‘…. Sasa kwanini usiwe na amani,
wakati mtoto keshafikishwa kwa wenyewe…?’ akauliza mama, akimuuliza huyo mdada
aliyekuwa kajifunika usoni.
‘Mama, hivi kweli kuna mzazi anaweza
kumuacha mtoto wake kwa watu baki..sawa tunaweza kusema labda, mtoto kafikiswa
kwa watu ambao unajua ni damu yao,…labda,
lakini je mtoto mchanga kama huyo anawezaje kukaa mbali namama yake..?’ akawa kama anauliza na
mama akamuelewa na kusema;
‘Kiukweli hakuna, lakini mbona
hatukuelewi, wewe ulimuokota ukatimiza wajibu wako au sio….?’akauliza mama
‘Mama mimi…’akasema hivyo halafu
akamgeukia ndugu yake, halafu kwa mashaka akataka kumuangalia dereva, halafu,
akatizama chini, akawa kama anawaza, halafu akainua kichwa na kumuangalia
shemeji wa mtu…kwa haraka akarudisha uso kwa mama, na kusema;
‘Mimi mwenyewe ndiye mama mzazi wa
huyo mtoto…’akasema
‘Nini, mbona hatukuelewi..ina maana
wewe ndiye uliyemzaa huyo mtoto, sasa ilikuwaje uje kumuokota jalalani…?’
akauliza
‘Ni hadithi ndefu sana,…ila nimekaa
na kufikiria sana, na kufikia uamuzi kuwa nimfuate mtoto wangu,…nije nimchukue
mtoto wangu, siwezi tena kuendelea na mpango huo…’akasema
‘Mpango huo, mpango wako na nani…?’
mama akamuuliza huku akimtupia jicho dereva, na dereva alionekana kuwa na
wasiwasi!
‘Kiukweli nimeamua kuja kufichua
siri yote ili moyo wangu uwe na amani,…mama mimi ndiye mama halisi wa mtoto
huyo, na nimekuja kumchukua mwanangu….’akasema na mara akawa anajifunua uso
wake, kubakia wazi, na wote humo ndani wakawa wameshikwa na butwaa..
Tuendelee n kisa chetu
******************.
‘Wewe….’aliyesema hivyo alikuwa dereva
‘Haiwezekani…’akasema Soldier
‘Unafanya nini sasa…’alisema Shemeji
‘Dada….mbona unaharibu tena…’akasema Yaya akimuangalia dada
yake, lakini dada yake akawa anatizama chini, kuonyesha aibu au fadhaa,….na
aliacha muda kidogo ili watu wajirizishe na wanachokiona , na baadaye
akafunika, na kusema;
‘Nimefanya hivi ili watu wajirizishe, na yule ambaye
ananifahamu ajue kuwa mimi ndiye yeye, …na hasa huyo baba mwenye mtoto,..najua
huenda asinitambue tena kutokana na makovu haya, lakini sura inaonekana wazi,
au sio…?’ akamuuliza dada yake.
‘Dada usingelifanya hivyo jamani…’akasema mdogo wake.
‘ Nimeshindwa kuvumilia mdogo wangu, unisamehe kwa hilo, na
najua kwa njia hii tunaweza kufanya hicho kitakachowezekana, mungu atakuwa nasi
daima..’akasema.
‘Dada…’mdogo wake akazidi kulalamika.
‘Unajua mdogo wangu huwezi kujua mapenzi ya mama kwa mtoto mpaka
upitie uzazi, upitie miezi tisa, tena ile ya mateso, unaumwa, unajiuguza huku
mateso ya mimba yanakuandama huku hujui hatima yako ni nini, na bado uzae kwa
shida…....hapana, mimi siwezi kuachana na mtoto wangu kamwe…’akasema.
'Dada, unajua maisha ya familia yetu yalivyo, wewe ndio twakuhitajia ukafanye
kazi ili uweze kwenda kuwasaidia wazazi wetu.., je utafanyaje kazi ukiwa na
mtoto, na wakati baba yake yupo, …’akasema mdogo wake.
‘Baba yake…baba yake gani umesikia kauli zao, hakuna anayekubali
kuwa huyu ni mtoto wao, nimepata taabu muda wote huo namtafuta ….haya mtoto
huyu hapa, baba yake hamkubali…’akasema sasa akimuangalia dereva..
‘Lakini mimi sio baba yake….’akasema dereva, akatahayari.
‘Dada ni vyema kama wanamkataa huyo mtoto tufuate sheria, ili
haki ya mtoto ipatikane, na ….’akasema na dada yake akasema;
‘Sitafanya hivyo kamwe…wangapi wanafanyakazi na watoto
wao...nimeamua hivyo, nitaondoka na
mtoto wangu, nitaishi naye kwa vyovyote iwavyo,..’ akasema na mama akasema
akimuangalia huyo mdada;
‘Lakini wewe binti, hujatuweka wazi ni nani baba wa mtoto, mimi
ni bibi wa mtoto nipo tayari kumlea mjukuu wangu, lakini tupe uhakika, je baba
wa mtoto huyo ni mwanangu au ni dereva, na hata huyo dereva kwa mujibu wa baba
yake, huyo sasa naye ni mwanangu…’akasema mama.
‘Ni kweli mama..kama angelikuwa ni mtoto wangu , kwanini
nimkatae…’akasema dereva, na aliposema hivyo, Shemeji wa mtu akamsogelea huyo
binti na kumshika mkono, huku akisema;
'Sikiliza...kamchukue mtoto wako uondoke naye, na usionekane tena maeneo
haya...'alisema shemeji na kitendo kile kilimfanya Soldier amuangalie kwa
mashaka, ni kwanini huyu mtu anafanya hivyo,…lakini hakusema kitu.
'Nitafanya hivyo lakini ni lazima kwanza niuseme ukweli, ni vyema baba wa mtoto
aufahamu huo ukweli,..na sijui kwanini, lakini…sawa nitawaambi ilivyokuwa, ili hata nikiondoka hapa nisije
kulaumiwa….’akasema.
'Ukweli gani unaoutaka wewe…wameshamuona huyo mtoto au sio, sasa wataka kusema
nini tena, ..unataka kuharibu,… sikiliza kwanza nikuambie,.., unakumbuka
nilivyokuambia,…sitaki turudie kule tena,…kwanza ukumbuke, nilivyokuhangaikia,…
sasa kwanini unafanya hivyo…’akasema shemeji akikatiza katiza maneno kuficha
jambo fulani.
Soldier akawa anamuangalia shemeji yake huku akiwaza;
‘Nahisi huyo mtu kuna jambo na huyu mdada, kwanza huyu mdada ni
mkimbizi, amekujaje huku…ok, naanza kuelewa, inawezakana wana biashara za
pamoja, itabidi niwasiliane na watu wa usalama wa mpakani, ….kwanini
unamshurutisha huyo mwanamke aondoke…’akataka kuingilia kati na kusema;
‘Hebu kidogo hapo.., kuna kitu gani kip kati yako na huyo dada,
nahisi unataka kumuondoa hapa ili asiuseme ukweli, na huo ukweli huenda
unakuhusu, au utakuweka matatani…?’ akauliza Soldier.
‘Haya hayakuhusu wewe,..haya ni yangu na huyu mdada, unasikia,
usitake kuingilia mambo,…hujui katokea wapi huyu…na kwanza nyie mumeletewa
mtoto , damu yenu mnamkutaa, tunapoteza muda hapa bure,…sasa sikiliza huyu dada
anaondoka, na hakuna kudai mtoto tena...si mumemkataa….kila mtu kasikia, baba,
watoto, haya mnataka nini tena…’akasema na kumgeukia huyo mdada.
‘Umeshawaona walivyo hawa watu, hawa watu sio
waungwana…usitegemee huruma hapa..nashangaa kwanini umewaletea huyu mtoto wako,
nilikuambia mimi naweza kumlea, umeona sasa…, hapa hakuna baba wa huyo mtoto,
au nadanganya…umewasikia wenyewe wakikataa, kuwa huyo mtoto sio wa kwao,...umeonaeeeh,
wanachoshindwa kusema ni hivi; huyo mtoto ni mtoto wa haramu..' akasema.
‘Eti nini….?’ Akauliza kwa hasira,…’Sijasikia mtu akitamka maneno hayo, na
hakuna mtu anayeweza kumkataa mtoto wake, mtoto atakuwaje wa haramu, sitaki
kusikia kauli hiyo, na atakayesem hivyo, nitakosana naye, mnasikia,…’akasema
akiwaangalia Dereva na Soldier.
‘Hayo ni yak wake, bwana….’akasema dereva, Soldier yeye alikaa
kimia, akili yake ilikuwa mbali ikijiuliza maswali mengi, na hapo alikuwa
akijaribu kufahamu uhusiano wa Shemeji yake na huyo mdada, alishawawekea alama
ya kuuliza.
‘Hivi mnajua jinsi gani huyo mtoto alipatikana..hakuna anayejua
hilo..hata …sitaki kusikia jamani,…naona niondoke hapa tu…haramu haramu…acha
hizo kauli mbaya,…hata kama kamzaa nje ya ndoa, lakini sio kwa…hata mimi nataka
kuondoka..'akasema.
‘Lakini dada ukiondoka hujaweza kulitatua hili jambo, mwisho wa
siki utaumua mwenyewe..na wazazi wetu je…’akasema mdogo wake, na Shemeji mtu
naye akadakia na kusema;
'Ina maana hukusikia
walivyosema, japokuwa sura ya mtoto na wao huwezi kusingizia, lakini bado
wanamktaa…muhimu ni kuamua moja, …hebu twende, mimi nitakusindikiza…huyo mtoto
yupo wapi,..,'akasema shemeji mtu.
'Ngoja kwanza, je mpo tayari niondoke na huyu mtoto bila kuujua ukweli, je
hakuna baba wa huyu mtoto hapa ndani…?’ akauliza.
‘Baba wa mtoto halisi anayemfahamu ni mama, wewe ndio utuambie
huo ukweli…’akasema mama.
'Kama ingelikuwa mimi, ndio wewe ningeshaondoka na huyo mtoto, na baba yake
asingelimuona tena...'akasema shemeji.
'Kaka kwanini unamsisitiza huyu mdada afanye hivyo, mimi sioni sababu ya yeye
kufanya hivyo...kwanza ni lazima auseme ukweli, unakumbuka nilivyokuambia,
ukweli ndio utanifanya na mimi niweze kuchukua hatua hatua stahiki....
'Dada hatua hiyo haina mjadala, familia hii haikufai, umesikia baba
alichokifanya, kazaa, na mke wa rafiki yake, unakumbuka
alichokufanyia,anakwenda kunywa kwa ajili ya kutaka kuingili mke wa mwanae…
tabia ni hiyo hiyo, utaolewa hapa lakini kumbuka maneno yangu, kamwe hutakuwa
na amani..'akasema.
'Dada hebu tuambie ukweli ulivyo, nakuonea sana huruma, nahisi umepitia maisha
magumu sana, je majeraha hayo yalisababishwa na huyo mwanaume,...je ni huyu mume
alikutenda hivyo...?'akauliza akimnyoshea kidole Soldier.
'Hapana....'akasema huyo mdada kwanza akimuangalia Dereva halafu Soldier.
'Sasa kwanini husemi huo ukweli, ni nani hasa baba wa ukweli wa huyo mtoto...'akasema
mke wa Soldier. Na huyo mdada akamuangalia kwanza Dereva halafu Soldier, halafu
akainama, na machozi yakaanza kumtoka.
‘Sikiliza binti, mimi nawafahamu sana wanaume, ni kweli hawa
wanangu wote wawili wana wake zao, huenda kila mmoja anaogopa akiusema ukweli
kuwa huyo ni mtoto wangu mkewe atakosana naye..lakini hata iweje, ukweli ni
lazima ujulikane, baada ya hapo tutakaa na kuona tutalitatuaje hilo..au sio…?’
akasema mama akimuangalia mke wa Soldier.
‘Mama mimi, naona tusizunguke zunguke, bro,.. hebu kubali yaishe…huyo
mtoto ni wa kwako bro…unaona jinsi gani mnavyofanana….’akasema dereva
akimuangalia Soldier.
'Kwanini unasema hivyo dereva, kama kweli angelikuwa ni mtoto wangu kwanini
mimi nimkatae, wakati hata mke wangu keshampenda, kwanini niwe na roho mbaya
kiasi hicho..mimi nahisi huyo mtoto, ni wako, kwanini umkatae, najua ni kwanini
unafanya hivyo, ni kutokana na tabia zako chafu, za utapeli,..hili sio swala la
kutapeli tena, na nakuahidi tabia yako hiyo nitaimalize,sasa kama hutaki kusema
ukweli, ok, sawa mke wangu na mimi tutamchukua huyo mtoto, tusaidiane na huyo
mdada, hadi hapo ukweli utakapojulikana, na tutaujua tu, ngoje ufike polisi…'akasema
akimuangalia mkewe.
Mkewe akaishia kucheka, akacheka sana, halafu akasema:
'Sijawahi kuona hii, hivi kwanini mnaogopa kusema ukweli, kuwa mtawakosa wake
zenu wa ndoa....mume wangu, niliishakuambia, awali, ukweli wako ndio utakaonipa
matumaini kuwa kweli, ulichofanya hukukusudia, lakini mpaka hatua hii,
yaonyesha wazi kuwa ulikusudia,na kwahiyo, mimi naondoka, ila nataka tuongee na
dada hapa,yeye ni nesi, na mimi ni mfanyabiashara, nimeamua kujiajiri, kwahiyo
hatutashindwa kumlea huyo mtoto….’akasema mke wa Soldier.
‘Lakini mimi sihitajii tena msaada wa mtu, nimesema naondoka na
mtoto wangu, niwaombe msamaha kwa haya yote, ….sawa jamani…’akasema huyo mdada
aliyekuwa kajifunika.
‘Hapana huwezi kuondoka,…’ilikuwa kauli ya baba kitandani.
‘Kwanini baba…?’ akauliza huyo binti, na kabla hajajibu, mara
mlangoni akaingia mama mmoja, alikuwa ni mama mjane, akionyesha ana wasiwasi
sana. Kwanza akasimama pale mlangoni kwa muda kabla hajaingia ndani.
'Mama ingia umsalimie mgonjwa, keshapona, kaweza hata kukaa mwenyewe kitandani…'akasema
dereva. Na mama akaingia na kuanza kusalimiana na mgonjwa, baadae akageuka
kutaka kuondoka, huku akisema;
'Samahani, naona mpo kwenye maongezi,…lakini nataka kuongea na wewe...'akasema akimuangalia mtoto wake dereva
'Kuhusu nini tena mama, ngoja nimalizane na hawa ndugu zangu.
'Nimeshakuambia,…namtaka huyo mjukuu wangu, hakikisha unamchukua leo hii, yule
ni mtoto wako, nimemuangalia kwa makini, ile ni damu yako,…unasikia sitaki hiyo
tabia yako tena..kubadilisha badilisha mambo, unataka kupata nini kwa ajili ya
hilo…, hebu wewe fikiria mwaka sasa unatarajia kupata mtoto, hujampata, haya
umempata huyo ..hata kama sio kwa njia halali, lakini ndio damu yako,..’akasema
mama yake.
‘Mama huyo sio mtoto wangu, nakuhakikishia mama, docta
alishanipima, bado muda wangu wa kupata mtoto, kuna mapngufu mwilini, lakini
yataisha tu…’akasema dereva.
‘Mimi ni mama yako, huwezi kunificha kitu… nafahamu mengi kabla
yako, usifanye makosa hayo ya kukataa damu yako..’akasema mama yake.
‘Lakini umejuaje kuwa ni mtoto wa mwanao…’akauliza mama yake
Soldier.
‘Nimejua tu…’akasema mama yake dereva na kumgeukia mwanae
‘Mama…’akasema kutaka kujitetea
‘Sitaki kusikia zaidi…kama ni mke wako nitaongea naye, hakuna
shida…wewe umerithi uzazi wa baba yako, unasikia, kumpata mtoto mwingine
inaweza isipatikane, mkeo naye hajulikani, huenda ana matatizo, sasa kwanini
uikatae hii bahati…’akasema mama yake.
Na mara mlangoni tena akaonekana mdada mmoja akiingia, na wote
wakageukia mlango , na huyo mdada alipona hiyo hali akasita kuingia, baadae
akajongea taratibu, akionyesha mashaka mashaka.
‘Mke angu umekuja, mbona hukunipa taarifa…?’ akauliza dereva.
‘Nimeamua kuja tu, ….na nilipokuwa hapo mlangoni nimesikia mama
akiongea neno, Mama, mbona unasema hivyo, mwanao hana matatizo yoyote ya uzazi,
mimi hapa nina mimba,...mimba ya dereva…’akasema.
'Haiwezekani...'akasema dereva.
'Haya, kama ulijifanya huzai, ukatembea na binti wa watu, sasa huna cha
kujitetea tena, sasa una watoto wawili…’akasema Soldier.
‘Watoto wawili…?’ akauliza mke wa dereva.
‘Muongo huyu…’akasema Dereva.
WAZO LA
LEO: Kuna kauli nyingine zinaweza kutamkwa kwenye jamii, na
zikitamkwa kumuhusu mlengwa, labda ana mapungufu fulani, au kakosea jambo, au
mgonjwa..kauli hizo zinaweza kumvunja nguvu yule mtu, na kumkatisha tamaa, au kama
ni tatizo, huyo mtu anaweza kujisikia vibaya na kujiona kazalilishwa, na
ikaishia kuumia ndani kwa ndani, na kauli nyingine hazifai kuongea mbele ya
mgonjwa, kauli hizi zinaweza zikamuongezea mgonjwa tatizo badala ya kumsaidia,
tuweni makini sana kwenye ndimi zetu...
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment