‘Sasa hapo utaamua moja, mimi niondoke au huyo
hawara wenu aondoke, kama ikigundulikana kama ninavyofikiria mimi, basi utachagua moja kati ya hayo mawili... unasikia, mzee wewe,...'ilikuwa kauli ya mama mwenyeji akimuambi mume wake kabla hatujafika hopsitalini.
Tuendelee na kisa chetu..
***********
Waliongea wenyewe huko bila kujua ni nini
kimekubaliwa, ila subuhi ndio nikaambiwa nijiandae kwasababu nitakiwa kuepekwa hospitalini,…’nikaambiwa.
‘Na kule kwa wafadhili wako wa awali, wamepiga
simu na kusema kuwa bado mambo hayajakaa sawa, kwahiyo wameomba niendelee kukaa
na wewe hapa hadi muafaka utakapopatikana…’akasema mzee wa hapo
‘Lakini mimi siumwi kwasasa najisikia nafuu kwa
sasa..na kwa vile zile dawa nilizopewa awali bado zipo, naona ni bora niendelee
kuzitumia,, sioni ni kwanini twende huko hospitalini nikapewe madawa mengine
zaidi…’nikasema.
‘Hapana inabidi tukupeleke ukachunguzwe vizuri
afya yako, huenda kuna tatizo jingine limejificha, huko kuanguka-anguka sio
kuzuri, unajua kizungu zungu, kinaweza kuwa ni sababu ya matatizo mengi, sasa
ni tatizo gani, hatuwezi kulijua mpaka ukapimwe, …na vipimo ndio vitasema,…’akasema
mzee.
‘Sawa, lakini mimi sikuona sababu ya kwenda
huko, na mara nyingi mimi nikiumwa natumia dawa za miti shamba na zinanisaidia,
hazi dawa za hospitalini zinaniongezea matatizo tu…mimi najua dawa zangu, kama
tukienda kwa wauza madawa ya kienyeji nitawaonyesha…’nikasema
‘Hapana hayo matatizo, kama malaria, huenda una
upungufu wa damu, au shinikizo la moyo, halihitajii madawa ya kienyeji, usiwe
kama wazee, wao walifanya hivyo kwa vile hakukuwa na hospitali, au hospitali
zipo mbali, hapa hospitali zipo….’akaambiwa
‘Sawa mimi nawasikiliza nyie, kama siwatii
hasara, basi, mimi nipo tayari twendeni…’nikakubali tu kwa shingo upande.
Tuliondoka hapo nyumbani mimi na baba na mke
wake,…namuita hivyo baba kama wenzangu walivyozoea kumuita,…na hatukuchelewa
tukafika hospitalini, wao wakongea na docta na nikachukuliwa vipimo vya damu ,
choo na mkojo, na tukaambiwa tusubiria nje, na tulipokuwa tunasubiria mama
akamuona rafiki yake mmojwa, wakawa wanaongea, na baadae wakasema wao wanakwenda
kumuona mgonjwa aliyelazwa hapo, kama nikiitwa kabla hajarudi tuende mimi na
baba, basi mimi nikabakia na huyo mzee tukisubiria majibu ya vipimo.
‘Usiwe na wasiwasi kabisa…, kama ulivyoniambia
ni kweli, basi hakuna jambo la kuhofia…au sio, kama ni kweli lakini,
nilikuambia awali, usinifiche kitu, nichukulie mimi kama baba yako,…unasikia,..na
kuja kwtu hapa ni utaratbu wa kawaida tu wa kujirizisha, ni muhimu ukaijua afya
yako, sawa, kwahiyo usiwe na mawazo na wasiwasi…’akasema.
‘Kwani mnataka kujua ni nini zaidi baba..kuwa
labda nina..tatizo gani..?’ nikauliza
‘Hapana, sio kwamba tunahisi kuna tatizo
kubwa,lakini ni vyema upimwe, hakitaharibika kitu ukipimwa, …’akasema
‘Sawa baba, basi Itakuwa vizuri, ili mjirizishe
nafsi zenu, maana naona mna wasiwasi sana na mimi, na kiukweli hata mimi naona
iwe hivyo, maana sijawahi kujisikia hivi kabla, ..’nikasema.
‘Umeona eeh, sasa vipimo ndivyo vitasema ukweli,
…nikuulize tena,..umesema hujawahi kuwa na rafiki yoyote wa kiume, niambie
ukweli, hili ni mimi na wewe, kama yupo wewe usiwe na wasiwasi na mimi nitajua
jinsi gani ya kukulinda..?’ akaniuliza.
‘Sijawahi kuwa na rafiki yoyote wa kiume mzee
wangu, niamini kweli kabisa, kama angelikuwepo ningelikuambia wewe nakuamini
sasa kama baba yangu,…mimi sina tabia hiyo, mama alinikataza kabisa alipokuwa hai, na
siwezi kuvunja ahadi ya mama yangu..’nikajitetea.
‘Basi kama ni hivyo itakuwa vizuri sana, mimi
nimemuambia mke wangu haina haja ya kuwa na wasiwasi, wewe ni binti mwema kabisa,nimechukua
dhamana kwako, ..na nikuulize kitu kingine labda kuhusu zile ndoto, si ulisema
hujaota tena, tangia uje hapa kwangu, au sio… je kule ulipokuwepo, una uhakika
ilikuwa ni ndoto tu, maana hapa unatakiwa useme ukweli wote, docta takuuliza
yote hayo, kama kutatokea tatizo lolote, japokuwa kama ulivyoniambia ni kweli
hakuna tatizo,....’akasema huyo mzee.
‘Kweli kwa vipi baba…, ilikuwa ni ndoto tu, kama
kuna jingine mimi sijui, na kwa vipi, kwani ndoto inaweza kuwa kweli baba,
maana haya sasa yananitia mashaka..?’ nikauliza.
‘Unajua bint nyie wanawake mna mitihani mingi, …sasa ukiwa
msiri sana, unaweza ukaficha tatizo likaja kuwa kubwa,…mkiumwa maradhi kama
hayo,…, kuna mambo mengi sisi kama wazazi tunayafikiria, lakini usijali, kipimo
kitasema ukweli, nia ni kuondoa mashaka , hasa kwa mama yako, mimi nina imani
hauna tatizo lolote jingine…’akasema.
‘Tatizo kama lipi, analonifikiria yeye, naona
kanihoji maswala mengi akinihisi labda mimi ni wanaume, baba mimi sina tabia
hiyo kabisa, na wala siyajui mambo hayo, sijui anataka kujua nini..?’
akaniuliza na mara tukaitwa, kuwa vipimo vipo tayari na mama mwenyenyumba
alikuwa hajarudi,ikabidi tuingie na huyo mzee, na docta alipotuona tupo wawili
, akamuuliza mzee.
‘Huyu ni nani wako?’ akauliza
‘Mimi ni baba yake mlezi….’akasema, sijui
kwanini hakusema babu, lakini ndio hivyo, hata mimi nimezoea kumita baba
.
‘Je huyu binti ameolewa..?’ akauliza docta,
hapo nikahisi mwili ukinisisimuka, maana haya maswali ya kuolewa, mchumba,
mbona yanazidi kuwa mengi.
‘Bado hajaolewa, na wala hana hata mchumba,
kwani kuna nini umegundua docta…?’akasema na kuuliza.
‘Je ana rafiki yoyote wa
kiume…anayetambulikana..?’ akauliza na hapo mzee nikamuona sura ikimbadilika,
na haraka akasema;
‘Hapana, hana, nimekuambia huyu binti hana
rafiki wala mchumba, hana tabia hiyo kabisa…kama vipimo vyenu vinasema kweli
hamtagundua jambo lolote la mahusiano…’akasema mzee na docta akaniangalia
usoni, halafu akamgeukia mzee, na kusema;
‘Kwasababu hiyo mzee, mimi nakuomba utupe
nafasi kidogo, nataka kuongea na huyu binti peke yake, tafadhali ….’akasema
docta.
‘Lakini mimi ndio mlezi wake, nilitaka kufahamu
ana tatizo gani, yeye kasema hana tatizo, …..ndio maana nikajitolea kumleta
mimi na mke wangu, sasa ukisema unataka kuongea na yeye tu , basi
tungelimuambia aje peke yake..’akasema mzee.
‘Sawa naelewa hilo…, lakini kuna mambo ya
kitaalamu zaidi nataka kuongea na huyu binti akiwa peke yake, kuna maswali
naweza kumuuliza akashindwa kuyajibu kwa vile wewe upo hapa….’akasema na
mzee akaelewa na kusimama ili atoke nje,
nikamuona kama anasita sita, halafu akasema;
‘Basi ngoja nimuite mama yake aje… kama ni
mambo ya akina mama zaidi…’akasema mzee akiharakisha kutoka nje.
‘Usijali mzee, haina haja kumita yeye,…,
nitawaita wote nikimalizana na binti, ni bora niongee na yeye tu kwanza, sio
tatizo kubwa..ni jambo jema tu, usiwe na wasiwasi mzee.’akasema na mzee
akaondoka, na mlango ukafungwa.
***********
.
Docta akasimama na kusindika mlango vizuri,
mimi pale nikawa na wasiwasi, kukaa chumba na mwanaume halafu ndio kafunga
mlango kabisa, moyo ukaanza kunienda mbio, najiuliza huyu mtu anataka kunifanya
nini, nilishajipanga kupiga ukelele, kama lolote litatokea,…docta akahisi nina
wasiwasi. Kwanza akarudi kwenye kiti chake na kukaa, halafu akaichukua ile
karatasi ya vipimo, akawa kama anaisoma, halafu akasema;
‘Afya yako haina matatizo, huna maambukizi
yoyote, ni uchafu kidogo tu kwenye mkojo, itabidi uendelee na hizo dawa
ulizopewa awali, si bado unaendelea kuzitumia hizo..?’ akaniuliza, akiongea kwa
lugha nyepesi kuniweka sawa.
‘Ndio bado naendelea kuzitumia, niliwaambia
haina haja ya mimi kuja huku, lakini sijui wana wasiwasi gani…’nikasema.
‘Lakini hawajafanya vibaya, unajua ukipatwa na
tatizo, hata kama huna tatizo ni vyema ukajenga tabia ya kuchunguza afya yako,
yaonekana wazazi wako ni watu wema sana….’akasema
‘Nashukuru sana kwa kupata walezi kama
hao….’nikasema
‘Mhh…unajua umri , ukienda, mwili nao
unabadilika, na tabia ilivyo, kuna mambo yanakuja kujitokeza kwa kadri
tunavyokuwa, hiyo ni kawaida, kuna
maswali machache nataka kukuuliza ili usije kupata matatizo kama hayo
tena,…’akasema
‘Sawa niulize tu….’nikasema.
‘Mimi ni docta, na madocta ni wasiri wakubwa ,
kwa wagonjwa wao, usipomuamini docta basi wewe hutaki afya yako iwe njema,
…nataka uniamini sawa, …’akasema
‘Sawa mimi nakuamini docta….’nikasema.
‘Niambie ukweli, unajua nilipokuwa shule,
nilikuwa na rafiki wa siri, watu walikuwa hawalijui hilo, na wengi wanakuwa
hivyo, na wakati mwingine kuna ule mchezo wa baba na mwana, tunajificha..na
hata tunajikuta tunaanya mambo bila kutegemea…’akasema.
‘Mhh, mimi hata siku moja sijawahi kucheza hiyo
michezo ya baba na mama…, docta maisha yangu na mama ni ya shida, sisi tulikuwa
wakuhangaika barabarani kuomba, hatuna shamba, ni kibanda kidogo tu,hatuna
jamaa , tulizaraulika....basi ni shdia, namshukuru mungu kuwa nimepata hawa
wafadhili, na niliposikia kuwa mama kafariki, nilijua basi hata mimi nitakuja
kumfuta tu…’nikasema.
‘Hapana wewe ni kijana na maisha yapo mbele
yako, kamwe usikubali kushindwa, na matatizo iwe ni sehemu ya changamoto ya
kupiga hatua mbele…, inatakiwa ufike mahali ujipange upate kitu cha kufanya
ambacho kitakuingizia kipato, kama hivyo upo na walezi kama hao, wanakujali..
watumie, ujifunze jambo, ufundi, au kazi yoyote ya kuzalisha, ambayo itakufanya
usimame kwa miguu yako mwenyewe, usikate tamaa kabisa…’akasema docta.
‘Sawa nitafuata ushauri wako docta…’nikasema.
‘Na kama nilivyokuambia, uniamini, kuna jambo
nataka unifunulie kidogo, sio bay asana…, nataka uniambie kitu, kwasababu sote
tumepitia huko, nata uniambie ni nani huyo rafiki yako wa siri..usiseme huna
rafiki, kila mtu anaye…, hata awe siri,… unajua kuna jambo hapa, linatakiwa
wewe nay eye mtibiwe pamoja, tunaweza kupanga mimi na wewe jinsi gani ya
kumuita, hata watu wengine wasijue…najua unaye rafiki wa kiume, kwahiyo
nilipenda tusaidiane kwa hilo, unasemaje…? Akasema.
‘Mhh docta, ina maana huaniamini, mimi sina
rafiki hata mmoja wa kiume, na ..kwanini tena.., si umesema sina tatizo…au?’
nikauliza.
‘Ni kweli huna tatizo kabisa..umesema huna
rafiki wa kiume, au mchumba, lakin inaweza kutokea, ujana una mambo mengi mimi
naelewa, labda, nikuulize hujawahi kukutana na mwanaume, au kwa kulazimishwa au
kwa namna yoyote ukakutana naye kimwili,..inaweza ikawa ni kwa bahati mbaya.?’ Akaniuliza.
‘Kukutana na mwanaume kwa vipi..hapana
haijawahi kutokea, hapana wee, mama akijua hilo, yaani sio kwa ajili ya mama
tu, mimi mwenyewe nimeahidi sitaki mwanaume, hadi hapo mungu atakaponiongoza,
sitaki na sijawahi kuwa na rafiki mwanaume,..na hakuna, ..hata kushikwa kwa
nguvu. Haijawahi kutokea kabisa, mimi sijawahi kukutana na mwanume, sijawahi niamini docta..kwani
kuna nini mbona kama kuna tatizo, niambie kama kuna tatizo?’ nikauliza.
‘Huwa inatokea kwa umri wenu, wenu, na ni vyema
ukasema ukweli , maana ni vizuri sana hili swala likajulikana na wazazi wakajua,
ndio maana nikata tuongee uniambie ukweli, ukificha, itakuwa vigumu kwako
kusaidiwa, na mtu wa kukusaidia ni mimi, unajua sisi madocta kisheria
tunatambulikana sana, pia mimi nipo kitendo cha kuwasaidia wanawake walio
kwenye mazingira magumu, lakini siwezi kumsaidia mtu kama hasemi ukweli..’akasema
‘Docta unataka ukweli gani…?’ nikamuuliza
‘Unajua ukinificha, haitasaidia kitu, maana
mimi naweza kukupima kuona kama kweli hujawahi kukutana na mwanaume, na itabidi
nifanye hivyo kama utaendelea kunificha, bora useme ukweli ili tuanze sura
nyingine, na ukificha, nitawaachia wazee wafanye kazi yao…’akasema.
‘Docta niambie ukweli, kwani mimi nina tatizo gani, usinizungushe
zungushe…’nikasema.
‘Una mimba…na kwa maelezo yako na vipimo, una
mimba ya miezi miwili na kitu hivi hongera sana, lakini unanistajaabisha
ukisema hujakutana na mwanaume unaona hapo, unajidanganya mwenyewe, sasa iambie
ukweli ili niweze kukusaidia…’akasema.
‘Hongera, docta, unanitania, mimi mimba
nitaipataje..’nikasema kwa hasira
‘Binti, usifiche, hili swala sasa sio la
kuficha, unanielewe, inabidi umtambulishe huyo mwenzako ili muona jinsi gani ya
kuliweka sawa, ukiendelea kuficha, wazee watakuelewa vibaya, kwa ushauri wangu
umsema mapema, mimi nitakusaidi kuliweka sawa nikiongea na wazee wako…’akasema
*************
Docta aliponiambia hivyo, kwanza sikuamini, lkn
jambo lililonijia akilini ni kuhakikisha kuwa wafadhili wangu hao hawaipati
hiyo taarifa, na hata wakiipta niwe mbali kabisa na wao, wasije kuniona tena..
'Tafadhal docta, nakuomba nipo chini ya miguu,
unisitir na hii aibu…kama ni kweli..maana mpaka sasa mimi siamini….’nikasema.
'Kwann unasema hivyo, kwani huna mume, huna
mchumba, mimba hii umeipataje…haiwezekani, sema ukweli tu…’akasema.
'Docta mimi sijui nakuambi aukweli mimi sijui…
na ndio maana siamini, mimi sijawahi kukutana na mwanaume yoyote, nitapataje
mimba, kwani mimba unaweza kuipata hata kwa kupitia kwenye ndoto..sio kweli
docta…’nikasema
'Docta kwanza akasita, halafu akauliza;
'Unasema wewe hujawahi kukutana na mwanaume ila
uliwahi kuota kuwa umekutana na mwanaume, na ukawa na dalili hizo za kukutana
na mwanaume au sio niambie ukweli..?’ docta akauliza akionyesha uso wa
kushangaa na kutokuamini maneno ya huyo binti.
'Ndio docta,…huwaga naota hivyo, lakini sio
hapo kwa sasa, tena zilikuwa ni ndoto za majinamiz hata sura ya huyo mtu
sikuwahi kuiona, ni ndoto tu na sio kweli, mtu ananikaba, halafu nazalilishwa,
ni ndoto na sio kweli…’nikasema.
'Mhh, hili la ajabu eeh,… kwani awali ulikuwa
unaishi wapi, na ulikuwa ukiishi na nani..?’ akaniuliza docta
"Ni
hadith ndefu docta , ukitaka kuifuatilia historia ya maisha yangu utachoka....muhim,
usiwaambie hao jamaa zangu, nakuomba tafadhali sana docta, nipo chini ya miguu
yako, nitaumbuka mimi, na wala sina kosa, sijui ni nini hiki jamani, hivi mimi
nina tatizo gani, jamani..mungu wangu nisaidie na mitihani hii…’nikasema
nikiashiria kuomba kwa kuweka mikono kifuani na docta akawa ananiangalia kwa
uso wa kushangaa kidogo.
'Kwani hao jamaa zako ni nani kwako hasa….?’ Docta sasa akawa ana mashaka na mimi.
'Ni wafadhili wangu tu, mimi sina baba wala
mama, sina hata ndugu wa karibu, wao wamejitolea kunifadhili, na…awali sikuwa
na wao, na baya zaidi ni kuwa hawa wafadhili wangu wakilifahamu hili,
watanifukuza kama mbwa….nisaidia sana docta…’nikasema.
'Sasa
mimi sielewi, wewe ulitaka niwaambie unaumwa nini, maana kukusaidia kwangu ni
kuwaambia hao jamaa zao jinsi gani ya kuhakikisha afya yako inakuwa salam, hadi
muda wa kujifungua ukifika, sasa ukisema nisiwaambie, nitakuwa nafanya vibaya
…’akasema docta.
'Uwaambie ugonjwa mwingine wowote lakini sio
kwamba mimi nina mimba, kwasababu hata mimi simini kuwa nina mimba, ni mimba ya
nani wakati mimi sijawahi kukutana na mwanaume..’nikasema.
Docta,
akatikisa kichwa kutokukubalina na mimi lakin baadae akasema;
‘Sikiliza wewe nenda nje, waite hao jamaa zako
waingine na mimi nitajua jinsi gani y akuongea na wao, na wala usiwe na
wasiwasi, hakuna baya litatokea dhidi yako, niamini mimi..’akasema docta, na
mimi nikawa sina la kufanya,nikatoka, na wakati natoka, nikagundua kuwa mama
mwenye nyumba alikuwa hapo mlangoni, nahisi alikuwa akijaribu kuona kama
atasikia ni nini tulikuwa tunaongea huko ndani.
'Ehe tuambie ukweli, kulikoni masaa yote hayo…?’
akauliza mama mwenye nyumba
'Amesema muende, atawaambia mwenyewe tatizo ni langu
ni nini….’nikasema sasa nikikwepa hata kuwaangalia usoni.
'Kwahiyo kumbe una tatizo, mbona baba yako
kasema huna tatizo, ni mazungumzo ya kawaida ya kimalezi tu, kwa vile umekuwa,
..ooh, nilijua tu, una kitu wewe…’akasema baba mwenye nyumba.
‘Hakuna kitu mama, yote ni mitihani ya mungu
tu..’nikasema kwa sauti ya kutaka kulia, nilijitahidi sana nislie nisje
kuharibu , na baba mwenye nyumba, alikuwa mbali,akawa anakuja ili waungane na
mkewe kuingia kwa docta, akanitupia jicho, lakini mimi sikuweza kumuangalia
usoni.
‘Kwahiyo docta kasema twende ndani,
mumemalizana kuongea…najua hakuna tatizo au sio, mama yako ana wasiwasi bure tu…’akasema
baba mwenye nyumba.
‘Hahaha, eti hakuna tatizo, wewe unajidanganya
bure, kuna tatizo, humuoni huyo binti alivyo….huyo ana tatizo, na ole wake,
nigundue kuwa ni hivyo ninavyofikiria mimi, sizani kama kutakalika, sizani kama
nitaweza kuishi naye tena, unasikia wewe mwanaume, huyo utamtafutia makazi
ambapo mtaenda kukutana wawili sio nyumbani kwangu…’akasema huyo mama
‘Mke wangu kwani umesikia nini..mbona unanitia
aibu…’akasema mume wake
‘Mimi nakutia aibu au nyie ndio mnatutia aibu
sisi, familia yetu haina doa, tunahitajia kuijenga familaia yetu kwenye maadili
safi, sasa wewe unataka kuleta doa, kwa kuleta watu wenye tabia mbaya..huyo
bint ana mimba asitudanganey hapa…’akasema mke wake.
‘Eti nini, hapana hili sio kweli na
haliwezekani, umasikia wapi hayo, kakuambia huyu binti…?’ baba mtu akauliza kwa
mshangao, na jicho likamtoka kama kasikia jambo la kutisha
‘Unajifanya hujuiee,..wewe a utu uzima wako
wote huwezi kuliona hili, mimi nilitaka tuje huku, il uhakikishiwe kitaalamu,wewe
si unapenda hivyo, haya twende huko
ndani ukasikie mwenyewe, kwa octa, mtaalamu unayemuamini….’akasema na kufungua
mlango.
Baba mtu akawa kasimama, kaduwaa,
hakuniangalia, akakatikisa kichwa, halafu akamfuata mke wangu huko ndani kwa docta.
Na mimi nikatulia kidogo, halafu nikasimama, nikaanza kutembea kwa haraka
kuelekea kitu cha boda boda, akili hapo ilikuwa sio yangu,..
NB: Mdada anazidi kuingia kwenye mitihani,
tuone jinsi gani watu wanavyoteseka,…
WAZO LA LEO: Ukiona kwako
kuna fuka moshi ujue kuna kwingine kunawaka moto.. Ukiona wewe una shida, una matatizo
yanakuandama kila kukicha,…, ujue kuna mwingine shida hizo na matatizo ni zaidi
maradufu ya matatizo uliyo nayo wewe. Wapo wengine hawaijui raha duniani, wapo wengine
hawajui watakula nini,..wapo wengine kila siku ya mungu wanalia kwa mauimivu ya
mwili na akili, ….
Je hayo matatizo uliyo nayo ndio unafikia kukata tamaa…
Ndugu yangu…usikate tamaa ya maisha ilimradi
unapumua,.., mkabidhi mola wako matatizo yako, huku ukitafuta njia rahisi ya
kufanikisha mambo yako, lakini iwe ni njia ya halali…tatizo wengine wanatafuta
njia za haramu, ukitumia njia hizo, utakuwa unajipalia makaa..hutafanikiwa na
ukifanikiwa itakuwa ni kwa muda tu. Tukumbuke wakati wote kuwa Mungu hamtupi
mja wake, na kila mja ana riziki yake, ni namna tu ya kuitafuta riziki hiyo ,lakini
iwe sababu ya halali. Tumuombe mola wetu atufanikishie malengo yetu halali na
atujalie tuipate riziki ya halali, bila kuingie kwenye dhuluma..Aamin.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment