Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, July 6, 2011

Dawa ya moto ni moto-31Docta Mtani akiwa ofisini kwake akimilizia kazi zake baada ya shughuli nyingi za mchana,…akiwa kajinyosha kwenye kiti chake mara aksikia meseji ikiingia, alipoitizama, aliona ilitumwa muda, lakini inaonekana ilichelewa kumfikia, alipotizama akaugundua meseji hiyo imetumwa kutoka kwenye namba ya simu ya Inspecta…Akajikuta anashikwa na mshangao kuiona ile meseji na ilivyoandikwa ilikuwa ya kinamna. Na hapo akakumbuka kuwa kuwa alipokea simu ya Inspekta karibuni ikimuuliza kuwa na yeye atakuwepo huko, aliwaza na kujiuliza hayo maneno `na yeye atakuwepo huko ‘….Huko wapi… na mwanzoni alidhania kuwa labda alimuhitaji wakutane kule ufukweni kwenye mazoezi…lakini walikuwa hawajawasilina muda, na hawakuwa wameahidiana hivyo, kwani yale maneno yalionyesha kama vile waliongea kitu cha kufanya, na Inspekta alikuwa akitaka kujua kuwa na yeye atakwenda…wapi lakini
Alipowaza hivyo, na akijua Inspekta ni rafiki yake, aliamua kwenda ufukweni, ambapo mara kwa mara walikuwa wakikutana na Inspekta kwenye mazoezi, walikuwa wamesitisha hayo mazoea kwa muda hivi, akaona labda mwenzake alihitaji wayarudie, au…akakumbuka yale mazingumzo yao kuwa akijiunga na lile kundi aliloshawishiwa na rafiki yake, basi atakuwa akimpa taarifa wakikutana ufukweni, lakini alikumbuka kumibu kuwa hana mpango huo tena…akaona ngoja tu aelekee huko akajionee mwenyewe, basi akavaa nguo zake za michezo na kwenda huko ufukweni, lakini hakuona dalili yoyote ya Inspekta… hakumkuta, akabaki kuwaza bila majibu, na kila mara alipojaribu kupiga simu ya Inspekta alipata majibu kuwa simu hiyo inatumika, …inatumika mpaka lini?
 Sasa hii meseji ya mwisho ilipomfikia akahisi kuna jambo, hata hivyo hakuielewa vyema ina maana gani, akaisoma tena ile meseji iliandikwa hivi `+ufukweni H-bonyeza 9 mara tatu kwa haraka..uwe mwangalifu…’ akawaza sana kutaka kujua undani wa hii taarifa pepe, na mara akakumbuka enzi za jeshini wakati walipokuwa kombonia moja na Inspekta, walikuwa wakitoroka, na ili kupeana taarifa kuwa afande anakuja wakawa wamebuni maneno ya siri ya ufupisho, kama neno litaanza na x, ujue huko kuna hatari, kama neno litaanza Y, ina maana uje lakini akili kichwani kwako…kama litaanza na `+’  ina maana unahitaji msaada…sasa hii mesji ilianza na `+’…hapo akajua kuwa Inspecta yupo matatani!
 Alijiuliza afanyaje,kwasababu hilo lilitakiwa lifanywe na maasakari wenzake kama kweli yupo matatani, yeye sio askari, na mawazo hayo ya jeshini yalikuwa enzi hizo, ..yeye aliamua kuenedelza fani yake ya udakitari , mwenzake akakimbilia uasikari, sasa iweje amshirikishe kwenye fanisio yake…, akakumbuka kuwa Inspecta alishawahi kumwambia kuwa huko ofisini hakuaminiki tena, ina maana huenda kuna watu wanashirikiana na wabaya , au wanakuwa hawapendi kazi fulani ifanyike, kwasababu zao wenyewe, kwahiyo ndio maana kamuamini yeye, kutokana na urafiki wao wa siku nyingi… lakini hata hivyo, yeye sio askari, atakuwa na uwezo gani wa kufanya lolote, na ikiwa kuna hatari atafanyaje.. hana silaha, silaha aliyo nayo ni maalumu kwa kujilinda akiwa kazini kwake, sio nje ya ofisi yake Hapo pia akakumbuka maneno ya Inspecta kuwa ukishapitia jeshini, wakati wote wewe ni askari, …`wewe ni askari’, unatakiwa ujiandae kwa vyovyote, na ukiambiwa nenda vitani na taifa lako huhitaji kujiuliza mara mbili…
‘Huyu inspecta anahitaji msaada wangu…’ akasema na kuingia ofisini kwake , akavaa nguo zake maalumu na kuondoka hapo ofisini kwake bila kuaga, alikuwa anaijua vyema hoteli iitwayo `ufukweni’ kwahiyo akaona aelekee huko kama meseji livyotaja, kwani herufi `h’ mbele yake inamaanisha `hoteli’, haiwezekani ikawa `ufukweni  beach’ kwa ajili ya mazoezi. Akiwa anawaza hili ya Ufukweni Hoteli akamkumbuka rafiki yake katika fani ya udakitari aliyekuwa akija kumshawishi sana , eti ajiunge na kundi moja ambalo nia yao ilikuwa haieleweki kwakwe…akakataa kabisa, lakini alipokuja kumuulizia baadaye baada ya Inspekta kumshauri ajiunge, alishangaa kuona huyo rafiki yake wa udakitari akimruka na kushangaa hayo meneno, na kusema akamruka na kusema kuwa hajawahi kuja kwake kumshawishi kitu kama hicho…hakuamini siku hiyo, na ili kuondoa mtafaruku akaona anyamaze , na hajawahi kwenda kwake tena!
 Alipoamua hivyo akaondoka na kuelekea huko hoteli ya Ufukweni, na alipofika hapo kama ilivyo kawaida ya mahoteli makubwa ya kimataifa, alikuta taratibu nyingi za kiusalama,  hata hivyo kwa vile alizijua taratibu hizo kabla, haikumuwia taabu kwani ilikuwa sio mara yake ya kwanza kufika hapo, akajifanya anatafuta chumba kwa ajili ya wateja wake toka nje, na hili alishawahi kulifanya kabla akaambiwa kumejaa, lakini kwa vile yeye ni docta na anajulikana anaweza kupatiwa vyumba vya dharura, …na kweli akapewa chumba kimoja cha dharura kama walivyokiita, huwa analipa baadaye, kwa kujulikana kwake, akafanya taribu zote…halafu yeye mwenyewe akaelekea kwenye hicho chumba, akiwa kaweka masikio yake  wazi, kama atasikia lolote lakumsaidia.
 Wakati mwingine hisia hukutuma kwa lile unalolitarajia…huu ni msimamo wa docta, kwahiyo hakukata tamaa na wakati anapita pita nje, akasikia watu wakiongea mmoja alisema kuwa `leo kuna mnuso…naona wakubwa wote wapo humu…tusicheze mbali..’ akamwambia mwenzake, wote walikuwa katika sare za humo hotelini, hapo Docta akasimama kusikiliza huenda ikampa mwanya wa kujua zaidi…
‘Wewe na mnuso bwana , kwani kwenu huli..mnuso utakupeleka pabaya , kumbuka tumeambiwa tusiingie kabisa ndani,…mimi nilitumwa jana kuhakikisha kuwa mitambo ya chini inafanya kazi, nilikaguliwa kama sio mfanyakazi wa humu, nahisi kuna watu wanatakiwa huko chini, na nilipoichunguza ile mitambo, nikaona kuna jambo, …unajua kuna mitambo inayoingiza gesi kwenda chini, na gesi ile, sio salama, ..sijui kunapikwa nini huko chini, wanaunguza vyuma…kuna kitu nahisi …lakini tuyaache hayo…maana hayatuhusu…’ akasema mwenzake
‘Lakini wewe bosi anakuamini sana …, unafikiri kuna jambo baya analifanya huko chini..?’ akauliza mwenzake
‘Huwezi jua…Na sina maana ya jambo baya…huenda likawa sio baya, lakini …sijui. Hata hivyo mimi nimekuwa nikijiuliza huu utajiri wote kaupata wapi, hilo la kwanza,…na watu kama hawa wenye utajiri lazima wana maadui, …kwahiyo huko chini anaweza kapatengeneza kupambana nao…na kitu kingina  mimi huwa napewa taarifa kuwa nikafanye kazi fulani kwa maagizo ya mkubwa, lakini tangu nifanya kazi hapa sijawahi kumuona huyo bosi hasa wa hii kampuni, wengine wanasema ni docta, wengine wanasema ni mfanyabiashara wengine, wanasema hivi na vile,…lakini sura yake haijulikani kabisa…sasa hebu niambie huoni kuwa kuna jambo humu…’
 Docta akaona asisimame pale muda mrefu wakamshitukia akawa anaondoka huku akiwaza na kusema ‘Kumbe kuna jengo chini kwa chini..’ akakumbuka kuwa lipofika hapa siku moja alikaribishwa na kuambiwa bosi yupo ofisi za chini, hakuelewa wana maana gani  …lakini hakujua kabisa kuwa kuna jengo la chini kwa chini… akawaza  sana hilo na kutamani kuingia huko chini aone kuna nini…akasema kautundu kadogo kanaruhusiwa. Akaondoka hadi kwenye lifti ilipoingia akabonyeza namba ya kwenda chini, lakini haikusogea, akabonyeza mara nyingi haikusogea, na baadaye akatoka mle kwenye lifti na kuanza kutembea tembea,…mara akili ikamtuma kusoma ile meseji aliyotumiwa na Inspecta…`bonyeza 9 mara tatu haraka, lakini uwe mwangalifu..
 Alipokumbuka haya maneno alirudi  kwenye ile lifti akaingia na kubonyeza zile namba tisa kwa harakaharaka, mara waaah,…akashutikia kunafunguka kwa chini na akajiona akizungushwa kwenye ile lifti upande upande halafu ikatulia, alipoona hivyo akabonyeza tena ile namba tisa mara tatu…oooh, hiyo lifti ikaanza kushuka kwenda chini, ilishuka kwa haraka sana hadi chini. Alipofika chini akasubiri kidogo na lifti ikafunguka, akatoka nje ya ile lifti na kujikuta kwenye kivaranda chembamba, upande mmoja wa varanda ni vyumba na upande mwingine ni ukuta tu..akatizama vile vyumba, aliviona vimefungwa…
 Akiwa anawaza haya, akili yake ikamtuma kwenye ile mishale iliyowekwa kama kuelekeza mtu aelekee wapi , akasogea, lakini akawa anashangaa jinsi kulivyotulia, kulikuwa kimya cha kutisha, ingawaje taa zilikuwa zinamulika na unajiona kama upo nje, lakini ukimya wake ulikuwa wa kuogopesha, ilihitaji moyo kuendelea kufuatilia mambo ambayo hujui mwisho wake ni nini. Na moyoni akawa anajiuliza hivi akiulizwa anafanya nini humo atajibu nini, na je usalama wake upoje.
Docta tangu akiwa jeshini, alijifunza kitu kuwa hisia mara nyingi humtuma mtu kwenye usalama, na ukiona hisia zinakukataza jambo ujue kweli kuna tatizo, lakini kama zinakusukuma kulifanya ujue kuna heri, kwahiyo akaona afuatilie hizo hisia zake zinavyomtuma…akaanza kutembea kwenye ile varanda, akifuatilia ile mishale ambayo ilikuwa ikionyesha kwenda mbele…akaifuatilia hadi mwisho, alipofika akakuta ukomo wa ile varanda na kuna mlango , ulioandikwa usiguse huku…akaona kweli asiguse huko huenda kumeegeshwa umeme, akageuka kutizama alipotoka, hakuona dalili ya mtu, lakini mara akasikia kama kitu kinagonga…
‘Kweli nimesikia kabisa kitu kinagonga…’ akasema kimoyomoyo, na moyo ukamwenda mbio, akatuliza masikio ili kujua ni wapi, …sasa akasikia kwa uwazi zaidi, katika chumba kilichokuwa mkono wake wa kushoto alisikia sauti ya kugongwa kwa ndani…akakisogelea kile chumba, na alipofika hapo, akasikia sauti ya kugongwa kwa ndani, akaushika ule mlango kuufungua , haukufunguka, akautizama kwa makini…akachukua funguo zake, huwa ana ufungua mmoja aliowahi kupewa na rafiki yake mzungu, unaweza kufungua kitasa chochote, akaona ndio wakati wa kuutumia , potelea-mbali.
Potelea mbali, kajaribu mara ya kwanza haukufungua, akajaribu tena na tena, na wakati ameshakata tamaa, mara huo… ukafunguka, akajikuta akikohoa mfululizo, kwani harufu iliyotoka ndani ya kile chumba , ilikua mbaya…!!
 `Hii sio harufu ya gesi,…mamama…’ akajikuta akisema kwa sauti, na akataka kuurudishia ule mlango haraka, lakini macho yake yakatua kwenye mwili wa mtu aliyekuwa umelala pale ndani…akashangaa, na kujiuliza inakuwaje, katika hali kama hii kuwe na mtu ndani, akachukua kitambaa na kujifunika puani na mdomoni akajitosa, na kuingia mle ndani, halafu akamshika yule mtu mkono mmoja akamvuta kwa nje..
Alipomfikisha , akaufunga ule mlango ili ile harufu inayotoka mle isiendelee kusambaa kwa nje , hakutoa kile kitambaa alichokuwa kaziba mdomo na pua, akaendelea kumvuta yule mtu mbali kabisa na pale, kuikimbia ile harufu mbaya ya gesi….alipofika umbali mzuri, akatoa kile kitambaa na kuanza kukohoa huku akitafuta hewa …alikohoa mfulululizo, akitamani atoke mle, lakini akajua kuwa ana mgonjwa au maiti yupo mkononi mwake, lazima afanye kazi yake….akajitahidi hivyo hivyo, na kumuinamia yule mtu ili ampe huduma ya kwanza…mamamama..hakuamini macho yake…oooh, mungu wangu…

NB,Samhanini sana  muda wa kuendelea kwa leo hautoshi…naona niishie hapa kwa muda, tukutane sehemu ijayo!

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Subira said...

Mapigo ya moyo yanaenda mbio, yaani utafikiri mimi ndiye niko ndani ya hiyo hoteli uko chini. Hongera sana M3 ni hadithi chache sana za kiswahili siku hizi zinzoweza kusisimua kama hii.

Subira

emu-three said...

Subira nashukuru sana kwa kunipa moyo,kwani wakati mwingine ukiona hakuna mtu aliyesema chochote ninahisi huenda watu hawakuipenda.Tuendeleeni kuwa pamoja katika hitimisho la kisa hiki

samira said...

m3 mambo yamenoga tupo pamoja yaani nimeguswa na kisa hiki siku ukiniona kimya sijacomment ujuwe nimetingwa sana si unajuwa mambo ya mbali

emu-three said...

Samira sina wasiwasi na wewe,nisipoona comment nitajua umetingwa ila kama binadam nitakuwa na wasiwasi kujiuliza vipi mpenzi wangu wa blog anaumwa nini! Nakushukuru sana kwa mapenzi yako ya dhati. Na wengine wote tupo pamoja:-)

Candy1 said...

Nilipotea kidogo lakini nipo kama kawa kaka yangu...naona mambo yanaendelea kupamba moto na jinsi unavyoendelea kusoma yaani uhondo unazidi..natamani isiishe hehehe...haya sijui Inspekta kapona...na hao wengine wote mmh...wamejua kuwapata!...Maneno nae sijui kapotelea wapi mmmmh...kama nilivyosema nipo ili nijue!

emu-three said...

Candy, wangu, nilikuwa na wasiwasi, kweli, cha muhimu TUPO PAMOJA tena kama kawa, KARIBU TENA

emu-three said...

Jamani computa ninayotumia imevamiwa na huyu `mrusi'..oh, virus, sasa inafanyiwa ukarabati nashindwa kujua itachukua muda gani, kwa leo, ikiwa safi, basi sehemu yenu inayofuata tutairusha hewani...mambo yapo pale pale...je Inspecta atapona, au ndio kayeyuka na ile gesi, je Maua , Maneno, Bosi, wapo wapi? na wale wazee je? na huyu jamaa ni nani? Haya na mengine mengi tutayapata kwenye mfululuzo wa hitimisho...TUWE PAMOJA

Anonymous said...

Aaaaaaaah!!!! m3 my Boss. Pole sana. Tupo pamoja, ila ndo kazi za watu zinatushika.

Nilifungua Blog hii kwa hamu ya kusoma ile hadith yetu. Masikini kumbe komputa ni mbovu? Pole sana. Tumemis jamani. Natamani isiishe Boss. Hadith hii ni Bombaaaaaaa!!! ile mbaya visa ndani ya visa. God bless u. Tunga vitabu Boss wangu. Wasije wajanja wakakifanyia kazi na kukitoa wao jasho lako. Mjini hapa Boss Take Care.

Jitahidi my Boss, kuonana na watu wahusika na utoe vitabu vyako. Mi ninaimani vitanunuliwa tu. Kwani ni vizuri na vina mafunzo.

Au mkuu tuanze kupa-blish vitabu, vijarada na magazeti kama Chigongo. Usikate tamaa anza kutafuta wawekezaji, ufungue ofisi na uanze ku-deal na hii kitu my Boss. Nitasikia uchungu sana kama kazi zako zitaibia na wajanja wa mjini. (Hayo ni mawazo yangu tu mkuu). Lakini Mungu wako yupo Pamoaja nawe.

Kazi njema mkuu.

BN

emu-three said...

Bosi wangu BN, usikate tamaa, siunajua zile zangu za kutokukubali kushindwa, nimekorokochoa hapa na pale, wakati hawa mafundi wanasua sua...na mungu bariki nimeweza kuingia kwenye mtandao na harakaharaka nikaweka sehemu inayofuata, nilikuwa sijaipitia vyema, lakini nahisi ipo sawa..TUPO PAMOJA BOSI WANGU NA WENGINEO