Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, September 16, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-27


Rose alikuwa kapita kila sehemu anayohisi huenda Sweetie wake atakuwepo lakini hakuona dalili yoyote ya kuwepo kwake, na hata alipoulizia majirani na jamaa aliokutana nao, hakupata jibu muafaka, na wote walisema hawajamuona mtu kama huyo. Alifika hadi ufukweni, akiulizia, na kutafuta huku na kule lakini wapi, na mwishowe akajikuta kachoka kutafuta akaamua kujirudia nyumbani , huku akiwa hana raha, alijiona mpweke sana, lakini moyoni akawa anajipa moyo kuwa huenda atamkuta Sweetie wake kesharudi, labda alitoka mara moja, atarudi tu…, lakini hata alipofika nyumbani hakukuwa na mtu kama yeye…upweke, mawazo na wasiwasi ukamtanda, na hali ile ilimsadikisha kuwa huyo jamaa alishamkaa moyoni, na alishamuona kama mwenza wake , ingawaje ni uwenza wa mgonjwa na dakitari wake.

Wakati anatafakari achukue hatua gani simu yake ya mkononi ikaita, akaichomoa haraka toka kwenye mkoba wake, akiwa na shauku kuwa huenda anayempigia atakuwa na taarifa njema labda atapata kile anachokitafuta, lakini alipoangalia simu yake akanona jina la Adam likonyesha kuwa ndiye anayempigia….akasonya, na kutamani kutoipokea, akataka kuikata , moyo ukamsuta, na baadaye akaingiwa na matumaini kuwa usikatae mwito, isije ikawa Adamu ana jambo jema la kumwambia, ….labda kamuona mgonjwa wake, akaipokea ile simu;

‘Ndio bosi niambie….’ Akasema Rose, akiwa anawaza nkuwa bosi wake atasema atamtamkiamaneno haya. …`Rose, mgonjwa wako kaja kunitembelea, usiwe na wasiwasi, …..’ Lakini haikuwa hivyo, ilikuwa ile ile kauli ya kila siku ambayo alishachoka nayo…

‘Nimepokea barua yako toka kwa wadhamini, naona sasa hivi hawataki mchezo, na inavyoonyesha hawaniamini tena, wanaulizia kuwa umeshakubaliana na masharti yao waliyokuandikia kwenye ile barua yao waliyokupa, maana ulitakiwa uisome na baada ya kuisoma, uwajibu kuwa kwa maandishi kuwa umekubaliana na msharti yao au la wachukue hatua nyingine…..’ akasema Docta Adam. Rose yeye alikaa kimiya akijaribu kuyaweka sawa haya matukio yanayomsonga, akanyamaza kwa muda, akiwa kakunja uso, na ndoto zake za kusikia kauli njema zikaota mbawa….Baadaye akasema;

‘Masharti …….ooooh, …’ akasogea na kuegemea ukutani, halafu akasema kwa mshngao…`Bosi, samhani sana …sijapata hata muda wa kuisoma…naomba uniambie yalikuwa masharti gani gani hayo’ akasema Rose, huku akiitafuta ile barua, maana siku ile alipoipewa, aliitumbukiza kwenye bagi lake akijua ni yale yale ya kumkumbushia kuwa anadaiwa..

‘Rose, …mbona uanafanya utani, ina maana hata hukuwahi kuisoma ile barua, unaleta mchezo wa jambo la hatari kama hilo, unategemea mimi nitakuwa na kubeba mpaka lini ….na wakati wewe mwenyewe hubebeki, Rose, barua ile ni nyeti kweli kweli, kwani hata mimi nilipoisoma niliogopa….na muda mwingi nimekuwa nikiwaza jinsi gani ya kukusaidia, lakini kumbe mwenzangu huna hata mawazo nayo…ajabu kabisa…yapo masharti mengi, ila kubwa ulitakiwa uisome kwa makini, kwani waliyaweka kwa mitego, wakiwa na nia ya kukuondoa kazini…siwezi kukuambia hapa kwenye simu kama hujaisoema ni bore uje…’ akasema Adamu.

‘Kwano Bosi nini hasa kinahitajika, mapaka wafikie kuniteha kwa masharti hayo…kilikuwa kinahitajika nini hasa,….kama nii deni nitalilipa, nilisaha-ahidi, ….naomba kesho nifike mjini, nikirudi, ….ngoja nitakupigia baadaye, maana sasa hivi…’ akawa anaongea huku anatafuta kitu kwenye begi lake, ile barua ilikuwa haionekani, sijui amekwenda wapi, …na alipohakikisha haionekani , akaamua kuingia ndani huku simu ikiwa bado sikioni….

‘Sasa hivi unamtafuta Sweetie wako…..unanishangaza sana Rose, huyo Sweetie kakukaa moyoni kama unalea mtoto mdogo, ndio kusema nini, kupenda au…, badala ya kuwazia maswala muhimu ya ajira yako, unapoteza muda kwa kumuwaza mtu usiyemjua, hana matatizo ya kuwaziwa, sio mtoto mdogo kuwa atapotea, una nini wewe binti……yeye ni mtu mzima unafikiri atachukuliwa na mtu….’ akasema Adam.
‘Una maana gani kusema hivyo, bosi niambie ukweli umamchukua huyo mgonjwa kumpeleka wapi, ….’ Akauliza Rose akiwa na mashaka kuwa huenda bosi wake kamchukua huyo mgonjwa.

‘Hahahaha, nimchukue kwani yeye ni mtoto mdogo wa kuchukuliwa , au yeye ni kifurushi…achana kabisa naye, atakutia presha ya bure, nakuomba ufike hapa haraka, kwanza nakuita kama bosi wako , pili kama mtu anayekujali, hiliswala la hii barua ya hawa watu ni swala zito kidogo, sivyo kama wewe unavyofikiria…’akasema Adam

‘Nimeshakuambia ….bosi nimekuomba ruhusa ya kesho, kuwa kesho nafuatilia hizo pesa, na kama mambo yakiwa mazuri nitalipa deni lote mwenyewe, na sasa hivi siwezi kuja, kwasababu huyu mgonjwa haonekani, na ukumbuke alikuwa katika dhamana yangu, kwahiyo siwezi kuvunja dhamana, nitamtafuta hadi nimuone huyo mgonjwa, …’akakata simu.

Baadaye aligundua kuwa kafanya kosa kubwa sana, kwa kuhamaki kwa bosi wake na kukata simu, huenda angelifanya subira na kumdadisi vyema, kama ndio yeye kaamua kumchukua yule mgonjwa ajue, huenda ni yeye tu kamchukua, kwasababu zake mwenywe, …kama angelimdadisi vyema angelimgundua, akajaribu kumpiga simu bosi wake tena, simu ikawa inaita mpaka inakatika, bosi haipokei, akahisi kuna kitu, bosi kakasirika…..

Akaliendea lile kabati lake analoweka vitu vyake vya siri, kwanza alishituka, maana jinsi alivyokuwa kaweka vitu vyake awali aliona sivyo kabisa, harakaharaka akautafuta ule mfuko wa ngozi , …akaukuta haupo, jsaho likaanza kumtoka, nani huyu kaweza kuingia hadi kufungua kabati lake la nguo , hadi sehemu yake ya siri, haiwezekani…..akawa na wasiwasi kuwa lazima kuna mtu anamchezea, haiwezekani aingie mtu humo ndani na kupekua sehemu kama hiyo kama hajiamini kupita kiasi,…lakini baadaye alikumbuka alichokuwa kakifanya, alishukuru sana kwa mungu alimuonyesha ile njia, ….akafungua kabati lake sehemu ya pili na kufungua sehemu nyingine ya siri na kukuta ule mfuko upo kama alivyouweka, alichofanya ni kuchukua sehemu ya zile dhahabu na kuziweka kwenye mfuko mwingine, na akachukua sehemu anayoihitaji na kuiweka kwenye begi lake….akajiuliza sasa aondoke kwenda mjini kwanza au akaendelee kumtafuta Sweetie wake….

Wakati anawaza hayo mara simu ikaita akaipokea harakaharaka bila kuangalia nani aliyempigia, sasa sauti aliyosikia kwa bosi wake alijua kabisa bosi wake kakasirika, na alianza kwa kumwambi anamuhitaji haraka sana nyumbani kwake…sasa sio ofisini ni nyumbani kwake,…alisisitiza kuwa kama kweli ana nia ya kumtafuta sweetie wake afike nyumbani kwake….aliposikia hivyo hakupoteza muda, akakimbili kwanza dukani na kununua kitasa kipya na kumtafuta fundi wa haraka haraka akamsaidia kukiweka, na haikuchukua muda, kukawa na kitasa kipya na funguo mpya…..

Alipofika nyumbani kwa Docta Adam akakumuta mwanamke mmoja kasimama nje, akamsalimia, lakini yule mwanamke hakumjibu, alipompita yule mwanmke akasonya, Rose akageuka kuangalia kwanini yule mwanake amesonya, alishituka alipomuona yule mwanake sura yake, kabadilika utafikiri siyo yeye, oooh, alikuwa mke wa bosi wake ambaye wameachana, …kwanini kakonda hivi, akajiuliza Rose.
‘Wewe ndiye Malaya uliyesababisha ndoa yangu ivunjike…’ akasema yule mwanamke, na kusimama, ilionyesha kabisa anataka shari. Rose hakumjibu akasogelea mlango kubisha hodi, lakini kabla hajagusa mlango akashitukia yule mwanamke keshamfikia na kumsukuma pembeni . Rose ahakusema kitu akatulia kimiya….

‘Nakuuliza halafu unaleta kiburi, wewe unaelewa jinsi ninavyoteseka, wewe unajua tulitoka wapi na huyu mwanaume, leo unajileta leta hapa kujiuza, nitakukomesha leo, ama zako ama zangu…’ akasema yule mwanamke huku anamkwida Rose shingoni. Rose alikuwa kabakia kushangaa tu, na hakutarajia hayo, akawa anamwangalia yule mwanamke bila hata kufanya lolote..

‘Nyinyi mnajiita madocta, huko mahospitalini mnafanya mambo yenu…mimi siogopi hata mkija kunipiga sindano ya sumu, …kwanza nimeshajifia, nasubiri nini….lakini lazima nidai haki yangu, huyu mwanaume kanifukuza, na kunibambikia makesi kibao kuwa eti kanifumania, ….yeye hayo anayoyafanya huko hospitalini na wewe anafikiri hatuyajui, leo nimekutana na wewe nataka nizitoe hasira zangu zote, kama ni jela, nitakwenda tu…..’ akamsukuma Rose kwa nguvu, na kwa vile Rose hakuwa amesimama vyema, akaserereka na kudondoka chini.

‘Wewe mwanamke unaleta fujo gani hapa kwangu,….’ Ilikuwa sauti ya Adam, akiwa kasimama kati kati ya mlango, na alipoona Rose kalala chini,harakaharaka alimwendea na kumsuka yule mwanamke pembeni halafu akamshika Rose mkono kumsaidia kusimama, lakini Rose akakataa kusaidia alijiinua na kujfuta michanga, na halafu akataka kuondoka…

‘Rose samahani kwa hili sikujua kuwa huyu kichaa amekuja ….ngoja nimuonyeshe kuwa na mimi ni kichaa zaidi yake…’ akasema na kumgeukia yule mwanamke alianza kumpiga vibao, na yule mwanamek akawa anazuia kwa mikono yake, halafu akaokota kibao, kibao hicho kilikuwa na misumari, na kabla Docta Adam hajamuwahi kile kibao kikatua kwenye mikono yake na kwa vile kilikuwa na misumari, kikamchoma, na hapo hasira zikampanda, alianza kutembeza kipigo, hadi majirani wakaja kuamulia, na Rose alipoona hivyo, akajiondokea mapema.

Rose alipofika nyumbani kwake akakuta mtu kaka pembeni ya ukuta, akamsogelea na kabala hajamsalimia yule mtu akasema;

‘Kwanini unapata shida kwa ajili yangu Rose, ….nimekuja kukuaga ili kukuondolea madhila unayoyapata, kwani imefikia hatua natishiwa amani , ….nakuomba niingie nichukuea nguo zangu, niondoke…’ ilikuwa sauti ya Sweetie.
‘Sweetie, usihamaki, hayo yote yatakwisha, hayo yote yanatokea ili iwe sababu, nahakikisha kuwa nitakulinda kwa nguvu zangu zote, twende ndani, ….’ Akafungua mlango na Sweetie akaingia, lakini Sweetie alipoingia akafuta nguo zake na kuziweka kwenye begi akitaka kuondoka.
‘Sikiliza Sweetie, huwezi kuondoka humu ndani, kwasabaabu mimi ndiye docta wako, mimi ndiye niliyekudhamini, vinginevyo ukitoka humu ukajikabidhi polisi, wewe tulia huyo aliyekutishia amani hana lolote anatafuta njia za kunirubuni tu, kwanza nakuomba ujiandae tuinakwenda mjini , nafikiri tukiwa wote nitakuwa na usalama, tunakwenda kutafuta pesa za kulipia deni lako…’ akasema Rose

‘Pesa za kulipia deni langu uankwenda kuzichukulia mjini kwa nani..?’akauliza Sweetie kwa mshangao

‘Nitakuambia mbele ya safari, wewe vaa nguo zako, mimi najiandaa tunakwenda mjini, na huedna tukalala huko…’ akasema Rose na kuingia chumbani na baada ya dakiak chache akatoka, na wakafunga mlango kuondoka, na wakati wanatoka jirani yake akaja, na kumuuliza; `Vipi naona umabadili kitasa, …?’

‘Umejuaje irani yangu, samahani nilikuwa sijakuambia…’ akasema Rose.
‘Sawa mimi ni jirani yako wakati mwingine lazima nitizame usalama wa ndani kwako…na, unakwenda wapi, hujaniambia?’ akauliza jirani yake.

‘Nafika mjini, samahani sikukuambia, nilijua upo kazini, mbona umerudi mapema leo…?’ akauliza Rose

‘We acha tu, nilikutana na jamaa mmoja kanibabaisha kweli, anajifanya anauza madini, basi kumbe kanipa madini bandoa karibu niishie polisi…’ akasema yule jirani yake na kumwacha Rose akishangaa, lakini hakutaka kuonyesha mashangao wake, akamwambia jirani yake;

‘Ni kweli biashara ya madini bandia imeshamairi hapa kwetu, unaweza ukafungwa usipokuwa mwanaglifu, na bishara hiyo inavunja hata imani za watu, uaminifu umekwisha kabisa, hata ndugu, hata majirani wanaweza kuuana kwa kitu kidogo kisicho na thamani…’ akasema Rose

‘Una maana gani kusema hivyo, unadhani kuwa nimechukua madini yake bandia….mimi siwezi kufanya hivyo….kama unatka nikupe ya kwangu ngoja nikupe haya, hayana thamani yoyote…’ mara akatoa mfuko, na wakati anafanya hivyo, Rose akagundua kile kimfuko cha ngozi, ambacho alipewa na wake maasakri, lakini yule jirani yake hakukitoa kile kwani inavyoonyesha alikuwa kayahamisha kwenye mfuko mwingine na akautoa huo mfuko na kumpa Rose

‘Haya chuku haya, ninayo mengi sana….’ Akasema yule jirani yake.
‘Siyahitaji tena, wewe mwenyewe umesema ni bandia , niyachukue ili iweje…yachukue, huenda yatakusaidia, mimi siyahitaji tena,….’ Akasema Rose.

‘Kama ulijua ni bandia kwanini ulikuwa nayo….kwanini …kwanini…’ akajikuta anajiuma uma.
‘Jirani yangu, hakuna kitu kizuri kama kuwa waaminifu na hii ndio siri ya ujirani mwema, unajua wapi tulipotoka, toka shuleni tu marafiki, leo unavunja urafiki kwa kitu kidogo kama hiki, nakushngaa sana, hamna shida, kama nilivyokuambia sina haja nayo…na tuombe mungu nikirudi salama nitakulipa lile deni lako maana nimekuwa mtu wa madeni kila kona…’ akasema Rose na kuondoka huku akiwa kamwacha rafiki yake kaduwaa.

‘Rose wewe ni mtu mwema sana, nashindwa hata kukulinganisha na mtu mwingine, unanifanya niwaze mbali kuwa ningelifurahi kuwa wewe ndio mke wangu, na kama sina mke ,….lakini haiwezekani umri kama huu wangu kutokuwa na mke, najua yupo…swali ni kuwa kama yupo yupo wapi nan i nani na kwanini nakuwaza wewe kuwa ndiwe mke wangu…ila kwa ujumla Rose natamani wewe uwe mke wangu, …’ akamgeukia Rose na kumwangalia kwa makini, halafu akasema `Rose hebu niambie kwanini mrembo kama wewe hujaolewa…?’ akauliza Rose.

Swali hilo lilikuwa kama kisu kilichopitishwa moyoni mwa Rose, ….alitulia kwa muda bila kujibu na kumbukumbu za machungu zikawa zinagubika moyo wake, na alitamani kuondoka hapo mbele ya muuliza swali , lakini mwili haukuwa na nguvu hizo, alibakia kimiya na kujikuta akitoa machozi kabla hajasema kitu, na ili kuficha ile hali aligeuka pembeni haraka na kufuta yale machozi, lakini jamaa alishaiona ile hali..

‘Samahani sana Rose, sikuwa najua kuwa nikikuuliza swali kama hilo ningelikuumiza moyo wako na kukutia kwenye majonzi makubwa. Unajua Rose, mara nyingi nawaza kuwa kwanini wanadamu tuwe tunaumizana, nini faida yake, kwanini tusipendane ili kuijenga hii dunia iwe kama pepo. …sijui labda kwa vile sian kumbukumbu, lakini mimi kamwe sitamuumiza mke wangu, …’ akasema jamaa.
‘Heri ya huyo mke wako kama kauli uisemayo ni kweli maana nakumbuka kauli kaam hiyo niliwahi kutamkiwa na mtu aliye…jifanya anaipenda, name kwakweli nilikuwa nikimpenda sana, lakini mwisho wa siku alikuwa yeye wa kwanza kunisaliti, na sio mmoja tu, ndio maana nikatokea kuwachukia wanaume sana,….lakini cha ajabu….’ Akanyamaza na kugeuka kumwangalia jamaa
‘Cha ajabu nini…mbona umekatisha maneno hayo…..’ akauliza jamaa

‘Cha ajabu siku nilipokuona wewe, nimebadilika kabisa, nikawa nimeanza kuwaona wanaume kama watu wa akwaida kuwa na wao wana udhaifu wao, na hili linaweza likatokea sio kwa wanaume tu hata kwa wanawake kuwafanyia wanaume….sio nateta, bali hili nimelishuhudia kwa bosi wangu mwenyewe alivyofanyiwa na mke wake, bosi wangu nimeishi naye kwa muda mrefu nimemuona insi alivyoo, hajawahii kumsalitii mkewe, lakini mke wake….oooh, ngoja nisimtete, maana dunia hiii…’ akasema Rose.

‘Rose kweli umabadilika kwa sababu yangu, ina maana unanipenda, ….na je kama sina mke nikikuambia kuwa nataka wewe uwe mke wangu utakubali…?’ akauliza jamaa.
‘Weweeee…untaka kusema nini tena, mbona haraka hivyo, halafu kwanini mimi uniweke namba mbili, kama huna mke….naona huanitendea haki, lakini …mmh, nakuombea upone haraka ili kumbukumbu zako zirejee, ili nikujue vyema, ….’ Akasema Rose na kujikuta akiwa na mafikira mengi kichwani.
‘Hujanijibu swali langu Rose...!’ akasema Jamaa
‘Swali gani…? ‘akauliza Rose

NB, Jamani muda, jamani, kwanini nashikwa na vikwazo hivi, natamani kuwa an komputa yangu yenye internet, nahisi kama ningelilala usiku wa manane nikiiandika…TUWEPO

4 comments :

Anonymous said...

YAANI UKIFIKA KATIKA MATUKIO HAYA YA DKT ROSE NA SWEETIE NAFURAHI SANA NA NASHIKWA NA HAMASA KUJUA NINI KITAFUATA! I WISH NINGEKUWA UWEZO KUKUPATIA HIYO COMPUTER ILI UTUWEKEE MAMBO MAZURI KILA MARA. KAZI NZURI SANA MIRA

Anonymous said...

Du! story inafika patamu, jirani kaiba madini feki yaliyokuwa kwa Rose jamani marafiki wengine bwana sasa mtu kukupa ufunguo ndo waingia hadi chumbani hata kama ni rafiki si hivyo. Usijari M3 mungu ni mwaminifu siku zote na atakupa haja ya moyo wako, inaweza ichelewe lakini itakuja tu usichoke kumwomba. Jane

Anonymous said...

happy for u dr Rose, ulipe deni lkn pia pole kwa maumivu ya mapendo ya kutaka kuwa first choice!!!! Mhuja anampenda mke wake hata ktk kupoteza kumbukumbu zake....
kazi nzuri m3 na weekend njema

emu-three said...

Wapendwa wangu mliotangulia kuwa nami kivitendo nashukuru sana kwani nilikuwa na wasiwasi kuwa kuna makosa mengi maana sijapata nafasi ya kukagua(ku-edit), wakati nimefika sehemu hiyo nilipoishia bosi huyo kaingia....do nashukuru sana kwani nilikuwa na wasiwasi kuwa kuna makosa mengi maana sijapata nafasi ya kukagua(ku-edit), wakati nimefika sehemu hiyo nilipoishia bosi huyo kaingia....