Nilimwangalia Yule mama pale alipokaa na mtoto wake, nikajua
mambo yameshaharibika, tayari mtoto anachemka homa! Hata bila kumuuliza Yule mama,
nikaiona hiyo dalili, mtoto macho yalionyesha, yanaonekana kama yanasinzia,
kalegea….nilipoiona ile hali hapo hapo nikakumbuka maneno ya huyo jamaa, akisema, …usije kukiuka hiyo miiko,…mwisho ni mara
tatu, basi….sasa jiulize ni hii ni mara
ya ngapi…
Nilipokumbuka hayo maneno nikamwangalia jamaa, jamaa alikuwa
kama hana habari, anashughulika na simu yake, nahisi alikuwa anachat..au anaandika ujumbe wa maneno..
‘Shemeji hawa watu
hawajui tunavyoteseka na huyo mtoto, na hiyo hali ikijirudia hatuna la kufanya,
mimi nanawa mikono yangu, mimi ni baba
yake lakini kutokana na mtaalamu, sitaweza kufanya lolote tena…unakumbuka ulivyoambiwa,….
Hii kama ikitokea tena itakuwa ni mara ya nne, ina maana kwa
mujibu wao huyo mtoto kuumwa, ilishazidi kile kiwango, kwahiyo kupona kwake ni mashaka,
kwa mujibu wao,…na huyo jamaa hawezi kufanya lolote tena…..nilipoiona hiyo
hali, akili ikaanza kuchemka, nifanyeje sasa…, je kama ni kweli itakuwaje…..
‘Ooh, sio kweli , hawa ni wajanja tu…’ mimi nikajipa moyo
kwa kusema hivyo kimoyo moyo…., huku nikimtupia macho Yule mama, ….yule mama
alikuwa kamshikilia mtoto wake kama kashikilia nini, kampakata mithili ya
kumkumbatia, ….huku machozi yakimtoka, nahisi moyoni anaumia sana, lakini hanacha
kufanya….
‘Huu sasa ni mtihani, …’Nikajikuta nikisema kwa sauti bila
kujua, na jamaa akanitupia jicho,….uso
ulionyesha dharau fulani.
Bila kupoteza muda nikaona sasa na mimi natakiwa nicheze karata yangu ya
mwisho, kwa sauti ya haraka nikasema;
‘Umesema huniogopi, kwa maana huogopi maswali yangu, au sio….na
ina maana kuwa unajiamini kuwa wewe huna
makosa….,si ndio hivyo…sasa nataka tupambane mimi na wewe ili nihakiki hilo kama kweli huna
makosa, ….nataka tupambane mwanaume kwa mwanaume, ….’nikasema
‘Uliza hayo maswali yako bwana …’akasema akiwa haniangalii
usoni akaonyeshea kwa mkono huku kainamia simu yake.
‘Tatizo wewe ni mnafiki na muoga,…’nikasema, na maneno hayo
yalimfanya ainua kichwa na kuniangalia, uso ukambadilika, akasema;
‘Eti nini…mimi ni nani, …?’ akauliza sasa akiniangalia kwa
hasira, na mimi nikatulia tu nikimkagua, kweli maneno hayo yalifanya kazi yake,
aliacha kile alichokuwa anakifanya na kuendelea kuniangalia, akiwa kakunja uso.
‘Mimi sipendi ugomvi….umesema unataka kuniuliza maswali,
nimekubali, sasa hiyo ni lugha gani, , hii inaonyesha wewe huna nia
nzuri,…unanitaka ugomvi, na inaonyesha wewe ndiye mwoga…na mnafiki, sio mimi...’akasema na mimi
nikaendelea kukaa kimia,
‘Kwanini unasema mimi ni mwoga na….kwa vipi…wakati….nimesema
uulize hayo maswali,….uliza sasa?’ akasema akiwa kashusha hasira yake….huyu mtu
ni mjanja sana, ….anajua kuigiza, anajua kucheza na utashi wa watu kwani kazoea
kupambana na watu wenye tabia tofauti kwenye biashara yake, mtu kama huyo
hutarajii kumkasirisha kwa haraka hivyo.
‘Wewe kama unajiamini kwanini unapambana kwa kupitia mtoto,…’nikasema
hapo kashtuka kidogo, akamwangalia Yule
mtoto, halafu akajirekebisha na kunigeukia akasema
‘Mimi sikuelewi, napitia kwa mtoto kwa vipi…?’ akaniuliza
akigeuka kidogo kumwangalia mtoto, au shemeji, halafu akageuka kuniangalia mimi
lakini kwa jicho la pembeni.
‘Hivi wewe kweli una uchungu na hii familia, hivi kweli wewe
una ubinadamu, …unajiita baba…..’nikasema na yeye akaniangalia na kusema;
‘Hebu ongea kwa kujiamini…niambie mimi nimefanya kosa
gani,…?’ akauliza akinikodolea macho
‘Nikuulize wewe hivi, kama angelifanyiwa mtoto wako hivyo,
kweli ungelifurahi, kumbuka ….ubaya umtendao mwenzako ipo siku utakurejea wewe
mwenyewe…kumbuka haya maneno yangu…’nikasema akawa sasa katulia, akiniangalia
mimi, na mara akageuka kumwangalia Yule mtoto na mama yake kwa macho yenye
kujiuliza!
‘Una maana gani wewe, kwani shemeji kuna nini kimetokea….?’
Akauliza na shemeji yake akawa kimia, kamuinamia mtoto wake tu huku machozi yanamtoka,
alivyomshika mtoto wake utamuonea huruma!
‘Unajifanya hujui….nikuulize kwanini wewe unamtumia mtoto
katika kushinikiza mambo yako,…kama kweli unajiamini na huna kosa, kama kweli
una ubinadamu,… kwanini umtumie mtoto ambaye hana kosa, huyo mtoto anajua nini,…hajui
kabisa kinachoendelea..’nikasema nikimkimuangalia moja kwamoja usoni, nia yangu
ni kumchanganya kichwa, akasirike. Mtu akikasirika huropoka ovyo…
Ilikuwa kama nimemmwagia maji, akataka kusema kitu, lakini
kikawa hakitoki, akatikisa kichwa, halafu akasema;
‘Unajua mimi nilikuheshimu sana, nilikuona ni mtu wa maana,
sasa sijui nikuite nani, nimejaribu kukulezea kwa busara, lakini wewe hutaki
kunielewa, na sasa unataka na….hivi wewe unanijua mimi…tatizo wewe hunijui,….’akasema
akitikisa kichwa.
‘Nakufahamu sana, wewe ni dalali, na mbinu zako za udalali zinajulikana,
ukitaka kitu ni lazima ukipate, si ndio hivyo, kwa njia yoyote ile, na ndio
maana umeamua kutumia mbinu hii chafu, ili ushinikize upate kile ulichokusudia,…wewe
na huyo mtaalamu mumeamua kumtumia huyo mtoto…unabisha..?’nikasema.
‘Hayo ndio maswali yako….?’ Akaniuliza na mimi nikabakia
kimia nikitaka kujua atachuku hatua gani, alikuwa bado amekaa, sasa uso ukiwa
umetahayari. Mbinu ya kumshinda mnafiki ni kumwambia ukweli, mbinu hiyo
ikafanya kazi, japokuwa hadi muda huo, nilikuwa bado sijakuwa na uhakika na kauli yangu hiyo!
‘Wewe sasa huna la kuniambia,…huna lolote lengo lako ni
kunipakazia ubaya kwa shemeji…shemeji huyu ni mwongo, mchonganishi….usimsikilize….halafu,
naona hata hayo maswali yako hayana
maana, na kwa kauli yako hiyo tunaweza kufikishana kubaya…nikuambie
ukweli..ohoooh’akasema, na mimi nikamwambia;
‘Sasa nikuambie kitu…nina uhakika kuna sababu ya huko kuumwa
mtoto na haya yanayoendelea , ili kumtisha mama yake asihangaike kupata haki yake na
familia yake,…na hii mbinu ya kishetani, imefanywa kwa kumtumia huyo mtaalamu
na wewe….nitakuja kukuthibitishia hilo…, sasa sikiliza kwa makini, kama hali ya mtoto ikiwa hivyo, mimi
nakuhakikishia utakwenda kuozea jela…’nikasema
Hapo akaniangalia kwa macho ya mashaka, akasema;
‘Ina maana kweli umedhamiria na hiyo kauli yako, ina maana
sasa unanitisha,….kwanza unasema nini, ina maana unafikiri mimi ndiye namfanya huyo mtoto hivyo…wewe….sikiliza…’akatikisa
kichwa na kugeuka kumuangalia shemeji yake, halafu akanigeukia na kusema
‘Kwanza wewe unasema
hivyo kama nani,….hahaha, eti nitaozea jela…unanitisha mimi, hahaha, tatizo
lako hunielewi…hivi wewe ni nani, unajua nilikuwa nakuheshimu, sasa….unataka
nini kwangu?’ akaniuliza sasa akasimama, na mimi nikawa nimetulia tu, akavuta
hatua, kama ananijia, halafu akasita, akageuka kumwangalia shemeji yake.
‘Shemeji huyu ni nani kwako…..?’ akauliza na shemeji yake
akawa kamkumbatia mtoto wake,kama vile hataki amtoke huku machozi yakiendelea
kumtoka, kama maji...mimi nikaona napoteza muda, nikasema;
‘Wewe si mwanaume, na huogopi maswali yangu, kama mwanaume kweli
kwanini unatumia kiumbe hicho kisicho na hatia, unamtesa mtoto wa watu bure…nimakuambia
hivi angekuwa mtoto wako kafanyiwa hivyo ungejisikiaje,….au unafiria mungu
haoni,…’nikasema na kabla hajasema neno nikasema;
‘Sasa mimi nakuambia hivi kama wewe unajiamini, basi pambana
na mimi, sio kwa kupitia huyo mtoto, nifanyie mimi hayo unayomfanyia huyo
mtoto, …mimi sasa nimeamua kufanya hayo usiyoyataka, hamisha hayo …kwangu
unasikia,….’nikasema
‘Mimi sikuelewi, unaongea nini….’akasema akionyesha mikono
ya kukata tamaa
‘Wewe kama huna hatia,…..basi mwachieni huyo mtoto, upambane
na mimi, acheni kumtesa huyo mtoto, unaona hapo…homa hiyo imeshaanza kupanda…na
unalijua hilo…umeshawasiliana na jamaa yako afanye hivyo, …unafikiri mimi
iyajui hayo….’nikasema na yeye akaguka kidogo kumwangalia huyo mtoto halafu
akageuka kuniangalia mimi. Akasema
‘Sasa mimi naona….unanitaka makubwa, unasema mimi ndio
namtesa huyo mtoto, ina maana mimi ni mchawi au sio,…au mimi ni mzimu, maana
hayo yanatokea kwasababu ya mizimu, wewe, ….wewe, kwa kauli hiyo mimi sizani
kama tutaelewana….shemeji , kama huyu ni ndugu yako, ….muonye kwa mara ya
mwisho, nitakachokifanya hapa,msije kunielewa vibaya…unanifahamu vyema shemeji
mimi ni mvumilivu sana lakini ikivuka mpaka,…ohoooo!’ Akasema sasa
akinionyeshea kidole.
‘Sikiliza,….nijibu maswali yangu nitakayokuuliza,….sitaki
uwoga hapa… na nia yangu ni kuhakikisha kuwa kweli wewe huna makosa, wenye
makosa labda ….labda, tuseme ni benki, au labda tusema kuna mtu mwingine yupo
nyuma ya hili, ….sasa kama sio wewe, nataka tulijue hilo kwa kupita kinywa
chako,…na tumgundue huyo mtu mwingine ni nani, kwa masilahi ya hii familia,
hawa watoto wanahitaji haki yao, kwanini wateseke, kwanini tusiwe na mioyo ya
huruma,…’nikasema
‘Sawa….mimi nimekustahi, sitaki kugombana na wewe, maana
kutokana na kazi yangu ninapambana na watu wengi kama wewe…hasira zangu zipo
mbali saana….sasa nakuambia uliza
maswali yako…uondoke zako….’akasema na kurudi kukaa.
‘Siwezi kukuuliza maswali wakati mtoto yupo katika hiyo hali….wewe
si mjuzi, umefundishwa na huyo mtaalamu
wako, fanya uwezavyo huyu mtoto asipandwe na hiyo homa ili mimi na wewe tuweze kuyaongea
haya na unijibu maswali yangu kwa amani…’nikasema na yeye akashika magoti, kama
anataka kusimama, na mimi nikaendelea kusema
‘Kama huyo mtoto anachemka homa hapo, nitakuulizaje hayo
maswali, kama huyo mtoto anaendelea kuchemka homa, mimi sina namna, ni lazima
nichukue hatua nyingine, na si zaidi, nitawaita polisi,nina ushahidi kuwa kuna
namna inafanyika ili kuwatisha watu wasitatufe haki yao, na namna hiyo
inafanywa kwa kupitia huyu mtoto, huo ni unyama, huo ni ushetani, polisi wakija
hapa nitawaonyesha huo ushahidi na wewe utakwenda kuozea jela na huyo mtaalamu
wako…..’nikasema kwa hasira.
‘Mimi nilishasema, sina namna ya kufanya kama hali ya mtoto
ikijirudia, kama homa ikimpanda tena, dawa tuliyopewa haiwezi kufanya kazi,….
hiyo ni kutokana na mtaalamu alivyosema,…mimi
kwa hivi sasa siwezi kufanya chochote ni miiko niliyopewa… unielewe hivyo, sio
mimi, ni mtaalamu kasema hivyo,….’kabla hajamaliza mara shemeji yake akadondoka
sakafuni….
Oh,….mtihani!
‘Shemeji vipi….’akauliza alipoona ile hali,na mimi nikaona
mambo yamekuwa sasa manzito, ikabidi kwanza niende kumchukua Yule mtoto maana
anaweza na yeye kudondoka, …mtoto alikuwa anatetemeka,…nilipomshika nikaona
joto lipo juu,…nikambeba hadi kwenye sofa nikamlaza,…nikageuka kumuangalia mama
yake, alikuwa kalala sakafuni,…kapoteza fahamu!
Shemeji mtu kuiona
ile hali, akasimama na kumuendea shemeji yake, akainama kumuangalia, akasema;
‘Sasa unaona, haya yote umeyataka wewe…unaona wewe mtu…sijui
umetoka wapi wewe hunielewi, sasa umeharibu, …hali ya shemeji ikirudia tena,….oh,
sijui itakuwaje….’akasema bila kuniangalia mimi, na mimi nikasema
‘Nimeyataka mimi au wewe, ngoja polisi wafike hapa , utasema
yote …..’nikasema
‘Shemeji, shemeji…..’akawa anamtikisa tikisa shemeji yake,
halafu akageuka kumwangalia mtoto, pale nilipomlaza kwenye sofa, akasema;
‘Kwanza kwani vipi ina
mtoto kapandwa tena na homa, sasa…niliyowaambia, mtajionea wenyewe, mimi sipo..
wewe umemshawishi shemeji akafanya mambo kinyume na miiko aliyopewa, mimi hapo sijui
tena la kufanya….maana hii ni zaidi ya mara tatu, na miiko imenikataza kufanya
lolote, shemeji, shemeji, hebu amuka, …’akasema akiwa anamtikisa tikisa shemeji
yake kumshitua aamuke!
Oh, nikaona mambo sasa makubwa, shemeji shinikizo la damu limeshapanda…kwanza
nikamuacha mtoto, nikaenda pale alipolala huyo shemeji mtu, na kuanza kumfanyia
huduma ya kwanza . Wakati nafanya hayo, nikamgeukia jamaa na kusema;
‘Sasa hivi nawaita polisi, ..waje waione hii hali jinsi gani
mnavyofanya hawa watu kwa tamaa zenu…sasa kabla hilo halijafanyika …, nataka
huyo mtoto hali yake ijirudie ili huyu mama akiinuka hapa amkute mtoto wake
yupo salama, vinginevyo, ….’simu yangu ikaita, kwa haraka nikaichukua na
kuangalia ni nani mpigaji, …walikuwa vijana wangu, nikaanza kuongea nao .
‘Vi-vipi mumeshafika kituo cha polisi, …..sasa waambie waje
hapa haraka, mtu wao yupo hapa,
…’nikasema na kusikiliza
‘Ok…wewe ….uje na huo ushahidi, ..fanya haraka…’nikasema na
jamaa kusikia, hivyo akamwendea mtoto, pale kwenye sofa, akachukua ule unga kwenye karatasi, akafanya alichofanya, akampaka mtoto, halafu,…mtoto
akapiga chafya. Mimi nikaendelea kumfanyia huyo mama huduma ya kwanza mpaka
akazindukana.
Jamaa alipoona shemeji yake kazindukana akasema;
‘Mbona mtoto yupo safi….ila sijui kama itachukua muda, sijui,
kama itafanya kazi….maana hii ni mara ya ngapi sijui, …shemeji mimi nilishawaambia…kwani
kitu gani mnafanya, kwanini mnamtesa huyu mtoto…’akasema huku akiangalia saa yake na nilimuona kama anataka
kuondoka, nikamkabili na kusema;
‘Unataka kwenda wapi…subiria maswali yangu….?’ Nikamuuliza,
na yeye akasema
‘Mimi nilishakuambia nina mambo yangu, nilikupa muda wa
kutosha kuuliza hayo maswali yako hukutaka kuniuliza kwa haraka, ….halafu sasa
nashangaa kwanini umewaita polisi ili iweje,…mimi naondoka zangu, sitaki
maswala ya kukutana na polisi hapa, nina
kazi zangu za kufanya za haraka…’akasema sasa akianza kuondoka.
‘Sikiliza, …huwezi kuondoka mpaka ujibu maswali yangu, na
polisi wanajua upo hapo, na amri yao ni kuwa uisondoke hapa mpaka wafike,…ukiondoka
hapa umekiuka amri ya serikali, sasa utatafutwa kama mhalifu..’nikasema , nikamuona akibadilika usoni, uwoga…., akasema
‘Kwanini mimi nimefanya kosa gani, …?’ akaniuliza
‘Polisi watakuja hapa…wao watakuambia kwanini wanataka
kukuona….ila ninachosema ni kuwa kama watakuta mtoto yupo kwenye hali mbaya,
itakuwa ni moja ya ushahidi wao, na …wewe ndiye utakuwa umesababisha hayo yote,
wewe na huyo mtaalamu…mtahitajika kuisaidia polisi…, kwanini mnamtesa huyu
mtoto…’nikasema.
‘Ngoja…kwanza,….wewe unasema nini…...’akasema na kumuendea
huyo mtoto pale kwenye sofa na kwa muda ule mtoto alikuwa kalala, sasa akawa
anamkagua huyo mtoto mwilini kuona kama ana joto….akasema;
‘Lakini mbona hakuna joto…huyu mama yake vipi…huyo mtoto kalala
tu, hana tatizo…lakini sijui zaidi ya hapo,….’akasema akimuangalia shemeji yake
‘Sawa sasa ni hivi sisi tutaendelea na maswali, na wakati
tunafanya hivyo,…sitaki itokee mtoto kupandisha homa tena, na sitaki hiyo hali
ijirejee tena iwe mwanzo na mwisho, ….’nikasema;
‘Mimi siwezi kuendelea kukaa hapa,…nimeshakuambia, ni lazima niondoke…maana mimi, nina wateja
wangu wananisubiria, kama mnaona nina kosa, waambie polisi wanifuate nyumbani
kwangu….’akasema na mara simu yangu ikalia, nikaipokea na kusema;
‘Hali ya mtoto ipo shwari…mnaweza kuwaambia hivyo, waambie
bado namuuliza huyu mtu wao maswali, na kama nitaona ana hatia basi
nitawaarifu…nini anakuja,ok….’nikasema na jamaa akaniangalia akiwa kasimama,
….halafu akasema ;
‘Hivi wewe unahisi kuwa mimi nahusika na haya yote, kuwa
mimi naweza ku….ku…mtesa mwanangu….hivi wewe una akili kweli….shemeji
usimsikilize huyu mtu…huyu mtu ni-ni-ni….’akashindwa kumalizia na mimi
nikasema;
‘Ni nani, ….malizia, usiwe na kigugumizi, toka lini dalali
akawa na kigugumizi…vinginevyo naona maji yameshakufika shingoni, utapeli wenu
utawatokea shingoni…’ nikasema
‘Mimi siwezi kufanya kitu kama hicho, kwanini niifanyie
familia yangu…niajiibia mwenyewe..hujui hawa ni familia yangu, hebu muulize shemeji,mimi
na kaka tulikuwaje,….kaka hayupo, mimi hapa nasimama kwa niaba ya kaka….hayupo
mimi nipo,…tatizo lako wewe unaingilia mambo bila kutaka kujua zaidi…hayakuhusu
haya’akasema
‘Sasa nataka tulihakikishe hilo,….kama kweli unaijali hii
familia,… kama kweli unasimama kwa niaba ya marehemu kaka yako au…kwa niaba ya utapeli, kwa nia ya kupata
mali ya marehemu kwa udanganyifu, na kumtumia mtoto kama silaha ya kushiinikiza
hayo…’nikasema
‘Hahaha..wewe mtu bwana,…una mawazo duni,…unasema hivyo
unafikiri nitapaniki…hunipati kwa hilo, nikuambie kitu, walinikabili polisi, wapelelezi wakashindwa,
….wewe sijui ni nani, utaweza nini wewe, sasa sikiliza kwa vile sitaki
kuelekeweka vibaya mbele ya shemeji , wewe yaulize hayo maswali yako ya
kipuuzi, nayaaita ya kipuuzi maana ni ya kubuni, ….uchonganishi tu, wivu….’akasema
halafu akamgeukia shemeji yake akasema
‘Shemeji mtoto kalala huyo,kwa hivi sasa hana tatizo, zaidi ….mimi
sijui, anajua mtaalamu, nenda kamlaze huyo mtoto ndani….’akasema na shemeji
yake ambaye kwa muda huo alikuwa kakaa karibu na mtoto wake, akasema;
‘Jamani,…mimi sitaki tena haya mambo….mimi sitaki tena haya
maisha, mimi sitaki tena kumtesa mtoto wangu, kama ni hii nyumba chukueni, waache wachukue, …niachieni
mtoto wangu salama…, sitaki jamani, basi …basi,…sitaki…’akasema huyo mama
akimbeba mtoto wake….’
‘Dada niamini mimi haya yote yanakwisha,…. leo hii hii
utaujua ukweli….’nikasema.
‘Hapana mimi sina haja tena …..waache wachukue
wanachokitaka, na mimi nitamuachia mungu,kama kapanga iwe hivyo, yote haya ni
kwa mapenzi yake, waache wachukue kila kitu watakacho, waniachie wanangu,,
…wachukue kila kitu watuachie amani yetu, mimi na watoto wangu, mimi sitaki
tena, ..sitaki sitaki, nimechoka jamani….’akasema na shemeji mtu akawa kashika
kidevu.
‘Dada wewe kamlaze mtoto, haya nayamaliza sasa hivi, haki ya
mtu haipote, nakama hali ya mtoto ikibadilika haraka polisi watafika sasa hivi,….
Usiwe na wasiwasi, haya maswala sasa yamefika kwa wenyewe…’nikasema na mara
simu yangu ikaita,ilikuwa namba ya mpelelezi mmoja wa polisi….nikaipokea ,
‘Afande vipi?’ nikauliza na kusikiliza ….jamaa akawa
ananitazama kwa macho yalijaa wasiwasi nikamuona akigeuza shingo kutizama
uelekeo wa mlango….
NB: Kuna nini kinaendelea….
WAZO LA LEO: Tutafute mali
kwa njia za halali, tuutafute utajiri kwa njia za haki…, lakini sio kwa kutumia
jasho la mtu mwingine. Jasho la mtu ni ushahidi , na malipo ya kudhulimiwa
jasho la mtu ni kwa Yule mdhulumaji kuishi maisha ya mashaka na mwisho wake
dhalimu huyo ataishia kudhalilika kwa mabalaa mbali mbali.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
imenigusa sana
Bonge la simulizi tupo pamoja miram
I admire sana simulizi zako but unaweka late sana jitahidi bhana but keep it up bro
Post a Comment