Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSunday, December 27, 2009

Tusipoziba ufa

`Kuna jamaa kakuibia, wakati tunapanda, kwenye msukumano, nilimuona akikupapasa mfukoni, lakini nilishindwa kukuambia , nilichelea asije mmojawapo yupo nyuma yangu akanichoma kisu’ Ni sauti ya jamaa mmoja tuliyekaa naye akiwa ananieleza kuwa nimeibiwa, nilitamani nimzabe kibao palepale, lakini nikaona haitasaidia kitu.


‘Sasa unaniambia hivi sasa isaidie nini, ulitakiwa uniambie wakati uleule ili hatua zichukuliwe, sasa jamaa mwenyewe unamkumbuka sura?’

‘Walishuka kituo kilichofuata, nilimuona wakati anatoka kweney gari, lakini muda huo nilikuwa mbali na wewe’

‘Bado ulikuwa na muda wa kuniambia au ungemwambia konda, hii inaonyesha kuwa huenda mpo kundi moja’ nilimwambia kwa hasira.

Abiria waliokuwepo wakaanza kuingilia kati, wengine wakiniunga mkono kuwa huenda kweli jamaa huyo yupo kundo moja na huyo mwizi, wengine walipinga, ikawa mzozo. Kwangu mini nilikuwa najipapasa mfukoni kuangalia kuwa huenda nina akiba ya nauli, lakini sikuwa nayo, kwani hela niliyokuwa nayo ndiyo hiyo wezi wamajichukulia kilaini. Ilibidi konda anionee huruma , na nashukuru konda yule alikuwa muungwana, tatizo likawa jinsi gani ya kurudi nyumbani!

Visa kama hivi ni vingi, na wanasababisha hali kama hii iendelee ni sie wenyewe wananchi, kwa kupuuzia sheria. Ni vyema tukaelewa kuwa kama sie wenyewe tutashirikiana, mwizi au mvunja sheria anakuwa hana nafasi. Uzaifu wetu wa kuogopa, au kuwalinda wakosaji pale kosa linapofanyika ndio unaokuza makosa na kumfanya mkosaji ajiamini. Kuna maadili mema tuliyopewa kuwa, unapoaana kosa, ni vyema ukachukua mkono wako kuliondoa lile kosa, au ukalikemea au ukalijutia. Kulijutia ni hali duni, ndio kama hiyo unaona mwizi anamuibia mwenzako unanyamaza kimya.

Yupo mama mmoja ambaye mtoto wake alikuwa kibaka, mama yule alikuwa akijua, baba mtu akajaribu kumzibiti yule kijana na mama mtu akawa anamtetea mwanae. Mama alikuwa akipinga vikali, haiwezekani mwanangu awe mwizi, usisikilize maneno ya mitaani hayo. Siku kadhaa wakashuhudia wenyewe mtoto wao akiiba nyumba ya jirani, ikabidi wamwite mtoto wao wamuonye. Lakini tabia ya yule mtoto ikawa ni ileile, na kesi nyingi zikawa zinaletwa kwa wale wazazi, wakawa wanamtetea. Siunajua tena mtoto akiiba siku hiyo wanakula vizuri, wanapata vijizawadi na duka lao linaongezeka.

Wazazi wale hawakujua kuwa wanafuga nyoka ndani ya nyumba. Siku kadhaa wakatembelewa na ndugu yao, huyu alikuwa mfanya biashara, na bahati ikabidi alale chumba kimoja na yule mtoto. Kwa vile yule mgeni, hakuwa nawasiwasi na yule mtoto, akawa anahesabu pesa zake na mali yake mle chumbani ili kesho adamkie Kariakoo kununua bidhaa zake. Mtoto akaziona zile pesa, ibilisi la wizi likamtanda ubongoni, na kwa vile aliziona zile pesa zilipowekwa, na akatoka nje akawabonyeza rafiki zake.

Usiku akajifanya anaenda kukojoa, na mara kundi la vijana wenye nguvu na silaha wakamvamia yule mjomba mtu na kumpora pesa yake yote. Mjomba mtu hakuamini, ni nani angeweza kujua kuwa anapesa, ikabidi amuulize dada yake kuhusu mtoto wake kuwa isije ikawa ndiye kawaambia wezi. Dada mtu akapinga na kumtetea mwanae.

`Sawa dada, lakini mimi ninawasiwasi na huyu mtoto, sidhani kama wezi hawa wangejua kirahuisi kama nina pesa, nawaonya kuwa kama mnajua kuwa mwanenu ni mwizi na mnanyamaza kimya mjue mnafuga nyoka’ Mjomba mtu akaaga akaondoka zake!

Familia ile ilikuwa na duka, na tabia ya udokozo wa yule mtoto ilianzia kwenye hilo duka, mara aibie pip, mara shilingi mia, na wazazi wale waliona wakawa wanamkemea wananyamaza. Kundi la yule kijana likawa kimebanwa kiasi kwamba likawa halina njia ya kuiba, ikabidi wamuombe yule kijana kuwa ili waishi na waendelee kutesa inabidi waibe kwenye duka lao. Kijana mara ya kwanza alikataa, lakini baadaye kwa ushawishi akakubali, kwa mpango kuwa yeye awe nyuma, aihusike moja kwa moja.

Usiku ule wakaliingilai duka na kupora pesa na vitu kadhaa, wakati wanatoka baba mtu akawaona ikabidi aanza kukimbizana nao. Yule kijana muda huo alikuwa kwenye gari na hakujua kuwa anayewafukuza ni baba yake, na kwa vile kulikuwa na uchochoro wa giza akaona huyu mzee anayeingilia mambo yasiyomhusu atawanyimia bahati yao, ikabidi alitoe gari kwa kasi na kumgonga yule mzee.

Kesho yake akarejea nyumbani akakuta mama na baadhi ya ndugu wamejaa, alipouliza nini kulikono, akaambiwa baba yako yupo hoi Muhimbili, niwakusikilizia.

‘Mama, kumbe alikuwa baba, sasa kwanini aliamua kutoka nje, jamani nimemuua baba yangu’ Kijana alipagawa, akajiukuta anaropoka. Mama mtu aliposikia vile naye akaangua kilio, jamani nimemkosea nini Mungu mtoto wangu amenishinda…

‘tulikuambia kuwa mwanao ni mwizi ukakataa sasa umejionea jirani, mwanao kawaibia na sasa hatujui, huenda akawa kamuuana baba yake mwenyewe.

Ilibidi wanachi wachukue sheria mkononi nakuanza kumpiga yule kijana na hatimaye kufikishwa kituo cha polisi na huko alikri makosa yake yote na kuwalaumu wazazi wake kuwa hawakumfuatilia vyema alipokuwa mtoto, hawakumsomesha na wala hawakujali maendeleo yake.

Uvunjaji wa sheria unapoachiwa, unatoa mwanya wa kuonekana kuwa ni kitu cha kawaida. Tumeshuhudia madaladala yakikatisha njia, na sie abairia tunashangilai kuwa dereva wetu anajua kuwahi. Tumeshuhudia mabasi ambayo yanapandisha nauli kinyemela na abiria wanakubali kutoa hizo nauli. Visa kama hivi vinachangia kukuza uhalifu na madhara yake ni kwetu sisi wenyewe. Jamani tusaidieni kulinda sheria zetu kwa manufaa yetu , kwasababu tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Hiyo ni kweli wezi tunawafuga wenyewe, na nina uhakika kama tutashirikiana vibaka wadogo wadogo hawewezi kutuibia