Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, February 2, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-78 hitimisho-22
‘Kwa maelezo ya Rose, nahisi kuna jambo ambalo tunahitajika tulifanyie kazi mkuu…’akasema yule mpelelezi huku akimkabidhi mkuu wake jarida la uchunguzi wake. Mkuu wake alilipokea na kuanza kulifungua huku akimsikiliza kwa makini mtenaji wake.

‘Rose altuambia kuwa, huyo mtu aliyekutana naye huko India, kuna ufanani fulani wa kimatendo na yule mtu aliyekutana naye kule hotelini siku za nyuma, kwa ,muondoko wake, na baadhi ya vitendo vinalandana, ingawaje alikiri kuwa hana uhakika wa moja kwa moja, lakini kitu ambacho alikinasa ni mwendo wa huyo mtu unafanana, anavyotembea, wepesi wake, na macho…anasema vinafanana kati ya wawili hawa…’akasema mpelelezi.

‘Lakini sura ni tofauti au sio, huyo wa hukoIndia hafanani kabisa kisura na huyo wa huko hotelini hapo utaliwekaje kisheria, na wanauhusiano gani na mtu wetu tunayemzungumzia…yaani Docta Adam,….’akawa kama anauliza, lakini kabla hajatulia vyema akaendelea kusema;

‘Na hapa kweney maeelzo yenu, mumesema hata alama za vidole hazifanani, kwahiyo hawo ni watu tofauti kabisa…kufanana kwa miondoko sio hoja, watu wanatembea sawasawa kama maaskari kwenye gwaride, umesahau hilo, na pia watu hufanana, kama walivyosema watu wamezaliwa wawili wawili duniani…bado nahisi kuna jambo limejificha, tunahitajika kulifanyia kazi, kabla ya kufikia kwenye hitimisho hilo….’akasema mkuu wa usalama.

‘Mkuu dunia hii ya sasa sio ya jana, mimi bado nina mashaka, siku hizi mbinu , utaalamu umepevuka, nahisi nionavyo mimi, huenda huyo mtu ni mmoja, na ….sisemi nina uhakika mia kwa mia, hapana, ila hisia zangu zinanituma hivyo, cha muhimu…..’akatulia kwa muda huku akiwa kashika kichwa kwa kidole kimoja cha mkononi, halafu akaendelea kusema ‘Njia pekee ya kupata uhakika ni kumkamata huyo mtu, mengine yatajitokeza yenyewe….’akasema mpelelezi.

‘Kumkamata sio hoja sana, tunaweza tukatoa kibali hata leo, lakini unatoa kibali kumkamata nani… huoni hapo kun utata, utaandika jina gani, ili liendane swan a huyo mtu, ukumbuke, sheria sasa zinafuatiliwa kwa makini….’akasema huku akilifunika lile jarida lenye kumbukumbu za uchunguzi.

‘Najua hilo mkuu, ndio maana nimesita kuchukua hatua hiyo, lakini kila nikiwaza zaidi, naona tusipofanya juhudi za ziada tutachelewa na huyu mtu anaweza akatupotea kabisa, huyo huyo tukimkuta , na tukahisi ana tabia, mienendo, za huyo aliyemuhisi Rose, tumkamate angalau kwa masaa machache, tutagundua jambo tu…’akasema yule mpelelezi.

‘Lakini ukumbuke hawa watu wenye hela zao wanatumia mawakili, …na huwezi ukampelekea mwanasheria wetu wa serikali kesi isiyo na vizibiti kamlifu, na hata ukivileta, hatakubali kuvipokea kama vimepatikana kwa njia isiyo halali, …ukumbuke, ukivurunda, kibarua kimeota majani, sikatai kumkamata huyo mtu, ni wajibu wetu kumkamata mtu utakayemshuku kuwa ni muhalifu, lakini hakikisha una vigezo vya kumkamata….’akasema mkuu.

‘Hilo niachie mimi, wewe nipe kibali bubu, hakihitaji mshukiwa, hakihitaji jina kwanza, baaada ya hapo utaona jinsi gani tutakavyoyaweka mambo sawa,….nina uazoefu na haya mambo, huyo mtu nina wasiwasi naye, atakuwa mtu mmoja anatuchezea akili zetu tu, na nahisi kama tukimkamata huyo mtu, tutakuwa tumemaliza kazi, kwani inavyoonyesha yeye ni ufunguo wa kundi hilo, na yeye ni ufunguo wa kumkamata docta Adam ….’akasema mpelelezi.

‘Sawa, kibali hicho nitakupa, ….kuna kitu kingine je umeshafanya mpango wa kuongea na huyo msichana Rose, nasikia wanatarajawa kuwasili hapa nchini karibuni na yule mgonjwa, ambaye nasikia kapona…au akitoka huko anaweza asirudi huko, ataelekea huko anakosma kwanza…?’ akauliza mkuu.

‘Watarudi wote hapa, kama nilivyosikia kwani kwa taarifa za kifamilia , watakutana kwanza hapa, na baaaye ndio huyo binti atakwenda huko anakosoma, wana mambo yao ya kifamilia wanataka kuyamalzia kabla hajarudi huko chuoni, na una habari kuwa huyo Rose ni mja mzito..?’ akasema na kumuuliza mkuu wake.

‘Eti,…hapana sina habari hizo, una uhakika na hilo , ..mmh, nani kampa hiyo mimba huyo binti, maana yule binti ni mgumu, alishawakataa wanaume kibao….siamini…lakini hayo hayatuhusu, ni mambo yao ya ndani, au sio…?’akasema mkuu.

‘’Mkuu ujauzito wa Rose una jambo ambalo huena likatusaidia, ndio maana nikakumabia hilo, sikuliongelea kama kujua mambo yasiyotuhusu, …kama hiyo mimba ni ya docta Adam, lazima atajitokeza kumfuata fuata huyo binti, na hata kama siyo yake, tunaweza kupenyeza maneno ya fitina, akahisi ni mimba yake….na lazima atamfuata huyo binti, huoni kuwa tunanweza kumtumia huyo binti kumpata huyo jamaa kwa njia hiyo, ikizingatiwa kuwa huyo binti keshakubali kuisaidia serikali yake…’akasema mpelelezi.

‘Una uhakika gani kuwa waliwahi kutembea naye…?’ akauliza mkuu.

‘Nina uhakika gani, kuna siku huyo binti alilalamika kuwa huyo docta kamuwekea madawa, na kumbaka….hili nililipata kwa siri sana, na …sina uhakika sana, ila baada ya hapo kukawa na uadui mkubwa sana kati ya huyo binti na huyo docta, nililipata hili wakati nafuatilia nyendo za wale watu wa msituni…’akasema mpelelezi.

‘Lakini muda , hiyo mamba na kipindi hicho vinaendana kweli…?’ akauliza mkuu.

‘Hilo nimelipigia mahesabu, vinaendana sana, nahisi hata huyo binti bado ana mashaka ya hiyo mimba, hajui kuwa ni ya nani hasa….., sijalipat akaribuni, kwasababu halikuwepo akilini mwangu mwanzoni kwasababu sikujua kuwa huyo binti ni mja mzito..’akasema mpelelezi.

‘Lakini swali kubwa hapa, huyo docta Adam, ni nani, na anamafungamano na familia ipi, kwasababu katika kumbukumbu zetu inaonekana, kuwa huenda ni hawa Wahutu au Watusi, waliohamia na kuishi humu kwetu siku nyini, na hata maumbile yao yanafanana fanana...ndio matatizo haya, nchi ikigubikwa na machafuko, hata utaratibu wa uhamiaji unakuwa mbovu, watu wanaingia na kusihi bila taratibu muhimu, ina maana hana familia yoyote hapa kwetu…?’ akauliza mkuu.

‘Mhh, hilo tulilitizama kihivyo tu, na tukahitimisha kuwa utaifa wake ni wa hapa, hatuna kigezo cha kusema sio mtu wa hapa, na kama ulivyosema sheria ina mambo yake, hatukutaka kuingilia upande huo kwanza, ingawaje linafanyiwa kazi…’akasema mpelelezi.

‘Linafanyiwa akzi kwa vipi, msiruke kitu muhimu kama hiki, kama sio raia wa nchi, hamuoni, kuna tatizo hapa, mlifikia wapi kwa hili, …?’ akauliza mkuu kwa sauti ya ukakamavu.

‘Hilo mimi mwenyewe nilikwenda hai alipokuwa akifanyia kazi, cha ajabu hakuna kumbukumbu zozote za historia, faili lake linaonyesha maelezo ya utaalamu wake, na majukumu yake, na hutaamini, sehemu nyingi zimetumia jina `Docta Adam, ..’ hakuna jina la baba, jina moja tu Adam, haya vyeti vyake vya shule, hakuna, hakuna hata nyaraka moja inayomuelezea historia yake …..hapo ndipo nilipoanza kuingiwa na wasiwasi…’akasema mpelelezi.

‘Halafu…?’ akauliza mkuu.

‘Nikawafata hata wadhamini wa hiyo hospitali, unajua nini walichosema, wao wanamjua kama docta Adam,…ThomasAdam…nikashangaa, haya majina, wao wanasema hawakuwa wakijali sana kuhsus hayo majina , wao wanamtambua sana kama Adam. Kwa uapnde wao walichojali ni kuwa yeye nimtaalamu, kama tunahitaji kumbukumbu zaidi tuzifuate huko ofisini kwao, wao hawaingilii sana mambo ya ndani, wakanionyesha hata mikataba yao ambayo haiwaruhusu kuingilia mambo ya ndani ya utendaji….nk…’akasema mpelelezi.

‘Inatia wasiwasi, nahisi hata hawo wadhamini wanajua , ni wahusika, lakini ndio wazee wetu, ndio wengi waliopo serikalini, ukiwausa hapo, mambo yatafika hadi ngazi za juu, lakini hata hivyo tunahitajika kuwachunguza na wao mmoja baada ya mwingine, mlifanya hilo…?’ akauliza mkuu.

‘Kama tusingelifanya hilo tusingeligundua kuwa Docta Adam, ni mhusika mkuu wa kundi hilo, kwa kupitia uchunguzi wetu, ndipo tukagundua kuwa wahusika wengi wa kundi hilo ni wataalamu, ni watu walioajiriwa, ni watu wenye makampuni yao, …huwezi hata kuamini kuwa watu kama hawo wamejiingizaje kwenye maswala ya kivita….’akasema mpelelezi.

‘Nchi ilishaingia kubaya, watu wengi walishachoka, na tamaa zao zikaona ni bora kujiiniza huko, huenda wakachuma mapema…lakini za mwizi ni arubaini….kwahiyo hakuna kumbukumbu zozote za familia ya huyu jamaa, na hata hawo wazee wanasema hawamjui zaidi ya kikazi, ..haiwezekani..?’ akasema mkuu.

‘Wanasema hivyo, …na wengine ndio hawo walidai kuwa alikuwa mkimbizi,aliyeishi humu akiwa mdogo, akasoma humu, hadi kufukia hatua hiyo….na hilo lilisemwa na wazee wengi…na tulipojaribu kuuliza ni nazi alimpokea, hakuna aliyeweza kusema lolote….,hapo, nikaundua kuna jambo, nikaanza kufuatilia makazi yake, …hakuna hata chembe cha kumbukumbu, ni makini ajabu, alipogundua kuwa anachunguza, akayeyeka kiaina, toka siku hiyo hatujamuoana tena.

‘Mhh, ina maana kweli alikuwa makini kiasi hicho, …hapana, fanya jushudi tumpate, maana hata mimi ninakuwa na hamu sana ya kumjua, kama ukishindwa nitaiafanay hiyo kazi mwenyewe….’akasema mkuu.

‘Mkuu hakuna kushinwa jambo, sijawahi kushindwa…wewe tulia mkuu, mwisho wa siku tutajua kila kitu. Kwanza ni kumpata mhusika,,..na mkuu unasemaej kuhusu ushauri wa Inspekta wa nchi ya jirani, yeye kasema tutoe tangazo kuwa tunahitaji usuluhisho, ili kukwepa umwagaji damu zaidi, ….’akasema mpelelezi.

‘Hayo ni mambo ya kisiasa, hayatuhusu, hata wakitoa tangazo kama serikali, sisi wajibu wetu upo pale pale, mhalifu lazima afiksihwe kwenye vyombo vya kisheria, sasa mahakama ndio itaamua, …sisi tufanye kazi, na wakijitokeza, ni heri kwetu, maana hapo tunawakamata tunaikabidhi mahakama, wao watajua nini la kufanya…’akasema mkuu.

‘Sawa, mimi siku ya leo natafuta ukweli kuhusu huyu Docta Adam, nina hamu sana ya kumjua, na nina uhakika nitamgundua tu siku si nyingi, sijawahi kusumbuliwa na mtu kama huyu…kila mara najiuliza huyu docta Adam ni nani, ametokea wapi,na katowekea wapi, haiwezekani apotee kimiujiza, au ni kinyinga,….mkuu nitakupa jibu siku si nyingi….’akasema mpelelezi na kuondoka.

‘Sawa nitashukuru kama ukimleta hapa na kuniambia huyu ndiye docta Adam,…Adam, mtu wa ajabu sana…’akasikika mkuu akilirudia hilo jina mara kwa mara.


‘Ndugu yangu, usitake kujua nipo wapi, ila ninachotaka kukufahamisha ni kuwa nina mkutano mfupi na wewe, nitakutana na wewe popote pale jiandae….’Tajiri mzungu alikuwa akijiuliza mara kadhaa kauli hii, ina maana ndugu yake hajakamatwa, na tetesi zilizoenea ni kuwa keshakamatwa.

Siku alipotua uwanja wa ndege aliwasiliana na wakili wa familia kuhususian na hilo, wakili wake alimwambia hana uhakika na kukamatwa kwa Docta Adam, na amejaribu kufauatilai vituo vyote hajawahi kumuona mtu wa namna hiyo, na alifanya hivyo kwa tahadhari maana waliogopa kuulizwa kuwa wanamjuaje huyo mtu..

‘Wewe kama wakili, hawana mamlaka ya kukudodosa dodosa eti wakuulize kwanini unataka kumdhamini mtu huyo, wewe unachotaka ni pesa, kwahiyo unaweza ukamfanyia kazi mtu yoyote au sio..?’

‘Na sio lazima kwa jina hilo, nahisi anaweza akatumia jina jingine, hata hivyo mmh, kuna mtu mwingine ambaye naye ni muhimu sana, unatakiwa kujua kuwa naye kakamatwa au la, kama kakamatwa unahitajika kumdhamini….’akatulia kidogo

‘Naye ni mshukiwa katika mambo haya ….?’ Akauliza mpelelezi.

‘Kama asingehusika na mambo haya nisingekutafuat wewe, wewe ni mtaalam wa kesi hizi, kesi za kawaida huwa sikupi wewe, ndio maana unalipwa pesa nyingi au sio..?’ akasema Tajiri kwa nyodo.

‘Ni kweli lakini kwa kesi ya watu kama hawa unatakiwa kuchukua tahadhari kubwa sana, nitakufahamisha kama nikimpata huyo mtu, …umesema anaitwa nani..na kazi yake ni ipi..?’

‘Anaitwa ThomasAdam,… usitake zaidi, wewe ukiona jina hilo nifahamishe haraka….

‘ThomasAdam, haya majina yameungana, au ni mawili tofauti…?’ akauliza

‘Yameungana….’akasema Tajiri

‘Jina la aina yake kweli, ThomasAdam, na huyo mwingine Docta Adam, kwanini Adam, Adam….ok, nitatafuta majina hayo yote, hata nikiona jina Thomas, sawa, hata nikiona jina Adam…yote nitakuambia, … kama kakamatwa mtu mwenye jina hilo mbona ni kazi rahisi tu kumpata…’akasema wakili.

Sawa akasema Tajiri na kuingia ofisini kwake, alipofika mezani tu, simu ikaita, ….akaipokea haraka na kusikiliza.

‘Mnasema mpo uwanja wa ndege, mbona hamkuniambia kuwa mnafika leo, ….ina maana umekamlisha ile kazi, mbona haraka hivyo…ooh, sawa, chukueni usafiri, sina muda wa kuja kuwapokea, sawa mke wangu, baadaye….’akakata simu huku akikunja uso kwa hasira. Na mara kabla hajatulia mlango ukagongwa, akashituka na kuinuka kwenye kiti, akafungua droo ya meza, na kutoa bastola yake…na kwa pembeni kwenye ukuta, akahisi kuna kitu, mwili ukamsisimuka, ….akageuza ile bostola kule ukutani, akataka kumimina risasi kwa hasira, lakini kabla hajafanya hivyo mlango ukafunguliwa…..

‘Wewe ni nani unaniingilia ofisini bila taarifa…’akasema kwa hasira huku akigeuza macho kuangalia ukutani, alichokiona kilimafanya aishiwe nguvu kabisa….akaanza kutetemeka.


NB Je huyu ni nani aliyeingia, ...mbona mzee mzima anaangalia ukutani na kutaka kuzimia, mambo hayo ya ajabu, ukiwambia huwezi amini, ...lakini yalitokea, Wazo la leo: Subira huvuta heri, usitaharuki ukisikia kila jambo, fanyia uchunguzi kwanza, kabla ya maamuzi, ingawaje lisemwalo lipo, kama halipo laja...
Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

mkuu usituone kimia tupo

Anonymous said...

duu kweli wewe mtunzi