Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 27, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni Mzazi-28
Tukireja kule porini, tuliona mzee akiwa katuma kikosi maalumu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa huyo kijana wa muhasimu wake hawarejei, kwani taarifa zilizokuwepo toka awali ni kuwa huyo kijana keshauliwa na mamba, ….

Lakini kwa ishara zao, zimeonyesha kuwa huyo kijana huenda bado yupo hai….na kwa ajili hiyo, wakaona waliharibu lile ua, ili hata kama huyo kijana ataonekana yupo hai, waweze kuhakikisha kuwa harudi tena kwenye himaya hiyo, je watafanikiwa hilo….tuendelee na kisa chetu.

******
Malikia mtarajiwa alipoona babu kaondoa bila kumpa jibu sahihi, akajua kuna jambo, akahisi kweli huenda mume wake keshauwawa, lakini akilini, hakukubaliana na hilo, kwani kama ingelikuwa hivyo ni kweli , taarifa zingelishaletwa kwake, lakini hakuna aliyewahi kumuelezea lolote kuhusuiana na tukio hilo.

Kitu kingine kilichumuweka roho juu, ni kuona watu wakiwa kama wanamkwepa, na zaidi ni pale alipokwenda kuliangalai ua lake, na kulikuta….limevunjika vunjia, vipende,….je liliwezaje kunyauka kwa muda huo mfupi hadi kuvunjika vunjia vipende,…hilli lilimtia shaka sana…

‘Lakini kwa vipi, itokee kwa muda mfupi, maana asubuhi, nilifia kulinyweshea maji nalilikuta likiwa limestawi vyema, na halikuwa na hata dalili ya kunyauka,…au ndivyo ilivyo, kuwa kama kuna bya limempaat mume wangu,….ua hilo litavunjiaka vunjika kama nilivyolikuta?’akajiuliza, na ili kuhakikisha hilo, akaamua kwenda kuliangalia tena, na safari hii alipofika hata vile vipande vipande hakuvikuta tena, ina maana kuna mtu kavichukua…

‘Mbona imekuwa kama vile kuna mtu kalipurura…hukua hata hivyo vipande vipande, au kuna mmoja wa wasaidizi wangu, aliliharibu kwa bahati mbaya, sasa ameamua kuvitupa hivyo vipande kwa kuogopa, na kwanini aharibu hilo ua peke yake, maana yapo mengine…..’akayaangalai maua mengine na kuyakuta yapo kama yalivyokuwa awali.

‘Hapa kuna mtu anajua hii siri, na huenda kafanya hivi makusidi ili kunivunja nguvu…’akasema na aliona mtu peke yake anayeweza kumsadia ni babu yao, lakini akakumbuka kuwa limuona akiomdoka, na ilionyesha kuwa anakwenda safari ndefu, ambayo hakutaka mtu aijue.

‘Ili kuondoa wasiwasi, inabidi nionena na wasaidizi wangu, ili nijue kama kuna mtu aliliharibu hilo ua kimakosa, au kama kuna mtu kamuona yoyote akipita maeneo hayo,. Kwani ni maeneo yake ambayo hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kufika zaidi yake yeye na mume wake.

Akiwa katulia, akamkumbuka ujio wa huyo kijana wa wahasimu wao, ambaye alikuja na zawadi, na maelezo kuwa mume wake keshafariki, na kwahiyo yeye kama malikia anahitajika kutoka hapo na kwenda sehemu huru kwa ajili ya kupata mume mwingine, kama mfalme mtarajiwa na akazidi kumuelezea kuwa yeye ndiye anayestahili kuwa mume waka…;

‘Hivi hawa watu wana akili kweli, hata kama ndio tuseme mume wangu keshafariki, ndio iwe haraka hivyo, hata sijapata muda wa uombolezaji, ndio wanakuja na mashauri ya kutaka eti anioe yeye , eti yeye ndiye aliyestahili kuwa mume wangu wa halali…hilo haliwezekani, na hili linanipa mashaka, huenda kuna kitu kimefanyika.

Alipowaza hivyo, akaondoka na kuwaita washauri wake, na kuwaulizia kuwa kuna yoyote alifika maeneo ya bustani yake, wote wakasema hawajawahi kupita maeneo hayo, kwani wanajua utaratibu ulivyo, kuwa maeneo hayo ni ya malikia na mumewe tu.

‘Tungelifika huko kama ungelituagiza tufanye hivyo…’akasema kionmgozi wa wasaidizi wake.

‘Nilitaka niwe na uhakika na hilo, na je hamkumuona yoyote , hata mtu wan je, akipita maeneo hayo?’ akauliza tena, na wote walisema hawakuona mtu yoyote akifika maeneo hayo, hata walinzi waliosema hakuna mtu aliyefika maeneo hayo.

‘Haiwezekani, ..lazima kuna mtu alifika meneo hayo…’akasema huku akizidi kuingiwa na wasiwasi, kwani kama kweli hakuna mtu aliyefika maeneno hayo, kwanini lile ua liwe hivyo…na je hivyo vipende vipande vilivyokuwepo, vimekwenda wapi, ina maana vimepeperishwa na upepo? Akawa akijiuliza maswali mengio bila jibu.

‘Kwa hili tukio nimewaita hapa mnisaidie…naomba tulijadili, maana nyie ndio watu wangu wa karibu, na kama mlivyoona, kuna mambo mengi ymetoeka hapa, na mume wangu mpaka sasa hajarudi,…mimi nina imani kuwa yupo salama’akasema na kuwaangalia wasaidizi wake, ambao wote walikuwa wameinamisha vichwa chini, kuashiria adabu zao, kwahiyo hakuweza kuona dalili yoyote yakushituka.

‘Je kama wasaidizi wangu mnashauri nini?’ akauliza hilo swali ili asikie wenzake watasema nini.

‘Mimi ninaona swali kama hili tungelimuuliza mzee wetu, maana sisi hatuna mamlaka ya kupekenyau mambo hayo, …tunaweza kusikiliza maoengezi, lakini hatuwezi kwenda kudadisi zaidi vinginevyo tuwatumie waume zetu’akasema mkuu wa wasaidizi wake.

‘Hili ni jambo letu …ndio maana nimewaita nyie, kama ningelihitaji msaada wa waume zetu, ningeliwaita, nina mamlaka hayo ya kuwaita na kuwaomba msaada huo, lakini sisi akina mama tunaweza kusikia mengi..’akasema.

‘Malikai tumekueelwa sana, kuwa tujaribu kuskiliza kuwa ni kitu gani kinaendelea has upande wa pili wa wahasimu wetu, hilo tunaweza kulifanya, kwani wenzetu wana mambo yao, na mengine sio mazuri’akasema huyo msaidizi wake.

‘Sawa kabisa, kwahiyo nataka tutege masikio, ili tusikie ni kitu gani kinandelea huko, lakini tuwe makini kwa hilo, kwani wenzetu wakigundua kuwa kuna matu anawafutilia , mnajua madhaar yake, na mimi sitsweza kuvumilia mtu yoyote aumie kwa ajili yangu.  Najua kuna namna nyingine zinaendelea ili kumwangamizi amume wangu, au kuna njama zimefanyika ambazo lengo lake ni kutaka  mume wangu asionekane.

Washauri wake , walitoa mawazo yao, na wengine wakajitolea kwenda kutafiti, ili kupata ukweli, huku wakijua kuwa jambo hilo lilihitaji uharaka, na umakini wa hali ya juu, kwani kosa dogo lingeweza kuwagharimu maisha yao  na ikizingatia wao ni wanawake, na kwa uratatibu wao kuna mambo mengine ambayo hawakupewa nafasi ya kuyaingilia.

‘Lakini Mzee wetu anasemaje, maana yeye ndiye mwenye kauli ya mwisho,?’ akauliza mmoja wa akina mama hawo, na kuongezea kuwa kwa taarifa zilizopo zikipita siku tatu, watachukua hatua, na moja ya hatua hiyo ni kumchukua yeye malikia.

‘Hakuna atakayeweza kuja kunichukua kwa nguvu….najua ni utaratibu, lakini lazima kwanza uchunguzi ufanyike ili kujua ni nini kimemsibu mume wangu’akasema malikia.

‘Kwani mzee wetu kaenda wapi, maana yeye ndiye anasubiriwa kuelezea na kutoa maamuzi ya mwisho?’ akauliza huyo msaidizi wake

‘Mzee inaonekena katoka, na hata nilipomuona hakuweza kuniambia lolote, aliondoka hapa akisema ana safari zake, na akirudi, atakuwa na cha kuelezea, na hivyo kuniweka mimi kwenye wasiwasi mkubwa kuwa huenda kuna jambo limempata mume wangu’alisema malikia, lakini hakuwaambia lolote kuhusu hilo ua kwani ilikuwa siri yake na mume wake, zaidi ya kuwauliza kama kuna yoyote aliyefiak bustanini kwake.

‘Sawa ngoja tumsubiri babu akirudi huko alipotoka huenda akaja na matumaini, au taarifa yoyote, na huku mkisikiliza ni nini kinandelea huko upande wa pili….’akawaambia na wao wakatawanyika na kumuacha malikia akimsubiria babu yao.

**********

Mzee wao, alirudi kesho yake, na kurudi kwake kulikuwa kwa siri, kama alivyoodoka kwa siri, na wengi waliomuona walisema muda wote alikuwa  kainamisha kichwa chini, kuashiria kuwa bado anatafakari, na hana jipya la kuwaelezea watu, licha ya kuwa aliwaahidi kuwa atawaambia jambo siku hiyo, lakini cha ajabu hajaweza kuitisha mkutano kuwaambia wajumbe lolote, na siku hiyo ikaonekana kupita, …

Siku ya tatu ikaingia, na minong’ono ikazagaa kila mahali, kuwa huenda kweli huyo kijana kaliwa na mamba, na wazee wanashindwa kujielezea, wakijua kuwa wenzao watashika madaraka yote, na huenda wao wakafukuzwa eneo linalotambukana kama eneo takatifu. Kutokana na minong’ono hiyo,  Mzee mmoja akaona ni vyema akamuulizie mzee mkuu kuna nini, mbona haitishi kikao kama alivyoahidi, .

Alifika ofisi ya mzee wao mkuu, na mlinzi alishaambiwa kuwa asiruhusu mtu kuingia, na kama ana shida yoyote amwambia kuwa afike siku nyingine,au aende kwa msaidizi wake. Lakini mlinzi kwa vile anamfahamu huyo mzee, kuwa ni mmoja wa wasaidizi wa mzee mkuu, na kuja kwake hapo ni lazima kuna jambo muhimu, ikabidi aende kumuelezea mzee mkuu kuwa kuna mzee mwenzake anataka kumuona.

‘Mwambia aingie….’akapewa kibali. Yule mzee akaingia na kumkuta mzee mwenzao akiwa kaka chini, akiwa kwenye maombi, ….akatulia kidogo hadi mzee huyo alipoinuka, na wakasalimia kama aada zo, na mzee huyo hakupoteza muda akaanza kuelezea kilichomleta hapo.

‘Mzee, mkuu wetu, uliahidi kuwa leo utatuambia lolote, lakini tumeona kimiya, wazee wanauliza nini kifanyike, ukumbue kuna taratibu zinatakiwa kufuatwa, na hizo taratibu tulitakiwa tuzianze leo, ili ikifika kesho tuwe tayari,…na kesho ndio siku ya tatu, inavyoelekea huko wenzetu wameshajiandaa kuja kufanya lolote’akasema huyo mzee.

‘Nimewaambia msubiri, ….subira huvuta heri, ..kwa sasa sina la kuwaambia wananchi wetu, tusubiri, tuvute subira, kuhusu hawo wenzetu, waacheni wajiandae, mimi nina imani kuwa mwisho wa siku, ukweli utadhihiri….’akasema na kumuomba huyo mzee aondoke. Na yule mzee akaondoka,  lakini haikupita muda malikia mtarajiwa naye akafika.

Mzee hapo akajikuta naye akiingiwa na majonzi, kwani hadi hapo hata yeye mwenyewe alishaanza kukata tamaa, maana muda unakwenda, lakini kama alivyoambiwa huko alipokwenda, alijipa moyo, na ikabidi atulie aone jinsi gani atamshawishi huyu binti, asiwe na wasiwasi, licha ya kuwa hata yeye mwenyewe ana wasiwasi.

Malikia ilibidi afike hapo, kwani muda wote alikuwa akimsubiria huyo mzee, na baada ya kusikia  tu kuwa mzee kesharudi, yeye moja kwa moja akafika hapo kwenye hiypo ofisi, na alipofika akaambiwa mzee anaongea na mzee mwenzake, asubiri kidogo.

Yule mzee alipotoka tu, akaingia, hakuweza kuvumilia zaidi, akamkuta huyo mzee akiwa kaka chini kwenye maombi yake, na mzee alipoona kuwa ni malikia,akainuka haraka, …licha ya kuwa yeye ni mzee mkuu, lakini kwao wao malikia ni zaidi ya mzee mkuuu. Akainama kidogo, ishara ya heshima yao kwa malikia.

Malkia alisalimia kwa adabu zao, hakupenda hiyo hali ya kuoenekana kuwa yeye ni mtu muhimu sana, ambaye kila mtu anamnyenyekea kama mkuu wa dini, yeye alimuona huyo mzee ni mtu wa heshima kuliko 
yeye, akataka kupiga magoti, lakini yule mzee akamwahi na kumwambia akae kwenye kiti cha enzi, ambacho alikuwa amekalia yeye.

Malikia akasita, lakini kwa heshima akasogea taratibu ka kukaa kwenye kiti hicho, na yule mzee akaenda kukaa kwenye kiti cha wageni, na kuanza kumsikiliza malikia, alijua nini kimemleta hapo, na hata ingelikuwa yeye , angelikuwa hivyo hivyo, akatulia,….

Mzee kichwani alikuwa anawaza yale aliyoambiwa huko, ambayo hayakuwa na jibu la haraka haraak wanalolihitaji wananchi na kwahiyo hakutaka kumuelezea mengi huyo binti, kwani yasingelimsaidia lolote, kwani hata wao huko, walisema kinachohitajiwa hapo ni kusubiri, kwani kama kweli huyo ndiye mfalme, atarudi na wanatajia kuwa huenda huo ni moja wa mitihani anayotakiwa kukabiliana nayo mfalme.

‘Binti yangu,  najua una wasiwasi sana, ….lakini nakuomba usiwe na wasiwasi,….japokuwa hata mimi sijui nini kimemtokea kijana wetu, lakini ninauhakika kuwa yupo hai, lakini kuwepo hai kwake, hakumaanishi kuwa yupo salama, ….huenda huko alipo yupo kwenye mapambano makali..na kila njia za kumsaidia tumejaribu zimeshindikana, sasa kilichobakia ni juhudi zake mwenyewe, na nina imani kuwa atashinda tu….’akasema mzee.

’Kwani yupo wapi, maana, yule mwanamke ambaye alitakiwa yeye amsaidie hakuweza kufanya hivyo, na nilivyosikia ni kuwa kweli huyo mwanamke alitupwa ziwani, na kuliwa na mamba,  sasa ni kitu gani kilichomuweka huko muda wote huo?’akauliza.

‘Ninachokuomba ni wewe kuvuta subira, na kuwa na matumaini kuwa mambo yatakwenda vyema, huo ni mmoja wa mitihani yenu, nina imani kuwa mkiwa na subiria,  mtakuwa ,mumefaulu, …najua kesho  kama hakuna lolote lililotokea hawa wenzetu watakuja kukudai utoke nje…’akasema babu.

‘Sasa wakija mimi nitafanyaje, maana mimi sitakubali kuolewa na huyo kijana wao, …..ni bora hata kama ni huo umalikia niuache tu…’akasema Malikia mtarajiwa na babu akaiunua macho na kumtizama mara moja huyo binti usoni, halafu akatizama chini, hakusema kitu akawa kimiya.

‘Kwahiyo mimi unanishauri nini, mzee wetu,….kama wakija hiyo kesho, nifanyeje?’ akauliza malikia mtarajiwa pale alipoona huyo mzee yupo kimiya.

‘Mimi ushauri wangu kwa sasa ni wewe kuvuta subira, hiyo ya kesho, itajulikana huko kesho…usiwe na wasiwasi, ..na uamuzi gani wa kuchukua, hilo lipo kwenye mamlaka yako, ni maamuzi yako,kama mama wa jamii hii, wote kwa sasa wanakutegemea wewe…..’akasema huyo mzee, na kumfanya malikia mtarajiwa ashituke, kwani, alitarajia kusikia lolote la kumzuia asiondoke.

‘Ina maana mtaniachia mimi mwenyewe, hamtawazuia hawo mahasimu wasinichukue?’ akauliza kwa kushangaa.

‘Kumbuka wewe ni malikia mtarajiwa, na usikatae hayo majukumu….ukumbuke kama malikia, mama wa miliki hii, wewe sio mama wa miliki hii peke yake, ni pamoja na hawo wenzetu, na wao wana kila haki ya kukupigania uende huko kwao,…ukumbuke kuwa raia wote ni watoto wako, je ni kuulize, kukitokea tatizo mama anawakimbia watoto wake?’ akamwangalia huyo binti machoni.

‘Hawezi kuwakimbia watoto wake, kwani mama ana machungu zaidi kwa watoto wake kuliko mtu yoyote…..’akasema malikia.

‘Sasa kumbe unajau jibu lake,….nenda nyumbani kwako katulie kimiya…ukijua wote ni wananchi wako, wote ni watoto wako, wewe ndiye malikia mtarajiwa na ni mama wa wote. ….’yule mzee akasema na kuinamisha kichwa chini.

Malikia alitulia akiwazia hayo maneno, kumbe umalikia anaotakwia kukabidhiwa sio kazi rahisi kama alivyokuwa akizania, kumbe ana majukumu makubwa, na kazi inakuwa kubwa zaidi kipindi kama hicho kukiwa na shida, kila raia anakutizama wewe, na ukizaingatia kuwa wanaamini kuwa yeye ni malikia na ana Baraka nyingi.

Malikia mara nyingi, ilibidi afanye tu kama wanavyotaka wao, maana kila siku watu humiminika kwake, wakiwa na matatizo mbali mbali, wanakuja kuomba baraka zake, na wakati mwingine wanaletwa wagonjwa, anatakiwa kuwaombea, ….watoto wachanga wakizaliwa yeye anatakiwa kuwashika kwanza na kuwapa baraka zake, kwani yeye ni mama wa wote.

Yule mzee alipoona malikia yupo kimiya, akasema;

‘Binti yangu nikuuliza swali,…najua hiyo ilikuwa siri yako na mumeo, lakini kwa kipindi kama hiki huna budi kuwa mkweli kwangu, najua  kuna ua alikuachia mume wako, umalikutaje?’ swali hilo lilimshitua kidogo malkia kwani mumewe alimuambia kuwa hakuna yoyote anayejua lolote kuhusu hilo ua, hata babu yake hajui.

‘Umejuaje kuhusu hilo ua mzee wangu, maana hilo lilikuwa siri yangu na mume wangu?’ akauliza malikia.

‘Mjukuu wangu, mimi ni mzee wenu,kuna mengi nyie hamjayajua bado, licha ya kuwa wewe ni malikia, mtarajiwa,…, makamo kama haya, nimepitia mengi, na ninafahamu mengi…huyo mjukuu wangu asingeliweza kulijua hilo kama isingelikuwa sisi wazee wenu kuwafichulia mambo hayo ya ghaibu, ambayo hata mimi mengine siyajui, nayajua toka kwa wazee wenzetu wanaojua zaidi…..najua atakuwa kakuachia ua, je ulilikutaje?’ akaulizwa.

‘Nililikuta halipo kama lilivyotakiwa liwe,….’akasema malikia baada ya kutulia kwa muda na kutafakari kwa kina, na alijua jibu lake hapo ni muhimu sana, alitakiwa kujibu kitu ambacho kitasaidia, na sio kuongea tu kwa hisia zake

‘Ulilikuta limenyauka, au limeharibika,?’ akaulizwa.

‘Hapana, muonekane wake sio ule wa kunyauka, mwanzoni nilikuta limevunjika vunjika vipende vipande,…na nilipoliona kwa mara ya kwanza nilipoteza fahamu,…lakini baadaye nikazindukana,..na nilipotizama vile vipande kwa makini, vingine, vilionekana ni vibichi..ni kama mtu aliyekuja na kulivunja vunja, na kuyafinyanga yale maua na matawi yake…’akasema malkia.

‘Kama ni hivyo…wewe katulie ndani, …..mambo yatakwenda vyema, usiwe na wasiwasi kabisa na wala msihangaike, kwa lolote lile’akasema babu, na hapo malikia akakumbuka kuwa alishawatuma watu kwenda kuchunguza nini kinaendelea upande wa pili, akaona hilo hawezi kumwambia mzee wao huyo, hayo ni mambo yake ya ndani.

‘Sawa Mzee wetu tupo pamoja…’akasema malikia na kuondoka, na alipofika kwake, akahisi kuna ugeni, na ugeni kwake ni kila siku, lakini kwa muda huo alihitaji muda wa kutulia na kutafakari hali halisi iliyopo mbele yake, hakuingia chumba cha wageni, akaeleeka moja kwa moja kwenye chumba chake, na kusubiri, na baadaye akaja mmoja wa wasaidiizi wake,na kumuarifu kuwa kuna wageni wamekuja.

‘Ni wageni gani hawo?’ akauliza

‘Ni yule kijana, wa wahasimu wetu, lakini safari hii hakufika peke yake, ameambatana na mtu mwingine…’akaambiwa.

Malikia alitaka kumwambia kuwa kama ni huyo kijana , amwambia kuwa kwa sasa hana nafsi. Wao wanawatambua huyo kama vijana, kama wanavyomuita mume wake kijana wa mzee, lakini ni wanaume hawo, kiumri ni mkubwa zaidi ya malikia.

‘Kaambatana na nani?’ akauliza malikia mtarajiwa.

‘Ameambatana , na mkunga mkuu, yule mkunga aliyemzalisha yule mwanamke aliyetupwa ziwani kuliwa na mamba….wamekuja na mtoto mchanga, ambaye ni wa yule mama aliyetupwa huko ziwani kuliwa na mamba’akaambiwa na Malikia mtarajiwa aliposikia hivyo, akainuka, …huku kumbukumbu maneno ya mwisho wa yule mama siku alipokuwa akipelekwa kujifungua, na baadaye atupwe kuliwa na mamba.

‘Nakuomba sana unitunzie mwanangu,…wewe ni mwanamke kama mimi, na wewe unajua machungu hata kama hujazaa…nakuomba sana, hakikisha mtoto huyo unamlea wewe…nakuomba sana tafadhali…’ alipokumbuka hivyo, akainuka haraka kuelekea huko walipo hawo wageni.


Ni mimi: emu-three

No comments :