‘Yupo
humu ndani ya mahakama, ..hajatoka, nahisi yeye ndio kavichukua hivyo vitu,…sikuwahi
kumuona, nimefika na kukuta askari wakifanya vitu vyao, nahisi hata wao,
hawajui ni nani kavichukua…
‘Sasa
fanyeni hivi, kabla ya kumuua, ni bora kuvipata hivyo vitu kwanza, …na msaidizi
wake ..ndio yule msaidizi wake, atakwua ndio yeye, kavichukua, lakini
hanavyo,…yeye, …ndio….yupo nje ya mahakama,…hajaingia huku, sijui kama wameweza
kum-maliza…ndio … naona bora na yeye amalizwe ili tubakiwe na watu wachache …’
Ilikuwa sauti ya huyo mzee, ndio akilini nikajiuliza kumbe na
huyu mzee naye yumo
**************
‘Kama
huamini, eeh,…basi mimi na wewe mguu kwa mguu twende huko…najua hapa huruhusiwi
kuondoa, mpo kwenye ulinzi, au sio..kwa usalama wenu, au sio, hivi mikitoka
hapa mnapelekwa wapi..?’ akauliza
‘Mimi
sijui,..leo hapa kesho kule..sina uhakika kuwa tutakwenda wapi, lakini huenda
leo wakaturuhusu tukaenda majumbani kwetu..’nikasema
‘Kama
itakuwa hivyo, itakuwa ni vyema sana,…mimi na wewe tutakwenda huko, lakini kwa
sharti moja….najua huenda usiamini, lakini utaamini tukifika huko,…’akasema
huyo mzee.
‘Huyu
mzee anataka nini kwangu..’nikajiuliza kichwani, kabla sijamuuliza swali kuwa
hilo ni sharu gani.. kichwani nikawa nazingirwa na kauli yake hii:
' Unajua nimegundua kitu,kumbe yule msichana hajafa..yupo hai..
‘Unajua hayo matukio yote, yamegubikwa na
ushirikina, sasa kama nilivyosikia, huyo bint hakufa...kuna mazingaumbwe
yalichezwa…’
Tuendelee
na kisa chetu
*************
'Kwa vipi, na sharti gani hilo….?’ Nikauliza
sasa nikikumbuka maneno yake aliyokuwa akiongea kwenye simu,(… Sasa fanyeni hivi, kabla ya kumuua, ni bora kuvipata
hivyo vitu kwanza, …….naona bora na yeye amalizwe ili tubakiwe na watu wachache
…’)
Japokuwa
kwa sasa huyu mzee anasema alifanya hivyo, kwa vile anataka kuwatega hao watu
ili waje kunaswa na polisi.
'Nitakuambia ilivyo,… lakini kwanza nikuulize,…. unajua mimi ni mjumbe wa
nyumba kumi, kwenye eno langu na sasa nilikuwa nataka kugombea udiwani…?’
akaniuliza.
‘Mimi
hayo siyajui mzee…’nikajibu hivyo, nikijiuliza kichwani hilo linakujaje hapo,
lakini akilini nikasema ngoja niende naye taratibu, maana hawa watu ni wajanja
sana.
‘Ili
nipate kura, ili wananchi wanikubali ni lazima nionyeshe juhudi zangu ,na moja
ya juhudi zangu ni kuhakikisha matatizo kama haya, yanaondoka…nitaonyeshaje
hilo, kama nisiposhikirikiana na polisi, kwahiyo,..nataka na wewe iwe siri
yako, kama nilivyoongea na polisi kuwa nitashirikiana nao, lakini sitaki
nijulikane..umenielewa hapo…?’ akaniuliza akiniangalia machoni moja kwa moja.
Nikakumbuka
kauli ya docta, kuwa watu hawa hutumia macho, kama njia ya kukuteka akili,
akikuangalia sana na wewe ukamuangalia, anakuteka akili na anakuja kujua
unachofikiria,…au unavutwa na hisia zake…
Hapa
nikaminya macho kama simuangalii…akatikisa kichwa kama kukubali, halafu mimi
nikasema;
‘Hebu
nifafanulie maana mzee, mimi sijakuelewa unachotaka ni nini kwangu, sawa ulitaka ukutane na mimi, kuhusu
huyo mtoto…huyo binti wa mzee au sio…., ambaye sisi sote tunafahamu kuwa ni
marehemu….ila wewe….’nikasema, na yeye akanikatisha kwa kusema;
‘Ndio
hivyo, hiyo ni siri,…na hata polisi hilo sijawaambia, ni kwanini unajua,…
kwasababu bado sijaweza kukusanya ushahidi wa kutosha, naweza kuwaambia hivyo,
wakaingiwa na kimuhe muhe cha kutaka kuona, si unajua polisi walivyo, wanapenda
kutumia nguvu …sasa hao watu wakifahamu,….maana hao watu sio mchezo, wana viona
mbali, hata hapa tunapooongea sijapaamini…’akasema akigeuka huko na huko.
‘Lakini
hapa ni mahakamani, kunalindwa, na kila mtu anapaheshimu, sizani kama kuna mtu
anaweza kuja kuweka vitu vyake humu…’nikasema.
‘Umesema
kweli…lakini huwezi jua,…sasa ni hivi, sio jana na juzi, siku hizi uchawi upo
hadi kwenye mitandao, unaweza kuamini hilo…’akawa kama ananiuliza huku
akitafuta macho yangu.
‘Sasa
ni hivi… unielewe sana vyema…, kwa vile mimi nataka kuwa kiongozi, nataka watu
wakunisaidia mambo fulani fulani, ya kampeni , si unajua tena, na mbinu za
kisiasa…eeh! Mbinu za kisiasa bwana.., zinatakiwa uume na kupuliza..huku
ujifanye upo, na huku unapalilia unga wako…hapo nafikiri nimekuacha mbali…au
sio’akasema
‘Sana…bado
sijakuelewa mzee…’nikasema sasa nikiangalia pembeni, na yeye akaangalia huko
kwa mashaka.
‘Mbinu
yangu ni hii, mimi ni mtu wa serikali, unasikia sana....sasa ili nipate faida
kwa ajili ya-serikali, kwa ajili ya- watu-wangu, …na, na…kwa ajili ya
kufanikiwa kwenye kupata kura…hahaha, kula….wengine wanasema hivyo…, natakiwa
nifanye kama ulivyosikia, nikiwadanganya, sio
kweli..mimi sio mnyama kiasi hicho..ni mbinu, ili waje..eeh, waingie
mkenge…’akatulia halafu kama ananinong’oneza akasema;
‘Natakiwa
niwe na mawasiliano na hao watu nijue wanachokifanya na huku upande mwingine,..natafuta
kula yangu…unga wangu baba, mjini hapa, umenielewa eeh…’akasogea kama
kunikaribia, halafu akatulia na badae akasema;
‘Unielewe
hapo, huko nafanya hadaa, …..huku kwenue jamii, nahakikisha wapo salama, na
kuwa kwao salama eeh, ni kushirikian na polisi,…umeona hapo…’akatulia
akinikagua machoni, nahisi aliona kama simuamini au kuna jambo halimuendei
vyema, halafu akasema;
‘Lakini
wakati huo huo,… sitaki kuwapoteza wafuasi wangu,…lakini hebu ona hapo, baadhi
ya wafuasi wangu, eeh,…ni wahalifu…unaona ilivyo ngumu hapo..sasa natakiwa
nitumie akili ya hali ya juu, nisiwapoteze, kwa wao kujua kuwa nawatekeleza kwa
polisi,….nakuwa upande wa hao watu..kinamna…, ili niwachote akili, na wakati
huo huo….nipo karibu na nani…’akatulia kama ananiuliza.
"Lakini
mzee watu gani hao…." maana unatumia neno watu, watu… nahisi unawafahamu hao
watu ..ni watu gani hao..?’ nikamuuliza
'Ni
hao wahalifu…’akasema kwa sauti ya kunong’ona, halafu akaendelea kuongea;
‘Lakini
..tatizo ni hilo..hao watu hawajulikani ni akina nani…., kwasababu hakuna
ushahidi wa kuthibitisha uhalaifu wao,…sasa mimi ni mjanja,..nautafuta huo
ushahidi kwa namna yangu,…nitaupataje huo
kivyangu, eeh,..mimi hapo ndio natumia mbinu za kiraia…mbinu na kupuliza
na kuuma….unaona nilivyo mjanja, kufanya nini, kuuma, na kupuliza,
umenielewa…ndio hivyo…’akasema
'Sawa nimekuelewa mzee, sasa niambie kuhusu
huyo binti…., unasema hajafa kwa vipi, wakati akizikwa na wewe ulikuwepo,…si
ulihudhuria mazishi yake, au sio… ukashuhudia mazishi yake, kwa macho yako, ….
iweje sasa aonekane yupo hai..?’ nikamuuliza.
‘Hapo
sasa..eeh, … ndio nataka ukubaliane na masharti yangu, ili twende sana, unajua
mimi ni mzee, nimeona mengi na ninajua mengi, nyie vijana mnakurupuka
tu…mlitakiwa mkae na watu kama sisi, muelewe dunia inavyokwenda kwanza..….umenielewa…’akasema
akijaribu kuniangalia machoni,lakini nikawa mjanja, nikawa natumia mbinu za
kumkwepa….nikasema.
‘Nikubaliane
na masharti gani zaidi mzee….?’ Nikauliza
‘Kwanza,..tukubaliane
hili, kama umenielewa vyema, nataka… hili… li-we-siri, kati yangu mimi na
wewe….unasikia, mimi-na-wewe, asijue mtu mwingine..hata huyo docta wako, eeh,
si unamuamini sana, lakini kwa hili, unisikie sana na unielewe, nata yeye asilijue
hili kwanza, utakuja kumuambia baadae, baada..!Hivi nikuulize kitu, hivi wewe
unamuamini sana huyo docta wako…?’ akauliza akiniangalia kwa macho ya udadisi
‘Kwanza
mzee, hapo mimi unanitia mashaka….’nikasema
‘Kwa
vipi tena, si umesema umenielewa au ?’ akauliza
‘Nimekuelewa
ndio..lakini…huo usiri unaoutaka wewe, sijakuelewa kwanini uwe usiri hadi ,
hata kwa docta,..….sawa naweza kufanya hivyo, lakini sasa…kwanini hata docta, najiuliza
sana hapo…unajua docta ni ndugu yangu,….’nikasema
‘Ndugu
ndugu..hahaha, mimi nimeshuhudia ndugu wanauana, sababu ya mali, sababu ya vitu
vidogo tu….wewe niamini mimi..najua, na nimeshamjua yeye ni nani….unasikia
sana, kwasasa huwezi kuamini, lakini utakuja kunikumbuka…’akasema
‘Kwani
docta ana nini, mpaka nisimuamini, nimeshakuambia yule ni kama ndugu yangu….yeye
ni mimi, tumetoka mbali…’nikasema
‘Hahahaha..yule
jamaa mjanja sana,..unajua kila mtu anayeingia hapa kwenye huu mji wangu,…maana
mimi ni aliwatani, nimezaliwa hapa nimekulia hapa, nazeekea hapa, na huenda
nikafia hapa, ya mungu mengi,..ndio maana watu wameniamini na kunichagua mimi kuwa
kiongozi wao wa eneo lile…kama mjumbe, sio huku, huku kuna watu wengine, unajua
ni …kwanini…’akawa kama ananiuliza
‘Ni,
kwasababu najua mengi,..masikio yangu yamesikia mengi na macho yangu yameona
mengi..na akili yangu ….ipo bara bara…hekima, na ufahamu, …sasa kuhusu eneo
hili nalijua awali hadi sasa..kule ninapoishi napajua mwanzo mwisho…, na kitu
cha mumimu..mimi nina hekima ya uongozi….shule. eeh,...’ hapa akashika kichwa,
halafu akasema
‘Ukiguzia
kuhus shule, kuwa nimesoma hadi wapi,..ndio nimesoma, sio saana…lakini akili
ninayo…maana nimepitia hata uaskari,..huyo mzee mwenye..rafiki yangu, eeh,
wanamuandama sana…tuli..niliwahi kumpangisha, namjua sana…ni rafiki yangu,
namuonea huruma sana..lakini wakati mwingine yeye ni mbishi, hanielewi…sasa
ndio hivyo, yatakwisha tu…’akatulia alipoona askari wanapita.
‘Hawa
watu,..’akasema akinielekezea kwa kichwa…
‘Eeeh,
wakati mwingine.. unatakiwa uwe makini nao,..ni watu wetu, vijana wetu,...lakini
wakati mwingine hawaaminiki…’akasema alipoona namshangaa kwa kitendo chake cha
kuwaangalia askari kama anaogopa vile.
‘Sasa
tusipoteze muda, upo tayari kwa masharti yangu…’akasema sasa alipoona hao
askari wamepita.
‘Yapi
hayo..?’ nikamuuliza
‘Kwanza
na la muhimu, iwe siri , kati yangu mimi na wewe, pili..wewe siunataka kuonana
na huyo mrembo, eeh, ujana una mambo yake bwana nakumbuka enzi yangu, nilikuwa
hivyo, ..na yule binti..alikuwa mnzuri..ni mnzuri..sasa wewe si unataka kuonana
naye,ili uhakikishe niliyokuambia au sio…wewe na mimi…, tufuatane, ili
nikuonyeshe hapo nilipomuona huyo binti, sio ndio hivyo…’akasema
‘Una
uhakika mzee…?’ nikamuuliza
‘Uhakika
uhakika gani…utaupata mimi na wewe tukiona kwa macho yetu…ila naona vyema ili
kuyaweka haya sawa…muhimu kwanza tukutane ….eneo la siri. Sio hapa….’akasema.
‘Wapi..?’
nikamuuliza, na yeye akageuka huku na kule kama ana wasiwasi na jambo fulani.
‘Kule
makaburini…’akasema sasa akageuka kuangalia upande mmoja, askari walikuwa
wakikagua watu, na yeye akaonekana kama hana amani….akasema;
‘Umesikia,
si umenielewa eeh,naona muda,..unajua muda ni muhimu sana, na naona hao jamaa
wanatekeleza wajibu wao,..sasa…basi, mimi naondoka, eeh…’akasema sasa akiinu
amguu kuondoka.
‘Sikiliza
wewe… ukiwa tayari nipigie, tukutane huko,..nilipokuambia… na kumbuka
niliyokuambia,..hilo ni mimi na wewe, sawa… ‘akawa kama kasahau kitu akageuka
kuniambia.
‘Umsikia,…na
hayo, uliyosikia, usimwambia mtu, …maana ukimwambi amtu, umevuruga upelelezi
wangu, na jingine uwe makini na docta, yule ana ajenda ya siri, ya kutaka
kukutumia ili afanikiwe mambo yake…hilo, tukikutana tena
nitakuambia,..ila..sasa ukifungua mdomo,..shauri lako…’akasema na kutabasamu,
na kuna kitu nilikiona kwenye macho ya huyu mzee, ana kitu kama makengeza,
lakini sio makengeza..ukiyaangalia unahisi mwili kusisimuka, lakini kwa vile
nina asili ya kutokuogopa niliona kama ya kawaida.
‘Kwaheri…’akasema
na kuondoka kwa mwendo wa haraka huku kainamisha kichwa chini , kama vile
hataki mtu amtambe.
***********
‘Docta,
docta,..docta….’nikawa sasa natamka hivyo, mara kadhaa, huku nikimuangalia yule
mlinzi,..alikuwa sasa anakoroma, nikajua sasa kalala..wakati huo namuwaza docta
kwa kitendo kile lichokifanya …ilikuwa kama ananitelekeza, japokuwa awali
alionyesha kunijali sana…
Kwanza
vitendo vya huyu mtu nashindwa kumuelewa…ana mambo ya siri siri mengi… , sasa naanza
kuingiwa na mashaka,…sio kwamba namuwaza hivyo kutokana na maneno ya huyu mzee,
hapana, …
Lakini
kwa jinsi alivyoweza kufanya mambo kama askari, basi hata kama ni docta, lakini
atakuwa ni askari, ungemuona alivyofanya pale…alivyoweza kukwepa zile risasi,
na kuniokoa na mimi..mmh, sawa..yawezekana ni hawa maaskari kanzu..'niliwazia
hivyo,
‘Kwa
jinsi alivyofanya pale alipokuja kuchukua vile vifaa, bastola na ule ufunguo wa
ajabu,…kweli sio mtu wa kawaida, sio raia yule..atakuwa ni njagu…’nikasema kwa
suti ndogo.
Ile sauti ya amri…lala chini, ..geuka..inuka,
geuka kule..fanya hivi… hivi..nk….zile n amri za kijeshi,….’ kiukweli aliokoa
maisha yangu…lakini sasa baada ya kuona askari wanakuja, ambao badae mimi
niligundua kuwa sio askari hasa, na kama ni askari hasa basi ndio hao
wanaotumiwa na hao watu..pale akaniacha njia panda..
‘Aliniacha njia panda ndio…’
Na
kwa jinsi alivyoniacha….akatahamini vile vitu zaidi ya uhai wangu, vile vitu
vina thamani gani.eeh,…’ ni kwanini vile vifaa vilipofika mikononi mwake,
vikawa ni muhimu sana kuliko maisha yangu.’
Eeh…akaniacha mikononi mwa adui, ili eti akavifiche hivyo vitu…hapa kuna
jambo sijalijua, hapa kuna ajenda ya siri, na hapa naungana na mzee, kuwa docta
ana jambo,…’nikawaza hivyo na kutikisa kichwa kukubaliana na hilo wazo.
Hapo na mimi nikaingiwa na mawazo ya kufanya
utafiti wangu, …docta alinituma kwa njia zake nikafanikiwa, …na ndio nikaweza
kumfunga yule mtu kamba..na sijui huyo mtu kama bado yupo pale, au la,..huyu
mtu anaweza akawa ndio kiongozi wa hili kundi, na kama ndio yeye, kiongozi basi, atakuwa anafahamu….kuhusu….mmh,
..kwanza
‘Mpenzi
wa facebook…’ huyo kwangu ndio muhimu, hilo la mzee kuwa huyo binti wa mzee
yupo hai,..haliniingi akilini,..hivi
kweli yawezekana huyo mpenzi wa facebook, akawa huyo binti..hapana,
..hapana…
‘Mpenzi
wa facebook….’ Hapo nikatamka kwa sauti kidogo, na nilipogundua nimetamka hivyo
nikainua kichwa kumuangalia yule askari..alikuwa sasa kalala, …sina shakana
hilo, sasa nifanyeje..nikajiuliza
‘Lazima
niende kule kwa yule mtu…nina uhakika yeye atanisaidia kumpata mpenzi wangu wa
facebook….kama mzee anasema kweli basi nitaweza kumuokoa huyo mpenzi wa
facebook…yes kumuoko,…, kutoka kwa hawa jamaa,…haina haja hata ya kumtumia huyo
mzee, nitalifanya mimi mwenyewe.. ..nikishindwa , eeh, nikishindwa hapo, ndio..nitamtafuta
huyo mzee..
‘Na
kuhusu docta…?’ nikajiuliza
‘Huyo
nitakuja kupambana naye baadae, najua nitagundua ukweli wake, kama yeye ni
askari,au ana ajenda gani, kuhusu hivyo vitu, sawa…nilimsikia yule kiongozi
wakati anapambana na yule mama, akisema kuwa hivyo vitu ni vya thamani sana..vina
siri kubwa sana ndani yake…, lakini ..aah, hata sijaelewa, nitaelewa nikikutana
na docta, lakini sio sasa, sasa hivi, nafanya mambo kivyavyangu..simuamini mtu
tena..’nikawaza hivyo.
Nikasimama na kuanza kutembea..nikitaka kutoka nje…
'Wewe
unataka kwenda wapi...’ nikagwaya kumbe yule askari alikuwa makini, nikasema;
‘Nataka
kufika nyumbani kwangu mara moja..mimi sio mfungwa, najua mnatuweka hapa kwa
ajili ya usalama wetu, lakini kuna mambo binafsi, natakiwa kuyatatua,…usiwe na
shaka na mimi, nitakwenda na kurudi mara moja..’nikasema
‘Huwezi
kuondoka hapa, hii ni kwa usalama wenu..na ukiondoka hapa nitakuwa nimevunja
amri…unasikia, kama kuna kitu, ukisema atatafutwa mtu wa kukifuatilia,
unasikia…’akasema
Sikutaka kubishana naye, nikarudi na kujifanya
nimelala, na yule askari alipoona nimelala na yeye akaendelea kulala…nikachukua
mto wangu nikawekeza kama mtu amelala,…hapo sasa, sikumpa muda..taratibu
nikanyemelea,…. taratibu, nikatoka mle ndani,..
Nilipotoka
nje tu, huyo nikajua usafiri wa haraka ni hizi bajaji zetu,..nikaipata
moja..nikamwambia jamaa naenda wapi, na yeye bila kuuliza zaidi akawasha
kibajaji chake mbio mbio tukaelekea huko, nilipomuelekeza…
'Nitampata tu....mpenzi wangu wa
facebook...'nikasema huku bajaji ikikari eneo hilo la makaburini…sikutaka afike
karibu sana na eneo hilo nilijua lazima kutakuwa na walinzi au watu wanalinda,
au kuchunguza eneo hilo…na bahati nzuri nikaona watu wanazika..na mimi huyo
nikajifanya ni mmoja wao..
Nilishiriki
kwenye hayo mazishi, nikasikia watu wakiongea mengi kuhusu eneo hilo, na
mmojawapo akasema;
‘Nasikia
humu kuna kundi limezuka, watu hao mkizika wanakuja kuchimbua makaburi,
wanachukua sehemu ya miili ya watu…’akasema mmojawapo
‘Hao
sasa ni wanga,…’akasema mwingine
‘Ndio
hivyo,lakini hao sio wanga kama hao ninaowafahamu mimi, hao wanachukua vifaa
wanauza…nasikia viungo vina bei kweli..’akasema
‘Huo
ni uwongo, mtu keshakufa, damu haifanyi kazi, …labda useme ni wachawi wanatumia
kwa mambo yao ya kichawi, na wachawi wanakula nyama za watu..mungu anawajua, na
kifo chao kinakuwa kibaya we acha tu.…’akasema
Kukawa
na malumbano kidogo, na kiongozi wa dini aliyekuwa akisimamia mazishi hayo
akaanza kuongea na moja wapo ya maongezi yake akaliongelea hilo, na mwisho
akasema;
‘Wapo
watu wana imani potofu, wamejiingiza kwenye nguvu za giza, niwaambie kitu ,
nguvu hizo za giza kiongozi wake ni shetani, na shetani ni adui wa mungu,
ukijiingiz huko ina maana umekuwa mfuasi wa shetani, umemuhalifu mwenyezimungu,
mwenyezimungu hazuriki na hilo,…mwisho wako utafika utafika mikononi mwake.
Kwahiyo
basi, sisi kama wanadamu tukumbuke kuwa duniani hapa ni mapito tu mwisho wake
ni hapa, wangapi walitamani wawe hai, walikuwa na malengo mengi tu, wakajenga,
wakawa matajiri, leo hii wapo wapi…angalia leo hii tumemzika mwenzetu,
hajaumwa,
…ghafla tu , kafariki,… kesho au hata sasa hivi inawezekana ukawa ni wewe au
mimi….sasa umejiaandaje kwa safari, hii….achanane na imani hizo za
kishirikina,..’ akaendelea kuongea na mimi nikaona nichomoke hapo kiaina maana
watu walishaanza kuondoka’.
Hilo
kaburi la yule binti ambalo sasa nimegundua ni kaburi kwa juu, kumbe kwa ndani
sio kaburi…lilikuwa limejificha kwenye miti…kwahiyo nilijifanya kama nakojoa,
nikafika eneo hilo, na nikaanza kazi ya kuusukuma ile sehemu ya juu, haikuwa
kazi rahisi, …na nikajitahidi sana baadae ikaanza kusogea, kidogo kidogo,
kukaanza kuwa na uwazi..na ilipofikia sehemu ya kuweza kuingia, ..
‘Umekuja..nilijua
utakuja, …’sauti iilishitua kutoka nyuma, na sijui ilikuwaje nilihis kama mwili
unaisha nguvu.
NB;
Ni nani huyo
WAZO LA LEO: Sasa hivi watu
wangi wametekwa na imani za kishirikina, …kila kikitokea kitu, kuna mkono wa
mtu, ni kwa vile ilikuwa hivi na hivi…na hata matajiri wengi wanatumia mbinu
hizo kwenye utajiri wao..imefikia hatua watu wanadanganyika kuwa viungo vya
wanadamu wenzao huleta utajiri, au wanajiunga na makundi yenye mlengo wa
kishetani, kwa kutoa makafara ya damu za watu...
Jamani
huo ni ushirikina na hizo ni njia za ibilisi, ukijiingiza huko umekuwa matumwa
wa ibilisi, shetani aliyelaaniwa, na mwisho wa yote ni kuenda motoni. Jiulize
waliokuwa magwiji wa mambo hayo wameishi milele,…haipo hiyo, kila mtu siku yake
itafika,..na huko, zawadi, kitu cha kukusaidia ni matendo yako mema, na hayo
mambo ya shetani, yatakuangamiza na adhabu yako itaanzia hapa hapa duniani.
TUMUOMBE MUNGU, ATUJALI TUWE NA IMANI THABITI YA KUMUABUDU YEYE, NA
SIVINGINEVYO..Aamin.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment