Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, October 6, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-34‘Docta wewe unajua taratibu, nani ni docta mtaalamu, kwa hali hii iliyofikia hatuwezi kuendelea kutumia haya mashine tena, inabidi tuyaondoe tu….hakuna jinsi, kama unavyoona mwenyewe…. maana muda mrefu umepita, na….’ Akasema Yule dakitari huku akiyasogelea yale mashine yakusaidia kupumua. Wakati anayasogelea yale mashine, mawazo yake yalikumbuka simu aliyopokea toka kwa rafiki yake, kuwa kama mgonjwa huyo anaonyesha kuzindukana ayatoe hayo amshine haraka…
‘Kwanini unataka nifanye hivyo rafiki yangu…?’ akauliza kwa mashaka.

‘Huyu ni adui yangu mkubwa, kupona kwake ina maana ni mimi kuingia matatani, na isitoshe huyo mtu hajulikanai wapi anakotoka, ni tahira…na nakuomba sana, sio kwamba napenda iwe hivyo, na sina unyama huo, lakini kama ataendela kuwepo duniani, ni hatari kwa usalama wangu, na kwa huyo binti anayetembea naye….siunamkumbuka vyema, ni yule uliyepata shida kumtaka awe mkeo akakutolea nje…lakini hilo sio tatizo…tatizo ni jinsi gani ya kumupusha na huyo jamaa, kwani atamuharibia masiha yake…kwahiyo ili kuepusha hilo, na kumuokoa huyo binti ili atulie kwenye kazi yake, ambayo ni muhimu sana, ni bora huyo jamaa…’ huyo rafiki yake hakumalizia hayo maneno, lakini docta huku alielewa mwenzake ana maana gani.

‘Nakuomba sana, kwani jamaa huyo nimemtibia mwenyewe, huku, nikajitolea kwa hali na mali, lakini inavyyonekana, kupona kwake ni zero…., kumbuka wewe ni rafiki yangu, na nisingeweza kukuambia hili kama sina sababau kubwa ya muhimu….’ Akasiki rafiki yake akiongea kwa huzuni na mashaka, ilionekana kuwa kakumbwa na tatizo fulani, hakutaka kulijua hilo tatizo kwa muda kama huo, ila hakuamini maneno hayo, kwani anamjua vyema rafiki yake , ni mtu mwenye huruma sana kwa wagonjwa…kama imefikia hatua ya kusema hivyo, lazima kuna jambo kubwa.

Akiwa anamsikiliza, alimwangalia Rose kwa mbali, alimtamani sana huyo binti, na alishawahi kuongea naye , lakini majibu aliyopata toka kwake, hakuamini, ….alikumbuka jinsi alivyomhangaikia hasa pale mkewe alipofariki, alimtaka Rose ashike nafasi yake, lakini Rose alimkataa kata kata, na siku alipohamia kufanya kazi katika hospitali ya Adam, ….akawa anamtumia rafiki yake Adam , ili amsaidie kumpata huyo binti, lakini hakufua dafu…akaishia kumchukia …Sasa yupo hapo na mgonjwa, na mgonjwa mwenyewe haeleweki, na…huyo mgonjwa amesikia ndio kikwazo, …..sasa…hata kama ni kikwazo, hawezii kufanya unyama wowote kwa mgonjwa, sio sifa njema ya dakitari, lakini huyo rafiki yake, anataka….hapana…..

Alikumbuka fadhila alizofanyiwa na rafiki yake huyo kama isingelikuwa yeye , leo angelikuwa mitaani, au keshajifia…..kwani wakati wanafanya kazi pamoja, yeye alifanya kosa kubwa sana la uzembe hadi kusababisha mama mja mzito kupoteza uhai na mtoto wake akiwa tumboni, na isingekuwa rafiki yake huyo kumsaidia angelifungwa na maisha yake kwa kipindi hicho yalikuwa hatarini….yalikumbwa na mitihani mingi….

Alikumbuka jinsi kipindi kile alivyokuwa kwenye shinikizo la kimaisha, alikuwa akihaha na familia, mke wake alikuwa akiumwa sana, na alihitaji pesa nyingi kwa matibabu, mama yake mzazi alikuwa anaumwa, naye pia alihitai pesa za matibabu, watoto wakawa wamefukuzwa shule kwasababau hela yote ilikuwa ikiishia kwenye matibabu ya mkewe na mama yake. Na hata vile alikuwa dakitari lakini kwa kipindi kile alikuwa dakitari mdogo tu, mshahara kidogo, …alijaribu kuomba mkopo, lakini mkopo wenyewe haukuweza kumfuikisha mbali,. Basi akawa anafika kazini, huku mawazo yapo katika familia yake.

Ndipo akaletwa huyo mama, akiwa na dalili zote za kuwa tayari kujifungua, lakini alikuwa akivuja damu sana, kwahiyo ilibidi akimbizwe chumba cha wazazi, ..yeye ndiye aliyekuwa dakiatari wa zamu siku hiyo, na alimpokea huyo mama vizuri na kuanza taratibu zote zinazostahili, kwa kumfikisha sehemu ya kujifungulia, lakini huyo mama inavyoonyesha hakuwa na tabia ya kwenda kliniki, kwahiyo hakukuwa na historia yoyote ya kuweza kufuatiliwa, ….wakatii anahngaika hivyo, ili ajue nini cha kyfanya, mara simu ikapigwa toka nyumbani kuwa mkewe yupo katika hali mbaya,…kazidiwa, na kabla hajauliza swali kuwa wamechukua hatua gani, akaambiwa tatizo ingine kubwa.

Alikuwa akitamani simu hiyo ikatike, ili akamsaidie huyo mama mzazi aliyeletwa na ikiwezekana kumtafuta dakitari mwingine aje ampe msaaada, lakini kabla mawazo hayo hayajaingia kilini, akamsikia mpiga simu akisema, kuwa katika heka heka za kumsaidia mkewe ambaye kwa muda huo alikuwa akiishi na mama wa huyo docta. Mama yake naye shinikizo la damu likawa limepanda, na akadondoka chini na kuzirai, ….aliposikia hivyo alichanganyikiwa hakukumbuka tena kuhusu yule mama mzazi, aliyekuwa kamtayarisha kule `leba’ tayari kwa kumsadia kujifungua, akatoka mbio kueleeka nyumbani, alipitia haraka kumpa taarifa msaidizi wake, ambaye alikuwa akiongea na simu, akawa anamuomba haraka aelekee hukoo `leba’….lakini mwenzake hakusikia vyema,,…

Alipofika nyumbani, ikabidi kuwachukua mke wake na mama yake hadi kwenye hiyo hospitli yao ili wapate matibabu, ile anafika anakuta wenzake wamejikusanya, kesi inanguruma, ni nani aliyempokea huyo mama mzazi…na kwanini akaachwa peke yake, na kupoteza damu nyingi hadii kufikia kupoteza maisha. Kesi ilikuwa kubwa, lakini mtu aliyeweza kumsaidia alikuwa rafiki yake huyo aliyempigia simu…, ambaye alitoa ushahidi uliowezesha kumsaidia kuwa mama huyo alikuwa keshapoteza damu kabla hata hajafikishwa hapo, na kwasababu ilishafikia muda wa kujifungua na ilikuwa haraka, mama huyo alikimbizwa sehemu ya kujifungua hata kabla ya kujulikana kuwa ana mapungufu ya damu, na bado aliendelea kutokwa na damu ….

Ingawaje docta huyo alipewa adhabu ndogo ya kufungiwa kwa muda, lakini adhabu ile ilikwisha akarejeshwa kazini, kwa msaada wa rafiki yake…tofauti na ilivyotegemewa , kuwa angelifungwa na huenda angelifia jela….almshukuru sana rafiki yake huyo na wakawa marafiki wakubwa, na aliahidi kuwa siku ikipatikana mwanya wa kumsaidia rafiki yake huyo atamsaidia bila masharti…..sasa kaombwa msaada, na ahadi ni deni…

‘Wewe kinachotakiwa ni kuondoa hayo mashine, kwa kisingizio kuwa muda umekwisha sana, kwasababu kama unavyoona muda mrefu umepita…hajazindukana, unasubiri nini wewe ondoa, ….’akasikia maneno ya rafiki yake yakijirudia masikioni.

‘Lakini dalili za kuzindukana zipo, nimeziona, na kuyaondoa hayo mashine na kummaliza, naogopa kufanya kosa hili…unakumbuka niliponea…’akajitetea.

‘Rafiki yangu, nakuomba sana, …..nisaidia kwa hilo,…na hakuna wa kukulaumu hapo…’akapata msisitzo. Basi aikabidi atafute njia ya kumshawishi Rose, wakabishana kidogo lakini baadaye ilionekan Rose kuamini, kwani tangu mwanzo dada huyo alishaonyesha dalili za kukata tamaa .
Mwanzoni ilibdidi wabishane kuhusiana na hilo, aliwaambia sio vyema kuiondoa hiyo mashine,kwasababu bado inaonyesha kuwa mgonjwa ana uhai, …lakini yeye kama mtaalamu ilikuwa kazi rahisi kuwashawishi wengine, na wao walikubalaiana naye mara moja kwasababu muda mrefu ulishapita, karibu siku nzima….wenzake wakakubaliana naye. Rose akabisha bisha ….mwishowe naye akakubali kwa shingo upande…wakati yule docta anayeshughulika na hiyo mashine akitaka kuiondoa, Rose alihisi kitu kwa mgonjwa akasema…

‘Docta…subiri kidooogo ,….mungu wangu, ina maana ndio basi tena…’ akasema Rose huku akijisahau kabisa kuwa hata yeye ni dakitari na hali kama ile inaonyesha kuwa uhai haupo tena, …alishaona dalili hizo akiwa naye kwenye gari na sasa juhudi zote zimefanyika, lakini hakuna unafuu, mtu yupo kama mf utu….lakini kitu kilichompa matumaini ni ile mashine kubwa inayoonyesha mapigo ya moyo…. Ila kwa utaalamu wake, mtu akifikia vile, mara nyingi haponi, ….labda miujiza ya mungu!
`Labda miujiza ya mungu, kwani historia ya mtu huyu umegubikwa na miujiza …watu walishakata tamaa naye walipomuokota, akapona kimiujiza..huenda bado …huenda miujiza ya mungu itasaidia…’ akajikuta akisema kwa sauti ndogo, na docta mwenzake akawa anamwangalia kwa macho ya huruma, akijua nini mwenzake anavyowaza, na hali kama hiyo hata kama ingelikuwa yeye na udakitari wake, bado angeliwaza hivyo, ila naye wka uzoefu wake, ile hali siyo ya kupona tena…labda kwa miujiza ya mungu…naye akawaza hivyo.

Rose alianza kuwaza mengi, kuwa huyu mtu ndio anamfia mikononi, kwanza kuacha yote, kuwa anmpenda, kuwa anamjali, lakini lawama kubwa utashukia kwake, hasa kutoka kwa Docta Adamu kuwa kamchukua huyo mtu ambaye alitakiwa kutulizwa, na kumtembeza mjini…na ….akawaza mengi hadi kufikia jinsi ya kuwapata ndugu zake, …atawapataje, ina maana sasa huo mzigo ni wake, inatakiwa aushughulikie kuutafutia mahala pa kuusitiri…alipofika hapo akageuka na kumwangalia Sweetie pale alipolala, alionekana kabisa hana uhaii tena.

Akamsogelea na kumshika mkonoo wake, akauweka juu ya mkono wake, na huku akiomba kwa ndani ndani, aliomba mengi, na alipofikia mahali fulani machozi yakaanza kumtoka, na sauti ikawa ikiongezeka , toka kuongea kimoyomoyo hadi kwa kuwewesa, alisema;

`Sweetie wewe ndiwe uliyebadili maisha yangu, kutoka kwenye chuki ya wanaume hadi kupenda wewe ulinifanya nipende tena, na nikatamani sana tuwe pamoja, na hili nililidhihirisha kwenye tukio la mwisho kabla hayajakukuta haya, nasikitika sana kuwa unaondoka, tena unaondoka mikononi mwangu, huku nakuangalia, kama akitarii nimeshindwa kuyaokoa maisha yako, lakini hapa wapo wataalamu zaidi yangu, wameshakata tamaa, iliyobakia ni kumuachia mungu….’ Akasogeza kichwa chake hadi pale alipolala mgonjwa wake na kumbusu shavuni, halafu akamwangalia usoni…
Wakati huo alikuwa bado kaushikilia mkono wa Sweetie, na kwa mbali alihisi mabadiliko fulani, toka kwenye ubaridi na kuongezeka hali fulani ya joto, akauminya ule mkono na kumwangalia docta aliyekuwa akiondoa yale mashine, na vipimo vya mashine kubwa vilishaanza kuonyesha kuwa uhaii unazima…

Yeye akasogeza kichwa chake tena karibu kabisa akamwangalia Sweetie usoni, ‘Macho yamefumba, ndimi zimefumba, …na sasa uhai umekwisha, kwaheri Sweetie wangu….’ Wakati anasema maneno haya kwa sauti ndogo, mara akahisi mkono wake ukiminywa, kama vile alivyomminya yeye mwanzoni,…akashituka, hakuamini…akauachia haraka ule mkono, kama vile kaguswa na umeme, …hutaamini, ubinadamu ulivyo, hebu fikiria umeambiwa kuwa jamaa yako anakufa ,halafu ghafla unamuona akiinuka toka kwenye wafu, unafikirii utafanyaje, wengii hukimbilia kwa kuogopa, wengine hupata mshituko wa ajabu, na Docta Rose, alijikuta akiachia ule mkono haraka, halafu akaushika tena kuhakikisha , na pale aliona kabisa vidole vikitikisika…

‘Docta hebu angalia huku….!’ Rose akasema kwa hamasa , akimuonyesha docta mwenzake kwenye vidole..Docta mwenzake alitupa jicho mara moja, na hakuwa an shauku ya kuangalia mara mbili alijua ndio ile hali ya kukata roho, …roho labda ilikuwa haijatoka sasa ndio roho inaachia mwili. Kwani rohoo ikitoka mara nyingi watu huhangaika, hata kama alizimia atainuka kidogo na kupata yale machungu…

‘Hiyo ni kawaida Rose, unakuwa mgeni wa mambo haya nini….’ Akasema yule Daikitari, akiwa keshatoa ile mashine na kuiweka sehemu yake. Aligeuka kumwangalia Rose, halafu akatikisa kichwa kuwa anataka kuondoka.

Rose macho yake yalikuwa yakimwangalia Sweetie, na sasa alikuwa kaushika ule mkono ambao vidole vilikuwa vikitikisika, na sasa alihisi kabisa mabadiliko, mwili ulikuwa una joto la uhai, hakutaka kumwambia docta mwenzake, aliamua kuingia kazini mwenyewe na kuanza kazi yake ya udakitari,….mwenzake kwa muda huo alikuwa keshaondoka na vifaa vyake akisema atarudi baadaye…
Wakati anamuaga kuwa anaondoka, hakutaka kumweleza lolote kuhusu historia ya huyu mgonjwa, kuwa hata mwanzoni ilitokea hivyo, watu wameshaua kuwa kafa, lakini akazinduka….hii inatokea, ….alichofanya ni kumwambia huyo Docta ‘Sawa Docta , usiwe na shaka nipo naye kwa muda…’ akasema Rose, na wakati huo alikuwa akijishughulisha kidakiatari, alijua nini afanye kwa mtu kama huyo,…..
**********
‘Una taarifa ganii toka huko hospitalini…?’ aliuliza Adam kwenye simu, akiongea na mtu wake

‘Taarifa za karibu ni kuwa huyo mgonjwa, hana uhai na mashine zimeshaondolewa, kwani hawaoni umuhimu wa kuendele kumwekea hizo mashine kwahiyo nahisi hivi sasa watakuwa wanauhamisha huo mwili kwenda sehemu ya kuhifadhia maiti…’ akasema huyo jamaa

‘Lakini huna uhakika na hilo…?’ akasema Adam

‘Hatujamuona akitolewa, kwahiyo siwezi kusema moja kwa moja nina uhakika…’ akasema huyo jamaa

‘Naomba ufuatiliea hilo, na kama kuna mashaka, hakikisha unamalaiza kazi,…unajua kama atazindukana na kumbukumbu zipo atasema lolote….kuwa mwangalifu…’ akasema Adam, huku akiwaza na kujuta kwanini alifanya hivyo, lakini aliona ndio bora, kwasababuu kazi ilishaanza na kuiachia nusu inaweza kuleta utata, dawa ni kuondoa kabisa ushahidi.

Adamu alikuwa kachoka sana, kwani mchana kutwa alikuwa akipambana na wadhamini ambao walishasema kuwa Rose aondolewe kazini kwa kutokuwajibika na uzemba, walisema, walishatoa muda wa kutosha, na uchunguzi umefanyika na kuonekana kuwa Rose alijiamulia mwenyewe, kutibia watu bure, bila ya kushirikisha utawala, na kinachowashangaza ni jinsi gani Rose alivyokuwa mkaidi , kwanza hakutaka kuandika barua kama walivyomuagizia, halafu hakutaka hata kusema lolote kuwa kwanini kafanya hivyo, kwahiyo imeonyesha ujeuri fulani…

Alijaribu kumpigia simu Rose, lakini ilikuwa haipatikani, kwani alitaka kumwambia kuwa aje haraka kwanii huku mambo sio mazuri, lakini cha ajabu simu ilikuwa imezimwa kabisa….na ndipo akaamua kumpigia mtu wake anayemfuatilia Rose, na alipoongea naye akagundua kuwa kinachomkwamisha Rose ni huyo Sweetie wake, na kama huyo Sweetie ataenedela kuwepo, Rose atakuwa hafanyi kazi, na huenda akampoteza kabisa, ….alipowaza hilo, hasira na wivu ukamshika. Lakini ndani ya kikao hicho alijaribu kila nia kumtetea Rose, hakukata tamaa, akakiambia kikao kuwa;
‘Jamani kwa taarifa alizonipa ni kuwa kaenda mjini kuzichukua hizo pesa, na kinachohitajika hapa ni pesa, naomba tumpe muda kidogo…’ akatetea Adam.

‘Hizo ni hadithi zako, na kwa vile imeshaonyesha kuwa una hisia za mapenzi kwake, tunakuona kuwa mpo pamoja, na hili tulishakuambia kuwa halikuhusu tena wewe, hapa utakuwa kama msikilizaji na mtekelezaji, unasikia Docta…’ akasema mwenyekiti wa kikao.

Katika kikao hicho cha awali, kilichtokiwa Rose kuwepo, kutokana na barua aliyopewa awali , na moja ya sharti kama hajalipa hiyo hela alitakiwa kuwemo humo kujielezea, lakini hakufika, na kutokufia kwake kikao hakikuarifiwa kibaru kama ilivyoanishwa kwenye masharti . Na badili yake aliagiza kwa mdomo kupitia kwa bosi wake Adam, kitu ambacho kilishaondolewa, kuwa kutokana na tuhuma hizo alitakiwa yeye mwenyewe kufika au kutoa taarifa kwa barua kwa mwenyekiti wa wadhamini, na hilo halikufanyika, ….
Nini zaidi kingemtetea Rose,...ni Adamu, Adamu, hakutakiwa kumtetea Rose... basi barua ikatayarishwa kuwa Rose atasimamishwa kwa muda, huku uchunguzi zaidi ukiendelea na uchunguzi huo ulipangiwa siku tatu, kama itabainika kuwa kuna uzembe, au kuna sababu ya yeye kufanya hivyo kwa maslahi yake binafsi basi Rose itabidi aachishwe kazi mara moja, na mtu mwigine atafutwe….siku tatu hizo zilitolewa wakati Rose yupo mjini, na siku tatu za uchunguzi zikapita na kikawa kikao cha pili cha kutoa hiyo taarifa na pia Rose alitakiwa kuwepo, lakini hakuwepo, ….

NB Je jaje....itakuwaje .....? Mungu wangu nakuomba nipate nfasi ya kukimalizia hiki kisa kabla...kabla...oooh!

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Pam said...

jamani sweetie ucfe....plz!!!

Precious said...

Safari bado mbichi ya Rose na Sweetie....M3 uko kwenye maombi yangu ya kila siku.

samira said...

no usife sweetie docta adam namchukia m3 pole kwa yote mungu yu pamoja nawe