Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, September 16, 2009

UJIRANI MWEMA

Nilipofika nyumbani tu kitu cha kwanza nilichohitaji ni kitanda, kweli malaria ilikuwa imenishika na dakitari alinishauri nipumzike nyumbani. Kwasababu ya usafiri mgumu, foleni njiani nilijikuta nafika nyumbani nikiwa nimechoka sana huku kichwa kikiuma zaidi na zaidi.

Nilijitosa kwenye kitanda huku nikiwaomba jamaa zangu wasinisumbue hadi hapo nitakapoamuka mwenyewe. Wakati nageukia ukutani nilisikia sauti kali ya mziki ikitoka nyumba ya jirani, nilitamani nikimbie, lakini kila muda ulivyozidi ndivyo sauti ilivyozidi kusikika kwa nguvu zaidi, na kama vile kuna mashindano, mwingine chumba cha pili yake akafungulia mziki wa taarabu. Nilichukua mto kujifunika masikio ili sauti ipungue lakini haikusaidia kitu. Uzalendo ulinishinda nikamuita mke wangu aende kuwaomba hawo majirani zetu wapunguze sauti za redio zao.

Ilipofika saa tisa, watoto wakawa wamerejea mashuleni, walifika kunisalimu nikawaitikia na kuwaomba wasipige makelele. Lakini dakika tano baadaye watoto wa majirani wakawasili hapo nyumbani. Jirani kuna eneo la kiwanja ambacho kimekaa muda bila kujengwa, kwahiyo watoto hufanya uwanja wa mpira. Watoto wa majirani walipofika kwangu, kuwaalika watoto wangu wajiunge na wao kwenda kucheza mpira walianza kupiga mpira huku na huko,kelele, vurugu zikatawala. Niliwaza sana, hawa watoto wetu wanahitaji maeneo maalumu ya kuchezea, lakini maeneo kama hayo hayapo, wafanyeje? Matokeo yake ndio haya, mpira hadi bustani za maua. Nilijipa moyo, nikawaomba watoto wangu wawashauri wenzao wasipige kelele, kwasababu mtoto wa mwenzako ni wako pia. Kwa hilo nilikuwa kama nimechochea, wale watoto wakafanya kama mzaha, nakuwakebehi watoto wangu, huku wakirusha mpira juu ya bati.

Ilifika jioni sijapata usingizi na kichwa kikawa na maumivu makali,kiasi kwamba niliona dawa hazifanyi kazi. Nilitoka nje nikaoga nakuelekea msikitini huko ndipo nilipata kausingizi kidogo.

Haya ndio maisha ya maeneo ya kwetu na ndio maisha tunayoishi nayo, maisha haya wengine huyaita ya uswahilini, kwangu mimi neno hili silipendi kulitumia kwani halileti maana kamili zaidi ya kujizalilisha, na kuzalilisha lugha yetu ya kiswahili. Ni bora tuyaite maisha ya mitaani kwetu kuliko kutumia jina ambalo limepangwa kuizalilisha lugha yetu.

Mimi najiuliza inakuwaje mtu una redio yako au TV, unaamua kufungulia sauti ya juu kiasi kwamba hata wewe mwenyewe ndani hufaidi huo mziki wenyewe au hicho unachokisikiliza. Hii ni kasumba ya ubinafsi, kasumba ya kujifikiria mwenyewe na kutokujali wengine. Kwanza sauti kali kamahizo zinatuasiri masikio yetu bila kujua, pia inawaathiri watoto wadogo ambao ngoma za masikio yao bado ni laini , na baya zaidi huwaumiza wagonjwa ambao wapo kitandani, wanahitaji utulivu au wale wenye magonjwa ya shinikizo la damu nk.

Matatizo kama haya yanatokea pia kwa wale wenye shughuli zao za harusi au shughuli nyinginezo ambazo zinahitaji miziki au ngoma, na shughuli hizi ni za kukesha. Shughuli hizi nyingine zinafanyika kwenye maukumbi ambayo yapo kwenya makazi ya watu au pia hufanyika nyumbani kwa mtu binafsi. Kelele za usiku kucha zinawafanya watu wasilale kwa amani. Je hivi kwanini hatupendi kuwafikiria na kuwajali wengine ambao kutokana na kelele hizo wanaathirika, achilia mbali watoto.

Nahisi serikali za mitaa wangeliangalia hili, kwa kuhakikisha viwanja vya wazi vinakuwepo na pia maukumbi yaliyopo kwenye makazi ya watu wajenga namna ambayo itafanya sauti zisitoke nje, hili linawezekana kama kweli viongozi wetu watalisimamia. Lakini pia sisi wenyewe tunatakiwa tuwe wastaarabu, kwa kujichunga wenyewe. Kuna vitu ambavyo kila mmoja anatakiwa ajichunge mwenyewe kwa kuthamini ujirani, jirani yako ni mtu muhimu sana,kama ungelijua hilo, ukimthamini na yeye atakuthamini. Ni vyema kila jambo tunalotaka kulifanya tukawa tunajiuliza je hili ninalolifanya halimuathiri mwingine, na je kama mimi ningetendewa hivi ningefurahi.

From miram3.com

1 comment :

Anonymous said...

Umelonga wanawane, wape vidonge vyao