Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, November 23, 2009

Usafi ni tabia

Ni msimu wa matunda, na msimu huu wa matunda hasa, maembe, tunashuhudia pia kulipuka kwa ugonjwa wa kipindupindu. Sina uhakika, kuwa huenda harufu ya maembe huvutia sana inzi. Nimesema sina uhakika, kwasababu haiji akilini kuwa tunda zuri kama hili linaweza likageuka pia kivutio cha wadudu. Lakini tukumbuke kuwa kila kizuri kama kitawekwa mahali sio pake hugeuka kuwa uchafu.
 Tukiwa ndani ya daladala tunashuhudia watu wakila matunda haya na hatimaye kuyatupa makokwa nje ya barabara, bila kujali kuwa huko ni kuharibu mazingira. Huenda ungebuniwa mtindo wa kila gari kuwa na sehemu au chombo cha kuwekea matakataka.
 Usafi ni tabia, na kama tabia hiyo hujaijenga katika maisha yako utaona kila ufanyalo ni sawa tu. Ukivuta sigara hadharani unaathiri afya za watu, lakini wewe unajionea sawa tu. Utakuta watu wanatema mate ovyo, na wale wenye mafua wanatoa mafua yao na kuyabwaga popote pale. Hizi ni kasoro za kibinadamu, na huenda zimejijenga tangu utotoni.
 Nakumbuka wakati tunasome sekondari ya Umbwe, tuliambiwa ni lazima kila mmoja awe na leso. Tuliambiwa hivi kwasababu, sehemu ile ina baridi sana, na baridi na mafua ni ndugu. Hii ilisaidia sana kwani tungeshuhudia uchafu wa mafua kila mahala. Baada ya kumaliza pale wengi wetu hatukupenda kuachana na leso. Naona kama kweli tuanataka kujenga tabia ya usafi basi jiji lijitahidi kuweka sheria na kuzifuatilia. Mfano kama atapatikana mtu akitupa takataka, apewe adhabu kali , ya faini au hata kifungo. Angalia wenzetu Kenya hili wamefanikiwa je sisi kwanini tushindwe.

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Sheria ni msumeno, lakini msumeno huo unahitaji mshikaji ili muweze kukata. Sheria zetu ni kama povu la soda