Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, November 4, 2009

Taswira na hali halisi

Jana alikuja nyumbani rafiki yangu mmoja katika maongezi yangu na yeye aliniambia neno moja ambalo lilinifanya nitafakari sana na hatimaye kuja na wazo la kutunga hadithi itakayoitwa `Dunia yangu'
Aliniambia kuwa `unajua bwana Mira, kila ukionacho usifikiri ndivyo kilivyo. Chukulia mfano, jua, au mwezi, hivi kweli uvionavyo ndivyo vilivyo. Hapana, ile ni kama taswira tu. Jua ni kubwa na kali, mwezi ni mkubwa, lakini vyote tunaviona kwa udogo ule.
Maisha yetu mengi yamejaa utaswira, mambo yanavyotendeka ni kinyume na huenda ikawa tofauti kibisa na kusudia au ukweli halisi. Angalia wanasiasa wakija majuukwaani, ahadi wanazozitoa, utafikiri ni kweli, lakini kihalihalisi ni utaswira wa kukugubika macho ili yeye anayetaka akipate kwa kupitia kwako.
Unapoajiriwa mwajiri anakupa matumaini ya kuwa utapata ajira nzuri, kipato kizuri, na unajituma. unamzalishia mamilioni, lakini unacholipwa ki kiduchu kati ya mamilioni yake, siku ya siku unaondoka hakujali. Hii ni kukuonyesha kuwa katika dunia hii kila tukionacho usidhani ndio ukweli, au ndio umbile halisi. Wewe amini, usiamini.
Je mwenzangu unaweza kumuelewa huyu jamaa, niliwaza peke yangu mwishowe nikaamua kutunga hadithi hii ya jamaa aliyeamua kuunda dunia yake kwa kutumia `rasilimali ya watu' Aliwachukua watu wenye utaalamu wa halio ya juu, akawapeleka shule, akawajenga anavyotaka yeye, ili baadaye aiunde dunia yake kwa kutumia utajiri wake. Pesa anazo, uwezo wa kuwasomesha anao, ananafasi nzuri serikalini...je ataweza, ngoja tujaribu kuitunga hii hadithi, ingawaje muda wa internet ni mdogo na uwezo wangu kifedha haupo, lakini kila nikipata nafasi nitaiendeleza na hatimaye tutaona `ubinadamu wetu katika ndoto za kujitajisha na kujijengea usultani hapa duniani
Ninachotaka kusema ni kuwa chochote tutakachotaka kufanya tujue yupo rabana, yeye ni mjuzi na anajua nini tunachotaka kufanya. Usivuke mpaka nakujiona wewe unaweza ukamiliki, ukatakabari na kujiona wewe ni wewe. Hakuna, wapo waliokuwepo na utajiri uwezo na sasa wapo wapi, imebaki historia. Soma, mwanzo wa hadithi, `dunia yangu.
From miram3

No comments :