Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, December 20, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-67 Hitimisho-11
‘Wow, siwezi kuamini kuwa nilikuwa na ndugu, tena ndugu mwenyewe ni pacha mwenzangu, nikikuangalia ni kama najiangalia mwenyewe kwenya kiyoo, …hebu nikuulize kweli utamsamahe mama, kwa haya waliyotufanyia …mimi nampenda kama mama yangu, kwasababu kanibeba tumboni miezi tisa, lakini hakunilea,…utashangaa ni kikuambia kuwa hakuwahi kunilea, sikuwahi kunyonya ziwa lake… lakini kwa hisia zangu, nahis alifanya hivyo tu kwasababu nimezaliwa kwake, na hakuwa na jinsi ya kufanya, na huenda kama angelipata nafasi angeliitoa hiyo mimba…’akasema Rose.

‘Usiseme hivyo ndugu yangu, hujui kwanini walifanya hivyo, lazima kuna sababu, sizani mtu na akili yake anaweza kuzaa halafu aamue kutelekeza watoto wake bila sababu ya msingi…’akasema Maua na kumwanglia Rose machoni, huku moyoni akifurahi, alifurahi kwasababu kampata ndugu, lakini zaidi alifurahi kuona anafanana na huyo ndugu yake, na kwa kila kitu, akajiulza moyoni, ina maana kumbe mimi ni mzui kiasi hicho.

Na kabla Rose hajasema kitu Maua akaendeela kuongea kwa kusema `Ni jambo jema tuwakubali tu kama wazazi wetu, mimi kuna kipindi niliiumia sana, pale nipoambiwa kuwa shangazi sio mama yangu, sikuamini kabisa, niliumia sana moyo wangu, nikasononeka, hata kuuliza ina maana wazazi wangu wamekufa, nikaambiwa hawajakufa, sasa kwanini hawakunilea wao wenyewe, angalau kipindi cha uchanga ili niwaone, ili nijsikie nipo na mama yangu…’akasema Maua, na Rose akawa anamwangalia usoni, alijiona kama ndio yeye anaongea.

‘Unajua hadi kesho, mimi namuona shangazi yangu kama mama yangu, kwasababu alinilea nikiwa kichanga, akanitunza kile kipindi nikiwa mtoto mchanga, kipindi ambacho mtoto anatakiwa kuwa karibu na mama yake,na sikuona kuwa kuna mama mwingine zaidi yake, achilia mbali mjomba,ambaye nilimuona kama baba yangu, akirudi kazini namrukia kwenye mapaja yake ni kumuita baba umeniletea zawadi, basi anacheka na kuniambia mimi sio baba yako, niite mjomba,..basi kisema hivyo nakasirika, akiona nimekasirika, ananibembeelza na kuniambia basi niite baba, ipo siku utafahamu hilo…haya mwanangu chukua zawadi yako hii, hapo natulia nafurahi maana nipo na baba yangu, kumbe sio baba yangu, ni mjomba wangu…’ akasema Maua huku wote machozi yakiwa yanawalenga lenga.

‘Unajua nilipoambiwa na hata kujua kuwa kweli hawo sio wazazi wangu wa kunizaa, ilifikia mahali nikasema hata nikiwaona hawo wazazi wangu wa kunizaa, siwataki tena, ina maana gani kwao kama hawakutaka kunilea, kwanini wakakwepa majukumu yao yakunilea, …hili wazazi sijui walifikiria nini, kuwa kazi yao ilikuwa kututoa duniani ili waondoe uzia kama mtu kukamua jipu au ilikuwaje, nilijiuliza sana, lakini siku zilivyokwenda , nikaona haina haja, …nitawasamehe tu, na kuwakubali kama wazazi wangu,…’akasema Maua.

‘Halafu nikasikia kuwa hata mama huyo anayeishi na baba sio mama yangu, nikaanza kujiuliza mama yangu yupo wapi, amekufa, naikamuuliza shangazi , shangazi hakunijibu, alisema ipo siku atanijibu, nikawa sijali, kwasababu sikuwa na haja naye, wanini…kama isingelikuwa hili tukio, ambalo chanzo

‘Tutawasamehe sawa, lakini tunahitaji maelezo yenye kina, .. sitakubali kubali kirahisi hivyo, tatizo lako, kwa vile umelelewa kinamna yako, unashindwa kujua kuwa kuna haki za watoto…wanatakiwa kuzijua,na wewe ulihitajika kuzijua , lakini ungezijuaje wakati hukupata hata muda wa kusoma, na hata waliokulea, hawakulijua hilo..hilo ni tatizo …lakini sasa wanatakiwa kulijua, …sio kwa jaili yako tu, lakini hata kwa vizazi vijavyo,…’Rose akasema na huki akionyesha uso wa kutafakari, na Maua naye akawa anafanya hivyo hivyo, mawazo yao yalikuwa yakiwaza moja na bila kuambiwa wote wakaangalia eneo la tumbo.

‘Unajua Maua inabidi kabla ya kuwasamehe hawa wazazi wetu tujiulize maswali mengi, kwani sisi ni mayatima, kwani wazazi wetu hawajiwezi, hebu nikuulize huyo baba ni masikini, sizani kwamba ni masikini, nina hamu sana ya kumuona…najua wote wanajiweza,…’akaongea Rose na kumwangalia Maua ilia toe maelezo kuhusu baba yao, lakini alipoona Maua ansita kuongea lolote kuhusu baba yao, akaendelea kuongea na kusema.

‘Najua wote wana uwezo wao kabisa, lakini kwasababu zao wenyewe wakafanya hilo walilolifanya , sasa wanaona tumekuwa wakubwa, wenzao wameumia kutulea, wakataabika, leo wanajifanya kututafuta…ok, kwangu mimi sina matatizo, kwasababu ninaweza kusimama kwa miguu yangu mwenyewe, silaumu sana, …licha ya kuwa mama hakuwa karibu sana lakini kila nilichohitaji nilipokuwa mdogo, …kuacha matunzo ya kunyonya na kuwa karibu naye, nilipata…’akasema na kutulia.

‘Lakini najiliza kwa mfano kama wewe una kazi gani, ulisoma hadi kiwango gani, hiyo ni haki yako kuidai,ni haki yako toka kwa wazazi …na hili nitalihakikisha linatendeka, hata kama limechelewa, utapata haki yako yote toka kwa mama, mama ni tajiri, …unajua tajiri, mama anakwenda vikao vya serikali anatoa misaada, ile ya kujionyesha,..anasaidia mayatima, ile ya kujifagilia, lakini nyumbani kwake…mmh..sasa mtu kama huyo utasema hajiwezi, …hilo niachie mimi…’akasema Rose, ingawaje Maua hakuwa anataka lolote toka kwa mtu yoyote, alijali maisha yake kivyake.

‘Sasa kwa mfano unahitaji pesa kwa jili ya huyo mume wako, ..unamuona mume wako, pale kitandani, hajiwezi, unatakiwa kumhudumia, …nashukuru kuwa nimemsaidia mume wa ndugu yangu sitaumia sana…ingawaje nilimpenda sana, na hata pale, nilipogundua kuwa….’alipofika hapo akakatisha, akaona lile alilotaka kuongea sio mahali pake, kwani pale alipogundua kuwa yule mgonjwa ni mume wa ndugu yake, aliahidi kuficha mtu aliyempa hiyo mimba, alishaamua kuwa atailea hiyo mimba bila mzazi wa kiume,…hakutaka kabisa kuliweka hilo wazi kwa ndugu yake.

‘Hata pale nilipogundua kuwa huyo mwanaume kanitoroka…ile chuki ya wanaume ilitaka kunirudia, maana ndugu yangu nina mengi ya kukusimulia kuhusu hawa watu waitwao wanaume, lakini sio leo, hilo sio mahali pake, leo ni kuhusu hawa wazazi, …ila kiujumla, nilipoamuka na kuona huyu mwanaume kaondoka niliumia sana, …kwasababu yeye nilimuona kama mtu aliyekuja na kunitoa katika kiza cha chuki, chki kwa wanaume….’akatulia akiwaza jambo, lakini akaona asiendelee na hilo wazo.

‘Chuki kwa wanaume…kwani wao wanahusika nini na haya yetu…?’ akauliza Maua.

‘Unajua Maua , huyo mwanume, alikuwa ni mtu wa peke katika maisha yangu, …sikujua kuwa ni mume wa mtu…sikujua kabisa, kama ningelijua, ningelishajitoa, hata hivyo niliwaibika tu kama dakitari amtendeaye mgonjwa wake…’akasema Rose bila kujali swali aliloulizwa na Maua, huku akingalia pembeni.

‘Nilikuwa nimeamua kumpigania kwa nguvu zangu zote…nikijua kuwa huyo ndiye atakuwa mume wa maisha yangu, kumbe…ni shemeji yangu…balaah, ..’akasema Rose huku akiangalia pembeni, alikuwa akiwaza, itakuwaje kuhusu huo mzigo alio nao, lakini kama mume huyo alikuwa naye miaka miwili, sasa hiyo mimba ya mwenzake imetoka wapi, hakutaka kuliuliza hilo swali kwa muda huo, akatulia, …akamwangalia Maua kwa muda.

‘Sasa Maua hebu niambie huyo mume wako alikuacha, baada ya hiyo ajali, ni miaka miwili, kama sikosei mlikuwa hampo naye,…na ghafla akanitoroka, sijui kama alikua huko au vipi, tutamuuliza mwenyewe, mungu akijalia, au sijui…nashindwa hata kukuuliza hili swali, maana haliuliziki maana sizani kama mliwahi kuonana baada ya hapo, ili nikuulize kuwa aliwahi kuongea lolote akauambia nini kilitokea, kwasababu aliponitorokam sikujua kaenda wapi,…’Rose akawa anaongea huku akiwa kama anajiuliza mwenyewe.

‘Siku hiyo ambayo niliiona kama pigo, asubuhi nimeamuka, nakuta mgonjwa hayupo, mgonjwa ambaye niliamua kuwa sitamuachia mpaka nione muda wake,naamuka subuhi, hayupo, kaenda wapi haijulikani, niakasema basi, katoweka tena kama walivyonitendea wanaume wengine,…nikatamani kulia, nikashindwa, bahati ndio nikaondoka kusoma …nilipata taarifa baadaye kuwa kaonekana na hali yake ni mbaya, je alikwenda wapi, sijajua hilo kabisa, ila pale hospitalini ndio nikasikia kutoka kwa mama kuwa huyo ni mume wako…duuh, nilishituka, nilijikuta mwili ukiisha nguvu…sasa hebu niambie, ilikuwaje…?’ akauliza Rose.

‘Rose ni kweli,…lakini mambo yalibadilika sana, hasa ilipotokea hiyo ajali ya MV Bukoba, ilibadili kila kitu, sikutegemea kuwa itakuwa hivyo, ….unajua Rose, siku nilipopata hiyo taarifa, kuwa mume wangu ni miongoni mwa watu walioptea,….sikuamini kabisa, sikuamini kuwa kweli amekufa kwenye hiyo ajali, nilimuota, na hata kumuona kimawazo , akinijia kuonyesha kuwa yupo hai, niliteseka miaka miwili, ilifikia hatua nilitaka kujiua, …lakini nilipona, isingelikuwa huyo Maneno, basi labda sasa hivi usingeliniona kabisa…’akasema Maua.

‘Maneno ndio nani tena..?’ akauliza Rose, na kabla Maua hajajibu wakaingia shangazi na wifi yake, wakakaa kwenye kiti. Shangazi na mama yao walitulia bila kusmea kitu kila mmoja alionekana ana mawazo yake, Rose akawaangali akwa makini halafu akainuka kuondoka, lakini Maua akamshika mkono na kumwambia;

‘Sasa unataka kwenda wapi, tulia hapa kuna mengi ya kuongea, tunahitai kuongea mimi na wewe, lakini pia tunahitaji kuyajua yaliyotokea hadi kufikia hali hii, na mtu wa kutuambia ni mama yako…ooh, ni mama yetu, kuna mengi tunahitajika kuyajua, ukiondoka ndio itasaidia nini..?’ akasema Maua na kumuuliza Rose.

‘Ili iweje, …mimi nahitajika kwenda zangu angalau nipate muda wa kupumzisha kichwa changu, mimi na wewe tutaongea, tena tutaongea sana, maana kama nilivyokuambia, lazima mama awajibike, na tutaanzia kwa wewe twende ukasome….’akasema Rose kwa kumnong’oneza Maua huku shangazi na mama yako wakiwa wamesimama kuwaangalia.

‘Mama , na …shangazi, mna nini cha kutuambia, sina uhakika kuwa mna jambo kubwa sana la kutushawishi kwa hili lililotokea, labda lipo, ngoja nisubiri…hasa kutoka kwa mama, mimi sina kinyongo na shangazi, sijui kama anahusika sana na hili…labda mlikuwa na ajenda ya siri, hebu tuambieni…’akasema Rose na kukaa kwenye kiti, huku akimuegemea ndugu yake kwenye bega. Tendo lile lilimfanya mama yao kutoa machozi kama maji, na shangazi akageuka pembeni kuficha machozi yake, ….

‘Mimi sioni kuwa kuna haja ya kulia, kwani hakuna msiba hapa, ..na ni maajabu sana kuona machzo ya mama leo, hii ni ajabu kubwa, lakini najaribu kujiuliza kwani mumefanya makosa gani,…nahisi mlifanya hivyo katika mambo ya kutafuta maisha au sio, mama ulijali sana biashara zako, au pesa, au sijui mume wako, na hukutujali sisi, uliniachia yaya ambaye ndiye alinilea tangu nikiwa machanga, …’akasema Rose, na alipomuona mama yake akitaka kuongea akatulia, lakini alimuona shangazi akimzuia mama kumkatiza, nay eye akapata muda wa kuendelea kuongea na kusema.

‘Mama hukutaka hata mimi ni nyonye ziwa lako,uliogopa kupoteza usichana, au sio, au uliogopa kupoteza muda, muda kwako ni pesa …unafikiri hayo siyajui…uliogopa nitayajua zaidi ndio maana ukamtimua yule yeye, lakini baadhi alishanisimulia, yeye nilimuona kama mama yangu, kwa jinsi alivyonilea na kunipenda kama mwanae,…’akasema Rose, sasa alikuwa kaka vizuri, lakini kainamia chini, na Maua akajiegemeza kwenye bega lake kama alivyofanya Rose.

‘Mama niliona ajabu sana,ulipokuja na mambo yako ukamtimua yule mam-yaya, mama wa watu alikuwa na kosa gani, hilo liliniumiza sana, ndio maana niliona nijiondokee hapo nyumbani,… eti ulidai kuwa ananiharibu, kwanini hukuyaona hayo alipokuwa akinilea nikiwa mchanga, umesahau kuwa ulikuwa hupatikani unakaa miezi, hunioni ananilea yeye…kwakeli iliniuma sana, …lakini nashukuru kuwa kakusamehe mama wa watu…’akasemea Maua kwa unyonge na kipindi hicho Maua alikuwa kama anambembeleza kwa kupitisha mikono yake mgongoni kwake.

Kila mara mama yule alipotaka kuongea, shangazi alimzuia, akamwambia ni vyema awaachie watoto waongee, waongee kila kitu kinachowaumiza mioyoni mwao, hiyo itawasadia, kuliko kubishana nao,…mama yule akakubali kwa shingo upande, na kukaa kimiya, licha ya kuwa huyo mama hakupenda kufanyiwa hivyo, kama angelikuwepo peke yake na hawo watoto, angashaliwaka, na hata ikibidi kutembeza vibao, hapendi kunyong’onyea, au kumtetemekea mtu, hata ile hali ya kufikia kutoa machozi, ilikuja tu bila kutegemea, lakini huwa hana tabia ya kujishusha…lakini kwa siku ile na muda ule, alihisi tofauti kidogo, na kila hatua iliyopita, alijikuta akishindwa kuvumilia, moyoni ahisi uchungu, na kujuta, akajiona kweli alikosea, lakini hawezi akajishusha kiasi hicho kwa watoto, alitaka apate muda wa kubishana nao angalau kidogo…

Akakaa kimiya na kumsikiliza Rose, huku moyoni akisema, huyu yeye anajifnaya kuongea saana, naona kanirithi ujasiri wangu, langu huyo mwingine katulia kimiya, sijui ndio kamrithi baba yake, sijui, nitajuaje wakati sikuwahi kuwa na huyo baba yao kwa muda mrefu, sijui naye anajua kuwa ana watoto wa mapacha, na je nikikutana naye tutaongea nini....aah, haijalishi kwanza kaoa, na anaishi na familia yake, hawa ni wangu, wakihitai baba yao, wataua wenyewe...akatulia na kumsikiliza Rose akiongea.

‘Sasa kumbe pia yupo ndugu yangu, naye kalelewa na shangazi, …ina maana kumbe kweli hukujiandaa kuzaa, kwanini basi ulikubali kubeba mimbayetu, au utasema ilikuwa bahati mbaya…hapana, usitudanganye kwa hilo, mimi nahisi kuna sababu nyingine, ambayo hasa tunayoijua sisi ni kuwa ulikuwa bize na kutafuta pesa, zijui kwa ajili ya nini….hebu tuambie kilikufanya nini usiwajibike kama sio huko kutafuta pesa..pesa…!’akazidi kuongea Maua, na kila mmoja likuwa akimsikiliza yeye.

‘Mama mimi sielewi, ulikuwa ukitafuta pesa kwa ajili ya nani, maana mimi niwazavyo , watu wanatafuta pesa kwa ajili ya kujijenga hasa kwa ajili ya familia zao, wewe ulikuwa ukitafuta pesa kwa jaili ya nani, sijui…labda kwa ajili yako na baba, …sasa sitaki nikuumize zaidi, mimi nashukuru kuwa angalau pesa zako zilinisaidia kusoma, hadi nimefikia hapa, ..nashukuru sana, lakini je ndugu yangu huyu, pesa zako zimemsaidia nini…?’ akauliza Rose na kutulia kimiya.

Mama na ujasiri wake akajikuta akilia, alishindwa kabisa kujizuia, akamwangalia wifi yake ili amsaidie, lakini shangazi alikaa kimiya na huku akisema kimoyomoyo, sasa angalau kidogo upate machungu ya ulezi, ….’ Akatabasamu na kumuonyesha ishara kuwa aongee tu, na huku akiendeela kuwaza kuwa leo mwanamke wa shoka kapatikana…

NB Nini ataongea huyu mama , tusameheane hivyo hivyo hata kama ni kidogo

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

MKUU POLE SANA NA KAZI NZITO YA KUTUJALI, LAKINI WEWE NI TAJIRI, KIPAJI CHAKO NI UTAJIRI, LAKINI TATIZO NDIO KWA VILE UPO NCHI YENYE UTAJIRI, LAKINI MASIKINI NA KILA KITU KINAENDA HIVYO-HIVYO, IPO SIKU UTAGUNDUA HILO,...