‘Huyo
mtu hana kitu tana..., nimeshauchukua mkoba wake ndio maana anatapatapa, haniwezi tena…..’
Wale
akina mama wakaangaliana na kunyosha mikono juu ya ushindi,
‘Sasa
mzee, muda tuliopewa wa kukaa humu kwenye ofisi ya watu umekwisha, na tumeongea
mengi, na mpaka hapa tulipofikia, umeshakiri kuwa wewe pamoja ya kuwa ni mganga wa
kienyeji, lakini pia wewe ni mchawi, hilo halina mjadala…na huo mkoba wa uchawi mkuu unao wewe, kama ulivyosema hapa sasa hivi....’akaambiwa na yeye
akabakia kimia tu.
Tuendelee na kisa chetu.
***************
‘Unajua
wanadamu tunajisahau, na tunapofanya majambo tukafanikiwa tunajiona sisi ni
washindi, tunasahau kuwa dunia hii ni ya kupita tu, wangapi walikuwa majbali,
wachawi, wengine matajiri, watawala wenye nguvu..lakini sasa wapo
wapi..nikujisahau tu…’akasema huyo mama.
‘Sasa
ndugu yangu kwa ushauri, kama ulivyosema awali, wewe una shida na sisi pia tuna
shida,..lakini shida zetu chanzo chako ni wewe…usilikatae hili kupoteza muda,
kama utazidi kubisha sisi tutaingia kwenye sehemu nyingine ambayo haitakuwa
nzuri kwako, hilo tuna uhakika nalo, sio kwamba sisi tumekuja hapa hivi hivi
tu, sio kwamba tunafanya haya tukikisia tu, hapana….’akasema na jamaaa
akaendelea kukaa kimia.
‘Kuingia
kwenye majumba ya watu kwa namna yoyote ile bila idihini ya wenyewe ni
makosa,utasema ni nani aliniona kwasbabu umefanya kwa njia ya uchawi, usiku
watu wamelala, huonekani,…na nikuambie kitu,.uchawi japokuwa kwenye sheria
hakuna namna ya kuithibitisha, lakini matendo yake yanaweza kuthibitishwa, kama
yataonekana jinsi gani yanavyoathiri jamii, unawafanya wengine wasiishi kwa
amani, kuna mauaji, kuna madhara ya kuumiza wengine wakawa wanaumwa, ..sasa
hayo yakifika mbele ya sheria ni makosa makubwa.
‘Umesikia
hata kwenye vyombo vya habari, kuna watu wanajiita ni waganga, lakini kazi yao
kubwa ni kuwapotosha watu, wanafanya mambo ya kichwai, ushirikina mtupu...wao
wanasema kuwa wanaweza kuleta utajiri, lakini waangalie hali zao, kama wanaweza
kufanya hivyo kwanini wao wasiwe matajiri, kwanini ili waifanye hiyo kazi mpaka
walipwe, yeye atakuwa na shida gani kama aweza kutengeneza huo utajiri.
Watu
hao wamefikia hatua mbaya, ya ku-ua, wanaua, wanadamu wenzao, kwa imani hizi za
kishirikina, iweje miili ya watu itumike kuleta utajiri, kama miili yao
inegkuwa ni sababu ya utajiri mbona hao watu wanaouliwa sio matajiri, ni mtu
kufikiri tu, ngozi kuwa tofauto ni madhara ya kimaumbile tu, angeliweza kuwa
mweusi, au mweupe, lakini ni viasilia vimekosekana tu, …hao wachawi wanatumia
utofauti huu kuwapotosha watu,..
Haya
kuna hao wanaosema wanaweza kuvuta mapenzi, lakini yeye mchunguze kwenye ndoa
yake, hana mapenzi na mke wake, hana maisha mazuri na familia yake, au hana
familia kabisa, sasa kwanini yeye alishindwa kwanza kujitengeza mwenyewe,…ipo
mifano mingi kadha wa kadha…ukichunguza watu wa aina hii, kazi yao umegubikwa
na utapeli tu, tamaa za kidunia, ya kuwapumbaza wengine wenye uoni hafifu
wakubali na kufanikisha malengo yao…ambayo kifupi ni ushatani tu.
‘Sisi
hatutaki kufika huko, kukufikisha wewe mbele ya sheria, maana awali ulitaka
kujua sisi tutafanya nini kama hutatii masharti yetu hayo….hatua nyingine ni
wewe kufikishwa mahakamani, lakini sisi tupo tayari, kumalizana na wewe kama
utakubaliana na sisi, tumeshaongea na waathirika wa uchawi wako, wamesema kama
utakubaliana na hayo masharti wapo tayari kukaa na wewe meza moja na
kuyamaliza….’akaambiwa.
‘Hahaha,
nyie watu, hao watu mumewajuaje,..na hivi, haya ..sawa, mimi nawasikilia tu…’akasema.
‘Muhimu
kwako wewe kama wewe kumbuka jambo moja tu, kuwa hii dunia ni ya kupita
tu,..hakuna atakayeishi milele, na mwisho wa yote tutarejea kwa mola wetu,
aliyetuumba, na yale yote tuliyokuwa tukifanya huku duniani, yatahukumiwa, na
hakimu wa mahakimu ..mola wetu, …
Sasa kama uliua, ulifanya madhambi mengi kwa
siri, siku hiyo yote yatadhihirishwa, sote tukiona…na nikuambie kitu adhabu
nyingine huanzia hapa duniani.. huwezi kumfanyia mtoto wa mwenzako madhambi,
halafu mungu akuache hivi hivi..hutahukumiwa,kuanzia hapa hapa duniani.
Magonjwa
mengine mabaya ni adhabu, licha ya kuwa mtu yoyote anaweza kuumwa, hata kama
hana madhambi hayo, lakini wengine wanaumwa, kutokana na matakwa ya muumba, iwe
kama adhabu, ili wamkumbuke mola wao , ili waweze kutubu dhambi zao..na watu
hao wakitubu ukweli wa kutubu, na kumuomba mola wao, wanapona, wangapi
tumewaona wakipona,…au hilo wewe hulijui…?’ akaulizwa
‘Mhh..’akaguna
akijitizama mguuni, lakini hakusema neno.
Nimechukua
muda huo kwa maelezo hayo, nia ni kukutanabahisha hili kwa mifano, ili
unielewe, kabla sijafikia huko kwenye masharti yenyewe…’akaambiwa na yeye
akabakia kimia tu.
‘Sasa
je ndugu mpendwa, upo tayari kutubu madhambi yako…?’ akaulizwa, kwanza
akacheka, na kutikisa kichwa,
‘Hahaha,
unajua mimi nimekusikiliza sana, sio kwamba siwezi kupingana na wewe, lakini
kama ulivyosema, muda umetutupa mikono, na lengo letu halijakamlika bado, nia ya
nyie kufika hapa bado hutajaweza kufanikisha lolote, sijui nyie muelekeo
wenu,..lakini, sawa, mimi nipo tayari
kusikiliza hayo masharti yenu, kama nitaweza nitayatimiza, maana kiukweli hata
mimi nina shida,…’akatulia kwanza.
‘Sasa
tunakusikiliza wewe…’akaambiwa
‘Nilikuwa
nafikiria kwanza, maana umenigusa sehemu ambayo nashidwa hata nisemeje, ingelikuwa
nipo mzina sina tatizo, ningekujibu kwa matendo..sikufichi, unajua nilifikia
sehemu nikaapa, kuwa kw haya yaliyonikuta, yoyote yule atakayekuwa nyuma ya
hayo atajibu, kwa mapigo makali…,..lakini nifanyeje sasa…’akasema sasa
akishusha sauti kwa uchungu.
‘Kwahiyo
kumbe ipo sababu kuwa yaw ewe kujiingiza huko kwenye uganga na uchawi…?’
akaulizwa, na hakujibu hilo swali, yeye akaendelea kuongea kuendeleza maelezo
yake ya awali…
‘Kama
ulivyosema yawezekana,….’akauangalia mguu wake, na huku anaongea,
‘Na
sio yawezekana hata mimi nimeambiwa kuwa haya yote ni sababu na makosa yangu,
sawa nimekubali kuwa na mimi nina makosa…, lakini mbona watu hawaangalii undani
wa sababu za makosa hayo,mimi sio mnyama kihivyo, kunasababu,..lakini nani
atakusikiliza kwa hivi sasa….’akatuli kidogo.
‘Sawa
utakuja kutuambia, ili tukimbizane na muda, tuendelee na ajenda yetu…’akaambiwa
‘Sawa
tusipoteze muda, niambieni mnataka nini,.?’ Akauliza akiwaangalia hao akina
mama.
‘Sisi
tunachotaka ni wewe kukubaliana na hayo masharti tutakayokupa, ili tuende sawa,
au vinginevyo, maana sisi, tumeathirika, na uchawi, wako, kama
ulivyotuthibitishia,…tuna haki ya kuchukua hatua nyingine ambayo hutaipenda..?’
akaulizwa
‘Niwaulize
kwanza ni hatua gani hiyo nyingin, maana tusitishane, huruma yangu ndio
iniponze, hapana, tusitishane, kabisa,…kwasababu kwanza, hamfahamu nikwanini
haya yote yemetendeka,…hamjui, lakini nyie mumelichukulia hili swala juu kwa
juu, na hamjui kabisa kuwa mimi nimejitokea kwa ajili yenu, vinginevyo
ningelikaa kimia tu…’akasema akitikisa kichwa
‘Jamani
hamjui tu, …hivi ni vita, na kwenye vita hakuna mcho tena, adui akiwa mbele
yako pambana na kama kuna kikwazi cha kumficha adui kiharibu, jenga ukuta,
jilinde, na uweke sababu za maadui kukuogopa, na kwanini nikae kimia wakati
nafahamu kuwa napigwa vita,..walianza wao, acha na mimi nimalize, mimi sasa najibu
mashambulizi, na sitakoma mpaka wasalimi amri, wasijiche nyuma ya pazia, mimi
nawaona.. sasa ni mimi au wao…hapa sasa naona wameshashindwa sasa wana tapa
tapa, na nyie mnatumika tu…’akasema
‘Mhh…unatufumba,
kama ni vita, kama kuna sababu, hizo utakuja kutuambia, lakini kwanza
tukubaliane kwa haya ili tuweze kumalizana kwa leo, tutakuja rasmi siku
nyingine au tutapanga wapi pa kukutana kwa ajili ya utekelezaji, kwa yale
ambayo hayataweza kutekelezwa haraka, ..’akasema mama
‘Sawa
wewe yataje hayo masharti, mimi nitayasikiliza, na mimi nitayatimiza yanayowezekena
kutimizika, mimi ni binadamu siwezi kuahidi kitu ambacho sijakisikia, je
nikishindwa,…’akasema
‘Kushindwa
huwezi, maana sisi tumeyapitia na kuyaona kuwa yapo ndani ya uwezo wako, ni
utashi wako tu …muhimu ni wewe kukubali, na kutiikia, halafu kutekeleza…’akaambiwa.
‘Lakini
mkumbuke kuwa mimi nipo hospitalini, mimi natakiwa kupata pesa za matibabu,
mimi naumwa, kwahiyo vyovyote iwavyo, mnatakiwa mliangalie na hili pia, na hapa
nilipo nimekwamba kipesa, nyie ndio wakunisaidia ili na mimi niweze kuwasaidia,….’akasema
‘Hayo
yote yapo ndani ya uwezo wako, tatizo ni
akili yako imefungwa na maagano yenu, sio kwamba huwezi kujitibia, uwezo huo
unao, labda ni kwasababu ya imani zenu, na mipaka mliyojiwekewa, huo ndio
ukweli …’akaambiwa
‘Kwa
vipi…hivi mnaniona mimi ni juha au, niwe na uwezo huo nisubiria nini,
kufa…hapana, sina uwezo huo kwa sasa, na sina muda wa kurudi nyumbani na kuanza
kufanya michakato mingine nimeshaambiwa na madocta..sasa labda mniambie
nyie..kwa vipi?’ akauliza.
‘Kwanza
,ni kwanza…upo tayarii sasa kuyasikiliza hayo masharti, na ukishaanza kuyasikiliza,
hatuna tena kurudi nyumba, ukija kukataa, sisi hatutajiuliza mara ya pili,
hatua zingine zitachukuliwa, …na hapo utapambana na mkono wa sheria, hilo
tunaweza na tumeshajipanga ikibidi, maana ushahid tunao, na mashahidi
wapo…’akaambiwa
Hapo
akatulia kidogo, halafu, akamuangalia mdada, halafu mimi, halafu akainama
chini, halafu akasema
‘Sawa
niambieni ni masharti gani hayo, nipo tayari kuyasikiliza…?’ akauliza, na
kusema
****************
‘Ni
masharti gani hayo?...umetuuliza, ikiwa na maana umeshakubaliana na sisi
Haya, sisi
tuna nakala tumezichapisha,..zinaweza kurekebishika hatua kwa hatua, maana tuna
nakala yake kwenye komputa zetu,…wewe unachotakiwa, kila kipengele kwenye ukurasa
wake kuna sehemu yakuweka sahihi yako, nitatoa maelezo kila sharti, moja baada
ya jingine ili uelewe, na uliza pale ambapo hutaelewa,..sawa..?’ akaambiwa
‘Sawa….nyie
wasomi bwana, mpaka muandike, …hahaha, haya bwana, tuendelee..’akasema, na huyu
mama akatoa bahasha kubwa, na kutoa nakala zenye maelezo , na kumkabidhi jamaa
karatasi zenye maelezo, na kutoa nakala
nyingine na kuwakabidhi wengine, na alipohakikisha watu wametulia, akaanza
kusema…
‘Kama
unavyoona, kwanza kabisa tumeanza kuwa wewe umekubali makosa,…sawa ? yakuwa
wewe umekubali kuwa umekosa, hilo ni sharti namba moja, …umekosa kwa vipi,
maelezo hayo hapo chini, kuwa umekubali kuwa wewe ni mganga na pia wewe ni
mchawi, na umekuwa ukiutumia uganga wako, kama sababu, lakini huku unafanya
mambo ya kishirikina, je unakubaliana na hilo…?’ akaulizwa.
‘Hapana..sikubaliani
nalo, siwezi kusaini, kitu kama hiki, kipengere hichi tukiruke, tuendelee na sehemu
nyingine,..’akasema.
‘Mzee
tunapoteza muda hapa, haya ni kwa manufaa yako, kwani baada ya hapa, tutakuwa
sasa tunaanza kazi nyingine ya kuangalia jinsi ya matibabu yako, sasa
tukiendelea kuvuta muda, hatutafika kokote, kukubali kwa kuweka sahihi, ni kitu
kingine lakini kwa kauli yako umeshakubali, na ushahidi tunao,…’akaambiwa.
‘Huo
ushahidi upo wapi…?’ akauliza na mdada akamuashiria mwenzake na kuanza kuwasha
simu yake na jamaa akasikia jinsi alivyokuwa akiongea awali, alivyokuwa
akiulizwa maswali na kuyajibu, halafu kwanza alitulia baadae akasema;
‘Nyie
watu, ina maana yote hayo mlikuwa mnanitega, au sio…hahaha, huo kwangu hauwezi
kuwa ni ushahidi hata mkiupeleka mahakamani, huo hauwezi kukubalika kama
ushahidi mnajipotezea muda wenu bure..’akasema
‘Unajua
ni kwanini tulikuuingiza kwenye hii ofisi, angalia pale juu, kile pale ni kifaa
maalumu kinachochukua matukio yote humu ndani, tuliomba watuhifadhie, wanatumia
kwa kazi zao, lakini kwa tukio hili, tutaweza kupata nakala zake, kwa ajili ya
ushahidi…, sasa kama huu wa simu unauona sio ushahisi na huu wa video je, sas
aunasemaje,…maana sisi hatujafikia huko …tuliona hili jambo halina haja ya
kwenda mbele…ukikubaliana na sisi…..’akaambiwa
‘Nyie
ni wajanja sana, lakini mtakuja kujuta…kwa hili, nyie hamnijui tu, huwa
sijaribiwi….’akasema
'Una
maana gani sasa, kwanini unatoa lugha ya vitisho, huo ni ushahid mwingine wa
tabia yako…?’ akaulizwa na kuambiwa.
‘Sawa
tuendelee…’akasema.
‘Kwahiyo
kama umekubaliana na kipengele hicho weka sahihi yako hapo chini, …’akaambiwa,
na kupewa peni,
‘Sikilizeni
kwanza…mimi siwezi kukubali kuwa mimi ni mchawi, maana hamjui ni kwanini haya
yalifanyika, kwanini tusiendelee na vipengele vingine, halafu tukimaliza
kupitia vyote, ndio hapo, kama ni lazima tutafikia huko kwenye kuweka sahihi
yangu, lakini mkisema mimi nikubali moja kwa moja kuwa mimi ni mchawi, hahaha,
hivi mnaniona mimi ni juha, nisiyeelewa mambo eeh, hamnipati kwa namna
hii…’akasema.
‘Lakini
ulishakubali, au…?’ akaambiwa.
‘Kukubali,
mimi, a wapi…hahaha, nikubali kuwa mimi ni mchawi, nani kasema hivyo….’akasema
‘Ulikubali
kutokana na maelezo yako wakati tunakuhoji,….’akaambiwa
‘Mimi
nilitoa maelezo hayo kwa ujumla wake…, kuwa waganga pia wanaweza kuwa wachawi, lakini
sio kukubali kuwa mimi ni mchawi, sijaweza kufikia huko, msinifanye mimi ni
mjinga…’akasema
‘Lakini
wewe ni mganga wa kienyeji, au sio, na ulikubali kuwa mlikuwa mnafanya uchawi
kwa kupma dawa zenu, mliweza kupambana na maadui zenu, na mliweza pia kufanya
mambo ya kichwi ili kumshinikiza mtu akubaliane na matakwa yenu, hayo ulisema
na kukubali, sasa …usitake turejee huko nyuma…’akaambiwa
‘Hapana
msinifanye mimi ni mjinga, siwezi kusaini, nifanyeni mnalolitaka, hayo
unaongeza wewe, mimi hapa sisaini, umenisikia, siwezi kufanya hivyo kamwe…’akasema
‘Kwahiyo
wewe unatakaje…?’ akaulizwa
‘Mimi
nataka hivi, tuyasome yote haya, na itafikia mahali nitajieleza, lakini kwanza
tuyasome moja baada ya jingine ili mimi niyaelewe, lakini sio kwa kunitega,
kila kipengele niweke sahihi hapana, hapa kuna mtego, na mimi siwezi kutegeka
kirahisi, kihivyo…’akasema
‘Ok,
sawa, sisi tutayasoma na maelezo kidogo, ..lakini tukifikia mwisho, kama
utaendelea kukataa basi tutawaachia wenyewe serikali, wafanye kazi yao, na
hutaamini kitakachofuata baadae, ukumbuke kuna watu wengi wameathirika
kwasababu yako uchawi wako, wameshafika kutoka huko kijijini kwako,kwa ajili ya
kutoa ushahdi, sasa ni wewe kukubali, na kutuachia sisi tuone jinsi gani ya
kukusaidia, ili haya yaishe kwa amani…’akaambiwa.
‘Tuyasome
…mimi sio kama mnavyonifikiria,…kuwa labda, mimi ni mchawi, hapana, haya
yametokea kwasababu tu, mimi napambana na maadui zangu na nimfanya hivyo kwa
madhumuni ya kujilinda, sasa ilitokeaje, mpaka ikawa hivyo… nitakuja kuwaelezea
ikibidi… lakini kwanza nninataka kuyasikia hayo masharti yenu,…’akasema na
kunitupia jocho mimi, halafu akaangalia kile kifaa alichoambiwa kina mumulika yeye
na kuchukua matukio ya humo ndani
‘Sawa
tuendelee, sisi hatuna shida, nia ni kukusaidia wewe…ambaye umeyataka haya…’akaambiwa
‘Hata
mimi nia ni kuwasaidia nyie, nyie hamjui tu…’akasema
‘Haya
tunarudia maelezo yetu,…kama tullivyoandika, ila hapo sasa tutarekebisha na
kuandika hivi…
Kwanza
ukubali ukweli kuwa kwa maelezo yako wewe, wewe ni mganga lakini pia umekuwa
ukitumika kwenye uchawi…labda tuiweke hivyo, tutahitajia sababu zako, kwanini
ulitumika hadi kufanya mambo hayo ya kichwai, sawa, hapo tupo sawa….’akaambiwa
‘Hapo
kidogo tupo sawa, japokuwa bado mumenibana kiunjanja…’akasema
Utakuja
kutuambia ni kwanini ulijiingiza huko hadi kufanya uchawi, ngoja kwanza
tuendelee sehemu na sharti la pili, maana muda umekwenda…’akaambiwa.
‘Sawa…tuendelee…’akasema
sasa kipiga miayo.
Pili ukiri makosa yako uliyofanya, maana kama
ulijihusisha na mambo ya uchawi, utakuwa ulifanya mambo mabaya mengi kwa watu
mbali mbali, sasa ili toba yako ikubalike, tutahitajia toba yako kwanza kwa
maneno, pili kwa vitendo,wewe ndiye unayewajua hao uliowafanyia huo uchawi,
sizan kama utashindwa kuwakumbuka,..lengo hapa kama umewafanyia hivyo,
utahitajika kuwatibia, …unaelewa hapo…’akaambiwa.
‘Ni
ngumu….’akasema
‘Kwanini
ni ngumu..?’ akaulizwa
‘Siwezi
kuwataja wote, halafu, nitakwendaje kwa kila mmoja wao nianze kumwambia
nilikufanyia hivi, sasa nimetubu, sasa nataka nikuponye, haiwezekani jamani…mnataka
nipigwe, niuwawe…hahaha, mimi sio juha kihivyo…’akasema
‘Unaelewa
maana ya toba, maana sasa unatakiwa kutubu madhambi yako…, kuwa hayo
yaliyotokea huko nyuma hutarudia tena, si ndio hivyo..?’ akaulizwa
‘Hivyo
sawa, …nitatubu sawa, …ni kweli kwa jinsi hali inavyokwenda nahitajika kufanya
hivyo, kuachana kabisa na shughuli hizi, lakini sio rahisi kama mnavyofikiria
nyie…’akasema
‘Shughuli
gani , hebu fafanua hapo, kuachana na shughuli gani….?’ akaulizwa
‘Hizo
za uganga ambazo wkati mwingine nahitajika kuwasaidia watu, au wale wanaotaka
niwauzie, madawa ya kuwafanyia wengine uchawi, hayo nitaachana nayo kabisa,
nikijiweka vyema, maana sio kazi rahisi,…’akasema
‘Na
wewe je..maana na wewe mwenyewe ulikuwa ukiyafanya kwasababu zako au sio, sasa
na wewe unatakiwa ukubali kuwa hutayafanya tena hayo mambo, muhim utuhakikishe kuwa
wewe kama wewe, hutajishughulisha na uchawi tena,na wale uliowafanyia hivyo, utawatibia
kuondoa huo uchawi wako kwao, ili usiendelee kuwatesa, na pia utakwenda
kuwaomba msamaha kwa hayo uliyowafanyia….likifanikiwa hilo, nina imani
watakusamehe, haina haja tena ya kwenda mahakamani
‘Hivi
mnafikiri hilo ni rahisi hivyo, hebu fikirieni zaidi, hapana siwezi…’akasema
‘Sisi
tutakusaidia, tumeshajipanga kwa hilo…’akaambiwa
‘Kwa
vipi nyie mtanisaidia, haya sawa,…kama nyie ndio mtanisaidia kulifanya hilo,
aah mimi sina kikwazo,…’akasema
‘Kukusaidia
kwetu nikuwasiliana na hao watu, ukitutajia ni huyu na yule, sisi tuna watu
wametoka huko, watashirikiana na sisi kuwasiliana na hao watu wengine, lakini ikija
kwenye uwatibia, kuwarejeshea hali zao, kama uliwafanyia hiki na kile hiyo ni
kazi yako…sawa…’akaaambiwa
‘Ndio
hapo nasema hivi hilo ni gumu, halitawezekana kwa kiasi hicho…’akasema
‘Ugumu
wake ni nini hapo, kwani wewe hutaki kupona, kwani wewe hutaki kuachana na
madhambi yako, kwani wewe huogopi kuumbuliwa , kupelekwa mahakamani,…mbona
wenzako wamefanya hivyo na sasa wapo huru…’akaambiwa
‘Akina
nani wamefanya hivyo..…?’ akauliza, na huyo mama akaendelea kusoma maelezo;
‘Wewe unatakiwa uwaombe msamaha uliowakosea,
japokuwa ni ngumu kama unavyodai,…, lakini wapo wengine tupo hapa, sisi pia ni
wahanga wa uchawi wako,.. sawa? Kwahiyo wewe ukiri kwetu, kuwa ulitufanyia
hivyo, na ututibie, na kutuhakikishia kuwa hutarudia tena, ….’akaambiwa
‘Kwahiyo
, kumbe mnataka hivyo, wajanja kweli nyie…si simseme tu, kuwa ni nyie mnataka
kutibiwa,.. kuwa hayo mazindiko yaliyofanyika kwenu yaondolewe, hahaha, si ndio hivyo mnataka….?’ Akauliza
‘Kwani
sio wewe uliyetufanyia hayo mazindiko,,…kwani sio wewe uliyewafanyia hawa
madada wawili hadi wakafikia hapo walipo, nia ni kutokana na kumtaka huyo mmoja
na alipokukatalia ukataka kumuonyesha kuwa wewe ni nani…kweli si kweli..?’
akaulizwa
Hapo
akawageukia wale madada wawili, akakunja uso, kuashiria chuki fulani, halafu
akasema
‘Najua
hawa ndio sababu ya haya yote kwenu nyie…, sawa, mimi kwenu nyie nitajitahidi
kufanya hivyo, nitatubu mbele yenu, kuwa nayfahamu hayo, … na nitawatibia,
lakini …nawapa angalizo moja.., msifikirie ni rahisi hivyo…kwanini nasema
hivyo…, kwasababu hayo mambo yanatokana na sababu nyingi kutoka huko nyuma, sio
kwamba yamefanyika tu, kama navyofikria nyie, haya ni matokea ya historia, na
mapambani kati yangu na hao maadui zangu …’akasema
‘Hizo
sababu utakuja kuzisema, ikibidi tutapoteza muda mwingi, waakti tunahitajia
haya mambo yaishe,..lakini kidogo kidogo, tujeshaanza kukuelewa, kuwa hufanyi mambo
haya kwa matakwa yako, kuna sababau,…lakini muhimu ukubaliane na hili kuwa upo
tayari, kutubu, kuwaomba masamaha uliowafanyia hivyo,..kuwaponya, na tutataka
kusikia hizo saabu, lakini tunaogopa
muda, ila tukiwa hapa, ututibie uondoe huo uchafu wako kwenye majumba yetu, na
uape kuwa hutarudia tena....’akaambiwa
‘Lakini
hapo hapo na nyie mkubali kunisaidia pesa za matibabu yangu…’akasema
‘Hilo
litakuja baadae, halina shida ..muhimu ni wewe uanze kazi hiyo…’akaambiwa
‘Sawa,…’akasema
na hapo hapo akaweka sahihi kwenye kipengele hicho, na kusema,
‘Unaona
kwa hili nimekubali na halina shida,..lakini sio hilo la kipengele cha kwanza,
hilo mlitaka kunifunga hapana mimi sio mchaiwi, narudia tena, mimi sio mchawi,
na haya yaliyotokea yana sababu kubwa sana, nitakuja kuwaelezea , ….’akasema
‘Sawa
tuendelee na kipengele kingine…?’ akaulizwa
‘Sawa..ila
hapa, nimeweka sahihi mapema, nilitakiwa tuendelee kusoma hadi mwisho,halafu
ndio tuanze kazi ya kuweka sahihi…’akasema
‘Usijali,
tupo pamoja…’akaambiwa
‘Nyie
wajanja sana, hasa wewe, kiukweli sitakusahau, kwa hili aah, sijui…’akasema na
huyo mama akasema
‘Usije
kujaribu kuniloga tena, ..mimi nimefanya ubinadamu tu, ila ningeamua kukufanyia
malipizo, usingeliweza kuinua mdomo wako, ogopa malipizo ya kunyanyua mikono
juu na kumkabidhi mwenyezi-mungu, usije
ukalogwa, ukasema, ni duwa ya kuku tu,
haiwezi kumpata mwewe, kama ulivyowahi kusema kumuambia huyo binti,... wewe…..ogopa duwa ya mwenye kudhulumuwa, unaona
unavyoonza kupata taabu, kabla hujachelewa tubia,maana huijui kesho yako, utakuja kujuta muda umeshakwisha…’akaambiwa
‘Sawa
nimekuelewa, ..si ndio hivyo tunaanza kuelewana, mimi sio mbaya kihivyo, …’akasema
‘Sasa kwa vile kuwachawia watu wengine,
kumeleta madhara, kuna watu wameathirika, mfano familia yangu, kumetokea
mataizo makubwa, ushakubali kuwa unahusika kwa hilo na utaitibia, hewala,…
lakini wapo hawa mabinti wawili,wapo wenzangu hapa, unatakiwa, uwatibie wote
kwa gharama zako wewe mwenyewe,,,, kwa kuondoa hayo mazindiko yako, na uwahakikishie
usalama wao, na ikibidi uwafidie..’akaambiwa.
'Wacha
hiyo,…haiwezekani kabisa, kwa vipi..hapana hapo pa kuwafaidia kwa vipi, mimi
sina pesa ..ningekuwa kwanini ifikie mahali pa kuwaomba mnisaidie hapana hapo
hapana, hicho kipengele kigumu…’akasema.
‘Tutakirekebisha,
hapo kwenye kufidia muda ukifika, si umesema tusome kwanza, hapa tunaweka alama
kuwa kunatakiwa kurekebishwa, au turekebishe sasa hivi..?’ akaulizwa
‘Mhh…nyie
ni wajanja sana, hebu endelea kipengele kingine…’akasema.
'Kipengele
kingine kutokana na hayo madhara, kwa Mfano hawa mabint, huyu mmoja sasa hivi ni mja mnzito, utuambie hiyo mimba
imeingiaje mwilini mwake, maana ulisema hiyo mimba sio mimba ya kawaida, ni
mimba ya namna gani wewe unajua hilo, sasa utafanyaje iwe mimba ya kawaida wewe
unalijua hilo, lakini pia, wewe unajua ni mimba ya nani,,..maaana wewe ndiye
ulifanya , ukasimamia, ukawepo vikifanyika, na huenda na wewe umeshiriki kumzalilisha huyu
binti wa watu…sasa hili nalo, ni sehemu ya masharti yetu…’hapo akakatiza na
kusema
‘Hapana,
mimi sijashiriki, kumzalilisha hapo napo kuna utata, ….wapo waliotenda, lakini
sio mimi, sikutakiwa kufanya hivyo kabisa, ndio maana nilimtaka huyu binti
nimuoe, sikutaka kumzalilisha, kama ningelitaka ningelifanya hivyo, naweza hapo
sikatai… …’akasema
‘Ungeliweza
kwa vipi, si kwa uchawi, au…?’ akaulizwa
‘Kwa
namna ya madawa ya kumvuta, ukiita uchawi sawa, lakini sikutaka nikataka njia
ya kawaida, akakataa, sijaendelea kumlazimisha…’akasema
‘Lakini
ulimfanyia mambo, ma athari zake ndio hizi zimetupata na sisi…au sio…?’
akaulizwa
‘Yaliyotokea
ni katika mapambano, muulizeni ni mimi peke yangu niliyemtaka kumuoa,….muulizeni
labda hilo hajawaelezea, ndio maana nataka kuja kutoa maelezo zaidi, isije
kutokea kuwa hayo katendewa na wengine na mimi natumbukizwa kiaina…’akasema
‘Ni
nani mwingine alitaka kumuoa..?’ akaulizwa
‘Anamfahamu
yeye, kwanini hamumuulizi yeye mwenyewe…’akasema
‘Wewe
ndiye unatakiwa kuweka sahihi hapa tumalizane na wewe, maana kipengele hiki
kinakuhusu wewe, tunaweza kuongeza kuwa wewe ulikuwa ukishindana na mtu
mwingine katika kumpata huyu binti, au sio, sasa ni nani huyo, tuambie..?’
akaulizwa
‘Mimi
siwezi kumtaja amtaje yeye mwenyewe, na kwa sababu hiyo kipengele hicho nacho
kinahitajia marekebisho, kabla sijakikubalia…’akasema
‘Kwa
upande wako wewe…tuache kwa huyo, wewe unajua huo ujauzito upoje umeshatuambia
kuwa sio wa kawaida, kwa vipi, ukubali kulifafanua hilo, na ukubali kutuambia
ulivyoingia, na utausawazishaje uwe uja uzito wa kawaida, lakini pia…ni nani
walishiriki kwa mauchawi yako hadi wakampachika huo uchawi…utatuelezea, sawa….’akaambiwa
‘Hao,…watu,
unataka niwataje, wewe unataka, ili iweje, huogopi kuwa itaathiri ndoa yako…’akasema
‘Kwa
vyovyote iwavyo, wao hawakupendelea hilo, wewe ndio sababu, …’akaambiwa
‘Ndio
maana nasema mengine yana ugumu kutoka na taaluma yenyewe, sitaweza kufanya
kama nmnavyotaka nyie….’akasema
‘Utaweza,
hili hapa ni lazima uweze, kama wewe ulifanikisha hili, ukaingia ndani kwangu,
ukafany aulivyofanya, familia yangu ikahusika, nataka uwaelezee ni nani na
nani,..na ilifanykaje, na ni nani alihusika..kama ni wao waanhsuiak na huo uja
uzito, ninataka kujua,…’akaambiwa
‘Hahaha
wewe…lakini nikuambie kitu, kwenye maeleo nitakayotoa, kwanini nilifikia huko,
utaweza kuona kuwa haina sabbu yaw ewe kutaka kujua hayo, ila ukitaka, sawa…hata
kama sio mimi niliyefanikisha hilo, ila kwa vile family yako imehusika, basi,
nitakusaidia kuwataja…lakini sikupendelea iwe hivi, mbele ya watu hawa…’akasema
‘Sawa
nimekuelewa, tutalirekebisha, kuwa wewe utanitajia nikiwa mimi na wewe, ..sawa,
ili kuondoak hicho unachosita, mimi isogoi wakisikia, maana hawa ni wenzangu ni
marafiki zangu, na tumeamua kulibeba hilo kwa pamoja..’akasema
‘Sawa,
tuendeee…’akasema
‘Kwa
hawa mabinti kuna kipengele cha gharama, na majukumu, maana sababu ya mimba hii
ni wewe, sasa wewe ndiye utabeba hizo gharama, hadi kujifungua, huduma za mtoto,
nk….na hilo tutakuja kuliweka vizuri, kuwa utafanya hiki na kile pale ukija
kutuambia ni nani walioshiriki, na ni nani aliyempa mimba huyu binti, sawa…?’
akaulizwa
‘Hapo
pagumu….’akasema
‘Kwanini…ni
pagumu kwanini.., usipoteze muda hapa.., unaanza kunifanya nisikuelewe, kwanini
ni pa gumu hapo, wewe hukuwepo wakati linafanyika, wewe hukulisimamia hilo, …ukahakikisha
huyu binti wa watu anazalilishwa, huyu ana kosa gani na wewe, hebu tuambie,
huyu ulimtaka na yeye akakukatalia, ni unyama ulioje ulioufanya…, hili
litakufikisha kubayai usipokubaliana na sisi, na mimi nitalisimamia, hatua kwa
hatu, unanielewa,.?’ Mama sasa akawa aoangea kwa ukali,
Jamaa
akanitupia jicho mimi, na mimi nikawa namuangalia kwa uso uliojaa hasira, na kabla
hajasema neno, mara docta akaingia na kumnong’oneza yule mama mwingine ambaye
ndiye katumika kuongea na huyo docta, ilionekana kuna jambo.
Huyo
mama aliyeongea na docta, akaja kwa huyu mama muuliza maswali akamnong’oneza
kitu sikioni, na huyu mama muuliza maswali, akaonekana kuwa mashaka, …akatupa
jicho kuangalia kile kifaa cha matukio, halafu, akatikisa kichwa kukubaliana na
huyo mama, na kusema
‘Sawa….iwe
hivyo, hatuna muda tena….’akasema, kitendo hicho sasa kilimfanya huyu jamaa awe
na mashaka,…akaonekana kuwaangalia akina mama hao kwa makini, akatupa jicho
kuangalia kile kifaa alichoambiwa kinachukua kumbukumbu za humu ndani, akawa
anakuna kichwa kwa haraka haraka, na akaanza kuhema kwa kasi,..
Ilionekana
jamaa hayupo vizuri…hali ikaanza kumbadilika,…..
NB:
Kidole kinauma
WAZO LA LEO: Kuwatendea wengine ubaya, tunaona ni
jambo rahisi sana, lakini kitendo kama hicho kikitokea kwako, kitakuumiza sana,
swali ni kwanini ukaona ni rahisi kwa wengine lakini kwako ikawa ni maumivu,
kama hivyo, kabla ya kuwatendea wengine ubaya, hebu tujaribu kujiuliza, je
nikitendewa mimi naitarizika, hili litasaidia kutushtua tusiendelee kuwatendea
wengine mabaya.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment