Tukireja kule porini,
tuliona mzee akiwa katuma kikosi maalumu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa huyo
kijana wa muhasimu wake hawarejei, kwani taarifa zilizokuwepo toka awali ni
kuwa huyo kijana keshauliwa na mamba, ….
Lakini kwa ishara zao,
zimeonyesha kuwa huyo kijana huenda bado yupo hai….na kwa ajili hiyo, wakaona
waliharibu lile ua, ili hata kama huyo kijana ataonekana yupo hai, waweze
kuhakikisha kuwa harudi tena kwenye himaya hiyo, je watafanikiwa hilo….tuendelee
na kisa chetu.
******
Malikia mtarajiwa alipoona babu kaondoa bila kumpa jibu
sahihi, akajua kuna jambo, akahisi kweli huenda mume wake keshauwawa, lakini
akilini, hakukubaliana na hilo, kwani kama ingelikuwa hivyo ni kweli , taarifa
zingelishaletwa kwake, lakini hakuna aliyewahi kumuelezea lolote kuhusuiana na
tukio hilo.
Kitu kingine kilichumuweka roho juu, ni kuona watu wakiwa
kama wanamkwepa, na zaidi ni pale alipokwenda kuliangalai ua lake, na
kulikuta….limevunjika vunjia, vipende,….je liliwezaje kunyauka kwa muda huo
mfupi hadi kuvunjika vunjia vipende,…hilli lilimtia shaka sana…
‘Lakini kwa vipi, itokee kwa muda mfupi, maana asubuhi,
nilifia kulinyweshea maji nalilikuta likiwa limestawi vyema, na halikuwa na
hata dalili ya kunyauka,…au ndivyo ilivyo, kuwa kama kuna bya limempaat mume
wangu,….ua hilo litavunjiaka vunjika kama nilivyolikuta?’akajiuliza, na ili
kuhakikisha hilo, akaamua kwenda kuliangalia tena, na safari hii alipofika hata
vile vipande vipande hakuvikuta tena, ina maana kuna mtu kavichukua…
‘Mbona imekuwa kama vile kuna mtu kalipurura…hukua hata
hivyo vipande vipande, au kuna mmoja wa wasaidizi wangu, aliliharibu kwa bahati
mbaya, sasa ameamua kuvitupa hivyo vipande kwa kuogopa, na kwanini aharibu hilo
ua peke yake, maana yapo mengine…..’akayaangalai maua mengine na kuyakuta yapo
kama yalivyokuwa awali.
‘Hapa kuna mtu anajua hii siri, na huenda kafanya hivi
makusidi ili kunivunja nguvu…’akasema na aliona mtu peke yake anayeweza
kumsadia ni babu yao, lakini akakumbuka kuwa limuona akiomdoka, na ilionyesha
kuwa anakwenda safari ndefu, ambayo hakutaka mtu aijue.
‘Ili kuondoa wasiwasi, inabidi nionena na wasaidizi wangu,
ili nijue kama kuna mtu aliliharibu hilo ua kimakosa, au kama kuna mtu kamuona
yoyote akipita maeneo hayo,. Kwani ni maeneo yake ambayo hakuna mtu mwingine
anayeruhusiwa kufika zaidi yake yeye na mume wake.
Akiwa katulia, akamkumbuka ujio wa huyo kijana wa wahasimu
wao, ambaye alikuja na zawadi, na maelezo kuwa mume wake keshafariki, na
kwahiyo yeye kama malikia anahitajika kutoka hapo na kwenda sehemu huru kwa
ajili ya kupata mume mwingine, kama mfalme mtarajiwa na akazidi kumuelezea kuwa
yeye ndiye anayestahili kuwa mume waka…;
‘Hivi hawa watu wana akili kweli, hata kama ndio tuseme mume
wangu keshafariki, ndio iwe haraka hivyo, hata sijapata muda wa uombolezaji,
ndio wanakuja na mashauri ya kutaka eti anioe yeye , eti yeye ndiye
aliyestahili kuwa mume wangu wa halali…hilo haliwezekani, na hili linanipa
mashaka, huenda kuna kitu kimefanyika.
Alipowaza hivyo, akaondoka na kuwaita washauri wake, na
kuwaulizia kuwa kuna yoyote alifika maeneo ya bustani yake, wote wakasema
hawajawahi kupita maeneo hayo, kwani wanajua utaratibu ulivyo, kuwa maeneo hayo
ni ya malikia na mumewe tu.
‘Tungelifika huko kama ungelituagiza tufanye hivyo…’akasema
kionmgozi wa wasaidizi wake.
‘Nilitaka niwe na uhakika na hilo, na je hamkumuona yoyote ,
hata mtu wan je, akipita maeneo hayo?’ akauliza tena, na wote walisema
hawakuona mtu yoyote akifika maeneo hayo, hata walinzi waliosema hakuna mtu
aliyefika maeneo hayo.
‘Haiwezekani, ..lazima kuna mtu alifika meneo hayo…’akasema
huku akizidi kuingiwa na wasiwasi, kwani kama kweli hakuna mtu aliyefika
maeneno hayo, kwanini lile ua liwe hivyo…na je hivyo vipende vipande
vilivyokuwepo, vimekwenda wapi, ina maana vimepeperishwa na upepo? Akawa
akijiuliza maswali mengio bila jibu.
‘Kwa hili tukio nimewaita hapa mnisaidie…naomba tulijadili,
maana nyie ndio watu wangu wa karibu, na kama mlivyoona, kuna mambo mengi
ymetoeka hapa, na mume wangu mpaka sasa hajarudi,…mimi nina imani kuwa yupo
salama’akasema na kuwaangalia wasaidizi wake, ambao wote walikuwa wameinamisha
vichwa chini, kuashiria adabu zao, kwahiyo hakuweza kuona dalili yoyote
yakushituka.
‘Je kama wasaidizi wangu mnashauri nini?’ akauliza hilo
swali ili asikie wenzake watasema nini.
‘Mimi ninaona swali kama hili tungelimuuliza mzee wetu,
maana sisi hatuna mamlaka ya kupekenyau mambo hayo, …tunaweza kusikiliza maoengezi,
lakini hatuwezi kwenda kudadisi zaidi vinginevyo tuwatumie waume zetu’akasema
mkuu wa wasaidizi wake.
‘Hili ni jambo letu …ndio maana nimewaita nyie, kama
ningelihitaji msaada wa waume zetu, ningeliwaita, nina mamlaka hayo ya kuwaita
na kuwaomba msaada huo, lakini sisi akina mama tunaweza kusikia
mengi..’akasema.
‘Malikai tumekueelwa sana, kuwa tujaribu kuskiliza kuwa ni
kitu gani kinaendelea has upande wa pili wa wahasimu wetu, hilo tunaweza
kulifanya, kwani wenzetu wana mambo yao, na mengine sio mazuri’akasema huyo
msaidizi wake.
‘Sawa kabisa, kwahiyo nataka tutege masikio, ili tusikie ni
kitu gani kinandelea huko, lakini tuwe makini kwa hilo, kwani wenzetu
wakigundua kuwa kuna matu anawafutilia , mnajua madhaar yake, na mimi sitsweza
kuvumilia mtu yoyote aumie kwa ajili yangu.
Najua kuna namna nyingine zinaendelea ili kumwangamizi amume wangu, au
kuna njama zimefanyika ambazo lengo lake ni kutaka mume wangu asionekane.
Washauri wake , walitoa mawazo yao, na wengine wakajitolea
kwenda kutafiti, ili kupata ukweli, huku wakijua kuwa jambo hilo lilihitaji
uharaka, na umakini wa hali ya juu, kwani kosa dogo lingeweza kuwagharimu
maisha yao na ikizingatia wao ni
wanawake, na kwa uratatibu wao kuna mambo mengine ambayo hawakupewa nafasi ya
kuyaingilia.
‘Lakini Mzee wetu anasemaje, maana yeye ndiye mwenye kauli
ya mwisho,?’ akauliza mmoja wa akina mama hawo, na kuongezea kuwa kwa taarifa
zilizopo zikipita siku tatu, watachukua hatua, na moja ya hatua hiyo ni
kumchukua yeye malikia.
‘Hakuna atakayeweza kuja kunichukua kwa nguvu….najua ni
utaratibu, lakini lazima kwanza uchunguzi ufanyike ili kujua ni nini kimemsibu
mume wangu’akasema malikia.
‘Kwani mzee wetu kaenda wapi, maana yeye ndiye anasubiriwa
kuelezea na kutoa maamuzi ya mwisho?’ akauliza huyo msaidizi wake
‘Mzee inaonekena katoka, na hata nilipomuona hakuweza
kuniambia lolote, aliondoka hapa akisema ana safari zake, na akirudi, atakuwa
na cha kuelezea, na hivyo kuniweka mimi kwenye wasiwasi mkubwa kuwa huenda kuna
jambo limempata mume wangu’alisema malikia, lakini hakuwaambia lolote kuhusu
hilo ua kwani ilikuwa siri yake na mume wake, zaidi ya kuwauliza kama kuna
yoyote aliyefiak bustanini kwake.
‘Sawa ngoja tumsubiri babu akirudi huko alipotoka huenda
akaja na matumaini, au taarifa yoyote, na huku mkisikiliza ni nini kinandelea
huko upande wa pili….’akawaambia na wao wakatawanyika na kumuacha malikia
akimsubiria babu yao.
**********
Mzee wao, alirudi kesho yake, na kurudi kwake kulikuwa kwa
siri, kama alivyoodoka kwa siri, na wengi waliomuona walisema muda wote alikuwa
kainamisha kichwa chini, kuashiria kuwa
bado anatafakari, na hana jipya la kuwaelezea watu, licha ya kuwa aliwaahidi
kuwa atawaambia jambo siku hiyo, lakini cha ajabu hajaweza kuitisha mkutano
kuwaambia wajumbe lolote, na siku hiyo ikaonekana kupita, …
Siku ya tatu ikaingia, na minong’ono ikazagaa kila mahali,
kuwa huenda kweli huyo kijana kaliwa na mamba, na wazee wanashindwa kujielezea,
wakijua kuwa wenzao watashika madaraka yote, na huenda wao wakafukuzwa eneo
linalotambukana kama eneo takatifu. Kutokana na minong’ono hiyo, Mzee mmoja akaona ni vyema akamuulizie mzee mkuu
kuna nini, mbona haitishi kikao kama alivyoahidi, .
Alifika ofisi ya mzee wao mkuu, na mlinzi alishaambiwa kuwa
asiruhusu mtu kuingia, na kama ana shida yoyote amwambia kuwa afike siku
nyingine,au aende kwa msaidizi wake. Lakini mlinzi kwa vile anamfahamu huyo mzee,
kuwa ni mmoja wa wasaidizi wa mzee mkuu, na kuja kwake hapo ni lazima kuna
jambo muhimu, ikabidi aende kumuelezea mzee mkuu kuwa kuna mzee mwenzake
anataka kumuona.
‘Mwambia aingie….’akapewa kibali. Yule mzee akaingia na
kumkuta mzee mwenzao akiwa kaka chini, akiwa kwenye maombi, ….akatulia kidogo
hadi mzee huyo alipoinuka, na wakasalimia kama aada zo, na mzee huyo hakupoteza
muda akaanza kuelezea kilichomleta hapo.
‘Mzee, mkuu wetu, uliahidi kuwa leo utatuambia lolote,
lakini tumeona kimiya, wazee wanauliza nini kifanyike, ukumbue kuna taratibu
zinatakiwa kufuatwa, na hizo taratibu tulitakiwa tuzianze leo, ili ikifika
kesho tuwe tayari,…na kesho ndio siku ya tatu, inavyoelekea huko wenzetu
wameshajiandaa kuja kufanya lolote’akasema huyo mzee.
‘Nimewaambia msubiri, ….subira huvuta heri, ..kwa sasa sina
la kuwaambia wananchi wetu, tusubiri, tuvute subira, kuhusu hawo wenzetu, waacheni
wajiandae, mimi nina imani kuwa mwisho wa siku, ukweli utadhihiri….’akasema na
kumuomba huyo mzee aondoke. Na yule mzee akaondoka, lakini haikupita muda malikia mtarajiwa naye
akafika.
Mzee hapo akajikuta naye akiingiwa na majonzi, kwani hadi
hapo hata yeye mwenyewe alishaanza kukata tamaa, maana muda unakwenda, lakini
kama alivyoambiwa huko alipokwenda, alijipa moyo, na ikabidi atulie aone jinsi
gani atamshawishi huyu binti, asiwe na wasiwasi, licha ya kuwa hata yeye
mwenyewe ana wasiwasi.
Malikia ilibidi afike hapo, kwani muda wote alikuwa
akimsubiria huyo mzee, na baada ya kusikia tu kuwa mzee kesharudi, yeye moja kwa moja
akafika hapo kwenye hiypo ofisi, na alipofika akaambiwa mzee anaongea na mzee
mwenzake, asubiri kidogo.
Yule mzee alipotoka tu, akaingia, hakuweza kuvumilia zaidi,
akamkuta huyo mzee akiwa kaka chini kwenye maombi yake, na mzee alipoona kuwa
ni malikia,akainuka haraka, …licha ya kuwa yeye ni mzee mkuu, lakini kwao wao
malikia ni zaidi ya mzee mkuuu. Akainama kidogo, ishara ya heshima yao kwa
malikia.
Malkia alisalimia kwa adabu zao, hakupenda hiyo hali ya
kuoenekana kuwa yeye ni mtu muhimu sana, ambaye kila mtu anamnyenyekea kama
mkuu wa dini, yeye alimuona huyo mzee ni mtu wa heshima kuliko
yeye, akataka
kupiga magoti, lakini yule mzee akamwahi na kumwambia akae kwenye kiti cha
enzi, ambacho alikuwa amekalia yeye.
Malikia akasita, lakini kwa heshima akasogea taratibu ka
kukaa kwenye kiti hicho, na yule mzee akaenda kukaa kwenye kiti cha wageni, na
kuanza kumsikiliza malikia, alijua nini kimemleta hapo, na hata ingelikuwa yeye
, angelikuwa hivyo hivyo, akatulia,….
Mzee kichwani alikuwa anawaza yale aliyoambiwa huko, ambayo
hayakuwa na jibu la haraka haraak wanalolihitaji wananchi na kwahiyo hakutaka
kumuelezea mengi huyo binti, kwani yasingelimsaidia lolote, kwani hata wao
huko, walisema kinachohitajiwa hapo ni kusubiri, kwani kama kweli huyo ndiye
mfalme, atarudi na wanatajia kuwa huenda huo ni moja wa mitihani anayotakiwa
kukabiliana nayo mfalme.
‘Binti yangu, najua una
wasiwasi sana, ….lakini nakuomba usiwe na wasiwasi,….japokuwa hata mimi sijui
nini kimemtokea kijana wetu, lakini ninauhakika kuwa yupo hai, lakini kuwepo
hai kwake, hakumaanishi kuwa yupo salama, ….huenda huko alipo yupo kwenye
mapambano makali..na kila njia za kumsaidia tumejaribu zimeshindikana, sasa
kilichobakia ni juhudi zake mwenyewe, na nina imani kuwa atashinda tu….’akasema
mzee.
’Kwani yupo wapi, maana, yule mwanamke ambaye alitakiwa yeye
amsaidie hakuweza kufanya hivyo, na nilivyosikia ni kuwa kweli huyo mwanamke alitupwa
ziwani, na kuliwa na mamba, sasa ni kitu
gani kilichomuweka huko muda wote huo?’akauliza.
‘Ninachokuomba ni wewe kuvuta subira, na kuwa na matumaini
kuwa mambo yatakwenda vyema, huo ni mmoja wa mitihani yenu, nina imani kuwa mkiwa
na subiria, mtakuwa ,mumefaulu, …najua
kesho kama hakuna lolote lililotokea
hawa wenzetu watakuja kukudai utoke nje…’akasema babu.
‘Sasa wakija mimi nitafanyaje, maana mimi sitakubali kuolewa
na huyo kijana wao, …..ni bora hata kama ni huo umalikia niuache tu…’akasema Malikia
mtarajiwa na babu akaiunua macho na kumtizama mara moja huyo binti usoni,
halafu akatizama chini, hakusema kitu akawa kimiya.
‘Kwahiyo mimi unanishauri nini, mzee wetu,….kama wakija hiyo
kesho, nifanyeje?’ akauliza malikia mtarajiwa pale alipoona huyo mzee yupo
kimiya.
‘Mimi ushauri wangu kwa sasa ni wewe kuvuta subira, hiyo ya
kesho, itajulikana huko kesho…usiwe na wasiwasi, ..na uamuzi gani wa kuchukua, hilo
lipo kwenye mamlaka yako, ni maamuzi yako,kama mama wa jamii hii, wote kwa sasa
wanakutegemea wewe…..’akasema huyo mzee, na kumfanya malikia mtarajiwa
ashituke, kwani, alitarajia kusikia lolote la kumzuia asiondoke.
‘Ina maana mtaniachia mimi mwenyewe, hamtawazuia hawo
mahasimu wasinichukue?’ akauliza kwa kushangaa.
‘Kumbuka wewe ni malikia mtarajiwa, na usikatae hayo
majukumu….ukumbuke kama malikia, mama wa miliki hii, wewe sio mama wa miliki
hii peke yake, ni pamoja na hawo wenzetu, na wao wana kila haki ya kukupigania
uende huko kwao,…ukumbuke kuwa raia wote ni watoto wako, je ni kuulize, kukitokea
tatizo mama anawakimbia watoto wake?’ akamwangalia huyo binti machoni.
‘Hawezi kuwakimbia watoto wake, kwani mama ana machungu
zaidi kwa watoto wake kuliko mtu yoyote…..’akasema malikia.
‘Sasa kumbe unajau jibu lake,….nenda nyumbani kwako katulie
kimiya…ukijua wote ni wananchi wako, wote ni watoto wako, wewe ndiye malikia
mtarajiwa na ni mama wa wote. ….’yule mzee akasema na kuinamisha kichwa chini.
Malikia alitulia akiwazia hayo maneno, kumbe umalikia
anaotakwia kukabidhiwa sio kazi rahisi kama alivyokuwa akizania, kumbe ana
majukumu makubwa, na kazi inakuwa kubwa zaidi kipindi kama hicho kukiwa na
shida, kila raia anakutizama wewe, na ukizaingatia kuwa wanaamini kuwa yeye ni
malikia na ana Baraka nyingi.
Malikia mara nyingi, ilibidi afanye tu kama wanavyotaka wao,
maana kila siku watu humiminika kwake, wakiwa na matatizo mbali mbali, wanakuja
kuomba baraka zake, na wakati mwingine wanaletwa wagonjwa, anatakiwa kuwaombea,
….watoto wachanga wakizaliwa yeye anatakiwa kuwashika kwanza na kuwapa baraka
zake, kwani yeye ni mama wa wote.
Yule mzee alipoona malikia yupo kimiya, akasema;
‘Binti yangu nikuuliza swali,…najua hiyo ilikuwa siri yako
na mumeo, lakini kwa kipindi kama hiki huna budi kuwa mkweli kwangu, najua kuna ua alikuachia mume wako, umalikutaje?’ swali
hilo lilimshitua kidogo malkia kwani mumewe alimuambia kuwa hakuna yoyote
anayejua lolote kuhusu hilo ua, hata babu yake hajui.
‘Umejuaje kuhusu hilo ua mzee wangu, maana hilo lilikuwa
siri yangu na mume wangu?’ akauliza malikia.
‘Mjukuu wangu, mimi ni mzee wenu,kuna mengi nyie hamjayajua
bado, licha ya kuwa wewe ni malikia, mtarajiwa,…, makamo kama haya, nimepitia
mengi, na ninafahamu mengi…huyo mjukuu wangu asingeliweza kulijua hilo kama isingelikuwa
sisi wazee wenu kuwafichulia mambo hayo ya ghaibu, ambayo hata mimi mengine
siyajui, nayajua toka kwa wazee wenzetu wanaojua zaidi…..najua atakuwa
kakuachia ua, je ulilikutaje?’ akaulizwa.
‘Nililikuta halipo kama lilivyotakiwa liwe,….’akasema
malikia baada ya kutulia kwa muda na kutafakari kwa kina, na alijua jibu lake
hapo ni muhimu sana, alitakiwa kujibu kitu ambacho kitasaidia, na sio kuongea
tu kwa hisia zake
‘Ulilikuta limenyauka, au limeharibika,?’ akaulizwa.
‘Hapana, muonekane wake sio ule wa kunyauka, mwanzoni nilikuta
limevunjika vunjika vipende vipande,…na nilipoliona kwa mara ya kwanza
nilipoteza fahamu,…lakini baadaye nikazindukana,..na nilipotizama vile vipande
kwa makini, vingine, vilionekana ni vibichi..ni kama mtu aliyekuja na kulivunja
vunja, na kuyafinyanga yale maua na matawi yake…’akasema malkia.
‘Kama ni hivyo…wewe katulie ndani, …..mambo yatakwenda
vyema, usiwe na wasiwasi kabisa na wala msihangaike, kwa lolote lile’akasema
babu, na hapo malikia akakumbuka kuwa alishawatuma watu kwenda kuchunguza nini
kinaendelea upande wa pili, akaona hilo hawezi kumwambia mzee wao huyo, hayo ni
mambo yake ya ndani.
‘Sawa Mzee wetu tupo pamoja…’akasema malikia na kuondoka, na
alipofika kwake, akahisi kuna ugeni, na ugeni kwake ni kila siku, lakini kwa
muda huo alihitaji muda wa kutulia na kutafakari hali halisi iliyopo mbele
yake, hakuingia chumba cha wageni, akaeleeka moja kwa moja kwenye chumba chake,
na kusubiri, na baadaye akaja mmoja wa wasaidiizi wake,na kumuarifu kuwa kuna wageni
wamekuja.
‘Ni wageni gani hawo?’ akauliza
‘Ni yule kijana, wa wahasimu wetu, lakini safari hii
hakufika peke yake, ameambatana na mtu mwingine…’akaambiwa.
Malikia alitaka kumwambia kuwa kama ni huyo kijana , amwambia
kuwa kwa sasa hana nafsi. Wao wanawatambua huyo kama vijana, kama wanavyomuita
mume wake kijana wa mzee, lakini ni wanaume hawo, kiumri ni mkubwa zaidi ya
malikia.
‘Kaambatana na nani?’ akauliza malikia mtarajiwa.
‘Ameambatana , na mkunga mkuu, yule mkunga aliyemzalisha
yule mwanamke aliyetupwa ziwani kuliwa na mamba….wamekuja na mtoto mchanga,
ambaye ni wa yule mama aliyetupwa huko ziwani kuliwa na mamba’akaambiwa na
Malikia mtarajiwa aliposikia hivyo, akainuka, …huku kumbukumbu maneno ya mwisho
wa yule mama siku alipokuwa akipelekwa kujifungua, na baadaye atupwe kuliwa na
mamba.
‘Nakuomba sana unitunzie mwanangu,…wewe ni mwanamke kama
mimi, na wewe unajua machungu hata kama hujazaa…nakuomba sana, hakikisha mtoto
huyo unamlea wewe…nakuomba sana tafadhali…’ alipokumbuka hivyo, akainuka haraka
kuelekea huko walipo hawo wageni.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment