Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, February 22, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-84 hitimisho-28Mkuu ashituka aliposikia sauti kama ya mtu akitembea nje ya ofisi yake, alipiga simu nje kwa walinzi kuwauliza kama kuna mtu yoyote kaingia ndani, walinzi wakashangaa na kumwambia hakuna na kama anatilia mashaka wapo tayari kuingia kukagua,

‘Hapana, kama mna uhakika na hilo kuwa hakuna aliyeingia ndani, basi nitahakikisha mwenyewe…’akasema na kuinuka pale kwenye kiti, akafungua mlango na kukagua kwa macho sehemu yote ya mapokezi, hakuona dalili ya mtu, akataka kurudi ndani, lakini hamu ikamjia achunguze zaidi, akafunga mlnago wake na fungua, akaanza kuchunguza sehemu zote, hadi chooni, akakuta hakuna mtu, akarudi ofisini kwake huku akilaani, kujiotezea muda wake.

Akachukua makabrasha mbali mbali na kuyaweka kweney kabati, na alipohakikisha kuwa kila kitu kipo sawa, kwa ajili ya mwenzake ambaye atakuja kesho yake kukaimu nafasi yake, kwani yeye alishaomba likizo, likizo maalumu kwa ajili ya mambo yake,

‘Hii likizo ndio kwaheri, maana nikitoka hapa naenda kuanzisha maisha mapya, kurudi hapa ni kipindi maalumu, kusaidia, na kujipigia debe, maana demokrasia ndio inakuja , usipojiandaa nayo, utaachjwa kwenye mataa, unafikiri nani atakuwa kiongozi, kama sio sisi matajiri wan chi hii…hahaha…’akasema huku huku akiangalia fomu ya likizo yake siku akiitayarisha.

Leo ilikuwa siku ya kukabidhiana na mwenzake, lakini kukatokea dharura, mwenzake hajafika bado, kwahiyo ikabidi abakie ofisini akimalizia mambo yake, na ni kawaida yake kutoka ofisini usiku. Akaangalia saa yake, akakuta muda bado sana, lakini hata hivyo hakupenda kuendela kuabkia mle ofisini, ofisi alishaiona kama inanuka damu.

Alipohakikisha kuwa kupo salama , akarudi ofisni na kukaa kwenye kiti, lakini kila alipotuliza akili , akawa anhisi kuna kitu kinatemebea nje ya ofisi, hisia zake zikamtuma hivyo, na yeya amekuwa kwenye hulka hiyo, na isitoshe amekuwa kweney hiyo ofis kwa muda sasa, kama hakuna watu, akituliza kichwa huwa kama kuna mtu anatembea nje ya ofisi anasikia nyayo zake kihisia, na mara nyingi imekuwa ni kweli.

Akataka kuinuka kutoka nje kuangalai tena, lakini akaona haina haja, hata hivyo hakuwa na amani moyoni, kiti kilikuwa hakikaliki, akawa kila analoshika linakuwa halishikiki. Mwishowe akachukua simu ya mezani na kumpigia mmoja wa watu wake ili kupoteza muda, simu ile ikawa inaita tu haipokelewi, hapo akazidi kuchanganyikiwa, akajaribu kumpigia tena huyo mtu, lakini hali ilikuwa ile ile, akaona ajaribu kumpigia mtu mwingine, nayo kwanza hakupokelewa, na baadaye ikapokelewa alikuwa ni mke wake;

‘Vipi hakuna mtu aliyekuja huko kuniulizia..?’ akauliza, na alipoambiwa hakuna mtu, akahema kidogo, na kukaa kwenye kiti akaangalia saa yake ya mkononi, halafu akainuka kwenye kiti, na kwenda kwenye kabati kubwa lililopo kwenye ukuta, akalifungua kwa namba maalumu, likafunguka taratibu, akawa analiangalia jinsi linavyojifungua, lilipokuwa wazi, akaangalia kwenye moja ya droo, na kuifungua kwa namba vile vile, humo akakuta kikasha kidogo na kukitoa nje,

‘Sasa naona hakuna haja ya kusubiri, muda ndio huu huu, ngoja…..’akakifungua kile kikasha na kutoa, kikadi kidogo cha komputa, ambacho kinahifadhi kumbukumbu, akakiangali kwa makini, akachukua pochi yake na kuifungua , akakiweka humo ndani.

‘Huu ndio utajiri wangu , hapa hagusi mtu, akakitoa kingine na kukiweka mezani, akakiangalia kwa makini na kusema;

‘Huu ndio mgawo wa watu wangu, lakini wote….nani kabakia, oooh, huyo ….sijui yupo wapi kwa sasa, kama nikimmaliza, kila kitu changu, …na nisipommaliza nitakuwa kwenye matatizo…..’ akasema huku akikiangalia kile kikadi, akakirudisha kwenye kile kikasha, na akainuka kikirudisha kwenye kabati, …lakini akasita , akakiweka kile kikasha mezani na kugeuka akatembea hadi kwenye dirisha,…

Akawa kasimama akiangalia dirishani kwa muda, ghafla akahisi kitu, akageuka na kuangalia mlangoni, kabla hajafanya lolote akakiweka kile kikasha kwenye ile droo, na kufungua kidroo kingine cha mezani na kutoa bastola yake, akafungua sehemu ya risasi , akakizingusha kile kitufe kinachokaa risasi, halafu akafungua kidroo kingine na kutoa kiboksi kilichojaa risasi na kuzijaza ndani ya ile bastola.

Hakutosheka na hiyo, akaona hiyo haitamsaidia sana, akaangalia kwenye sehemu anapoweka silaha zake maalumu akaikuta ile bastola yake, hii alipewa kama zawadi akiwa mafunzoni huko Marekani, hiyo ndiyo aliyoitka mwenyewe akasema kwa sauti ndogo; .

`45 ACP Chief's Special — Model CS45…..’ Akaiangalia kama imejaa risasi, alipoona imejaa akaguna na kutoa sauti ya kama ya simba, halafua akasema;

‘Nikiwa na kitu kama hiki sina wasiwasi, huyu ndiye mshirika wangu, ….’akasema huku akiishikilia ile bastoa kama anamlenga mtu mlangoni, akatulia kwa muda akama anamsubiri huyo mtu atokee,….

Akiwa kaishikilia ile bastola, mawazo yake yakaenda mbali sana akawa anawaza mipango yao ilivyokwenda hadi alipofikia, na kila mara aliziona sura za wenzake alioanza nao hiyo mipango, ambao wengine ndio waliokuwa waasisi wa mipango hiyo, lakini wengi wao hawapo hai, akajaribu kuzikariri baadhi ya sura ambazo aliziona zikipita akilini mwake kama mtu anyeangalia picha mbele yake, na kila sura iliyopita. Ikawa kama inamsuta yeye kuwa ndiye aliyesababisha wao kuuwawa, na hapo wasiwasi ukaanza kutanda moyoni mwake, wasiwasi na huzuni, lakini mwishowe akajipa moyo na kusema;

‘Hii ni vita, huwezi kutarajia kuwa umekwenda mstari wa mbele vitani na bataliani yako, halafu utarajie kuwa mtarudi wote salama, yapo mawili , kufa au kupona, …… wapumzike vyema huko walipo, na nawashukuru sana, siku nyingine muwe waangalifu….’akasema huku akifungua kabati na kutoa kile kikasha alichoweka kile kikadi, na kutabasamu, halafu akaongezea kusema;

‘Sasa kilichobakia ni sisi tuliobakia kuangalia nini cha kufanya…nashukuru sana kwa juhudi zenu, huenda hii ikawa ni njia njema ya kuanza maisha mapya, nami nitawaombea kwa hali na mali, nitawasaidia watu, nitajenga mashule, nita….kuwa kiongozi bora, …..sasa, …. nitafanyeje zaidi ya hayo…’akasema na kuiweka ile bastola mezani na maandishi yake yakawa yapo juu yakisomeka;

'45 ACP Chief's Special — Model CS45…..'

huku akitoa pochi lake na kulifungua tena na kukitioa kile kikadi kingine ambacho ndicho chenye hazina kubwa, na kukiangalia kwa makini, baadaye akakirudisha kwenye pochi, akalifunga pochi lake na kabla hajaliweka ndani ya briefcase yake, akasikia mlango ukigongwa;

`Nani tena huyu…’ akasema na kuiangalia ile bastola yake pale mezani, akaichukua ile bastola na kushikilia mkononi, akasogea pale mlangoni, kabla hajafungua, akageuka na kuichukua `briefcase’ yake na kuiweka kwenye kabati, akalifunga lile kabati, na kusubiri kidogo, alishangaa huyo mgongaji mbona kagonga mara moja halafu akatulia.

Muda ulivyozidi kupita ndivyo alivyozidi kupata mashaka, akawa anajiuliza ni nani huyo aliyegonga mara moja tu, halafu akae kimiya, …akaona kwanini asubiri tu, kwanini asifungue mlango mwenyewe akahakiki, na kuangalia ni nani,…akasogea mlangoni na taratibu kama vile sio mlango wake aliouzoea, akaufungua, kwa haraka na huku bastola ikiwa mkononi…hakuna mtu….sasa alikuwa na uhakika kuwa kuna mtu nje ya ofisi yake, na hajui ni nani na aliingiaje bila walinzi wake kujua…

‘Hivi nani huyo ananichezea akili yangu, anakuja na kugonga mlango mara moja halafu anaondoka….’akasema kimoyo moyo, akasogea na kutoka nje ya ofisi, akaangaza huku na kule, kwa muda, ilikuuwa na uhakika sio walinzi wake, kwani kama ni mlinzi asingeliweza kuja kwake mara moja bila kumpigia simu, kwahiyo huyo aliyeingia atakuwa ni mgeni, atakuwa ni mtu ambaye sio mlinzi wake, na aliye na tabia ya kuja kwake moja kwa moja, …..ni….oh, akakumbuka,….mwili ukamzizima….

Alipokumbuka hivyo, moyo ukalipuka kwa wasiwasi, moyo ukaanza kumwenda mbio, akageuka huku na kule, bastola mkononi, ….akatizama kushoto na kulia, huku akiwaza enzi zake akiwa msituni,…hali kama hiyo ukiwa msituni na unajua kuwa maadui wamekuzingira na iliyobakia ni kupigania roho yako, ….hapo kila sehemu ya mwili inakuwa na hisia zake, …..

Alisikia kitu, ….akageuka haraka na kutizama upande wa pili, hakuona kitu, lakini akili na hisia zake zilimuashira kuwa kuna kitu, na hisia za mwili wake, zilimtuma kuwa kuna mtu anamwangalia, lakini atakuwa upande gani, na hapo aliposimama hakuna kinga yoyote, akaangalia huku na kule, halafu akaruka upande wa pili, na kuwa mbali kabisa na mlango wa ofisi yake, hapo aliposimama, kuna kinga, na anaweza kumuona mtu atakayeingia ofisini kwake, akasubiri…

Tangu awe mkuu, kazi ya kusubiri imekuwa sio fani yake tena, kazi hiyo alikuwa nayo kipindi akiwa mpiganaji, sasa hali ile ya kusubiri inampa shida sana, hana mazoezi, mwili umejaa mafuta, akajikuta kama shinikizo la damu likipanda, akaona hataweza kuendelea kusubiri zaidi, kama kuna mtu ana nia mbaya na yeye atamuoana tu,…kwanza anamshirika mkononi, …… akaona atoke pale alipokuwa na mara simu yake ya ofisini ikalia,….ilimshitua sana, karibu afyatue risasi.

Moyoni akajiuliza atakuwa nani huyo anayempigia simu muda kama huo, hajui kuwa yupo vitani, na akaona haina haja ya kujibanza pale alipokuwa, akijitokeza na kusimama mbele ya mlango,…alijua kwa kufanya vile ni hatari kwake, sasa afanyeje, na simu bado inaendelea kuita, akaona ajitose aende akaisikilize hiyo simu. Ile anatoka pale hatua moja, akasikia kitu kikitua nyuma yake, na kabla hajageuka, alisikia kitu kama gunia limetua kifuani kwake, na teke likapiga mkono ulio na bastola, bastola ikamtoka na kuserereka mbali na yeye.

Kabla hajajiweka sawa, akajikuta akigongwa na vitu kama mawe kichwani , akajua hizo ni ngumi za mpiganaji, hakuna mtu mwenye ngumi, kavu kama hizo, …zikigonga mahali zimeacha atahari….kweli akaanza kuviona vinyota…..

Akajitutumua, …..‘Nani wewe na unataka nini…’akasema na huku akijitutumua, na kuirudisha hali yake ya kikomandoo, na hapo akageuka chui aliyejeruhiwa, alipogeuka kumwangalia adui yake akakutana na teke, akalikwepa, akasogea pembeni, ili aweze kujenga nafasi kati yake na adui, alipomuona vyema, kwanza alishangaa, mbona ni mwanamke, hapana, huyu sio mwanamke, atakuwa kava nguo za kike, ngoja kwanza nipambane naye, ….

Hakukawia kufanya vitu vyake, na alijua kuwa ni bora haraka, kwani pumzi ya muda mrefu hana, akajirusha na kutupa mateke mawili ya harakaharak moja lilimkosa huyo adui , la pili likafanya kazi yake, na matunda yake akayaona, kwani adui ambaye hakutarajia hivyo akayumba na kusimama pembeni.

‘Kumbe bado wamo, ….’akasema adui, sauti ikamuumbua kumbe sio mwanamke, kumbe ni….

‘Sikiliza Kinyonga, hakuna muda mchafu wa kupimana nguvu hapa, hapa sasa hivi hakukaliki, tunahitajika kuondoka hapa haraka iwezekanavyo, maana ninavyohisi huyo mpelelezi yupo njiani…’akaseam huku akihema, na kuhisi maumivu ya kifuani.

‘Hahahaah…hilo unaliona sasa, wakati ulishajiandaa kukimbia peke yako, unafikiri sijui kuwa umeshakata tiketi ya kukimbia ncho ukijidai unakwenda likizo, halafu unataka kukimbia na mali za watu, ….ulifikiri sitajua kuwa wewe umekuwa ukituzunguka, unauma huku unapulizia, nisingelijali hilo, kama usingeligusa damu yangu, nami nimeahidi kuwa kwa yoyote aliyegusa damu yangu, naye atamwaga damu yake….hiyo ni ahadi kwangu na nimeitoa kwa wazee wangu….’akasema huyo adui yake.

‘Damu gani hiyo, mbona sikuelewi…wazee….kwani …mbona unanichanganya….?’ akauliza mkuu huku akionyesha mshangao.

‘Hutanielewa, maana siku zote ndio mtindo wako, una uma huku unapuliza, ….umenigusa pabaya, na nilishakuambia huko usipaguse, lakini wewe ukawa mkaidi, sawa wewe ni bosi wangu, lakini ubosi huo umevuka mpaka, leo sikutambui tena kama bosi wangu, ….ina maana toka sasa wewe sio bosi wangu tena, wewe ni adui yangu, ama zako ama zangu….’akasema huyo adui na kuruka juu alipotua alikuwa kasimama karibu sana na ile bastola.

Na mwenzake akafanya hivyo hivyo haraka kabla mwenzake hajaichukua ile bastola, ikawa piga ni kupige, kila mmoja akijitahidi kuichukua ile bastola, na bahati mbaya wakaipiga mateke ikaserereka na kwenda mbali na walipokuwa wakipambana.

‘Sikiliza nikuambie, huyo unayemzungumzia kama ndiye, ulishaniambia kuwa sio ndugu yako, unakumbuka nilikuuliza mara nyingi ukakana hilo, na kuna sababu za msingi zilizonifanya nimuondoe duniani, alikuwa kagundua siri kubwa sana ambayo kama ningelimuacha angetuangamiza sote, na…..’akajitetea mkuu huku akihema kwa wasiwas.….

‘Sina muda wa kukusikiliza kwanza ili tueleweni kwa kuchelewesha kifo chako, kipo wapi kikadi cha amana zetu, maana wewe ndiye unayekihifadhi, na najua lengo lako nikuondoka nacho, sasa hicho kinaweza kuahirisha umauti wako kwa muda, kipo wapi…’akauliza huku akitizama kwa jicho la kujiiba wapi ilipo ili bastola, na mwenzake alikuwa na lengo hilo hilo.

‘Sikiliza, kama tutaendelea hivi, ujue askari wangu watajaa humu na kila kitu kitaharibika, sasa twende ndani tukaongee , hapa hapatufai…’akasema huyo mkuu, akiwa na malengo yake.

‘Twende, …huko huko, sogea mbele, tangulia huko si ofisni kwako, unajua wapi ulipoweka bastola, ukijaribu ujanja, tutakufa sote…..’akasema adui huku akionyesha kitu mkononi.

‘Nini hiyo , acha uoga wako, ….’akasema mkuu.

‘Hili ni bomu, na hii hapa ni ufungua, nyumbani kwako kuna bomu jingine, likifyatuka hili la hapa linafuatia lililopo nyumbani kwako, familia yote inateketea, kama unabisha mpigie simu mke wako….’akasema adui.

‘Sikiliza hizo sio sifa za mpiganaji, kwanini unataka kuwaumiza watu wasio na hatia….wake watoto, hawastahili kuumizwa….kaa tuongee…’akasema mkuu kwa wasiwasi.

‘Kuumiza wasio na hatia unaona kwa upande wako, huyo jamaa uliyemua karibuni ambaye ni damu yanu ni askari yule, au kwako wasio na hatia ni wanawake na watoto, tu, unasahau kuwa kuna raia wasiojua mambo hayo, sio askari…tena unaua kinyama kwa kuvizia kwa nyuma, askari gani wewe, mwoga….hilo sitakusamehe , wewe nipe hicho kikadi, halafu maongezi yatafuata baadaye….’akasema adui.

‘Kikadi kipo hapa , kwanza nipe ufungu wa hilo bomu, pili tuelewane, sin aubaya na wewe, wewe ni mshirika wangu, nimekufundisha mwenyewe na …..yule mwalimu wako yupo wapi, ….maana ulisema una mwalimu wako, ….una visa wewe….’akasema huku akipoteza malengo, ili afike kwenye droo za kabati atoe bastola yake.

‘Usijifanye mjanja, usisogee kabisa huku, kama …..’ Wote wakahisi kuna mtu mwingine zaidi yao, wakageuza kichwa kuangalia mlangoni, na hapo hapo mkuu akapata nafsi ya kuvuta droo akitaka kuitoa ile bastola yake, na mwenzake alishaiona ile hali, lakini hata hivyo kuna mtu anakuja uelekeo wa mlango, wakaangaliana, ….

NB : Ni nani huyo, je nini hatima yake....kidogo kidogo hujaza kibaba mwishowe tutakuta tunamaliza kisa chetu, hivyo hivyo kwa ugumu tutafika.

WAZO LA LEO: Dhuluma haidumu…

3 comments :

Anonymous said...

Tatizo unachukua muda sana kuandika sehemu mpya, hata hivyo nimekukubali, wewe ni James Hadley Chase wa Bongo

Anonymous said...

Tatizo unachukua muda sana kuandika sehemu mpya, hata hivyo nimekukubali, wewe ni James Hadley Chase wa Bongo

Anonymous said...

Tatizo unachukua muda sana kuandika sehemu mpya, hata hivyo nimekukubali, wewe ni James Hadley Chase wa Bongo