Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, October 24, 2022

MUNGU AKIPENDA -54

 


MUNGU AKIPENDA-54
------
Mtu wa jamii alisimama na kumuendea baba wa watoto watatu..
'Ndugu yetu, baba wa watoto watatu, wengi hawajapata nafasi ya kukusikia ukiongelea masahibu yako...
'Wamekuwa wakikuongelea tu, na hata kukushutumu...una haki ya kuelezea na kujitetea..au sio..?' Akauliza
Na mtu huyu akatabasamu na kutikisa kichwa kukubali.
'Mimi ninajua pamoja na changamoto ulizopitia umeweza kuitetea familia yako vyema...' akamshika mkono jamaa huyo, kama kumpa hongera!.
Mtu wa jamii akawageukia watu waliofika hapo, sasa walishaongezeka, akasema....
'Kabla baba wa watoto watatu hajaongea, kuna maswali mengi yameulizwa...na mengi ya maswali hayo yalishatolewa majibu yake.
Kiukweli..kutokana na muda tuliopewa...hatutaweza kurudia kila kitu leo ...
'Ila Kuna jambo ninataka kuliweka wazi kumuhusu mtu mashuhuri kwa cheo ni mpelelezi wetu...'
Aliposema hivyo watu wakaanza kusema sema maneno....
'Ni vyema nilielezee hili mimi mwenyewe..' aliposema hivyo watu wakatulia...
'Mpelelezi sivyo kama wengi walivyoanza kumuhisi, na hata kumteta huko mitaani, kuwa labda na yeye ni miongoni mwa hao watu wasiojulikana...hapana!
'Hata mimi kwenye mikutano yetu ya wazi, nilikuwa kama namshutumu hivyo, kwangu ilikuwa natumia tu, ya kumshinikiza, ili afunguke tumjue nani yupo juu ya hayo yote.
'Mpelelezi ni mchapakazi na muadilifu.. huko tulipomdhania hayupo kabisa, alitimiza wajibu wake, akiangalia pande zote...' mtu wa jamii akageuka huku na kule kama kumtafuta mpelelezi alipo.
Siku hiyo Mpelelezi hakuwepo kwenye kikao hicho..
'Hebu kwa leo tupitie kidogo siku ile hospitalini ....
Kuna swali limeulizwa, je kwenye jeneza, kulikuwa na nini...mbona kama tunakwepa kuliweka hilo wazi ...
Ni kweli kuna maswali hapo...je ulikuwa mchanga, maiti, au ...si ndio hivyo...?'
'Mnakumbuka niliwaambia nilirudi kumfuata mpelelezi, nilipofika ndio wakati mpelelezi na mwalimu wanatoka, ndani ya kile chumba wakiteta jambo..
Niliwasikia...., je walikuwa wakiongea nini...!!!'
---
'Mwalimu ulichoona mle ndani ya jeneza usiseme lolote hasa kwa mtu wa jamii..'
'Kwanini sasa mpelelezi! Ile ni mali halali ya watoto, imetoka kwenye eneo Lao .!
'Naelewa hilo kabisa, kuna maswala nyeti siwezi kukuelezea , ni maagizo toka juu,..
'Maagizo toka jùu, kwa vipi tena ! Mimi nahisi hayo maagizo yametoka kwa mmoja wa hao hao watu wasiojulikana...au na wewe umo..?'
'Hapana...ni kwa ajili ya usalama tu , siwezi kukuelezea kila kitu, ila wewe ukiulizwa sema uliona udongo, tumia uwongo wowote hadi hali itakapokuwa shwari..
'Baada ya hapo..?' Akauliza mwalimu
'Baada ya hapo, inabidi tusubirie tu, tutapata maagizo mengine...'
'Sijui kama nitaweza kudanganya, hasa kwa mtu wa jamii, unamjua alivyo kwenye maswali yake..'
'Wewe sema hivyo, huyo mtu wa jamii niachie mimi,... ninajua yeye kapewa kazi na hiyo familia, atajitahidi ili apate malipo mazuri..
'Lakini si ndio kazi yake, na kiukweli, kuacha hiyo dhana ya kulipana, anachofanya ni kutetea haki, ni vyema tumuunge mkono au...
'Sikiliza hayo ni maagizo nyeti, mimi ni lazima nitimize wajibu wangu...wewe fanya nilivyokuelekeza mengine niachie mimi.. unasikia...!
'Sawa mkuu....' akasema mwalimu.
Hapo ndio mtu wa jamii akajua kuwa huko kwenye chumba kuna mali....je inahusikanaje na kuchumbuliwa lile shimo .
Mtu wa jamii aliposikia hivyo, akasogea nyuma na kujificha, kuhakikisha hao watu hawamuoni, baadae akachukua simu na kuwapigia watu wake.
Hakutaka tena kuongea na mpelelezi, akaamua kuchukua hatua nyingine kwa watu anaowafahamu yeye...
Swali likabakia je hayo madini ndio yalichimbuliwa kwenye lile shimo. Na nani alifanya hivyo... ...na kwanini yalifichwa kwenye jeneza..!!!
----
'Ndio maana nikamtambulisha baba wa watoto watatu, atuambie yeye alipotuacha pale kwenye kile kikao cha dharura
Huyu jamaa yetu, alienda wapi, na huko alipokwenda aliwakuta watoto, au alikutana na nini...
Akageuka kumkaribisha baba watoto watatu aongee
Baba wa watoto watatu akasimama, na watu wakampigia makofi.
Akiwa kavalia vizuri, suti na tai shingoni...
'Niwashukuru sana wote...ni kweli, katika maisha ya kulea familia sisi wanaume tunakutana na changamoto nyingi..
'Nilikutana na mama mdogo mumuitavyo, nikawa nafanyakazi kwake..naendesha magari yake ya kusafirisha bidhaa hadi nchi za nje !
'Kuna kipindi nililemewa sana na madeni, kila nikikwama nakopa kwake...nikijua nitarejesha ..lakini haikuwezekana..!
Deni likazidi kuwa kubwa..
'Na kuna kipindi niliwahi kupata ajali, sio mimi, nilikuwa naendesha hilo gari, nilimpa rafiki yangu gari afanyie kazi, huko mbele akapata ajali..
'Mimi ndiye mwenye dhamana, na jamaa yangu leseni yake ilikuwa imepitwa na wakati..kwahiyo deni likawa kwangu.
'Sikuwa na jinsi deni lilipozidi kuwa kubwa ikabidi niweke dhamana ya nyumba....ndio maana mama mdogo akadai nyumba ile ni kwake .
'Kwa muda ule sikuwa naelewa mikakati ya mamdogo na watu wake...
Hii mikakati nimekuja kuifahamu baadae sana!
'Japokuwa kwenye kesi tulishinda...lkn kwa masharti nilipe kwanza deni la watu...
'Ni dhahiri kuwa tungeliweza kulipa deni la mama mdogo, na tukachukua nyumba yetu lkn kiubinadamu, tukaona tumuachie tu hiyo nyumba.
'Ni kweli, alinitega akijua eneo hilo litakuwa na thamani ya mali ardhini..lkn pia alilenga ayachukue maeneo yetu mengine, kwa jinsi deni lingeliongezeka.
Lakini mungu alitusaidia tuliandikisha meneo hayo mengine kwa watoto..sehemu ambayo ndio ilikuwa na madini. Na hata hivyo awali hatukujua kuwa eneo hilo chini lina madini!.
'Nilifungwa jela kwa makosa ya kushutumiwa kuwa mimi nahusika na kifo cha mke wangu, hii ni kesi ya kubuniwa tu..hebu hata nyie fikirieni shutuma kama hiyo, nitahusikanaje kumua mke wangu
Ilikuwa ni kesi ya uwongo tu!
'Kuna mengi yalitokea hadi kufikia huko, lkn nilikuja kugundua kuwa wao walitaka wanipate kwa njia hiyo, waniweke sehemu, wanifanye ndondocha, nikubali kuuza eneo la watoto.
Tuachane na huko....sasa twende siku ile nilipoachiwa jela...
'Siku ile nilijua nitaachiwa, nililiona hilo kwenye njozi...na niliona wapi watoto wapo...niliona kuwa sasa watoto wapo salama...lkn kuna mali yao inaporwa.
'Mali gani hiyo...'
'Kwenye njozi..sikuweza kuelezewa moja kwa moja, nilionyeshwa jeneza linagombaniwa na watu..na limechukuliwa kutoka nyumbani kwangu.!
'Hebu wewe fikiria Jeneza na mali wapi na wapi....nilijaribu kuoanisha vitu hivyo viwili.. sikupata jibu...!
'Kuna njozi nyingine nilielekezwa niitafute ile namba. Kuna namba awali niliipata hivyo hivyo, nikiambiwa ina siri kubwa, hiyo namba nimpatie mlinzi!
'Mnakumbuka nilifanya hivyo....
Kuna mambo mengine binafsi kati yangu na mlinzi huyo, hayo mambo hayahusiani na hili jambo letu....huko tupaache...!
'Siku ile wakati natoka kwenye kikao, niliwaaga wajumbe niliowakuta mle kikaoni...kuwa nawatafuta watoto, lkn akilini ilikuwa kwenda kuiokoa hiyo mali ya watoto.
'Ni mali gani, kiasi gani...sikujua hilo..nilielekezwa hivyo tu...ni ndoto zisizo na mpangilio.. mara jeneza, mara mali..!
'Kuna kitu pia sikukielewa hapo...kumbe kuachiwa kwangu kule gerezani, nikiambiwa sina kesi..' hapo akatikisa kichwa kama kusikitika.
'Mhh.... kumbe pia ilikuwa ni mtego, siku nilipoachiwa kulikuwa na watu nyuma yangu, watu hao walipewa kazi ya kunifuatilia kila hatua.
Sasa ni watu wa upande gani...mimi sijajua hilo ..!
'Kwenye njozi nyingine...niliona napita njia nyembamva kuipata hiyo mali, pembeni kuna wanyama hatari..
Kuna kitu ambacho kilijitokeza kwenye kila njozi....namba..hiyo namba ilionekana kuwa na siri nyingine ya jinsi ya kugundua wapi mali inaweza kupatikana!
'Nilivyoonyeshwa awali..kabla hata sijaachiwa, watoto au mali vipo kwenye jengo kuu, hata nilipompatia mtu wa jamii ile namba, nilijua watoto wataenda kupatikana...!
'Pamoja na mambo yetu mengine na mlinzi, nilijua hata watoto wangu watakuwa wamefichwa huko.
'Njozi hiyo ya mwisho ndipo niachiwe, haikunielekeza tena jengo kuu, ilinielekeza niende hosp, nikaonane na doct..
Docta gani sasa....nilijiuliza ndani ya njozi...sikujua zaidi kumuhusu docta mkuu!
Mara ndani njozi..nilijiona namuendea docta msaidizi...na ndoto ikakatika hivyo, haikuendelea...
'Kwa taarifa ambazo nimezisikia hapa....ni kuwa mali hiyo iliibiwa jengo kuu, na ilipelekwa wapi,... ndio hapo sikuweza kujua siku ile nilipoachiwa..
'Na aliyeiiba hiyo mali, hakuwa na lengo baya, lengo lake ni kuiokoa hiyo mali kutoka kwa watu wabaya, na kuihifadhi kwa ajili ya watoto.
'Nafikiri hadi hapo mtajua ni nani aliyeifanya hiyo kazi..sasa alifanyaje, kama mtahitajia atawaelezea yeye mwenyewe..
Hebu sasa niwarejeshe siku ile nilipofika pale hospitalini ilikuwaje.
-----
Nilifika hospitalini, niliwakuta madocta wa kawaida tu..
'Docta msaidizi yupo wapi ..' nikauliza
'Wapo kwenye kusimamia ukarabati wa jengo..'
'Jengo gani...' niliuliza, kwa vile wale madocta na wafanyakazi walikuwa hawajui kinachoendelea wakanielekeza
Nilipofika kwenye eneo hilo nililoelekezwa, nikasikia mashine zikifanya kazi...ni mashine za kuchimba
Chumba kimefungwa kwa ndani..lkn unasikia mngurumo fulani...
Kwenye njozi nilionyeshwa jeneza..jeneza ni la maiti...je mali na jeneza vina uhusiano gani ...ilikuwa ni fumbo kwangu!
'Labda jibu hilo nitalipata kwa docta msaidizi....huyu mtu hatukuwa tunaivana tokea awali, kutokana na historia za nyuma
'Ila akaja kuwa rafiki yangu nilipokubali kushirikiana nao kumuhusu mke wangu, kipindi hicho sikuwa nafahamu lolote....nikaona nije kutumia urafiki huo..
Sikujua kadara hii...
'Nikafika kwenye eneo nilipoambiwa docta msaidizi yupo, unajua hata sijui nikikutana naye nitamumbia nataka nini kwake...watoto , mali, au jeneza..
'Ila akili yangu ilinituma nikaonane na huyo docta...na jinsi ninavyokwenda inakuja sawa sawa na njozi...ni vitu ambavyo...mola mwenyewe anajua!
'Nikagonga mlango, kulikuwa na kelele za mashine huko ndani....nahisi kwa sababu za hizo kelele hawakunisikia...
'Kwa kimuhe muhe cha kuona...sijui mali, au watoto..nikaona nitumie mbinu zangu kufungua huo mlango
Mlango ukafunguka....!
'Ile naingia mle ndani, ndio nakuta shimo, ni kama wanataka kulifukia hivi...sikuelewa shimo hilo ni la nini!
Docta hayupo...na hata nikirejea kwenye njozi, sokuwahi kuona shimo...!
'Sasa huyo docta hayupo....yupo wapi..?'
Nikawa najiuliza....na mle ndani, yupo mtu anaendesha mashine , ya kufukia au kuchimba hilo shimo! Sikutaka hata kumuuliza..
Mimi nikatoka nje....nainua kichwa kuangalia mlangoni, naiona ile namba...ina tofauti kidogo...hiyo namba imeandikwa mlangoni !
Ehee...hii namba....!
'Ni hapa hapa....sijakosea...sasa nifanyaje, docta hayupo, humo ndani nimekuta shimo, shimo la nini, sielewi kitu hapo
'Kichwa hapo kinanizunguka...ni kama kuna jambo karibu, lkn jambo gani...sielewi...
'Nikaingia tena ndani...na wakati nataka kuingia chumba kile chenye shimo.., ndio nikasikia sauti ya mtu anaongea kwenye simu..sehemu ya pili ya kile chumba..
'Ukiingia humo ndani kuna vyumba viwili, kimoja ndio cha docta mkuu kingine ni cha uchunguzi..
Nikasikia sauti inatokea chumba hicho cha uchunguzi..
'Ile mali ninayo, niliichimba jana,...natafuta namna yakulifukia hilo shimo kinamna...' sauti ya mtu anaongea na simu.
'Ndio kama nilivyokuwa nikikisia, ni kweli, ile mali ilifukiwa kwenye ofisi ya docta mkuu,....ndio ipo vilevile ndani ya jeneza.... ndio nimeshaitoa, ..
'Nini...unasema..nani, kaachiwa...ooh!
'Kwanini walimuachia, niliwaambia nitaipata tu, huyo alitakiwa afie huko huko jela....ooh..sasa...ooh, sasa...
'OK niachieni mimi huyo mtu, akija nitajua cha kumfanya..ndio ndio.... lile lile bomu litamuangamiza...'
Hiyo ni sauti ya docta msaidizi..sikuwa na uhakika...unajua jela...mambo mengi..sio rahisi kukumbuka sauti za watu
'Niliposikia hivyo, nikataka sasa nigeuke kuondoka hapo...lkn hata nikiondoka mali hiyo iliyopo kwenye jeneza ipo wapi...
'Nikageuka tena, nia nikaongee na huyo mtu, nahisi ni docta...yaani hapo miguu kama imekufa genzi hivi...kuondoka au kuongea na huyo docta!
'Mara mlango ukafunguliwa nakutana uso kwa uso na msaidizi wa docta mkuu...!
Aliponiona macho yakamtoka kama kushangaa....au kushtuka hivi...!
Hata kabla sijasema neno...akafungua mlango na kuanza kutoa sauti kuwaita walinzi..
'Mkamate huyo mfungwa katoroka toka gerezani...'akasema docta msaidizi, akiwaita walinzi wa hapo!
'Ukumbuke bado nilikuwa na sare za gerezani, kwahiyo kauli yake ilionekana ni kweli..
'Hata nilipojaribu kujielezea hawakutaka kunisikiliza, nikafungwa kamba...
'Sasa..baadae huyu docta msaidizi akanijia pale nilipolala nimefungwa miguu na mikono, akaniambia...
'Umejua siri sio...ajuaye siri zetu, kama sio mwenzetu ni maiti...najua kabisa umesikia nikiongea na simu umesikia nini, na umefuata nini hapa...?'
'Mimi sijui kitu...sijasikia kitu' nikasema sasa nikiwa na wasiwasi!
'Hahaha, kama hujui ulifuata nini hapa, ndugu yako docta alijifanya mjanja kuficha mali hapa...'
'Hiyo mali ni ya familia yangu..mumeichimbua mnataka kuiiba...'nikasema, sikujua kama alinitega kujua nafahamu kiasi gani!
'Hahaha, kumbe wajua eeh...na umejua nini ninachokiongelea...sasa sikiliza...watoto wako ni maiti..
Watoto wangu ni maiti...!!!
Kauli hii ilinishtua kidogo, mimi njozi zangu huwa hazidanganyi.
Nikakumbuka kwenye njozi, niliambiwa watoto wangu wapo mikono salama...
'Watoto wangu waacheni, kama ni kuniua niueni mimi...'nikasema
'Nyie familia nzima wote hamtakiwi kuishi.......wewe ndio pekee uliobakia hai.., sasa na wewe ndio mwisho wako leo....' akasema
Hapo nikajiwa na moyo wa ujasiri nikasema...
'Kama mola kapanga iwe hivyo, sina budi..lkn kufa kwangu ni kwa uwezo wake mola, sio kwa uwezo wako wewe..'
Kiukweli nilisema hivyo nikiwa sasa nina imani moyoni...nikijua kumbe hata huyu mtu hajui lolote kuhusu watoto!
'Hahaha...ngoja tuone, kama utapona kwa miujiza yako...wewe si mtu wa miujiza sio...! Utafia humo shimoni na hakuna atakayejua kinachoendelea . 'Akasema
'Aliagiza watu wake maalumu, wanifunge vyema, wakaniingiza kwenye kile chumba chenye shimo, kukafungwa bomu...!
Mungu wangu, nitakufa kwa bomu...!!!
'Hapa tunaliegesha hili bomu, hilo bomu, mtu akifungua mlango linalipuka na jengo sehemu yote hii inabomoka na wewe utafukiwa humo humo....'akasema huyo msaidizi wa docta mkuu
'Hatutaki kusikia habari ya kizazi chako tena, mali, maeneo utayapatia huko kuzimuni...' akasema
'Walivyopanga wao, alitakiwa mtu aje awe ndio chanzo cha kulipuka hilo bomu, na yeye atakuwa maiti na mlipuko....na huenda ikadhaniwa yeye ndio kalipua hilo jengo!
'Hii sasa ni hisia yangu ya baadae..., kuwa walivyokuwa wamepanga ni kuwa wamuite mtu wa jamii..kwasababu yeye anajua mengi..akija hapo alipuliwe pamoja na mimi.
'Na huyo mtu atakayetumwa asijue nini kinachoendelea....hizo ni hisia zangu ..sijui...., mtu wa jamii anaweza kuwafafanulia zaidi mkitaka!
'Akilini nikawa najiuliza hiyo mali ipo wapi sasa...wanasema ipo kwenye jeneza..na hapa lile fumbo la mali na jeneza limefumbuliwa..
Lakini hadi hapo sijui hilo jeneza lenye mali lipo wapi....
'Walipomaliza kunifunga wakatoka..na haikupita muda mrefu, mara mtu akaingi, nilivyolazwa naona kwa juu
'Ajabu, bomu halikulipuka...na mtu huyo kajifunika uso, siwezi kujua ni nani...sijui yeye alifanya nini hadi bomu lisilipuke..
'Awali nilisikia mlio fulani,...tii-tii..tii..' Kama ile milio ya hatari kuashiria kuna bomu..na kuna kitu kama saa inatembea...
'Sasa huyu mtu alipofika mlio huo ulinyamaza na ile saa ikawa haitembei....nahisi alifanya kitu kuunyamazisha huo mlio...!
'Ina maana gani hiyo , kwanini kafanya hivyo, nikawa najiuliza mwenyewe nikihesabu siku za kuishi..!
'Wakati mwingine kwa kujipa moyo, nilihisi hilo bomu limezimwa..ni hisia tu za kujipa moyo!
'Sasa, kwanini huyo mtu afanye hivyo, na aliwezaje kuingia bila hilo bomu kulipuka..sijui...labda wameghairi, waniache nife tu na njaa.. labda....!!!
Nilizidi kumuomba mungu!
'Kingine cha ajabu mtu huyo baada ya kumaliza shughuli zake, wala hakuangalia ndani kuna nini..alitoka kwa haraka..!
'Nikabakia mwenyewe mle ndani...tokea asubuhi nilikuwa sijala kitu, sasa njaa na kiu vinanitesa...!
'Sikuweza kupiga kelele, kwa maana nimezibwa mdomo ...kwa jinsi walivyonifunga mikono kwa nyuma, na miguu..haikuwa rahisi kufanya ujanja wowote!
'Nakumbuka nikiwa jela, kuna namna ilikuwa inanitokea , hata kama wamefunga, niliweza kujifungua, lkn hapo hiyo hali haikuweza kutokea...
'Nikajua ni kadara za mola, huenda ilipangwa iwe hivyo, nife, labda kwa dhambi zangu, nilikiri makosa yangu, nilivyokosea kushirikiana na mama mdogo kuifisidi familia yangu
Moyoni ..nilitubu kila dhambi niliyoikumbuka...
'Baadae nikamuomba mola wangu, japo aniache hai niweze kuirejesha hiyo mali kwa familia yangu kama ipo hai...
Kiukweli..haikutokea akilini wazo baya kuwa familia yangu haipo hai...nilijua ipo hai na ipo salama...
'Kama ni hivyo.... ni lazima haki yao waipate...kwa vipi sasa, na mimi nasubiria kulipuliwa na bomu
Nikazidi kumuomba mola wangu!
Baadae nilikuja kusikia kwa mbali kama milio ya bunduki nikajua watu wanagombea hizo mali
------
Na baadae ndio akaja mtu wa jamii, na wataalamu wa mabomu, wakanisaidia na kunitoa mle ndani!
'Hili bomu limeteguliwa na nani...uliona mtu aliyefanya hivyo...?'akaniuliza mtu aliyekuja na mtu wa jamii
Niliwaeleza ilivyotokea...
'Nahisi huyo huyo aliyelitega, hakuliwekeza sawasawa, akijua baadae atakuja kulitegua, sasa ni nani ....'
'Kwanini afanye hivyo...?' Wakaulizana wenyewe kwa wenyewe.
'Sio watu wote wana roho katili kupitiliza, huwezi jua..huenda pia ni mtu wa usalama, au kuna kusalitiana...muhimu hili limeisha salama...'akasema huyo mtaalamu.
'Ni kweli, mola alisikia duwa zangu, na familia yangu ipo salama,...!
'Jamani nduguzanguni... kimekuwa kipindi cha furaha lkn nikiwaza yaliyopita wakati mwingine nahisi machozi...' akainamisha kichwa chini.
Halafu akageuka kumuangalia mtu wa jamii na kusema...
'Ninakushukuru sana mtu wa jamii, umetimiza kazi yako, .....hata nikulipe nini, haitatosha...'
Halafu akawageukia watu waliohudhuria na kusema...
'Ninawashukuruni wote kwa ujumla..tuna mipango ya kufanya jambo la kijamii liweze kusaidia watu..ndio ahsante yetu kwa wote.. zaidi mola ndiye mlipaji..'
Baba wa watoto watatu alipofika hapo akatulia ...baadae akasema
'Kwahiyo mumepata jibu la nini kilikuwepo kwenye lile jeneza,... sasa ni nani alilificha hilo jeneza humo kwenye ofisi ya docta na kwanini...' akatulia kidogo.
'Natumai..hiyo sio nafasi yangu kulisemea hilo.....ahsanteni sana..'
Baba wa watoto watatu alipofika hapo akageuka kumuangalia mtu wa jamii..
Mtu wa jamii akawasogelea wale watoto watatu..., akawashika kichwani mmoja mmoja... na kusema..
'Tumshukuru mola...na kweli, watoto waliwahi kuniambia Mungu akipenda watakuwa pamoja na mama yao na baba yao....' akawaangalia hao watoto.
'Watoto si mungu amependa...?'
Wale watoto wakatikisa kichwa kukubali, na kwa pamoja wakamkumbatia mtu wa jamii..
Baadae mtu wa jamii akiwaangalia watu waliohudhuria hapo, akasema...
'Mimi nitoe shukurani zangu kwenu wote, natumai kazi tuliyopewa, na hasa niliyopewa mimi tumeimaliza...mengine hayatuhusu.., au sio jamani...' akauliza na watu wakashangilia.
'Ahsanteni na kwaherini...'
MWISHO..
NITOE SHUKURANI KWENU WOTE MLIOSHIRIKI NAMI KUKIKAMILISHA KISA HIKI...HASA WASOMAJI WANGU WA KILA SIKU.NA HASA WALE WALIOTOA COMMENTS
TUKIJALIWA KUKITENGENEZEA KITABU, KUTAKUWA NA MABORESHO MENGI, ZAIDI YA HAPO..NIA KWASASA NI KUTUNGA VISA VYA AINA YAKE, VISA AMBAVYO NI RAHISI KUIGIZA .
WAZO LA LEO : Ukiwa na imani ya dhati kwa mola wako, hutatetereka, kwani unajua, yeye ni muweza wa yote tatizo likitokea mola wako atakuokoa kwa rehema zake.

 

Ni mimi: emu-three

No comments :