Bro, hutaamini kesi ilianza kupigwa
dana dana, kila siku inaahirishwa kwa kisa hiki na kile, mimi nasota huko
gerezani, nateseka,...niliumizwa, niliteseka,
nikanyanyasika,
nikazalilika,..sijawahi maishani mwangu, na ilifikia muda sasa nikasema nikipa
sumu najiua...’akasema mdogomtu
‘Lakini si ulisema alipofika mama
mtemi alisema kuwa keshaweka mambo sawa na wakili wako akasema kesi iliyobakia
ni ya kawaida tu, sasa tatizo lilikuwa wapi, au ndio ulikuwa unalipa dhambi za
watu...?’ akauliza kaka mtu.
‘Kwaweli hata mimi sikuelewaa...kuna
muda nilikuwa naitwa mahakamani kesi inatajwa, inatolewa sababu fulani kuwa
shahidi muhimu hayupo, mara kuna uchunguzi haujakamilika,...ikawa ndio
hivyo,nikitaka kuongea na wakili wangu, ananiambia atakuja gerezani, ikawa ni
kupigana chenga,....walichokitaka wao wamekipata wanahitajia nini
tena...’akasema mdogomtu
‘Hali yangu ya kiafya ikawa mbaya
sana, nikawa naumwa, na hata wakati mwingine kupoteza fahamu, na kuna muda
waliona kuwa mimi ni mtu wa kufa tu, kwani nilikuwa nimebadilika na kuwa na
sura ya mfu...walipoona hali yangu ni ,mbaya sana, ndio nikapelekwa kulazwa
hospitali ya uraiani,huku nikiwa chini ya ulinzi...’akasema mdogo mtu
‘Siku zikaenda,siku zikapita,..karibu
mwaka kukamilika..simuoni mama mtemi, hata wakili nilikuwa nakutana naye
mahakamani, ....’akasema mdogo mtu
‘Je kijana wetu...?’ akaulizwa
‘Huyo ndiye hata hakutaka kusikia
nikitajwa mvele yake... eti nimemchafulia jina lake...’akasema
Tuendelee na
kisa chetu..
******
‘Ndugu
hakimu, tunasikitika kuwa kesi hii imechukua muda mrefu sana....’akaanza
kuelezea muendesha mashitaka walipofika kwa hakimu
‘Kutokana na
mambo yaliyojitokeza tumeona tuje mbele yako kwa mapendekezo ambayo tunaona
yatawezesha kuimaliza hii kesi,na hili tatizo katika jamii zetu..’akasema
muendesha mashitaka.
‘Kwani kuna
tatizo gani, hebu niambieni...hili hatuwezi kulivumilia kesi kuchukua karibu
mwaka sasa, kuna tatizo gani?’ akauliza hakimu na muendesha mashitaka akiwa na
mpelelezi,akasema...
‘Ndugu
muheshimiwa hakimu, kesi hii imetuchanganya sana,...na kilichotuachanganya
zaidi ni kuhusu mambo yaliyokuja kujitokeza baadaye, tumegundua matukio mawili
ya kamera za nje, zikionyesha watu wawili wengine tofauti...’akasema
‘Na watu hao
hawakuwepo kabisa kwenye mashitaka yetu, lakini kutokana na ushahidi tuliouata
tumegundua kuwa ni wahusika,....’akasema
‘Walionekana
wakitokea ndani wakikimbia kama alivyoonekana mshitakiwa wa awali kwa upande
mwingine wa nyuma, ...lakini tofauti na mshitakiwa wao hawakuwa na silaha,
lakini kwa uchunguzi wa ndani kama alama za vidole, ilionyesha dhahiri walikuwa
ndani ya chumba alipokuwepo marehemu..’akasema mpelelezi
‘Tumefuatilia
hilo na uchunguzi huu mpaya umetupa uhakika kuwa watu hao wanaweza kuhusika na
mauaji hayo, kwa hivi sasa mmojawapo tunaye, na kakiri kuwa alikuwepo kweli kwenye
chumba alipokuwepo marehemu, na kwanza aliongea naye akaondoka, na aliporudi
mara ya pili akakuta mwili wa marehemu ya kuwa alishauwawa ....’akasema
‘Na yupo
mwingine huyo yeye alikimbia nchi, kwa hivi sasa hayupo hapa nchini, aliwahi
kukimbia mapema... yeye tuna imani anaweza kuwa muhusika mkuu....’akasema
‘Ni nani
huyo....?’ akaulizwa
‘Huyu alikuwa
mmoja wa walinzi wa kujitegemea, amekuwa akikodiwa kufanya kazi hizo za ulinzi na
watu tofauti na mara ya mwisho alikuwa akimlinda dada mmoja aliyekuwa muhudumu
wa hoteli,dada huyu alikuja kurubuniwa na mshitakiwa wetu na wakafanya mipango
ya mlungula ambayo ndiyo iliyosababisha hadi marehemu kuuwawa...’akasema
mpelelezi
‘Yeye na
huyu binti waliwahi kutoroka nchini, na kiasi kikubwa cha pesa, na
tulivyofuatilia tumegundua pesa hiyo ndiyo hiyo ya mlungula....’akasema
mpelelezi
‘Tumekuwa
tukiahirisha hii kesi mara kwa mara ili kuwapata hawa watu tukiwa
tunawafuatilia ili kujua wapi walipo, lakini cha ajabu, hawakuwahi kufika huko
nchini kwao ambapo tulifikiria ndipo walipokimbilia..., na hii imetupa mashaka kuwa,
yawezekana hawa watu walibadili safari wakiwa njiani tofauti na nyaraka zao
zilivyoonyesha kuwa walikuwa wakirudi nchini mwao ...’akasema
‘Inawezekanaje
hao watu watoweke kihivyo, ....maana siku hizi kuna utaalamu wa kufuatilia
nyendo za mtu kwa njia ya mitandao, wanapotoka hapa hadi huko wanapokwenda,
imekuwaje hawa watu wasipatikane kwa harakai...?’ akauliza hakimu.
‘Hawa watu
walitoroka na pesa nyingi sana,...kwahiyo walipofika sehemu ya kubadili ndege,
hawakufanya hivyo, wakitumia pesa zao, waliingia kwenye nchi ya jirani, na
wakatumia usafiri wa kawaida, au meli kwenda nchi nyingine,lakini bado
tunawafuatilia,watapatikana tu muheshimiwa hakimu...’akasema mpelelezi.
‘Sasa kuhusu
huyu mshitakiwa na wenzake mumefikia wapi?’ wakaulizwa
‘Kuna wahanga
wengi wa kuthibitisha kuwa wahalifu hawa wamekuwa wakifanya hiyo biashara ya
mlungula...,na sasa wahanga hao wamekuwa tayari kuelezea ilivyo kuwa....’akasema
mpelelezi.
‘Wapo tayari
kusimamishwa mahakamani....?’ akauliza hakimu
‘Hapana
muheshimiwa hakimu,ndio maana tumekuwa tukiahirisha hii kesi mara kwa mara ili
kuona jinsi gani ya kulimaliza hili tatizo bila ya wahanga hao kupata madhara
kutokana na mitego waliyotegewa....’akasema muendesha mashitaka.
‘Mara nyingi
wahanga wa biashara hii huogopa kujitokeza, kutokana na kashifa iliyopandikizwa,kwani
huwa kweli wamefanya hiyo kashifa na ikijulikana wanaogopa kukosa ajira, kuvunjika
kwa ndoa zao,au kuadhirika kwenye jamii...’akasema muendesha mashitaka.
‘Na kutokana
na kesi hii wengi wametegewa kwenye matendo yanaoweza kuvunja ndoa
zao,...walinaswa wakiwa wamekiuka sheria za ndoa zao,na waliambiwa kama
wasipotoa pesa taarifa itafikishwa kwa wake zao, au waume zao, na wake zao , au waume zao, wanaweza kuvunja
ndoa... na ndoa hizo zina masilahi kwao’akasema muendesha mashitaka.
‘Na kama
tulivyokuambia awali tunajaribu kuangalia, jinsi gani ya kufanya ili tusije
kuingilia mambo binafsi, kwahiyo tumekuwa makini kuliweka hili hadharani,kutokana na maombi ya hao wahanga
ambao wamekubalia kushirikiana na polisi,ndio maana tumekuwa tukiahirisha
ahirisha hizi kesi,na kwa vile umetuita, tunaona ni wakati muafaka wakuliweka hili
wazi mbele yako muheshimiwa hakimu...’akasema muendesha mashitaka.
‘Je kwa
kufanya hivyo hamuoni kuwa mnahalalisha makosa yao ya kuvunja amri na sheria za
ndoa zao, na mnataka mahakama iwatete kwa hilo...?’ akasema muheshimiwa hakimu.
‘Muheshimiwa
hakimu tumeliona hilo,...lakini sisi tumeona kuwa , hayo yabakie kati ya
wanandoa wenyewe, tusikiuke ahdi tuliyoiweka kuwa wakijitolea kusema ukweli,
sisi tutajitahidi kuficha siri zao... kwani tukiwafikisha mahakamani kila kitu
kitajulikaa na hapo tutakuwa tumeshiriki kuvunja ndoa za watu...’akasema
‘Kwahiyo kwa
usaidizi wako tunaomba iwe hivyo, kuwa japo watu hao wamekiuka sheria za ndoa
zao, makosa hayo yawe kati ya wanandoa , sisi tuweze kuikomesha hii biashara ya
mlungula bila kuleta athari nyingine za kijamii...’akasema muendesha mashitaka.
‘Kwahiyo
mumefanyaje ili hao wahanga wawe tayari kutoa taarifa na hizo kashifa zao
zisiweze kuvunja ndoa zao, ...mjue yote hayo yakifika mahakamani yatawekwa
kwenye kumbukumbu, na ili hii kesi iishe hatuna jinsi inabidi muwasimamishe
mahakamani,...’akasema hakimu
‘Ndio maana
tumekuja kwako kuomba msaada, kama unavyojua, wengi wanakuwa wagumu
kushirikiana na polisi, sisi tukaona haina haja,...tukatumia mbinu za
kuwafuatilia hawa watu bila ya hata wao wenyewe kujifahamu, tukawafahamu ni
nani,tukakutana nao na baadaye ikabidi wakubali, na wakasema wapo tayari kutoa
ushahidi kama ushahidi huo hautaweza kuwekwa wazi na kuathiri ndoa zao...’akasema
mpelelezi
‘Mbinu kubwa ilikuwa kupitia kwenye benki
zetu, huko tuna watu wetu ambao waliweza kutupa taarifa za akaunti zenye
uwalakini, na kila kiasi kikubwa kilivyotolewa isivyo kawaida ya mteja huyo,
tulipata taarifa, na kuanza kufuatilia ni kwanini pesa hiyo ikatolewa....na hili
limetusaidia sana.....’akasema mpelelezi
‘Kwa kufanya
hivyo mnakiuka sheria za usiri wa mteja, huyo mteja ana haki ya kuwashitaki...mnalifahamu
hilo...?’akasema hakimu
‘Ilibidi iwe
hivyo, ili kuwabaini hawa watu, ...lakini kiukweli tulikuja kugundua mambo mengi
yaliyojificha, yanayotendeka kwenye jamii,na watu wanaumia lakini wanashindwa
kushitaki, wanaogopa kushirikiana na polisi....na ni bahati mbaya tu hatukuweza
kuzuia haya mauaji, ...’akasema
‘Ina maana
mlihisi kuwa kunaweza kutokea hayo mauaji...?’ akaulizwa
‘Hapana hatukulitarajia
hilo kabisa, mara nyingi biashara hizi zimekuwa zikifanyika, na mauaji ni
nadra, na ikitokea inakuwa labda mtu kujiua mwenyewe, anapoona kadhalilishwa,
au atadhalilishwa....’akasema huyo mpelelezi
‘Turudi kwa
hawa washitakiwa, kuna huyu mshitakiwa mkuu, je mligunduaje kuwa huyu mshitakiwa
ni kiongozi wa biashara hiyo au anatumiwa, au mnataka sasa aweje,maana bado
hajahukumiwa...?’ akaulizwa
‘Tulimchunguza
sana huyu mshitakiwa, tukawa tunafuatilia nyendo zake,na sasa wengi waliowahi
kufanyiwa hii hujuma wameelezea wazi alivyokuwa akifanya, tumehakiki sauti
aliyokuwa akitumia sehemu mbali mbali, tumegundua kuwa ndio yeye, hatuna shaka
na hilo...’akasema mpelelezi
‘Mhh....kwahiyo
mliweka watu mpaka kwenye vyombo vya mawasiliano,...?’ akauliza hakimu
‘Ilibidi
tufanye hivyo muheshimiwa hakimu ,ili kukomesha kabisa hii biashara yenye
kuumiza jamii...’akasema mpelelezi
‘Na badaye
tulikuja kugundua kuwa huyu mtu alikuwa na mshirika mwenza, kama tulivyosema
kulikuwa na watu wanaisaidia polisi, na mmojawapo ni aliyekuwa mshirika wa
mshitakiwa....mara kwa mara watu wanaondesha biashara hzii hizi walikuwa
wakienda kwa huyu jamaa anayejulikana kama mtaalamu,tukajiuliza ni kwanini...’akasema
mpelelezi
‘Mtaalamu ni
nani..?’ akaulizwa
‘Ni huyu
mumiliki wa kampuni ya mitandao, ndiye mbunifu wa biashara hizi za mitandao,na
yeye ,ndiye alishirikiana na mshitakiwa kukamilisha hiyo biashara haramu
iliyosababisha kifo cha huyo marehemu...’akasema
‘Huyo
mtalaamu yupo wapi...?’ akaulizwa
‘Huyo
Mtaalamu kwasasa bado anaisaidia polisi, tumeamua kumtumia na kazi aliyopewa
ikikamulika na yeye atafikishwa mbele ya
mahakamani yako tukufu kujibu mashitaka yanayomkabili...’akasema muendesha
mashitaka wakiwa na mpelelezi
‘Kwahiyo
mnataka kusema nini...?’ akauliza hakimu
‘Tunachotaka
kusema ni kuwa tumegundua kuwa
mshitakiwa tuliyenaye kwa hivi sasa anapunguziwa mashitaka yake, ....na
tuna maombi mengine dhidi yake, kwani hata yeye kakubali kutoa ushirikiano kwa
makubaliano kama mahakama yako itakubaliana na hilo...’akasema muendesha
mashitaka
‘Kwanini mnasema
mnataka kumpungizia mashitaka, ....kwasababu kutokana na ushahidi mlioutoa hapa
mahakamani mtu huyo kasababisha hayo mauaji yatokee, akishirikiana na wenzake, au....?’ akauliza hakimu
‘Ndio
muheshimiwa hakimu, sisi tulimshitakia kama muuaji,.... kitu ambacho tumegundua
kuwa sio kweli, yeye hastahiki kushitakiwa kama muuaji kwa vile muuaji
tumeshamfahamu, japo hajafikishwa mahakamani, tunamtafuta wapi alipojificha,....’akasema
‘Baada ya
uchunguzi wa kina tumegundua kuwa mshitakiwa alifika eneo la tukio wakati
mauaji hayo yalishafanyika...vielelezo hivyo tunavyo...’akasema muendesha
mashitaka.
‘Kwahiyo mnataka
mshitakiwa ashitakiwe kwa kosa gani...?’ akauliza hakimu
‘Mshitakiwa anashitakiwa
kwa kosa la kuendesha biashara ya mlungula, na kutokana na biashara hiyo akawa
mmoja wa waliosababisha kifo cha marehemu,lakini sio aliyemuua
marehemu...’akasema muendesha mashitaka
‘Mnasema huyo ni msababishi
lakini sio muuaji, mnawezaje kuweka ushahidi wenu mbele ya mahakama,kutofautisha hilo ...?’
akauliza hakimu
‘Ndio muheshimiwa hakimu tutaliweka hilo bayana mbele ya mahakama yako tukufu, kwani huyu mshitakiwa yeye
alitumika, akachochea hiyo biashara ili kupatikana hiyo pesa ya mlungula, na
pesa ikawa inagombewa na watu wengi,...lakini yeye sio aliyemuua marehemu...’akasema
‘Pesa ikagombewa na watu
wengi...!’ hakimu akasema kwa mshangao na muendesha mashitaka akasema;
‘Ndio muheshimiwa
hakimu, kuna watu wengi walikuja kufahamu kuwa kuna pesa kama hiyo imetolewa na
mhanga wa mlungula, ukiacha watayarishajii wenyewe, na watu hao wakaona ni pesa
ambayo ipo nje, ni rahisi kuipata...’akasema muendesha mashitaka
‘Kama
ujuavyo watu ambao hupenda pesi bila hata kuzitolea jasho,...walifuatilia na
kugundua kuwa pesa hiyo ni nyingi, wakaanza
kufuatilia kuona wapi itapelekwa,...tutakuja kuelezea hilo hatua kwa hatua
ilivyofanyika, kwenye ushahidi wetu,..’akasema muendesha mashitaka
‘Katika
kufuatilia huko, ndipo kukatokea kunyang’anyana,...ndipo muuaji akalitenda hilo
kosa, ....’akasema
‘kwahiyo kwa
usemi wako, muuaji hakukususia...?’akaulizwa
‘Kukusudia
yawezekana, ...tukimpata huyu mshitakiwa mwingine tutakiwa tumelithibitisha
hilo, ...’akasemapata mpelelezi
‘Kwahiyo
kumbe bado hamjawa na uhakika...?’ akauliza hakimu.
‘Uhakika upo
muheshimiwa hakimu, ila tutakuwa na maelezoo yaliyojitoshelea tukimpata huyo
mshitakiwa mwingine..’akasema muendesha mashitaka
‘Kwa mantiki
hiyo, huyu mshitakiwa tuliye naye mpaka sasa ambaye mashitaka yake inaendelea
ndiye msababishi wa haya yote,...lakini sio muuaji, na muuaji hajapatikana ?’
akauliza
‘Ndio
muheshimiwa hakimu...’akasema muendesha mashitaka
‘Na mahakama
haiwezi kuthibitisha hilo, mpaka mulete ushahidi na huyo mshitakiwa, mpaka sasa
huyu mshitakiwa ndiye anatambulika kama mshukiwa, ni lini mtamfikisha au mtawafikisha hao washukiwa wengine mahakamani
...?’ akauliza na muendesha mashitaka akageuka kumuangalia mpelelezi.
‘Mumetumia
muda mwingi kwenye hii kesi, hatuwezi kuendelea na kesi kama hamjakamilika, na
hatuwezi kuendelea kumshikilia huyo mshitakiwa kwa shitaka hilo, kama
hamjakamilisha ushahidi wenu, ...hii sasa inakaribia miezii mingapi,mnafanya
utani na kazi zenu...?’ akasema hakimu kwa sauti ya ukali.
‘Ndio
muheshimiwa hakimuni kweli kesi hii imachukua muda kinyume na tulibvyotarajia,
ni kutokana na kuingiliwa na ... ‘akakatiza kuongea na hakimu akauliza
‘Ni nani
yupo juu ya sheria, niambieni, kama kuna kikwazo wekeni wazi, hakuna aliye juu
ya sheria...’akasema hakimu
‘Ndio muheshimiwa
hakimu, ndio maana tunaiomba mahakama yako tukufu itusaidie...’akasema
muendesha mashitaka
‘Mahakama iwasaidie kuhusu nini...?’ akauliza hakimu akionyesha mshangao
‘Kuhusu ombi
la hawa mashahidi , hawa wahanga wa mlungula,... kutokana na ombi lao kuwa hawataki
wajulikane, na sisi tutahakikisha huyu
mshitakwia mwingine anakamatwa,ili kumpata muuaji halisi...’akasema muendesha
mashitaka
‘Sasa kati
ya hao wawili ,...mnasema mmoja hamjamkamata
na mwingine mnaye tayari ambaye kakubali kushirikiana nanyi,
mumeshagundua ni nani hasa mmuaji ...?’
akaulizwa hakimu,na muendesha mashitaka akageuka kumuangalia mpelelezi.
‘Japo bado
kuna utata, ..lakini tuna imani kuwa tukimpata huyo mshitakiwa mwingine,
tutaumaliza huo utata....na kuimaliza hii kesi kabisa’akasema muendesha
mashitaka akigeuka kumuangalia mpelelezi , ikionyesha kuwa alihitajia maelezo
kutoka kwake kwa swali hilo.
Mpelelezi akionekana
kusita kutoa hayo maelezo,kwanza akakohoa kusafisha koo, akitaka kuongea kitu,
na ilionekana ni jambo nzito kulitamka, lakini hakuwa na jinsi...
‘Muheshimiwa
hakimu ....’akaanza kusema, na kabla
hajaendelea simu ya mpelelezi ikatoa sauti ,...kwa haraka akainua hiyo simu na
kuiangalia , ulikuwa ni ujumbe wa
maneno, mpelelezi akasema tafadhali, akawa anausoma huo ujumbe,halafu akainua
kichwa, na kukitikisa kama kukubali
kitu, akasema;
‘Mwishowe
tumempata...’akamuangalia muendesha mashitaka halafu akageuka kumuangalia
hakimu akasema;
‘Muheshimiwa
hakimu, mtu tuliyekuwa tukimtafuta ameshakamatwa akiwa na mwenzake...’ akasema
huku akitabasamu.
‘Sasa kazi
imekwisha....’akasema muendesha mashitaka na hakimu akauliza
‘Huyu
mshitakiwa mwingine naye ni nani?’
hakimu akauliza, huku akimuangalia mpelelezi, na baadaye muendesha
mashitaka, muendesha mashitaka akitabasamu akasema....
‘Muheshimiwa
hakimu, ngoja mimi nikujibu hilo swali ...naye ni miongoni mwa
walioomba....lakini ...’akaanza kusema
NB:
Tunaishia hapa kwa leo,....naona sasa tunafikia kwenye hitimisho, kama kuna
mawazo, nyongeza, tunakaribisha, pia unaweza kuwasiliana nami kwa barua pepe, miram3.com@gmail.com . Huku tukiwa tunajiandaa
kwa kisa kingine, tuombeane heri, tuweze kushinda mitihani hii ya maisha.
WAZO LA LEO: Kuna tabia ya kulindana, mtu
kafanya kosa, kwa vile ni mtoto wa fulani, mtoto wa mkuu, au muheshimiwa fulani,
basi yeye analindwa,kesi yake itapigwa danadana...hii pia inaenda zaidi kwenye
sehemu za kazi, wanaopata kipaumbele ni watoto wa waheshimiwa au wakuu fulani,
kama unabisha nenda sehemu za kazi, kwa namna hii tunajenga matabaka, wenye
nacho na wasio kuwa nacho. Je lini hawa wasio kuwa nacho watapata watu wa
kuwalinda, kuwatetea, kuwapa kipaumbele, ....
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment