazi mema peponi, Na pia tuwaombee matajiri,wale wenye uwezo, wenye utawala, waweze kuwakumbuka mayatima wafanyakazi wao, wananchi wao, wakijua kuwa kupata kwao, sio kuwa  wao ni wajanja saaana, …..yote ni  majaliwa ya muumba.

Blog yenu inawatakia heri za mwaka mpya 2013, msherehekee kwa amani na kumkumbuka mungu

 
Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Thank you for the auspicious writeup. It in fact was a amusement account it.
Look advanced to far added agreeable from you!

However, how can we communicate?
my website :: sex gif

Anonymous said...

If some one desires to be updated with latest technologies afterward he must be go to
see this web site and be up to date all the time.
My website :: oreck vacuum bags

Anonymous said...

HONGERA ZA MWAKA 2013 MKUU, TUWE PAMOJA

Rachel siwa Isaac said...

Kheri na Baraka katika mwaka huu mpya ..Ndugu wa mimi na Familia pia...Pamoja Daima.

Anonymous said...

Just as the gods used WWII to justify an influx of new technologies, including the voice in your head, so will they use the impending pestilence which kills over half the world's population to justify historical medical advances, including the "cure of aging", initiating the "1000 years with Jesus on Earth", despite biotechnology already accomplishing these goals.
We've seen this tactic used recently with AIDS, targetted at homosexuals and blacks in Africa with the biotechnology product. The gods control everything on Earth, and althugh sold AIDS to your enemies as revenge, their real purpose was to enlighten you regarding sex:::Back-handed help. It was very effective with homosexuals in the USA, but sex is among the most powerful temptations with Africans. Remeber it is always the gods:::Slavery, AIDS, drive-bys, crack babies, pimps prostituting 10 year-old girls. And, contrary to your belief the victim doesn't go anywhere, they are reincarnated back to Earth like everyone else when we die.
Then, as promised, The End will come with fire::::Global tectonic subduction.

There was a very real perception that bi-racial was much worse for the white than it was for the person of color. The liberal culture, which was designed and promoted with the god's tools to achieve their Apocalyptic goals, screamed racism when there was a very reasonable explanation for this reality::::
In this white punishment known as the United States the person of color has already adopted the disfavors/temptations intended for another race. But by associating/mating with a person of color the white is newly adopting the disfavors of another culture.
And this is the reason why people of color are not welcome in the United States. The gods control everything:::The perception they want to create, the thoughts they want you to have.
People of color can't recover from absorbing the temptations from two cultures. And why they become more and more like so many blacks in America:::Veterans at absorbing the temptations of two cultures.
To further illustrate this is why California's educational system/funding was ranked #1 when California was white:::Education being the basis of the affluent economic system. Now even public higher education has become unaffordable.

Don't forget the lessons the 'ole white preacher taught:::Dancing is a sin, spare the rod spoil the child.
The gods used the liberal tool to ridicule away so many taboos, paving the way for the decay of society and ultimately the End Times::::::
Black behavior was controlled by the KKK. Men's behavior was controlled by marriage for thousands of years.
When married by 15 men never gained the taste of promiscuity. Once the gods used the budding liberalism tool the men set the tone for the deteriorating enviornment centered around their gross disfavor.
Women's relinquishing control of pre-arranged marriage will be what costs mankind everything in The End. It's all their fault. Men are pigs, essentially just primally responsive disfavored beings who if given the freedom will abuse based on the impulses the god's push them into. Whereas under pre-arranged marriage this behavior was contained now the promiscuous fraternity house epitomizes the pinnicle of what a "real man" should be like. And sadly the women fall into line.

The gods behave monsterously in the course of managing Planet Earth but they demand people be good if you are to have a chance to ascend in a future life.
Not only is doing the right things important (praying, attoning for your sins, thinking the right way:::accepting humility, modesty, vulnerability), so is avoiding the wrong things important as well:::"Go and sin no more".
You NEED active parents who share wisdom to have a real chance to ascend into heaven in a future life, and you MUST be a good parent as well to have that opportunity. Once your children have been raised something changes, something has been decided about you. This is exactly that.


Anonymous said...

Definitely believe that which you stated. Your favorite justification appeared to be on the web the easiest thing to be aware of.
I say to you, I definitely get irked while people consider
worries that they plainly do not know about. You managed to hit the nail upon the
top and defined out the whole thing without having side effect ,
people could take a signal. Will likely be back to get more.
Thanks

my web blog; start a window cleaning business