Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 8, 2011

Mpende jirani yako-3


Mara lilikuja gari dogo zuri, lapiga kona na kuingia barabara ndogo ambayo tulikuwa tumesimama, akapiga hodi kuomba tumpishe, sote tukapigwa na butwaa, ikabidi tusoge pembeni naye akapita na gari lake na kuligeuza kuingia kwenye geti. Sijui alikuwa haoni huo mosho uliotanda ndani, au aliuona na alikuwa na nia ya kusaidia au ndio mwenye nyumba kaja…tulikuwa tunajiuliza kinafsini.


Mara mlango wa gari ukafunguliwa na taratibu tukauona mguu ukitoka nje, ndio ulikuwa mguu wa mwanadada, na baadaye akajitokeza nje, mwanadada mrembo, mweupe, akiwa kavaa mawani meusi, akatizama getini , halafu akatizama ule moshi unatoka ndani, …hakugeuka kutuangalia, alichofanya na kurudi ndaniya gari lake akiwa kaacha mlango wazi, na kuchukua simu yake, na kuanza kutafuta namba halafu akaita `halloh’ ya kizungu

Aliongea kwa kiingereza na sauti tuliisikia akimwambia huyo anayeiongea naye kuwa ndani ya nyumba kunatoka moshi na inaonakeana kuna moto au umetokea ndani, na anashindwa kuingia kwani hajui nini kimetokea, akawauliza je wana taarifa yoyote, kwani kuna watu wamejaa hapa nje, na uslama unaweza ukawa mdogo…’ akasikiliza, halafu akataka kufunga mlango, nafikiri akiwa na maana ya kuondoka. Lakini kabla hajaondoka polisi akamsimamisha na kumhoji,…

Yule msichana akavua ile miwani yake kidogo kuonyesha nyusi za macho na kumwangalai yule polis kwa dharau, halafu sijui alihisi nini , akafungua mlango wa gari lake na kuangalia mbele akimsikiliza polis anasema nini, kama vile anampotezea muda wake, na hakuwa na haja ya kusikiliza nini polisi anamuuliza

‘Tulikuwa tunataka kujua wewe ni nani, kwani kama unavyoona kuna moto umetokea ndani ya hiyo nyumba, je wewe una uhusiano wowote na wenye nyumba hii?’ polisi akamuuliza kwa unyenyekevu.

‘Ndio mimi ..eeh, ni mudogo wa..mweny nyuma, I am a young sister of her…so, wunasemaje?, nikusaidie nini zaidi…’ akasema kwa Kiswahili cha kujilazimisha. Huenda kweli hakijui vyema, au ndio kalowea lugha ya kiingereza au ndio kujionyesha yote kwetu ilikuwa sawa.

‘Sasa kwanini huulizii kuhusu watoto, kuwa wapo salama na kama hawapo salama wapi walipo kumetokea nini huko ndani, unakuja kwa dharau, au unatuona sote humu hatuna maana…’ akahoji mjumbe. Na yule msichana aliposikia habari za watoto akashituka na kutoka nje ya gari, akaishika simu yake kutaka kupiga, lakini polisi akamzua.

‘Subiri kwanza, tukuelezee nini kimetokea hapa, kwani naona una utoto-utoto, hiyo ndiyo tabia ulioyoionyesha hapa. Kwa ufupi kumetoka moto, na bahati nzuri majirani waliwahi kuuzima, ila watoto…’ kabla polisi hajamaliza yule msichana macho yakamtoka kwa wasiwasi na kushika kichwa, huku anarukaruka,…

‘Mama yangu wee, ina maana watoto walikuwa ndani, …mimi najua wapo shuleni…mungu wangu…’ akaanza kupiga kelele. Watu wakashangaa kume ni mswahili na Kiswahili anakijua vyema.

‘Sikiliza mwambie dada yangu watoto waokolewa na majirani, na wamepelekwa hospitali ya Amana, apitie huko…kwasababu walichukuliwa hapa wakiwa wamezimia’ akasema polisi

‘What,…Amana, yaani nyie mnawapeleka watoto Amana…you’r not serious…ok, let me call my sister..sorry’ akasema na kuchukua simu na kumwelezea ndugu yake kuwa aende Amana awachukue watoto wapeleke Agakhana…’ akasema huku anatizama nyumba ikiwa sasa inafuka moshi tu.

Kila mmoja pale alikata tamaa na wengine wakaanza kuondoka , kwani waliona hawo watu sio binadamu wa kawaida. Polisi nao wakamuacha na kuendelea kulinda hapo, ili wamsubiri mwenye nyumba aweze na kuhakikisha kuwa kila kitu kipo salama na sisi tukajiondokea, tukishukuru mungu kuwa watoto wapo salama , kwani walioongoizana nao alitoa taarifa kuwa wamazindukana na hawana majeraha, zaidi ya kukosa pumzi na mshituko. Aliyeumia kidogo ni yule mfanyakazi, yeye aliteguka mguu.

Ikawa tunasikilizia tukiwa na wasiwasi wakushitakiwa kuwa tumevunja mageti ya watu na kuingia ndani bila idhini. Lakini hilo halikutokea na siku ya pili yake mjumbe akatupitia kuwa mwenye ile nyumba katualika kwake ana jambo la kuongea na sisi majirani zake, ikiwemo kutoa shukurani. Mjumbe akasisitiza kuwa ni muhimu kama majirani kuonyesha moyo wa upendo hata kama jirani yetu hana huo moyo.

‘Nawaombe mfike, mimi kama mjumbe wenu nina jambo la kuongea siku hiyo na tutaona kuwa kweli jirani yetu kajirudi au katuita kutukoga. Mimi kama mjumbe lazima niweka mazingira ya eneo langu kuwa salama na watu waishi kwa upendo….Nawaomba sana msikose.

Watu walijitokeza kwa wingi, hata mimi nilishangaa, kwani nilidhani watu hawatakuja, wangedharau, lakini haikuwa hivyo, nikajiuliza wamekuja kwasababu kuna chchote, na huenda kwasababu jamaa anazo anaweza akagawa ahsante, au kuna ambalo mimi silijui…nikatulia kujionea.

Nilipofika getini, nikakutana na mlizi mpya, akaniuliza nina shida gani, nikamjibu kuwa ni jirani na tumeambiwa na mjumbe tufike kuna maongezi…Yule askari akanifungulia , nikaingia ndani na kukuta mafundi wakiwa katika harakari za matengenezo. Sikuona ajabu kwani jamaa alisema atajenga haraka iwezekanavyo, na hali itarejea kama kawaida.

Nilikuwa kwa pembeni viti vimepangwa na kulikuwa na akina dada wawili wa kutukaribisha. Nilimuona baba mwenye nyumba akiongea na simu na mama mwenye nyumba alikuwa kaka kwenye kocho lililotolewa pale nje, na alikuwa amekaa akiangalia mlangoni jinsi watu wanavyoingia, huku kashika kipepeo kujipulizia upepo kwani ni kipindi cha joto.

Nilisogea karibu na mwenye nyumba ili nimpe pole ya janga lile, lakini alijifanya kama hanioni akasogea pale alipokaa mke wake na kumnong’oneza kitu halafu wote wakainuka na kuingia ndani. Nilibaki nimeduwaa, nikajigeuza na kuelekea pale walipokaa wenzangu.

‘Mjumbe katuitia ili tuje kunyanyasika, au,…tunakuja humu ndani tunahojiwa kama wahalifu wakati katuita mwenyewe, halafu ukimsalimia baba mwenye nyumba hakuitikii, wala hataki kushikwa mkono…’ akalalamika jamaa moja.

‘Msiwe na wasiwasi, nyie tulieni, mimi mjumbe wenu nipo, mimi na msaidizi wenu tunajua nini la kufanya, msihofu kabisa, ila tuwe pamoja..’ akasema mjumbe na kabla hajamaliza geti likafunguliwa na gari lile la mdogo wa huyu mama mwenye nyumba likaingia. Na likaelekea sehemu yanaposimama magari.

Akatokeza yule mwanadada na nguo ambazo, …kila mtu aliguna, labda alikuwa kwa ajili ya kuogela ndio maana akavaa hizo nguo, lakini ina maana hakuambiwa kuwa kuna sherehe fupi ya kuwashukuru majirani, au ndio kusema nini…watu wakaguna na kukaa kimiya. Yule mwanadada bila kujali akapita na kuelekea ndani huku akiwa anashika pua, …nini maana ya ksuhika pua, tukajiuliza, ina maana kuna harufu ambayo imemkera…tukapata jibu la haraka.

Baada ya muda wakatoka baba mwenye nyumba na mkewe na mdogo mtu akatokeza, sasa hivi akiwa kavaa nguo ya heshima, lakini alionekana kukwerwa na kitu, kwani kila mara alikuwa akishika pua, na kukunja uso kuonyesha kukerwa, na mimi kwa vile nilikuwa sehemu ninayowasikia wa kiongea …nilimsikiwa waziwazi akiseme;

‘Its too hot and stinky…’

‘Eeeh, keep cool, they will leave soon, we …’ sikuweza kusikiliza zaidi nikamsogela jamaa ynagu kuwa tuonoke zetu. Jamaa yangu akasema, subiri, kuna jambo linakuja la maana sana. Nikatulia kwenye kiti.

Jamaa yetu alisimama na kuongea kwa kufupi kuwa anashukuru sana kuwa watu wamemsaidia kuokoa watoto na mfanyakazi wao, …ingawaje amepata hasara kubwa ya geti la ndani kwani hilo lilitenengenezwa kitaalamu, na limevunjwa bila kufuata utaratibu mzuri na sehemu kubwa ya nyumba kwa nyumba imeungua, lakini walikuwa na bima na bima wamesema watalipa, kwahiyo hiyo haina shaka..’ akaendelea kuelezea uzuri wa nyumba yake na mambo mengi ambayo yalionekana kama kujionyyesha kuwa hana shida na haikumgusa sana.

‘Lakini nimesikitika sana kuwapeleka watoto wangu hospitali kama ile, mungewapeleka hospitali nyingine kama Aga khan halafu sisi tungelipa tu…’ akaongea mengi na kila hatua watu walizidi kukerekwa. Kwani badala ya kuomba msamaha na kuonyesha kuwa majirani wamefanya la maana kubwa ilionekana kama kulaumu zaidi.

Alipomaliza akamuomba mkewe aseme lolote, lakini mkewe akaonyesha mkono , akionyesha saa, nafikiri alikuwa akionyesha kuwa wanapoteza muda. Na hapo mjumbe akasimama, kwani liona huo ndio muda muafaka. Akasogea mbele ya watu na kuonyesha mkono kuwa wakati umefika…

‘Ndugu jirani yetu, ingawaje nakumbuka ulisema kuwa `huna jirani’ lakini majuzi umeona kuwa kweli una jirani, na kama una chembe ya ubinadamu, ungewabusu majirani zao miguuni, kwani leo ungekuwa huna watoto…watoto walikuwa wamekwisha zimia wakati tunaingia na moto ulikwa ukiwajia,..hebu jaribu kufikiria hilo..je unawapenda watoto wako? Ni swali utaliona la kijinga, lakini kama kweli ulikuwa uanwapenda watoto wako, basi leo hii ungempitia kila jirani na kumpa mkono wa ujirani mwema..’

Mke wa yule jamaa akainuka na kuingia ndani huku akilalamika kwa kiingereza, ambacho wengu hatukukisikaia kwani mawazo yetu yalikuwa kwa mjumbe wetu. Na baadaye mdogo mtu akamfuata dada yake kuonyesha wazi kuwa tunawapotezea muda.

‘Kama mnavyoona, mimi nilidhania kuwa umetuita kama majirani kuonyesha kuwa mumejifunza kitu fulani, lakini …sijui labda mwenzangu unasemaje..’ mjumbe akamgeukia msaidizi wake kumnongoneza kitu. Na wakati huohuo waandalizi wakawa wanapitisha vyakula kwenye masinia maalumu ani yake kukiwa na vyakula vikiwa vimefungwa vizuri, na vinywaji, …watu wakawa hawahangaiki na hivyo vyakula wanamsikiliza mjumbe wao.

Ndugu mwenzetu, jirani ni muhimu sana katika maisha yetu, huwezi jua leo na kesho, huu ni mtihani mdogo sana, na huwezi jua kwanini mtihani kama huu ulitokea..kwahiyo kwa niaba ya wote walioshiriki kuikoa familia yako na nyumba yako kwenye janga, hilo tunakuomba msamaha kwa hayo uliyoona tumekuharibia,nia yetu ilikuwa njema sana, kuwaokoa watoto. Naomba niishie hapa ili tusikupotezee muda wako, na wenzangu kama mna lolote la ziada manakaribishwa, mimi naomba niondoke nawahi kwani nina majukumu muhimu sana…’ mjumba akageuka na kuanza kuondoka, akafuatiwa na msaidizi wake, na majirani wakainuka na kutoka mmoja baada ya mwingine.

‘Sasa mbona mnaondoka, vyakula hivi atakula nani, …you people, what….’ Akawa anapayuka mwenywe, watu wote wakatoka na kumwacha yeye na waandazi wake na chakula chake. Sijui ilkuwaje badaye. Lakini ilipofika usiku tuligutushwa na milio ya bunduki, na kalele za watoto. Ilichukua nusu saa, kukiwa na majibishano ya milio ya bunduki ya hapa na pale. Ilikuwa kama vile mnasikiliza picha ya masikioni, nani ainuke, nani atoke nje,…tulipoona kimya ndipo watu wakatoka nje.

‘Vipi ilikuwa wapi..?’ tukaulizana,

‘Kwa jirani yetu aliyetualika mchana kutukoga, na sijui kama kuna usalama, maana ilikuwa kama vita..’ akasema jirani mmoja. Na wakati akisema hivi tukasikia vilio vya ving’ora vya polisi vikifika, na baada ya nusu saa vikaondoka na hakuna hata mmoja aliyetka kuisogela hiyo nyumba.

Kesho yake yakawa mazungumzo ya hapa na pale, ilisadikiwa kuwa waliofika sio majambazi, bali ni wanachama washirika wa huyo jamaa, kumbwa alikuwa na kundi lake la uharamia, na wao kwa wao wakadhulumiana, na katiuka kudhulumiana wakawa makundi mawili kila moja likitetea sehemu yake. Matokeo yake ikazuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika pilika pilika hizo jamaa akajeruhiwa vibaya sana na baadhi ya watu wakapoteza uhai.

Uchunguzi ulioendeelea baadaye uligundua kuwa jamaa hakuwa raia wa halali , bali ni wale raia wakimbizi waliojipenyeza na kuishi uraiani, na kuzoeleka , akaoa na hatimaye akazaa, …

Kazi kubwa ya Jamaa huyu na wenzake ilikuwa uharamia wa usiku na husafiri usiku hadi mbali sana na kufanya ujambazi wa hali ya juu, na wakirudi mchana wanavaa vyema wakiwa wafanyabiashara, na wajasiriamali wazuri, hata huwezi kuwafaikiria vinginevyo. Na pia polisi waligundua chumba cha chini kwa chini ambacho kilikuwa kikihifadhi madawa ya kulevya, silaha na madini. Chumba hiki ndipo moto ulipoanzia, na ni sababu ya moja ya milipuko kuleta hitalafu na kufayatuka!

Kundi hilo la ujambazi halikukubaliana na hoja hiyo kuwa mlipuko ulitokea wenyewe, wakamdhania jamaa yao kuwa alipanga njama hiyo ili mlipuko utokee na hatimaye afiche mali na pesa. Katika kutokuelewana huko, wengine wakikubaliana naye na wengine wakipinga , ndipo ikaishia kutupiana risasi!

Huyu ndiye jirani yetu. Kumbe kutokupenda kwake majirani ipo kwenye damu, na hata hivyo licha ya chuki binafasi, pia kumbe alikuwa akificha madhambi yake, na alijenga maeneo kama hayo ili watu wasimshitukie. Na kilichogundulika baaadaye ni kuwa jingo la aina kama hiyo limejengwa kwenye mikoa mingine, na likiwa na malengo hayohayo. Kutokana na `nyodo’ zao wakaambuka’ hata hivyo wahenga walisema za mwizi na arubaini na laana ya kuotokupenda majirani zake ikamwandama, sasa yupo hospitalini akiwa na pingu, anasubiri apone akatumikie kifungo.

Huo ndio mwisho wa kisa hiki.

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Anonymous said...

Kweli huyo jamaa hana uungwa ule tunaujua wa Kiafrica. Lakini nashukuru kuwa kagundulika na hawa jamaa wapo wengi, wanajifanya wanazo, wanajenga mahekalu, na humo ndani wanaficha mambo yao!

John Maembe said...

Jamani Mnaona mambo hayo!!! yamefukia mpaka ukweli umejulikana.
Halafu kuna kitu kilikuwa kinanitatiza nilihisi lakini sikutakata kuandika hisia zangu za kuwa huyu jamaa si wa kwetu kabisa kwani watz hawanatabia hizo lakini hata kama wapo hawawezi kuifikia tabia ya jamaa na mkewe, pia kuna wakati niliona jamaa ana akili kuliko mkewe kumbe wote ni Boggers na hicho walichokivuna ndio dawa yao.
Kisha na Wanawake wetu wasijirahisishe namna hiyo 7b jamaa ana mawe au katoka nje au vp ujue mi sielewi?
Jamii ya EA ijifunze kutokana na kisa hiki hasa Wanawake ndo mi nawaona kama wamejisahau hivi au niseme kweli "ULIMBUKENI NI UJINGA"

Leo ni siku yenu mjifunze mengi ikiwemo kuondokana na ugonjwa huo wa ulimbukeni, Kila la kheri womens.
Mwisho sina zaidi. Ahsante Em-3

emu-three said...

Ni kweli kabisa mkuu(John Maembe, nakushukuru kwa kuwa mpenzi mzuri wa blog hii),
Kama ulivyosema, hisia zako hazikuwa mbali kabisa na hisia za watu wengi hapa, walishahisi kuwa sio mzawa(mbongo), na hata ile tabia ilijionyesha, lakini sio kuwa watu wasio wazawa wana tabia kama hizo, ila ukiangalia mila na desturi zetu, tunaoishi pamoja, tunajuana `ujirani wa kuombana chumvi haukwepeki'...ujirani wa kusaidiana hili na lile, kutembeleana na nk, sasa huyu alijionyesha toka awali kuwa yupo mbali kabisa na tabia hizo!
Tahadhari sana , Watu kama hawa wapo sana, tusifiche nyoka chumbani, ipo siku atakugeukia mwenyewe. Ni vyema tukihisi `sintofahamu' ya mtu aliyehamia karibuni, ni vyema tukawajulisha wenye dhamana ya usalama wa nchi, ili keshoo na kesho kutwa likitokea jambo, ...tukujue tumeosha mikono yetu!

Candy1 said...

Yes, story yenyewe sana inaonyesha vipi huyu mtu na familia yake hawakuwa majirani wema ila ukiangalia upande mwingine je anaweza akawa anawalinda majirani zake pia? I know it is very unlikely but it is possible, hujui alikuwa na malengo gani. Anyway its a very interesting story na ni fundisho zuri sana kwa wote. Tuwapende majirani maana hujui kitakutokea nini...yes keep your things private but know the boundaries. Naishia hapo

emu-three said...

Kweli dada Faith, umenipa kitu muhimu sana, kuwa pia alivyofanya hivyo ilikuwa bora kwa majirani, ...aliwalinda kinamna ambayo hata yeye au wao walikuwa hawajui. Unaweza ukafanya jambo, likaonekana ni baya, lakini kumbe lina heri yake humo ndani.
Chunguza kisa kwa makini na soma utagundua nini dada Faith(Candy alimaanisha)
rejea maneno yake haya...`ukiangalia upande mwingine je anaweza akawa anawalinda majirani zake pia?'
Shukurani TUPO PAMOJA, NATUMAI SIKU YA KUZALIWA KWAKO NA SIKU YA AKINA MAMA ZIMEENDA SALAMA.
Kuna kisa kidogo cha siku hiyo, nakiweka vyema.

Anonymous said...

Jamani mi nasuuzika na hizi simulizi zako, yani
kama ukitunga kitabu au movie utauza bt, nahisi watu wanaweza
kukuibia watunge vitabu kama uinaweza uwawahi, ushauri tuu
Dina I.

Anonymous said...

MKUU KULE KWA MICHUZI UMEANDIKA POINT KWELI NA MIE NILILIFIKIRIA HILOHILO MZ. KUHUSU WAKINA MAMA KUNA WAKINAMAMA USWAZI WAMEPIGWA NA WAUME ZAO WAMEBADILIKA MAISHA KUNA WAKINA DADA WLAIKUWA MALAYA SABABU YA MATATIZO PENGINE WAMEJIKAMUWAM PAKA KUFUNGUA BIASHARA NA KUSAIDIA, UKIENDA USWAZI UTAONA VITUO VYA KINA MAMA VINASAIDIA WENYE MARAZI... VINALEA WATOTO BILA KUTAKAK UTOKEAK ILA SIKU MICHUZI KUONESHA KAMA WANASAIDIA. SABABU WENGI NIMEONA WANAOSAIDIA MICHUZI WANAOPIGWA PICHA NI KUTANGAZIA MANUFAA YAO TU. MZ

Yasinta Ngonyani said...

Nimesoma kisa hiki tangu mwanzo na nimefuatilia mpaka mwisho. Watu kama hao wapo wengi sana ALIDHANI AMEPATA kumbe amepatikana. Yaaani we kweli utaishije bila majirani? Halafu walikuwa wajinga sana maana wao walichojali ni mali tu hawakujua kama wanaweza kupatwa na ajali. Kama angeonyesha utu siku ie nyumba na watoto walipata shida nadhani asingekuwa katika hali hiyo leo kwani majirani wangekuja na wangemwokoa lakini sasa AMEKIPATA CHA MTEMA KUNI hiyo ndiyo zawadi yake. ...

emu-three said...

Nashukuruni sana , Dina, mkuu MZ, dada Yasinta. Tupo pamoja, na kwaweli ni muhimu kutunga kitabu , najaribu kutafuta `wafadhili' au watu wanaojua jinsi gani ya kufanya, kwani kilichobakia ni kuweka hivyo visa sawasawa na kuongezea minofu hapa na pale. Lakini wapi utaanzia!
Nashukuru sana kuwa TUPO PAMOJA