Mdada
alipoinua macho na kutuangalia, haikupita muda akaanza kutoa machozi, na
ilichukua muda kidogo kabla hajatulia vyema, na muda huo alikuwa ameshasogea
kwenye kile kiti alichoambiwa akae, akawa kakitizama kwa muda bila
kukaa,…hakuna aliyemsemesha sote tulibakia kimia
Kwa haraka
nikajua ndiye mdada, mrembo malikia wa kijiji….
Nikajaribu kumchunguza vyema huyu mdada, pamoja
na matatizo yote hayo, lakini bado alikuwa na uzuri wake wa asili, na mwili wake
umejengeka vyema, nikisema hivyo mtaelewa vyema, kiujumla ana umbile lenye
mvuto, nahisi ndio maana hawa watu walimuhitajia sana kwenye uigazaji….
Alikaa
kwenye kiti, na sasa akawa katulia, lakini muda wote alikuwa kainamisha kichwa chini,
hakuinua uso wake kumwangalia yoyote,na mara kichanga kikaanza kulia, ikabidi
Yule mdada mwingine aliyekuwa kambeba huyo mtoto, kusimama na kutembea pale
alipokaa huyo mdada, mama wa hicho kichanga, na kumkabidhi
‘Naona
anataka hoteli yake….’akasema na mdada akamchukua, na haikupita muda kichanga
kile kikanyamaza , kilikuwa na shughuli ya kupata hoteli yake.
‘Jamani
naona tuendelee kwani kwa mujibu wa ratiba ya docta, mzazi huyu atachukuliwa
ili akapate matibabu yake na taratibu nyingine za dawa, lakini tukaona kuwa
kuna umuhimu aje mumuone , ili kama ana lolote au nyie mna lolote liongelewe,
na kumalizana, kwani baada ya hapa,hatutaruhusu mtu yoyote kuonana naye,
…kiusalama zaidi..’akasema huyo mpelelezi
‘Wanandugu
kutananeni na Mdada, au mrembo, au malkia wa kijiji….’akasema na mdada akawa
kinama vile vile….
‘Japokuwa
mwenyewe kasema hayo majina hayataki tena, lakini wapi utapita huko kijijini
umtaje usisikie sifa zake…japokuwa pia sasa zimeharibiwa, lakini ndivyo ilivyo,
wenye sifa zao hupitia kwenye changamoto hizo…’akatulia
‘Mdada…,
hawa waliopo hapa ni marafiki zako, kila mmoja amekuwa akijaribu kukusaidia kwa
namna yake…’akasema halafu akamgeukia docta na kusema
‘Yule pale
unamfahamu sana, ni docta wako mshauri na nasaha, na yule pale ni jamaa yenu wanhuko
kijijini…wote hao unawafahamu vyema, huna haja ya kuigopa, ila kwa hawa wawili
labda ndio watakuwa wageni kwako, lakini ….sio wageni….’akatulia akituangalia….’hapo
akasita kidogo, halafu akasema
‘Ni wageni
usoni kwako, lakini ni wenyeji wako , kwani walishakufahamu kutokana na taarifa
uliyowatumia..’aliposema hivyo, mdada akainua uso kutuangalia kwanza alitutupia
jicha la haraka, akainama lakini baadaye akainua uso na kutuangalia vyema.
‘Labda nia
yako uliwatumia hiyo barua pepe, ukitaka iwe siri, labda hukutaka ifahamike
kwetu…, lakini kutokana na haya yaliyotokea imekuwa sio siri tena,…kuwa imetoka
kwanani, au sio,… labda kama wewe mwenyewe utasema wasiandike chochote tunaweza
kuwazuia, hili tutakuachia wewe na wao, mtakavyoaminiana na kukubalianai….eti
nyie waandishi, sizani kama mumeshaiweka hiyo habari yake hewani….’akasema
akituangalia sisi.
‘Bado….’tukasema
‘Hawa ni
watendaji wa diary yangu, natumai unawafahamu sana kimtandao…wewe uliwatumia
barua pepe, ukitaka waweke hewani, ili watu, au ….wasome’aliposema hivyo mdada
akainua uso tena kutuangalia, na baadaye akiinamisha kichwa chini.
‘Utashangaa
kwanini wamekuja kukuona,….wao baada ya kupata ujumbe wako, au taarifa
uliyowatumia, kwa haraka walifika hospitalini wakitarajia kuwa watakukuta na
kukuokoa…’akasema na mdada akainua uso tena kutuangalia
‘Kuniokoa…lini
walikuja…?’ akauliza
‘Najua
utashangaa hivyo, hata sisi tumeshangaa vilevile, kwa
vipi waje kukuokoa, ….wakayi tukio hilo lilitokea muda… ni wiki ya tatu sasa
zimepita, inakimbilia mwezi, hawa ndio wanaonekana kulikoni…’akatulia
‘Labda ni
kwasababu ya mtandao, …ndivyo ilitakiwa au inatakiwa ionekane hivyo, bado
tunachunguza….ila kiukweli taarifa yako ilichelewa kuwafikia kwa wakati
muafaka,..na wao walijua kuwa ni tukio la siku hiyo kumbe muda
ulishapita…’akatulia
‘Sasa wao
walikuwa na haja sana ya kuonana na wewe, kuongea na wewe, kukuuliza maswali
kujua unaendeleaje…hatukupenda watu wakusumbue tena na tena, lakini kwa ajili
ya hili,..tukaona ni bora tulimalize hivyo, kwani kutokana na wao, pia wataweza
kusaidia watu wasiendelee kukufuatilia, maana wakiiweka hewani taarifa yako
kila mmoja atakuwa na hamasa ya kukuona, na kujua ni nini kinachoendelea…’akatulia
‘Labda
niwaachie wao wakuulize maswali, kabla hujasema lolote , …’akatulia
akituangalia
‘Pole sana
mdada kwa mitihani iliyokupata, …kiukweli tuliposoma kisa cha maisha yako, sote
tulijiukuta tukitoa machozi, hatujui tukikiweka hewani wengine itakuwaje, na
hatutaweza kukiweka hewani mpaka wewe mwenyewe utupe idhini yako, japokuwa
ulisema tukiweke hewani ili huyo mlengwa aweze kujua…’nikatulia nilipoona
anataka kusema neno, lakini alikaa kimia
‘Tulitaka tukuwahi kwanza…kukuokoa, ikiwezekana.’akasema
mwenzangu, na mimi nikaendelea kutoa maneno yangu
‘Maisha yana
changamoto zake, na milango ya kutokea kwenye hizo changamoto inatofautiana,
mingine ni migumu sana kufunguka, na hata ikifunguka inaweza ikawa na
changamoto nyingine milango mingine zaidi ya kufungua….ili ufike kuzuri zaidi,
lakini hatutakiwi kukata tamaa, kwani mwisho wa yote ni ushindi.’nikazidi
kumwambia.
Na mwenzangu
akaendelea kusema;
‘Tunajua
umepitia machungu mengi, na hata kufikia kukata tamaa, kutaka kujiua….hebu
tujiulize ni nani hatakufa, kila mtu atakufa, kwa siku yake maalumu, kama ni
hivyo ni kwanini ulazimishe kufanya hivyo,…’akasema na mimi nikasema
‘Nii kweli
kama kila mtu atakufa basi kila mtu inambidi kuisubiria hiyo siku yako huku
tukiomba iwe njema, tuombe mwisho mwema, na sio mwisho mbaya utakao kuwa
ushahidi wa kuingia motonu,…hivyo basi kila mmoha wetu anahitajika kuwa na
maandalizi ya matendo mema, na kama ukiteleza, ukafahamu jirudi, tubia, na tena
mema….’nikasema
‘Ni
kweli,…mkuu, ..mdada niongezee hapo, kuwa,
sisi sote ni wasafiri, hapa duniani ni kituoa tu cha kupumzikia, …,
tukumbuke kuwa safari hiyo haina kurudi, je una masurufu gani…..hilo nimuhimuu
sana tukajiuliza….tunakuambia haya ili moyo wako ujae imani, imani ya kumuogopa
mungu…’akasema mwenzangu.
‘Swali letu
ni kwa hivi sasa maana mengi tumeshayafahamu, je ni
kwanini ulifikia hatua ya kujiua, baada ya ushauri nasaha, na hata wewe
mwenyewe kuonekana kukubali …..je ni kwasababu ya shinikizo au ni kutokana na
hizo nakama za maisha….?’ Akauli mwenzangu alipoona nataka kuzidi kuongea.
Mdada alitulia hakujibu kwa haraka ni kama vile
alikuwa akifikiria cha kuongea,…, alikaa kimia kwa muda, na mimi nikasema
‘Mdada ujue
kuongea, ni sehemu ya kujisaidia …na ukiongea unapunguza mzigo uliopo moyoni
mwako, sisi hapa tupo pamoja na wewe, ….na hilo la kuambiwa sikio la kufa, ni
namna ya kukukatisha tamaa,….sisi tunaamini, kila tatizo lina ufumbuzi wake, na
sisi hata kuja hapa ni kutaka kushirikiana nawe kutafuta dawa hadi sikio hilo lipone na kama ni kufa iwe na kwa
uwezo wake mungu, kapanga iwe hivyo….’nikasema na nilipotamka hivyo `sikio la
kufa’ akainua uso na kuniangalia, akasema
‘Dawa gani
ya sikio la kufa..kama ni la kufa, ni la kufa tu…jamii ilinitenga, wazazi na
kila niliyewahi kukutana naye alinisakama kwa hili au lile, kisa eti mimi
nimekuwa mhuni, ‘Mimi nimetwika sifa ya uMalaya…..nilijiuliza sana kwanini
mimi…ni umalaya gani nilioufanya ambao haujawahi kufanyika…sijui, labda mimi
nilitembea uchi barabarani nikijiuza…na mimi sikufikia huku…yote yaliyotokea ni
kwa mitihani tu….sikudhamiria, ndio sikuwasikia wazazi wangu awali, nilikuwa
nikikaidi, lakini ni kutokana na upendo wangu kwa aliyekuwa mchumba wangu, yeye
ndiye sababu…..’akatulia na kuanza kulia, baadaye akatulia
‘Mchumba
wangu nitamlaumu sana kwa haya yote, aliniaminisha akanifanya nimuamini….mungu
amsamehe……japokuwa marehemu hatakiwii kusemwa kwa mabaya, lakini yote haya
yasingelitokea kama isingelikuwa ni yeye…’akasema na sisi tukadakia
‘Ina maana
mchumba wako ameshafariki…?’ tukauliza
‘Ndio ni
marehemu kwa hivi sasa….ndio hiyo ninayosema toka lini sikio la kufa likasikia
dawa, mimi najua yeye kaondoka na sisi tupo nyuma yake,…tutakwenda wengi kwa
hilo…., najua na mimi nipo njiani, lakini hata huyu kiumbe wa watu, ana hatia
gani ….’akatulia akijizuia kulia
‘Usijali
mdada, kutokana na vipimo vyako, asilimia kubwa ya hiyo sumu imeshaondolewa…na kwa
taarifa tu mtoto hana tatizo, yeye dawa zimefanya kazi haraka na inainyosha
hata kuwa na tatizo hilo tena, ila inahitajia ufuatiliaji, na vipimo, vya mara
kwa mara…, ‘akasema docta
Mdada
akatikisa kichwa kutokukubaliana na yeye na docta akaendendelea kusema;
‘Mdada hilo
nakuthibitishia, nimekaa na wataalamu wenzangu, wamesema kuwa kwa hali uliyo
nayo…, kama utaendeela hivyo hivyo, ukafuata matibabu, na masharti,…dawa za
kurutubisha kinga, utapona
kabisa….’akasema mshauri nasaha.
‘Hahaha…ugonjwa
wa upungufu wa kinga upone hiyo dawa iligunduliwa lini, au mnanifanya mimi ni
mjinga,…mnanipa matumaini ya kuishi au sio…, sawa, nitaishi kwa matumaini, kwa vile
siku zangu hazijafika, lakini msinidanganye kuwa nitapona…’akasema akitikisa
kichwa kukataa
‘Tunaosema
hivyo ni sisi wataalamu, ujue ugonjwa huo uliona nao, ni wa kutengenezwa, sio
sawa na ugonjwa huo wa kawaida, hawa watu ni wabaya sana, hata ma vyakula haya
tunayokula ya makopo, tuwe makini nayo sana…’akasema docta
‘Na hata
hivyo mdada ukumbuke hata huo ugonjwa wa
kawaida wa kupunguza kinga za mwili siku hizi una dawa za kupunguza makali yake
na watu wengi wamefikia hatua ya kupona…’akaambiwa.
‘Kupona!!!
Hayo nimeyasikia sana hapo kwenu…hata siamini tena…,eti jamani mliwahi kusikia
mtu kapona akipatwa huu ugonjwa…?’ akatuuliza na sisi tulibakia kimia, akasema
‘Najua…huwezi
kupona,ni kunipa moyo na matumaini tu….’hapo akawa analia halafu akatulia na
alipokuwa akilia sote tulikaa kimia, na yeye mwenyewe akasema
‘NI kwanini
ninalia,… kinachoniliza ni …ni huyu mtoto, kila nikimuangalia, nawazia mbali,
najiona mimi kama muuaji, nilitaka kukiangamiza kiumbe hiki kisicho na hatia,
sijui nitakuja kumueleza nini akiwa mkubwa, kama nitafikia huko…kama kweli
tutafika huko’akasema kwa huzuni akimuangalia Yule mtoto.
Docta
ushauri akasema;
‘Hayo
yasikutie shaka, kila kitu na wakati wake, na huyo mtoto, atakua na akisoma
vyema, akasikia huko ulipotokea atakusifia sana, kuwa wewe ulikuwa mama mjasiri
sana…muhimu kwasasa ujue huyo ndiye jembe lako, mtunze, mpende, na wala
usionyeshe hayo machungu mbele yake maana ukilia lia utamjengea huzuni moyoni
mwake…’akaambiwa
Kukapita
kitambo, tukiogopa kumuuliza maswali mdada tulitaka atulie kwanza na mwenzangu
akaukatiza ukimia kwa kusema
‘Samahani
mdada kwa kukuuliza hili swali tena,…Je ulitaka kujiua kwa shinikizo au kwa
hisia zako kuwa hutaweza kuishi tena?’ jamaa yangu akauliza hilo swali tena. Na
mdada akatulia kama anawaza halafu akasema
‘Hata sijui
niwaelezeje…ilifikia hatua nikahisi hivyo, …ndio ni kweli hawa watu walitutisha
sana, na nilijua hata nisipojiua wao watakuja kuniua tena kwa mateso makali,..na
zaidi wangeliwaendea wazazi wangu wakawatesa, hadi kufa…’akasema
‘Una uhakika
na hilo, kuwa huwa kweli wanakwenda kwa wazazi na kuwatesa?’ akaulizwa
‘Nyie
mnahitajia ushahidi wa moja kwa moja…ndio maana hawa watu wanawashinda, kuna
wazee wanauwawa kwa kusingiziwa uchawi, je ni kweli ni wachawi..?’ akamgeukia
ofisa upelelezi
‘Mliwahi
kulichunguza hilo vyema, ni wazee wa watu hawana hatia, maisha magumu mpaka
macho yanabadilika, eti kubadilka kwa macho, kubadilika kwa sura kutokana na
shida, inaonekana kweli ni wachawi…’akasema
‘Ina maana
ni wao wanasababisha hayo…?’ akaulizwa
‘Wanapotaka
kuua, kutesa, wanatafuta mbinu za kila namna , ili kuwe na sababu, ili
uchunguzi uamini hivyo, , ..lakini kumbe ni mbinu za hawa watu…wazee wanachomwa
moto, wanakufa kifo kibaya, cha mateso kweli mnachungaza hivyo vifo kwa undani…?’
akawa kama anauliza
‘Hamuwezi
….mtajifanya kuchunguza na wananchi kwa vile wameshahadaiwa kiakili na hawa
mawakala wao…mkiwauliza hawatakosa sababu….’akatulia
‘Na hata
hivyo….hii aibu ya haya yote,…..najua kijijini huko najulikana kwa jina baya
sana,…nakumbuka babu aliniambia, ukitaka kumuua mbwa kwanza umuite kwa majina
mabaya, ndivyo ilitokea kwangu,..kwahiyo pamoja na haya yote,mmh,
nilichanganyikiwa, niliona ni heri kufanya hivyo…’akatulia kidogo kama anawaza
jambo, halafu akasema;
‘Naikumbuka
sana siku ile, nilitaka kweli kutimiza dhamira yangu..
‘Kiukweli …nilishadhamiria
kutimiza hilo, sikuwa na kurudi nyuma…baada ya kuitoa ile bahasha yenye dawa,
…. ndio nikasikia mtu anakuja…kwa haraka nilitoa kidonge kimoja nikakiweka
kwenye ukucha, kuna jinsi tulifundishwa…’akanyosha kidole kidogo juu na
kukiweka mdomoni.
‘Kile
kidonge ukikiweka hapa kwenye ukucha, ikifika muda unakitumbukiza
mdomoni,…kinatotaka tu maana kikikutana na umaji maji kinayeyukia…hata sijui walivyoniokoa,
‘Ila kuna
kitu natilia shaka, …huyu nesi, ni kama aliniona, akajifanya hanioni, na
alipohakikisha nimeweka kidole mdomoni, ndio akanifuata na kunishikilia mkono,
akaita saidia…saidia…lakini sina uhakika na hilo…’akasema
‘Huna
uhakika kwa vipi..?’ akaulizwa
‘Kama
alikuwa ana nia ya kuniokoa, asingelifanya vile , hakutumia nguvu kunivuta
mkono…nashindwa kuongelea hili, …lakini, mhh, hata sijui, ngoja niache
tu…’akasema.
‘Usiwe na
shaka, hilo tunalifuatilia…’akasema ofisa upelelezi
‘Unajua Ile
dawa, ni kidonge kidogo sana, ukikifikisha mdomoni, kinayeyuka, na kuteleza, kwahiyo
kitatoka kwenye ukicha na kuingia mdomoni,…i…sasa pale, nahisi wakati nainua
mkono…nahisi ni kwa vile…, mkono ulikuwa na maji maji ya jasho…kwahiyo nahisi
kilidondoka kabla hakijafika mdomoni…nahisi hivyo, …’akasema
‘Kwanini
unahisi hivyo…?’ nikauliza
‘Kwahiyo ilikiona
kikidondoka chini..?’ mwenzangu akauliza
‘Sikukiona
kikidondoka, muda huo nilishafumba macho…, ila kwa vile kidole kilipofika
mdomoni, sikuhisi hiyo dawa, ulikuwa ukicha tu.. na nikahisi hakijayeyuka, …ila
nina uhakika wakati nainua mkono ili niweze kulifanya hilo tendo, nilikiona
kikiwemo kidoleni….sasa kilikwenda wapi, kama kweli hakikudondoka
chini…’akasema
‘Na bafuni
kulikuwa na maji , kama kilidondoka kitakuwa kiliyeyuka na kupotelea kwenye
maji, tulichunguza hivyo, lakini hatukuona dalili hiyo…’akasema ofisa
upelelezi.
‘Kwanini
sasa mlichunguza…kwani mlikuwa na uhakika kuwa hakukimeza…?’ tukamuuliza ofisa
‘Ni kawaida
ya uchunguzi wetu kuchunguza kila kitu…na wakati wengine wanamchunguza watu wa
huduma za kwanza na madakitari waliendelea kumchunguza mdada kuhakikisha
tunawahi kumuokoa, …lakinii hakukuwa na dalili za dawa yoyote….’akasema
mpelelezi
‘Na
tulivyoona hivyo, tukaingiwa na hamasa ya kuchunguza eneo lote, ….’akasema
‘Mdada aliwaambiaje kuwa alishakunywa hiyo sumu au la, hakuweza
kutoa ushirikiano…?’ akaulizwa
‘Kwa muda
huo alikuwa kama kachanganyikiwa, hakutaka kusema chochote, alikuwa kimia
tu…’akasema docta
‘Kwa hali
kama ile, tulichelea kumfanyia upasuaji,…tukasubiria hadi siku ya pili
yake, na siku zote zote hizo alikuwa
kimia, haongei…. lakini wenzangu walipompima na kuona hana shinikizo, hana
tatizo lolote wakasema wanaendelea na huduma za upasuaji…ikafanyika hivyo, na
upasuaji ulifanikiwa….’akasema docta
‘Kwa kifupi
ni kuwa mdada hakufanikiwa kukimeza hicho kidonge…?’ nikauliza
‘Hakufanikiwa….hilo
tuna ihakika nalo kabisa, kama angelikimeza asingelichukua muda angelikata
roho…vile vidonge vimechunguzwa, ni hatari ….na dalili zake za mwanzo, muathirika
au muhanga anatoka na mapofu, lakini hayakai muda, yanakauka kwa haraka
sana..ukifika huwezi kugundua kitu, tulipofika kumuokoa, hakukuwahi kutokea
kitu kama hicho….na ni muda mfupi sana!
‘Au nesi
alichelewa kuwaita…’akasema mwenzangu
‘Hapana…tuna
uhakika hakukimeza…nawaambia ile ni simu kali, inakimbilia haraka kwenye damu
na kukata mawasiliano ya mapigo ya moyo’akasema docta
‘Kwanini
mdada uliamua kukimeza hicho kidonge huko bafuni..na usisubirie ukiwa
kitandani?’ akaulizwa
‘Nilishahisi
kuna kitu kinaendelea, nikahisi huenda wameshanishtukia, kuna sauti iliniambia
nifanye haraka kwani wanataka kunizuia, nikumbuke wazee wangu watateswa. Huyu
mtu alikuwa ni nani..’akawa kama anauliza
‘Kuna mtu,
au sauti au hisia zako…?’ akaulizwa
‘Hata mimi
sijui.. ndio maana nasema huenda hata humo hospitalini wapo hao watu, sizani
kama ni sauti za majinamizi, au hisia zangu tu….ndio maana nikaona bora
nijikate mwenyewe kihivyo, niende nikajipumzikie kama huko kuna kupimzika…’akasema
‘Una maana
gani kusema kuwa huenda hapo hospitalini wapo hao watu?’ akaulizwa
‘Kila usiku
kuna mtu alikuwa akinijia na kunitishia,…’akasema
‘Huyo mtu
mwanaume au mwanamke, ni docta au ni nani,..?’ akaulizwa
‘Kiukweli
siwezi kusema ni nani…maana inavyotokea inakuwa kama naota, mtu ananiambia
jambo, kwa sauti nzito, lakini cha ajabu …nikiamuka simuoni huyo mtu, ….’akasema
‘Unasikia
sauti kabisa..?’ akaulizwa
‘Nasikia
sauti kabisa nikiwa usingizini, sizani kama ni ndoto…na jingine…’akatulia kama
anasita kuongea
‘Na jingine
lipi…?’ akaulizwa
‘Jamani hebu
jiulizeni hata nyie, ni kwanini hiyo barua pepe haikufika kwa hawa watu kwa
wakati muafaka, mna uhakika kweli, kuwa ni tatizo la mtandao….lakini mimi
sijui, labda ni hisia zangu tu…’akasema
‘Hilo
usijali tumelifanyia kazi, hebu tuambie, kuna Jambo jingine lolote linakufanya
uhisi kuna watu humo hospitalini, au…, wewe sema tu usijali…?’ akaulizwa na
mpepelezi, na mdada alionyesha kama kusita kuongea
‘Na kwanini
nilielekezwa niende kwenye hiyo hospitalini…na wakati kule hospitalini walisema
nipelekwe muhimbili. ….’akasema akimuangalia mpelelezi halafu kwa haraka
akamtizama docta mara moja na kugeza kichwa kumuangalia mpelelezi.
‘Yawezekana
waliokuelekeza huko wanakifahamu kituo hicho kuwa taasisi inayohudumia wagonjwa
wa namna hiyo kwa haraka…’akasema mpelelezi
‘Mhh…mimi
nimejiuliza sana hilo swali, sijui nyie wenzangu, labda ni sawa ni hivyo,
waliona hivyo…au ndio imetokea tu, labda ni hisia zangu tu, ila inanipa maswali
mengi yasiyokuwa na majibu…!’akasema na dakitari mshauri akatikisa kichwa kama kuonyesha
kuwa mgonjwa hajakuwa sawa.
‘Hebu
nikuulize ni nani alikuwa mara kwa mara akikuhudumia pale hospitali, ambaye
mara kwa mara alikuwa nawe …?’ akaulizwa
‘Kuacha
docta..au?’ akauliza na hakusubiria kujibiwa akaendelea kuongea
‘Mtu ambaye
alikuwa yupo name nami mara kwa mara ni nesi,…huyo alikuwa anaonekana kila mara
mle ndani…na ikitokea tatizo huyo nesi huwa anamuita Yule dakitari
msaidizi…’akasema
‘Je hiyo
sauti unayosema inatokea ya kukutisha kuwa ujiue,…. ni sauti ya kike au ni ya
kiume?’ akaulizwa
‘Mhh, ni
vigumu kusema, maana ni sauti nzito, ya kiume, lakini wakati mwingine nahisi
kama ni sauti ya kike ila anailazimisha iwe nzito kama ya kiume, …si unajua
…lakini huyo hata kama ni mwanamke, basi atakuwa na sauti nzito ya kiume ume
hivi…’akasema
‘Mhh,
kwanini unasema hivyo..?’ akaulizwa
‘Kwanini iwe
kama ya kulazimisha,…unajua mwanaume akiwa na sautii yake nzito, hahitajii
kulazimisha iwe nzito zaidi,…sasa huyo anakuwa kama anailazimisha zaidi isikike
kama ya kutisha…’akasema na docta mshauri akataka kusema neno, halafu akaacha
akamuangalia ofisa upelelezi
‘Unajua kuna
kitu kitu nimekikumbuka,….’akasema
‘Kitu gani….?’
Akaulizwa
‘Unakumbuka
tulivyoongea siku ile….haiwezekani ikawa hivyo…?’ akauliza na mwenzake
akatikisa kichwa kaka kukubali.
‘Basi ngoja
nihakikishe kitu….’akasema na kuchukua simu, akapiga namba , na kuanza kuongea
kwenye simu.
‘Huyo nesi anayehudumia wagonjwa mahututi
yupo?’ akauliza na kusikiliza
‘Kaenda
wapi, dharura gani imempata, ok mimi nilikuwa sijui maana leo nimepitia huku
kituo cha polisi moja kwa moja…, ok sawa….?’akakata simu akamgeukia ofisa
upelelezi, na kusema.
‘Unajua huyo
nesi ana sauti nzito, na siku moja aliwahi kunitisha kwa kuongea sauti nzito
kama ya kiume nikiwa nimeinama bila kumtizama, nikajua kweli ni mwanaume
anaongea....na mdada alipoongea hivyo…nikashtuka kidogo, ..hata hivyo nesi huyo
ana dharura kaomba ruhusa ya siku kadhaa….’akasema docta
‘Usijali
docta, hilo limeshafanyiwa kazi, vijana wangu wanafuatilia, hatutakiwi
kuharakisha haya mambo…na kwa safari hii, wote wanahusika watakamatwa,..wengine
ambao watashirikiana nasi tutawashikilia tu kwa usalama wao…, docta, tupo
pamoha, wewe utapata taarifa badaye…’akasema ofisa upelelezi, na docta akawa
sasa kama hana amani fulani hivi.
Sisi pale
tukawa tunaangaliana, ni nani aulize swali kwani mambo yalikuwa yakiongezeka,
na mlengwa wetu ni mdada, hatukutaka kuingilia kazi zingine….na ofisa Upelelezi
akasema;
‘Kwa ujumla
tatizo hili ni kubwa sana, kinyume na Inavyofikiriwa…inahitajia muda mrefu sana
wa kulimaliza, ngoja tuone hii awamu, awamu ya kazi, wengi wataibuliwa…’akatulia
akiangalia saa yake
‘Ni sawa
tunakuunga mkono kwa hilo, lakini ni kama hao watendaji wenye dhamana watakuwa
kwa ajili ya wananchi, wawe karibu na wananchi na kazi iwe kazi kweli,…maana
pia hawa watu wabaya wana mbinu nyingi ni wajanja sana,…sasa hivi
wameshajigeuza na hutaamini , kwa ujanja wao wameshajipenyeza kwenye `system’
lakini nina imani kuwa watagundulikana tu, …’akasema docta
‘Unavyoongea
hivyo ni kama vile mnawafahamu…’akasema mwenzagu
‘Kwa tabia
zao…mali walizonazo…wewe fikiria wamewekeza hadi nje, wana dhamana za benki
huko nje…walipata wapi hizo pesa, tukianza kurudi kinyume nyume tukachunguza
nyendo zao…watajulikana tu hebu jiulize kwanini viwanda vingi vya serikali
vilikufa ni nani walikuwa wakurugenzi, na sasa wana nini,….yaonekana kabisa
ilikuwa ni mbinu ya kujinufaisha…’akasema docta akimuangalia ofisa na ofisa
akaitikisa kichwa kama kukubali
‘Sasa
kwanini hawakamatwa, ni kwasababu kila jambo na wakati wake…, kulikuwa na uhuru
wa kuwekeza, ukaja wa kulipa kodi, ukaja wa miundo mbinu sasa ni kuwajibika….ni
hatua hizo za utekelezaji….nyie mtaona tu, waaminini viongozi wenu’ akasema
ofisa mpelelezi
‘Mimi nina
wasiwasi..,maana kila awamu, sio kwamba hawa watu wamelala,wao wanajua ni nini
na nani atakuwepo ….wameshajipanga, na watu wao wameshatayarishwa…sasa sijui
mtawabana kwa mbinu na ushahidi gani…’akasema docta
‘Ushahidi
sio lazima…ila matukio kama haya ndio yatatusaidia, tunajua hawa watu ni
matajiri,wana pesa, wana mawakili wao, na ukumbuke na tunajua kuwa kuna watu
wao pia wanawabeba, wamewekeza kwa hilo, na watu waliosoma sana , huwezi
kuwatilia mashaka,…na ndio maana kesi
zinakuwa ngumu sana na hata kutukatisha tamaa….lakini wakuu wamejipanga
kwa hilo, maana hawa wakuu wa sasa wametoka wapi, wanawafahamu, walikuwa
wakiumia sana, na sasa wamepata nafasi ya kuwabana, ni swala la muda tu…’akasema
‘Haya sisi
tutawasikiliza nyie, hasa watu wa usalama, muwafichue, na muhakikisha
mnawawajibisha mkifanya hivyo kila mtu ataogopa, na nchi haitakuwa shamba la
bibii tena, lakini bado, bado…’akasema docta akisita kuendelea
‘Ni
kweli….ila tutambue hii kazi sio ya viongozi peke yao, ….kila mtu asiogope
kufichua haya maovu, maana wavumao baharini ni papa,…lakini samaki wengine
wapo…..swali ni nani ni nani, kama alivyosema mdada , hawa watu ni waigizaji wakubwa, wanakwenda na
nyakati, hivi sasa wameshavua ngozi zao , ni watakatifu kweli, wachapakazi wa
kikweli ukiwaona, na wanajifanya kutetea watu, hutaweza hata kumtambua yupi ni
yupi, ….’akatulia kidogo
‘Mimi naona
huu muda serikali ingewashirikisha wananchi, wananchi wanawafahamu sana hawa
watu,…kama kutakuwa na namba fulani za kura za siri…mnaweza kupata msaada
mkubwa…majambasi wanaishi na watu, achilia mbali hao mafisadi ambao sasa wana
maeneo yao tofauti wamejenga mahekalu yao, lakini wanajulikana,……..’akasema
jamaa yangu
‘Sheria ina
namna yake, kushuku ni kitu kingine, na kuwa mkosaji ni kitu kingine, sisi kama
wapelelezi tunafanya kazi yetu na tunajua ni nini tunachokifanya, …ni kweli
kuna changamoto zake maana haya hayakuanza leo, ushahidi, ukiupata unakutwa
umeshachakachuliwa, na siwezi kukataa, hata huku kwetu hao watu wapo, lakini
hatua kwa hatua tutalimaliza…’akatulia akiangalia saa yake
‘Kila mtu
analishaona kumbe, …..ujanja kuwahi, kumbe…na mimi nikizubaa nitakosa, kila mtu
akawa anachukua chake mapema,wakawekeza watoto wao kwenye elimu, shule za
kimataifa..ili waje kushika madaraka…. Kwahiyo huu ni mtandao mpana, na ndio
maana hivi sasa huwezi kuwabaini tena wamaeshajibadili kabisa,….ngozi ya
kondoo, hili ni tatizo sugu….’akasema
‘Lilikuwa
kama kama sikio la kufa,…’akasema docta akimuangalia mdada na wakati huo ,mdada
alikuwa kama hayupo, alionekana kuwaza mbali
‘Lakini
niwaambie kitu,…`system’, mfumo ni tatizo kubwa ….’akatulia, hata hivyo
tusikate tamaa, ni tatizo lakini linaondokeka, na hili ni rahisi sana, kwa mwananchi wa kawaida kuliondoa kama
watakuwa na umoja, huyu mtu wa kawaida akiamuka, akajitambua, akajua haki yake
ni ipi, mabadiliko yatakuja tu….na viongozi wa kweli watatokea huko…kwa mwananchi wa kawaida
anayejua shida,….’akatulia pale mlango ulipogongwa.
Mara akaja
mtu akasema
‘Mdada
anahitajika kwenye taratibu zako za dawa..’
Na mdada akabakia
amekaa, akageuka kutuangalia, na kusema
‘Ahsanteni
sana wanandugu, najua mumetoka huko mbali kuja kuniona, kuja kunisaidia, lengo
lenu lilikuwa jema, …japokuwa,….’akasita kuendelea
‘Hatukufanikiwa
kufika kwa wakati….’akasema mwenzangu
‘Lakini sio
kusudio langu kuwa mfike kwa wakati, kuja kuniokoa, nilitaka huo ujumbea ufike
kwa mlangwa….hata hivyo, imanipa faraja kuwa bado wapo watu wenye huruma,
nawashukuruni sana kwa hilo. Na kwa ajili hiyo, nimeridhia …. muiweke
hewani, ili watu wajifunze kutoka
kwangu…nataka jamii ielewe mambo yaliyojificha nyuma ya pazia….’akageuka
kumuangalia ofisa upelelezi.
‘Huko
uraiani hali ni mbaya,…na hii ni kutokana na maisha magumu, wenzetu mjini wana
huduma zote muhimu, kijijini zippo wapi, hata umeme ni shida, barabara mbovu,
maji tunategemea chemu chemu au kwenye mabwawa machafu tunapokezana na mifugo
…..mnajua wenyewe hali ilivyo, …
‘Kwahiyo,
watu, hasa vijana wakisikia watu
wanatoka, wana maisha mazuri, magari, nyumba nzuri, …wanakuwa na hamasa ni kwa
vipi, ni sababu ya kazi za ofisini, au ni sababu ya sanaa, muziki, urembo, au
..basi wanavutika kuiga,…’akatulia kama anawaza jambo
‘Ni kama vile
unavyoangalia kwenye sinema ukavutika na ‘stelingi’, zile sifa zake, ushupavu
wake, au utajiri wake au muonekano wake, basi kila mtu atapenda kujiigiza kama
yeye, japokuwa ni kuigiza tu,…ni hivyo,…’akabenua mdomo idogo
‘Na maishe
yetu huko kijijini, ndio hivyo, watoto,
vijana ni ya kuiga iga tu, kila mmoja anatamani kuja huku mjini, na hili la
kuiga iga, sio huko kijijini, tu…nadhani hata huku mjini, ndio hivyo hivyo, au
nadanganya, huku wanataka wawe kama wazungu, au sio…..si-unaona watu walivyo,
wanaiga hata kuvaa uchi, hatuwezi kuiga kutengeneza magari…kwasababu hakuna
vifaa, mhhh, ….’ Akajitahidi kutabasamu
‘Ni kutokana
na maisha…wenzetu wamewahi,….na wanataka kuendelea kutunyonya, sasa wafanye
nini, wanabuni mbinu, wakagundua kumbe… wanaweza kuwekza jambo kwenye hali hiyo,…wajanja
kweli kweli wakabuni hayo madawam ili kutumbaza akili,…’akatugeukia
‘Kama mungu
atanijalia nikapona na mwanangu, na mimi nitajitahidi…, nije tuungane kuielimisha
jamii kuhusu haya yaliyonikuta…mungu akipenda
‘Lakini
jamani kwa hivi sasa sitaki kabisa mtu kunifuatilia,…niachane, haya
ninayopambana nayo yanatosha, kwasababu hapa nilipo bado nipo kwenye mapambano,
ya kufa au kupona,..na sijui kama nitapona…ni kunipa matumaini tu….na huyu
mwanagu….’akamwangalia mtoto wake
‘Utapona tu
mdada,….haya yote utayasahau….’akasema docta
‘Mungu ndiye
anajua zaidi, …mimi na mtoto wangu, tupo kwenye ukingo wa kaburi, kwahiyo,
tumuombe yeye, akijalia, kama nitaishi, ….nitawatafuta,…’ akasema huku akimwangalia
mtoto wake, na docta ushauri akamkatiza akisema….
‘Jipe moyo
mdada,…sote tupo kwenye ukingo wa kaburi, hakuna anayejua ya kesho, mungu pekee
ndiye ajuaye hayo, lakini kwa mwanadamu, hatutakiwi kukata tamaa,..muhimu ni
kujipa matumaini, kuwa nitaishi, nitaiona kesho na kesho kutwa na hata miaka
ijayo, kama vile utaishi milele, usikate tamaa, na pia kumuomba mungu ni wajibu
tumuabudu mungu kama vile safari imewadia, yote ndiyo maisha ….’akasema
akionyesha mikono juu
‘Kwa hivi
sasa mdada, Inatosha, umesikia ulivyo ambiwa, hivi sasa unahitajika kwenda
kwenye dawa, ….’akasema docta na yule mwanadada mwingine akasogea na kumchukua
mtoto, wakatangulia kuondoka, na baadaye Yule ofisa upelelezi akatugeukia na
kusema
‘Na nyie mpo
huru kuondoka..’ akasema na hatukuwa na zaidi, tuliwashukuru na kuondoka.
MWISHO
WAZO LA LEO: Maisha ya mwanadamu ni kupambana na
mazingira, kuhangaika, kitafuta, kama vile tutaishi miele, lakini kwa njia
zilizohalali, na wakati huo huo, tunahitajika kumcha mola wetu, kumuabudu yeye
na kumshukuru kwa neema alizotupa kama vile hatutaiona kesho. Yote ndiyo maisha
yetu. Tusitende yasiyo haki na kujaa
kiburi.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Ndugu wa mm kid a kimetupa fundisho sana na changamoto nyingi alopitia huyu dada namuomba awe strong mungu yupo
Tupo pamoja
Tupo pamoja kwa saana
Post a Comment