Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 5, 2009

Miti ni rafiki wa kweli

Jua lilikuwa kali kiasi kwamba mate yalianza kukauka mdomoni, nilitafuta sehemu ya kutuliza mwili angalau maji, lakini ilionekana yote yapo mbali. Mbele kidogo tukakuta sehemu ya miti, kivuli kilionekana kidogo, lakini kutokana na ule upepo wa miti, tulijihisi tupo ufukweni mwa bahari, mmmh, ama kweli miti ni marafiki wa binadamu. kwani haikuchukua muda uchomvu na kiu vilipungua, na moyoni nikasema, kama kweli wanadamu tungekuwa wapenzi wa miti kama miti ilivyo wapenzi kwetu, tungeneemeka.

Hali ya joto hivi sasa Dar, inatisha, na sehemu nyingine na nchi, na huenda sababu kubwa tunachangia wenyewe. Kwa mfano inakuwaje mtu akakata miti kabla hajapanda miti mingine, ni sawa na kubomoa nyumba ukitaraji kujenga nyingine,sasa je kwa muda huo ukiwa kwenye ujenzi utaishi wapi?

Jiji la Dar, limekuwa likiongezeka watu siku hadi siku, na zile sehemu za pembeni mwa jiji ambapo kulikuwa na miti, kama miembe na minazi sasa inaishi watu na miti hiyo imekatwa, na ingefaa basi kila nyumba ingekuwa na mkakati wa kupanda miti. Kwa maoni yangu halimashauri ya jiji au kila kata kungekuwa na sheria kuwa kila nyumba ni lazima kuwe na miti angalau minne, iwe ni sheria. Na ni bora ichaguliwe aina ya miti yenye mashina yasiyo na unene mkubwa, ila iwe na majani mengi, na kama ingewezekana, miti ya matunda ingekuwa bora.

Kama hili la kupanda miti kila kaya lingepita, nina imani kuwa baada ya mwaka tu jiji la Dar lingebadilika na kuwa la kijani, na raha yake tungeiona, kwasababu miti ni rafiki wa binadamu, wewe ukitoa hewa chafu kwao ni hewa nzuri na miti ikitoa hewa chafu kwetu sisi ni hewa nzuri.

Ndugu wapenzi nilikuwa na mengi ya kuandika ili tueleimishane, lakini nipo kijiweni na gharama za internet cafe ni kubwa, tuombe mungu nikipata kibarua tutakuwa pamoja kila siku.
Ujumbe wangu ni kuwa, panda mti kwanza ukisha ota vizuri ndipo ufikirie kukata mti, kwani ukikata kabla ya kupanda, huenda mti ulioupanda ukafa kwa sababu mbalimbali, na matokeo yake ni joto kuwa jingi, ukame na afya zetu kuzorota. Tupende uhai wetu na afya zetu kwa kuipenda miti, kwani miti ni rafiki wa kweli.
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Umenena kweli muungwana, kama wangeipitia blog yako wahusika, wangekupa mkono kama sio wanafiki