Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, March 18, 2010

Kazi kwelikweli

`Baba mimi nataka nisomee umeme' mwanangu alisema wakati nawasha mshumaa, kwani umeme ulishazimka, na hatujui utarudi saa ngapi.
'Vizuri mwanangu, kwanini usomee umeme, wakati ulisema awali unataka kuwa dakitari' nilimuuliza
'Baba sasa utasomeaje udakitari kwenye giza. Kila ikifika usiku wanatuzimia umeme, nashindwa hata kufanya homework...' alilalama huku akijaribu kutafuta mwanga wa mshumaa kama anaweza kujisomea.
'Ni kweli mwanangu, tunahitaji wataalamu wengi, wa umeme, wa udakitari wa ndege nk, lakini utaalamu huo hauji kirahisi , unahitajika kusoma kwa bidii, usisubiri usiku, usiku hatuna mamlaka na umeme, muda wowote wanauondoa..' nilisema huku nikkumbuka taarifa niliyoisikia kuwa mgawo wa umeme utaanza tena.

 Hapa maeneo niapoishi tunapata umeme toka njia ya Kisarawe, kitu mgawo ni desturi yetu, kwani kila ikifika saa moja za usiku hadi saa nne lazima umeme ukatwe, na kurejea ni majaliwa. Nimesikia kuwa transfoma ina matatizo, lakini mpaka lini! Sasa mgawo ndio huo umetangazwa, sijui tutakuwa na migowo mingapi, huu wa dharura na huo ulio rasimi, na bado upo wa kuchangia mkondo(line) ambapo leo mkondo huu unawaka kesho ule....
 'Ni kweli mwanangu kuna haja ya kusomea umeme, huenda katika kusoma huko, mtagundua njia mabadala, badala ya kutegemea maji na mashine za kutoka nje, mnaweza mkagundua umeme wa asili wa jua, na mkagundua mashine nyepesi..' nilimwambia huku nikijua kuwa hiyo sio kazi nyepesi kwani atasomea wapi kama usiku hakuna umeme.
Mchana yupo shuleni, huko nako wanatolewa kwa kutokulipa ada kwa wakati. Sehemu nyingine ya wakati inapotea kwenye usafiri, mpaka akifika nyumbani giza limeshatanda, akitegemea kuwa atajisomea usiku.Na usiku nako, duu, kazi kwelikweli!
From miram3

No comments :