Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, October 28, 2009

Msongo wa kimaisha

  Ilikuwa saa nne asubuhi, nikiwa nawahi ofisi moja kwa rafiki yangu, nikiwa nakatisha mtaa, niliona kitu cha ajabu sana, sikuamini kuwa inaweza ikafikia hatua ile kwa binadamu. Nilitafakari huku naharakisha kufika huko ninakokwenda ili nipate angalau nafasi yakuchungulia kwenye blog yetu hii, kama kuna ujumbe wowote na ili niongezee chochote.
 Tukio hili lilinifanya nikumbuke kisa nilichokuwa nimekiandika kwa Kiingereza mwaka 1996 kutoka katika diary yangu nakukiita `mind confusion’ ikiwa na maana kuchanganyikiwa. Hii hali inaweza ikamkuta mtu yoyote, lakini kama hujawahi utaona ni kitu cha ajabu kwako.
 Jamaa alikuwa amevaliwa `vipande vitatu’(three pieces suit)’ mkononi ameshikilia begi la mkononi(briefcase) na huenda humo ndani kuna kikomputa kidogo(laptop), akiwa nadhifu kabisa(anakwenda na wakati)
 Kwanini nikasema lilikuwa tukio la ajabu, kwasababu jamaa mmoja tuliyekuwa naye alisema jamaa huyu kamaliza mlimani, akapata kazi mahala, lakini ghafla kampuni yao ikaweweseka kimasoko, kwahiyo baadhi ya wafanyakazi wakapewa barua ya kupunguzwa akiwemo yeye, huyo jamaa na huyu anayetuhadithia.
 Alituambia kuwa, wote na huyo jamaa walikuwa wakifanya kazi pamoja, na anamjua jamaa ilivyo, kuwa ni mchapa kazi na huwa hana muda wa maongezi na watu mpaka amalize kazi yake. Na walishangaa kumuona na yeye kapewa hiyo barua, lakini kila mtu alijua kuwa haitachukua muda atapata kazi sehemu nyingine, kwasababu ya elimu, uchapakazi na lugha inapanda kama kazaliwa nayo, lakini imekata miezi sita wanashangaa jamaa hajapata kazi, ofisi hadi ofisi na kila anapofika anaambiwa kazi hakuna acha viambatishi vyako tukipata nafasi tutakuita, siunajua tena kazi za Tanzania ni kujuana au mkono kwa mkono kama wasemavyo wamitaani.
 Cha ajabu sasa ni nini? Watu wanakosa kazi watu wanahangaika hii ni kawaida. Lakini kwa tukio hili nililolishuhudia kwa macho yangu nililiona silakawadia. Kwasababu ilichotokea ni ile hali ya mtu kufikiri na bila kutambua yale mawazo unayofikiri ukayaweka kwenye vitendo bila kukusudia. Hii inawatokea watu wengi, na ukiwauliza watasema sio kweli. Ushawahi kumkuta mtu mwenye akili zake barabara anaongea peke yake njiani? Sio kuongea tu, bali mikono kichwa hata miguu ikawa inatenda matendo bila mwenye kukusudia?
 Wakati napishana na huyu jamaa nilimsikia akiongea peke yake; `haki ya mungu sasa nikienda ofisi nyingine wakinijibu nyodo nitaongea kiingereza changu cha Kimarekani, na najua watabaki midomo wazi, siunajua tena wengine moofisini kiingereza nicha kubahatisha na kwa vile watakuwa hawajanielewa vyema watanipa nafasi haraka yakuongea na bosi wao, na nikifika kwa bosi wao nitaongea Kiingereza cha Muingereza mwenyewe, na najua kwa vile yule bosi wao ni Muingereza atazimia na kusema `welcome sir, I like your English…’ na najua atasimama na kunikumbatia namna hii. Bahati mbaya au nzuri, mbele yake alikuwa akija mama mmoja wa kizungu, mama huyu alikuwa na haraka zake akitaka kuvuka upande wa pili wa barabara, na ghafla akawa uso kwa uso na jamaa huyu na ghafla akawa amemkumbatia mama wa watu bila kutegemea
 Yule mama akawa ameduwaa, na yule jamaa hali ilivyomrejea vyema akagundua amefanya jambo la ajabu na hapohapo aibu ikamuingia. Alichokifanya ni kuomba msamaha na kuangusha Kiingereza chake amabacho hata yule mama alizimia nacho. Yule mama alibakia kucheka na bila yeye kujalia akamshika yule jamaa mkono na kumuomba wavuke upande wa pili alipoegesha gari lake ili waongee vizuri. Kilichotokea baadaye tuliona yule jamaa akiondoka na yule mama wa Kizungu ndani ya gari lake. Watu wakabaki kutunga hadithi.
  Tukio hili linamaanisha jinsi gani ubongo wetu unavyofanya kazi, ukishirikiana na mwili, inafikia hatua hali mwili unajituma bila kujua kutokana na madhila yaliyokuzonga. Ndio maana nasema kwa yule ambaye hajapatwa na matatizo ataona ni jambo la ajabu, lakini wengi wetu tunajkuta tukiongea wenyewe njiani bila kukusudia. Mawazo matatizo na hali ngumu za kimaisha zinafanya akili zetu zisiwe na amani, ingawaje nchi yetu ni ya amani, lakini sio akili zetu. Na kama yale tunayofikiri yangeliwekwa hadharani na kutendeka, huenda ya Burundi na Ruanda yangelikuwa ni `trailer’. Huu ni msongo wa mawazo, unaotaokana na maisha magumu.
From miram3

From miram3

No comments :