Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, December 19, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-40Tukumbuke kuwa malikia mtarajiwa kaamua kwenda kumtembelea Maua ili kumfahamisha nini kinachoendelea kuhusiana na mtoto wao. Ili kufika huko inabidi kukatisha msitu ambao una kila aina ya hatari kuanzia ya wanyama na sasa kuna hatari ya adui wa kivita,..Mzee Hasimu na kundi laki.

Tukumbuke pia kuwa kipindi hicho ilifahamika kuwa mtoto huyo bado yupo na kundi la mzee Hasimu, wakimshikilia kama chambo ili kuwezesha madai yao. Na pamoja na kumtumia huyo mtoto kama chambo, lakini pia walishapeleka malalamiko yao huko wanakokuita makaoni.

Pamoja na hayo, kundi hilo lilishajiweka kwenye hali ya kivita, wakitafuta sababu yoyote, …na hata kama kuua kwa kusingizia ….propoganda potofu, za kuwadanganay raia, na kila mbinu za kisiasa. Na kulionyesha kuwa wao ni zaidi, kundi hilo liliwasili sehemu hiyo yenye ulinzi mkali inayojulikana kama sehemu takatifu bila kutegemewa, japokuwa kulikuwa na ulinzi mkali, lakini kundi hilo kwa utalaamu wao liliweza kupenya na kufika hapo ofisi kuu, kitu kilichomshitua sana mfalme,

Je ni nini kitaendelea baada ya hapo, je malikia atafika safari yake salama, ?hebu tuione sehemu kidogo, kabla hatujaendelea na mchakato wa mgangano wa kisiasa katika kugombea madaraka, tuwe pamoja …..

******
Malikia mtarajiwa alisonga mbele akiongozwa na kikosi maalumu, wakikatisha msitu, na kujaribu kukwepa kabisa sehemu ambazo zinakisiwa kuwa ndio ngome ya mzee hasimu, na kila hatua waliyopita ilimfanya malikia aanze kuingiwa na wasiwasi na hata kujijutuia kwa mauamuzi hayo ya kwenda kumuona Maua, aliona ni heri kumbe angekubaliana na mume wake kuwa wasubiri kwanza hadi kutulie, lakini yeye alishinikiza kuwa lazima akaonane na Maua ili kumwelezea hali halisi.

Alijipa moyo kuwa raia wote wa jamii hiyo ya msituni wana imani ya kumuheshimu malkia na hata kuamini kuwa hata wanyama hawawezi kumdhuru malikia, kwani kabarikiwa, na analindwa kimiujiza, na hilo lilipma moyo kuwa hakuna anayeweza kumfanyia lolote baya, kwani kwa imani yao kumdhuru malikia ni sawa na kumdhuru mama yako mzazi, …. 

Imani za hawa watu, zinamtukuza sana Malikia kama na wanafikia kusema kuwa mkono wa malikia  una baraka, ndio maana kila mmoja anahijika kushikwa kichwani na malikia huyo, na huweze kukutana nay eye ukuiachia hiyo bahati, ni lazima ujitahidi akushike kichwa na kukubariki ….

Kwa imani zao hizo, kama ingeliwezekana kila siku walihitajika kupata baraka hizo kwa kushikwa kichwani na mkono wa malikia, lakini kwa ajili ya majukumu na wingi wa watu isingeliwezekani kufanyika hivyo kwa kila siku. Na wengi hujitahidi angalau wafike kwa malikia mara moja kwa wiki, hapo utaona jinsi gani malikia alivyokuwa na kazi kubwa. 

Wao wanaamini kuwa mtu akiumwa, akiwa na shida yoyote, wa kumlilia ni mama wa wanafamilia, yaani malikia nay a kuwa yeye ndiye mwenye baraka za kuondoa ugonjwa, au matatizi yoyote yale ambayo yameshindikana ndani ya familia husika, kwahiyo malikia anakuwa kama dakitari mkuu wa magonjwa yote…

Malikia mkuu ndiye mtendaji wa mambo ya kijamii, kwa mfano raia akijifungua yeye anahitajika kumbariki mtoto, na kumpa jina linalomfaa, yeye anaheshima kuwa ndiye mkuu wa wakunga wote , malikia anatakiwa kubariki ndoa za watu zikifungwa, hata kama ni kwa mbali, lazima apewe taarifa na yeye hubariki hapo hapo alipo, na akitoa idhini  ndoa zinafungwa.

Licha ya kuwa safari hiyo ilikuwa ni kificho, lakini wakuu wa ulinzi wa sehemu ambazo alitakiwa kupita walishapewa taarifa, kwahiyo kila alipokatisha vikosi vya ulinzi, alisimama kidogo na kutoa mkono wa baraka kwa wawakilishi hawo ambao walikuwa ni wakuu wa vikosi ambao waliaminika sana. Na, askari wengine walikuwa hawajui ujio wa malikia, lakini kama kuna waliokuwepo hapo karibu, ilibidi wajitahidi angalau na wao washikwe kichwa kupata baraka.

Msafara huo ulitakiwa uonekane kama vile malikia alikuwa na ziara za kubariki vikosi vya ulinzi,haikutakiwa kabisa ijulikane kuwa malikia alikuwa na safari ya kwenda kumuona Maua, kwani Maua anajulikana kama mtu asiyehitajika katika jamii, na alishahukumiwa kuliwa na mamba, japokuwa hukumu hiyo ilitiliwa mashaka na wengi, lakini ilikuwa haijabatilishwa.

Kwa ajili ya ujio wa malikia kwenye vikosi vya ulinzi,  ulinzi uliongezwa, na kwa askari wa kawaida waliambiwa kuwa ulinzi huo unaimarishwa kama moja ya juhudi za kuhakikisha kuwa wahasimu hawapati mwanya wa kuingia uraiani na kuleta fujo, hawakuambiwa kuwa kuna msafara wa malikia.

Msafara huo wa malikia uliongozwa na watu wanaojua siri za huo msitu na njia zote salama, …..lakini hata hivyo, shaka haikuwatoka, kwani wenzao na wao walikuwa wakijua mengi ya njia za siri, na kwa asilimia kubwa waliokuwa wakijua siri za njia za msituni, walikuwa watu wa mzee hasimu kwa vile wao ndio waliokuwa na jeshi kubwa lililokuwa likilinda huo msitu….

Pamoja na kuwepo na ulinzi mkali, vikosi hivi vitiifu vya serikali iliyopo madarakani, hawakujua kuwa hasimu na kikosi chake maalumu walishapita kwenye njia za siri na huenda kwa muda huo vikosi hivyo walishafika kwenye makao, au sehemu inayotambulikana kama sehemu takatifu.

Malikia na watu wake wakaendelea na safari yao huku malikia akimkumbuka mumewe ambaye alijitahidi sana kumzuia asiondoke, ….lakini haikiwezekana, kwani alishazamiria safari hiyo iwepo;

‘Mke wangu, naona safari hii tuiharishe, maana kama unavyoona tupo vitani, na haitawezekana mimi kama mkuu na jemedari wa nchi niondoke, …’akasema mfalme.

‘Hiyo safari ni muhimu, hiyo ni moja ya sehemu ya vita,…tusipofanikiwa kwa sasa, tunaweza tukaeleweka vibaya, hatujui mpaka sasa mtoto yupo wapi, mimi kama mwanamke najaribu kujiweka kwenye nafasi ya Maua, na kuhisi jinsi gani ningelijisikia kama ningelikuwa mimi ni Maua,…ni muhimu nifike nionane nay eye ‘akasema malikia.

 Mfalme mtarajiwa akatulia akiwaza, akijua kuwa hili la safari kwa sasa haiwezekani kwake yeye kutokana na majukumu ya kijamii, yeye anatakiwa awepo hapo wakato wote, na zaidi ya hayo kesho yake anatakiwa kukutana na ujumbe uliotumwa kutoka makaoni, na hajui hatarai ya hiyo safari, hata kama ni kuondoka na kurudi siku hiyo hiyo.

Kiutawala angeliweza akatoa amri, akaenda na kufika huko, lakini sio hekima, na hataeleweka vyema, akageuka na kumwangalia mkewe, mkewe akamuelewa na kusema;

‘Mke wangu tuna majukumu mengi na hasa wewe ambaye kwa hivi sasa jicho la wengi linakutegemea wewe, hutakiwi kuondoka hapa hata kwa saa moja, je huoni kama ukiondoka na akaletwa raia anahitaji huduma yako, utakuja kusema nini…?’ akauliza mfalme.

‘Moja ya huduma yangu ni kusaidia raia wote, na mmoja wa raia hao ni huyo mtoto aliyepotea, na kwa vile ninatakiwa kufutilia taarifa zake, inabidi nionane na mama yake, ili na yeye asisononeke, ajue kuwa mtoto wake yupo kwenye mikono yetu, japokuwa tunajau yupo kwa wahasimu’akasema malikia.

Walitulia kwa muda kila mmoja akiwaza lake, na ndipo malikia akaireejsha ile hoja ya mtoto akasema;

‘Nimekuulizia kuhusu huyo mtoto aliyepotea, inaonekana kama huna wasiwasi sana kuhusu huyo mtoto, kwa mawazo yangu, mimi nitaenda ….wewe kwa vile kwa hali ilivyo huwezi kuondoka hapa, mimi acha niende, najua raia wote hapa wananiheshimu, hata hao wahasimu, hawataweza kunifanya lolote?’ akasema malikia

‘Hilo kwasasa halitawezekana mke wangu, hakuna ambaye atakuewa, kutoka kuondoka katika hali kama hii, usalama ni mdogo, na wenzetu kama wataona hiyo ndio nafasi ya kufanikiwa mambo yao hawatasita kukufanya lolote,….’akasema mfalme

‘Hilo niachie mimi…hakuna atakayeweza kunudhuru mimi….na nikifika huko nitajua jinsi gani ya kuongea na huyo mama wa mtoto, ….mimi nawafahamu sana wanawake wenzangu, na sisi wanawake tunajuana,…hilo niachie mimi, wewe kubali kuwa twende tukamuona, ili ajue kuwa bado tunamjali’akasema malikia.

‘Sawa kama una uhakika na hilo, ….lakini…nachelea sana kufanya lolote kabla sijaonana na hawa wahasimu, najua watakuwa wamemshikilia huyo mtoto, na huenda wana matakwa yao kuhusu huyo mtoto, wanaweza kumtumia kama chambo….’akatulia akiwaza.

‘Vyovyote iwavyo,..ngoja mimi niende nikamuona huyo mama wa huyo mtoto, na ningelipendelea safari hiyo iwe ni ya siri, mimi nitaondoka na wasaidizi wangu wawili na walinzi wawili waaminifu,…unasemaje kwa hilo?’ akasema malikia na kuuliza.

Mfalme alitulia akiwaza usalama wa mkewe, kweli alijua kuwa kwa imani zao malikia sio rahisi kudhuriwa, lakini wahasimu wanapoona ndio njia pekee ya kutimiza malengo yao, hawatasita kufanya lolote, na hata kama ni kumuua wanaweza kufanya hivyo, wakitumia maaskari mamluki ambao hawajui imani hizo.

Mzee hasimu alipoona kapungukiwa na askari, alituma ujumbe kutafuta maaskari mamluki ambao wengi wanaishi kwa njia hizo, wanaajiriwa katika mapigano, baadaye wanalipwa mali nyingi walizokubalina nazo na kurejea huko walipotoka. Na hili ndilo waliloliogopa sana mfalme mtarajiwa, kwani askari mamluki haangali ni nani wa kumua, anaua hata watoto, akina mama na hata wazee, kitu ambacho katika imani zao, hakikubaliki.

Na pia mfalme alikuwa na wasiwasi, kuwa huenda mkewe akatekwa kama alivyotekwa mtoto, ili kuweza kushinikiza matakwa yao. Hata hivyo aliona kuwa kweli kuna umuhimu wa mtu kufika huko kwa huyo mama kumuonyesha kuwa wapo pamoja na yeye, na kwa vile yeye ni mtawala, hatakuwa na ugumu wa kufika yeye, au kutuma ukumbe,….hapo akayasifu mawazo ya mkewe, japokuwa ni hatari tupu.

Na ndio maana safari hiyo ya kisiri iliandaliwa, na malikia akaondoka na watu wake, wakikatisha msitu wenye hatari za kila aina,na wakati wanakatisha huo msitu, na vikosi vikiwa vimewekwa kwenye tahadhari, kikosi maalumu cha hasimu kikapenya, na waliweza kupenya, bila hata kugundulika, na kufika huko ofisi kuu

Taarifa za ugeni huo zilipofika kwa mfalme, ikabidi amuite mkuu wa ulinzi kumuuliza imewezekanaje hawo watu kupenya hadi kuingia hapo bila kujulikana, na mkuu wa ulinzi hakuweza kutoa majibu, ikabidi uchunguzi mkali ufanyike, kwani ilionekana huenda kuna askari walioshiriki kwenye kufanikisha hilo, hasa askari waliojiunga kutoka kwa hasimu.

‘Hawa wenzetu wanaujua huo msitu kuliko hata sisi, kwahiyo uweze wao wa kupenya hadi kufika huku ni mkubwa sana, cha muhimu ni kuwa tumeliona hili, kwahiyo tunahitajika kuongeza nguvu zaidi, na hata ikibidi tunahitajika kuchukua askari wa akiba’akasema mshauri wa mfalme.

Mfalme aliinama na mawazo yalikuwa mengi,akimuwaza mkewe ambaye alikuwa ndani ya huo msitu kwa sasa, na pale aliona ni vyema atume watu wafuatilie usalama wa mkewe, lakini hilo akaliona halitafaa, na akaona kama atahidi hatari yoyote, kwa vile yupo na wahasimu wake, atahakikisha sheria zilizokuwepo zinatumika.

‘Mjukuu wangu, utawala wako unahitajika kutumia akili, unahitajika kutumia hekima, lakini pia kuna wakati 
unahitajika kutumia nguvu, ….na sio nguvu tu, wakati mwingine utahitajika kufanya yale ambayo katika hali ya kawaida usingelifikiria kufanya hivyo, kwa ajili ya raia wako…’akakumbuka maneno ya babu yake.

‘Kweli …kama kuna lolote litamsibu mke wangu, hawa watu sitawasamehe,…’akasema.

********

Mfamle mtarajiwa alibakia akimuwaza mkewe wake, na hapo akagundua kuwa mke kweli ni sehemu ya mwili wake, masaa machache baada ya kuondoka mkewe, alihisi mapungufu kwenye mwili wake, akili ikiwa inamuwaza mkewe….alijitahidi kiume, lakini bado moyo wa wasiwasi ulimuandama, hasa katika swala zima la usalama wa mkewe.

Japokuwa  baada ya kukubali kuwa mkewe aondoke kwenda kuonana na Maua alihakikisha kuwa njia atakayopitia kuna watu muhimu wa kikosi chao cha wanajeshi wanainda, lakini kwa maadui, kama watajua kuna msafara kama huo, wanaweza kutumia mbinu nyingine yoyote ili wamteke na kufanya lolote wanalotaka,

‘Hilo naomba limuepuke mke wangu….sitasamehe kama lolote litatokea kwa mke wangu…’akasema kimoyo moyo.

Katika mawazo yake kuna muda alijijutia kwanini kakubali mkewe aondoke peke yake, aliona ingelifa waongozane kila mara,  lakini pamoja na hayo, alijua kuwa wakati mwingine inabidi iwe hivyo, hawawezi wakaongozana kila safari, hata kama ni ya hatari,  inabidi wajitolee kwa maslahi ya wananchi wao. Akakumbuka jinsi alivyomwambia mkewe pale alipokuwa akimuga;

‘Mke wangu nakubali kwa shingo upande kuwa uondoke ukamuona Maua, lakini nafahamu fika, kuwa huu msitu, una hatari nyingi, za kila aina na ukumbuke wenzetu wameshatega mitego yao kila kona…ukikosea tu ukaingia kwenye anga zao, hawatakusamehe’akasema mfalme mtarajiwa.

‘Usiwe na wasiwasi mume wangu, umesahau kuwa mimi ni malikia mama wa wananchi wote ikiwemo wao wenyewe, kama kweli wana imani na imani zenu, hakuna lolote linaweza kutokea juu yangu…usiwe na wasiwasi mume wangu, mimi maisha yangu nimeshayakabidhi kwa ajili ya kuwatumikia raia wetu, ikiwemo wao wenyewe…’akasema malikia.

‘Nashukuru sana mke wangu, kwani kweli wewe ni malikia alyetabiriwa ambaye haogopi lolote kwa ajili ya raia zake, nakutakia safari njema, na ukimuoa Maua mwambie tupo pamoja na yeye, na tutafanya kila iwezekanavyo kuhakikisha kuwa anampata mtoto wake na tutamfikisha mikononi mwake salama usalamini’. Akasema mfamle mtarajiwa na akambusu mkewe kwenye paji la uso, na baadaye mkewe akaweka mkono wake juu ya kichwa cha mumewe kama ada yao.

Mfamle mtarajiwa akajaribu kuyafuta hayo mawazo na kutoka nje kuelekea kwenye ofisi yake, na kabla hajaingia kwenye hiyo ofisi , mara akamjia mlinzi wake wa karibu, alipofika alitoa ishara ya salamu, akainama na kusubiri kupewa kibali cha kuongea, na alipopewa akasema kuwa kuna ugeni umefika.

‘Ugeni kutoka makaoni….mbona wamewahi hivi…,?’ akauliza mfalme mtarajiwa, kwani ndio ugeni aliokuwa akiutarajia, ugeni huo ulitakiwa uje kwa ajili ya kusimikwa mfalme huyo, lakini shughuli hiyo ilibidi iahirishwe kwanza, baada ya wahasimu kupeleka pingamizi makaoni. Lakini wakaahidi kutuma ujumbe kwa ajili ya kuliangalia hilo tatizo lililofikia hadi kuwekewa pingamizi.

‘Hapana huo ni ugeni wa mzee hasimu na kijana wake na wazee wenzake’ akasema huyo mlinzi.

‘Ugeni wa Mzee hasimu….ooh, wamejileta wenyewe, safi kabisa…lakini wamefikaje hapa , bia kuonekana na askari wetu? ’ akasema mfalme mtarajiwa alijaribu kukificha mshituko alioupata moyoni . Aliwaza kama wao wameweza kufika hadi hapo bila kuonekana, je askari wao watashindwaje kuingia uraiani na kuanzisha vita.

Hapo akageuka kushoto kwake , ambapo ndipo wageni wanaposubiria na  kule aliona kundi la watu, na miongoni mwake akiwemo Mzee hasimu na kijana wake, walikuwa wote wamekunja uso kwa hasira.

Kundi lile lilikuwa limezingirwa na askari wa usalama, na walinyang’anywa silaha zao zote, na kuwekwa chini ya ulinzi, kitendo hiki walikiona kama kuzalilishwa,….hawakuwahi kufanyiwa hivyo kabla kwa vile muda mwingi wao walikuwa ndio watawala.

Mfalme mtarajiwa akamgeukia mlinzi wake wa karibu na kumwambia;

‘Sawa hakikisha wanakirimiwa na mwambie mwenzako akawaite wasaididizi wangu na mzee wangu na washauri wangu haraka iwezekanavyo’akasema na kuingia ofisini kwake, akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani, je hawa watu wamekuja kwa jambo gani. Je wamekuja kwa ajili ya huyo mtoto, na kama ni kuhusu huyo mtoto watakuwa na masharti gani, na je wana ajenda gani ya siri na huyo mtoto, je huo msafara hakuwahi kukutana na msafara wa mke wake….?

Wakati anawaza hilo akakumbuka ushauri wa wasaidizi wake, kuwa kundi hilo hasimu, halitatulia kamwe kumletea chochoko , hata kama watawapa kila kitu, lakini kama watawanyika madakara, haa amdaraka makubwa, ya kuiongoza jamii yao, hawatatulia ….

‘Sasa dawa yao ni nini?’ akauliza

‘Dawa yao ni kutumia sheria hiyohiyo waliyoitumia kuwauniza wenzao, ambayo japo kuwa ilikuwa na lengo jema, lakini wao waliitumie kwa masilahi yao, hasa kwa ajili ya kuwazima wapinzani wao, bila kujua kuwa sheria hiyo ipo siku itawabana wao wenyewe, kwani dawa ya moto ni moto…’akaambiwa, hakupenda kabisa huo ushauri, lakini kila hatua anayopita, anajikuta akilazimika kuitumia.

‘Labda, kuepuka haya kwa ajli ya wananchi…hawa watu inabidi na wao waionje sheria yao, ili na wao wajue machungu yake….’akasema na kutulia. Na mara wakaanza kuingia wasaidizie wake, na wazee mbali mbali, kila moja akiwa akionyesha hasira zake kwa wahasimu ambao walionekana wakiwa wanasubiri nje, kuleta hoja zao

WAZO LA LEO: Hekima kwa kiongozi ni jambo muhimu sana, pamoja na elimu uliyo nayo , pamoja na  uwezo wa kuongea kama huna hekima hutaweza kuwawa na maamuzi sahihi ya kuwarizisha watu wako
Ni mimi: emu-three

1 comment :

emu-three said...

Wapendwa, leo nilijiandaa kuweka kitu kipya lkn kama walivyosema wahenga cha mtu ni nini....basi nikashindwa, tuombe mungu kesho, mweneyzi akijalia, tutaendelea na kisa chetu