Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, December 10, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-36
Marejeo, tulipoishia: ‘Wewe ni nani…?’ akasikia sauti ya kutisha nyuma yake, na alipogeuka akamuona yule mama wa msituni ambaye alikuwa akimnywesha maziwa huyo mtoto, mama mkunga, mama ambaye alihakikisha kuwa anamzalisha na kuwakabidhi maaskari wakamtupe kwenye mto wa mamba, mama mtiifu wa mzee Hasimu.Haya tuendelee na kisa chetu


Mama huyu ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa mzee Hasimu, na huwa haendi kinyume na atakavyoagizwa na mzee wao huyo, na wazee wengi wanamuheshimu kama mama , miongoni mwa akina mama wanaozifuata sheria na desturi zao. Na wanasema mama huyo ana karama nyingi na mojawapo na kuwatambua wachawi,…na anaweza akamfuatilia mtu alitenda baya kwa kutumia hisia za pua yake.

Yule mama mkunga, alipokuwa kapumzika, alijiwa na ndoto mbaya, akiwa kwenye usingizi huo mdogo wa mchana, alijikuta anaota kuwa yupo karibu na mto, akiwa anamzalisha mwanamke, na pembeni yao, akawa ananyemelewa na mamba,....akawa anafanya haraka amaliza kazi yake, ili akimbie kabla yule mamba hajamfikia, na akawa hajamaza na mamba huyo akawa anamrukia yeye.

Hapo hapo akazindukana na akajikuta akihema , na jasho likiwa linamtoka. Akafumbua macho na kutuliza akili, na alipoikumbuka hiyo ndoto, akaingiwa na wasiwasi mkubwa, kwani kwa imani zao ukiota hivyo kuwa unapambana na mamba, au nyoka, ...., ujue kuna jambo baya linataka kukutokea au litatokea kwenye jamii, yenu,.

Hapo hapo akainuka na kujinyosha huku akiwaangalia wenzake pale alipokuwa kawaacha, aliwaona wapo pale pale, ikimaanisha kuwa hawajainuka pale, na bado walikuwa wakiongea. Akawaangalia askari, akamuona yupo askari mmoja, na anaonekana kasinzia.

Haraka, haraka akainuka, na kumwangalia yule askari mwingine, akamuona yupo jikoni , sehemu wanapopikia akiongea na mpishi wao mkuu, akahisi hasira zikimwingia mwilini, akatembea kwa haraka hadi kwenye kile kibanda maalumu walipomuweka  yule mtoto.

Alipokikaribia tu , akahisi mwili ukimsisimuka, akasimama, akamgeukia yule mlinzi , akamuona bado kasinzia, akachukua jiwe na kumrushia, …..Yule mlinzi alishituka na kwa haraka akasimama, na alipomuona yule mama akasimama pale karibu na kile kibanda cha mtoto, akakurupuka na kumfuata.

‘Mama kuna tatizo lolote nikusaidie?’ akauliza.

‘Una maana gani  kusema hivyo, ….hivyo ndivyo unavyotimiza wajibu wako,…nyinyi mnafahamu mzee Hasimu au mnamsikia,....hebu ingia ndani uone kama kuna usalama’akasema yule mama hakutaka kuingia yeye kwanza, kwani alihisi kuna tatizo.

Yule mlinzi akachungulia kwanza kwa ndani , na akarudisha kichwa kwa haraka na kumwangalia huyo mama , akachungulia tena, na safari hii akainuka mguu na kuingiza mguu mmoja ndani, akatulia, na baadaye akaingia ndani kabisa, na yule mama alikuwa kasimama pale pale mlangoni, akihisi kuna jambo baya.

‘Haya niambie kuna usalama huko ndani niingie na je huyo mtoto ana hali gani, maana naona kimiya kama vile hakuna uhai humo ndani?’ akauliza huyo mama na wakati huo yule mlinzi mwingine alikuwa keshafika, na alikuwa kashikilia kipande cha mfupa akimalizia kula nyama , na kwa muda ule alikuwa hajamuona huyo mama ,alipogeuka upande wa kibanda na kumuona yule mama akatupa lile fupa na kusema;

‘Mama kuna tatizo lolote nikusaidie?’ akauliza huku akiwa katoa jicho, na haraka akageuka kule alipokuwa mwenzake , akahituka alipoona sehemu ile ipo tupu, akamgeuka yule mama ambaye alikuwa kasimama huku akiangalia kule mlangoni mwa kile kibanda.

Yule mlinzi alipoona hiyo hali, akajua kuna tatizo, haraka akaingia ndani ya hicho kibanda na kwa haraka akawa anakagua mle ndani kwa macho, na macho yake yalipofika kwa huyo mlinzi mwenzake, akatulia kwani huyo mlinzi alikuwa kasimama kaduwaa, akiwa anaangalia pale alipokuwa kalazwa mtoto, ….

‘Ina maana Mtoto alikuwa jajarudishwa toka muda ule?’ akauliza huyo askari.

‘Kurudishwa vipi , wakati nilimrudisha mkiwa mnaona, ….'akasema huyo mama, akiwa bado yupo nje.

'Kuna dada alikuja akamchukua, muda kidogo, akitaka kumnyonyesha, …kipindi kile mwenzangu alipokwenda kuchukua maji’akasema huyo mlinzi.

‘Ina maana tangu muda ule walikuwa hawajamrudisha?’ akauliza huyo mwingine.

‘Sikuona wakimrudisha,…’akasema na mara huyo mama akaingia ndani, na macho yake yakatua pale alipokuwa kalala mtoto mwanzoni, na kuuliza.

‘Dada gani alimchukua huyo mtoto, kwani wanawake wote waliobakia hapa mnawafahamu, ni yupo kati ya wanawake hawo aliyemchukua huyo mtoto?’ akawageukia hawo walinzi.

Wale walinzi wakawa wanaangaliana, na hakuna aliyekuwa na jibu la moja kwa moja, ikawa kama vile wanategeana kutamka neno lolote.

‘Nawauliza mtoto yupo wapi, mbona hamnijibu, mnapoteza muda,hivi nyie hamjui hatari gani ipo mbele yenu, mimi sitakuwa na jinsi ya kuwatetea, wanangu...ooh, balaa hili tena jamani….’ Yule mama akawa anaongea kwa uchungu, huku akiwaangalia wale askari wawili.

‘Mimi nina uhakika kuna mmoja walimchukua, na kwa muda ule nilikuwa kwenye usingizi,Kuna dada limchukua …….’akasema huyo mlinzi.

‘Dada yupi,…kwa mara ya mwisho nilimrudisha mimi na hakuna dada yoyote aliyekuja kumchukua huyo mtoto, …semeni ukweli huyo mtoto kaenda wapi, na tusipoteze muda hapa, kwani ….’akasema na alipoona wale walinzi hawana jibu, akatoka haraka na kuwaita wenzake.

‘Jamani eti ni nani alikuja kumchukua mtoto wakati nimepumzika?’ akauliza.

Wale akina mama wengine wakawa wametulia wakishangaa, na mmojawapo akasema;
‘Mbona hakuna hata mmoja aliyeinua mguu wake, tangu ulipompeleka kumlaza ulipomaliza kumnywesha maziwa ….na tulijua kalala, ‘akasema mmojawapo.

Wale walinzi wakawa wametoka pale ndani ya kibanda wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini, kila mmoja akiwazia adhabu ambayo ipo mbele yao, …kama huyo mtoto kachukuliwa , basi wanajijua kuwa wao sasa ni chakula cha mamba, na kabla ya kupelekwa huko, watakatwa  kidoo kidogo,..
Kwanza vitakatwa vidole vyao, baadaye itafuatia mikono yote,….na baada ya hapo watachukuliwa juu kwa juu na kwenda kutupiwa mamba,….hapo hakuna msamaha kwa huyo mzee wao.

‘Sasa mnasubiri nini….mtafuteni huyo mtoto,…’akasema huyo mama kwa hasira na wale askari wakatoka mbio, kuanza kutafiuta huku na kule, na wale akina mama wengine wakaanza kuhangaika huku na kule kutafuta, kwani walijua kuwa mzee akirudi hapo, wote watakuwa maratani.

Yule mama alipoona wote wameondoka,  akatembea hadi kwenye kile kibanda, akaingia ndani, na kutizama chini,akatulia kwa muda, akizivuta hisia zake, hadi akahisi hisia ya harufu ya kike,akaidaka puani mwake, na hapo akatoka na kuanza kutembea, akiifuatilia hiyo hiyo harufu, na kutumia pua yake, kunusa huku na kule akawa anatembea hivyo, hadi akawa katoka kabisa kule msituni….

*************
Maua alipogeuza kichwa nyuma kumwangali huyo aliyetoa sauti, na kumgundua kuwa ni nani. Alichofanya kwanza ni kugeuka na kumwangalia yule mtoto ambaye alikuwa katulia kimiya kwenye mikono yake, yule mtoto kwa muda ule alikuwa kalala, lakini alipogeuka kumtizama kwa muda ule, yule mtoto akaunua macho mara moja na wote wakawa wamengalia, na yule mtoto alibenua domo kuonyesha tabasamu, halafu akafummba macho yake.

Mama alishangaa jinsi mtoto yule alivyokuwa katulia kwenye mikono yake, alihsi ni kwa vile keshahisi ujoto wa mama yake, akasema kimoyo moyo;

‘Kweli mtoto na mama yake,..na naapa safari hii, sitakubali hata kwa njia yoyote mtoto huyu kunitoka hapa mikononi,…’alipojiapiza hivyo, aligeuka kumtizama yule mama ambaye alikuwa sasa keshamkaribia, mkononi kashika silaha zao za jadi, huku kakunja uso kwa hasira, tayari kwa kutoa kipigo.

Silaha ni mshale, ambao una sumu kali, …na ni silaha maalumu kwa wanawake, ambazo,walitakuwa kuwa nazo kipindi cha vita. Silaha hiyo ina ncha kali, na ukimchoma adui yako, sumu ile hutembea haraka na kumfanya adui yako apoteze fahamu, na kama hatawahiwa dawa, anakufa.

Yule mama alipomuona Maua, mwanzoni hakujua kuwa ni huyo mama mwenye mtoto, akili yake, ailijua kuwa ni mama ambaye alikuwa na lengo la kumwiba huyo mtoto, alikuwa alikuwa mama aliyetumwa na wahasimu wao, ….na pale aliona njia njema ni kummaliza huyo mama, ili amchukue huyo mtoto na kumrejesha kambini kwao, kabla mzee na kundi lake hawajaikia, Alijua moja kwa moja, kama huyo mzee atafika, na kumkuta huyo mtoto hayupo, walinzi wote watauliwa, na hawo walinzi ni watoto wake.

‘Yule mama aliomkaribia Maua na Maua akawa kemgaukia na macho yao yakakutana, yule akashikwa na mshangao wa ghafla, na hata ile nguvu ya kuinua ile silaha aliyokuwa nayo, iliyokuwa imeshajijenga, akapotea ghafla, na kujikuta kitoa kicho la mshangao ukimwangalia Maua  na baadaye akasema;.

'Siamini…, wewe ni mzuka wa yule mama aliyetupiwa mamba, unataka kumwiba huyo mtoto, ukamfaney nini….ukamnyonye damu yake, hapana  .....'? akawa anaongea huku katoa jicho la uwoga na kushangaa, na  hapo akainua ile silaah yake, tayari kwa kumaliza Maua .

********

Maua mwanzoni hakuhisi hatari, alijua kuwa huyo mama atataka mabishano na kumnyang’anya huyo mtoto, hakujua kuwa mwenzake ana silaha ya hatari, aligundua pale huyo mama alipomkaribia na pale alipokuwa akitaka kuinua huo mkono wenye silaha, na yala maneno aliyotoa mdomoni.

Maua kwanza alitaka kuruka kwa nyuma, ili kujenga umbali, na ili mtoto asije akazuriwa, na kugeuza bega la kushoto, ili huyo mama akimrushia hiyo silaha isitue kwa mtoto, atue kwenye bega, na huku akilalia upande mmoja, kama vile kukwepa …..

Lakini haikuwa hivyo, kwani alipeinama upande mmoja, akajikwaa, na hata vile alivyofanya juhudi za kujizua asianguka, hakuweza kufanikiwa, ajikuta anaserereka kwenda chini, nay eye akafanay juhusi ili adondokee upande na mtoto awe juu, lakini aliogopa kuwa huyo mama anaweza akamuumiza mtoto na hiyo silaha.

Mvutano wa mawazo, adondokee upande gani ulimkuta keshalala chini, mtoto akiwa mbali na mwili wake, lakini akiwa karibu na viganja vyake vya mikono, akainuka haraka, na kumsogelea mtoto wake, huku akiinua kichwa kumwangalia adui yake, kwani sauti kali ilikuwa imetoka wakati yupo kwenye harakati hizo za kujiokoa asidondoke vibaya akamuumiza mtoto wake;

'Aaaaah,...'

Akainua uso na kumwangalia yule mama akiwa katoa  jicho la uwoga, na wakati huo alikuwa akielekea kudondokaka chini mbele karibu na miguu ya Maua. Maua akainuka haraka na mtoto wake, hakutaka kuangalia zaidi, alijua kuwa kuna mtu mwingine aliyemuwahi huyo mama, na huenda huyo mtu akawa mbaya zidi ya huyo mama, akaanza kukimbia;

Wakati anakimbia akahisi sauti ikimwambia ; `kimbia mama, kimbia umuokoe mtoto wako…’ na kweli alikimbia zaidi ya alivyotegemea na hatua ya mwisho ilimkuta yupi kwenye nyumba anayoishi yeye na huyo mwanaume mzee.

Aliingia ndani haraka na kumweka mtoto wake kitandani, na kumwangalia kwa makini, akamwinua juu, na kumchekesha, na mtoto akawa anacheka kwa furaha,..lakini kabla hajatulia vyema, akasikia sauti ya mtu akija na ilionekena dhahiri kuwa huyo mtu alikuwa akikimbia, kwanza akachukua panga, na pili akamchukua mtoto wake, na kusimama naye pembeni karibu na mlango.

‘Sitakubali  kabisa mtu akuchukue…’akasema na wakati huo mtoto alishafunua macho,..kwani likuwa keshaamuaka na mama akatabsamu, na yule mtoto akacheka.
Mara mlango ukafunguliwa kwa fujo,..na Maua alikuwa tayari alikuwa keshainua panga kuchamcharanga yoyote atakeingia hapo mlangoni…….

 NB: Jumatatu njema.

WAZO LA LEO: Kuna ambao wamejaliwa kuwa na hali nzuri, ukilinganisha na wengine, hiyo ni hali ya kawaida, kwani vidole havilingani. Lakini kuna baadhi ya hawo watu, kutokana na kujaliwa huko wanajenga tabia ya kiburi zarau na kejeli, kwa wenza wao wasiojaliwa,…hiyo sio tabia njema, ukumbuke aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima huyo unayemzarau, na inawezekana kabisa ikawa kinyume chake.

Ni mimi: emu-three

No comments :