'Unafahamu kuwa kijana wako naye amegeuka kuwa adui yako , kaungana na watu wasiokutakia mema,.....?' akaulizwa
'Kijana wangu yupi...!?' Profesa akauliza kwa mshangao
'Kwani wewe una vijana wangapi,.....?' akaulizwa na kabla hajasema neno akaambiwa kwenye simu
'Ni huyo huyo kijana wako aliyekuwa akikuweka hapa mjini kipindi cha nyuma kama hukumbuki vyema, .....umemkumbuka eeh...huyo kijana alikuwa akikufanya upate pesa za wafadhili, na baadaye, sijui ikawaje...alipojitegemea kitumbua kikaingia mchanga....'akaambiwa
'Haiwezekani.....'akasema profesa akitoa macho ya kutoamini
'Sasa ikawaje......' kaka mtu aliyekuwa akisikiliza kwa makini simulizi hilo toka kwa mdogo wake,....baada ya kusikia mtoto wake sasa anatajwa ndio akauliza hilo swali
Tuendelee na kisa chetu
**********
‘Kijana wako
ameungana na yule mama mtemi kuhakikisha unapatikana ushahidi kuwa wewe ni
wakala wa watu wanasumbua wakazi wa hapa kwa shughuli ya mlungula(blackmail)...’akasema
‘What ! Hawezi huyu huyu kijana wangu ,
hapana huyo hawezi kunifanyia hivyo mimi ni baba yake mlezi, nimetoka naye
mbali, haiwezekani...’akasema profesa
‘Kayasema
hayo akiwa na binti wa huyo mama, na kwa hiyo ndio akakubaliwa kuwa mchumba wa
huyo binti , si unamfahamu huyo binti wao, wanayempenda kama nini,...?’
akaulizwa
‘Nisimfahamu
wakati mimi nilikuwanafanya kazi kwao, au unamaana gani kuuliza hivyo...?’
akauliza nay eye
‘Unamfahamu
kwa maana kuwa alishakuwa na mahusiano na kijana wako,...na akawa anakataliwa
huyo binti kuwa na ukaribu na kijana wako....unalifahamu hilo?’ akaulizwa
‘Mhh...hilo
la kukataliwa silifahamu, maana kijana mwenyewe alishakuwa mbali na mimi....’akasema
‘Huyo kijana
hakutakiwa kabisa kuwa karibu na huyo binti, wakawa wanakutana kwa kujiiba,
siku wakabambwa,kijana akataka kupelekwa polisi, binti akamtetea.....’akasema
‘Mhh,
ilifikia hapo, ....sijakutana na huyo kijana muda sasa...’akasema
‘Ndio hivyo,
mwanzoni walimkataa kwa vile walimuhusisha na wewe, wakaona kuwa binti yao, hawawezi
kuwa na mahusiano na kijana wako, kwa vile wewe ni mtu mbaya, kwa tabia yako!’
akaambiwa
‘Hawa watu
nitawafanyia kitu mbaya....hawanijui, eeh....’akasema
‘Upo tayari
kupambana na huyo mama...?’ akaulizwa
‘Nilishamweka
pabaya, akaniwahi, lakini....’akatulia
‘Huwezi
bwana, ..huyo mama humuwezi kamwe, na kwa vila alishakufahamu, ujue akitaka
kukweka ndani anakuweka ndani,....si ndiye huyo anakudai,...’akaambiwa
‘Sasa kama
kakubaliana na huyo kijana wangu kwanini asiniheshimu,kwa vile tumeshafunga
udugu...’akasema
‘Sasa
sikiliza, huyu kijana wako Ili kuwathibitishia kuwa yeye hana uhusiano na wewe
,...ndio akasema yupo tayari kuhakikisha wewe unakamatwa kwa makosa ya
kuwamkorofi kwenye jamii, ....’akasema
‘What, I cant believe this....Haiwezekani,
haiwezekani kabisa....kama huyo kijana atafanya hivyo nitamharibia maisha yake
yote, anafahamu alipotokea una uhakika na hilo,....’akasema profesa
‘Hebu
nikuulize kwanza, ...Je wewe kweli ni mzazi wake...?’ akauliza mtaalamu, na
profesa alikuwa na jibu la haraka, akasema;
‘Hapana mimi
sio baba yake kabisa, mimi ni baba mlezi tu, nilimuokota akiwa porini, nikaweza
kumfikisha hapo alipo, na sasa anataka kunisaliti...’akasema profesa
‘Mimi sasa
sijui,...ila ninakuonya kwa hilo, uwe makini sana, maana naona kila aliyekuwa
karibu nawe anageuka kuwa adui yako, uajua hii inaashiria nini..?’ akaulizwa
‘Mhh kuwa
nitafukuzwa haya maeneo au sio...?’ akasema na kuulizwa
‘Sio
kufukuwa, wewe sasa jela inakukodolea macho,...’akaambiwa
‘Jela,
lakini...’akataka kujitetea
‘Lakini nini!
.... Na pia ukumbuke unapokuwa kwenye shughuli hizi, na wenzako wakahisi kuwa
unaweza kuwa ni tatizo, hawatasita kukumaliza, ukapotea duniani...’akasema
‘Eti
nini...ina maana mtaniua.....!?’ akauliza kwa mashaka
‘Tutakuua! ?
Nani kasema tutakuua, nakuelezea hali halisi, hivi nikuulize kama kuna njia
nzuri za kujipatia pesa, na ndio kazi yenu, na kukatokea mmojawapo ni kikwazo
cha kupatia masilahii na akiwemo anaweza kuwatumbukiza hatiani, kama ni wewe
kiongozi, utashauri nini...?’ akaulizwa
‘Kwani kuna
kiongozi wa mambo haya kila mtu anajifanyia aonavyo, na wewe unatumika tu kama
mchanga dili wa mlungula(blackmail)...au
wewe ndio kiongozi wao....’akasema profesa
‘Mimi nimekuuliza
swali tu...., usije ukasema nimekulenga wewe, ila nimetolea kama mfano kwako,
ikatokea hivyo, mtu anakuwa ni kikwazo, kwa haya mambo yetu....na mkimuacha
anaweza kuwatia hatiani, unafikiri ni ipi njia sahihi...?’ akaulizwa
‘Lakini mimi
sio tatizo, mambo kama haya yanatokea kwa yoyote, au sio, ni moja ya changamoto
kwenye hizi kazi, sioni kama ni tatizo kubwa,mimi nitapambana nao....au una
wazo lolote....au mumekaa kunijadili kuwe mniondoe ,mniue..?’ akauliza
‘Nani kasema
hivyo, mimi nafahamu weweni mjanja, na unajua mwenyewe jinsi gani utakavyojiokoa,
kwa ushauri wangu kwa jinsi hali ilivyo, ....ikibidi njia sahihi ni wewe
kuondoka eneo hili,...lakini ikibidi,kwa hivi sasa ni muhimu kuimaliza hii
dili.. ...’akasema
‘Niondoke,
niende wapi na kibali changu cha kuishi huku ni eneo hili....na nikitoka hapa
nitakwenda wapi na mimi hapa ndipo ninapohemea...’akasema profesa
‘Lakini
ukumbuke, yule mama mtemi anakutafuta na sasa anataka umlipe pesa nyingi tu, utazipatia
wapi hizo pesa, na sizani kama utaweza kupata pesa kwa hizi sasa za kuweza
kumaliza deni lake, na hata ukimlipa pesa sizani kama atakuacha, ataendelea
kukukamua. Si unajua alivyo...’akasema
‘Haya huyo
kijana wako kajitolea kumsaidia huyo mama, ambaye sasa keshakuwa mama mkwe wake,...huoni huyo mama sasa keshakuweka
pabaya, kijana wako anamtaka binti, na njia rahisi ni kupitia wewe, wewe
ukamatwe , uwekwe ndani, ili kijana ampate huyo binti...hayo ndio makubaliano
yao...’akaambiwa
‘Hawaniwezi,
huyo mama anajua kabisa nafahamu siri zake, na kijana naye anajua mimi ndiye
niliyemuweka hapa Ulaya....wakijaribu kunifanyia lolote, kabla sijaingia jela,...’akatulia
‘Na ukumbuke
kuwa,... huyu mteja mpya hajakufahamu kuwa ni wewe, siku akija kukugundua,
umekwisha!’ akasema
‘Mhh,
kwahiyo...?’
‘Karata yako
hii ni muhimu sana,...usipocheza vyema, ukapata pesa, ya kukutosha, ukamalizana
na hao maadui zako, hasa huyo mama mtemi, ndugu yangu tutakusahau...hilo siwezi
kukuficha...’akaambiwa
‘Lakini
nakumbuka nilikuuliza kuwa je kuna uhakika wa kuzipata hizo pesa, kama benki
wameleta utata, kama mke wa huyo jamaa kaingilia kati...huoni hilo ni tatizo,
kama haiwezekani, basi tutafute dili nyingine kabla mambo hayajaharibika....?’
akauliza profesa
‘Pesa
kupatikaa nina uhakika zitapatikana,...na nina uhakika huyo jamaa alivyo,
umemshika kubaya, huyo jamaa mkewe ndiye mwenye kila kitu, kwahiyo anaogopa
sana huyo uchafu wake, uje kuonekana kwa mkewe, anachotafuta kwasasa ni kuhakikisha,
anapata wapi hiyo video ipo,na wahusika ni akina nani,....’akaambiwa
‘Sasa huyo
mama mtemi akija kumuambia kuwa muhusika ni mimi, huoni kuwa mimi nipo
matatani...?’ akauliza
‘Ni mpaka
huyo mama mtemi agundue kitu kama hicho...huyo mama mtemi anapeleleza kutaka
kujua wapi unapozipatia hizo pesa, hajagundua, anakisia tu, akigundue, anaweza
akaichukua hiyo dili akawa ndiye anazichuma hizo pesa....’akasema
‘Haiwezekani....’akasema
profesa
‘Mimi
namfahamu huyo mama kuliko yoyote, mbele ya pesa huyo mama hana
urafiki,....hilo la kusema kabadilika....sahau, ila, kwa vile anataka
kujijengea jina, atakuwa ndumila kuwili tu...sasa wewe endelea kucheza karata
yako vyema kwa huyo jamaa...’akasema
‘Mhh, hii
dili ni hatari, kama ningelijua nisingeichukua, sasa....’akasema profesa kabala
hajamaliza,mtaalamu akasema
‘Wewe
endelea kuleta pesa kutoka kwa huyo mtu, kwani huyo jamaa hana ujanja, ila kwa
sasa anatapatapa tu, kwani kafikia hatua ya kutaka kutafuta mpelelezi...’akasema
‘Oh, ....una
uhakika na hilo...?’ akauliza profesa akizidi kuchanganyikiwa
‘Mimi
ninayokuambia sio maswala ya kuambiwa nafahamu na nina uhakika kwa kila kitu,
mimi huwa sibahatishi...’akasema
‘Mhh, huoni
sasa hilo ni tatizo....hii dili naona sitaiweza...itanipeleka kubaya?’ akauliza
‘Hiyo dili ni
kazi yako, ni dili nzuri tu kama ukicheza vyema, mimi hayo nimekupa kama
angalizo, na ukimbana vyema huyo jamaa atachanganyikiwa, wewe ni profesa bwana,
hii pesa si ya kuachia....kama umeshindwa nimpe mtu mwinine aimalizie...naweza
kuiuza kwa bei mbaya..’akaambiwa
‘Lakini si
umesema huyo jamaa kamtafuta mpelelezi, huoni kama nitakuwa hatarini....nitajulikana,na
mimi nitakwenda wapi..?’ akauliza
‘Hayo ni
mambo ya kawaida,..., na wapelelezi wote wa hapa nawafahamu, hiki
ninachokuambia ni uhakika kuwa huyo jamaa katafuta mpelelezi, na ni jana tu,
huyo jamaa alikwenda kumuona yule mpelelezi...’akasema
‘Mpelelezi
yupi...?’ akauliza
‘Mpelelezi
mmoja wa njaa kali, anayefanyia kazi
hapa kwenye ofisi zangu...’akasema
‘Oh,...ina
maana kumbe keshamtafuta mpelelezi tayari,
na ni nani huyo mpelelezi,ni...Njagu
nini...?’ profesa akauliza
‘Ndio huyo
huyo...’akasema
‘Hilo sasa
ni tatizo,maana huyo mpelelezi ndiye aliyechukuliwa na huyo mama
mtemi,...akanigundua kuwa ni mimi....my,
God,...this now is disaster.’akasema
NB: Tuishie
hapa
WAZO ZA LEO: Tumshukuru mungu kwa kilajambo,tunaweza kuoana huenda tumeonewa, au ukafikia hata kukufuru kuwa kwanini mimi, lakini yote hayo yanaweza yakawa ni heri kwako,ikawa ni njia katika kufikia mafanikio fulani,ikawa ni mwanzo wa neema..kamwe tusikate tamaa.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment