‘Siamini niliyoyasikia huko mahakamani…moyo wangu
unaniuma sana…’akasema
‘Kwanini kwani kumetokea nini…?’ nikamuuliza
‘Ni kwanini wanadamu wanakuwa na roho mbaya kiasi
hicho…’akasema mama mjane, na bado nilikuwa sijamuelewa. Nikasubiria maana hapo
alikuwa analia.
Nilisubiria
mpaka alipotulia, …na kabla hajaanza kuongea zaidi, ndio akaingia mpelelezi.
…akatuangalia,alimuona mama mjane akifuta machozi, hakuuliza kwanini mama huyo
analia, yeye akasema;
‘Tatizo ni kuwa…sis hatuna ushahid wa maandishi, na
benki wanayo ushahid wa maandishi, japokuw tumejaribu kuleta hoja kuwa
maandishi hayo pia yanaweza kuwa yamegishiwa, sasa kwa vipi, kwa vipi ina maana
tulete maandishi yaliyo sahihi, yapo wapi…’akasema
‘Mhh…lakini..’nikataka kusema akanikatisha kwa kusema.
‘Hata hivyo, hadi hapo tulipofikia, tuna uhakika,
haki itatendeka, hakimu keshaingiwa na shaka, kuwa hukumu ya awali haikumtendea
haki mdaiwa…mama mjane usikate tamaa, bado kesi inaendelea…’akasema akimuangalia
mama mjane.
Mama mjane akabakia kimia tu, hakuonyesha dalili ya
kukubali au kufurahia kauli hiyo,.
‘Kwani Ilikuwaje…maana mimi mnaniweka roho juu, …?’
nikauliza
‘Muda ulikwisha, …pale alipofika huyu mtu
wako…’akasema
‘Mtu wangu gani huyo…?’ nikauliza
‘Chizi…’akasema na kutabasamu, kama vile anaongea
kitu cha mdhaha.
‘Oh…sasa mbona mtamfanya arejee kwenye uchizi wake,
…kwa jinsi alivyoniambia alipotoka hapa, haitakiwi kucheleweshwa, oh, sasa
ikawaje…’nikasema na kuuliza.
‘Ndio hivyo, sheria za mahakama zina muda wake..hata
hivyo, wakili wa benki, alishaanza
kuweka pingamizi kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili, kwahiyo , yeye hawezi
kutoa ushahdi mbele ya mahakamani…’akasema.
‘Kwahiyo…ikawaje, maana naona hamnifanyi niwe na
amani…’nikasema hivyo
‘Docta alihitajika, kuthibitisha kuwa kweli, huyo mtu
kapona,na anaweza kuongea ukweli, mbele
ya mahakama…’akasema;
Oh….docta yupi huyo aliyekuwa naye hapa,…mimi
simuamini sijui kwanini…’nikasema
‘Hata mimi, lakini ndiye anayeweza kulithibitisha
hilo…’akasema
‘Ok, kuacha hilo, hakukuwa na ushahid mwingine wa kusaidia, kabla ya huyo jamaa…wengine
hawajasaidia kitu..?’ nikauliza.
‘Wengine waliongea sawa, ikaonekana kweli benki
kulikuwa na hujuma, lakini hujuma hizo utaziwekaje kwenye sheria…wakati benki
wana ushahid wao wa kimaandishi, ushahidi wa kisheria…’akasema.
‘Ni ushahidi wa kisheria kimaandishi, lakini ushahidi
huo, si ulitengenezwa, ..ukapitia sheria, lakini kwa hujuma,..hamkuweza
kulithibitisha hilo…?’ nikauliza.
‘Yote hayo yalifanyika, ndio maana hakimu akavutika
kuendelea na kesi hiyo, na lile pingamizi la kuendesha mnada huenda
likakubaliwa, …japokuwa alisita kutoa kibali hicho,…akasema inabidi kesi hii ya
kukubali au kutokukubaliana na pingamizi hilo iahirishwe…’akasema.
‘Safi kabisa…kwahiyo bado kesi hii ya pingamizi
inaendelea, kwetu sisi kuchelewa hivyo itatusaidia zaidi, japokuwa shahidi wetu
muhimu, huyo wanayemuita chizi, anataka kutoa ushahid wake haraka, swali je ana
nini …maana hataki kuliongea hili nje ya mahakama…’nikasema.
‘Mimi naona kuwe na namna nyingine ya kutafuta huo
ushahidi wa maandishi, bila huo bado kuna walakini…’akasema mpelelezi
‘Je mimi naweza kuongea na huyo Chizi…?’ nikauliza.
‘Utaongea naye nini, kasema kutokana na kiapo chake
ushahid wake wote atautolea mahakamani…kwani anaogopa akiongea nje ya mahakama,
ushahid wake utaharibiwa, na inaweza ikawa ni hatari kwake…’akasema Mpelelezi.
‘Sasa yupo wapi huyo mtu…?’ nikauliza.
‘Yupo kituoni, hospitalini anapotibiwa, na ulinzi mkali umewekwa, najua unataka
kulisema hilo…’akasema.
‘Ni muhimu, huyu mtu anatafutwa na sehemu mbili kwa
sasa, tusiwadharau benki, maana wao pia wanataka kushinda, na wakiona kuwa huyu
mtu anaweza kufanya wakakosa…kumpata mdaiwa, wanaweza kufanya kila mbinu huyu
shahidi ashindwe kufika mahakamani…’nikasema.
‘Hawawezi, hilo tumeshalifikiria mapema…hata hivyo nasikia
wakili huyo na benki hawaelewani…kuna mambo hawakubaliani…’akasema.
‘Kwanini…?’ nikauliza.
‘Ilianzia kwenye malipo, sasa imefikia kwenye sura
nyingine…benki wanasema huyo mtu, ana kazi nyingi za watu, kwahiyo hayupo
makini na kesi hiyo…’akasema mpelelezi.
‘Hilo kwetu ni nanafuu pia…’nikasema na nikajikuta
nimeuliza swali jingine …
‘Vipi Dalali naye anaendeleaje..?’ nikauliza.
‘Bado…haeleweki…’akasema.
‘Una uhakika kuwa huyo mtu hawezi kutembea..?’
nikauliza na mpelelezi akaniangalia kwa uso wa kushangaa, akasema
‘Kwanini unauliza hivyo, wewe mwenyewe si ulimuona
yupo kitandani kama mzigo, mwili ule umepooza, na docta anasema itachukua muda,
hadi aweze kusimama tena…’akasema mpelelezi.
‘Hahaha…’nikacheka hivyo, na mpelelezi akasema
‘Docta kalithibitisha hilo…’akasema akiniangalia kwa
uso wa kujiuliza.
‘Sio kweli..huyo mtu ni muongo, anaweza kutembea
kabisa, sema labda kwa shida, lakini anaweza kutembea, huyo mtu, aliweza
kutembea usiku mmoja hadi huko wanapokutana na huyo mtu wake aliyemfuata, sijui
ni nani…’ nikasema.
‘Unasema ukweli au uliota ukiwa kwenye marue rue ya
upasuaji..hilo haliwezekani kabisa, …wewe si ulimuona pale hospialini..?’
akauliza mpelelezi.
‘Ukitaka kulihakiki hilo, kamuulize yule mdada wa
mapokezi, au ..yule mlinzi, mimi nilijua kakuambia kila kitu..’nikasema.
‘Hawajaniambia kuhusu hilo, na wala sikuwa na wazo la
kuwauliza hilo , maana mtu mwenyewe nimemuona kwa macho yangu…’akasema
akiangalia saa yake.
********************
Siku nyingine kesi ikaendelea,…na leo akaitwa shahidi
aliyesababisha mabishano ya mawakili hawa wawili…
‘Huyu mtu ana matatizo ya akili ushahidi wake hauwezi
kukubalika..’akasema shahidi wa benki.
Hakimu akaingilia kati na kuuliza,
‘Je ni kweli kuwa huyo mtu ana matatizi ya akili…?’
akaulizwa
‘Ni kweli huyo mtu alikuwa na matatizo ya akili, alikuwa
kweli kachanganyikiwa awali, na kuchanganyikiwa kwake ni kutokana na dhuluma,
na moja ya dhuluma ni hii ya kesi hii tunayoizungumzia,…’akasema wakili .
‘Hakuna dhuluma kwenye hili deni, hio ni kauli yako,
na mawazo yako, je ushahidi wetu hautoshi kulisadikisha hilo, …kama ulitosha na
mahakama ikakubaliana na ushahidi wetu iweje leo uuite ni dhuluma…’akasema
wakiliw a benki
‘Ushahidi wenu umegibikwa na sintofahamu nyingi,
ambazo, mashahidi wetu wameendeela kuutoa, na huyu shahid anataka
kulithibitisha hilo, na nafahamu mnaogopa, kwa vile mnaufahamu ukweli wake …’akasema
wakili mtetezi.
Mjadala wa mawakili hawa ukaendelea, kila mtu
akivutia kwake, na ikabidi hakimu aingilie kati tena;
‘Ili kuondoa huu mjadala , nataka docta wa magonjwa
ya akili aje alithibitishe hilo kuwa kweli huyu mtu anaweza kutoa ushahidi , je
kapona,….’akasema hakimi, na hapo ikabidi docta aitwe , kinyume na walivyotarajia kuwa labda
ataitwa docta wake wa awali, sasa hivi aliitwa docta mwingine bingwa wa magonjwa hayo
ya akili
‘Akaulizwa kama aliwahi kumtibia huyo mgonjwa na
anamfahamu matatizi yake, docta akasema
'Nimewahi kumtibia huyo mtu…, niligundua jambo moja,
huyu.mtu sio mgonjwa wa akili ya kawaida kama walivyo wagonjwa wengine,..,
ugonjwa wake ni kama unapuliziwa, ni kama mtu anayetumia madawa ya kulevya,
lakini hajawahi kutumia hayo madawa..’akasema docta
‘Kwanini unamuita mgonjwa wa akili asiye kuwa mgonjwa
wa kawaida…?’ akaulizwa
Mgonjwa huyu
anakuwa na muda wake wa kuumwa, ..na ukipita hajambo kabisa na mnaweza kuongea
kila kitu…na kama unavyomuona mgonjwa huyu ni msafi sana, huwezi kumdhania kuwa
ni mgonjwa…’akaendelea kuongea.
‘Na zaidi mgonjwa huyu ana akili zaidi ya akili za
kawaida, anaweza akafahamu unajikiwaza, ana vipaji vingi sana vya kitaalamu,
kimadawa,..hutaamini hata dawa zake anazifahamu, akianza kuumwa, atakuambia
nipeni dawa hii, na kweli hiyo dawa inamsaidia…’akasema
‘Ila anaonekana ana msomgo wa mawazo, kuna kitu
kinamtatizo, ..na huwa na muda wake wa kukifikiria hicho, kitu akikiwaza,
analia sana, na hapo hasira humpanda, na kuanza kujipiga au kuwapiga waliopo
mbele yake…’akaulia docta
‘Sasa, mwezi huu hali yake ilizidi sana.., na kila
mara amekuwa akinisihi kuwa, tatizo lake litakwisha yeye akitubu dhambi zake.na
kutubu dhambi zake ..inahitajia safari ndefu, kwanza aanza kujitenga na watu,
..ndio maana alikuwa akipotea, na kuishi sehemu ambayo watu hawafiki fiki…’akasema
‘Sasa wiki hii ndio kasema muda umefika wa yeye
kutubua mbele ya jamii, na hasa mbele ya mahakama,…kwahiyo hili la kuto
ashahidi ni sehemu ya toba yake, na amesema wazi, isipofanikiwa hivyo, ndio
itakuwa mwisho wa maisha yake,…’akasema docta
Hakimi akamuangalia huyo shahidi, na baadae
akamuangalia wakili wa benki, ambaye naye alikuwa akimuangalia huyo mgonjwa,…baada
akauliza
‘Wewe ni docta, au sio…?’ akauliza
‘Ndio mimi ni docta…’akasema docta
‘Huyo mgonjwa ana matatizo gani…?’ akauliza wakili wa
benk
‘Ana matatizo ya akili…’akasema docta
‘Kwenye vifung vya sheria mgonjwa kama huyo
anastahiki kutoa ushahidi, ….?’ Akauliza wakili.
‘Kama nilivyosema awali..’kabla hajamaliza wakili
akauliza tena
‘Je mgonjwa huyo ana matatizo ya akili au la…’?’
akauliza wakili
'Mimi kama docta wake, naona njia pekee ya kumsaidia huyo
mgonjwa ndio hiyo kwani kia alichokiomba afanyiwe tukamkubalia chenye manufaa
kimekuwa kikimsaidia kimatibabu…’akasema huyo docta na hapo hakimu akaingilia
kati, na kusema;
'Sio jambo la kawaida, na kesi hii imegubikwa na
mambo mengi yasiyo ya kawaida, lakini imebidi tuyakubali ili tuone ukweli
halisi wa kesi hii,..mimi ninamkubalia mtu huyo atoe ushahid wake, kutokana na
kauli ya docta wake…’akasema hakimu.
Yule shahidi akasogea mbele, sehemu ya kutolea
ushahidi, kiukweli huwezi amini kuwa jamaa huyo ana matatizo ya akili,…akatulia
akisubiria utaratibu wa kimahakama.
Alipomaliza zile taratibu zote akaulizwa jina;
‘Jina lako ni nani…?’ akaulizwa na hapo akabakia
kimia, akaulizwa swali hilo mara ya pili, na hapo akageuka kwa hakimu, akasema;
‘Unajua ni kwanini nimeshindwa kulijibu hilo swali,
ni kwasababu mbele yangu nawaona watu ambao nyie hamuwaoni, walikuwa
wakiniuliza maswali mengi kwa wakati mmoja,..’akasema na hakim akageuka
kumuangalia docta, ni kama vile anataka kusema
‘Mbona umetuletea mgonjwa hapa, …’ na kabla hakimu
hajasema kitu shahidi huyo akasema;
‘Hii kesi ni yangu, kote huko mumezunguka tu, na
kweli ilitakiwa iwe hivyo, …na kama kweli isingelikuwa hao mzimu,…hahaha,
msingelimpata mtu…’akasema.
‘Unaniuliza jina langu ni nani…nitakuambia, ila kabla
sijajibu hilo swali lako, kwanza nataka niwaambia jambo moja…’akasema.
‘Hivi kweli mtu mwenye akili zake timamu anaweza
kumdhulumu yatima…mjane,..au marehemu..?’ akauliza sasa akimuangalia hakimu,
hakimu akabakia kimia.
‘Ikimia wenu unasema neno moja, …’hakuna..’
‘Ni kwanini sasa hayo yanatokea,…?’ akauliza
‘Ukimia wenu unaeleza neno moja,..’hatujui..’
‘Basi mimi niwaambie neno moja…mimi nina akili sana,
mimi sio kichaa, wenye kichaa, ni hao wasio na akili, ambao, wanayafanya hayo
kwa siri wanawadhulumu mayatima wanapuuza wajane…na wengine ni matajiri tu…’akatulia.
‘Mimi nimeliona hilo, ndio maana leo nimeamua kutubia
dhambi zangu, ..leo wakili wa benki ananiita mimi ni ‘kichaa’ wakakati yeye
amewahi kusaidia watu kushinda kesi ya kuwadhulumu mayatima,…anabisha,..?’
akauliza na watu kimia.
‘Habishi maana ndio kazi yake, je mimi na yeye ni
nani kichaa..?’ akauliza watu kimia.
‘Basi mimi nataka nisema ukweli , na ukweli huo
utambulikane kuwa unatoka kwa mtu ambaye ana akili sana, sio kichaa, maana
vichaa wapo na hamuwatambui kuwa ni vichaa…’akamuangalia wakili wa benki.
‘Je muheshimiwa unanifahamu mimi…?’ akauliza.
‘Sikufahmu ndio maana tumehitajia jina lako…’akasema
wakili.
‘Wewe ni muongo…na muongo sana,..mimi na wewe
tumesoma shule moja,..wewe ukachukua masomo ya sheria na mimi nikasomea masomo
ambayo yamenifikisha hapa nilipo…mimi na wewe tumekuwa marafiki, …hata tukiwa
kazini, lakini leo unasema hulijui jina langu…’akasema na watu wakaguna.
‘Je mimi na yeye ni nani kichaa…?’ akauliza, na watu
kimia.
‘Mimi naitwa… M.AL.M…’akasema na hakimu akasikiliza
kwa makini..na hata aliporeja jina hilo bado haikueleweka…
‘Hebu taja jina lako kwa harufu moja moja…na
alipotaja ndio ikagundulikana kuwa ni kifupi cha majina..
‘Majina yako kwa kirefu ni nini..?’ akaulizwa.
‘Maozo..aliyetupwa, majalalani aka, MOTO…’ Akasema na
watu wakacheka
‘Mnacheka,…hii inaonyesha kuwa nyie ni vichaa zaidi
yangu mimi, jiulizeni lini mlilipata kusikia jina kama hilo, mliwahi kulisikia
hilo jina wapi…?’ akauliza
‘Hakuna hatujawahi…’akajibu mtu mmoja.
‘Na wewe wakili wa benki…?’ akamuuliza.
‘Nililisikia kipindi nipo shuleni, lakini mara nyingi
hukuwahi kulitaja kwa kirefu hivyo,…’akasema.
‘Kwanini nilifanya hivyo..?’ akauliza
‘Mimi sijui…’akasema
Hapo akatulia, akawa kama anawaza jambo, …halafu
akasema
‘Leo sitalia..leo sitabadilika na kuwa kichaa…leo
nitaongea, na leo mtanifahamu kuwa mimi ninani, na kwanini niliitwa maozo..ni
kweli nilikuwa uozo mbele ya jamii, mbele ya baba yangu aliyenizaa…’hapo
akatulia,
Alikaa hivyo kwa muda, hata hakimu ataka kuongea,
ndio jamaa akasema
‘Hilo jina alinipatia mama yangu na ndiye
aliyeliandikisha …na alitaka sio kwamba alitaka liwe hivyo,..na muda huo mama
yangu alikuwa hawezi kuongea vizuri, hawezi kutamka hayo maneno vizuri..jina
langu lilikuwa Mansa Majaliwa Moto…’aliposema hivyo, watu wakaangaliana.
‘Docta au aliyeandika kadi hiyo akaandika, MAOZO,AL,
MOTO…kwa jinsi mama alivyoshindwa kutamka, ulimi wake ulikuwa kama umemezeka,
kutokana na mtindio wa ubongo aliupata,..ndio jina langu likawekwa hivyo kwenye
karatasi…hadi nipo shuleni na mimi nikalipenda liwe hivyo…’akatulia.
‘Sasa naanza kuelezea..nyie si mnataka ushahidi, wa
hii kesi, au sio ..kuwa je ni kweli hilo deni ni la marehemu au la…, je kweli
hilo deni ni sahihi kwake…?’ akauliza na aliyejibu ni hakimu, akasema.
‘Ndio, tunahitajia hilo jibu…’akasema.
‘Kwa jibu
rahisi na la haraka ni ‘KWELI’’..’akasema
‘Unasema ni nini…?’ akaulizwa wakili wa benki
‘Kwa jibu la haraka ni kweli…’akasema
Aliposema hivyo wakili wa benk, akamsogelea na kutaka
kumpa mkono wa shukurani, lakini shahidi huyo hakuupokea huko mkono, …na Wakili
wa utetezi, akawa kimia, kama vile hana wasiwasi, na mtu huyu
Huyo shahidi akasema;
‘Nimesema naongea ukweli mtupu, na haya
nitakayoyaongea ndio ukweli, na hilo deni linatokana na ukweli wa maisha yangu…mnielewe
hapo, hilo deni ni stahiki ya marehemu kwa sababu…nitakayokuja kuielezea…’akatulia
na kikasikika kilio kwa watu waliofika
‘Ninajua anayelia ni nani..ila anivumilie tu, ukweli
unauma, na ukweli utasaidia kizazo chako dada yangu,na baada ya kilio, huja
nini, huwezi kulia milele au sio mwisho wake atacheka tu,…’akasema.
‘Kwanini unasema hilo deni ni la marehmu…’akauliza
wakili mtetezi wa madeni
Huyu shahidi akamuangalia kwa makini huyo wakili kama
anamsoma mawazo yake, halafu akasema.
‘Una shaka na mimi..?’ akauliza.
‘Nijibu swali langu…’akasema.
‘ Nitakujibu,…lakini jibu lake siwezi kulielezea kwa
jinsi mnavyotaka nyie, jibu la swali lenu litakuja kutokana na kisa cha maisha
yangu…naomba muheshimiwa hakimu unipatie wasaa nilielezee hilo jibu, lakini
kutokana na kisa cha maisha yangu,….ili haki ije kutendeka…’akasema.
Hakimu akaangalia saa,…
NB: Na mimi nikaangalia saa, bosi anakuja.
WAZO
LA LEO:Ukweli wa maisha ni upi..ni jibu la haraka au ni
jibu la maelezo marefu. Maisha ya mtu sio jibu la haraka, NDIO AU HAPANA, maana
MAISHA yalivyo yana mlolongo wake mrefu, hata kama ni mtoto kazaliwa leo na
kufariki leo. Maisha yalivyo, yanatokana na michakato mingi, na zaidi ya hayo
anayefahamu zaidi ya hayo ni yule aliyetuumba. Katika maisha tusikate tamaa
maana mengi ya yanayotokea ni kwa mpenzi yake yule aliyetuumba.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
I'm truly enjoying the design and layout of your website.
It's a very easy on the eyes which makes it much more pleasant
for me to come here and visit more often. Did you hire out a
developer to create your theme? Superb work!
Post a Comment