Docta aliyakuwa akishuhudia hayo yote, akajua
keshampoteza mpelelezi, alijilaumu kwanini hakumtahdharisha kuhusu huyo mtu ,
na ilitakiwa ahakikishe kuwa silaha, hiyo ipo mbali na huyo mtu, kama mpelelezi
angelikuwa na utashi wake mwenyewe angelijua jinsi gani ya kufanya, lakini kwa
hali ile, mmh…akajiona kafanya kosa na anahitajika kuwajibika kwa hilo…, kwa
haraka akawapigia simu askar waliokuwepo humo, ili waingie ndani waone kama
wataweza kumuokoa huyo mtu.
‘Mpelelezi ni mtu muhimu sana…’akajisemea.
Na wakati anafanya hivyo, mara mitambo ikagoma, kukawa
na ujumbe kuwa kuna mtafaruku wa mitambo…muingiliano wa mitambo, na sasa
imefanya mtandao mzima kushindwa kuendelea.
Alimpigia jamaa yake, na jamaa yake akasema,
inahitajia muda wa kusubiria, na kama hao jamaa wameshaanza ‘ku-reboot,’…basi muhimu ni kuhakikisha
hawawezi kuendelea kabla mtandao huo haujaanza tena kufanya kazi.
‘Lakini…mtandao wao umeshazimwa…haupo hewani tena…’akasema
docta akiongea na huyo jamaa
‘Umezimwa ndio,… lakini bado wana vifaa vinavyoweza
kutumika sehemu nyingine, wana simu zenye huo mtandao, wanaweza wakawa na
visaidizi vya nje vya komputa, (external
drive)....na mbaya zaidi ni kama wana ‘kifungio’ cha huo mtandao…’akaambiwa,
na docta hakutaka kumuambia kuhusu hiyo ‘key’ aliyo nayo huyo kiongozi wao.
‘Oh, sasa nifanyeje mpaka sasa, kama vile virusi
vilishindwa kuharibu kila kitu..?’ akauliza
‘Subiri, na mimi nione kama kuna njia
mbadala..’akaambiwa, na kwa muda huo ndio akawasiliana na mkuu kuona kama
wanaweza kwenda kumuokoa mpelelezi, kama bado yupo hai.
‘Mkuu fanya juhudi , kadri uwezavyo, ukamuokoe
mpelelezi, ….’akasema docta.
'Tatizo kama
tulivyopanga awali, watu wakiingia huko ndani kwa wakati huu, wataleta vurumai,
ukumbuke jengo hilo ni kubwa,…na lina ofisi nyingi,..kuacha hiyo ofisi yao
wanayotumia kwa biashara zao na mambo yao, na sisi tunataka tufanye kazi bila
kuingilia makazi ya watu wengine,…na nia hasa ni kuhakikisha ushahidi wote
unapatikana....'akasema mkuu huyo msaidizi.
'Mpelelezi
anahitajia huduma ya haraka,… sijui kama mtamkuta akiwa hai,..tatizo mtambo
umezima siwezi kumuona tena..'akasema docta.
'Ngoja tuone la
kufanya, maana hata yule kiongozi wao katutoroka, sijui hawa maaskari wana
nini, niliwaambia kabisa wahakikishe huyo mtu hawatoki..na nasikio alikuwa na
silaha iliyokuwa inapiga risasi nyingi, risasi..zinakuwa kama zinamuandama mtu
aliyelengwa.siwaamini…’akasema
‘Oh, kumbe ameshaipata hiyo silaha, sasa hilo ni
balaa…’akasema docta.
‘Silaha gani…?’ akauliza mkuu
‘Na unajua hata msaidizi wako kapoteza fahamu, na hao
mabinti halikadhalika…na hata mama yao, tulijua huyo mama amekufa, kumbe bado
yupo hai amekuwa kama kachanganyikiwa…na vyema alipopoteza fahamu, na mmbo hayo
yametokea kwa mara moja,…imekuwa ni ghafla sana kwetu…’akasema
'Hilo
nalifahamu sana..ni katika hali ya kuwarejeshea kumbukumbu zao, nilishaondoa
uchafu waliopandikiziwa, uchafu ule ulikuwa kama mzigo mwilini mwao, na
ulipoonadoka, ni lazima wadondoke, na kupoteza fahamu, na kilichokuwa kimebakia
ni kuwarejeshea kumbukumbu zao na utashi wao wa kawaida, ....’akasema docta.
'Kwahiyo huwezi kuwaona kabisa….?’ Akauliza mkuu.
'Nakuambia mtambo mzima umegoma…nahisi yule mtu wao
alipofyatua ile bastola, akitaka kumuua mpelelezi, risasi iligusa ile komputa
kubwa inayoongoza huo mtambo…au pia ni kutokana na muingiliano wakati wanataka
kurejesha mawasiliano yao, na wakati huo, mimi nautumia..umona hapo..ni
shiida..’akasema docta.
'Sasa tutafanyaje…?’ akauliza mkuu, alionekana kuongea
na watu wengine kabla hajasikilizana na docta.
'Muhimu ten asana ni kupata huo ufunguo wa ajabu….na
hiyo bastola…hivyo ni vitu hatari sana vikiangukia mikononi mwa hao
watu…’akasema docta
‘Bastola…una maana hiyo bastola, iliyokuwa inatoa
risasi kiajabu…’akauliza
‘Hiyo ni hatari sana, inatafutwa sana….na muhimu
ipatikane, vinginevyo,..nyote nyie mtauliwa….’akasema docta
‘Ok…askari wamesambaa eneo lote hawezi kutoka humo…’akasema
huyo mkuu.
'Je hao askari huko n- nje,....unawaamini, sawa sawa…?’
akaulizwa
'Sina shaka na hilo…wapo vijana wangu hawababaishwi na
pesa, wanajua ni nini wanachokifanya…..’akasema huyo mkuu.
'Nina mashaka kuwa huyo kiongozi anaweza kutoka nje na
asijulikane kuwa ni yeye
'Kwanini….?’ Akauliza docta
'Ujanja wao wa kujibadili sura….wanavyaa ngozi,…kama
ulivyoona ile ya huyo kiongozi, nina mashaka, bado ana ngozi nyingine mwilini,…huyo
jamaa ni hatari sana , mwenyewe anajiita shetani wa kibinadamu,.., ‘akatulia.
‘Sasa muhimu cha kufanya kama hatujachelewa,
hakikisheni hakuna mtu yoyote, wa jinsia yoyote, ambaye ataruhusiwa nje mtu
yoyote, bila wewe kumtambua..na huko uwanja wa ndege, …nilikuambia hilo,
wahakikishe kuona ni nani na nani kaingia leo,….’akasema docta.
‘Ok, hilo nimeshawatuma vijana wangu…hakuna mtu yoyote
kiongozi au watu wetu waliokuja na ndege leo mpaka muda huu….’akasema mkuu.
‘Safi kabisa……tutaona uwaongo wao….’akasema docta.
‘Mimi hapo sijakuelewa….’akasema mkuu.
‘Utakuja kuelewa baadae…’akasema docta..
‘Mimi bado najaribu kuwasiliana na jamaa yangu wa huko
ulaya, tuona kama nitaweza kuwaokoa hawa watu…’akasema kwani mtu wake wa huko
nje alianza kumpigia..lakini siku ikakatika.
'Kuwaokoa una maana gani tena, si umesema umeshaondoa
uchafu waliokuwa wamepandikiziwa hao watu au sio…?’ akaulizwa
'Hawa watu ni mashetani, waliweza kuwawekeza hao watu
walio wataka kwenye mitandao yao,…inakuwa kama unavyowekeza jambo kwenye
komputa,..hii ni kitu kigeni sana..hakielezeki…, katika moja ya majaribio yangu, na tafiti zangu, ilikuwa
hiyo..kuona kama kweli jambo kama hilo linawezekanaje…, je yawezekana nguvu za
giza ukaweza kuziingiza kwenye mitandao…sasa hawa jamaa wamejaribu,….’akasema
docta
'Nakumbuka uliwahi kuniambia kitu kama hicho mimi
mpaka sasa siwezi kukubaliana na hilo,haiwezi kuingia akilini,..na hayo ya
imani za giza, utayawekaje kisheria,…ndio maana mimi nahangaikia kupata
ushahidi unaoshikika, sio mambo hayo ya kiimani imani tu…’akasema mkuu.
'Unajua mkuu siku zote nilikuwa nawatafuta hawa watu,
hata nikiwa huko mikoani, nilijua naweza kujifunza kitu kwao, lakini nimegundua
kuwa hao sio watu, ni mashetani, nilijua wana kitivo cha wataalamu, wanaofanyia
kazi hiyo uchunguzi, kama kweli nguvu za giza unaweza kuziingiza kwenye mtandao
ni kweli wana wataalamu humo wanaojua komputa vizuri,…lakin mtu wao, huyo hana
jema, zaidi anataka kuiangamiza dunia…..
'Lakini ni watu gani hao…inaonekana kama unawafahamu
kabla,.. ni huyo huyo…kiongozi wao, na huyo mtaalamu na hao tuliowakamata, na
huyo kiongozi wao ni nani hasa, ..mwanzoni nilimuona,…anafanana kama..eeh, hebu
subiri…’akasema alikuwa akiwasiliana na watu wake. Akawa anatoa maagizo na
baadae akaendelea na docta;
‘Oh, …docta, wamefanikiwa kuingia ndani…’akasema mara
tena akawa anawasiliana na watu wake..
‘Ok, ok….sasa..hakikisha wote wanakamatwa, na
mchukueni mpelelezi kwa haraka afikishwe hospitalini…unasema bado yupo
hai…’akatulia.
‘Oh….ok, mbebeni hivyo hivyo…fanyeni haraka, na huyo
mtu wao ambaye alikuwa humo, yeye ndio bingwa wao,…mnasema nini, .. hamjampata??
,…haonekanani kwanini,… katokea wapi…mtafuteni haraka,….’akasema.
‘Nani, Binti??!….ok….nani kasema alikuwepo binti…wapo
wengi, na..huyo ni nani, ..binti, ….? Sasa kaenda wapi,…alikuwa kwenye chumba
peke yake, ni nani huyo…kwahiyo, …hayupo, kaenda wapi…mtafuteni sasa, …..hao wafungeni
wote haraka …’kwa vile huyo mkuu alikuwa hajazima simu akiwasiliana na docta, docta alikuwa akisikializa jinsi amri
zinavyotolewa huko upande wa pili.
Baadae mkuu akarudi hewani kwa docta, sasa akawa ndio …akauliza;
‘Kuna binti wanasema alikuwa kwenye chumba chake peke
yake, …wengine walikuwa sehemu tofauti, ..najiuliza tena na tena, hawa mabinti wa
nini, na kwanini walikuwa wamefungiwa huko ndani..na hawajulikani ni mabinti wa
watu gani,…je unaweza kufahamu walikuwa humo kwa kazi gani, maana ni warembo
kweli…?’
‘Hahaha…hao ndio chambo kwenye mitandao….wanatumika
kuwateka watu…kama nilivyokuambia awali, picha ya mrembo kama huyo ikiwekwa
kwenye mtando, kimvuto, mtu atavutika nayo,..na kwa jinsi atakavyomuangalia kwa
matamanio, basi akili yake hutekwa na hao mashetani…ni ujanja ujanja fulani wa
kuteka akili za watu, na hao watu wanakuwa watumwa wa shetani…’akasema docta
‘Hata sielewi…’akasema mkuu
‘Unasemaje kuhusu huyo kiongozi wao tuliyempata,..japokuwa
katutoroka…, nina uhakika tutamkamata tu….’akasema huyo mkuu.
‘Ni mpaka mumkamate…huyo sio mara ya kwanza kuingia
humu nchini..alishawahi kuja akafanya mambo ya kutisha, baadae akatoweka hivyo
hivyo…na nahsi ndio huyo huyo,karudi tena…’akasema docta
' Inavyoonekana, huyo wanayemuita kwa jina la mkuu,
sio huyo kiongozi tuliyempata hapo kwa hivi sasa au sio,.?’ Akauliza mkuu.
‘Sina uhakika na hilo, yawezekana akawa ndio huyo au
mtu mwingine kapewa hiyo kazi, kwa kutumiwa, ndio maana anajibadili
sura..’akasema docta.
‘Kwa maana hiyo,….huyo mkuu yupo mahali, hatujaweza
kumpata…?’ akauliza na docta akasema;.
‘Vyovyote iwavyo, bado kuna mtu mwingine nyuma ya pazia, huyu
kiongozi inawezekana kweli akawa anatumika tu,…unajua hawa watu ni wajanja
sana, kiongozi wao analindwa na kufichwa sana, kama mchwa au nyuki
wanavyomlinda malikia, ….’akasema docta.
‘Tutampata tu…hata afichwe vipi…’akasema mkuu.
‘Kwa kutumia nguvu zenu, itachukua muda, mnaweza
kuwakamata watu wengine kabisa na huyo mtu akatoweka tena,…sina uhakika kama
ndio huyo …inahitajia muda kumgundua, lakini ngoja tuone..mtandao utasema….’akasema
docta.
‘Je mpelelezi hawezi kutusaidia kwa hili…naona kama
alishaweza kuingia kwenye anga zao…sijui kwanini hakupenda kunielezea jambo
hili mapema…’akasema mkuu.
‘Sababu ndio hizo, …walishaiweka familia yake reheni…na
kwasasa mpelelezi hawezi kutusaidia kitu, kupona kwake kutachukua muda…kama
bado yupo hai…’akasema docta.
‘Mhh…kwahiyo una maana kuwa ni kweli mpelelezi alishaingizwa ndani ya kundi hili,
kwa lazima fulani, sio kwa hiari, na…nimeshaanza kukuelewa, lakini kwanini
wamchukue yeye, kwanini…na kwanini mkuu wangu wa kituo, hakutaka kuniweka wazi
kuhusu hili, nahisi hapa kuna jambo, unasemaje docta..?’ akauliza
‘Ndio hivyo,…mpelelezi takuwa kashindikizwa kwa
kupitia familia yake,…na huyo binti yake alitakiwa sana…wana maana yao,
kiukweli huyo binti kaponea tundu la sindano…na vipi hali yake, anaendeleaje
maana siwaoni tena huko…?’ akauliza docta.
‘Huyo binti hajaweza kuongea mpaka sasa hivi…kapagawa,
yaani ukimuona ni kama zezeta fulani hivi, katoa macho tu.….hajijui…’akasema
mkuu.
‘Unajua na yeye pia ni miongoni mwa watu
waliologezewa, kulogezewa hapa nina maana , watu hao walipandikiziwa ushetani
fulani kichwa ni mwao..lakini yeye, baadae waliyatoa,…waliona yeye, sio lengo
la makafara yao, ila baadae walipokosa mtu, wakaona hata yeye anafaa, anaweza kutumika
vile vile.., kwa masharti yao…kwanza ana damu ya hizo familia japo kwa mbali,
pili binti huyo bado ni mbichi, kwa mambo yao ya kishetani,…’ docta akakatizwa .
‘Ana damu yao kwa vipi..?’ akauliza lakini kabla docta
hajajibu mara huyo mkuu akasema;
‘Docta,…. mpelelezi keshatolewa, katapaa damu, docta
anasema ni mpaka wafike hospitalini waone kama wanaweza kumuokoa, hivi sasa anapelekwa hospitalini, kapoteza fahamu…’akasema
huyo mkuu.
‘Ina maana ile risasi imempata sehemu gani…?’ akauliza
docta.
‘Docta anasema imepitia sehemu ya tumbo, ..humo
imekwaruza, lakini sehemu ya kwapani…ndio kuna tatizo, maana wanasema risasi moja imetoboa meza, na
kuharibu kabisa keyboard ya komputa,
na nyingine ndio iliyompata mpelelezi..…, ngoja afikishwe huko hospitalini ,
tutajua kama ni mtu wa kupona au ndio basi tena…’akasema mkuu.
‘Oh,…sijui tufanyeje,…maana kama watawahi kurejesha
mambo yao, kabla mimi sijaweza kuingia huko, inaweza kuwa balaa kwa hawa watu, hao
watu wanaweza wakawa na matatizo ya akili, maisha yao yote….hata sijui
itakuwaje…’akasema docta.
‘Jitahidi docta, hilo lipo mikononi mwako..na mungu
atakusaidia…’akasema mkuu.
‘Ni kweli, …lakini kwa hivi sasa, siwezi kusema lolote,
nashindwa hata kuamini, muda umepita sana, na huyu jamaa anapiga simu, kila
nikipokea inakata…kuna tatizo mahali…ngoja nitoke humu ofisini..’akasema docta.
‘Docta usiondoke humo….hiyo amri ya polisi…’akasema
mkuu huyo.
‘Hahaha, sasa hivi sifuati amri yoyote, nafuata amri
ya mungu peke yake, nikiwafuata nyie, hawa watu, msaidizi wangu, wale mabinti,
mama yao… watakuwa kwenye hatari kubwa, na mwisho wa siku nitakuja kulaumiwa
mimi, kwani huko mumefikia wapi…?’ akauliza
‘Mhh..,hata siamini eti wanasema huyo jamaa katoweka
kama alivyotoweka huyo kiongozi wao, hawajui alipitia wapi… na wanahisi kuna
sehemu wamejificha, ssasa kajificha wapi, ndio haijulikani, wametafuta kila
sehemu hakuna mtu kama huyo,….na mawasiliano ya kunasa matukio humo ndani
ilishazimwa,..’akasema.
‘Najua atakachokifanya…’akasema docta
‘Kuwa hata yeye alikuwa akitumia sura bandia…’akasema
mkuu
‘Ahaahaha…, ndivo hivyo, wameona ndio njia rahisi ya
kuficha maovu yao, lakini hiyo ni danganya toto,…wewe subiria mtandao ufanye
kazi yake, ninachoombea kwa sasa ni wawili hao, wasikutane kwa sasa…’akasema.
‘Kiongozi na huyu mtaalamu wao…?’
‘Ndio, hao pia, lakini nazungumzia hawa wapenzi
wawili,…mkuu endelea na kazi,…..hakikisha njia zote zimezuiliwa …uwe makini
kwani kuna njia za chini kwa chini, …zilijifunga muda ule,..kabla mtandao
haujajifunga, sasa sijui kwa hivi sasa na kwa vile huyo jamaa ana huo ufungua
wa ajabu, anaweza kufungua na kupita…’akasema docta.
‘Mtandao bado…?’ akauliza mkuu.
‘Oh…mbona hivi….ngoja hebu suria niongee na huyu mtu
wangu kwanza, naona kama mambo yanazidi kuharibika,…’akasema docta, na mkuu
akawa naye anaongea na watu wake.
*************
Docta na mkuu walipopigiana simu tena, mkuu akawa na
maswali kwa docta, akauliza;
‘Hebu niambie, kuhusu hiyo silaha, maana imekuwa ni
gumzo kwa askari wangu, hiyo silaha imatokea wapi..?’ akauliza mkuu.
‘Historia yake ni ndefu kidogo, ..silaha hiyo, kiatu,
vilikuwa ni vifaa vya watawala wa enzi hizo, huko uzunguni, lakini inasadikiwa
kuwa silaha hiyo iliundwa huku kwetu, na ikapelekwa huko, kipindi mtawala wa
enzi hizo, aliporotoka,….na kwenda kuishi huko ughaibuni.
‘Kwanini alitoroka..?’ akauliza mkuu.
‘Alitaka kuimiliki hiyo silaha na kiatu ,na alitaka
akajiimarishe huko akirudi, anakuja kutwaa madaraka, na kutawala sehemu kubwa
ya nchi, lakini haikutokea hivyo, akapatwa na umauti akiwa huko, na vitu hivyo
vikabakia kwa jemedari mmoja wa vita..
Jemedari huyo, akawa anavimiliki hivyo vitu, lakini
hakujua undani wake, akawa anavitumia tu…lakini vikaanza kumletea madhara,… na
alipoona anataka kufa, akaacha urithi kwa familia yake kuwa vifaa hivyo vitafutiwe
namna ya kuviondoa kwenye familia yao…akawaarifu kuwa vifaa hivyo ni janga
kwenye familia hiyo..
‘Kijana wake,..msomi, sasa… alikuwa kiongozi fulani wa kijeshi,
kijana huyo hakupendelea mambo hayo ya urithi nk…akataka kuhakikisha mambo hayo ya kizamani yote
anayaondoa kwenye hiyo familia,..na enzi hiyo ndio, ambayo, mzee alikwenda huko
kwenye mafunzo, na kushiriki kwenye jeshi la umoja wa mataifa.
Mzee akiwa jeshini alikuwa kweli bingwa wa silaha,
shabaha, na mtaalamu wa kuunda zana za kivita kwa haraka sana… Wenzetu wazungu
walimpenda sana, kuna kipindi mzee aliweza kushirikiana na hao wazungu, nia yao
wao ni kuiba ujuzi wake.
Mzee hakupenda
kuajiriwa huko ulaya, kama angelikubali tu angelikuwa mtu mwingine kwa hivi
sasa.., unajua tena mambo ya zamani, wazee wake walimkatalia kabisa kufanya
kazi huko. …
‘Mimi sijaelewa, kwanini..ok...., umesema alipewa viatu na
bunduki kama zawadi, sasa inaingiliaje kwenye matatizo yote haya…’akauliza mkuu.
‘Labda nianzia
hivi,…kuvipata hivyo viatu, na bunduki, sio jambo la bahati …ilipangwa kuwa
atakuja mtu,,,,mtu hayo atafnya jambo kubwa sana,.. yalisemwa na huyo aliyeviacha hivyo vitu, alikuwa na karama
fulani za utabiri wa baadae.. akawaelezea familia yake hivyo lakini hakuna aliyetilia maanani, lakini lililopangwa litokee , litatokea tu, …maana kama nilivyosema awali,
vitu hivyo asili yake ni afrika..unaonaeeh…’akasema
‘Wanavyodai, mizumu ya afrika ilivihitajia vifaa hivyo
virejeshwe huku, hapo hakuna mungu wanachojua wao ni mizimu, huku afrika, ilitokea muda familia hiyo inayohitajia hivyo vitu ikapatwa na matatizo, ikaambiwa kuna vitu vinahitajiaka virejeshwe, familia hii haikujua, na ikapuuza, maisha yakaenda mbele..…ni mambo ya imani wanajua wazee wetu zaidi...’akasema docta
‘Sasa ukichunguza familia ya mke wa huyu mzee wetu
huku…, ukarudi kinyume nyume, utakutana na hiyo familia, vifaa hivyo
vilivyotokea,…familia ya mke wa mzee, huko nyuma ilikuwa ya machifu, viongozi
watawala..na utawala wao ulikuwa wa nguvu sana, na mambo ya giza giza, si
unajua mambo ya kizamani…’ akatulia docta.
'Lakini kuna mgongani kati ya familia mbili,..rejea maelezo yangu, kuna huyo alitoroka na vitu hivyo akaenda huko nje, na kuna familia ilibakia hapa, ambayo ndio ya mke wa mzee, na familia hiyo nyingine ina uhusiano na huyo aliyetoroka na hivyo vitu, ambayo lidai kuwa ndiyo ilitakiwa iwe watawala enzi hizo..kizazi kikazaa chuki hizo, ..na chuki hizo, za tamaa, sisi ni sisi zimeendelea hadi leo....
'Eneo alilonunua mzee..lilikuwa mali ya familia hizi..lilikuwa kubwa tu, lakini likaja kugawiwa baadae utawala ulivyobadilika kutoka wa kikabila na hadi kuwa wa kitaifa,..lakini hulka na tabia bado zipo, kizalia, cha hapa kwangu , hapa kwetu bado zipo..eneo lilobakia lilikuwa na mgogoro mkuba huko nyuma...lakini haya yapo chini kwa chini...
'Sasa basi...kuna huyu mtu alitoweka, alikwenda wapi....swalii hilo jibu lake ukilipata unaweza kuhitimisha hii kesi, na mengine yote yanazunguka, mbinu zinatafutwa, kiini chake kimejificha,...hulka, tabia, vizalia, vinazua mambo, ..ajenda imejificha, na sio rahisi , hata kwa hao wanaohangaika kujua sababu ilikuwa ni nini hasa, shetani anachochea tu......sasa ukiwaelezea watu hayo yote, wanakuja kukuuliza kwa ushahidi gani, na huyu mtu ni nani, mbona havieleweki.....ushahidi ni hivyo vifaa...ni nani sasa..ndio tunamtafuta...tukimaliza hili kesi imekwisha, ....'akasema docta
'Mhh...'akaguna hivyo tu mkuu, aliona ni mambo mengi juu ya mambo ambayo hayawezi kumsaidia kitu.
'Sasa niakuambie kitu...kuna kitu kilikuaj kugunduliwa baadae..na mzawa mmoja,...wa huyo mtu aliyekimbilia huko,...ufunguo wa mitandao...huyu mtu alikuwa na miujiza yake...akawaweza kugundua mambo mengi tu...ila alikuwa mbinafsi..yaani hapendi mambo yake yajulikane, na watu wengine akafanya mambo yake na mashetani, hadi akapata ufunguo...ni asili fulani huwezi kuijua, ufungua huo awali ulikuwa na namba tatu tu..sita sita sita...au tisa tisa tisa....
'Una maana gani....si ndio hayo wanazungumza watu...?' akauliza mkuu
'Hizo namba alizitumia huyo mtu kuwasiliana na mashetani wake..na alipokufa, ufunguo huo ukabakia kwenye hazina yake,..baadae watu wakagundua kuwa ufungua huo unaweza kutumiwa kwenye kitu chochote...ukitaka kufungua mtandoa,..milango...ukawa unatumika kuibia ..ulipoingia kwa watu wabaya..huu ukawa unatafutwa sana...
Swali ulifikaje kwa hawa watu huku...hilo mimi sijagundua....ila upo mikononi mwa huyu kiongozi, kama upo kwa huyu kiongozi aliupata wapi....hapoo ukiunganisha mambo unaweza ukapata jambo..lakini kwa ushahidi gani...huyu mtu ni muhimu sana, akipotea matatizo haya yatajirudia tena...'akasema docta.
'Ok, sawa....'mkuu akasema hivyo, aliona muda unakwisha na hajapata hicho anachokihitajia.
‘Swali ilikuwa je vitu hivyo ,vimewezaje kurejea kwenye
hii familia...'akasema docta.
'Ama kwa viatu na bastola, hilo tumalipata..maana ,..kila kitu hutokea kwasababu fulani..kuna tukio lilitokea hadi
vifaa hivyo vikafika mikononi mwa mzee, wakati huo ni kijana, mpiganaji,
mtaalamu..lakini sio kwamba vilihitajika kuwa kwake,..hapana, kwake ilikuwa
kama daraja tu…vilitakiwa vifike kwa familia ya hicho kizazi husika, na wakati huu,
kizazi kilichobakia ni mke wa mzee, na ndugu hawa wengine, ambao hawajijui..na hata huyu mke wa mzee,..hajui hilo mpaka kwa undani wake,.sasa uone
miujuza ya aina yake ilivyotokea.
‘Siku moja mzee huyu, tunatumia jina mzee, japokuwa
kwa muda huo hakuwa mzee,…walikuwa kwenye doria, pamoja na mafunzo, walitakiwa
kutumikia jeshi, kwahiyo walikuwa wametmwa kwenye kisiwa kimoja kulitokea
maasi.
Mzee, na
mwenzake wakawa wanatembea maeneo hayo, hawakujua kuwa sehemu hiyo kulikuwa na
njama za kumteka binti wa tajiri mmoja, ambaye pia ni kiongozi wa polisi wa
huko..maharamia hao walimtaka huyo binti ili awe ni surti la kuachiwa wenzao.
Sasa wakati mzee na mwenzake wanatembea , wakiwa
wawili tu, …mara kukatokea maharamia
hao, walikuwa maharamia kweli, wanateka wasichana, mabinti wadogo,
wanazalilisha…
Binti wa huyo tajiri, kiongozi wa polisi, akiwa na
gari , yeye na mama yake wakapita maeneo ambayo ilikuwa ni mtego wa hao
maharamia,…wawili hawa wakawa wamsimama tu hawana habari, wakiangalia mandhari
ya huko,…mara wakamuona binti, akitokea kwenye gari,…akienda kwenye eneo la
miti, kuna bustani na maua,nia yake kuchuma maua,..
Wakati huyo binti anaelekea huko, mijamaa iliyovaaa sura mbaya ikatokea, wawili
wakamkamata huyo binti, wengine watano, wakavamia gari lao,..mama na watoto
wengine wakawekwa chini ya ulinzi…
Mzee akawaona, ..muda huo walikuwa wawili tu yeye na
mwenzake, japokuwa walikuwa na silaha, lakini kundi hilo lilikuwa ni la watu
wengi wenye silaha….na kutokea kwao ilikuwa ni jambo la haraka sana na kumshika
yule binti wakamuingiza kwenye gari, wakataka sasa kuondoka kwa kasi….mzee na
mwenzako wanaliona hilo tendo, na wao wapo humo kwa ajili ya kulinda…
Yeye ni mtaalamu wa shabaha,….akaishika silaha yake,
gari lile likawa sasa linataka kuondoka, lakini …wanawasubiria wale walimchukua
binti..waje waingie, mzee yeye, akainua silaha yake, akalenga shaba kwa dereva,
…hakumkosa..pega begani…wengine,…mmoja baada ya mwingine aliwalenga mabegani tu…kwa
umabali ule ilihitajia shaba, na kulenga shemu hiyo hiyo tu…
Na mwenzake akawa anawasiliana na wenzo kikosini,…wanafika
pale maharamia hao wote majeruhi…hawajiwezi….ni bahati tu. Bosi huyo wa polisi
kusikia kazi waliyoifanya wawili hao, alifurahi sana…
Baadae ndio wakapewa kazi ya kuhakikisha maharamia hao wote wamekamatwa, au
kutokomezwa kabisa, na mzee akapewa jukumu hilo kama kiongozi wa kikosi hicho,
na kweli kundi hilo likamalizwa na eneo hilo likawa na salama, na ndipo mzee
akapewa zawadi hizo …
Taarifa zilikuja baadae ni kuwa mzee alipewa zawadi
hizo kwasababu ya shabaha, hizo, sababu nyingine zilifichwa kiaina,,…ila ndio
ikawa nafasi ya vifaa hivyo kurudi tena Afrika, na kwa wahusika, lakini hakuna
aliyefahamu hilo kwenye hiyo familia…
Mke wa mzee, akaja kuambiwa kuhusu vifaa hivyo, na
kaka yake wa kambo, kaka yake huyo walikulia pamoja, kama unavyojua familia
zetu, watoto wa baba huyu wanaishi na baba huyu…ikatokea ndugu hawa wawili
kuivana sana, mpaka ilifikiriwa vibaya, lakini wao walijenga urafiki huo kama
ndugu tu.hakukuwa na mengine kama walivyovumisha watu wengine.
Huyu ndugu yake,… alikuja kupotea
kimuijiza,..haijulikani wapi alikwenda, lakini akaja mtu mwingine wanafanana
naye…akajifanya ndio ndugu ..sijui ilikuwa ni sababu gani, wengine wanahisi ni
wapelelezi waliokuja kuvitafuta hivyo vifaa…maana huyo ndugu alikuwa na mambo
yasiyojulikana huku kwetu, …kula vitu vizivyoliwa, na wengine wanasema
walimsikia kuwa anakula hata nyama za watu, akaja kukamatwa na polisi.
Hata hivyo alitoroka polisi na kupotea kabisa….
Miaka ya baadae,..ndio tetesi zikazuka kuwa kumezuka
kundi la kichwi, wanakula watu, wanafanya mambo ya ajabu,…kama unakumbuka eneo
hili kulikuwa hakukaliki kipindi fulani, lakini watu hawafuatilii matukio,
hawakujua kuwa yule yule aliyeondoka ..ndio huyo huyo alirudi na kuanzisha kitu
kama hicho…na baadae walipozidiwa huyo jamaa tena akatoweka.
‘Unataka kusema nini, kuwa huyo jamaa ndio huyu
kiongozi wao…?’ akauliza mkuu.
‘Sina uhakika…lakini kwa vipi huyu mtu awe anakuja,
anakamatwa anatoroka, anapotea, anarudi tena…ni nani huyu …’akasema docta.
‘Sasa ni nani…?’ akauliza mkuu
‘Nitakumalizia historia hiyo baadae maana naona
mitambo kama inataka kuanza, na sitaki kupoteza muda tena…’akasema docta.
‘Sawa…ngoja na mimi nimalizie hii kazi, naona vijana
wangu wameingia ndani na nimepata taarifa kuwa kuna mapigano kidogo huko ndani
ya hayo mapango waliyoyatengeneza…’akasema huyo mkuu.
‘Atakuwa huyo kiongozi wao, kama ana hiyo bastola,
muwe makini sana…’akasema docta.
‘Sawa mimi mwenyewe
naelekea huko, kama utaweza kurejesha hiyo mitambo na kuwa hewani tena uniambie…’akasema
huyo mkuu…na docta hakumjibu maana akili yake ilikuwa kwenye kusoma ujumbe
uliojitokeza kwenye komputa yake, ujumbe uliomfanya mwili ufe ganzi kwa muda…
NB: Ni ujumbe gani tena huo…sehemu hii ilikuwa ndefu,
ina matukio mengi nimejaribu kuifusha hivyo.
WAZO LA
LEO: Tusikate tamaa tunapokutwa na matatizo, maana matatizo hayo
yanaweza kuwa ni namna ya kutututoa
sehemu moja kwenda nyingine, ambayo huenda ikawa ni bora zaidi, au kutuokoa
kwenye hatari,…muhimu ni kujibidisha kutenda mema, na kuyachukulia matatizo yetu
kama mitihani ya maisha, kama ni maradhi, basi huku tunamuomba mungu , huku
tunatumia dawa, huenda maradhi hayo ni namna ya kujenga kinga fulani mwilini
mwetu, mungu mwenyewe anajua zaidi. Tuzidi
kumuomba mungu atusaidie kwenye mitihani, atuongoze kwenye njia njema na
kutufanikishia malengo yetu mema. Aamin…
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment