Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 31, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-43
Adamu, akiwa katulia nyumbani kwake, alianza kutafakari ni wapi kakosea safari hii, akaona kila kitu kilikuwa kama kilivyotakiwa kiwe, na hakuwahi kufanya makosa, sasa iweje siri za mikakati yake ivuje, haiwezekani, labda kuwe na mtu kavujisha, na ni nani, …akajaribu kuwachuja watu wake, hakuona anayeweza kufanya hivyo, ni watu wanaoaminika sana…sasa tatizo lipo wapi,….akaanza kuchunguza mfulululizo wa matukio mbalimbali hadi kufikia siku ya leo, ili atafute kama kuna kosa limetokea mahali, lakini kila alivyowaza hakuona wapi kwenye kosa. Sasa ina maanisha nini, …ina maana huyu jamaa kaweza kupeleleza na kupenya kwenye himaya yake, ….haiwezekani, kama ni hivyo inamaanisha nini, ina maanisha kuwa mwisho wao umefikia, hapana, bado kabisa,…

Akamuwaza Inspekta, ambaye anaogopwa kama nyoka, huyu wamemjaribu kwa kila njia ili awe kwenye watu wao lakini wameshindwa, walipoona hivyo wakabuini njia ya kummaliza, lakini wakahofia kufanya hivyo, kwani yeye sio raia wa nchi na mtu wa serikali ya nchi jirani, wa ngazi ya juu, kummaliza kunahutaji mikakati ya hali ya juu. Baadaye walikubaliana kuwa wasimmalize kama wanavyowafanyii wengine, wakabuni nia mbadala, na hapo akaumbuka hotuba yam mmoja wa walimu wao alivyosema…, ….

‘Katika kazi zenu zote hakikisheni hamuwagusi watu wa mataifa mengine, majirani , …hatutaki uadui na mataifa mengine au majirani zetu, lengo letu ni kuitengeneza nchi yetu kwa kuwaondoa watu wabaya, lengo letu ni kuondoa mafisadi walioifanya nchi hii ya kwao, ..lengo letu sio kuleta uadui na majirani zetu….’alikumbuka hotuba ya mwalimu wao akiwa kwenye mafunzo mafupi.

‘Mfano mzuri ni Inspekta aliyeletwa toka nchi jirani, huyu ni mbaya sana, lakini kaja kwa mkataba wa muda mfupi, ataondoka, tutaendeela na mambo yetu, kinachotakiwa ni kumbabaisha kwa kesi nyingi, kiasi kwamba atashindwa ashike ipi ache ipi….’ Walielekezwa jinsi ya kufanya, na ndivyo walivyofanya na kweli walifanikiwa, maana kila kukicha kuna tatizo…

Akakumbuka jinsi alivyokutana na Inspekta siku ya leo,kuja kwake imekuwa ni kwa kushitukiza sana, na hakujua kwanini hakupata taarifa toka kwenye vyanzo vyao vya habari, na hili linampa mashaka kuwa watu wao waliopo huko wanazembea, inabidi kutoa taarifa kwa wafuatiliaji, waangale kuna kosa gani. Haiwezekani mtu mkubwa kama huyo kuamua kuja huku bila ya watu wao kujua, haiwezekani… . Alitaka kupiga simu kwa vyanzo vyake vya habari, lakini akaona itakuwa sio vyema,inahitaji muda wa kufanya utafiti.

Kuja kwa Inspekta kwa kushitukizia kumeharibu mipangilio yake yote ya siku, …ilibidi amuwahi Rose kabla hajaondoka, na alimpomkumbuka Rose, mwili mzima ulisisimuka, akaivuta sura yake na kuiweka mbele ya uso wake, akatabasamu, ….`kwanini huyu binti ananipa shida sana, …kwanini nismpate mwingine badili yake, …oh jamanai kupenda kubaya…’ Akainama cini kwa huzuni, akijua kuwa sasa Rose keshamkosa, ….Alipomuona mchana ule kule ofisini, alijua sasa mambo yanaanza kuja vyema, alijua Rose kajileta mwenyewe, ..kwanza kwasababu yule mtu aliyekuwa kikwazo keshaondoka, …huyo ni kazi ya polis kuhangaika kutafuta muuaji ni nani.

Lakini alisngaa kusikia kuwa Rose ana mtu mwingine, na mtu huyo ana sifa za kufuga ndevu, …aliwambia watu wake wamchunguze ni nani,lakini taarifa alizokuwa kazipata zilimtia mashaka kuhusu utendaji wa watu wake, …akawaagiza wafanye lile aliloona ni muhimu kwake, …akatumia ujuzi wake na hatimaye akafanikiwa kwa kuua ndege wawili kwa jiwe moja, …kumuondoa mbaya wake na kumbambikia kesi huyo jamaa ambaye alionekana naye kajificha, kwani tangu aingie humo hotelini hakuwahi kuonekana tena, hiyo sasa ni kazi ya polisi kumtafuta yupo wapi nan i nani, wakimuona watamuandama kama muuaji, siku zinakwenda mambo yanakwenda kama walivyopanga.

Lakini ghafla Inspekta kaibuka ….inaonyesha kuna siri zimevuja mahali, na hii inaashiria balaa, lazima uchunguzi mkali ufanyike. Hata hivyo inavyoonekana kuna tatizo , huenda ni la uongozi au kuna watu wameshaanza kuisahau, inasikitisha kuona kwamba baadhi ya viongozi wameshaanza kum,uingilia katika utendaji wake, nah ii inaweza ikawa sehemu inayochangia kuvujisha mambo, …katika makubaliano yao, haikuwa hivyo…..

Baada ya kuachana na Inspekta, aliangalia saa yake na kukuta muda umekwenda sana, na kwa vyovyote kama Rose alikuwa mtu wa kurudi mjini, atakuwa keshaondoka, kwahiyo hana jinsi, kama kweli bado ana nia naye lazima amfuate mjini, na hilo ni lazima, ..ni lazima amshawishi arudi kazini, nan a kumweleza ndoto yake ya kuanzisha hospitali yao,…alipowaza hilo alimlaani sana Inspekta, hakuwa anataka kabisa kutembelewa na mtu kama huyo, kutembelewa na mtu kama huyo akiwa haumwi, inabashiria hatari…

Akaangalia saa yake tena kuona kama anaweza kwenda kumbahatisha Rose, akasema kimoyomoyo, kwa vile alikuwa hana kazi ya kufanya kwa muda ule ajaribu kumbahatisha, kama hayupo basi atakwenda ufukweni kupoteza muda, akatoka pale nyumbani kwake huku akiwaza mazunguzmo yake na Inspekta, yalivyokuwa, licha ya kumpiga chenga kwa maswali yake, lakini aligundua jambo kuwa keshamhisi kitu, kuna kitu wamgendua, lakini kama wamgeundua kitu mbona hajapata taarifa yoyote, haiwezekani kuwa watu wao waliopo ndani ya polisi hawakuweza kujua lolote linaloendelea huko, …akawaza baazi ya maswali aliyoulizwa na Inspekta kujaribu kuangalia kuwa anaweza kugundua kitu..

‘Sikiliza Docta, wewe ni mtu muhimu sana katika nchi yetu hii, na kwa ujumla tulikuwa
tunawahitaji sana, sio tu katika utaalamu, lakini katika kuhakikisha nchi yetu inasimama vyema, …katika uchunguzi wetu, tumejikuta tunakuhitaji wewe katika kutusaidi maswali machache…’akasema Inspekta.

‘Kama ni maswali yanahusiana na polisi na sheria naomba niwe na wakili wangu, tafadhali…’alisema Docta Adam, akajirabu kumkwepa Inspekta, lakini haikuwa akzi rahisi.

‘Kwanini mnapenda kukimbilia wakili, …kama kweli unajiamini huna hatia, kwanini umuhitaji wakili, sio mbaya ni haki yako,sawa, …kwasababu mna pesa za kuwatumia hao watu, lakini ninachotaka kuongea nawe sasa hivi ni maswali ya kirafiki tu,…nia yangu kubwa ni kutafuta jinsi ya kuleta amani na utengamano, kwa njia ya majadiliano…sipo huko kwenye kutiana hatiani, …’alikumbuka hotuba ya Inspekta.

‘Nawajua sana nyie mapolisi, mnapenda kujifanya kuwa mnaongea kama marafiki, lakini mwisho wa siku kila ulichoongea hapa kinachukuliwa kama ushahidi…hapana, sipo tayari kwa hilo…’aliongea kwa mbinu za kujitetea, lakini alijiona kama anakwepa kupambana na adui yake, kitu ambacho hakukikupenda .

‘Kuna mgonjwa aliwahi kuletwa hapa kwako, mgonjwa huyo alikuwa amechanganyikiwa na huyo mgonjwa alikuwa akifanyakzi kwenye kikosi maalumu cha jeshi cha silaha, na alikuwa mtalaamu sana, alikuja hapa mkamtibia na baadaye akaondoka,unamkumbuka huyo mgonjwa…?’ swali hilo aliliona lina mtego, lakini alishajiandaa kwa swali kama hilo, kwaahiyo halikumpa shida ya kulijibu.

‘Yawezekana, kwasababu wanakuja wagonjwa wengi, na sisi hatuna dhamana ya kuwauliza wagonjwa kila kitu kinachohusu yeye kama hakihitajiki katika matibabu yake,…kwa ujumla sina kumbukumbu ya mtu kama huyo, ikizingatia kuwa mimi sio docta wa kukutana na wagonjwa wote, labda iwe ni kwa tatizo maalumu, hata hivyo, siwezi kukataa kuwa wagonjwa kama hawo hawajawahi kufika hapo hospitlini, wamefika wengi, sasa kujua yupi ni yupi unayemuulizia itakuwa kazi kubwa kuhisi…’alikubuka jinsi alivyomjibu Inspekta.

‘Utakuwa unamjua namzungumzia nani, …unachojaribu ni kukwepa kuniambia ukweli, ila kama unataka nikukumbusha kidogo, ni kuwa huyo jamaa, alikusababishia mpaka ukachukuliwa hadi kikosi cha jeshi,…kwa ujumla huyo mtu ni mtu hatari sana, kwani yeye anautaalamu wa silaha, ndiye anayetengezeza silaha za hatari hapa nchini, pia ana utaalamu wa kila namna, …tunamtafuta sana, …na licha ya hilo huwa akianza kuchanganyikiwa anaua ovyo…inawezekana utaifanya humjui, lakini ni kwa manufaa ya taifa lako, ni kwa manufaa ya kizazi chako, kwasabaabu kizazi chako kitahitaji maendelea, jamaa na ndugu zako wanahitaji amani, na amani haitapatikana kwa namna hii…ubinfasi wa kutaka kupata zaidi wakati wengine wanaumia, huo ni uufisadi..’

‘Kwanini unaniambia haya yote, kwanini unanipa huu muhadhara…sijaelewa Inspekta…’akauliza Adam
‘Najua unaelewa, lakini tatizo ni kuwa hatutaki kuona mbele pale tunapojiona kuwa tumefika, fikiria hali ya jamii, hali ya vizazi vijavyo, fikia maendelea ya watu, …je umemkumbuka huyo jamaa?’ akauliza inspekta.’

‘Mimi ninayemkumbuka ni...jamaa mmoja ambaye baadaye hata hawo wanajeshi walikuja kugundua kuwa sio yeye walimfananisha tu, na wengine walikuwepo, lakini labda warudi tena hapa nianza kuwakumbuka, …’akasema A dam.
‘Kwahiyo unakumbuka kuwa walikosea wakamshika jamaa asiyehusika, unaweza kuniambia kwanini huyo jamaa unamkumbuka vyema…?akauliza Inspekta.

‘Kwasaababu aliendeela kuwa mgonjwa wetu baadaye, na akawa katika mikono ya msaididzi wangu , kwani ilionekana kuwa hajapona vyema, na ata hivyo ametoweka, sijui yupo wapi, kama ndio hilo unalohitaji…’akasema Adam.

‘Ametowekaje, na wakati wewe umesema alikuwa katika mikono na msaidizi wako, huyo msaidizi wake ni nani na yupo wapi? ‘akauliza Inspekta.

‘Msaidizi wangu anaitwa Rose, yupo likizo, zaidi kama unahitaji kuhusu huyo mgonjwa utayapata kwake…..’akabla haja,alaiza simu ya Inspekta ikaita, na inspekta ilisikiliza kwa muda, halafu akaikata na kutulia kimiya kwa muda baadaye akasema;

‘Nitakuacha kwa muda, kama hutojali, nitakuja kukutembelea muda si mrefu, nina mangi ya kuongea na wewe, hasa kuhusiana na kazi nyingine unayofanya zaidi ya huo udakitari, ni vyema tukasaidiana kwani kila jambo lina mwanzo namwisho, na lazima hali kama hii ifike mwisho, tusema basi, sasa turudi nyuma na kuamua kulienga taifa…’akasema Inspekta na kumuacha Docta akiwa kaduwaa….

*******
Inspekta hakuamini, jinsi huyo mtu alivyotoweka kama upepo, hakuamini kabisa, kwani alikuwa na uhakika kuwa yupo nyumbani kwa Rose, na alionekana wakati anaingia, lakini hakuonekana wakati anatoka, ina maana Rose alimficha, haiwezekani, …alitafuta kila kona ya nyumba, lakini hakuona dalili ya mtu huyo, na hali ya hewa ingelibadilika mle ndani, kwani mtu huyo kinachomponza ni harufu inayotoka mwilini mwake, licha ya harufu ya majasho, lakini ana harufu fulani ambayo humtoka hasa akitokwa na jasho.

Hakuiskia hiyo haurufu na wala hakumkuta huyo mtu, na haiwezekani awe amejificha mahali, haiwezekani, …Inspekta akiwa kairudisha bastola yake kwenye koti lake, alimwangalia Rose akiwa kasimama huku akiangalia huku na kule bila kujua nini kinachoendelea..

‘Binti, kuna mtu alikuwepo humu ndani, na hatukumuona akitoka, hebu niambie kaelekea wapi, au umemficha wapi, …huyo jamaa ni hatari, anatafutwa akiwa hai au mfu, tunakuomba kama unajua wapi alipo utuonyeshe, …’akasema Inspecta akiwa anamsogela Rose.

‘Hivi ndio heshima gani, …au ndio tuseme kwasababu nyie ni maaskari mnaweza mkaingia nyumba ya mtu bila hodi na kuanza kupekua pekua kila mahala, …hiyo sheria imetoka wapi, …’Rose akapata ujasiri wa kuongea.

‘Kama ungelikuwa hatarini usingeliweza kusema maneno kama hayo, ninakuhakikishia kuwa huyo mtu uliyekuwa naye muda mchache uliopita ni hatari kuliko unavyowaza wewe…tafadhali binti , usinipotezee muda, naomba uniambie wapi alipoelekea huyo mtu..’akasema Inspekta.

‘Mim sijui unachozungumza, mtu gani, …kama engelikuwepo humu na mumemuona sasa kaenda wapi, …huyo aliyekudanganya nenda kamuulize vyema,. …tafadhali naomba nifunge mlango kwani naondoka..’akasema Rose akionyesha kukasirika.

‘Nchii bwana, kweli mnanishangaza, mnaishi na nyoka, hamuogopi, na wakati watu tunataka kuwaondolea hatri hamtaki kutoa ushirikiano, haya, …kaeni na nyoka zenu, lakini nawaambia kuwa hilo mnalolianya ni jambo la muda mfupi tu, halitawasaidia mbeleni, kizazi kijacho kitakuja kuwalaumu, kwasababu hawo watu ni waharibifu wa mali , ni waharibifu wa kuhamisha maliasili kwenda kusikojulikana, wakiagiza masilaha, yasiyoisaidia serikali, sisi tunajitahidi kuwaondoa ili kuwa na amani, lakini raia mnatuangusha,kwasababu mnaishi na hawa watu, mankula nao, …mnatembea nao, mnawajua, lakini hamtaki kuwataja, ili tuyamalize haya matatizo….’akasema Inspekta.

‘Tatizo mimi sijui nini unachokiongea, ningelijua ningelikusaidia,…’samahani sana, …’akasema Rose, akionyesha kidole kuwa Inspekta atoke nje. Inspekta hakutaka ubishi alitoka nje huku akimwangalia Rose kwa makini, na akilini alikuwa akijisema `huyu binti haiwzekani akawa anshirikiana na hawa maharamia, haiwezekani akawa jambazi,…sikubaliani na hilo…’

‘Sawa binti, ila kama unaijali serikali yako,na unawajali watu wasio hatia, ambao kila siku ya mungu wanauwawa bila makosa, ungelisaidia …na pia nilikuwa na mazungumzo na wewe, nashukuru kuwa nimekukuta kabla haujarudi mjini, …ila kama una haraka, basii tutakutana huko mjini, lakini tukikutana huko mini, nitakuwa mtu mwingine….unasemaje , nakuomba tuongee kwa marafiki wanaotka kuiondoa ncho hii kwenye majanga yasiyofaa…unasemaje..binti…’akasema Inspekta.

‘Kwani wewe ni nani, kwasababu ulipoingia hukujitambulisha, nimekuona kama jambazi fulani…sasa hivi tunshindwa kujua nani mwema na nani mbaya, …’akasema Rose huku akiwaza, kuhus huyu mtu alimuona wapi, sura inaanza kumjia kuwa ni mtu fulani aliyewahi kumuona mahali, lakini hakuweza kukumbuka vyema.

‘Mimi ni mwanausalama, mimi ni askari polisi na lengo langu kubwa lilikuwa kuja kumkamata huyu jambazi mkuu, huyu aliyekuwa humu ndani ni miongoni mwa viongozi wanaoendesha hujuma maporini, sijui kwanini wanafanya hivyo, kama wanataka uongzi kwanini hawajitokezi wakapewa nafasi ya kuomba kisiasa, wao wanatka fujo, umwagaji damu, hatuendi hivyo, na kama wewe utagundulika kuwa unashirikiana na wao basi sheria itachukua mnkondo wake…’akasema Inspecta.

‘Mimi huwezi kunitisha kwa hilo, kama wewe ni polis naomba kitambulisho chako, maana kila mti sasa ni polisi..’akasema Rose.

Inspekta akamwangali kwa makini, halafu akatumbukiza mkono wake kwenye mfuko wa shati, ambali lilikuwa limefunkwa na koti alilovaa, akatoa kitambulisho chake na kumsogela Rose, …Rose akanyosha mkono kukipokea, lakini Inspekta akawa amekishika , huku amekifunua, …ile picha ple kwenye kitambulsisho ilionyesha dhahiri kuwa huyo ni nani, akamkumbuka ….

‘Mungu wangu…samhani sana, …Inspekta, sikukujua kabisa, samhani sana,…’akasema Rose huku akitaka kupiga magoti.

‘Usijali, ni haki yako kufanya kama ulivyofanya ndio maana sikutka kutumia nguvu ya dola, na nakuomba kama una nfasi naomba tuongee, kama huna nafasi basi tukifika mjini nitakuhitaji ofisini tuongee…’akasema Inspekta, hakutka kuyachukuli ahay amaswla kiharaka haraka kama wenzake wanavyofanya, alishaua njia iliyokuwa ikitumika ya ubabe kwasasa haina nafasi, watu wataishia kuuana na kuwekeana visasi bila mafanikio, lazima atumie njia nyingine ambayo ni ya taratibu lakini ana uhakika italeta mafanikio.

‘Kwakeli nina haraka natakiwa kufika leo huko mjini kabla ya saa kumi na mbili kutokana nakibali nilichopewa, sasa naona muda umekwsiha sana, sijui nitafungwa….’akasema Rose.

‘Basi tutaongozana, usiwe na wasiwasi gari langu lipo njiani linakuja kunichukua, na wakati tunalisubiri nilikuwa naomba nikuulize maswali machache kama hutojali, hayahitaji kuwepo wakili wako, ni ya kawaida tu..

Rose liposikia wakili, akaukumbuka onyo la yule mtu anayetafutwa na huyu polisi, kuwa huyo wakili ni miongoni mwa maadui zake, sasa atafanyaje, …akawaza kwa uandani na kuahidi kutokumtegemea tena, na akainua kichwa na kumwangalia huyu askari, …akaumbuka jinsi watu wanavyomuongelea kuwa ni mtu wa msimamo, mchapakazi, na hata moyoni akaingiwa na imani naye, akaona ajaribu kumwamini lakini hakuwa na uhakika, kwani hakuna mtu aliyekuwa akimwamini kama Docta Adam, kumbe sasa…

‘Maswali gani hayo, maana kama nikuhusiana na mauaji ya kule mjini mambo yapo kisheria na sisitahili kuongea kinyume na makubaliano, kwahiyo naomba kama ni mongezi yawe ya kawaida tu…’akajihami Rose.

‘Unajua Rose. Wewe ni msomi...' alisema Inspekta na kumsogelea karibu.., `Na zaidi upo katika idara ya kuhudumia wananchi, ili wasipoteze maisha yao, na hili ndilo hata mimi najaribu kilifanya, watu wanauliwa ovyo, hawana hatia watu wanaishi maisha ya wasiwasi, yote kwasababu ya vikundi vya watu wachache wanaojifanya wanajua kutumia silaha…na ili tuweze kuwashinda hawa watu tunahitajika kuwa na umoja…kati ya sisi maaskari , na nyie raia wema, …’akasema Inspekta.

‘Sawa nakusikiliza, uliza hayo maswali, nitaangalia kama naweza kuyajibu au la…
Mara wakasikia mlango ukigongwa, Inspekta akachomoa bastola na kujibanza pembeni ya mlango na kumuonyeshea ishara Rose afunhue mlango na asiseme lolote kuhusu yeye, …Rose akasoegelea mlango na kwa wasiwasi akaufungua mlango….oh…..

NB:Tuonane sehemu ijayao...Najiuliza mbona maoni yanapungua siku hadi siku, au labda kisa kimekuwa kirafu sana,...nahitaji maoni na ushauri wenu!


Ni mimi: emu-three

4 comments :

Marie Makulilo said...

Hapo raha kweli, Dokta Adam kagonga mlango..uso kwa uso na Inspekta tena

Ngoja tuone.

Weekend njema EM3

Anonymous said...

M 3 we jiandikishe uandishi wa vitabu tutakusapoti kwani kazi zako zinanikumbusha yule marehemu ambaye alikuwa mtu wa hadithi za kusisimua za WILLY GAMBA.
mdau wako.

ROGER -UK

Mimi said...

doctor adam kazi kwake sasa akileta vitisho kasikika na inspector. sio kama maoni yanapungua dear ni vile tu nafikiri unavyochelewa kupost tu si kama zamani ukipost leo kesho yake asubuhi au mchana tayari ukifungua unakuta umeshaweka post nyingine, kwa sasa unachelewa sana. ila all in all bdo inasisimua sana na kutuelemisha mpka kutamani kitabu.

Swahili na Waswahili said...

Hapana si kirefu, kisa kinafikirisha zaidi mpendwa, duuhhh wewe kiboko ndugu yangu!!!!Pamoja daima ndugu wa mimi!