Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, June 8, 2015

Wagombanapo mafahali, zinazoumia ninyasi

 'Mbona umeshika shavu mwanangu, una matatizo gani’ nilimsogelea mtoto wa jamaa yangu niliyekuja kumtembelea na Yule mtoto alinikimbilia na kunipokea, na wakati ananisindikiza ndanii nikamuuliza kuwa ana matatizo yoyote akasema hana ila mara nyingi anamkumbuka mama yake.


‘Wewe mwanzoni siulisema aheri mama yako kaondoka, kwani ulikuwa hupati raha’ nikamuuliza tena.

‘Mama ni mama tu, ingawaje kweli walikuwa hawanipi raha kwa kugombana kwao, lakini mara nyingine namkumbuka’ akasema.

 `Kila siku baba na mama walikuwa hawaachi kugombana kiasi kwamba niliombea waachane na kweli wakaachana, manake raha ya ndani ilikuwa haipo, siunajua sisi watoto tunapenda kufurahi, sasa ilikuwa tofauti, baba akirudi kazini akimkuta na mama naye karudi wanaanza kutofautiana kitu kidogo tu, mara ugomvi, hata wakati mwingine wanapigana mbele yetu…’ akasema kwa uchungu sana Yule mtoto.

Nilimuuliza kuhusu mama yao mpya akasema wangelitamani mama yao awe kama huyo mama yao mpya. Huyu mama ana roho nzuri ajabu, anatutenda kama watoto wake, hatunyanyasi , hawagombani na baba, sijui labda itokee baadaye kwani hata mama na baba mwanzoni walikuwa wakipendana hivi hivi, lakini huyu naoana yupo tofauti kidogo..’ akasema Yule mtoto, na kauli hiyo ilinipa matumaini kwani mama mzazi anapoondoka katika familia kitu cha kujiuliza ni hali ya watoto, je watapata matunzo sawa na alivyokuwa mama yao?

Niliingia ndani na kukuta familia ya baba na mkewe mpya na binti yao wakiwa wamekaa kwenye makochi yakifahari wakiangalia luninga, nikawasabahi na binti yao kwa adabu akaaga kwenda nje. Baada ya mongezi na salamu mama wa nyumbani mpya naye akaaga kwenda jikoni.

‘Vipi unaonaje maisha mapya?’ nikaadodosa.

‘Sijui nikuambiaje, manake wakati mwingine unakufuru nakusema aheri ningelimjua huyu mapema, kwani ile raha ya ndoa sasa naiona. Huyu ndiye mke ambaye nilitakiwa nimuoe, lakini yote hupangwa na mungu. Unajua kilichoniuzi sana kuhusu mke wangu wa kwanza ni ule ugomvi wake usiochagua mahala tulipo, alikuwa hajali kuwa kuna watoto au wageni, na hakujua kuwa wakigombana mafahali zinazoumia ni nyasi.

‘Watoto walikuwa hawana raha, na hicho ndicho kilichonifanya nami nikose raha na hata siku naitoa ile talaka nililia sana, nikifikiria kuwa mwenzangu anaondoka na watoto je, hutaamini yeye alikuwa na raha ya ajabu, kwasababu kapata uhutu kama alivyodai, na kweli keshaolewa na mume tajiri, na hiyo ndiyo raha yake?

Na mimi nilishasema sioni tena, kwani nilichelea watoto wasije teseka, lakini bahati njema nikampata huyu kimiujiza, hutaamini, na hapo nikawa nimepata jibu la nani anayefaa kwa watoto wangu, je watapata raha na matunzo ninayotaka, jibu hilo nimelipata sasa, watoto wamepata mama wa kweli.

Wanalelewa ile mimi nataka. Jaribu kuwauliza kama wanapata matatizo, kama yapo labda wanifiche, lakini nilishafanya utafiti wa kina na nimegundua kuwa huyu hana ile kasumba ya mama wa kambo’ akawaita watoto wake na baada ya utani wa hapa na pale akawauliza waseme mbele yangu kwani mimi na yeye ni marafiki kama ndugu, kama mama anawatesa au hawamtaki wasema.

Wote kwa kauli moja walisema wanampenda sana huyo mama yao mdogo na hawajawahi kuteswa na mama huyo tangu ajae hapo nyumbani, nilifurahi sana nakajisemea kimoyomoyo kuwa nitajitahidi kufuatilia ili nione kweli huyo mama hana mambo ya chini kwa chini na hawo watoto.

Kwanini nimelileta hili tukio mbele yenu leo, ni huu usemi usemao wagombanapo mafahali(baba na mama) wanaoumia ni watoto (nyasi).

Na hii ipo wazi kwa wanandoa wengi lakini hatutaki kuliangalia swala hili kwa undani wake. Na ubaya wake ni pale wanandoa hawo wanposhindwa kuuficha ule ugomvi wao mbele ya watoto wao. Watoto wanapoona hili wanateseka sana, hata kama hawatasema mbele yenu, lakini akili zao zinawaza mengi, na hali hiyo inawajengea dhana potofu kuwa huenda ndoa ni ugomvi, mbona baba alikuwa akimpiga mama, mbona mama alikuwa akimsema baba mbele yetu na kubishana naye hata kupigana, kwani mimi nina tofautii gani…dhana kama hizo hujijenga kichwani mapema, chanzo ni kutowajali watoto wakati mpo kwenye migogoro yenu nyie wanandoa.

Je suluhisho ni kuachana? Hebu tuchangie hili kwa hekima na busara!

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

5 comments :

Anonymous said...

Sikubaliani na dhan kuwa talaka ndio suluhishi la wanaogombana. Je ikitokea bahati mbaya kila unayeoa ni matatizo utaishia kuoa na kuacha.
Ndiyo yapo matatizo yanaweza kukufanya uakasema basi naacha, lakini mimi sishauri hivyo kabisa, kwani ndoa ni shida na raha.

chib said...

Nimepita kukusalimia ndugu yangu.
Nashukuru kwa kunitembelea pia

emu-three said...

Nashukuru sana Chib, tupo pamoja, na natumai utakuwa ukifanya hivyo kila siku

Anonymous said...

mvumilivu hula mbivu lakini unaweza pia ukala vilivyo oza. usitese nafsi yako kwa ajili ya mtu cha msingi ni kuangalia yupi anaweza kukufaa wewe na watoto wako

Anonymous said...

Mvumivu hula mbivu, lakini usivumilie sana kwani kuna swala la muda, weka nafasi na malengo ikishindikana amua moja, asikudanganye mtu, huna uhakika na mungu kuwa huyo ndiye aliyepangwa kwako, kwahiyo angalia nini unataka ilimrdi usikiuke sheria, kama mume ni mlevi anakupiga au kama mke ni kibaka , mhuni wewe utavumilia tuuu...hapana mungu hajasema hivyo