‘Sasa kabla sisi
hatujaondoka, maana tunasafiri mimi na mke wangu leo…, basi mimi ninataka
kutimiza ile ahadi yangu kwako…, ile ahadi niliyokuambia kuwa ukiweza kumfanya
mke wangu akarudi, basi kwanza kwa moyo mmoja, nitakuwa nimeweza kukusamehe
kiukweli-kweli kutoka moyoni…nilishakusamehe…lakini bado nafsi yangu ilikuwa
inaendelea kusononeka….
‘Sasa ….nipo na
furaha,..sina kinyongo na wewe hapa duniani na kesho ahera…’akasema.
‘Nashukuru kwa
hilo…’nikasema.
‘Lakini hata hivyo
..nitakuwa na uwezo sasa wa kukuambia kile nilichoagizwa, ambacho kilitegemea
haya yote,….baada ya hayo uliyoyafanya… natumai hili lililobakia ndio itakuwa
kazi yako ya mwisho…kwa hili sasa utakuwa umepata msamaha wa huyo
aliyetuagiza…., labda kama una mengine, ambayo ulikuwa bado hujayatekeleza…’akasema
docta.
‘Mhh…sijui,
nimejitahidi kadri ya uwezo wangu,..mimi
sijui nimeshatubu, nimemuomba mungu msamaha, nimawaomba wote niliowakumbuka …ambo
aniliwakosea, na yote hayo nimeyafanya kwa moyo mkunjufu…sasa sijui kama wao
wamenisameeh kweli kama walivyonitamkia,….mmh, sasa docta wewe niambie tu…hicho ulichoagizwa…’nikasema.
‘Hili agizo, kama
nilivyokugusia awali, linatoka kwa mke wako mwenyewe….’akasema
‘Mhh, sawa, alisema
nini,..au kakugiza nini tena…maana wewe na mke wangu, kweli mlishibana, …lakini
usijali mimi nimekuelewa wewe niambie tu…’nikasema
Docta kwanza
akasimama, na kujinyosha, akatembea hatua kadhaa hadi kwenye dirisha akaangalia
nje,..halafu baadaye akanigeukia, akasema
‘Kwanza nikuulize
yule binti anayekusaidia hapo nyumbani bado yupo…?’ akaniuliza, na mawazo yangu
yakaenda mbali, najua wengi, hawaniamini, wanasema labda huyo binti kawa hawara
yangu, lakini kiukweli,…sina hisia hizo kabisa , huyo binti yupo hapo nyumbani
kama hayupo,
‘Kwanini
unamuulizia, ninajau wengi mna hisia mbaya dhidi yangu,…nikuambie ukweli,
mimi.. sina hisia zozote kwa huyo binti, na bahati mbaya nimetokea kumchukia
sana, na nimekuwa nikimkemea kumsema mabaya, kila anachofanya lakini amekuwa
akinivumilia tu…nilitaka aondoke, lakini haondoki….sijui kwanini….
‘Mimi sina wazo
hilo, nimekuuliza tu, maana ni lazima uwe na mtu wa kukusaidia,…ni kawaida,
nilitaka niwe na uhakika huo, na kama hakuna mtu nikutafutie…’akasema docta
‘Wa nini…sihitaji
mtu, ningefurahi kama ningebakia mwenyewe, huyo binti bado yupo, nilishamwambia
aondoke, lakini anasema eti alishauriwa na mke wangu awepo kunisaidia,
..kiukweli mimi simtaki…’nikasema
‘Kwanini humtaki,
kwanini unamchukia kihivyo, nakumbuka siku moja ulianiambia kuwa yeye ndiye aliyekuchonganisha
wewe na mkeo, ya kuwa yeye ndiye anayemuambia mkeo siri zako, na kumfanya mkeo
akufikiria vibaya, lakini..sio kweli, kutokana na maelezo ya mke wako..huyo
binti hajawahi kumwambia lolote kukuhusu wewe, hata alipojitahidi
kumuuliza…’akasema docta.
‘Kwani
atakubali..achana naye….’nikasema.
‘Huo ndio
ukweli…’docta akasema, na kuongozea.
‘Au una jingine
kubwa la kukufanya umchukia huyo binti…?’ akaniuliza docta, na kabla sijamjibu
akasema;
‘Huyo binti wa watu
hana kosa…hebu fikiria, yeye yupo nawe usiku na mchana…anakusaidia sana, hakujali
kuwa uliwahi kutaka kumdhalilisha, hajaogopa kukaa karibu na wewe…na sijui
unamlipa shilingi ngapi..lakini hajali hicho kiasi kidogo unachomlipa…’akasema
‘Kasema namlipa
kiasi kidogo, unaona jinsi alivyo…naona anatoa siri za ndani kwaa watu sasa,
yaani leo nikifika anaondoka,…’nikasema kwa hasira.
‘Jirani
…hajaniambia hivyo, ila kama upo na hali mbaya useme, nikusaidie kumlipia,
maana huyo ni mfanyakazi, na moja ya sharti la mfanyakazi, ni kuwa alipwe kabla
jasho lake halijakauka….’akasema
‘Nikuulize docta,
huyo mwanamke, ..mmh, huyo binti, amekuja kwako kulalamika kuwa sijamlipa
mashara wake,…?’ nikamuuliza.
‘Hapana,..sijawahi
kukutana naye tokea mkeo afariki, nilijua labda keshaondoka kwenda kwao, lakini
nikasikia kwa watu kuwa bado yupo….sasa nilitaka uhakika tu…na najua hali yako,
…kama naweza kusaidia hilo niambie tu…’akasema
‘Huyo binti bado
yupo lakini ataondoka, kama sio leo basi, kesho, mhh…mimi simtaki…’ nikasema,
ni kweli moyoni nilishatokea kumchukia huyo binti sijui kwanini, ..pamoja na
moyo wangu kuwa kwenye imani, na ya kuwa sitakiwi kumchukia mtu, lakini kwa
huyu binti, kila nikimuona nahisi hasira tu…sijui kwanini..ninamchukia sana
huyu, nahisi nifanya jambo baya, kama kumpiga,..kumsema ovyo… wakati mwingine
natamani kusema yeye ndiye kachangia mke
wangu…lakini nihisia tu!
‘Huyu binti wa
watu, hana tabia mbaya, kama unavyomfikiria, na kama una hisi zozote mbaya
dhidi yake…, unahitajika kumuomba msamaha, vinginevyo utakuwa hujakamilisha
zoezi lako la toba….’akasema
‘Na hilo lipo
kwenye hayo maagizo,na je ulitaka kuniambia na hilo..mimi sijamdhania huyo
binti kihivyo, ila simpendi tu, na naona akiendelea kuwepo hapo, watu wataendelea
kunifikiria vibaya,..kwa hivi sasa mimi sipendi kueleweka vibaya na watu…nata
niwe huru, kimwili na kiroho…’nikasema
‘Haya kama humtaki
huyo binti akusaidie, basi mimi nipo
tayari kukutafutia mtu mwingine ambaye atakusaidia kwenye kipindi hiki kigumu,
na nitakusaidia kumlipa, unasemaje kwa hilo…?’ akasem na mimi nikasema;
‘Hapana, haina haja
…’ Na niliposema hivyo, docta akatulia kama anawaza jambo, na mimi nikasema;.
‘Mhh..unaonaje ukiniambia
hilo agizo, au hicho ulichataka kuniambia, au ndio hilo la kumuomba huyo binti
msamaha, kama ni hilo, nilishalifanya, ila nimeona akiendelea kuwepo hapo
nyumbani, nitazidi kumchukia, kumsema sema, na…sipendi tu awepo…’nikasema nilipoona
kama anapoteza muda.
***********
‘Jirani, kwanza
mimi natimiza kile alichoniagiza mke wako…sifanyi haya kwa matamanio yangu,
maana mambo mengine ni mambo binafsi, na mtu akishafiwa inachukua muda sana
kusahau, hasa akifiwa na mwenza wake…’akasema
‘Mhh..’nikaguna
hivyo tu
‘Lakini mkeo
alitusisitizia sana kuhusu hilo…aliyaona maisha yako ya mbeleni kabla
hajafariki, na aliwekeza kwa hilo, akapanga mambo mapema, uone jinsi gani alivyokuwa
anakupenda…’akasema na mimi nikakaa kimia
‘Mkeo alituagiza
kuwa, akishafariki,… ukapita muda wa mambolezo, ukapita muda muafaka, na
ukayatimiza yale yote uliyokuwa ukifuatilia, likiwemo hilo, la wewe kufanya
jambo litakaloweza kunirizisha mimi,..na moyo wangu ukawa mweupe dhidi yako,
basi alisema kwa kauli yake kuwa wewe uoe haraka iwezekanavyo..’akasema
‘Eti nini..acheni hayo
jamani, hata nyie..…huo sasa ni uhuni, mimi nioe, hahaha….hapana,..hilo siwezi
ku-ku-kubalia, hata siku moja, sitaki kusikia swala la kuoa, niliyempenda
keshaondoka, na mimi nilishakufa kihisia, sitaki sitaki tena mahusiano na
wanawake……’nikasema.
‘Kwanini, unasema
hivyo, una wasiwasi gani,…?’ akaniuliza docta
‘Sio swala la
wasiwasi,… wewe unasema hivyo kwa vile hayajakukuta, na hata hivyo, mimi
mwenyewe nafahamu matatizo yangu, sitaki tena haya yaliyopita yaje kunitokea
tena, sitaki, namuomba mungu anisaidia nibakia hivi mpka siku ya kuitoa roho
yangu …mmh’ nikatulia kama vile nimetamka neno gumu sana.
‘Hebu jirani, nipe
sababu za msingi mimi ninakusikiliza,…maana hujanishawishi ni kwani ni hutaki
kuoa… unakumbuka nimekuambia nikirudi nitahakikisha nafuatilia afya yako,
nataka nikupime nione tatizo lipo wapi, ….’akasema.
‘Ili iweje….tatizo
gani, ..mimi siumwi..sina tatizo, na yaliyopita, haya maana tena kwangu, sitaki
hata kuyasikia, maana nafsi yangu ilijawa na ubinafsi wa kutaka kutafuta mtoto,
kumbe namuumiza mwenzangu, na kwa hilo nastahiki kuadhibiwa, …na moja ya adhabu
yangu nikubakia hivi…peke yangu bila kuoa…halafu nyie mnasema nini, eti nini…?’
Nikawa kama nauliza.
‘Unakumbuka mkeo
alikuhangaikia sana, na nia yake ilikuwa nyie mpate mtoto kweli si
kweli....unakumbuka mke wako alikuhangaikia sana, nia uweze kuishi maisha ya
furaha, hata kama yeye hayupo hapa duniani, kwahiyo wewe, sasa unataka juhudi zake zipotee bure, ndio
maana yako….’akasema.
‘Docta, ninataka unielewe,
mimi sasa siyo yule mtu wa zamani aliyekuwa na tama hizo, mimi sina hisia
zozote tena, nioe ili iweje, kifupi mimi…sitaki kuoa,..hilo liondoe akilini
mwako, ..hata angelikuwa nani, nimeshasema ninataka kuishi hivo hivi mpaka siku
ya kumfuata mke wangu huko alipo,…’nikasema.
‘Sikiliza,…sio mimi
ninayetaka wewe uoe…hili ni agizo la marehemu mke wako, kama kweli unampenda,
na kama kweli bado unaendelea kumpenda basi ulitimize hilo, na kama ulikuwa
unampenda kinafiki, basi endelea kukaa hivyo unavyotaka wewe…, mimi siwezi
kukulazimisha kwa hilo…, lakini nina uhakika hutaishi kwa amani, utakuwa ukitokewa
na mkeo mara kwa mara..’akasema.
‘Hilo docta,
siwezi, acha nieleweke hivyo, ni bora tukosane tu…ni bora na hata yeye kama
alilitaka hilo, basi anielewe hivyo,… kwasababu hizo ni hisia zangu,….kifupi
mimi sitaki , sitaki kabisa kuoa tena…kama agizo lilikuwa ni hilo basi ngoja mimi niondoke…’nikasema na
kusimama kutaka kuondoka.
‘Unajua, mimi
nimeshafahamu ni kwanini hutaki kuoa….najua unajiuliza baada ya haya yote ni
nani atakayekukubali wewe umuoe, kwa hali ilivyotokea ni kama ulijiweka uchi
kwa jamii, naelewa sana hilo..lakini mkeo alishaliona hilo na alishajipanga kwa
hilo…, na kila kitu alikiweka wazi,…’akasema
‘Hawezi kuingilia
hisia zangu…na ni kitu gani alikiweka wazi kuhusu mimi, kama ni hilo la kuoa,
hilo siwezi kukubaliana naye, sawa, hapo mimi na yeye hatutaelewana, na najua
huko alipo atanielewa,…kwahiyo jamani, kama ni hilo, naona tuachane,
kwaherini….’nikasema sasa nikiwa nimedhamiria kuondoka.
‘Jirani, mimi ni
metimiza wajibu wangu,…kwanza kukuambia agizo hilo, lakini hilo agizo
halijakamilika, kama nilivyokuambia,…mkeo alipanga kila kitu juu yako, kwa nia
ya kukusaidia,..sasa subiri kwanza nimalizie agizo lake, halafu wewe mwenyewe
utakuja kuamua …kwenye maamuzi ni sisi hatutaweza kukuingilia…’akasema docta.
‘Agizo gani
jingine…maana hilo peke yake sijakubaliana nalo, …kama kuna jingine la namna
hiyo, basi nyie acheni tu, maana naona nyie mnafikiria kirahisi rahisi tu, mtu
afiwe na mkewe, halafu haraka akimbilie kuoa, ..hivi mnalionaje hili,
mnanionaje mimi…’akageuka kumuangalia docta na baadaye akageuka kumuangalia mke
wa docta
Mke wa docta muda
wote alikaa kimia, akisikiliza, na alipoona anaangaliwa, akajua kuwa na yeye
anahitajika kutoa mawazo yake, akakohoa na kusema;
‘Samahani niwaingilie
kidogo, maana hilo hata mimi linanihusu, hata mimi niliwahi kupewa hayo
maagizo,…wakati marehemu mkeo ananiambia mimi kuhusu hilo,mimi nilichukulia
kimzaha tu, sikulitlia maanani, lakini
sasa nimeliona lina umuhimu wake…’akasema
‘Shemeji mimi ni
mwanamke, na hayo aliyokuambia mume wangu, kama ningekuwa sijaisikia kauli ya
marehemu mke wako, ningelipinga….kabisa, ningepinga swala la wewe kuoa
kwasasa…maana ningelichukuliaa kuwa ulisubiria mkeo afariki ndio ukimbilie
kuoa…lakini mimi niliambiwa na kukokotezewa, nikasisitiziwa…kwahiyo hata mimi
nilazima nitimize wajibu wangu huo kukuambia…hayo ni usia kutoka kwa mkeo…’akatulia
na mimi nikabakia kushangaa, halafu nikasema;
‘Kwahiyo shemeji
unamuunga mume wako mkono..hujielewi kuwa na wewe ipo siku unaweza ukaondoka,
na mumeo akakimbilia kuoa kwa haraka kweli inapendeza …’nikasema
‘Naelewa sana
shemeji,…..na hujui kwanini mkeo alisema hayo, hujui ni kwanini mkeo
alikuhangaikia hivyo…alijua angekuambia muda ule akiwa hai usingelikubali hilo…,
alikuwa tayari umuolee mke mwenza…lakini …’hapo akatulia.
‘Mwambie…’akasema
mume wako alipoona mkewe kabakia kimia
‘Lakini alisubiria
umalize maombi yako ya toba…na alishaona dalili za toba yako kuwa ni za
kweli,..aliniambia wewe sasa ulishaiva, yamebakia mambo machache tu , ..na sasa
hata akiondoka, utakuwa umeshafanikiwa kuwa mume mwema….hata sio kwake, lakini
kwa huyo utakaye muoa… na hilo la wewe kuoa, alilitaka ulifanye kwa haraka,
usichelewe, ili upate matunda yake, sijui kwanini alisema hivyo…’akasema mke wa
docta.
‘Jamani kama ni
hilo, niacheni tu..kama agizo lenyewe ndio hilo, ..mimi sipo tayari kabisa leo
a hata kesh…mimi kwasasa niseme hivi…, nawatakia safari njema, ..’nikasema
nikianza kuondoka.
‘Lakini
hatujamaliza, mkeo hakutuagizo hilo tu…’akasema docta na mimi nikasita
kuondoka, nikatulia.
‘Na mimi siweki
kuondoka bila kukuambia yote aliyotuagizia mkeo…maana hayo maagizo hayataki
kuchelewesha, kama ni kuchelewesha iwe juu yako….na lolote likitokea tusije kuja
kulaumiwa na mbele ya mungu tuwe salama, ….’akasema docta, na mimi nikasimama
pale pale…moyo ukianiambia ondoka haraka lakini miguu ikawa mizito.
Niliyoyasikia baadae, sikutaka hata kusubiria,...niliondoka humo ndani hata bila kuaga, nikiwa nimejaa hasira..…..
NB: Alisikia nini….
WAZO LA LEO: Tupende kuwa na subira na baadae kushukuru pale tunapopewa nasaha au ushauri, hata kama anayekupatia huo ushauri
kwako unamuona hana maana, labda kihali .kielimu, kiumri, ..hata kitabia,
lakini yeye akaamua kukupatia nasaha, au ushauri. Usikilize kwanza, na ufanye
busara kumshukuru huyo mtu. maana ushauri mwingine waweza kupitia kwa
mtu, lakini umetoka kwa muumba wako.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Mkuu mbona wachelewesha mambo
Naona wewe sasa kazi imekushinda...
Vipi sehemu ya mwisho..ulisema ni sehemu ya mwisho au?
Post a Comment